You are on page 1of 3

#World Water Day na #Wiki ya Maji: #Maji na Mabadiliko

kwa Maendeleo #WaterIs #MaMaMa


Leo ni siku ya maji duniani ( #WorldWaterDay )na kwa Tanzania ni
kilele cha wiki ya maji. #MajiNi maisha, #MajiNi maendeleo
( #WaterIs Life, #WaterIs Development ). Shiriki na Umoja wa
Mataifa
katika
maadhimisho
kwa
kutembelea
http://www.unwater.org/worldwaterday na kushiriki kupiga picha
za #WaterIs ( #MajiNi ) na kuweka katika mitandao ya kijamii.
Ujumbe wa wiki ya maji kitaifa ni maji kwa maendeleo endelevu
na maadhimisho yanafanyika Musoma ambao Rais anatajiwa
kuhutubia. Kwa kuwa maadhimisho haya ni ya mwisho kwa
utawala wake, anapaswa kulieleza taifa ni kwa nini ameonyesha
udhaifu wa kushindwa kutekeleza ahadi yake aliyoitoa wakati
akizindua Bunge mwaka 2005 ya kwamba anatambua kuwa maji
ni kero nambari wani na kwamba Serikali yake ingeandaa
mpango kabambe wa kuhakikisha matatizo ya maji yanakuwa
historia.
Ameonyesha udhaifu 2005-2010 na ameendeleza udhaifu huo
mwaka 2010-2015 hivyo aelekeze Waziri Mkuu atekeleze ahadi
iliyotolewa na Waziri Mwandosya kwa niaba yake ya Serikali
kuwasilisha katika kila Mkutano wa Bunge Taarifa ya Mpango wa
dharura kwa kuwasilisha katika Mkutano huu wa 19 wa Bunge
taarifa hiyo.
Aidha, nabashiri kwamba Rais atatumia maadhimisho ya Musoma
kwenye uzinduzi wa miradi kueleza mafanikio makubwa
yaliyopatikana kutokana na Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa
(MMS)- Big Results Now BRN.
Hata hivyo, Rais azingatie kwamba MMS/BRN kwenye Sekta ya
Maji haijaweza kushughulikia kwa ukamilifu matatizo niliyoyaeleza
kwenye hoja binafsi niliyowasilisha Bungeni kuhusu Hatua za
Haraka za Kuboresha Upatikanaji wa Maji Safi na Ushughulikiaji
wa
Maji
Taka
Jijini
na
Nchini
(Rejea:

http://mnyika.blogspot.com/2013/02/maelezo-na-hoja-binafsi-yakupendekeza.html ). Ilani ya CCM ya mwaka 2005 iliahidi ifikapo


2010 maji yangepatikana mijini ikiwemo Jijini Dar Es Salaam kwa
asilimia 90 na vijijini kwa asilimia 75 ahadi ambayo
haijatekelezwa.
Ili Rais asiendelee kuonekana dhaifu zaidi walau kupitia siku hii ya
maji awaagize watendaji katika ofisi yake watekeleze agizo
alilowapa la kuitisha kikao cha kazi Ikulu kuhusu matatizo ya maji
katika Jiji la Dar Es Salaam mwezi Machi 2013 kama alivyoahidi
(rejea:
http://gkitalima.blogspot.com/2013/03/jakaya-kikwetekukutana-na-mnyika.html
na
http://www.matukiotz.co.tz/2013/03/mnyika-aitwa-ikulu.html ).
Namshukuru Rais kwamba kuna hatua katika upatikanaji wa fedha
na utekelezaji wa miradi ya Ruvu Chini na Ruvu Juu na pia miradi
mingine ya visima vya dharura ikiwemo katika Jimbo la Ubungo
ikiwemo mradi wa Mpiji Magohe ambao tumeuzindua siku chache
zilizopita kama sehemu ya maadhimisho ya wiki ya maji; hata
hivyo kasi, nguvu na ari ya mpaka sasa hailingani na ahadi za
kufanya tatizo la maji kuwa historia 2010, 2011, 2012, 2013, 2014
na hata 2015.
Zipo hatua zaidi zinaweza kuchukuliwa katika kipindi cha miezi
mitatu kuanzia sasa iwapo tukikutana na kujadili udhaifu uliopo
katika utekelezaji wa Mpango Maalum wa maji Dar es Salaam;
hivyo kwa kuwa nimeshamkumbusha yeye mwenyewe na
wasaidizi wake mara kadhaa bila kikao hicho kuitishwa ni wakati
sasa wa wananchi wa Dar Es Salaam kushiriki kumkumbusha kwa
njia mtakazoona zinafaa.
Kwa kuzingatia hali hii kwa wote wenye kutaka kushiriki ujumbe
wetu kwake na kwa wengine kitaifa unapaswa kuwa #Maji Na
Mabadiliko Kwa Maendeleo ( #MaMaMa ) ili tuitumie siku hii na
zijazo kuhamasisha mabadiliko yenye kuwezesha kupatikana kwa

maji kwa maendeleo ya wananchi na nchi kwa ujumla. ( #WaterIs


#MaMaMa ).
Wenu katika uwakilishi wa wananchi,
John Mnyika (Mb)
Jimbo la Ubungo
22 Machi 2015

You might also like