You are on page 1of 17

KIKUNDI CHA MUUNGANO MBAGALA

" A"

KATIBA

YA

KIKUNDI

(MUUNGANO MBAGALA "A")

2022@
FOUTH DRAFT
YALIYOMO

1. SEHEMU YA KWANZA..........................................................................................................4

1.1 TAARIFA YA KIKUNDI.................................................................................................................4

1.2 UFAFANUZI WA MANENO...........................................................................................................4

2. SEHEMU YAPILI.....................................................................................................................5

2.1 MADHUMU NI YA KIKUNDI........................................................................................................5

3. SEHEMU YA TATU.................................................................................................................5

3.1 UANAKIKUNDI..............................................................................................................................5

3.1.1 Sifa za kuwa Mwanakikundi...........................................................................................................5

3.1.2 Haki za Mwanakikundi...................................................................................................................6

3.1.3 Wajibu wa Mwanakikundi kwa Kikundi........................................................................................6

3.1.4 Maadili ya Mwanakikundi..............................................................................................................7

3.1.5 Ukomo wa Uanakikundi.................................................................................................................7

4. SEHEMU YA NNE....................................................................................................................8

4.1 Michango...........................................................................................................................................8

4.1.1 Mchango wa Kiingilio....................................................................................................................8

4.1.2 Michango(Ada) ya kila mwezi........................................................................................................8

4.1.2Michango Mingine..........................................................................................................................8

4.2.Faini(Penalty) na Adhabu Nyingine ..................................................................................................8

4.3Kuhifadhi Fedha na Akiba za Kikundi ...............................................................................................9

5. SEHEMUYATANO.................................................................................................................10

5.1 Vyanzo vya Fedha...........................................................................................................................10

6. SEHEMU YA SITA.................................................................................................................11

6.1 Mikutano ya Kikundi.......................................................................................................................11

6.1.1 Mkutano Mkuu wa Wanakikundi.................................................................................................11


6.1.2 Mkutano wa Kawaida wa kila mwezi ..........................................................................................11

6.1.3 Mkutano Mkuu wa Dharura ..................................................................................................11

6.1.4 Mkutano Maalum wa Uchaguzi ............................................................................................11

6.2 Utoajiwa Taarifa za Mikutano au Vikao ...................................................................................12

6.3 UongoziwaKikundi..........................................................................................................................12

6.3.1 Mfumo wa Uongoziwa (KamatiKuu) ya kikundi .........................................................................12

6.3.2 Wajibu na kazi za viongozi wa kikundi .......................................................................................12

6.3.3 Muda wa Uongozi wa Kikundi ....................................................................................................13

6.3.4 Kusitishwa kwa Uongozi.......................................................................................................13

7. SEHEMUYASABA.................................................................................................................14

7.1 Kamati za Kikundi Kikundi.......................................................................................................14

7.1.1 KamatiTe.8.nkdaji.................................................................................................................14

7.1.2 Kamati ya Nidhamu na Maadili ............................................................................................14

7.1.3 KamatiyaFedhanaMikopo......................................................................................................14

8. SEHEMU YA NANE ..............................................................................................................16

8.1 Utaratibu wa Kutoa Maoni/Mapendekezo.......................................................................................16

8.2 Utatuaji wa Migogoro au Malalamiko ............................................................................................16

8.3 Mialiko ya Kikundi .........................................................................................................................16

8.4 Marekebisho/ Mabadiliko ya Katiba ...............................................................................................16

9. SEHEMU YA TISA ................................................................................................................17

9.1 Kufutwa kwa Kikundi ....................................................................................................................17

9.2 Kuthibitishwa na Kusainiwa ...........................................................................................................17


1. SEHEMU YA KWANZA

1.1 TAARIFAYA KIKUNDI:


(a) Jina la kikundi litakuwa:Muungano Mbagala A
yaani kikundi kamili kwa watu waishio ndani ya Tanzania
(b) Anuaniya Kikundi: S.L.P 19,Igunga
(c) Tarehe ya kuandikishwa:……………..
(d) Nambari ya kuandikishwa: ……………
(e) Wanakikundi waanzilishi:……………..
(f) Eneo la shughuli za Kikundi litakuwa:Ndani ya jamhuri ya muungano wa Tanzania
(g) Makao makuu ya kikundi yatakuwa:Dar es salaam
(h) Lugha rasmi ya kuendesha shughuli za kikundi itakuwa:Kiswahili au Kiingereza

1.2 UFAFANUZI WA MANENO:


Maneno yafuatayo yanapotumika katika masharti haya yatakuwa na maana kama inavyoelezwa
hapana chini:-
(a) “Kikundi”lina maana ya Kikundi cha Kinachopatikana Kitongoji cha Nkokoto Mtaa wq Mbagala
A
(b) “Mwanakikundi”ni mtu yeyote aliyejiunga na kikundi na anayeshiriki kikamilifu kutimiza
kanuni na taratibu za kikundi.
(c) ”Viongozi”ni wanakikundi waliochaguliwa au kuteuliwa kwa mujibu wa katiba hii au
kanunizakikundi,kusimamia mali au uendeshaji wa shughuli zote za kikundi
(d) “Mtoto”ni mtu mwenyeumrichini yamiaka18.
(e) “Kitega uchumi ”(Investment) ni uwekezaji wenye kuleta tija kwa kikundi
(f) “Kanuni”za kikundi ni taratibu zote zilizopitishwa na wanakikundi kutumika kwenye kikundi
katika kuitekeleza katiba hii na kufanikisha madhumuni/malengo ya kikundi.
(g) “Ndani ya Tanzainia” Ndani ya nchi ni mipaka ambayo kijiografia inahusisha maeneo
yotendani ya jamhuri ya muungana na nje ya nchi itamaanisha maeneo yote yasiyokuwa
yaTanzania
(h) “Mkutano halali ”ni kikao chochote au mkutano wowote wa wanachama ulioitishwa
kulingana na katiba hii au kanuni za kikundi na uliofanywa kwa utaratibu uliowekwa.
2. SEHEMU YA PILI

2.1 DHUMUNI KUU KIKUNDI


a. Kushirikiana kijamii na kiuchumi

Malengo mahususi:
(a) Kushirikiana na kusaidiana wakati wa shida naraha.nk
(b) Kuwezesha wanakikundi kuimarishana kiuchumi na hali ya maisha kwa:-
i. Kupokea na kuweka michango ya fedha za wanakikundi
ii. Kuanzisha na kuendeleza shughuli zozote halali za kiuchumi kwa manufaa ya
wanakikundi kama itakavyokubaliwa katika Mkutano halali wa wanakikundi
iii. Kuwezesha kifedha shughuli binafsi za wanakikundi kwa masharti yaliyokubaliwa na
wanakikundi
iv. Kuhamasisha ushirikiano na wanakikundi wenye changamoto mbalimbali kama
ulemavu,uzee,uyatima,uathirika wa ukimwi na watoto wa mitaani.

3. SEHEMU YA TATU

3.1 UANAKIKUNDI

3.1.1 Sifa za kuwa Mwanakikundi


(a) Awe raia waTanzania.
(b) Awe ni mtu mwenye akili timamu na wakuaminika.
(c) Awe anayefanya kazi iliyo rasmi ama isiyo rasmi au shughuli zinazokubalika kisheria
(d) Awe ametimiza umri wa miaka18.
(e) Awe ni mtu aliye tayari kuiheshimu,kuitetea na kuongozwa kwa katiba yakikundi na
kanuni zake
(f) Awe ametimiza taratibu zote za kujiungana kikundi %:
i. Kujaza fomu ya maombi na kukubaliwa na uongozi kisha kupitishwa na
mkutanomkuukuwamwanachama.
ii. Kulipa kiingilio kama inavyoonyeshwa katika kanuni za kikundi, au kama
itakavyoamuliwanaMkutanohalaliwa kikundi.
iii. Ili kuondoa tofauti ya michango kati ya mwanakikundi ambaye yupo na yule
anayetaka kujiunga ,wanakikundi watakubaliana kiasi cha fedha atakachotakiwa
kuchangia mtu anayetaka kijiunga na muda wa kukamilisha mchango huo.
3.1.2 Haki za Mwanakikundi
Mwanakikundi atakuwa na haki zifuatazo:-

1. Kutumiana kupata huduma zote za kikundi bila ubaguzi.


2. Kupokea taarifa za kikundi,kuona
3. taarifa au kumbukumbu za kikundi kwa utaratibu unaokubalika
4. Kuchagua (yaani kupiga kura)na kuchaguliwa(yaani kupigiwa kura) kwenye nafasi
yoyote katika kikundi
5. Haki ya kura moja kwa kila mwanakikundi bila kujali kiasi cha michango aliyoweka
kwenye kikundi kikundi.
6. Haki ya kujitetea dhidi ya jambo lolote litakalomkabili katika uhusiano wake na
wanakikundi wengine.

7. Haki ya kutoa hoja yoyote inayohusu mwenendo wa wanakikundi ndani ya mikutano ya


kikundi

8. Haki ya kujitoa kwa hiari kwenye kikundi

3.1.3 Wajibu wa Mwanakikundi kwa Kikundi


Mwanakikundiatakuwanawajibuufuataokwakikundi:-

1. Kuchangia fedha kila mwezi (ada) namichango


mingineyoyotekamaitakavyoanishwakwenye kanun5þiauiliyopendekezwa
nakuidhinishwana wanakikundi

2. Kuhudhuriana kushiriki katika mikutano yote halali ya kikundi.

3. Kuwa mtu Mwaminifu,Mwaadilifu,na Mwenye Kujitolea kwaajili ya kikundi


4. Kufuata kanuni,sheria na masharti ya kikundi yaliyokubaliwa

5. Kutii na kufuata maazimio yote ya Mkutano wowote halali hata ikiwa hakuwepo kwenye
mkutano huo,au kutoshiriki katika kupitisha azimio hilo

6. Kueneza sifa nzuri za kikundi

7. Kuwa na nidhamu wakati wa vikao au mkutano

8. Kushiriki kikamilifu kubuni miradi ya kuendeleza na kuimarisha kikundi

9. Kutunza siri zote za kikundi

3.1.4 Maadili ya Mwanakikundi


Kila mwanakikundi atapaswa kufuata maadili yafuatayo:
(a) Kupendana na kuheshimiana
(b) Kukubali kukosolewa endapo maadili yamekiukwa
(c) Mwanakikundi haruhusiwi kupokea wala kutoa rushwa
(d) Kuepuka dharau,kiburi,chuki na hasira
(e) Kutoshiriki mikutano yoyote itakayofanyika kinyume na katiba na kanuni za kikundi
(f) Mwanakikundi anapokwenda kinyume na maadili ya kikundi ataonywa mara ya kwanza
kwa mdomo,tatu kwa maandishi na Kamati tendaji; asipobadilika kipengele cha
kumwachisha uwanakikundi kitatumika

3.1.5 Ukomo wa Uanakikundi


(a) Kifo
(b)Kushindwa kuchangia michango ya kila mwezi kwa muda wa miezi mitatu (3)
mfululizokwasababuzozote zilebila taarifa ya mdomo au kwamaandishi
(c) Mwanakikundi kujiuzulu au kuomba kuacha uanakikundi yeye mwenyewe kwa sababu
zozote zile
(d)Kutoa au kupokea rushwa kwa viongozi au mwanakikundi yeyote
(e) Kuachishwa uanakikundi kwa azimio litakaloungwa mkonona Wanakikundi
wasiopungua theluthi mbili (2/3)ya Wanakikundi waliohudhuria katika Mkutano halali
(f) Kushiriki katika kuiba au kuhujumu mali za kikundi(ikiwani pamoja na fedha)
(g)Mtu aliyeacha au kufukuzwa uanakikundi anaweza kuomba kujiunga tena kwa mujibu
wa masharti ya uanakikundi kama yalivyo lakini atatakiwa kuwa na wadhamini wawili
(2)ambao ni wanakikundi hai.
4. SEHEMU YA NNE

4.1 Michango

4.1.1 Mchango wa Kiingilio


(a) Mwanakikundi mwanzilishi anawajibika
kulipakiingiliochashilingilakimoja(Tshs100,000)kablayatarehe31/01/2015.
(b) Mwanakikundiatakeyejiungabaadayatarehe31/01/2015hatakuwamwanzilishinaatatakiwa
kulipamchangokulingananakanunizakikundi.
(b) Mtu aliyejiungana kikundi atastahili haki za Mwanakikundi pale atakapokuwa
amelipamchangowakiingilio.
(c) KilaatakayejiunganaKikundiatapatiwafomuyausajiliambayoitaonyeshakiasianachotakiwa
kulipa kuwa Mwanakikundi, kiasi alicholipa na utaratibu wa kukamilisha kiasikilichobaki.

4.1.2 Michango(Ada) ya kila mwezi


(a) Mwanakikundi atatakiwa kulipa kwa wakati kiasi kilichopitishwa kama ada ya kila
mwezikamailivyoainishwa katika kanunina taratibuza kikundi.

(b) Endapo mwanakikundi atachelewa kulipa kiasi hicho, au asipolipa kabisa, utaratibu wa
faini(penalty)naadhabu nyinginezilizokubaliwa katikakanuniza kikundizitatumika.

(c) Mtunza fedha wa kikundi atatoa taarifa sahihi za michangoyote iliyokusanywa siku
yamkutano akionyesha wale waliolipa, wanaodaiwa, aina ya michango iliyokusanywa na
habari nyingine inayofaa kadiriyautaratibuwahesabuza fedha.

4.1.3 Michango Mingine


(a) Kikundi kitakuwa na michango mingine kadiri itakavyopitishwa katika kanuni,ikiwa ni
pamoja na michango ya msiba,harusi,ugonjwa au matukio mengine.

(b) Kila mwanakikundi atatakiwa kulipa kiasi cha fedha kilichopitishwa kwa wakati sahihi, na
kwa utaratibu utakaowekwa na wanakikundi.

.
4.3 Kuhifadhi Fedha na Akiba za Kikundi
(a) Fedha za Kikundi zitahifadhiwa katika taasisi HALALI za kifedha Kama vile Benki au
kuwekezwa katika rasilimaliinayotoa faida kwa kikundi.
(b) Fedha yote ya kikundi itahifadhiwa katika taasisi za kifedha kama vile Benki.Hata hivyo,
Uongozi unaweza kutenga kiasi kidogo (Pettycash) ilikukidhi matumizi madogo mdogo
(c) Fedha za kikundi zilizokusanywa zaweza kutumika kuwasaidia wanakikundi kukabiliana
na dharura au hali za maisha kwa njia ya mkopo kwa utaratibu ulioainishwa kwenye kanuni
zakikundi.

4.4 Kutoa Fedha na Akiba za Kikundi


(a) Fedha za kikundi zinaweza kutolewa wakati wowote kulingana na
mahitaji yatakayopendekezwa na wanakikundi.
(b) Malipo yatafanyika kwa njia ya hundi au taslim(cash) baada yakukamilika kwa utaratibu
wa utoaji wa fedha za kikundi

4.4.1Mgongano wa kimaslahi katika kusaini.

Bila kuathiri matakwa ya kuidhinisha malipo, iwapo watajwa katika ibara 4.4(c) (i) na
(ii)watakuwa na mgongano wa kimaslahi aidha ya kindugu ama kwa namna yeyote
ilebasinilazimaikaepukwa kwamaslahiyakikundi.
5. SEHEMU YA TANO

5.1 Vyanzo vya Fedha


i. Fedha ya kiingilio anayotoa kila mwanakikundi wakati anapojiunga.

ii. Vitega uchumi mbalimbali(Investments),mashamba,Viwanja,biashara nk.


iii. Mikopo kutoka vyombo vya fedha au chombo kingine chochote baada ya kupata idhini ya
wanakikundi kwa idadi ya theluthi mbili ya wanachama au Zaidi.
iv. Misaada au Ufadhili kutoka sehemu mbalimbali.
v. Chanzo kingine chochote halali kwa mujibu wa sheria za nchi na katiba ya kikundi.

5.2 SEHEMU YA SITA

6.1 Mikutano ya Kikundi

6.1.1 Mkutano Mkuu wa Wanakikundi


(a) MkutanoMkuu waWanakikundi utaitishwa na mwenyekiti na utafanyika kila baada ya
miezi mitatu
(b) Uhalali wa mkutano au kikao chochote cha kikundi ni mahudhurio ya wanakikundi kuwa
zaidi ya nusu ya idadi yote.
(c) Mambo yafuatayo lazima yajadiliwe katika Mkutano Mkuu wa mwaka:-
i. Kusoma nakuthibitisha muhutasariwa mkutano uliopita.
ii. Kupokea na kujadili taarifa ya mwaka ya mapato na matumizi namatumizi.
iii. Kupokeanakujadilitaarifazamaendeleoyakikundikutokakwenyekamatimbalimbaliz
akikundi
iv. Kuidhinisha makisio ya mapato na matumizi ya mwaka unaofuata
v. Kuzungumzia mikakati inayohusu maendeleo ya Kikundi kwa jumla na kutoa
maelekezo ya utekelezaji kwa watendaji wa kikundi.

6.1.2 Mkutano wa Kawaida ni kila baada ya miezi miwili


(a) UtafanyikakilaJumapiliyakwanzayamwezi
(b) Utapokeataarifambalimbalizauendeshajiwakikundizakilamwezi
(c) Utapokeamaoni/mapendekezoyamipangoyamaendeleo yakikundi
(d) KuthibitishakuingizwanakufukuzwakwaWanakikundi
(e) Kupokeawanakikundiwapyakamawapo

6.1.3 Mkutano Mkuu WaDharura


(a) Mwenyekiti,Katibu wanakikundi kwa idadi isiyopungua theluthi mbili
ataitisha/wataitisha Mkutano Mkuu wa Dharura kwa jambo la dharura linalohusu
kikundi kama vile Msiba, Ugonjwa, Kuibiwa mali za Kikundi na yanayofanana na hayo.

(b) Mkutano wa Dharura unaweza kuendeshwa na idadi isiyopungua roto tatu ya wanakikundi.
6.1.4 Mkutano Maalumu wa Uchaguzi
(a) Mkutano utakuwa ni maalumu kwa ajili ya uchaguzi wa viongozi wa kikundi baada
ya viongozi waliopo madarakani kumaliza kipindi chao cha uongozi

(b) Ikiwa kiongozi yeyote atasitishwa uongozi kama inavyoelezwa katika kipengele
cha 6.3.4,utaitishwa mkutano maalum wa uchaguzikwa nafasi yake.
6.2 Utoaji wa Taarifa za Mikutano au Vikao.
(a) Taarifa za mkutano zitatolewa kwa wanakikundi wote kwa kutumia taratibu
zinazokubalika.Taarifa hii itabidi ionyeshe waziwazi tarehe ya Mkutano,Idadi ya
wanakikundi waliohudhuria,muda,mahali pa mkutano na dhumuni la mkutano.
(b) Taarifayoyote ya dharura inayohusu kikundi itatakiwa kufikishwa kwa uongozi kwanza na
uongozi utatoa utaratibu wakuwafahamisha wanakikundi wote na taratibu nyingine.

6.3 Uongozi wa kikundi


Kutakuwa na mfumo rasmi wa kisheria katika uongozi ambao ni Kamati Kuu,Kamati tendaji za
kudumu/Muda kama itakavyoonekana inafaa.

6.3.1 Mfumo wa Uongozi (Kamati Kuu) wa kikundi

(a) UongoziwaKikundiutakuwana watu watano:

i. Mwenyekiti
ii. Katibu
iii. Mweka Hazina (Mhasibu)

(b) Mwenyekiti wa kikundi

i. Atakuwa ni msemaji mkuu wa kikundi


ii. Ni kiongozi/msimamizi wa shughuli zote zakikundi
iii. Atahakikisha kikundi kinaimarika na kusimamia katiba kikamilifu
iv. Ni mwenyekiti wa vikao vyote vya kikundi

(c) Katibu wa kikundi

i. Ni Katibu Mtendaji Mkuu wa kikundi


ii. Ni mwandishi na mwekaji wa kumbukumbu za vikao vyote vya kikundi
iii. Ni mtayarishaji wa taratibu zote za vikao vya kikundi kwa kushirikiana
namwenyekiti
iv. Mfuatiliaji wa maazimio na mipango ya kikundi.
v. Mwandishi mkuu wa barua au taarifa nyingine zinazokihusu kikundi.
(d) Mweka Hazina wa Kikundi
i. Mtunzaji fedha na taarifa zote za fedha za kikundi
ii. Ni mtoaji wa taarifa zote zihusuzo mapato na matumizi ya kikundi
iii. Ni mtengenezaji/muandaaji wa bajeti ya kikundi
iv. Kufuatilia na kuwakumbusha wanakikundi kuhusu madeni yao kwa barua,simu na/au
barua pepe
v. Kutoa taarifa ya mapato na matumizi ya kikundi wakati wowote inapohitajika
vi. Kutoa taarifa za dharura zitakazohusu mfuko wa kikundi.

6.3.2 Muda wa Uongozi wa Kikundi


(a) Muda wa uongozi katika kikundi utakuwa ni miaka miwili(2)
(b)Viongozi waliomaliza muda wao wanaweza kuchaguliwa tena lakini wasiwe
wamekalia nafasi hiyo hiyo kwa zaidi ya vipindi vitatu mfululizo.

6.3.3 Kusitishwa kwa Uongozi


(a) Uongozi/Kiongozi unaweza/anaweza kusitishwa wakati wowote kabla ya muda wa
uongozi kuisha iwapo:

i. Uanakikundi wake umefikia ukomo (angalia kipengele 3.1.5 Ukomo


waUanakikundi)

ii. Kumekuwa na kutokuwajibika ipasavyo kuleta maendeleo ya kikundi kwa mujibu


wa katiba ya kikundi

iii. Wanachama watakosa imani nao/naye kwa idadi ya thelulthi mbili ya


wanachama wote.

iv. Ataamua kujiuzulu kwa ridhaa yake mwenyewe kwa maslahi ya kikundi; na
zaidi ya nusu ya wanakikundi wamekubaliana na ombi lake la kujiuzulu

(b)Kiongozi aliyesitishwa kuongoza atawajibika kukabidhi mali na taarifa sahihi kwa


kikundi(au kiongozi mwingine aliyechaguliwa) kwa utaratibu ulioanishwa kwenye
kanuni za kikundi.
6. SEHEMU YA SABA

7.1Kamati za Kikundi
(a) Kikundi kitakuwa na kamati za kudumu zitakazosaidiana na Kamati Kuu kufanikisha
mipangonashughulizakikundi

(b) Kamati nyingine zozote za Muda zinaweza kuundwa katika mikutano ya kawaida ya
mwezi kulingana na matukio au umuhimu wa kuwepo kamati hizo.

7.1.1 Kamati Tendaji


(a) Itakuwa na viongozi wakuu watatu wa kikundi (kifungu6.3.1(a) pamoja na wenyeviti wote
wa kamati mbalimbali zilizoundwa kwa mujibu wa katiba au kanuni za kikundi.

(b) Kamati tendaji itakuwa na kazi zifuatazo:

i. Kupitia na kujadili mapato na matumizi ya kikundi kabla ya kufikishwa kwenye


Mkutano Mkuu wa Wanakikundi

ii. Kujadili na kupitisha maombi ya wanakikundi wapya watakaoomba kujiunga na


kikundi

iii. Kusimamia utendaji na utekelezaji wa mipango na shughuli za kikundi.

iv. Kusimamia masuala yote ya katiba na kanuni za kuendesha kikundi.

7.1.2 Kamati ya Nidhamu na Maadili


(a) Watachaguliwa na wanakikundi wasipungua wawili ya wanachama katika uchaguzi mkuu
wa kikundi.

(b) Itakuwa na watu wasiopungua watano .

(c) Itakuwa na jukumu la kushughulikia masuala ya nidhamu na maadili ya kikundi kwa


viongozi na wanakikundi wa kawaida

SEHEMU YA NANE

8.1 Utaratibu wa Kutoa Maoni/Mapendekezo


(a) Maoni , Mapendekezo au Malalamiko yoyote kwa mwanakikundi/wanakikundi yatatolewa
kwa maandishi au kwa kusema kwa viongozi au mwanakikundi kwenye kikao halali cha
wanakikundi

(b) Ikiwa jambo husika linahitaji maamuzi ya wanakikundi wote, Kamati Tendaji itawasilisha
mapendekezo yao kwenye mkutano wa wanakikundi wote kwa uamuzi wa mwisho.

8.2 Utatuaji wa Migogoro au Malalamiko


(a) Migogoro au malalamiko yoyote yanayohusu kikundi au wanakikundi yatatatuliwa kwanza
na wahusika kwa njia ya udugu (majadiliano na maelewano) kwa msaada wa uongozi wa
kikundi

(b) Ikiwa njia ya kwanza itashindikana, msaada wa mahakama na taratibu za kisheria


zinawezakufuatwa.

8.3 Mialiko ya Kikundi


(a) Kikundi kitakuwa nafursa na uwezowa kutuma mialiko kwenye vikundi vingine kwa lengo
la kushirikishana uzoefu, mawazo, michezo, huduma, shughuli za kiuchumi, kijamii na
mengineyo yenye maslahi kwa kikundi.

(b) Utaratibu wa mialiko itakuwa kama ulivyopitishwa katika kanuni za kikundi

8.4 Marekebisho/Mabadiliko ya Katiba


(a) Mapendekezo ya Mabadiliko ya Katiba ni lazima yajadiliwe katika Mkutano Mkuu na
yaidhinishwe walao na robo tatu(75%)ya wanakikundi wote

(b) Mapendekezo yoyote ya katiba yanayotakiwa kujadiliwa yatakusanywa na Kamati


tendajikatika kipindi chote cha mwaka, kwa ajili ya kuidhinishwa/kutoidhinishwa na
wanakikundi siku ya Mkutano Mkuu wa Mwaka.
7. SEHEMU YA TISA

9.1 Kufutwa kwa Kikundi


(a) Kikundi hiki kitafunga kabisa shughuli zake kwa sababu za msingi zitakazokubalika na
zaidi ya nusu ya robotatu(75%)ya wanakikundi wote katika Mkutano Mkuu.

(b) Endapo Kikundi hiki kitavunjwa,Mali zote za kikundi zitafilisiwa ili kulipia madeni
yatakayokuwa yanakikabili kikundi hadi wakati huo

(c) Fedha zitazobakia baada ya kulipa madeni,zitagawanywa kwa wanakikundi wote kulingana
na muda na kiasi cha michango ya kila mmoja.

(d) Endapo fedha zilizopo hazitoshi kulipa deni,salio la deni litagawanywa kwa utaratibu sawa
na wakipengele9.1(c)hapo juu.

(e) Usimamizi wa zoezilaufilisiutafanywachiniyaMahakama

9.2 Kuthibitishwa na Kusainiwa


Katiba hiiimethibitishwanakupitishwanawaanzilishiwotewakikundiambaoni:

Na. J C Namba ya Mawasiliano Sahihi


i he Kitambulisho
n o cha Taifa
a
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32

MWISHO.

You might also like