You are on page 1of 20

2020

KANUNI ZA JAMII, 2020

Kwa Matumizi ya Wanachama


wa Ushirikiano Group DSM tu.
Marekebisho ya kanuni hizi
yalifanywa mwezi Februari
2020 na kupitishwa tarehe
26/7/2020.

Toleo la 4.0

Julai 2020

1
YALIYOMO
1.TAFASIRI YA MANENO....................................................................................................................... 3
2. TARATIBU ZA KIJAMII ZA KIKUNDI CHA USHIRIKIANO.................................................. 4
3.0 VIKAO YA KIKUNDI CHA USHIRIKIANO ............................................................................. 6
4.0 UTARATIBU WA KUTOA TAARIFA ........................................................................................ 7
5.0 UTARATIBU WA KUSHIRIKI KWA MGONJWA .................................................................. 8
6.0 UTARATIBU WA KUSHIRIKI KWENYE MISIBA. ................................................................ 9
7.0 UTARATIBU WA KUSHIRIKI HARUSI/SENDOFF NA SHUGHULI ZINGINE ZA
JAMII. ........................................................................................................................................................ 13
8. USHIRIKI WA WANACHAMA WALIO NJE YA DAR ES SALAAM / ...................................... 14
TANZANIA NA NJE YA NCHI .............................................................................................................. 14
9. SIKU YA USHIRIKIANO YA MWAKA. ...................................................................................... 14
10. MIIKO NA FAINI KATIKA SHUGHULI ZA KIJAMII. ........................................................ 15
11. UDHURU ....................................................................................................................................... 16
12. IDARA YA AKINA MAMA ........................................................................................................ 16
12.3 VIONGOZI WA IDARA YA AKINA MAMA .......................................................................... 18
12.4 MNUFAIKA WA IDARA YA UMOJA WA AKINA MAMA ................................................. 18
12.5 MAWASILIANO KWA AKINA MAMA................................................................................... 19
13.0 VIKAO VYA SEKRETERIETI. ..................................................................................................... 19
14.0 MABADILIKO YA KANUNI ZA KAMATI YA JAMII .............................................................. 20
15.0 MUDA WA KUANZA KUTUMIKA KANUNI HIZI ................................................................... 20

2
1. TAFASIRI YA MANENO.

1.1 Kushirikiana - kujitoa kwa Hali na Mali ikiwemo kutoa Michango ya mawazo na mali

pamoja na kushiriki katika matukio mbali mbali ya kikundi.

1.2 Mwanachama - Ni familia kwa mujibu wa katiba na katika Shughuli za kijamii ni

ushiriki wa baba na mama Katika shughuli za kijamii.

1.3 Mtoto - Mtoto wa kuzaliwa na mwanachama kwa mujibu wa sharia za nchi.

1.4 Baba/Mama Mkwe - Ni wazazi wa kike na kiume wa wanandoa wawili wa wanachama.

1.5 Ndoa - Muunganiko wa Mke na mme (mmoja) unaofanya familia, wenye ndoa

inayotambulika kisheria (Kimila, kidini au kiserikali).

1.6 UG Women – Ni idara ya akina mama ndani ya kikundi cha ushirikiano.

1.7 Sekreterieti – Ni kamati inayojumuisha viongozi wakuu wa Umoja yaani Mwenyekiti,

Katibu na Mweka Hazina pamoja na wenyeviti wa kamati nne za kudumu kwa mujibu

wa katiba hii.

3
2. TARATIBU ZA KIJAMII ZA KIKUNDI CHA USHIRIKIANO

2.1 Kwa mujibu wa sehemu ya 3(b) ya katiba ya ushirikiano Group, Kila mwanachama

atatakiwa kushiriki kwa hali na mali katika shughuli zote za jamii za kikundi.

2.2 Ili kuleta ufanisi wa kuendesha shughuli za kijamii mwanachama atatoa taarifa ya

tukio/shughuli kwa mujibu wa utaratibu za taarifa ulioonyesha hapo chini. (kwa

mujibu wa kifungu 2.7).

2.3 Kila mwanaushirikiano atahakikisha anatekekeleza wajibu wake wa kujitoa na

kujitolea kwa hali na mali bila kubagua katika shughuli zote za jamii za kikundi.

2.4 Kikundi hakitakubali majungu, umbea na uchonganishi katika shughuli zote za jamii,

taratibu za kueleza dukuduku/mawazo/changamoto ni pamoja na kueleza waziwazi

kwenye vikao husika. Kamati ya maadili itachukua hatua kwa mujibu wa kanuni kwa

mtu atakayeenda tofauti/kinyume na kanuni hizi za jamii.

2.5 Wakati wa shughuli au tukio Mwanachama (mume na mke) watapimwa ushiriki kila

mmoja ili kuleta nidhamu na uwajibikaji katika kikundi.

2.6 Ili kuleta ukaribu wa wanachama na familia zao, kamati itaandaa utaratibu wa

kutembeleana kwa mujibu wa vikao maalum vitakavyopangwa. Vilevile kamati ya

jamii itaandaa siku ya USHIRIKIANO ya mwaka itakayowahusu familia zote za

wanachama.

2.7 Taarifa za kutokushiriki katika shughuli zitatolewa kwa mwenyekiti wa kikundi au

mwenyekiti wa kamati ya kijamii, madaftari ya mahudhurio yatatayarishwa kwa kila

mwanachama kusaini katika ushiriki wa shughuli yeyote ya jamii.

4
2.8 Atakayeshindwa kushiriki bila taarifa atatozwa faini kadri ya utaratibu wa faini

ulioonyeshwakatika kifungu cha 9.0 cha kanuni hizi. Mwanachama atakayefikisha

faini ya matukio Matatu (3) mfululizo atafikishwa kwenye kamati ya maadili.

5
3.0 VIKAO YA KIKUNDI CHA USHIRIKIANO

3.1 Kutakuwa na kikao kila mwezi kwenye kikundi cha ushirikiano kiitakavyofanyika

kwa mzunguko kwa kila mwanachama kama itakavyopangwa na mwenyekiti wa

kamati ya jamii.

3.2 Vikao vya ushirikiano vitakuwa vya aina nne: - Kikao cha kila mwezi, kikao cha

dharura ambacho kitakuwa maalum kujadili masuala ya dharura, kikao cha kamati

tendaji ya sekretarieti na kikao cha kila mwisho wa mwaka cha siku ya ushirikiano.

3.3 Kila mwanachama ataandaa kikao hicho, zamu yake ikifika kama itakavyosomeka

kwenye ratiba ya vikao vya kila mwezi.

3.4 Mwenyekiti wa kamati ya jamii ataandaa ratiba ya vikao vya mwaka mzima na kuitoa

kwa wanachama.

3.5 Mwenyekiti wa kamati ya jamii atatoa taarifa ya mahala pa kufanyika kikao endapo

kutakuwa na mabadiliko ya mahala pa kufanyia tofauti na inavyosomeka kwenye

ratiba ya vikao vya kila mwezi.

3.6 Ikitokea mwandaaji wa kikao atakuwa na dharura, ni jukumu lake kumtafuta mtu

mwingine ambaye kulingana na ratiba ataandaa kikao hicho kwa makubaliano ya

kubadilishana naye. Taarifa itatolewa kwa mwenyekiti wa kamati ya jamii kwa

kumtaarifu atakayeandaa kikao ili awajulishe wanaUshirikiano.

3.7 Kikundi kitatoa (sh 50,000/=) shilingi elfu hamsini kwa mwanachama mwandaaji wa

kikao cha mwezi.

3.8 Kikundi kitatoa sha 50,000/= (shilingi elfu hamsini) kwenye kikao cha Kamati tendaji

ya sekretarieti kughalimia maji na chakula kwa wajumbe.

3.9 Vikao vya sekretarienti muda wa kukutana umeelezwa kwenye kifungu 13.4

6
3.10 Viwango vya kugharimia vikao vya kikundi tajwa hapo juu kwenye kifungu 3.2,

vinaweza kubadilika kulingana na wakati na mahitaji ya kikundi.

4.0 UTARATIBU WA KUTOA TAARIFA

4.1 Kama ilivyoelezwa katika katiba, shughuli za jamii zitakazowashirikisha

wanakikundi/ wanachama ni pamoja na:

4.1.1 Msiba

4.1.2 Ugonjwa

4.1.3 Ndoa/send off.

4.1.4 Matukio mengine kama kuunguliwa moto, siku ya ushirikiano n.k.

4.2 Taarifa za shughuli/matukio zitatolewa aidha kwa simu, mtandao (e-mail),

maandishi, ana kwa ana kwa Mwenyekiti wa Ushirikiano /Mwenyekiti wa

Jamii.Taarifa iwe kamili kwa kueleza ni wapi, lini, uhusiano na utaratibu upi

uliopo Shughuli/tukio husika.

4.3 Mwenyekiti wa kikundi/Mwenyekiti wa Jamii atatoa taarifa kwa wanakikundi na

kuwafahamisha wajumbe wa kamati ya jamii kama kuna utaratibu utakaofaa

kuendeshwa kulingana na tukio/shughuli husika. Taarifa hizi zitatolewa kwa

wanaushirikiano wote. Taarifa zisichukue muda mrefu ili kufanya utekelezaji uwe wa

haraka.

4.4 Taarifa zingine zisizo kwenye utaratibu lakini zinajenga mahusiano na upendo ndani

ya wanakikundi kama kuhitimu/kufaulu kiwango Fulani cha elimu kw mwanachama,

mtoto wa mwanachama, kufaulu kibiashara, kujenga/kununua nyumba, gari,

kusherehekea siku ya kuzaliwa, kipaimara, Ubatizo, kupata mtoto n.k. zitatolewa

kwenye kamati ya kijamii ili kuwashirikisha wanakikundi.

7
5.0 UTARATIBU WA KUSHIRIKI KWA MGONJWA

5.1. Taarifa zote za ugonjwa wa mwanachama au mwanafamilia wa mwanachama

zitatolewa kadri ya utaratibu wa kutoa taarifa kifungu (4.0) hapo juu.

5.2. Wanachama watashiriki kwa kwenda kumuona mgonjwa na kushiriki kumsaidia kwa

hali na mali ili kumwezesha apone. Upendo wa kumfariji kila wakati utakuwa ndio

utamaduni wa wanakikundi.

5.3. Mwanachama akiugua na kupata matatizo ya kumpelekea kulazwa hospitali Zaidi

ya siku tano, taarifa italetwa kwa mwenyekiti wa kikundi / kamati ya jamii kwa

utaratibu ulioelezwa kwenye kifungu (4) hapo juu.

5.4. Mwenyekiti wa kamati ya jamii atachukua taarifa za mgonjwa zilizoko kwenye

nyaraka za matibabu (prescriptions), majibu ya vipimo vya uchunguzi wa ugonjwa

zilizotunzwa kwenye faili la mgonjwa, taarifa za mgonjwa pia zinaweza kutolewa na

watumishi wa hospitali alikolazwa wodini (Daktari /Muuguzi wa wodi na watumishi

wengineo).

5.5. Mwenyekiti wa kamati ya jamii baada ya kupata taarifa za mgonjwa, atazifanyia

tathimini ya kina akishirikiana na wajumbe wa kamati yake, au wanachama wengine

waliofika kumuona mgonjwa hospitalini kwa kujirithisha na ndipo atawasiliana na

mwenyekiti wa kikundi kumuomba aidhinishe malipo, na baadaye mhasibu

huelekezwa kuandaa.

5.6. Kikundi kitatoa shs 200,000/= (shilingi laki mbili) kumsaidia mgonjwa kama ugua

pole. Ugua pole hiyo atapewa mwanachama anayemhudumia mgonjwa (anayekaa na

mgonjwa).

8
5.7. Ugua pole mgonjwa atapewa mara moja kila baada ya miezi sita, kwa mwaka

atapewa mara mbili tu, na hii itatumika kwa magonjwa ya kawaida na sugu ya

kuugua muda mrefu.

5.8. Mwanachama atakayestahiki kupata ugua pole ni yeyote aliye hai / aliyetimiza

vigezo vya kikatiba na kikanuni (yaani awe hadaiwi ada ya kila mwezi au

kulimbikiza ada zaidi ya miezi mitatu, amelipa mikopo yake aliyokopa kwenye

kikundi, mchango wa uwekezaji na michango mingine iliyopitishwa na mikutano

halali ya kikundi).

6.0 UTARATIBU WA KUSHIRIKI KWENYE MISIBA.

6.1 Kama ilivyoanishwa katika katiba (kifungu namba 7 - (a), misiba itakayo wahusu

wana kikundi moja kwa moja ni pamoja na: -

6.1.1 Msiba wowote utakaotokea nyumbani kwa mwanachama isipokuwa wa

kuhamishiwa.

6.1.2 Msiba wa mwanachama mwenyewe (mke au mme)

6.1.3 Mtoto wa mwanachama.

6.1.4 Baba / Mama mzazi wa mwanachama (wa mme /mke wa familia).

6.2 Taarifa zitatolewa kwa mujibu wa kanuni za taarifa (kifungu 4.0).

6.2 MSIBA WA DAR ES SALAAM

Wanachama watahudhuria wote kadri ya taarifa zitakavyotolewa, michango ya kuendesha

shughuli za msiba itatolewa kwa njia ya daftari kwa kushirikiana na makundi mengine ya

9
kijamii. Wanakikundi watakuwa mstari wa mbele wakati wote kufanikisha shughuli ya

msiba.

6.2.1 Daftari la mahudhurio litakuwepo wakati wote wa msiba ili wanachama

kuonyesha ushiriki wao.

6.2.2 Kila mwanachama atatakiwa kutoa mchango wa Tshs. 50,000.00 kwa ajili ya

kufanikisha shughuli za msiba. Kiwango hiki kitabadilika kadri wanachama

watakavyoona katika mkutano wa mwezi au wa Dharura.

6.2.3 Rambirambi ya kikundi itakuwa

6.2.3.1.1 Mwanachama - shs 700,000/=

6.2.3.1.2 Mtoto wa mwanachama - shs 700,000/=

6.2.3.1.3 Baba/baba mkwe - shs 600,000/=

6.2.3.1.4 Mama/mama mkwe - shs 600,000/=

6.2.3.1.5 Mtu mwingine aliyefia nyumbani - shs 500,000/=

6.2.4 Kiwango hiki kitabadilika kadri wanachama watakavyoona inafaa, mabadiliko

yatapitishwa na mkutano wa kila mwezi au wa dharura.

6.3 MSIBA NJE YA DAR ES SALAAM –

Mwanachama aliye nje ya Dar es salaam akipata msiba nyumbani

6.3.1 Taarifa zitatolewa kama kawaida, wanachama watashirikikishwa michango ya

kufanikisha msiba (Kama ilivyoanishwa kifungu (4.1.1), (4.1.2), (4.1.3) na (4.1.4)),

taarifa za maendeleo ya musiba zitakuwa zinatolewa.

10
6.3.2 Kamati ya jamii itapendekeza wawakilishi wa wanaushirikiano ili kushiriki vyema

kwenye musiba wa mwanakikundi aliye nje ya Dar es salaam.

6.4 MSIBA UTAKAOTOKEA NJE YA FAMILIA (MAKAZI) YA MWANACHAMA:

6.4.1 Msiba wa mwana kikundi unaotokea nje ya familia (makazi na mikoani) kwa

walengwa (kwa mujibu wa kifungu (6.1.2), (6.1.3) na (6.1.4), taarifa zitatolewa,

kikundi kitashirikishwa kutoa kiwango cha rambirambi. Rambirambi ya kikundi

itakuwa: -

6.4.1.1 Mwanachama - shs 700,000/=

6.4.1.2 Mtoto wa Mwanachama -shs 700,000/=

6.4.1.3 Baba/baba Mkwe - shs 600,000/=

6.4.1.4 Mama/Mama Mkwe -shs 600,000/=

6.4.1.5 Kiwango cha rambirambi tajwa hapo juu kinaweza kubadilika kadri

wanachama watakavyoona inafaa, mabadiliko haya lazima yapitishwe na

mkutano wa kila mwezi au wa dharura.

6.4.2. Msiba ukitokea nje ya Dar es Salaam, kila mwanachama atatoa rambirambi kiasi cha

shilingi elfu arobaini (shs 40,000/=)

6.4.3 Baada ya mfiwa kurudi kutoka msibani, taarifa itatolewa kwa wanachama na taarifa ya

siku ya kwenda kumhani mfiwa itatangazwa.

6.4.4 Majina ya familia za wanachama walioenda kuhani msiba yataandikwa kwenye daftari

maalumu la mahudhurio ya misiba iliyotokea kwenye kikundi.

6.4.5 Familia ambazo hazitashiriki kuhani tukio la msiba wa mwanachama mwenzetu

zitaadhibiwa faini ya shilingi elfu kumi (shs 10,000/=). Adhabu hii italipwa bila utetezi

11
wowote ili mradi taarifa ilishatoka na kila mwanachama aliipata, ila tu walipuuza

hawakwenda bila ya kutoa taarifa ya udhuru.

6.4.6 Endapo familia itafikisha adhabu tatu mfululizo bila kuhudhuria misiba ya wanachama,

kamati ya jamii itapeleka majina ya familia hizo kwa katibu wa kikundi, na katibu wa

kikundi ataziandikia barua familia hizo ziitwe mbele ya kamati ya nidhamu kujieleza

kwa nini hazihudhurii misiba ya wanachama.

6.5 UTARATIBU WA KUTOA RAMBIRAMBI KWA MFIWA KAMA MSIBA UNA

WANACHAMA ZAIDI YA MMOJA UNAOWAHUSU MOJA KWA MOJA.

Rambirambi iliyoainishwa Kikatiba & Kikanuni kila mwanachama mwenye sifa anastahili

kupewa kama ilivyoelekezwa.

6.6 MSIBA NJE YA UTARATIBU WA USHIRIKIANO:

Msiba ulio nje ya utaratibu itatolewa taarifa na kamati ya jamii kupitia kwa Mwenyekiti wa

Ushirikiano /Jamii ili kuwashirikisha wanachama kuendeeleza upendo kwa kushirikishana.

12
6.7 SIFA ZA MWANACHAMA KUPATA STAHILI ZA KIKUNDI KIJAMII NA

KIKATIBA

Awe mwanachama hai kwa mujibu wa Katiba na Kanuni za Kikundi cha Ushirikiano

Dar es Salaam.

7.0 UTARATIBU WA KUSHIRIKI HARUSI/SENDOFF NA SHUGHULI ZINGINE ZA

JAMII.

7.1 Wanachama watashirikishwa katika harusi, kumuaga binti (Send off) katika makundi

yafuatayo:

7.1.1 Mwanachama Mwenyewe.

7.1.2 MAtoto wa kuzaliwa na Mwanachama au kwa mujibu wa sheria za nchi.

7.1.3 Taarifa zitatolewa kwa mujibu wa taratibu za kutoa taarifa, wanachama

watatakiwa kushiriki bila kukosa kwa makundi yaliyo kadri ya katiba.

Ushiriki utaratibiwa na kamati ya jamii.

7.2 Kwa mwanachama asiyeshiriki bila taarifa atatozwa faini na akifikisha matukio 3

mfululizo atafikishwa kwenye kamati ya maadili ili kuchukua hatua kwa kadri ya

kanuni za maadili.

7.3 Siku ya Harusi/ kumuaga binti (Send off) wanachama watashiriki kutoa zawadi

itakayoondaliwa kwa mujibu wa kanuni. Zawadi zitatolewa kama ifuatavyo; -

7.3.1 Mwanachama - Tshs. 500,000/=.

7.3.2 Mtoto wa kuzaliwa wa mwanachama - Tshs. 400,000/=.

13
7.3.3 Uwakirishi utatumika kwa shughuli yoyote itakayofanyika nje ya Dar es

salaam.

7.4 Michango ya wanachama katika kufanikisha mandalzi ya harusi /send off kadri ya

makundi yaliyoainishwa katika katiba kitakuwa kuanzia shilingi laki moja (100,000/=)

na kuendelea. Kiwango kitabadilika kadri itakavyoamuliwa na Mkutano Mkuu.

8. USHIRIKI WA WANACHAMA WALIO NJE YA DAR ES SALAAM /


TANZANIA NA NJE YA NCHI
Wanachama watapata huduma kama kawaida kwa mujibu wa katiba na kanuni mbalimbali.

9. SIKU YA USHIRIKIANO YA MWAKA.

9.1 Kama ilivyoanishwa hapo juu siku hii itaweza kuwakutanisha wanakikundi na

familia zao ili kuweza kufahamiana kwa kushiriki chakula, vinywaji, kucheza kwa

pamoja.

9.2 Utaratibu utaandaliwa na kamati ya jamii wakishirikiana na kamati yake ndogo

iliyo chini ya mwenyekiti wa jamii, na kuwashirikisha wanachama katika

maandalizi kila mwaka, siku hii itakuwa mara moja kwa mwaka. Kila familia

itatakiwa kushiriki katika michango, maandalizi na kuwepo kwenye shughuli hii.

9.3 Siku ya ushirikiano itapangwa mwanzoni mwa mwaka husika ili kamati ya jamii

ianze maandalizi.

14
10. MIIKO NA FAINI KATIKA SHUGHULI ZA KIJAMII.

Kwa mujibu wa kanuni na taratibu za jamii za ushirikiano, ifuatayo ni miiko na faini

zitakazo-tuongoza (neno moja) na zitakazo-tumika (neno moja) katika utelelezaji wa

kanuni na katiba ya ushirikiano;

10.1 Uchelewaji Vikao mbalimbali - Ili kuleta nidhamu katika kikundi

mwanachama ni mwiko kuchelewa vikao husika vilivyotolewa taarifa na

viongozi.

10.2 Adhabu (FAINI): Tshs. 2,000/= kwa kila mwanachama (mume au mke)

atakayechelewa kwenye vikao. Mwanachama atakaye kosa vikao 3 mfululizo

bila taarifa atatakiwa kutoa taarifa kwa maandishi kamati ya Jamii kama

haitaridhika nayo itapelekwa kamati ya maadili.

10.3 Kutohudhuria shughuli/Tukio - Ili kuleta ufanisi na nidhamu katika ushiriki

kwemye shughuli zote za jamii ni mwiko kutokuhudhuria bila taarifa maalumu.

10.4 Adhabu (FAINI): Tshs. 5,000/= kwa kila mwanachama (mume au mke)

asiyehudhuria kwenye shughuli/tukio bila taarifa. Mwanachama atakaye kosa

vikao 3 mfululizo bila taarifa atatakiwa kutoa taarifa kwa maandishi kamati ya

Jamii kama haitaridhika nayo itapelekwa kamati ya maadili.

10.5 Kutoa maneno ya uchochezi/uchonganishi/umbeya katika shughuli za jamii.

Ni mwiko kama ilivoonyeshwa kwenye taratibu za jamii.

10.6 Adhabu (FAINI): Kamati ya jamii itahitaji maelezo kwa maandishi juu ya

tukio/kitendo na baadaye itapeleka tukio la mwanachama husika kwenye

kamati ya Nidhamu kwa hatua husika kadri ya kanuni za maadili.

15
11. UDHURU

Kutakuwa na udhuru unaokubalika kutohudhuria shughuli za vikao ni kama ifuatavyo:

11.1. Udhuru wa kutohudhuria kikao/ vikao vya ushirikiano: -

11.1.1 Ugonjwa.

11.1.2 Kuwa safarini.

11.1.3 Kuuguza/ kuuguliwa.

11.1.4 Kupata msiba.

11.1.5 Uzazi, baada ya kujifungua ndani ya miezi mitatu.

11.2 Udhuru unatakiwa utolewe taarifa kwa mwenyekiti wa jamii, au kikundi siku moja

au mbili kabla ya kikao, na wala sio siku ya kikao.

11.3 Mwanachama aliyetoa udhuru unaokubalika hatalipa faini yoyote, isipokuwa tu

kama taarifa imeletwa kuomba udhuru usiokubalika ambao haukutajwa kwenye

kifungu hiki. Utalipa faini kama inavyosomeka kwenye kanuni hizi (kifungu cha

9.2).

11.4 Udhuru wa kuchelewa kufika kwenye kikao kutokana na dharura isiyotarajiwa.

11.5 Udhuru huu utakubalika tu kama utawasilihwa kwa mwenyekiti wa jamii kwa njia

ya simu, meseji, barua pepe au njia yoyote inayokubalika na kueleza dharura

iliyokupata ukiwa unakuja kwenye kikao. Vinginevyo utalipa faini iliyoainishwa

kwenye kanuni hizi (kifungu 9.1).

12. IDARA YA AKINA MAMA

Kutakuwa na idara ya akina mama itakayoitwa “UG Women”. Kila mwanamama aliyeko

kwenye kikundi cha ushirikiano ni mwana “UG Women”.

16
12.1 MALENGO YA IDARA YA AKINA MAMA (UG WOMEN GOALS)

12.1.1 Kusaidiana kwa kutoa huduma mbalimbali za kijamii zinazowahusu akina

mama na familia zao.

12.1.2 Kupeana pole na kupongezana wakati wa kujifungua, harusi, kuhitimu

masomo na kumuaga binti (send off).

12.1.3 Kununua vifaa vya kutumika kwenye shughuli za kijamii kama vyombo vya

kupikia kwa ajili ya kurahisisha kutoa huduma lengwa.

11.1.4 Kuwa na mfuko wa jiko ambao unaweza kutoa mahitaj muhimu ya kuanzia

kwa familia ya mwanachama katika hali ya dharura kama misiba.

11.1.5 Na huduma zingine zinazokubalika kwa idara ya akina mama.

12.2 WAJIBU WA KILA MWANAMAMA NDANI YA IDARA HII.

12.2.1 Kuhudhuria vikao vyote vinavyoitishwa na uongozi wake.

12.2.2 Kulipa michango kila mwezi wa shilingi 5000 (Kiwango hiki kinaweza

kurekebishwa kulingana na thamani na mahitaji ya fedha).

12.2.3 Utunzaji wa fedha za idara hii zitawekwa kwenye akaunti ya ushirikiano na

zitafuata kanuni za fedha za ushirikiano.

12.2.4 Kushiriki katika shughuli za matukio ya kifamilia kwa mwanachama, kama

vile kwenda kutoa pole na hongera kwa mwanamama aliyejifungua,

anayeuguliwa na mtoto, muma au ndugu anayeishi naye na ugonjwa na

zingine zilizoorodheshwa kwenye kifungu cha 11.1.2 hapo juu.

12.2.5 Mwanamama asiyelipa michango yake mfululizo kwa miezi mitatu atakuwa

amekosa haki ya kupata huduma zilizoainishwa kwenye kifungu 11.1.

17
12.2.6 Mwanamama huyo atatolewa taarifa na Mwenyekiti au katibu wa UG

Women kwa mwenyekiti wa Kamati ya Jamii ili aandikiwe barua

kumkumbusha alipe michango yake anayodaiwa kwa lengo la kwenda

sambamba na wenzake katika kufanikisha malengo yaliyowekwa.

12.2.7 Asipolipa madeni ya michango yake kanuni za maadili za Ushirikiano

zitafanya kazi.

12.2.8 Matatizo yote ya idara ya akina mama yatatatuliwa na uongozi wa ‘’UG

Women’’ na kama bado hayajapata ufumbuzi yatapelekwa kwa mwenyekiti

wa kamati ya jamii.

12.3 VIONGOZI WA IDARA YA AKINA MAMA

12.3.1 Idara hii itakuwa na viongozi wafuatao: -

12.3.1 Mwenyekiti.

12.3.2 Katibu

12.3.3 Mweka hazina

12.3.2 Viongozi hawa watahudumu kwa kipindi cha miaka mitatu, na uchaguzi utafanyika

kuchagua viongozi wapya.

12.3.3 Uongozi wa idara ya akina mama utakwenda sambamba na mabadiliko ya uongozi

wa kikundi cha ushirikiano.

12.4 MNUFAIKA WA IDARA YA UMOJA WA AKINA MAMA

Ni familia ya mwana mama wa UG ikijumuisha watu anaoishi nao kama: -

11.4.1 Mume.

11.4.2 Watoto.

18
11.4.3 Ndugu anaokaa nao.

11.4.4 Wakwe (wazazi) wa wanandoa kwenye familia.

12.5 MAWASILIANO KWA AKINA MAMA

Taarifa zote zitatolewa kupitia mtandao wa kundi la whatsup la akina Mama lijulikanalo kama

“UG Women”, kupiga simu ama kuandika ujumbe mfupi wa maandishi (sms) au kwa kutumia njia

yoyote watakayoona inafaa kwa mwenyekiti au katibu.

13.0 VIKAO VYA SEKRETERIETI.

13.1 Sekretarieti ni baraza la viongozi wakuu wa kikundi cha ushirikiano, lina jukumu la

kutathmini na kuleta mapendekezo na mipango inayopelekea utekelezaji wa katiba,

kanuni na maamuzi mengine halali yaliyoamuliwa mkwenye vikao halali vya chama.

13.2 Sekretarieti ya kikundi cha Ushirikiano imeundwa na wenyeviti wote wa kamati wa

kikundi cha ushirikiano ambao ndiyo wajumbe wake ikijumuisha katibu na mwenyekiti

wa kikundi cha ushirikiano.

13.3 Mwenyekiti wa kikundi ataongoza vikao vya sekretarieti na katiba atachukua

kumbukumbu zote za vikao.

13.4 Vikao vya kawaida vya sekretarieti vitafanyika mara mbili kwa mwaka, yaani mara moja

kila miezi sita, isipokuwa ikitokea dharura vikao hivi vitaitishwa wakati wowote na

katibu wa kikundi kujadili jambo husika.

13.5 Posho ya chakula na maji ya shs 50,000/= (Elfu hamsini tu) itatolewe kwenye kikao cha

sekreterieti kama huduma kwa wajumbe ili kuwawezesha kutimiza majukumu yao.

19
14.0 MABADILIKO YA KANUNI ZA KAMATI YA JAMII

Kanuni za jamii zinaweza kubadilika kadiri ya mahitaji ya wanachama itavyoelekezwa.

15.0 MUDA WA KUANZA KUTUMIKA KANUNI HIZI

Kanuni hizi na mabadiliko yake zimeanza kutumika mara baada ya kupitishwa na

Mkutano wa wanachama wote kwa mujibu wa Katiba tarehe 26 Julai 2020

BI. HELLEN KIHEKA BW. SAMSON MANDA JEREMIAH

Katibu Kamati ya Jamii Mwenyekiti Kamati ya Jamii

BW. JOHN ATANAS MLYABOPE

Mwenyekiti Kikundi cha Ushirikiano.

TAREHE: 26/07/2020

20

You might also like