You are on page 1of 3

MAKUBALIANO YA UPANGAJI WA NYUMBA

Umefanyika leo tarehe……… Mwezi……… 20……

KATI YA
Ndugu __________ wa S.L.P……. .., anaeishi …… shehia ya ………., wilaya ya MJINI
MAGAHARIBI B, ZANZIBAR (ambaye ni mkodishaji).
NA
_______________wa S.L.P ………. Zanzibar anaeishi ………, shehia ya ………., wilaya ya
MJINI, ZANZIBAR (ambaye ni mpangaji).

A: MAELEZO YA AWALI

KWA KUWA MWENYE NYUMBA ni mmiliki halali wa sehemu ya nyumba namba ….……….

NA KWA KUWA MPANGAJI anapenda na ameonyesha nia ya kupanga kwenye nyumba hiyo na
MWENYE NYUMBA ameridhia maombi hayo.

BASI MAKUBALIANO HAYA YANASHUHUDIA YAFUATAYO:


1. MWENYE NYUMBA atampangisha MPANGAJI na MPANGAJI amekubali kupanga hiyo
kwa ajili ya makazi kwenye nyumba iliyotajwa hapo juu.
2. Kodi ya pango itakuwa ni Laki Tano (500,000) kwa mwezi.
3. MPANGAJI atalipa jumla ya ……………………… kwa mwezi sita.
4. Makubaliano haya yatakuwa kwa mwaka mzima na yataanza kufanya kazi tarehe ……
mwezi …… mwaka ….. mpaka tarehe …… mwezi …… mwaka …..
5. Fedha italipwa cash kwa mwenye nyumba.

B: MASHARTI YA JUMLA

6. a). MPANGAJI atatumia na kutunza kwa hali ya usafi kwa muda wote wa makubaliano
haya

b). Mpangaji atatoa ruhusa kwa mwenye nyumba kuingia ndani ya nyumba na kuifanyia
ukaguzi kulingana na ibara 6 (a) ya makubaliano haya.

c). Mpangaji haruhusiwi kuifanyia matengenezo nyumba bila ya ridhaa ya kimaandishi


kutoka kwa mwenye nyumba

d). Mpangaji atagharamia matengenezo yote ya uharibifu utakaosababishwa na mpangaji


mwenyewe, ama wafanyakazi wake au wageni wake.

7. a). Mwenye nyumba ataheshimu makubaliano haya ikiwemo kutoingia ndani ya nyumba
kwa ukaguzi pasipo na taarifa ya awali ya kimaandishi isiyopungua siku tatu.
b). Mwenye nyumba ataendelea kulipia kodi ya umiliki wa mali (Property Tax) kwa kipindi
chote cha makubaliani haya.

c). Mwenye nyumba atagharamia matengenezo ya nyumba ambayo yametokana na


hitilafu za ujenzi wa awali na/au hazihusiani na kuwepo kwa mpangaji ndani hapo.

C: UTATUZI WA MIGOGORO NA USITISHWAJI WA MAKUBALIANO

8. a). Endapo kutakuwepo kutoelewana basi migogoro kati ya pande zote mbili, kabla ya
kupelekwa mahakamani, utasuluhishwa na msuluhishi atakayependekezwa na
kukubaliwa na pande zote.

b). Makubaliano haya yatatawaliwa na sheria zinazolinda na kuongoza makubaliano


(mikataba) nchini.

c). Endapo mpangaji ataendelea kupanga nyumba hii baada ya kipindi cha makubaliano
haya kumalizika, itabidi atoe taarifa ya maandishi kwa mwenye nyumba katika kipindi
kisichozidi miezi mitatu kabla ya makubaliano haya kumalizika.

d). Endapo mwenye nyumba au mpangaji atataka kusitisha mkataba huu kabla ya
kumalizika kwa muda wake, atalazimika kutoa taarifa ya maandishi kwa upande mwingine
katika kipindi kisichozidi miezi mitatu kabla ya siku ya kusitisha makubaliano haya.

Pande zote mbili wanaweka sahihi na/au alama zao za vidole katika makubaliano haya
kuridhisha nia ya kusudi zao kama ifuatavyo

Tarehe …… Mwezi ….. 20…….

…………………………………………
MWENYE NYUMBA
NA

Tarehe….. Mwezi…… 20……


…………………………………………………………
SHAHIDI WA MWENYE NYUMBA

ABDULRAZAK ABUBAKAR ABDULRAZAK

Tarehe……. Mwezi ……. 20…..

……………………………………
MPANGAJI
NA

EDDIE JRILL

Tarehe….. Mwezi…… 20……

…………………………………………………………
SHAHIDI WA MPANGAJI

You might also like