You are on page 1of 4

Page 1 of 4

MKATABA WA KUPANGISHA CHUMBA CHA OFISI


(LEASE AGREEMENT)

MKATABA umefanyika Tarehe ……….. Mwezi …………………….Mwaka 2016 kati


ya Ndugu ABEL DAVIS MWAMUNYANGE wa P. O. Box 76666, Dar es Salaam
ambaye kwenye Mkataba huu atajulikana kama MWENYE NYUMBA, jina ambalo
litamaanisha kila mahali ambapo maudhui yake yataruhusu (yaani: Watendaji, Watawala
na Wawakilishi wa pande zote).

NA

MADRID GROUP OF COMPANIES (Mbeya Branch) wa P. O. Box


…………………DAR ES SALAAM ambayo ni kampuni iliyo anzishwa kwa sheria za
Tanzania kwenye Mkataba huu inajulikakana kama MPANGAJI – jina ambalo
litamaanisha mahali pote ambapo maudhui yake yataruhusu hivyo – (yaani Watendaji,
Watawala na Wawakilishi wa pande zote).

MWENYE NYUMBA na MPANGAJI kwa pamoja wanashuhudia:

1. KWAMBA:

(a) MWENYE NYUMBA amempangisha MPANGAJI Chumba cha


biashara (Ngonga Pub and Restaurant) kwenye nyumba yake iliyoko
Kitalu Na…… Block ….. Mbeya Forest, Dar es Salaam, ambacho
kitajulikana kwa jina la (“Office I”) kwa kipindi cha Miezi 12 (Mwaka
Mmoja) kuanzia Tarehe 01/8/2016 hadi 30/7/2017 kwa gharama ya TSh.
100,000/= (shilingi laki moja tu) kwa mwezi, ambazo zitakuwa zinalipwa
kwa mwaka kila mwaka.

(b) MPANGAJI amemlipa na MWENYENYUMBA anakiri kupokea kiasi


cha pesa (millioni moja na laki mbili za kitanzania(1,200,000 TZS ) kwa
ada ya kodi ya miezi kumi na mbili 12) hadi Mwezi Agosti, 2016 kama
Stakabadhi zinavyoonyesha. na ataendeelea hivyo hivyo hadi mwisho wa
Mkataba huu.

2. MAKUBALIANO MENGINE NI KWAMBA:

i) MPANGAJI atatumia chumba hicho kwa ajili ya matumizi ya biashara


iliyotajajwa hapo juu tu.

ii) MPANGAJI ataheshimu sheria zote na taratibu halali zinazokubalika na


jamii ili kudumisha usalama wa watu na mali zao.

iii) MPANGAJI ataweka chumba hicho katika hali ya usafi wa kuridhisha nje
na ndani; ikiwa ni pamoja na utunzaji wa kuta, milango, madirisha, nyaya
Page 2 of 4

na vifaa vya Umeme ambavyo ni MALI YA TANESCO vilivyomo ndani


ya sehemu ya ofisi hiyo.

iv) MPANGAJI haruhusiwi kumpangisha au kubadilishana upangaji na mtu


mwingine (kupasiana pango au Ku-sub-let) ofisi/eneo la biashara
aliyopangishwa, pia asije akafanya matengenezo yoyote ya kiujenzi katika
Ofisi hiyo bila ya kushauriana na kupata kibali kutoka kwa MWENYE
NYUMBA.

v) MPANGAJI atamruhusu MWENYE NYUMBA na MAOFISA


WAKAGUZI WA LUKU kutoka TANESCO kuingia muda na wakati
unaofaa (official hours)) kuona na kufanya matengenezo yatakayohitajika
baada ya kuarifiana na MPANGAJI au MWAKILISHI WAKE ili mradi
matengenezo hayo hayatachukua muda mrefu au kusababisha uhamishaji
nje wa vifaa vya ofisini hapo.

vi) MPANGAJI atalipia umeme (LUKU) kulingana na matumizi yake


mapema asingoje LUKU kumalizika kabisa na umeme kuzimika.

vii) Kwa vile nyumba haijawa na Kisima cha Maji, Mpangaji atajitegemea
kwa kujichotea maji yake kwa ajili ya matumizi yake ya Choo, usafi, n.k.
Vile vile MPANGAJI atasaidiana na MWENYE NYUMBA kuondoa
Maji Taka endapo tatizo hilo litajitokeza.

3. PANDE ZOTE ZIMEKUBALIANA KWAMBA:

(a) MWENYE NYUMBA atalipa Kodi ya Kiwanja (Land Fee), Kodi ya


Majengo (Property Tax), na zinginezo kwa mujibu wa Sheria za
Halmashauri ya Mji.

(b) Kwa kuwa suala la Taka-Ngumu limekuwa kero mijini, MPANGAJI


atahakikisha kuwa anajitegemea kwa kuondoa takataka zake atakazo
zizalisha muda wote wa pango.

(c) Ifahamike wazi kuwa iwapo MPANGAJI atalipa kodi


waliyokubaliana katika MKATABA huu, na kulipa Bills zake kama
inavyopaswa, atakaa raha mustarehe bila bugudha yoyote ile katika Ofisi
hiyo kutoka kwa MWENYE NYUMBA.

4. VILE VILE IMEKUBALIWA NA KUTAMKWA KWAMBA:

(i) Endapo MPANGAJI atanuia kuendelea kupanga nyumba iliyotajwa


kwa kipindi kingine baada ya kipindi cha Mkataba huu kumalizika, na
ikiwa nia yake ipo, atampa MWENYE NYUMBA taarifa kwa maandishi
Page 3 of 4

si chini ya siku 30 (mwezi mmoja) kabla ya kumalizika kwa kipindi


kilichokubaliwa katika MKATABA huu na iwapo hakuna ukiukaji wa
makubaliano yoyote yaliyo katika MKATABA huu unaomalizika.

( ii) MWENYE NYUMBA atampa MPANGAJI taarifa ya miezi 3 kutoka


kwenye Ofisi hiyo endapo atahitaji Ofisi hiyo kwa dharura au kwa
matumizi yake mwenyewe. Vile vile MPANGAJI atampa WENYE
NYUMBA Taarifa isiyopungua miezi 2 (miwili) endapo ataamua kuachia
ofisi hiyo kwa ajili ya wapangaji wengine, au vinginevyo.

(iii) MKATABA huu utaishia tarehe 30-05-2017. Endapo MPANGAJI


atapenda kuendelea kupanga ofisi hiyo, na atakuwa ameonyesha nia hiyo
kama ilivyo kwenye Kifungu Namba 4(1) juu, itabidi kufanya
makubaliano mapya na MWENYE NYUMBA kwa namna ambayo
wataafikiana wakati huo.

PANDE ZOTE ZINASHUHUDIA kwa kuweka Sahihi zao hapa kwa tarehe na Mwaka kama
ilivyo onyeshwa.

IMETIWA saini na ;

Abel Davis Mwamunyange ambaye


Ametambulishwa kwangu na
…………………………………………….. ………………………………………
Ninamfaham binafsi leo tarehe MWENYENYUMBA
……..June ,2016

IMETHIBITISHWA NA:

JINA …………………………………………….

SAINI ……………………………………………..

ANWANI ……………………………………………..

WADHIFA ……………………………………………..

TAREHE ……………………………………………..
Page 4 of 4

IMETIWA saini na ;

MADRID GROUP OF COMPANIES (Mbeya Branch)


Ambaye atatambulishwa kwangu …………………………………….
……………………………………… MPANGAJI
Ninamfaham binafsi leo tarehe
……..July ,2016

IMETHIBITISHWA NA:

JINA …………………………………………….

SAINI ……………………………………………..

ANWANI ……………………………………………..

WADHIFA ……………………………………………..

TAREHE …………………………………………….

You might also like