Professional Documents
Culture Documents
Malidavis Investment Limited
Malidavis Investment Limited
BAINA YA
(MPANGISHAJI)
NA
………………………………………………
(MPANGAJI)
Huuu ni mkataba wa leo ……………………. mwezi ………………….mwaka 20……………
BAINA YA
MALIDAVIS INVESTMENT LTD S.L.P 669, ARUSHA , (ambaye kwa minajili ya mkataba
huu atajulikana kama "mpangishaji') kwa upande mmoja.
NA
……………………………………………………………….mwenye namba ya simu ……………………….
(ambaye kwa minajili ya mkataba huu atajulikana kama "MPANGAJI" Kwa upande
mwingine.
WAHUSIKA WA MKATABA HUU WANAKUBALIANA KAMA IFUATAVYO:
1.0 MAELEZO YA NYUMBA
1.1 Sehemu ya nyumba inayopangishwa ni chumba chenye choo pamoja na
sehemu ya kupikia, katika nyumba namba 4 iliyopo Njiro Seminari, block
C1, kwa mjibu wa mkataba huu kitajulikana kama CHUMBA.
1.2 Kwamba, MPANGISHAJI anampangishia mpangaji kwa ajili ya Makazi na
kwamba taratibu za kupangisha nyumba zinazofahamika kisheria zifuatwe.
1.3 Kwamba,Mpangaji haruhusiwi kumpangishia mtu mwingine ila tu
ataitumia kwa matumizi yaliyoainishwa kwenye kipengele 1.2 Hapo juu.
2.0 MALIPO YA KODI YA PANGO KWA MWENYE NYUMBA
2.1 Kodi ya pango kwa kipindi cha kuanzia tarehe …………………. Hadi tarehe
…………………. ni shilingi ……………………….. na mpangaji atalipa kiasi hicho
kabla ya kusaini mkataba.
2.2 Mpangaji atawajibika kulipa gharama za umeme anaotumia pamoja na
kuchangia gharama za maji, ulinzi na usafi kama itakavyopangwa.
2.3 Mpangaji ataweka kiasi cha kodi ya mwezi mmoja kama dhamana, ambacho
kitarudishwa siku anakabidhi chumba kama hakuna uharibifu wowote
uliofanywa na mpangaji. Kama kuna uharibifu wa chumba au vifaa
vilivyopo chumbani au kwenye mazingira uliofanywa na mpangaji, basi
kiasi cha dhamana kitatumika kufidia uharibifu huo na kama uharibifu ni
mkubwa kuliko kiasi cha dhamana, mpangaji atalazimika kuongeza kiasi
cha pesa kufidia gaharama za uaharibifu.
3.0 MDA WA MKATABA
3.1 Mkataba ni wa miezi …… unaoweza kuongezwa baada ya pande zote
kuridhia. Mkataba unaweza kuvunjwa kwa kutoa taarifa mwezi mmoja
kabla au kulipa kodi ya mwezi mmoja kwa upande unaokusudia kuvunja
mkataba.
Mpangishaji……………………………………………. Mpangaji:……………………………………………...