You are on page 1of 9

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA MALIASILI NA UTALII

TAARIFA KWA UMMA


________________________________________________________
TAARIFA YA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII KUHUSU MALALAMIKO YA
KAMPUNI YA FRIEDKIN CONSERVATION FUND JUU YA UMILIKI WA KITALU CHA
UWINDAJI
1. UTANGULIZI
Wengert Windrose Safaris Ltd (WWS) ni mojawapo ya kampuni tanzu mbili za Friedkin
Conservation Fund (FCF) zinazojihusishanashughuli za uwindaji wa kitalii hapa
Tanzania. Kampuni nyingine ni Tanzania Game Trackers Safaris (TGTS) Ltd. Kampuni
hizo ziliwasilisha maombi ya kumilikishwa vitalu kumi (10) vya uwindaji wa kitalii kwa
msimu wa 2013-2018 kufuatia tangazo la Serikali lililotolewa tarehe 10 Februari 2011.
Orodha ya vitalu vilivyoombwa imeoneshwa (Jedwali Na. 1). Kabla ya ugawaji wa
mwaka 2011, kampuni hizo zilikuwa zinamiliki vitalu 14 (Jedwali Na. 2).
Jedwali Na. 1. Vitalu vya Uwindaji vilivyombwa na vile walivyomilikishwa makampuni ya
Fredkin Conservation Fund kwa kipindi cha uwindaji cha 2013-2018.
Jina la Kampuni
WENGERT
WINDROSE
SAFARIS

TANZANIA GAME
TRACKERS
SAFARIS LTD

1.
2.
3.
4.
5.
1.
2.
3.
4.
5.

Vitalu vilivyoombwa
(2013-2018)
Moyowosi GR South
Lake Natron GCA
(North-South)
Lake Natron GCA (N)
Moyowosi GR Njingwe 2
Moyowosi GR Njingwe 3
Ugalla GR (South)
Ugalla GR (North)
Ugalla GR (Central)
Moyowosi GR Njingwe 1
Maswa Kimali

Vitalu vilivyogawiwa
(2013-2018)
1. Moyowosi GR South
2. Lake Natron GCA (NorthSouth)

1.
2.
3.
4.
5.

Ugalla GR (South)
Ugalla GR (North)
Moyowosi GR Njingwe 1
Maswa Kimali
Maswa Mbono

Jedwali Na. 2. Vitalu vilivyokuwa vinamilikiwa na kampuni za Wengert Windrose Safaris


Ltd na Tanzania Game Trackers Safaris Ltd.
1

Jina la Kampuni
WENGERT WINDROSE SAFARIS

TANZANIA GAME TRACKERS SAFARIS LTD

Vitalu vilivyoombwa (2013-2018)


1. Moyowosi GR Njingwe South
2. Muhesi GR
3. Kizigo GR East
4. Kizigo GR Central
5. Lake Natron GCA (North)
1. Monduli Juu Open Area
2. Kizigo GR (West)
3. Maswa GR (Kimali)
4. Maswa GR (Mbono)
5. Ugalla GR (East)
6. Ugalla GR (West)
7. Moyowosi GR Njingwe North
8. Makere/Uvinza FR
9. Moyowosi GR (Central)

Baada ya matokeo ya ugawaji wa vitalu Kampuni zote mbili (TGTS na WWS)


ziliwasilisha rufaa kwa Waziri wa Maliasili na Utalii kupitia Kamati ya Ushauri wa
Ugawaji Vitalu (iliyokaa January 2012) kutaka kufahamu sababu za kutokupewa baadhi
ya vitalu walivyoomba kikiwepo cha Lake Natron Game Controlled Area (North).
Sababu za kutokupewa vitalu hivyo vilivyoombwa iliwekwa bayana kuwa ni kutokana na
ushindani mkubwa. Ushindani uliongezeka zaidi kutokana na mabadiliko ya sheria
ambapo kifungu cha 39(3)(b) ya Sheria ya Kuhifadhi Wanyamapori Na. 5 ya mwaka
2009 kinataka kampuni zitakazomilikishwa vitalu; asilimia 85 ziwe zinamilikiwa na
watanzania na asilimia 15 wageni.
Kamati ilipendekeza mgawo kwa kuzingatia matakwa ya sheria na ushindani, hali
ambayo ilisababisha kampuni hizo zisigawiwe vitalu vinavyokidhi idadi iliyoombwa na
maeneo yaliyokuwa wamemilikishwa.
2. YALIYOJITOKEZA
2.1. Mgogoro wa Lake Natron Game Controlled Area (North)

Kutokana na WWS kutogawiwa kitalu cha Lake Natron Game Controlled Area
(North) ambacho kampuni hiyo ilikuwa inakitumia hapo awali kwa shughuli za
uwindaji wa kitalii, iliwasilisha rufaa kwa Mhe. Waziri wa Maliasili na Utalii.

Tarehe 21 Novemba 2011, Kamati ya Ushauri wa Ugawaji Vitalu (KUUV) ilimshauri


Mhe. Waziri kuwa ili kusuluhisha mgogoro huo, kampuni ya GMS igawiwe kitalu cha
Ruvu Masai GCA ambacho walikiomba na Lake Natron GCA (North) wagawiwe
WWS. Hata hivyo, Mhe. Waziri hakuafiki ushauri wa Kamati.

Tarehe 25 Novemba 2011 KUUV ilikutana na WWS kusikiliza maelezo ya


ufafanunuzi kuhusu malalamiko yao.
2

Tarehe 12 Desemba 2011, KUUV iliitisha kikao cha pamoja kati ya WWS na GMS
kujadili uwezekano wa kutafuta muafaka wa suala la umiliki wa kitalu cha Lake
Natron GCA (North).

Tarehe 13 Desemba 2011, WWS ilikutana na GMS na kujadiliana makubaliano ya


kibiashara juu kitalu chake cha Lake Natron GCA (North). Hata hivyo, kwa mujibu
wa WWS, ilibainika baadae kuwa makubaliano hayo yasingeweza kutekelezwa kwa
sababu kulikuwa na mchakato wa kuanzisha Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori
ya Jamii (Wildlife Management Area).
WWS ilidai kuwa ilikuwa imeingia mkataba wa matumizi ya ardhi na vijiji 33 katika
eneo hilo hilo, hali ambayo ingesababisha mgogoro.

Kutokana na hali hiyo WWS ilishauri KUUV iendelee kufikiria ombi lao la kubakia na
kitalu hicho kwa kuzingatia sheria, mikataba na masuala ya kiikolojia. Sababu za
kiikolojia zilizobainishwa na WWS ni pamoja na kupinga eneo la Lake Natron GCA
North kugawanywa kuwa vitalu viwili (Lake Natron GCA (North) na Lake Natron GCA
(North-South).

Idara ya Wanyamapori ilihakiki ramani za vitalu vya uwindaji wa kitalii kabla ya


kuzigawa kwa kampuni zilizokuwa zimepata mgawo wa vitalu kama
zilivyowasilishwa na Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI) kwenye
KUUV. Uhakiki wa ramani hizo ulibaini kasoro za majina ya baadhi ya vitalu ambayo
hayakuzingatia uhalisia wa kijiografia na asili ya eneo na hivyo kupendekeza
marekebisho ya majina hayo.
Eneo
Lake Natron GCA
Selous GR

Jina la kitalu
North-South
North
South-West
MHJ1
MHJ2
MHJ3

Pendekezo la jina jipya


North
East
West
MJ1
MH1
MJ2

Ramani za vitalu ziligawiwa mwezi Oktoba 2012 kwa kampuni za uwindaji wa kitalii
zikiwa na mabadiliko ya majina hayo. Baada ya mgawo ramani hizo, WWS ilikuja na
hoja mpya kuwa kitalu chake cha Lake Natron GCA North-South kimebalishwa
(swapped) na kupewa kampuni ya GMS. Ramani ya Lake Natron GCA North-South
iliyofanyiwa marekebisho ya jina ilionesha ukubwa wa kitalu ulibaki vile vile na katika
eneo na daraja lile lile pamoja na jira za mpaka (GPS coordinates) zikiwa zile zile.
WWS iligeuza madai hayo mapya kuwa hoja ya msingi badala ya hoja za awali.

Baada ya hapo suala hilo likageuka kuwa mgogoro kati ya Serikali, WWS na GMS
kwamba kuna udanganyifu umefanyika wa kubadilisha vitalu.
3

Katika kikao cha tarehe 24 Mei 2013, kati ya Idara ya Wanyamapori, WWS, GMS,
TAWIRI, na Kitengo cha Sheria cha Wizara; Mkuruguenzi wa GMS alitaarifu kuwa
katika mojawapo ya majadiliano kati ya GMS na WWS kuwa WWS iliiomba GMS
kuiuzia kitalu chake cha Lake Natron GCA North lakini GMS ilikuwa tayari kuiuzia safari
na siyo kitalu.

Baada ya GMS kukataa ombi lao, WWS ilianza kampeni za kuichafua kampuni ya GMS
ikiwa ni pamoja na tukio la Reno-Nevada, Marekani wakati kampuni hizo zikiuza safari
za uwindaji wa kitalii Januari, 2015. Katika tukio hilo WWS iliifanyia fujo GMS kuwa
kampuni hiyo inafanya utapeli kwa kusambaza vipeperushi vinavyopotosha kwamba
inamiliki kitalu cha Lake Natron GCA North.

Hatua hiyo iliichafua GMS na kusababisha Mkurugenzi wake Bw. Awadhi Abdallah atoe
taarifa Safari Club International (SCI). SCI iliingilia kati kutuliza mgogoro huo.

Kwa mujibu wa Sheria ya Uhifadhi Wanyamapori Na. 5 ya mwaka 2009, kampuni zote
za uwindaji wa kitalii ikiwemo WWS zilitakiwa kuondoka katika vitalu tarehe 31 Machi,
2013 baada ya muhula wa umiliki wa vitalu kumalizika ili kupisha umiliki mpya ili
kutekeleza mabadiliko mapya yaliyoainishwa katika sheria hiyo. Hata hivyo, WWS
iligoma kuondoka na badala yake mwezi Mei 2013 iliamua kwenda Mahakamani kudai
haki.

Mmiliki mpya wa kitalu cha Lake Natron GCA North ambacho kilibadilishwa jina na
kuwa East, kampuni ya GMS aliwasilisha barua ya malalamiko kwa Mkurugenzi Idara
ya Wanyamapori kwamba anashindwa kuendeleza Kitalu pamoja na kujenga kambi ya
uwindaji kwa kuwa bado WWS wapo ndani ya Kitalu kinyume cha sheria. Mkurugenzi
wa Idara ya Wanyamapori aliiandikia WWS barua ya tarehe 20/05/2013 ya kuiamuru
kuondoka kwenye kitalu hicho katika muda wa siku tatu.

Amri hiyo haikutekelezwa na badala yake WWS ilirudi kwa Mhe Waziri wa Maliasili na
Utalii tarehe 23/5/2013 ikipinga amri ya kuondoka iliyotolewa na Mkurugenzi wa
Wanyamapori. Aidha, sambamba na hatua hiyo, WWS iliwasilisha Mahakama KuuKitengo cha Biashara kuomba zuio la GMS kufanya shughuli za uwindaji katika kitalu
cha Lake Natron GCA East.

Mhe. Waziri, alimwagiza Mkurugenzi wa Wanyamapori kuitisha kikao cha wadau wote
wanaohusika na mgogoro wa kitalu cha Lake Natron (GCA) (East) ili kulijadili tena suala
hili. Hata hivyo kikao hicho hakikufikia muafaka kutokana na WWS kuendelea kushikilia
msimamo wa kukitaka kitalu hicho kwa gharama yoyote ile.

Katika kikao hicho nyaraka zote muhimu ziliwasilishwa ikiwemo Ripoti ya Taasisi ya
Utafiti ya Wanyamapori Tanzania (TAWIRI) kuhusu Tathimini ya Vitalu vya Uwindaji wa
Kitalii Tanzania toleo la 3.1 ya Februari 2011. TAWIRI ndiyo Mamlaka ya kisayansi ya
utafiti wa wanyamapori Tanzania. Ikumbukwe kuwa, mabadiliko ya majina hayo
hayakuathiri ukubwa, mipaka na jira (GPS coordinates) za vitalu.
4

Katika kikao cha tarehe 24 Mei 2013 kilichotajwa awali, WWS iliwasilisha ramani
ambayo inadai kuipatia TAWIRI inayoonesha jina na mipaka kitalu cha Lake Natron
GCA (North-South) ili kuthibitisha uhalali wa madai yao. Ilipohojiwa kuwa imekuwaje
ipate ramani TAWIRI wakati Taasisi hiyo haina mamlaka ya kutoa ramani hizo kwa
kampuni za uwindaji, kampuni ya WWS ilieleza kuwa ililazimika kufanya hivyo kwa vile
haikuwahi kupewa ramani ya kitalu hicho na Idara ya Wanyamapori, jambo ambalo si
kweli.

Kikao hakikuridhishwa na maelezo ya WWS ambapo kampuni hiyo ilitahadharishwa


kutowatumia watumishi katika ofisi za umma kupata nyaraka za Serikali kinyume na
utaratibu. Aidha, WWS iliambiwa kuwa kitendo hicho ni cha ukiukwaji wa maadili na
kinaashiria mazingira ya rushwa jambo ambalo ni kosa la jinai kwa yule aliyetoa
nyaraka hizo na aliyezipokea.

Kampuni ya WWS iliendelea kufungua kesi mbalimbali katika Mahakama Kuu ya Ardhi
na Mahakama ya biashara bila mafanikio kama ifuatavyo;

i.

Miscellaneous Land Application No. 44 of 2013 Wengert Windrose Ltd


Versus Green Mile Safari Ltd and Others.

ii.

Commercial Case No.113 of 2013 Wengert Windrose Safaris Versus


Green Mile Safari Ltd.

iii.

Miscellaneous Commercial Case No. 88 of 2013 Wengert Windrose


Safaris (T) Ltd Versus Green Mile Safari Ltd

iv.

Commercial Case No.115 of 2013 Green Mile Safari Ltd Versus


Wengert Windrose Safaris Ltd.

v.

Miscellaneous Commercial application No.92 of 2013 Green Mile


Safari Ltd Versus Wengert Windrose Safaris Ltd.

vi.

Miscellaneous Commercial Cause No.26 of 2013Wengert Windrose


Safaris Ltd Versus Green Mile Safari Ltd.

vii.

Miscellaneous Commercial Application No.26 of 2013 Wengert


Windrose Safari Ltd Versus Awadh Ally Abdallah.

viii.

Miscellaneous Commercial application No.68 of 2014 Awadh Abdallah


Versus Wengert Windrose Safari Ltd.

Tarehe 05/07/2013 Mkurugenzi wa GMS aliwasilisha malalamiko kuwa kampuni ya


WWS ilizuia wageni wa GMS wasifanye uwindaji katika kitalu cha Lake Natron GCA
(East) ambapo wafanyakazi wa kampuni ya WWS waliandaa hila ya; kuyagonga
magari ya GMS yakiwa na watalii; walichimba mashimo kwenye uwanja wa ndege ili
5

kuzuia ndege za GMS zisitue; na walifunga barabara kwa magogo kuzuia magari ya
wageni waliokuja kuwinda yasipite.

Sambamba na fujo hizo, kampuni ya WWS iliwachochea wanakijiji cha Armani,


Longido kufanya vurugu dhidi ya wageni wa GMS. Hali hii ilisababisha Mkuu wa
Wilaya ya Longido kuitisha Kikao na wawekezaji wote na kutoa onyo dhidi ya
Mwekezaji yeyote ambaye angewachochea wananchi kuvuruga amani.

Kimsingi, kampuni za FCF (WWS na TGTS) zimekuwa na tabia ya ubabe na usumbufu


katika Tasnia ya uwindaji wa kitalii dhidi ya kampuni nyingine na Serikali. Tabia hizi
zimeendelea katika sehemu mbalimbali ambapo kampuni hizi zinafanya shughuli za
utalii.
Madai kuwa kampuni za FCFzinanyanyaswa na Idara ya Wanyamapori sio ya kweli.
Kimsingi, busara na uvumilivu mkubwa vimetumika kuendelea kufanya kazi na kampuni
hizo. Tunapenda kubainisha mifano ifuatavyo:i.

Ugawaji wa vitalu kwa uwindaji mwaka 2013-2018 umefanywa kufuata taratibu


zote kwa mujibu wa Sheria ya Wanyamapori Na. 5 ya mwaka 2009 na kanuni
zake za mwaka 2010 zilizorekebishwa 2015.

ii.

Hata pale ambapo kampuni zote mbili (TGTS na WWS) hazikuridhika na


matokeo ya ugawaji wa vitalu Wizara ilikuwa tayari kuwasikiliza zaidi ya mara
moja kupitia KUUV.

iii.

Pamoja na mbinu zisizoridhisha za kampuni hizo za FCF, ikiwemo kuwachafua


baadhi ya wajumbe wa Kamati na watumishi, bado Wizara iliendelea kujadiliana
na WWS na walipokataa na kukaidi maelekezo, Serikali ilikubali kuburuzwa
Mahakamani na WWS kwa kuamini kuwa haki itatendeka kama ilivyoainishwa
hapo awali.

iv.

Pamoja na WWS kushindwa kesi Mahakamani, Wizara ilionyesha uvumulivu kwa


kutotumia nguvu kuwaondoa kwenye kitalu ambacho hawakumilikishwa kihalali.

v.

Pamoja na WWS kuishtaki Wizara Mahakamani, Wizara ya Maiasili na Utalii


iliendelea kufungua milango ya majadiliano kila WWS ilipoomba kufanya hivyo.

vi.

Pamoja na WWS kuzuia Kampuni iliyomilikishwa kitalu kihalali (GMS), kutishia


usalama wa wageni wa GMS, kuifanyia fujo Kampuni ya GMS katika soko la
Kimataifa huko Reno, Nevada (Safari Club International) mwezi Januari, 2013,
kwa kumwondoa Mkurugenzi Mtendaji wa GMS kwenye Tamasha la Utalii wa
Uwindaji, kuikosesha Serikali mapato kutokana na wageni kuondoka, kuchochea
wanakijiji wafanye fujo dhidi ya kampuni nyingine, bado hatua za kidiplomasia
zimekuwa zinatumika kutafuta suluhu ya kudumu. Hata hivyo, kila kitu na kila
uvumilivu una mwisho.

2.2 Kuhusu Kampuni ya Green Mile Safari Ltd (GMS)


6

Wizara ya Maliasili na Utalii iliamua kuirejeshea leseni Kampuni ya Green Mile Safari
Ltd kufanya shughuli za uwindaji wa kitalii katika vitalu vyake vya Selous GR (MK1),
Lake Natron GCA (East zamani North), Gonabis/Kidunda WMA baada ya kupitia rufaa
yake dhidi ya Mkurugenzi wa Wanyamapori kupinga kunyanganywa leseni.
Kampuni ya GMS ilifutiwa umiliki wa vitalu na leseni zake zote za uwindaji kupitia
Taarifa ya Umma iliyotolewa tarehe 11 Julai, 2014. Uamuzi huo ulifikiwa kutokana na
ukiukwaji Sheria na Kanuni za Uwindaji wa Kitalii uliofanywa na wageni wa GMS wakati
wakiwinda kwenye kitalu cha Gonabis/Kidunda WMA mwaka 2012. Matukio ya
ukiukwaji yalibainishwa kupitia picha video (DVD) iliyowasilishwa Bungeni na Mhe.
Peter Msigwa (Mb) wakati wa Bajeti ya Wizara ya Maliasili na Utalii mwaka 2014.
Kampuni ya GMS ilirejeshewa leseni kunatokana na hoja zilizoainishwa kwenye rufaa
yake na tafsiri ya Sheria ya Wanyamapori Na.5 ya Mwaka 2009 katika kifungu 38(12)(c)
ikisomwa kwa pamoja na kanuni ya 17 (2) (b) ya Kanuni za Uwindaji wa Kitalii za
mwaka 2010 zilizofanyiwa marekebisho mwaka 2015.
Hukumu ya Mahakama
iliyotolewa tarehe 31 Machi, 2015 na Jaji Songoro dhidi ya Kampuni ya WWS pamoja
na tafsiri na ushauri kutoka kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa barua Kumb. Na.
AGC/A.130/2J/9 ya tarehe 14 Desemba, 2015 aliyoeleza kuwa kifungu cha 38(12)(c)
kinampa mamlaka Waziri wa Maliasili na Utalii kufuta umiliki wa kitalu endapo
Mahakama itakuwa imemtia hatiani mmiliki wa kitalu.
Ni kwa msingi huu Wizara ilitengua maamuzi yaliyotolewa na Mkurugenzi wa
Wanyamapori na kuirejeshea haki Kampuni ya GMS kufanya shughuli zake za uwindaji
wa kitalii. Aidha, Wizara ilitoa maelekezo kuwa waliohusika na uvunjifu wa sheria,
kanuni na taratibu za uwindaji zilizofanywa na wageni wa kampuni ya GMS huko
kwenye kitalu cha Gonabis/Kidunda WMA; wakiwamo Askari wa Wanyamapori
(waliosimamia uwindaji) pamoja na Mwindaji Bingwa wachukuliwe hatua za kisheria na
kinidhamu.
Pamoja na hatua hizi, Wizara ilielekeza kampuni ya Green Mile Safari Ltd, irudi
kwenye vitalu vyake na kuendelea na shughuli za uwindaji na kuwa Serikali itawapatia
ulinzi kila itakapohitajika. Kufuatia uamuzi huo, kampuni ya WWS ilifungua Shauri
tarehe 25 Mei 2016 katika Makahama Kuu, Kitengo cha Biashara kuomba zuio dhidi ya
utekelezaji wa amri ya Wizara ya kuiamuru kuondoka katika kitalu cha Lake Natron
GCA East ifikapo tarehe 31 Mei 2016. Shauri hilo lilisikilizwa na Jaji Mwambegele, J.
ambapo ombi hilo halikukubaliwa.
3. HITIMISHO
Maelezo haya yanabainisha mtiririko wa chanzo cha mgogoro na jitihada mbalimbali
zilizochukuliwa ili kufikia suluhu yake kama ifuatavyo;
i.

Taarifa za kukaribisha maombi kutoka kwa wadau wote wenye nia ya kufanya
biashara ya uwindaji wa kitalii zilitolewa kwa uwazi kupitia vyombo vya habari.

ii.

Kamati ya Ushauri wa Ugawaji wa Vitalu (KUUV) ilitekeleza majukumu yake kwa


kutumia taarifa halali zilizowasilishwa na kila muombaji wa vitalu. Aidha,
7

maamuzi yaliyofanyika kwa uwazi na kuzingatia sheria, kanuni na ushindani


uliokuwepo.
iii.

Kifungu cha 38(14) cha Sheria ya Kuhifadhi Wanyamapori Na. 5 ya mwaka 2009
kinatoa fursa kwa kampuni ambazo hazikuridhika na matokeo ya ugawaji kukata
rufaa kwa Mhe. Waziri na kusikilizwa kwa utaratibu wa mapitio ya kiutawala
(administrative review). Aidha, Kifungu cha 38(16) cha Sheria ya Kuhifadhi
Wanyamapori Na. 5 ya mwaka 2009 kinatoa fursa kwa kampuni ambazo
hazikuridhishwa na uamuzi wa Mhe. Waziri kukata rufaa Mahakama Kuu.

iv.

Baada ya kutoridhika na maamuzi mbalimbali Kampuni ya WWS ilitumia fursa


hizo zote za kisheria pamoja na vikao vya usuluhishi na baada ya kubaini
kwamba haikufanikiwa kufikia azima yake; ikaamua kuanzisha tuhuma mpya na
kutumia mbinu mbadala zenye hila ili kuuaminisha umma, taasisi za kimataifa na
vyombo vya juu vya Serikali kwamba imedhulumiwa haki yake.

v.

Mwenendo mbaya wa uhusiano baina ya kampuni tanzu za FCF na wananchi na


wadau wengine pia umeoneshwa na Mwiba Holdings Ltd ambayo imekuwa
ikituhumiwa kunyanyasa na kutesa wananchi, kuvunja mikataba halali kati yake
na wananchi kwenye eneo la Jumuiya ya Hifadhi ya Jamii - MAKAO(MAKAO
Wildlife Management Area ). Hivi karibuni mojawapo ya magari ya uwindaji ya
kampuni za FCF ilikamatwa ikisafirisha magunia kumi na moja (11) ya bangi
kwenda nchi jirani ya Kenya.

4.MSIMAMO WA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII


Vitendo vya kampuni ya Wengert Windrose Safaris Ltd sio tu vinawanyima haki wadau
wengine wa tasnia ya uwindaji wa kitalii nchini bali pia vinainyima Serikali mapato; fursa
ya jamii kushiriki na kufaidika na shughuli za uhifadhi; pamoja na kuiharibia jina nje ya
nchi kwa kujenga hisia ya kutokuwepo kwa hali ya usalama. Hii inajitokeza hasa pale
kampuni hizi zinapotishia maisha ya wageni wa kampuni ya GMS iliyojitokeza Lake
Natron GCA East. Aidha, kampuni hii inachafua taswira ya Serikali yetu dhidi ya
wananchi na watalii wanaoitembelea Tanzania kama wawindaji.
Kwa maslahi na heshima ya Taifa letu na tasnia ya uwindaji Wizara ya Maliasili Asili na
Utalii imetoa msimamo ufuatao:

Kuitaka Kampuni ya WWS kuondoka mara moja katika kitalu ambacho


haijamilikishwa kihalali.

Kwamba, FCF imewekeza nchini na kupewa hadhi ya uwekezaji mahiri (SIS) na


inachangia maendeleo ya jamii. Hata hivyo, FCF ijue kuwa hadhi hii ya SIS sio
kibali cha kudharau uhuru wa nchi; kuvunja Sheria zetu; kushawishi wananchi
kuvunja sheria; na kutishia uhuru na haki za raia wa kigeni wanaoishi kihalali au
kutembelea Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
8

Kwamba, Tanzania ni nchi huru (sovereign state) na kwamba Sheria ni


msumeno, hivyo makampuni ya kigeni hayana kinga pale wanapovunja sheria za
nchi.

Kampuni za FCF ziache kuwarubuni na kuwatumia wananchi kufanya fujo (to


use villagers and incite violence against competitors) kwa manufaa yao
kibiashara hakikubaliki na ni uvunjaji wa Sheria za nchi.

Wizara inashauri kuwa kampuni zinazojihusisha na shughuli za utalii zizingatie


na kuheshimu Sheria na Kanuni za nchi wakati wote zipofanya shughuli zao
Tanzania.
Imetolewa na;
Wizara ya Maliasili na Utalii
06 Julai, 2016

You might also like