You are on page 1of 7

YALIYOMO

1. UTANGULIZI

2. MADHUMUNI

3. SIFA ZA KUWA KATIKA UMOJA

4. UONGOZI

5. UENDESHAJI WA VIKAO

6. VYANZO VYA MAPATO

7. WANUFAIKA WA MAFAO

8. MAFAO YANAYOTOLEWA

9. MAMBO YATAKAYOTENGUA KUTOKUNUFAIKA KWA

MWANACHAMA

10. MWISHO

i.
1. UTANGULIZI
Ukoo wa MWAMBA ambao shina lake lipo Mtandi-Kilwa,
limeunda umoja huu ukihusisha wanaukoo wote ambao
wapo ndani ya nchi (Tanzania) na nje ya nchi.
Umoja huu sio wa kichama au wakidini bali ni umoja wa
watoto waliozaliwa na Abdallah Bi Halfani au mjukuu au
mtu yoyote mwenye nasaba ya Bi Halfani.
Umoja huu unaongozwa na katiba pamoja na sheria
ambazo zimewekwa na kukubaliana kwa pamoja. Hivyo
yeyote ambaye yupo ndani ya umoja huu hana budi kufuata
katiba hii ambayo ndio mwongozo wetu.

2. MADHUMUNI
a) Kujuana na kufahamiana kwa wanaukoo kwa sababu
watu wanaishi maeneo mbalimbali.
b) Kushirikiana na kusaidiana katika mambo mbalimbali
ya kijamii.

3. SIFA ZA KUWA KATIKA UMOJA


a) Awe mtoto aliyezaliwa na Abdallah Bi Halfani au mjukuu
na mtu yeyote mwenye nasaba ya Bi Halfani.
b) Mke/Mume atakuwa katika umoja huu kupitia mwenza
wake.
c) Awe amalipa pesa ya kiingilio iliyokubaliwa katika
umoja. (Tshs. 10,000/=).
d) Awe analipa ada ya mwezi (Tshs. 3,000/=) iliyokubaliwa
katika umoja.

1|Page
4. UONGOZI
4:1 MUUNDO WA UONGOZI

MWENYEKITI

MAKAMU
MWENYEKITI

KATIBU MKUU

KATIBU MSAIDIZI

MTUNZA FEDHA

KAMATI YA
UTENDAJI

KAMATI YA
MAADILI

2|Page
4:2 SIFA ZA VIONGOZI
a) Mwenyekiti, Makamu, Katibu wawe na elimu ya darasa la
saba na kuendelea na wawe wanajua kusoma na kuandika
vizuri.
b) Mweka hazina awe na elimu ya darasa la saba na
kuendelea na awe anajua vizuri somo la hisabati.
c) Kamati tendaji wawe ni watu wa kuwajibika bila
kusukumwa na wenye ushirikiano na viongozi wa juu.
d) Kamati ya maadili wawe watu wenye siri na hekima katika
maamuzi.

4:3 MAJUKUMU YA VIONGOZI


A. MWENYEKITI
i. Yeye ni msimamizi na muangalizi wa shughuli zote
za umoja.
ii. Kuitisha na kusimamia vikao
iii. Kutoa na kupokea mapendekezo ya umoja.
iv. Kulinda na kutetea haki za wanakikundi.

B. MAKAMU MWENYEKITI
i. Atasimamia shuguli za Mwenyekiti kama hayupo.
ii. Atakuwa ni mshauri wa Mwenyekiti.
iii. Atashika nafasi ya Mwenyekiti iwapo hayupo au
amejiuzulu.
4:4 KATIBU MKUU
i. Atakuwa msemaji mkuu wa ukoo.
ii. Ataitisha mikutano kwa kushauriana na Mwenyekiti.
iii. Atawasilisha kumbukumbu katika vikao.
iv. Ataratibu mipango yote ya ukoo.
v. Atasimamia katiba na kuilinda.
4:5 MAKAMU KATIBU MKUU
i. Atafanya kazi ya katibu mkuu kama hayupo.

3|Page
4:6 MTUNZA FEDHA
i. Atatunza fedha kwa kanuni za uhasibu.
ii. Atasimamia makusanyo na michango ya ukoo.
iii. Atatoa taarifa ya fedha kwa wanaukoo kila mwezi na
katika mkutano wa mwisho wa mwaka.
4:7 KAMATI YA UTENDAJI
i. Kuhamasisha na kuelimisha wanafamilia na ukoo
kufuata sheria na kanuni za katiba yetu.
ii. Kutoa taarifa au jambo lolote litakalojitokeza ndani ya
familia kwa viongozi wakuu.
4:8 KAMATI YA MAADILI
i. Itakuwa na wajumbe wanne ambao watachaguliwa
katika mkutano mkuu.
ii. Katibu na Mwenyekiti wa ukoo wataingia katika
kamati ya maadili kutokana na nafasi zao.
4:9 NAMNA YA KUWAPATA VIONGOZI
Viongozi wanaweza kupatikana kwa kupendekezwa au
kuteuliwa au kupigiwa kura inategemea makubalaino ya
wanaukoo katika mkutano mkuu.
4:10 MAMBO YATAKAYO MUONDOA KIONGOZI
MADARAKANI
i. Kiongozi yeyote anaweza kuondolewa madarakani
endapo atabainika na kosa la kuvunja katiba na
maamuzi yakapitishwa katika mkutano mkuu.
ii. Kwaridhaa yake mwenyewe akiamua kujihudhuru.
5:0 UENDESHAJI WA VIKAO
a. Tutakuwa na kikao kikuu kimoja ambacho kitafanyika
mwisho wa mwaka Mtandi – Kilwa
b. Tutakuwa na vikao viwili vya kanda kwa mwaka –
Kanda ya kusini na mashariki.

4|Page
c. Vikao vya dharura vitaruhusiwa ili kujenga na
kuimarisha umoja wetu.

NB: Maamuzi yote ya vikao vya kanda na vya dharura lazima


yafikishwe kwa uongozi mkuu.

6:0 VYANZO VYA MAPATO


Vyanzo vya mapato ni viwili;-
a. Pesa ya kiingilio ambayo mtu atailipa mara moja tu Tshs.
10,000/=
b. Ada ya mwezi ambayo kila mwezi mtu anapaswa kulipa
Tshs. 3,000/=
7:0 WANUFAIKA WA MAFAO
a. Mke na mume
b. Watoto wasiokuwa na kipato lakini wathibitishe na
kamati ya maadili, Kamati tendaji na viongozi wakuu.
c. Wazee wetu wasiojiweza.
8:0 MAFAO YANAYOTOLEWA
a) Matibabu; Mfuko utatoa kiasi cha kuanzia Tshs. 5,000/=
hadi 100,000/= kwa kuangalia ukubwa wa tatizo.
Endapo mnufaika akapewa kiasi cha mwisho Tshs.
100,000/= na tatizo bado basi viongozi watatoa taarifa
na itabidi tuchange kutoka katika mifuko yetu.
b) Kufiwa; Mwanachama atapewa pole ya kufiwa Tshs.
50,000/=
c) Majanga; Mfano kuunguliwa au kubomokewa na
nyumba kutokana na upepo au mafuriko, pamoja na
majanga mengine yakithibitishwa na uongozi kiasi cha
Tshs. 100,000/= kitatolewa.
d) Elimu; Mfuko utatoa kiasi cha juu Tshs. 50,000/= kwa
kumsaidia mtoto kupata elimu ya ngazi ya sekondari.
Hii itatokea endapo viongozi wamethibitisha kuwa mzazi
hana uwezo wa kukamilisha jambo hilo kutokana na
kuwa na kipato kidogo, Lakini mzazi lazima awe
mwanachama hai.

5|Page
NB: Harusi haihusiani na mfuko wetu bali watu tutachangia
kadri watakavyokubaliana.

9:0 MAMBO YATAKAYOTENGUA KUTOKUNUFAIKA KWA


MWANACHAMA
a) Mwanachama yoyote ambaye hatolipa ada kwa muda
wa miezi minne mfululizo hatoweza kunufaika kwa
kupata fao kwa changamoto yoyote ambayo
atakutana nayo.

10:0 MWISHO
Katiba hii itapitiwa upya na Mkutano mkuu kila mwaka ili
kuongeza ama kupunguza vifungu kwa matakwa ya wanaukoo.

………………………………….. ……………………………
MWENYEKITI KATIBU

6|Page

You might also like