You are on page 1of 8

JUKWAA LA KATIBA TANZANIA

P. 0. Box 78466, Plot No. 2u1 Block 46 Kijitonyama, Aujacent to Kijitonyama 0BSH Bostels,
Bai Es Salaam, TANZANIA
Tel: -2SS 22 277S79S Fax: -2SS 22 277S764 Cell: u78S 99Su88
E-mail: infojukwaalakatibatz.com, jukwaa.katibagmail.com, Web site: www.jukwaalakatibatz.com
MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIWA BAADA YA MAKUBALIANO
YA KUAHIRISHA MCHAKATO WA KATIBA MPYA MPAKA BAADA
YA UCHAGUZI MKUU, 2015
TAARIFA KWA UMMA
1. UTANGULIZI
Jukwaa la Tanzania Tanzania (JUKATA) tumepokea tamko la vyama vya siasa lilitokana na
makubaliano yaliyoIikiwa kwenye mikutano kati ya vyama vya Siasa vilivyo chini ya Kituo
Cha Demokrasia Tanzania (TCD) na Mheshimiwa Rais iliyoIanyika tarehe 30/8/2014 na
8/9/2014 Ikulu ndogo ya Chamwino Dodoma kwa Iaraja na matumaini makubwa. Kutokana
na Mazungumzo hayo, imekubalika kuwa Mchakato wa Katiba mpya uahirishwe kwa sasa
hadi baada ya uchaguzi Mkuu, 2015. Aidha, imekubalika pia kuwa kwa kuwa katiba mpya
iliyotegemewa sana kuondoa kero na malalamiko ya wadau wa uchaguzi haitakuwepo tena
kabla ya uchaguzi wa 2015, kuIanyike marekebisho ya kikatiba na kisheria ili kunyoosha
maeneo kadhaa yanayohusu uchaguzi ikiwemo: luipa uhuru Tume ya Uchaguzi; kuruhusu
mgombea binaIsi; kulazimu kuwa mshindi wa naIasi ya urais lazima apate zaidi na nusu ya
kura zote; kuruhusu matokeo ya urais kuweza kupingwa mahakamani na kupanua uhuru wa
vyombo vya habari na wanahabari wakati na baada ya uchaguzi. Pia, imekubalika kuwa nje
ya uchaguzi, kutazamwe namna ya kurekebisha sheria ya Mabadiliko ya Katiba ili
kuirejeshea uhai Tume ya Mabadiliko ya Katiba. Jambo moja ambalo labda limesahaulika
kwa bahati mbaya kuhusu uchaguzi ni kutazama upya naIasi ya majeshi hususani Jeshi la
Polisi katika uchaguzi ili kuaachia jukumu lao la asili la kulinda usalama wa raia na mali zao
na siyo zaidi ya hapo huku wakipunguziwa uwezo wa kutumia nguvu zinazovuka kiwango.
Kwa yote hayo, tunapongeza juhudi za wanasiasa zilizopelekea makubaliano haya muhimu!
Hata hivyo, imetushangaza sana kwa jinsi ambavyo mambo yaliyo wazi kama ya kukwama
kwa Mchakato wa Katiba yanavyoweza kuwachukua wanasiasa muda mreIu kuyaona kama
ilivyowachukua wanasiasa wa Tanzania pamoja na uchambuzi, ushauri na wito kutoka kwa
wataalam, wanaharakati na wananchi wenye mapenzi mema kwa nchi yetu ambao uliendelea

kutolewa kwa wakati wote wa takribani miezi sita iliyopita bila maIanikio. Ingawa
maaIikiano ya kuahirisha mchakato wa Katiba sasa yameIikiwa rasmi, pesa nyingi sana
zimekwishapotea bila sababu za msingi kwa sababu tu ya ugumu wa Wanasiasa kuIikia
maaIikiano. Inasikitisha pia kuwa hata baada ya makubaliano hayo ya kusitisha rasmi
Mchakato mzima wa Katiba, bado kumekuwa na kigugumizi cha kusitisha shughuli za Bunge
Maalum la Katiba na kuliacha likiendelea kutaIuna mabilioni ya ziada hadi tarehe 4 Oktoba
2014 huku ikijulikana wazi kuwa Bunge hili Maalum halitazaa rasimu yoyote mpya wala
katiba inayopendekezwa kwa kuwa tayari imeamriwa kuwa upigaji kura hautawezekana na
wala hautakuwepo tena. Aidha, yapo mambo mengine Kadhaa ambayo hayakupata Iursa
nzuri ya kujadiliwa katika mazungumzo ya vyama na Mheshimiwa Rais na kwa hivyo
yanatakiwa kutazamwa vizuri na kuzingatiwa tunapoelekea kutekeleza makubaliano hayo:-
1.1 KUAHIRISHA MCHAKATO WA KATIBA IKIWA NI
PAMO1A NA BUNGE MAALUM
Pamoja na wanasiasa kuchukua muda wote huo, kila Mtanzania mwenye nia nzuri na nchi
yetu anashukuru kwamba vyama vya siasa vimeamua kukubaliana kuahirisha mchakato wa
katiba mpya mpaka baada ya Uchaguzi Mkuu wa 2015. Jambo hili ni la busara kubwa na
limeIanywa kwa nia nzuri ya kuepusha uandikaji wa Katiba katika wakati ambapo kiwango
cha muaIaka na maridhiano kimetoweka kwa sababu ya joto la uchaguzi ujao. Pili, jambo hili
pia linaokoa mabilioni ya shilingi ambayo yameendelea kutumika huku misingi mikuu ya
uandishi na upatikanaji wa Katiba ya watu wote ikiwa imetoweka. Hilo lingeweza kupelekea
upotevu wa pesa na bado Katiba ya Nchi isipatikane. Aidha, imekubalika kuwa Bunge la
Katiba liendelee endelee mpaka tarehe 4/10/2014, ili kumalizia siku 60 za ziada ambazo
Mheshimiwa Rais alizipitisha kwa ajili ya Bunge Maalum la Katiba baada ya kumalizika kwa
siku 70 za awali mwezi Aprili 2014. Pamoja na Shukrani zetu, kuna hoja nzito na za msingi
ambazo ni vizuri kuzielewa ili bunge liweze kuahirishwa mara moja na bila kusubiria
kumalizika kwa siku 60 za nyongeza.
1.1.1 Bunge Maalum la Katiba (BMK) limekosa uhalali wa kisiasa kutokana na kutoka nje
ya bunge kwa kundi la UKAWA na mahudhurio duni kutokana na zaidi ya wabunge
25 wa CCM kutoshiriki vikao tangu Bunge lilipoanza Agosti 05, 2014. Aidha,
mahudhurio duni ya Mawaziri katika vikao vya Bunge hilo Maalum yamepelekea
kukosekana kwa akidi na uhalali wa Bunge hilo Maalum la Katiba mara kwa mara
katika awamu hii ya pili ya Bunge hilo.
1.1.2 Bunge pia limekosa uhalali wa kisheria itakapokuja kwenye kupata 2/3 kutoka
Zanzibar wakati wa kupigia kura viIungu na ibara mbalimbali za katiba, kwa hiyo
kuendelea kwa bunge la katiba ni kuendeleza wizi, uIujaji na kuIuru ya matumizi ya
Iedha za umma wa walipa kodi masikini wa Tanzania.

1.1.3 Mwenendo wa Kazi za Kamati 12 za Bunge Maalum la Katiba ambapo kumetokea


mpasuko mkubwa kati ya wanaotaka rasimu ya Katiba ibadilike sana hasa kuhusu
Muundo wa Muungano na wale wanaotaka misingi mikuu ya Rasimu ibaki kama
ilivyo katika Rasimu ya Katiba Mpya. Katika hali iliyoashiria kutopatikana kwa
suluhu, muaIaka wala maridhiano, walio wengi katika kamati walipendekeza mambo
ambayo mara zote yalipingwa vikali na walio wachache kuhusu mabadiliko katika
Rasimu. Aidha, mapendekezo ya kuondoa misingi yote muhimu ya uwajibikaji wa
serikali na Bunge kwa wananchi kutoka kwenye Rasimu yamedhihirisha kuwa Bunge
Maalum la Katiba halipaswi kushirikisha wabunge, wawakilishi na mawaziri moja
kwa moja kwa kuwa wao lazima watavutia upande wenye maslahi kwao. Utatuzi wa
tatizo hili ni kupendekeza kuwa Bunge Maalum lijalo liwe na watu wasio na nyadhiIa
katika Bunge, Baraza la Wawakilishi au Baraza la Mawaziri isipokuwa kama watu
hao wataamua kujiuzuru naIasi zao kwanza na kuomba ridhaa mpya ya watanzania
kuwa wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba na pia kukubali kuwa wakimaliza
kuandika Katiba hawataweza kugombea naIasi yoyote ya kuchaguliwa ndani ya
miaka 10 tangu tarehe ya kupitishwa kwa Katiba Mpya ili kuondoa uwezekano wa
mgongano wa kimaslahi.
1.1.4 Kujiengua kwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Mheshimiwa Othman Masoud
Othman kutoka katika Kamati ya Uandishi ya Bunge Maalum la Katiba kumekuwa
pigo kubwa kwa Mchakato wa Katiba Mpya na hususani Bunge Maalum la Katiba.
Habari kuwa kuondoka kwa Mwanasheria huyo Mkuu wa upande mmoja wa
Muungano kusingeleta madhara yoyote kwa uandishi wa Katiba Mpya kwa kuwa
kuna wazanzibari wengine walio katika kamati hiyo ya uandishi ni propaganda na
upotoshaji unaostahili kupuuzwa ikizingatiwa kuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar
ndiye kiongozi wa jopo la wanasheria na waandishi kutoka upande wa Zanzibar na
mshauri mkuu wa Kisheria wa SMZ na kwa hiyo kujiengua kwake kwa sababu za
kutoridhishwa na Mwenendo wa Mchakato ni ishara mbaya kwa Mchakato mzima na
ina athari kwa maslahi ya Zanzibar katika Katiba itakayopendekezwa. Hata
kiutendaji, kujiengua kwa Mwanasheria Mkuu kusingeishia na yeye pekee bali
kungepelekea kujiengua kwa wanasheria na waandishi wengine kutoka Zanzibar
ambao wana uaminiIu kwa Kigogo huyo wa tasnia ya Sheria katika visiwa vya
Unguja na Pemba. Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar pia ana dhamana ya kusimamia
nidhamu na taaluma ya wanasheria wote wa Zanzibar wakiwemo mawakili, majaji na
waendesha Mashitaka. Haitungii akilini kuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar
angeweza kujiengua kibinaIsi bila kuwasiliana na mamlaka ya uteuzi wake na kama
hali ndivyo ilivyokuwa, kujiengua kwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar kunaweza
kuwa na baraka za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na hiyo ikawa na taIsiri ya kususia
kwa Zanzibar katika uandishi wa Katiba. Hoja hii ya kujiengua pia inamhusu Waziri
wa Katiba na Sheria wa Zanzibar.
2. HA1A YA KUZUIA UWEZEKANO WA MCHAKATO
KUHU1UMIWA NA KUFA MO1A KWA MO1A

Kwa sababu ya uzoeIu wa michakato kama hii inapoIikia kuahirishwa kama ilivyotokea
hapa Tanzania, kumekuwa na wasiwasi juu ya endapo mchakato wa Katiba hautajikuta
ukihujumiwa na kuIutwa kinyemela. Jambo hili limewahi kutokea katika nchi kadhaa
AIrika ikiwemo Zambia ambapo Rais Mpya, tena kutoka upinzani, Mheshimiwa Michael
Satta (King Cobra) ameamua kuhujumu Mchakato wa Katiba Mpya ambao ulikwishaIikia
hatua nzuri ya Rasimu kama tulipoIikia sisi. Ili kuepuka hali Kama hiyo, inapendekezwa
kuwa iandaliwe ratiba Mpya ya Mchakato wa Katiba itakayoonesha matukio na tarehe
zote muhimu ikiwemo kuahirishwa na kuanza tena kwa Mchakato wa Katiba Mpya.
Ratiba (roadmap) hiyo mpya itapaswa kuingizwa na kupitishwa na Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania linalotarajiwa kukutana mwanzoni mwa Novemba 2014 ili iwe
sehemu ya sheria ya Mabadiliko ya Katiba ambayo italazimika kuheshimiwa na kuIuatwa
na yeyote atakayechaguliwa kuongoza Tanzania baada ya Uchaguzi Mkuu mwakani.
Pasipo kuweka kizuizi hiki cha uwezekano wa hujuma kwa Mchakato wa Katiba Mpya,
uhakika kuwa Katiba Mpya itakamilishwa baada ya uchaguzi utakuwa ni mdogo.
3. HA1A YA KUAHIRISHWA KWA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA
MITAA ILI UFANYIKE PAMO1A NA UCHAGUZI MKUU,
OKTOBA 2015
JUKWAA LA KATIBA TANZANIA tunaungana na wanaopongeza uamuzi wa
wanasiasa kuahirisha pia uchaguzi wa serikali za mitaa uliokuwa uIanyike mwezi
Septemba 2014 mpaka mwaka 2015. Hata hivyo zipo hoja za msingi kuhusu uchaguzi
huu pia:-
3.1 Uchaguzi huu umeahirishwa mpaka lini hasa? Hoja kuwa uchaguzi huu unaahirishwa
hadi mapema mwaka 2015 si halisia kwa sababu maandalizi ya uchaguzi huu
hayajaanza kabisa na kwa jadi huhitaji kati ya miezi mitano mpaka sita, kwa uchache.
Aidha, gharama za kuendesha chaguzi hizi mbili za serikali za Mitaa na Uchaguzi
Mkuu zingeweza kupungua endapo zitaIanyika tarehe moja. Hivyo, ni vizuri
ikajulikana kabisa ni lini uchaguzi huu muhimu sana kwa demokrasia ya nchi yetu
utaIanyika badala ya kuendeleza kigugumizi na kusema utaIanyika Mapema
mwakani`. Pia tunapendekeza chaguzi hizi ziIanyike siku ya kazi kama inavyoIanyika
katika nchi nyingine za Kenya, Zimbabwe, Malawi na AIrika Kusini ili kuweza
kuwapatia wananchi Iursa ya kutumia haki yao ya kidemokrasia kupiga kura badala
ya siku za mapumziko kama ambavyo imekuwa jadi hapa Tanzania.
3.2 Usimamizi wa uchaguzi huu wa Serikali za Mitaa utakuwaje? Kumekuwa na
malalamiko mengi juu ya uhuru wa chombo kinachosimamia uchaguzi wa serikali za
Mitaa. Kwa sababu hiyo, kuendelea kwa TAMISEMI kusimamia chaguzi hizi
kutaendeleza malalamiko na kuleta maaIa makubwa katika nchi yetu kwani
TAMISEMI sio chombo cha kitaalamu cha kiuchaguzi. JUKATA tunapendekeza
kuwa kwa kuanzia uchaguzi wa Mwakani, chaguzi zote zisimamiwe na Tume Huru

ya TaiIa ya Uchaguzi (INEC) badala ya oIisi ya TAMISEMI ambayo ni idara


inayosimamiwa na Waziri aliye chini ya Waziri Mkuu.
4. HA1A YA KUSAINI MAKUBALIANO YA KITAIFA
Kutokana na uzoeIu tuliopitia huko nyuma tunapendekeza maridhiano na makubaliano
yaliyopatikana kupitia wanasiasa yawekwe rasmi kwenye maandishi na kutiwa saini na
vyama vyote vya Siasa vilivyoshiriki na Rais Jakaya Mrisho Kikwete mwenyewe akiwa
shahidi. Kwa uzoeIu wetu wa huko nyuma na wanasiasa wa Tanzania, hilo lisipoIanyika
muda sio mreIu wataanza kuzozana tena kwamba yanayosemwa sio ya kweli na kwamba
wala hawakukubaliana hivyo. Aidha, ipo haja ya kuyaIanya makubaliano hayo kuwa na sura
ya kitaiIa zaidi ili wadau wote wa Mchakato wa Katiba na Masuala ya uchaguzi waIahamu na
kuwa sehemu ya makubaliano hayo. Katika hili, JUKATA tunajitolea kuIanya kazi ya
kusaidia kuyatambulisha makubaliano hayo na pia kusaidia kuboresha mambo ya msingi ya
mbeleni kuhusiana na yaliyokubalika. Tayari kuna toIauti zilizojitokeza kati ya vyama
wanachama wa UKAWA kwa upande mmoja na vyama vilivyotumwa kusoma makubaliano
hayo mbele ya umma vikiwakilishwa na UDP, TLP na UPDP. JUKATA tumechunguza kiini
cha toIauti hizo na kubaini kuwa ni kutokana na maslahi binaIsi ya baadhi ya viongozi wa
vyama. Tunaamua kujadili toIauti hizo kwa mapana zaidi na kutoa karipio katika kiIungu cha
6 cha tamko hili.
5. HA1A YA MAREKEBISHO YA VIFUNGU MBALIMBALI VYA
KATIBA YA 1MT, KATIBA YA ZANZIBAR NA SHERIA
NYINGINEZO ZINAZOHUSU UCHAGUZI
Kutokana na kuwa muda umeenda sana kuelekea uchaguzi Mkuu na jumuishi ujao, JUKATA
tunapendekeza kuIanyike mabadiliko ya 15 katika katiba ya Jamhuri ya Muungano ya 1977;
Mabadiliko ya 11 katika Katiba ya Zanzibar na Marekebisho katika sheria nyingine ziIuatazo
kupitia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania la mwezi Novemba 2014 na Baraza la
Wawakilishi Zanzibar ili kuwahi michakato ya maandalizi mbalimbali ya Uchaguzi Mkuu wa
2015. Sheria ambazo viIungu vyake vinahitaji kuIanyiwa marekebisho ni pamoja na:
(i) Sheria ya uchaguzi Na. 1 ya Mwaka 1985
(ii) Sheria ya Uchaguzi ya TaiIa, Sura ya 343
(iii) Sheria ya vyama vya siasa,Sura ya 258, July,1992 (R.E, 2002)
(iv) Sheria ya Jeshi la polisi, Sura ya 322
(v) Sheria ya gharama za uchaguzi, 2010
(vi) Sheria ya Uchaguzi wa Serikali za mitaa, Sura ya 292
(vii) Sheria za uchaguzi unaohusu Zanzibar

6. UPOTOSHA1I WA MAKUSUDI 1UU YA MASUALA YA


MCHAKATO WA KATIBA MPYA NA ULIPOFIKIA
Mbali na mambo ambayo yanazungumzwa kinyume kwa sababu ya wadau kutoIahamu
kwa sababu ya upya wa mchakato unaoendelea wa Katiba Mpya, kumetokea wimbi la
upotoshaji wa makusudi wa baadhi ya mambo kwa sababu za kimaslahi binaIsi ya
wapotoshaji. JUKATA tunaona hatari kubwa ya upotoshaji huu wa kimakusudi kwa
mchakato wa Katiba na kama ada yetu tumeshauriana na jopo la wataalam Wetu na
kukubaliana kutoa adhabu kwa wapotoshaji kadhaa waliovuka viwango vya msamaha.
Itakumbukwa kuwa tumekuwa na utamaduni wa kutoa hati chaIu kwa wavurugaji wa
mchakato wa Katiba tangu mwaka 2011. Kwa jinsi hiyo hiyo, leo tunawatangaza rasmi
maadui wane wa Katiba Mpya kama iIuatavyo:
6.1 Mheshimiwa Samuel 1ohn Sitta, MB
Huyu ni Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Waziri wa Masuala ya AIrika
Mashariki na Mbunge wa Urambo Mashariki. Akiwa mwanasheria yeye mwenyewe,
anaIahamu vema kuwa Bunge Maalum la Katiba linapaswa kutoongozwa na mtu mwenye
maslahi ya moja kwa moja katika serikali ya wakati wa kuandika Katiba lakini aliamua
kuingia katika kinyang`anyiro cha kugombea naIasi ya Mwenyekiti wa Bunge Maalum na
kukubali kuchaguliwa kwake katika naIasi hiyo. Aidha, amekuwa kinara wa kushambulia
vyombo vya habari na watu binaIsi kana kwamba Katiba Mpya ni mradi wake binaIsi
huku akijua Iika kuIanya hivyo ni kwenda kinyume na utaratibu wa uandishi wa Katiba
Mpya. Pia, amekuwa kinara wa upotoshaji katika siku za Karibuni akitamka mambo
kadhaa huku akijua kuwa si ya kweli. Kwa mIano, tamko lake kuwa hadhi ya Bunge
Maalum la Katiba iko juu kidogo ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba ni upotoshaji wa
makusudi kwa kuwa vyombo hivi vina hadhi sawa kwa mizania yoyote ile. Zaidi ya hiyo,
Mheshimiwa Sitta amesikika akisema kuwa pamoja na makubaliano ya kuahirishwa kwa
mchakato wa Katiba hadi baada ya uchaguzi Mkuu, upigiaji kura Rasimu ya Katiba
kiIungu kwa kiIungu uko palepale pamoja na uwezekano wa theluthi mbili kutopatikana
na kwamba utaratibu utaIanywa ili hata wajumbe walio nje ya nchi wakihudhuria ibada
ya hija, wagonjwa walio vitandani India na kwingineko pamoja na wawaziri walio
saIarini ughaibuni nao wataweza kusomewa Rasimu mpya` kiIungu kwa kiIungu kabla
ya kupiga kura huko huko waliko. Ni wazi kuwa Mheshimiwa Sitta anaIanya haya huku
akijua kuwa anapotosha umma kwa kuwa mipango ya miaka mingi hata kuwezesha
watanzania walioko nje ya nchi kupiga kura haijawahi kuIanikiwa. Aidha, tamko lake
linaleta hisia kuwa anataka kutumia upenyo wa walio nje ya nchi kuchakachua idadi ya
kura za Ndiyo kwa Rasimu ya Katiba. Mheshimiwa Sitta pia ameamua kuendelea na
Bunge Maalum la Katiba huku akijua kuwa kutokuwepo kwa idadi kubwa ya wajumbe
kiasi hicho ni doa kwa mchakato wa Katiba Mpya. Aidha, amekuwa kinara wa
kuwaaminisha watanzania kuwa Katiba mpya itapatikana bila tatizo pamoja na
kutokuwepo kwa ushiriki wa UKAWA, Waziri wa Katiba na Sheria wa Zanzibar na hata
Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar. Haya yanaIanywa huku Mheshimiwa Sitta, ambaye
mbali na kuwa mwanasheria ni mtumishi mwandamizi katika serikali ya Tanzania kwa

miaka takribani 50 na bungeni kwa miaka 40 sasa akiwa anaIahamu Iika kuwa Katiba ni
suala ya maaIikiano, makubaliano na maridhiano kati ya nchi mbili zilizoungana mwaka
1964 yaani Tanganyika na Zanzibar na kususa kwa vigogo hawa muhimu wa SMZ ni
sawa na kususa kwa Zanzibar na kunaondoa uhalali wa Katiba itakayopendekezwa.
6.2 Mheshimiwa 1aji Frederick Werema, Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya
1amhuri ya Muungano wa Tanzania
Akiwa nguli wa tasnia ya Sheria na mshauri mkuu wa sheria katika Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, amekuwa bingwa wa kutoa taIsiri tata ndani na nje ya Bunge
kuhusu mchakato wa Katiba Mpya. Kwanza, aliwahi kushauri kuwa taIsiri ya siku 70 za
Bunge Maalum ni pamoja na siku za mapumziko na sikukuu na kuIanya Bunge Maalum
kuIanya kazi hadio Jumamosi katika awamu ya kwanza ya Bunge hilo. Baadaye,
aliendelea kutoa taIsiri toIauti na kupelekea Bunge hilo hilo (yeye akiwa mjumbe)
kubadili utaratibu na kuanza kupumzika siku za Jumamosi, Jumapili na sikukuu katika
awamu ya pili na hivyo kukiuka amri ya Rais kupitia tangazo la serikali (GN). Ni katika
hali hiyo kulitokea mkanganyiko wa endapo Bunge liishie tarehe 04 Oktoba au tarehe 31
Oktoba huku yeye akikubaliana na yoyote katika tarehe hizo. Pili, Mheshimiwa Werema
amekuwa mshauri mbaya wa Bunge Maalum la katiba akimwaminisha Mwenyekiti wake,
wabunge waliomo ndani na watanzania kuwa mchakato wa Katiba utakamilika hata bila
ya wajumbe wote hao walio nje na mahudhurio duni. Ndugu Werema amekuwa kinara wa
kushauri kuwa hata muundo wa serikali tatu ulio katika Rasimu unaweza kubadilika
kiuandishi na kuwa Rasimu ya serikali mbili bila shida jambo ambalo linapingwa na
wanasheria na wasomi wenzake wengi akiwemo Waziri wa Sheria na Mwanasheria Mkuu
wa Zanzibar. Ni msigano huu ndio umeuIikisha mchakato wa Katiba Mpya katika
mgogoro mkubwa zaidi ukiacha ule uliotokana na UKAWA kutoka nje. TaiIa
litakumbuka kuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar amemwandikia Mwenyekiti wa
Bunge Maalum la Katiba kujitoa katika kamati ya uandishi wa Katiba inayopendekezwa
kwa kile anachoamini kuwa katiba mpya haiandikiki kwa mazingira ya uchakachuaji` ya
namna hii na kwamba maslahi ya Zanzibar yanakanyagwa` kwa uchakachuaji huo.
PENDEKEZO: Kutokana na makosa hayo ya upotoshaji ya Waheshimiwa hao,
JUKATA inawatangaza rasmi Mheshimiwa Samuel John Sitta, Mheshimiwa Jaji
Erederick Werema kuwa Maadui wapya wa Katiba Mpya Tanzania. Kwa tangazo hili,
JUKATA tunapendekeza kuwa watu hao wasiIikiriwe kwa naIasi yoyote ya kuchaguliwa
au kuteuliwa katika miaka kumi ijayo ili kutoa muda kwao kujitaIakari kwanza.
7. HITIMISHO
Kutokana na masuala ya Katiba kuwa na unyeti kwa taiIa zima na kwa jinsi
yanavyoshikamana na masuala ya uchaguzi ambayo nayo yana wadau wengi nje ya
wanasiasa; JUKWAA LA KATIBA TANZANIA tunaona haja ya kupanua wigo wa
mazungumzo na makubaliano yanayoendelea na yatakayokuja siku na miezi ijayo ili

makubaliano yoyote yanayoIikiwa yawe si tu makubaliano ya Vyama vya Siasa bali ni ya


taiIa zima. Katika kuIanikisha hili, ipo haja ya kuwa na juhudi za makusudi za kupanua
kamati inayoandaa mapendekezo ambayo hatimaye yatatiwa saini kuhusu Kuahirishwa kwa
Mchakato wa Katiba Mpya na Maandalizi ya kina ya Uchaguzi Mkuu ujao ili ihusishe
wawakilishi wa makundi mengine ya kijamii hususani AZAKI, Asasi na mashirika ya dini,
vikundi vya wazalishaji na wasomi na wataalam wa kada mbalimbali ndani na nje ya vyuo.
Hii itaepusha mazungumzo kama hayo kukwama katika siku zijazo kwa kuwa tu pande moja
au mbili zimekinzana. Ingawa Wanasiasa wana naIasi kubwa, ukweli ni kwamba nchi
haiwezi kuendeshwa na Wanasiasa peke yao kama tunavyoshuhudia ikishindikana sasa na
siku za nyuma.
Aidha, kutokana na kusita kwa Mchakato huu, Tanzania inapaswa kuchukua hii kama Iursa
mpya iliyojitokeza kwa ajili ya kutazama tulipojikwaa na kurekebisha kasoro zote
zilizopelekea hadi mkwamo huu. Kwa maoni tuliyayapata, inashauriwa kuwa kuwe na
Mjadala wa KitaiIa utakahusisha Mkutano Mkuu wa Katiba (NCC) ambao utakuwa kama
Bomas oI Tanzania` mwanzoni mwa mwaka 2016. Mkutano mkuu utapaswa kujadili na
kupasa suluhu ya masuala muhimu yanayoligawa taiIa kwa sasa ikiwemo Muundo wa
Muungano. Kwa sasa, kinachowezekana ni kuhiIadhi kumbukumbu zote za mijadala ya
Kamati kuhusu rasimu bila kupigia kura yoyote ili lolote lililojadiliwa liwe katika
makumbusho ya taiIa. Kupitisha Katiba inayopendekezwa kwa sasa haiwezekani kutokana na
ubatili wa mchakato wa Bunge Maalum la Katiba kutokana na kukosekana kwa muaIaka,
maelewano na maridhiano ndani ya chombo hicho.
Kwa maoni yetu, kutokana na makubaliano yaliyoIikiwa kati ya vyama na Mheshimiwa Rais
Bunge linapaswa kusitisha shughuli zake mara moja na JUKATA tunatoa wiki mbili tangu
leo liwe limeIanya hivyo. Vinginevyo, tutaIika Dodoma kwa wingi wetu tukiwa na makuIuli
kwa ajili ya kuIunga rasmi ukumbi wetu wa Bunge kama ishara ya kusitisha rasmi Bunge
hilo lisiendelee kuIuja pesa za walipa kodi wa Tanzania.
Imetolewa na kutiwa saini kwa niaba ya JUKATA na:
Deus M.Kibamba
Mwenyekiti
12/9/2014

You might also like