You are on page 1of 51

_______

SURA YA 16
_______

KANUNI YA ADHABU
_______

MPANGO WA MAFUNGU
_______

SEHEMU YA 1
_______

MASHARTI YA KAWAIDA

SURA YA 1
UTANGULIZI
1. Jina fupi.
2. Kazi yake badala ya Kanuni ya Adhabu ya Bara Hindi.
3. Kuepusha sheria kadha.

SURA YA II
TAFSIRI

4. Kanuni ya kawaida ya tafsiri ya sheria


5. Tafsiri.

SURA YA III
KUTUMIKA KWA KANUNI HII NCHINI

6. Kuenea kwa mamlaka ya mahakama za mwanzo.


7. Makosa yatendwayo nusu ndani ya mamlaka na nusu nje ya mamlaka

SURA YA IV
KANUNI YA KAWAIDA KUHUSU JUKUMU YA JINAI

8. Kutojua sheria.
9. Dai la haki kwa uaminifu.
10. Kusudio na sababu.
11. Kukosea hakika.
12. Kudhaniwa kuwa na akili timamu.
13. Wenda mazimu.
14. Kulewa.
15. Umri mchanga.
16. Maafisa wa mahakama.
17. Lazima.

1
18. Kutetea nafsi au mali.
19. Utumiaji wa nguvu katika kukamata.
20. Kulazimishwa na mume.
21. Watu wasipewe adhabu mara mbili kwa kosa moja.
22. Wakosaji wakuu.
23. Makosa ya kushirikiana.
24. Kumshauri mwingine afanye makosa.

SURA YA VI
ADHABU

25. Namna mbali mbali za adhabu.


26. Hakumu ya kifo.
27. Kifungo.
28. Adhabu ya kutandikwa.
29. Faini.
30. Kuhodhi.
31. Fidia.
32. Gharama.
33. Dhamana kwa kutunza amani.
34. (Imebatilishwa).
35. Adhabu ya kawaida kwa makosa madogo.
36. Kuzidi kwa adhabu isipokuwa imeamuriwa vingine.
37. Wafugwa waliotoroka watumike baki ya vifungo wakamatwapo tena.
38. Kuachilia kwa sharti au bila ya sharti.
38A. Kutenda kosa tena
38B. Matokeo ya hatia na kuachiliwa.
_______

SURA YA II

UHALIFU
______
Kigawe cha I. – Makosa ya Kuvunja Utulivu

_______

SURA YA VII

UHAINI NA MAKOSA MENGINE JUU YA UTAWALA


39. Uhaini.
40. Kuchochea mashambulio.
41. Kuficha uhaini.
42. Makosa makubwa ya kihaini.

2
43. Kuletesha vita vya wenyeji.
44. (Imebatilishwa).
45. Kuchochea uasi.
46. Kusaidia katika vitendo vya uasi.
47. Kushawishi utorokaji.
48. Kusaidia mateka wa vita kutoroka.
49. Ufafanuzi wa kitendo cha dhahiri.
50. Maelezo.
51. Uwezo wa kuzuia kuingiza matangazo.
52. Makosa yanayohusu matangazo ambayo uingizaji wake umepigwa marufuku.
53. Upelekaji wa tangazo lililopigwa marufuku kwa Sheha au kituo cha Polisi
54. Uwezo wa kukagua vifurushi.
55. Nia ya ufitina.
56. Makosa ya fitina.
57. Mashitaka.
58. Ushahidi.
59. Viapo visivyo halali ili kutenda makosa ya mauaji.
60. Viapo vingine visivyo halali ili kutenda makosa.
61. Kiasi cha malazimisho kuwa ni utetezi.
62. Kwata isiyo halali.
63. Tangazo la habari za uwongo ziwezazo kuleta hofu na mshituko kwa watu.
63A. Uchochozi wa kutumia nguvu.
63B. Kuchamua kutoridhika na chuki kwa madhumuni yasio halali.

SURA YA VIII

MAKOSA YANAYOINGILIA UHUSIANO NA DOLA ZA KIGENI


NA UTULIVU WA NCHI ZA NJE

64. Kuumbua watawala wa kigeni.


65. Uandikishaji askari wa kivita kwa nchi za kigeni.
66. Uharamia.

SURA YA IX
MIKUSANYIKO ISIYO HALALALI NA GHASIA NA MAKOSA
MENGINE YA KUVUNJA UTULIVU WA WATU

67.-73. (Zimebatilishwa).
74. Ufafanuzi wa mkusanyiko usio halali na ghasia.
75. Adhabu ya mkusanyiko usio halali.
76. Adhabu ya ghasia.
77. Kutoa ilani kwa wafanya ghasia kutawanyika.
78. Kutawanyika kwa wafanya ghasia.
79. Ghasia baada ya ilani.

3
80. Kupinga utoaji wa ilani.
81. Wafanyi ghasia kubomoa majengo, n.k.
82. Kuhasiriwa majengo na wafanya ghasia.
83. Kuyaingilia kwa ghasia reli, magari, n.k.
84. Kutembea na silaha hadharani.
85. Kuingia kwa nguvu.
86. Kukamata kwa nguvu.
87. Mapigano.
88. Kusai mapigano ya wawili.
89. (i) Matusi na mzozo;
(ii) Kutishia utumiaji nguvu.
89A. Kuvinjari.
89B. Kutishia.
89C. Kushawishi watu wasisaidie mipango ya kujitolea.
90. Mkusanyiko kwa ajili ya kufanya magendo.

Kigawe cha II. – Makosa juu ya Usimamiaji wa Mamlaka ya Halali


______

SURA YA X
KUTUMIA MADARAKA VIBAYA

91.-93.(Zimebatilishwa).
94. Maafisa wenye kazi maalumu juu ya mali.
95. Madai ya uwongo ya maafisa.
96. Kutukana madaraka.
97. Maafisa kutoa shahada za uwongo.
98. Kulisha kiapo kisichoruhusiwa na Sheria.
99. Kujipa mamlaka ya uwongo.
100. Kujifanya mtumishi wa Serikali.
101. Kutishia kuwajeruhi watumishi wa Serikali.

SURA YA XI

MAKOSA YAHUSUYO USIMAMIAJI WA HAKI

102. Ushahidi wa uwongo na kushawishi ushahidi wa uwongo.


103. Maelezo ya uwongo ya wakalimani.
104. Adhabu kwa ushahidi wa uwongo na kushawishi ushahidi wa uwongo.
105. Ushahidi juu ya shitaka la kutoa ushahidi wa uwongo.
106. Kutunga ushahidi.
107. Kuapa kwa uwongo.
108. Kudanganya mashahidi.
109. Kuharibu ushahidi.
110. Njama kupinga haki na kuingilia mashahidi.

4
111. ……… makosa makubwa.
112. …….. mashtaka yapasayo adhabu.
113. ……… mali iliyoibiwa.
114. ……… mahakama.
115. ……… kukinga uwasilishaji au utimilizaji wa hati.

SURA YA XII
…… NA KUWAKINGA WATUMISHI WA MAHAKAMA ZA SHERIA

116. ….
117. Kuhudhuria kwenye kazi ya kifungo cha jela baridi.
118. ….wafungwa kutoroka.
119. … mali iliyokamatwa kwa halali.
120. Imebatilishwa.

CHAPTER XIII
…YA MCHANGANYIKO KUITENDEA SERIKALI

121. … wa watumishi wa Serikali.


122. .. kazi kwa watumishi wa Serikali.
123. Taarifa ya uwongo kwa mtumishi wa Serikali.
124. Wajibu wa Sheria
125. .. amri za halali.
126. .. bendere au alama ya taifa.

Kigawe III – Makosa yanayodhuru watu kwa jumla

SURA YA XIV
MAKOSA YAHUSUYO DINI

127. …. dini ya watu wowote.


128. …. Mikusanyiko ya dini.
129. … maziarani bila idhini.
130. .. maiti kuzikwa.
131. …yanayoudhi imani ya dini.

SURA YA XV
MAKOSA KINYUME CHA UTU

132. ….. wa kubaka.


133. …. ya kubaka.
134. …. Kubaka.
Wasichana walio chini ya miaka kumi na sita….. la aibu kwa wanawake na kuwakashifu.
…msichana aliye chini ya miaka kumi na mbili.
… majuha na punguani.

5
138. Mume kunajisi mkewe aliye chini ya miaka kumi na mbili, n.k.
139. Ukuwadi.
140. Kufanya mwanamke anajisiwe kwa kuhofisha, n.k.
141. Mwenye nyumba kuruhusu kunajisiwa wasichana walio chini ya umri wa miaka
kumi na mbili nyumbani mwake.
142. Mwenye nyumba kuruhusu kunajisiwa wasichana walio chini ya miaka kumi na
sita nyumbani mwake.
143. Kuzuia kwa nia fulani au katika danguro.
144. Uwezo wa kupekua.
145. Kuishi juu ya chumo la umalaya.
146. Mwanamka anayesaidia umalaya.
147. Uwezo wa kupekua.
148. Madanguro.
149. Njama ya kunajisi.
150. Kutoa mimba.
151. Kutoa mimba kwa mwanamke mwenye mtoto.
152. Dawa ya vifaa vya kutolea mimba.
153. Kujua umri katika kuwafanyia makosa wanawake.
154. Makosa kinyuma cha maumbile.
155. Jaribio la kutenda makosa kinyume cha maumbile.
156. Shambulio la aibu kwa mtoto wa kiume chini ya miaka kumi na nne.
157. Matendo ya aibu baina ya wanaume.
158. Mwanamume kuzini na maharimu.
159. Amri ya uwalii.
160. Wanawake kuzini na maharimu.
161. Upambanuzi wa ndugu.
162. Idhini ya Mkurugenzi wa mashitaka wa Serikali.

SURA YA XVI
MAKOSA YANAYOHUSU NDOA NA LAZIMA ZA NYUMBANI

163. Ndoa ya hadaa.


164. Bigame (kuoa wake wawili au kuolewa na wanaume wawili).
165. Kufunga ndoa kwa njia ya hadaa.
166. Kutupa watoto.
167. Kupuuza watoto.
168. Kuacha kuwakimu watumishi au wakurufunzi.
169. Kuiba Watoto.

SURA YA XVII
ADHA NA MAKOSA KINYUMA CHA AFYA NA RAHA

170. Adha ya kawaida.


171. Nyumba za kamari.
172. Nyumba za kupingiana.

6
173. Bahati nasibu.
173A. Barua za msururu.
174. Mwekaji nyumba afafanuliwa.
175. Upitishaji wa matangazo ya kinyaa.
176. Wazembe na wakorofi.
176A. Kukaribisha Malaya wa kawaida.
177. Wahuni.
177A. Kuacha kueleza juu ya fedha zilichangishwa katika hadhara.
178. Uvaaji wa vazi rasmi bila mamlaka.
179. Kupuuza kuenea kwa maradhi.
180. Kughushi chakula.
181. Uuzaji wa chakula cha madhara.
182. Kughushi dawa.
183. Uuzaji wa dawa zilizoghushika.
184. Kuchafua maji.
185. Kuchafua hewa.
186. Biashara za makuruhu.

SURA YA XVIII
KUUMBUA

187. Ufafanuzi wa kashifa.


188. Kiumbuzi.
189. Tangazo.
190. Tangazo lisilo halali.
191. Kuruhusiwa kabisa.
192. Kuruhusiwa kwa sharti.
193. Nia njema.
194. Dhana ya nia njema.

Kigawe cha IV. – Makosa Juu ya Mtu

SURA YA XIX
KUUWA KWA KUNUWIA NA KUUWA BILA KUNUWIA

195. Kuuwa bila kunuwia.


196. Kuua kwa kunuwia.
197. Adhabu ya kuuwa kwa kunuwia.
198. Adhabu ya kuuwa bila kunuwia.
199. Hatia kwa kosa la kuuwa mwana mchanga katika baadhi ya kesi.
200. Nia ya uovu.
201. Kuuwa kwa kukasirishwa.
202. Kukasirishwa kunafafanuliwa.
203. Kusababisha kifo kunafafanuliwa.
204. Mtoto anapofikiriwa kuwa mtu.

7
205. Kikomo cha muda wa kifo.

SURA YA XX

WAJIBU KUHUSU KUHIFADHI MAISHA NA AFYA

206. Madaraka ya mtu mwenye uangalizi wa mtu mwingine.


207. Mkichwa wa ukoo.
208. Mtajiri wa kike na wa kiume.
209. Mtu afanyae shughuli za hatari.
210. Watu wanaoangalia vitu vya hatari.

SURA YA XXI

MAKOSA YAHUSIYO NA KUUWA KWA KUNUWIA NA KUJIUWA

211. Kujaribu kuuwa.


212. (Imebatilishwa).
213. Kuficha mauaji ya makusudi.
214. Kutishia kwa maandishi kuuwa kwa makusudi.
215. Njama ya mauwaji ya makusudi.
216. Kusaidia mtu mwingine ajiuwe.
217. Kujaribu kujiuwa.
218. Ufichaji wa kuzaliwa kwa watoto.
219. Kuangamiza watoto.

SURA YA XXII

MAKOSA YA KUHATARISHA MAISHA AU AFYA

220. Kudhofisha kwa nia ya kutenda kosa.


221. Kutia bumbuwazi kwa makusudi.
222. Vitendo vinavyokusudiwa kuleta dhara kubwa au kuzuia kukamatwa.
223. Kumzuia mtu asijiokoe katika mavunjiko ya chombo.
224. Kuhatarisha wasafiri wa reli.
225. Dhara kubwa.
226. Kuweka baruti kwa makusudi.
227. Kulisha sumu.
228. Kujeruhi bila halali ya kusumisha.
229. Kukosa kutoa vitu vya lazima.
230. Jukumu kuhusu utibabu wa kupasua.
231. Jukumu la jinai.
232. Kidakizo (exception).

8
SURA YA XXIII
KUTOJALI NA KUPUUZA KWA JINAI

233. Matendo ya kutojali na kupuuza.


234. Matendo mengine ya kupuuza yaletayo dhara.
235. Kutumia vitu vya sumu kwa kupuuza.
236. Kuhatarisha wasafiri wa relini.
237. Kuonyesha taa ya uwongo.
238. Chombo kilichozidi shehena na kisicho usalama.
239. Kuzuia njia ya Serikali au njia ya meli.

SURA YA XXIV
MASHAMBULIO

240. Shambulio la kawaida.


241. Mashambulio yaletayo dhara ya mwili.
242. Kushambulia mtu alindaye chombo kilichovunjika.
243. Mashambulio yenye adhabu ya kifungo cha miaka mitano.

SURA YA XXV
MAKOSA JUU YA UHURU WA WATU

244. Kunyakuwa mtu kutoka Tanganyika.


245. Kunyakua mtu kutoka kwa muangalizi wake.
246. Kupoka.
247. Adhabu kwa kunyakua.
248. Kunyakua au kupoka ili kuuwa.
249. Kunyakuwa au kupoka kwa dhamiri ya kufungia.
250. Kunyakua kwa dhamiri ya kuleta madhara.
251. Kumficha bila halali mtu aliyenyakuliwa.
252. Kunyakua mtoto kwa dhamiri ya kumuiba.
253. Adhabu kwa kumfungia mtu bila halali.
254. Kununua au kumsarifu mtu kama mtumwa.
255. Biashara ya utumwa.
256. Kazi za kulazimishwa.

Kigawe cha V. – Makosa kuhusu Mali

SURA YA XXVI
WIZI

257. Vitu viwezavyo kuibika.


258. Ufafanuzi wa wizi.
259. Mambo maalumu.

9
260. Fedha iliyozuiwa kwa dhamana au kwa maagizo Fulani.
261. Maajenti wa uuzaji.
262. Fedha iliyopokewa kwa ajili ya mtu mwingine.
263. Wizi wa mmiliki.
264. Mume na Mke.
265. Adhabu ya kawaida kwa wizi.
266. Kuiba wasia.
267. Kuiba kitu kilichotiwa posta.
268. Kuiba mifugo.
269. Kumuibia mtu, kuiba bidhaa inayosafirishwa, n.k.
270. Kuiba kwa watumishi wa Serikali.
271. Kuiba kwa makarani na watumishi.
272. Kuiba kwa wakurugenzi na maafisa wa kampuni.
273. Kuiba kwa ajenti.
274. Kuiba kwa wapangaji au wafikiaji.
275. Kuiba baada ya kuwa na makosa zamani.
276. Kuficha madaftari.
277. Kuficha wasia.
278. Kuficha hati.
279. Kuuwa wanyama kwa dhamira ya kuiba.
280. Kutunga kwa kusudi la kuiba.
281. Kuarifu kwa udanganyifu vitu vilivyowekwa rahani.
282. Kushughulika na madini machimboni kwa hadaa.
283. Kujipa uwezo kwa hadaa.
284. Kuhawilisha kusikofikia wizi.

SURA YA XXVII
MAKOSA YALIYO SAWA NA WIZI

285. Ufafanuzi wa ungang’anyi.


286. Adhabu ya unyang’anyi.
287. Kujaribu kunyang’anya.
288. Kushambulia kwa kusudi la kuiba.
289. Kudai mali kwa maandishi ya vitisho.
290. Kutishia kushtaki juu ya jinai kwa kusudi la kutoza kwa nguvu.
291. Kupata utumilizaji wa mkataba kwa nguvu.
292. Kudai mali kwa vitisho kwa kusudi la kuiba.

SURA YA XXIX
UVUNJAJI WA NYUMBA USIKU, UVUNJAJI WA NYUMBA MCHANA NA
MAKOSA SAWA NA HAYO

293. Ufafanuzi wa kuvunja na kuingia.


294. Kuvunja na kuingia nyumba ya kukaa watu kwa dhamiri.
295. Kuingia nyumba ya kukaa watu kwa dhamiri.
296. Kuvunja nyumba na kuingia na kutenda kosa kubwa.

10
297. Kuvunja na kuingia nyumba kwa dhamiri.
298. Kuwa na silaha kwa dhamiri ya kutenda kosa kubwa.
299. Jinai ya kuingilia bila idhini.
300. Kuhodhi.

SURA YA XXX
KUJISINGIZIA

301. Ufafanuzi wa kujisingizia.


302. Kupata bidhaa kwa kujisingizia.
303. Kupata kutimilizwa kwa dhamana kwa kujisingizia.
304. Kudanganya.
305. Kupata kuaminiwa kwa kujisingizia.
306. Njama ili kudanganya.
307. Udanganyifu juu ya uuzaji au rahani ya mali.
308. Kujifanya mpiga ramli.
309. Kupata kuandikishwa kwa kujisingizia.
310. Matamshi ya uwongo ya hati ya safari.

SURA YA XXXI
KUPOKEA MALI ILIYOIBWA AU ILIYOPATIKANA BILA HALALI NA
MAKOSA KAMA HAYO

311. Kupokea mali ya wizi au iliyopatikana bila halali.


312. Kukabidhisha mali iliyotuhumiwa kuibiwa.
312A. (1) Uwezo wa waziri kutangaza alama za vifaa vya Serikali.
(2) Kuwa na vifaa vya Serikali au vya idara ya Reli bila halali.
(3) Kuwa na vifaa vya kijeshi bila halali.
(4) Tafsiri.
313. Kupokea bidhaa iliyoibiwa nje ya Tanganyika.

SURA YA XXXII
UDANGANIFU WA WADHAMINI NA WATU WA KAZI ZA MUAMANA NA
HESABU ZA UWONGO

314. Kuhawilisha kwa hadaa kwa wadhamini.


315. Kuchukua mali kwa udanganyifu kwa wakurugenzi na maofisa wa Shirika n.k.
316. Matangazo ya uwongo juu ya makampuni, n.k.
317. Kughushi hesabu kwa makarani.
318. Kughushi hesabu kwa mtumishi wa Serikali.

Kigawe cha VI. – Kuharibu Mali kwa uhasidi

11
SURA YA XXXIII
MAKOSA YALETAYO UHARIBIFU WA MALI

319. Kuitia moto.


320. Kujaribu kutia moto.
321. Kutia moto mazao na mimea iotayo.
322. Kujaribu kutia moto mazao, n.k.
323. Kupeperusha vyombo.
324. Kujaribu kupeperusha vyombo.
325. Kujeruhi wanyama.
326. Uharibifu mwingine wa mali; adhabu maalum na za jumla.
327. Kujaribu kuharibu mali kwa baruti.
328. Kupelekea wanyama maradhi ya kuambukiza.
329. Kuondoa alama za mipaka.
330. (Imebatiliswa).
331. Kuharibu kazi za reli.
332. Vitisho vya kutia moto au kutekeeteza.

Kigawe cha VII. – Maandishi ya Kubuni, Utengenezaji sarafu na makosa sawa na hayo

SURA YA XXXIV
MAFAFANUZI

333. Ufafanuzi wa maandishi ya kubuni.


334. Hati.
335. Ufanyaji wa hati ya uwongo.
336. Kusudi la kudanganya.

SURA YA XXXV
ADHABU KWA KUBUNI MAANDISHI

337. Adhabu ya kawaida kwa maandishi ya kubuni.


338. Kubuni kwenye adhabu ya kifungo cha maisha.
339. Kubuni hati ya kimahakama au ya Serikali.
340. Kubuni kwenye adhabu ya kifungo cha miaka saba.
341. Kutengeneza au kuwa nazo karatasi za kubunia.
342. Kutoa hati za uwongo.
343. Kutoa hati zilizofutwa au zilizomalizika muda.
344. Kupata utimilizaji wa hati kwa kujisingizia.
345. Kufuta michanjo katika cheki.
346. Kuandika hati bila ruhusa.
347. Kudai mali kwa nyaraka za wasia za uwongo.
348. Kununua noti za kubuniwa.
349. Kughushi hati za kupatia fedha.
350. Kughushi daftari.
351. Shahada ya uwongo ya ndoa.

12
352. Maelezo ya uwongo kwa kuandikisha.

SURA YA XXXVI
MAKOSA YAHUSUYO SARAFU
353. Mafafanuzi.
354. Kubuni sarafu.
355. Matayarisho ya kutengeneza sarafu.
356. Kupunguza sarafu.
357. Kuyeyusha sarafu.
358. Kuzuia na kuharibu sarafu ya kubuni.
359. Kuwa na vikato.
360. Kutoa sarafu ya kubuni.
361. Kukariri utoaji.
362. Kutoa nishani au madini kuwa ni sarafu.
363. Kusafirisha sarafu ya kubuni.
364. Kuhodhi.

SURA YA XXXVII
MIHURI YA KUBUNI

319. Kuwa na kihesi (die) cha kufanyia mihuri.


320. Kuwa na karatasi za kutengenezea stampu za posta.

SURA YA XXXVIII
KUBUNI ALAMA ZA BIASHARA

321. Alama za biashara zafafanuliwa.


322. Kubuni alama za biashara ni kosa dogo.

SURA YA XXXIX
KUJIFANYA MTU MWINGINE

323. Adhabu ya jumla ya kujifanya mtu mwingine.


324. Kukubali kwa uwongo.
325. Kujifanya mtu aliyetajwa katika shahada.
326. Lazima hati ya shahada kwa kujifanya mtu mwingine.
327. Kujifanya ni mtu aliyetajwa katika shahada ya sifa.
328. Lazima shahada ya sifa.

13
SURA YA XL
TUME ZA SIRI

329. (Zimebatilishwa)

Kigawe cha VIII. – Majaribio, Njama za Kutenda Uhalifu, Mfichaji Uhalifu

SURA YA XLI
MAJARIBIO

330. Jaribio linafafanuliwa.


331. Adhabu ya jumla kwa majaribio.
332. Adhabu kwa kujaribu kutenda baadhi ya makosa makubwa.
333. Kupuuza kuzuia utendaji wa kosa kubwa.

SURA YA XLII
NJAMA
334. Njama ya kutenda kosa kubwa.
335. Njama ya kutenda kosa dogo.
336. Njama nyinginezo.

SURA YA XLIII
WAFICHA UHALIFU

337. Mficha uhalifu afafanuliwa.


338. Adhabu kwa waficha uhalifu wa makosa madogo.

SURA YA XLIV
USHAWISHI WA UCHOCHEZI

339. Kushawshi au kuchochea utendaji wa kosa.

14
SURA YA 16
______

KANUNI YA ADHABU
______

Sheria ya kuweka Kanuni ya Sheria ya JinaI


[28TH SEPTEMBER, 1945]
______

SEHEMU YA I
MASHARTI YA KAWAIDA
_______

SURA YA I
UTANGULIZI

Jina fupi Sh. ya 1. Sheria hii iitwe Kanuni ya Adhabu na baada ya hapa itakuwa
1945 No.21 f.2
ikitajwa “Kanuni hii”.

Kazi yake 2. Toka Kuanzia kwake Kanuni hii na baadaye, ile Kanuni ya
badala ya
Kanuni ya Adhabu ya bara Hindi itakoma kutumika nchini Tanganyika. Habari yoyote
adhabu ya Bara kuhusu sharti lolote liliyomo kwenye Kanuni ya Adhabu ya Bara Hindi juu
Hindi ya Sheria yoyote iliyoko mnamo tarehe ya kuanzi Kanuni hii, kwa kadri
yatakavyolingana maelezo yake, itafikiriwa kuwa ni sawa na sharti liliyomo
ndani ya kanuni hii.

Kuepusha 3. Ndani ya Kauni hii hakuna kitakachoathiri –


Sheria kadha
Sh. 1955 No. (1) kupasiwa, kuhukumiwa au kupewa adhabu mtu kwa kosa
49 f.2 C.A. Act ambalo ni kinyume cha Sheria ya kawaida au kinyume cha
2 f.3 Sheria nyengineyo yoyote itumiwayo nchini Tanganyika
isiyokuwa kanuni hii; au
(2) kupasiwa mtu kuhukumiwa au kupewa adhabu kwa kosa
ambalo liko chini ya masharti ya Sheria yoyote iliyoko nchini
Tanganyika ambayo yahusika na mamlaka ya mahakama za
mitaa kuhusu vitendo ambavyo vimetendwa nje ya mamlaka ya
kawaida ya mahakama hizo; au
(3) uwezo wa mahakama yoyote kumpa adhabu mtu kwa sababu ya
kuidharau mahakama hiyo; au
(4) kupasiwa au kuhukumiwa mtu au kutolewa adhabu kwa mtu
ambaye yuko chini ya hukumu iliyokwishatolewa au
itakayotolewa, kuhusu kitendo chochote kilichokwishatenda au
kilichoanzishwa kutenda kabla ya kuanzishwa kwa kanuni hii;
au
(5) uwezo wowote wa Rais kutoa msamaha wowote au kupunguza
adhabu au kubadilisha adhabu yote au sehemu ya adhabu au

15
kuahirisha utimizaji wa hukumu yoyote iliyokwishatolewa au
itakayotolewa; au
(6) mojawapo ya sheria yoyote au vifungu vyovyote vya sheria hizo
wakati vitumikapo kwa ajili ya Jeshi la Vita la Serikali ya
Tanganyika au katika jeshi lolote la Polisi ambalo limewekwa na
sheria.
Isipokuwa kwamba iwapo mtu ametenda kosa ambalo laweza
kutolewa adhabu chini ya kanuni hii na pia laweza kutolewa adhabu
chini ya sheria nyingineyo au sheria mojawapo ya namna hizo
zilizokwishatajwa katika fungu hili, mtu huyo hatapewa adhabu kwa
kosa hilo chini ya sheria au amri hiyo na vile vile chini ya kanuni
hii.
Angalia – Sheria ya 1963 No. 29 Mafungu 4 na 5 yanatoa masharti juu ya
chanzo cha adhabu ya kifungo na kutandikwa kwa makosa na majaribio ya
kutenda makosa kinyume cha mafungu 265, 268, 270, 271, 286, 294, 296
na 311 au Sura uya 16.

SURA YA II
TAFSIRI

Kanuni ya 4. Kanuni hii itatafsiriwa kwa kufuata misingi ya tafsiri ya sheria


kawaida ya
tafsiri ya sheria iliyoko Uingereza, na, isipokuwa ikielezwa kwa vingine, msemo
utakaotumiwa ndani ya kanuni hii, kwa kadri itakavyolingana na maelezo
yake, utachukuliwa kuwa na maana uliyo nayo katika sheria ya jinai ya
Uingereza na utafahamika kwa kufuata maana hiyo.

Tafsiri C.A. 5. Katika kanuni hii, isipokuwa ikielezwa vyengine -


Act 2 ss. 8 na
36 Act 1964 "mahakama" maana yake mahakama yenye mamlaka kamili;
No. 16 "nyumba ya kuishi" inachanganya nyumba yoyote au jengo lolote na
Nyongeza ya 2 sehemu ya nyumba hiyo au jengo ambalo kwa wakati uliopo
latumiwa na mwenyewe au na mpangaji wake kwa ajili ya kuishi
ndani humo, yeye mwenyewe, jamaa yake au watumishi wake au
yeyote katika hao, na haidhuru iwapo wakati mwingine huwa
halikaliwi; nyumba au jengo linaloambatana au linalotumiwa na
nyumba ya kuishi linahesabiwa kuwa ni sehemu ya nyumba ya
kuishi iwapo kuna ukifiano kati ya nyumba hiyo au jengo hilo na
nyumba ya kuishi, iwe ufikiano wa kuelekeana milango au njia ya
ndani kwa ndani itokayo kumoja mpaka kwengine; lakini isiwe
vyenginevyo;
"kosa kubwa" maana yake ni kosa ambalo limetamkwa na sheria ni kosa
kubwa au ikiwa halikutamkwa kuwa ni kosa dogo ambalo laweza
kutolewa adhabu ya kifo au kifungo cha miaka mitatu au zaidi bila
ya kuthibitisha kwa kuwepo makosa ya zamani;
"dhara" maana yake ni maumivu yoyote ya mwilini, maradhi au mchakuko,
uwe wa aushi au wa muda;
"dhara ya hatari" maana yake ni dhara inayohatarisha maisha;

16
"dhara kubwa" maana yake ni dhara yoyote ambayo yafikia kulemaza aushi
au ambayo huenda ikadhuru afya kuleta kilema cha aushi au kuleta
jeraha lolote la aushi au baya sana kwenye sehemu yoyote ya nje au
ndani ya mwili, kiungo au akili;
"shauri la mahakama" lachanganya shauri lolote ambalo lapelekwa mbele
ya mahakama yoyote, baraza, tume ya upelelezi, au mbele kwa
kiapo, au shauri litakalopelekwa katika baraza au mbele ya baraza la
wenyeji, liwe baraza hilo lachukua ushahidi kwa kiapo au sivyo;
"kwa kujua" hutumiwa kuhusu neno lolote ambalo laonyesha utoaji au
utumiaji, huonyesha hali ya kujua namna ya kitu hicho
kilichotolewa au kutumiwa;
"utawala wa mitaa” maana yake ni utawala wa mitaa ambao umewekwa
kwa mujibu wa sheria yoyote;
"kulemaza" maana yake kuiharibu au kutomwezesha aushi sehemu yoyote
ya nje au ya ndani ya mwili, kiungo au akili;
"kosa dogo" maana yake ni kosa lolote ambalo si …………………..
"fedha" inachanganya nyaraka za benki, noti za sarafu cheki na nyaraka
nyinginezo zozote au …………….fedha;
"usiku" au"wakati wa usiku" maana yake ni kile …………. moja magharibi
na saa kumi na mbili asubuhi.
“kosa” maana yake ni kitendo, jaribio au kuto……… kutolewa adhabu ya
sheria;
“mtu” na “mwenyewe” na maneno mengine kama ……kuhusu mali
yanachanganya shirika za namna …. Kingine chochote cha watu
wawezao kumiliki yatumiwapo hivyo, yanachangana na Jamhuri;
“mtumishi wa Serikali’ maana yake ni mtu yeyote ….mojawapo yoyote ya
ofisi zifuatazo au ambaye ofisi hizo, iwe kwa niaba ya mwengine
au ….
(i) afisi yoyote ya serikali kuchanga na …afisi yoyote ambayo
uwezo wa kuajiri mtu au kumtoa mtu kazini umepewa Rais au
…au Halmashauri; au
(ii) afisi yoyote ambamo mtu ameajiriwa au ame…… au sheria ya
Serikali; au
(iii)afisi yoyote ya Serikali ambayo uwezo wa kufanya kazi humo
au kumtoa umepewa watu wowote wenye kushika afisi ya
namna afisi mojawapo ya zile afisi zilizotajwa kati ……..
zilizotangulia za fungu hili; au
(iv) afisi yoyote ya muamuzi au mpatanishi kat……. Jambo lolote
lililopelekwa ili lipatanishwe lifany… kwa idhini ya mahakama
yoyote au kwa .. yoyote;
na zaidi ya hayo neno hilo pia lachanganya –
(i) mlinzi wa amani;
(ii) mjumbe wa tume ya kutafiti iliyoteuliwa … yoyote au kwa
kufuata Sheria yoyote;
(iii)mtu yeyote iliyeajiriwa kutimiliza utoaji wa ……. Mahakama,
pamoja na baraza la kienyeji;

17
(iv) watu wote waliomo katika jeshi la vita la …. Watumishi wote
wa Huduma ya Taifa;
(v) watu wote wafanyakazi katika idara yoyote ya ………
(vi) mtu ambaye ni mwalimu wa dini ya madhehebu …..mdhali
ashughulika na kazi zinazohusu taarifa ………. Kufunga ndoa
kwenyewe au zinazohusu ufanyaji …..wa daftari ya shahada
zozote za ndoa, uzazi, ……. Au mazishi, lakini si za kuhusu
jambo lolote ……..
(vii) mjumbe wa manispali;
(viii) muajiriwa katika utawala wa mitaa;
“kuwa na” (a) “iwe nacho” au “kuwa nacho’ si tu kwamba ….. na kitu
mikononi mwake mwenyewe bali pia kwachan…..hali ya kujua,
kuwa na kitu chochote mikononi mwingine yeyote au chini ya
ulinzi wa mtu huyo, au …….
…mahali popote (ikiwa ni mali yake, au chakaliwa naye au … kwa ajili ya
matumizi au faida yake au ya mtu mwingine …..(b) iwapo kuna watu
wawili au zaidi na mmoja kati yao …zaidi ya mmoja wao, kwa kujulikana
na kwa idhini ya wale wengine anacho au wanacho kitu chcohcote chini ya
ulinzi wake ulinzi wao au mikononi mwake au mikononi mwao,
huhesabiwa kchukuliwa kuwa kimo chini ya ulinzi na mikononi mwa kila
mmoja katika wao;
……. inachanganya kila kitu chenye uhai na kisicho uhai ambacho
kinaweza kumilikiwa;
….haina maana tu ya watu wote waliomo Tanganyika, lakini pia .. maana
ya watu wakaao au watumiao mahali popote mahsusi, …… idadi yoyote ya
watu kama hao na pia watu wasiojulikana …. Waweza kuhusika na maana
ya neo hili kwa namna utakavyotumiwa;
… serikali’ inachanganya njia yoyoe ipitwayo, mahali pa soko, … barabara,
daraja au njia nyingineyo ambayo ni halali kutumiwa na watu;
….pa hadhara” au “nyumba ya hadhara” inachanganya njia yoyote ya
kupita watu na nyumba yoyote, mahali au chombo chochote cha kusafiria
ambacho, kwa wakati huo, watu wana haki … wanaruhusiwa kuingia ama
bila ya sharti au kwa sharti la kulipa chochote, na jengo lolote au mahali
ambapo kwa wakati ule anatumiwa kwa ajili ya mikutano ya hadhara au ya
kidini, au … mkusanyiko au mahakama ya hadhara;
… likitumiwa kuhusu vitendo vinavyotendwa lina maana (a) kwamba
vyatendwa mahali popote pa hadhara ambapo vyaweza kuonekana na mtu
yeyote awe au asiwe mtu huyo katika mahali pa hadhara; au (b) kwamba
vyatendwa mahali popote pasipokuwa pa hadhara ambapo huenda
vikaonekana na mtu yeyote aliyeko mahali pa hadhara;
… ina maana ya Sheria ya Bunge la Uingereza au Sheria ya Bunge la Bara
Hindi na inachanganya amri zozote, kanuni, sheria, … za mji au sheria
nyinginezo ndogo ndogo zilizofanywa au kupitishwa chini ya mamlaka ya
Sheria yoyote ya Bunge la …….
…….. kunachanganya, kukitumia au kukishughulikia na kujaribu kutumia
au kukishughulikia na kujaribu kumshawishi mtu yeyote …

18
kukishughulikia au kukitenda hicho kitu chenyewe;
………muhimu: inachanganya hati yoyote ambayo ni mali ya mtu ………
na ambayo ni ushahidi wa kimiliki mali yoyote au yenye ………. Ya kudai
au kupokea mali yoyote.
“………..” kinachanga meli, mashua na kila namna ya chombo
kutumiwacho kwa kusafiria baharini au maji ya bara na inachanga ndege;
………….. mana ya mchanjo wowote au kutoboka ambako …………….
kwatia tundu sehemu yoyote nje ya mwili, na kwa ……….. ufafanuzi,
sehemu ya nje ya mwili ni sehemu yoyote ya ……….. ambayo yaweza
kuguswa bila ya kuchanjwa au kutobolewa.

SURA YA III
KUTUMIKA KWA KANUNI HII NCHINI

Kuenea kwa 6. Kwa makusudi ya Kanuni hii, mamlaka ya mahakama za


mamlaka ya
mahakama za Tanganyika yanaenea kila mahali katika Tanganyika au ndani ya maili tatu
mwanzo za pwani ya bahari yake zikipimwa kutoka alama ya maji kupwa.

Makosa 7. Iwapo kitendo kimetendwa ndani ya mamlaka ya mahakama na


yatendwayo
kuhusu ndani ambacho ni kosa kwa kufuata Kanuni hii, ikiwa baadhi ya kitendo hicho
yam ala na kimetendwa ndani ya mamlaka na baadhi yake nje ya mamlaka, kila mtu
nusu nje ya ambaye ametenda kitendo hicho chote au baadhi yake ndani ya mamlaka
mamlaka
ataweza kuhukumiwa na kupewa adhabu chini ya Kanuni hii kwa namna ile
ile kama kwamba kitendo kile chote kilitendwa ndani ya mamlaka hayo.

SURA YA IV
KANUNI ZA KAWAIDA KUHUSU JUKUMU YA JINAI

Kutojua sheria 8. Kutojua sheria hakuwi ni udhuru wowote kwa kutenda au


kutotenda kokote ambako pengine kungefanya kosa ila iwapo ujuzi wa
sheria kwa mkosaji umetamkwa wazi wazi kwamba ndicho kiini cha kosa
hilo.

Dai la haki kwa 9. Mtu hawi na jukumu ya jinai kwa ajili ya kosa lihusikalo na mali,
uaminifu
iwapo kitendo alichotenda au alichoacha kukitenda kwa ajili ya mali hiyo
alitenda ili kutimiza dai la haki kwa uaminifu na bila ya kusudio la
kudanganya.

Kusudio: 10. Kwa kufuata masharti yaliyoelezwa ya Kanuni hii kuhusu


sababu
kutenda au kutotenda kwa kupuuza, mtu hawi mwenye jukumu ya jinai kwa
kutenda au kutotenda ambako kumetuka bila ya kusudi la kutimiza nia
yake, au kwa tukio ambalo latukia kwa ajali:
Isipokuwa kwamba nia ya kusababisha tokeo Fulani yatamkwa wazi
wazi kuwa ndio kiini cha kosa ambalo limetendeka, kwa kutenda au
kutotenda, kwa ukamilifu au kwa baadhi, basi tokeo lilokusudiwa kwa
kutenda au kutotenda halidhuru.

19
Isipokuwa imetamkwa vingine wazi wazi, hiyo sababu ambayo
imemshawishi mtu kutenda au kuacha kutenda kitendo au kuleta nia sababu
hiyo hadhuru kitu kuhusu jukumu ya jinai.

Kukosea 11. Mtu ambaye atenda au aacha kutenda kitendo akiwa na imani
hakika
kamilifu na ya kukubalika, lakini kwa kukosea, kuhusu kuwapo kwa au
kutotenda kwake kutakakozidi hali ya mambo au kama ingelikuwa kama
alivyoamini.
Kutumika kwa kanuni hii kwaweza kuondolewa na masharti
yatakayotamkwa wazi au yatakayofahamika ya sheria kuhusu kanuni hii.

Kudhaniwa 12. Kila mtu anadhaniwa kwamba akili zake ni timamu, na kwamba
kuwa na akili
timamu ana akili timamu wakati wo wote ule mpaka itibitishwe kinyume cha hivyo.

Wenda wazimu 13. Mtu hawi na jukumu ya jinai kwa kutenda au kutotenda iwapo
wakati akitenda kitendo hicho au akiacha kukitenda yumo ndani ya hali ya
ugonjwa wo wote wa kuathiri akili yake na hawezi kujua kwamba hapasiwi
kutenda au kutotenda kitendo hicho.
Lakini mtu aweza kuwa na jukumu ya jinai kwa kutenda au kutotenda
ingawaje akili yake iliharibika kwa maradhi, iwapo maradhi yenyewe
hayamletei mojawapo katika shida zilizotajwa juu kuhusu kutenda au
kutotenda.

Kulewa 14.- (1) Isipokuwa kama yalivyo masharti ya fungu hili kulewa
haitakuwa utetezi katika kosa lo lote la jinai.
(2) Kulewa kutakuwa utetezi kwa shtaka lo lote la jinai iwapo
kwa sababu ya kulewa huko mshtakiwa wakati wa kitendo au kutotendeka
kulikolalamikiwa alikuwa hajui atendalo na–
(a) hali ya kulewa hiyo ililetwa bila ya hiari yake kwa kitendo
kiovu au cha kupuuza cha mtu mwingine; au
(b) kwa sababu ya ulevi akili ya mshatakiwa iliharibika kwa muda
au vinginevyo, wakati wa kitendo hicho au kutotendeka huko.
Sura 20 (3) Iwapo utetezi chini ya fungu lililotangulia umethibitika basi
kesi inayoangukia kwenye fasili yake ya (a) mshtakiwa ataruhusiwa na
katika kesi inayoangukia kwenye fasili (b) masharti ya kanuni hii na ya
Kanuni ya Mwenendo wa Jinai kuhusu wenda wazimu yatatumika.
(4) Kulewa kutafikiriwa kwa ajili ya kukata shauri kama
mshtakiwa alileta nia yoyote halisi au vinginevyo, ambayo kama
isingekuwapo asingelikuwa mkosaji.
(5) Kwa ajili ya fungu hili kulewa kutafikiriwa kuwa
kwachanganya hali inayoletwa na dawa ya kupoteza akili (nakotiki) au
madawa mabaya yanayolevya.

Umri mchanga 15. Mtu mwenye umri wa chini ya miaka saba hana jukumu ya jinai
kwa kutenda au kutotenda lolote.
Mtu mwenye umri wa chini ya miaka kumi na mbili hana jukumu ya

20
jinai kwa kitendo au kutotendeka, ila ithibitishwe kwamba wakati wa
kutenda au kuacha kutenda kitendo hicho aliweza kujua kwamba hapaswi
kukitenda au kuacha kukitenda -
Mtu mwenye umri wa chini ya miaka kumi na mbili anafikiriwa
kuwa hawezi kuundama.

Maafisa wa 16. Isipokuwa kama masharti yalivyoelezwa na Kanuni hii, afisa


mahakama
wa mahakama wa aina yoyote hana jukumu ya jinai kwa jambo lolote
lililotenda au lililoachwa kutenda naye katika kutimiza kazi zake zihusuzo
mahakama ingawaje kitendo hicho kilichotenda kimepitukia mamlaka yake
ya kimahakama au ingawa alilazimika kutenda kitendo kilichoachwa
kutendwa.

Lazima 17. Mtu hana jukumu ya jinai kwa kosa iwapo kosa hilo limefanya
na wakosaji wawili au zaidi, naiwapo kitendo hicho kimetendwa au
kimeachwa kutendwa kwa sababu tu kwamba katika wakati wote ambao
kitendo hicho kikitendeka au kikiachwa kutendwa mtu huyo analazimishwa
kukitenda au kuacha kukitenda kwa vitisho vya mkosaji mwingine au
wakosaji wengine vya kumuuwa papo hapo au kumtia dhara ya maumivu
makuu mwilini iwapo atakataa; lakini vitisho vya kumuumiza baadaye
haviwi ni udhuru wa kosa lolote.

Kutetea nafsi 18. Kwa kufuata masharti yaliyoelezwa katika Kanuni hii au sheria
au mali
nyingineyo yoyote itumikayo Tanganyika, jukumu ya jinai kwa utumiaji wa
nguvu katika kumtetea mtu au mali itaamuliwa kwa mujibu wa misingi ya
sheria ya Kiingereza.

Utumiaji wa 19. Iwapo mtu yeyote anashtakiwa kwa kosa la jinai litokanalo na
nguvu katika
kukamata kukamata ua kujaribu kumkamata mtu ambaye anapinga kukamatwa kwa
kutumia nguvu au anajaribu kuepuka kukamatwa, katika ku… kama njia
zilizotumiwa au kiasi cha nguvu kilichotumiwa ili kumkamata mtu huyo
kilikuwa cha kufaa, mahakama itafikiria uzito wa.. ambalo lilikuwa
limefanywa au likifanywa na mtu huyo na jinsi .. kosa hilo lilikuwa
limefanya au likifanywa na mtu huyo.

Kulazimishwa 20. Mwanamke aliyeolewa haepukwi na jukumu ya jinai kutenda au


na mume
kutotenda kitendo kwa sababu tu kwamba kutendeka kutotendeke huko
kunafanyika mbele ya mumewe, lakini kwenye .. juu ya mke kwa kosa
lolote lisilokuwa la uhaini au la kuuwa … utetezi wa kufaa kuthibitisha
kwamba kosa hilo lilifanywa mbele ya mumewe na kwa kulazimishwa
naye.

Mtu asipewe 21. Mtu hatapewa adhabu mara mbili, ama kwa kufaata ma… ya
adhabu mara
mbili kwa kosa kanuni hii au kwa kufuata masharti ya sheria nyingine yoyoe .. kosa moja.
moja Sheria
1955No. 49 f.3

21
SURA YA V
WASHIRIKI WA MAKOSA

Wakosaji 22. Iwapo kosa limetendwa, kila mmoja wa watu wafuatao


wakuu
atahesabiwa kwamba ameshiriki katika kutenda kosa hilo na kuwa …. Wa
kosa hilo na aweza kushtakiwa kwamba amelitenda hasa,… kusema –
(a) kila mtu ambaye atenda au ambaye aacha kutenda kitendo
ambacho kinafanya kosa hilo;
(b) kila mtu ambaye atenda au ambaye aacha kutenda kitendo
chochote kwa ajili ya kumuwezesha au kumsaidia mtu
mwingine kufanya kosa hilo.
(c) Kila mtu ambaye amsaidia mtu mwingine katika kufanya kosa
hilo;
(d) Mtu yeyote ambaye amshauri au kumfanya mtu mwingine ye
yote atende kosa hilo kuhusu kifungu kilichotajwa mwisho
aweza kushtakiwa kwa kufanya kosa hilo au kwa kushauri kwa
kufanya litendwe kosa hilo.
Kuonekana na hatia ya kushauri au ya kufanya kosa litendwe
kutaleta matokeo yale yale katika hali zote kama kuonekana na hatia ya
kulifanya kosa hilo.
Mtu ye yote ambaye amfanya mtu mwingine kutenda au kutotenda
kitendo cho chote cha namna ambayo, kama yeye mwenyewe angekitenda
au angeacha kukitenda, kutenda au kutotenda huko kungeleta kosa upande
wake, mtu huyu ni mkosaji wa kosa la namna hiyo hiyo na pasiwa adhabu
ile ile kama kwamba yeye mwenyewe ametenda au ameacha kutenda
kitendo hicho; na anaweza kushtakiwa kwa kutenda au kutotenda.

Makosa 23. Iwapo watu wawili au zaidi wanafanya nia moja ya kutumiza
yanayofanywa
na wakosaji kusudio lisilo halali kwa kuungana mmoja na wengineo na katika kutimiza
walioshikiana kusudio hilo kosa latendeka la namna ambayo kutendeka kwake yamkini
katika kutimiza kulikuwa ni tokeo la kutimiwa kwa kusudio hilo, basi kila mmoja wao
kusudio moja
atahesabiwa kwamba ni mtendaji wa kosa hilo.

Kumshauri 24. Iwapo mtu anamshauri mtu mwingine kufanya kosa, baadaye
mwingine
afanya kosa kosa hilo likafanywa hasa na huyo anayeshauriwa

SURA YA VI
ADHABU

Namna mbali 25. Adhabu zifuatazo zaweza kutolewa na mahakama:–


mbali za adhabu
(1) Kifo.
(2) Kifungo.
(3) Kutandikwa.
(4) Kutoza faini.
(5) Kuhodhi.
(6) Malipo ya fidia.

22
(7) Kutaka dhamana kwa kutunza amani na kuwa na tabia njema,
au kwa kuhudhuria kupewa hukumu.
(8) Adhabu nyingineyo yoyote inayotolewa na Kanuni hii au
sheria nyingineyo yoyote au amri.

Hukumu ya Kifo 26.-(1) Iwapo mtu yeyote amehukumiwa kifo, hukumu itaamuru
kwamba mtu huyo aning’inizwe kwa kitanzi shingoni mpaka awe
amekufa.
Sura 455 f.16 (2) Hukumu ya kifo haitatamkwa au kuandikwa juu ya mtu
yeyote ambaye, kwa maoni ya mahakama, mtu huyo ni wa chini ya umri
wa miaka kumi na nane, lakini badala yake mahakama itamuhukumu mtu
huyo awekwe kizuizini mpaka atakapotaka Rais, na ikiwa atahukumiwa
hivyo atapasiwa kuzuwiwa mahali ambapo kwa masharti ambayo Waziri
aliyepo mwenye madaraka ya mambo ya sheria ataamuru, na awapo
kizuwizini hivyo atahesabiwa kuwa yumo katika ulinzi wa halali.
(3) Iwapo mtu amehukumiwa kuwekwa kizuizini mpaka
atakapotaka Rais kwa mujibu wa kifungu cha mwisho kilichotangulia,
Kadhi anayehukumu atampelekea Waziri aliyepo mwenye madaraka ya
mambo ya sheria nakala ya maandishi ya ushahidi uliochukuliwa naye
ikiwa na mapendekezo au maoni yake juu ya shauri hilo kama
atakavyoona yafaa kufanya.

Kifungo 27.-(1) [Imeachwa kwa sababu ya f.3 la Sura 357.]


(2) Mtu atakayepasiwa kifungo cha maisha au cha muda
mwingine wowote aweza kuhukumiwa kifungo kwa muda mfupi zaidi ya
huo.

Adhabu ya 28. Iwapo katika kanuni hii yaamriwa kwamba mtu yeyote
kutandikwa
atapasiwa kupata adhabu ya kutandikwa, apewapo adhabu hiyo, adhabu
hiyo atapewa kwa kufuata masharti ya Sheria ya Adhabu ya Kutandikwa..

Sura 17 Faini 29. Iwapo hukumu ya faini imetolewa chini ya sheria yoyote, basi
pakikosekana masharti yaliyo wazi kuhusu faini hiyo katika sheria hiyo
masharti yafuatayo yatatumika:–
(i) Iwapo hakuna kiasi kilichoelezwa kwamba faini hiyo yaweza
kukomea, basi kiasi cha faini ambacho chaweza kutozwa
hakina kikoma, lakini hakitakuwa cha kuzidi sana.
(ii) Kwenye kosa linalopasiwa adhabu ya faini au kifungo,
utozaji wa faini hiyo au kifungo hicho litakuwa ni jambo la
hiari ya hiyo mahakama.
(iii) Kwenye kosa ambalo laweza kutolewa hukumu ya adhabu ya
kifungo pamoja na faini kwa ambalo mkosaji amehukumiwa
adhabu ya faini pamoja na au bila ya kifungo na kwnye kila
kosa ambalo laweza kutolewa hukumu ya adhabu ya faini tu
na mkosaji akahukumiwa adhabu ya kulipa faini tu,
mahakama inayopitisha hukumu hiyo yaweza kwa hiari yake

23
(a) kuamuri katika hukumu yake kwamba kukikosekana
malipo ya faini hiyo ni mkosaji aingine kifungoni kwa
muda fulani, kifungo ambacho kitaongezwa kwenye
kifungo kingine chochote ambacho amehukumiwa nacho
na ambacho aweza kupasiwa nacho kwa mujibu wa
tahafifu ya adhabu; na pia
(b) Kutoa hati ya kutoza kiasi cha faini hiyo kutokana na
mali isiyohamishika na inayohamishika ya mkosaji huyo
kwa kuishika na kujuza chini ya hati:
Isipokuwa kwamba ikiwa hukumu yaamuru kwamba
pakikosekana malipo ya faini hiyo mkosaji atiwe kifungoni, na
ikiwa mkosaji huyo ametumikia kifungo hicho chote kwa kukosa
kulipa faini, hakuna mahakama itakayotoa hati ya kushika na
kuuza mali ya mkosaji huyo ila kwa sababu maalum ambazo
zitaandikwa ikifikiria ni lazima kufanya hivyo.
(iv) Muda wa kifungo ulioamriwa na mahakama kwa ajili ya
kukosekana Malipo ya kiasi chochote cha fedha
kilichohukumiwa kulipwa kwa kuonekana na hatia au kwa
ajili ya kukosekana mali ya kuuzwa ili kutosheleza kiasi
hicho muda wa kifungo hicho utakuwa ule ambao mahakama
imeona utatosheleza kwa jinsi ya shauri hilo lilivyo lakini
kwa vyo vyote hautapindukia kikomo kilichowekwa cha kiasi
kifuatavyo:–

Faini isiyozisi Sh10/- siku 14


Faini inayozidi Shs. 10/- lakini haizidi Shs.20/= mwezi 1
Faini inayozidi Shs. 20/- lakini haizidi Shs.100/= miezi 3
Faini inayozidi Shs. 100/- lakini haizidi Shs. 400/= miezi 4
Faini inayozidi Shs. 400/- lakini haizidi Shs. 400/= miezi 6
(v) Kifungo ambacho kitatolewa kwa kukosekana malipo ya
faini kitakoma wakati wowote itakapolipwa faini hiyo au
itakapotozwa kwa njia ya sheria.

Kuhodhi Sh.1958 30. Iwapo mtu yeyote ameonekana na hatia kwa kosa mojawapo
No. 19 f.15 CA,
Act 2 f.12 chini ya lolote katika mafungu yafuatayo, yaani mafungu 111 au 112,
mahakama yaweza ikiwa ni ziada au badala ya adhabu inayoweza kutoa,
kuamuru mali yoyote ihusikayo na utendaji wa kosa hilo kuhodhiwa na
Jamhuri; au iwapo mali hiyo haiwezai kuhodiwa au kupatikana,
mahakama yaweza kuamuru kuhodhiwa kiasi cha fedha ….. kwamba ni
thamani ya mali hiyo. Malipo ya kiasi cho ………….kihodhiwe yaweza
kulazimishwa kwa namna ile ile …….. mwenendo ule ule kama ulivyo
kwenye malipo ya faini.

Fidia 31. …Kufuata masharti ya fungu la 176 la Kanuni ya


Mwenendo…yeyote ambaye ameonekana na hatia aweza kuhukumiwa
…mtu yeyote ambaye aliumizwa kwa sababu ya hatia … ya namna hiyo

24
yaweza kuwa ni ziada ua ni badala ya nyingine yoyote.

Gharama 32. …….viwango vilivyoamriwa na fungu la 173 la Kanuni …..


Jinai, mahakama yaweza kumuamuru mtu yeyote ……. Kosa kulipa
gharama za mashtaka au sehemu ya …….. au gharama zitakazotokea
katika mashtaka hayo.

Dhamana kwa 33. …….. ambaye ameonekana na kosa ambalo halitolewi ……..
kutunza amani
ya, au ziada ya adhabu yoyote ambayo anapa……… kujidhamini yeye
mwenyewe, pamoja na au bila …….. kiasi ambacho mahakama yafikiri
kuwa chafaa, …….atatunza amani na kuwa mwenye tabia njema kwa
……. Na mahakama, na aweza kuamriwa kufungwa ……..pamoja na
wadhamini, ikiwa imeamriwa hivyo……. …. Kwa kutojidhamini
hakitazidi mwaka hicho pamoja na muda wa kifungo kingine, kama
……..cha muda ambao aweza kuhukumiwa kifungo.

Imebatilishwa 34. [imebatilishwa: Sh.1961 No. 5 f.2.]

Adhabu ya 35. ……. Kanuni hii hakuna adhabu mahsusi inayotolewa ….


kawaida kwa
makosa madogo kosa hilo litakuwa na adhabu ya kifungo cha … miwili au adhabu ya faini
au yote mawili.

Kuzidi kwa 36. …. Baada ya kuonekana na hatia kwa kosa moja .. kwa kosa
adhabu isipokuwa
imeamriwa jingine, ama kabla ya kupitishiwa ya mwanzo au kabla ya kumalizika
vingine adhabu hiyo, … adhabu ya kifo au ya kutandikwa ambayo … peke kwa
sababu ya kosa lililofuata adhabu hiyo … kumalizika kwa adhabu ya
kwanza isipokuwa …. Kwamba adhabu hiyo itimilizwe pamoja na ile …
au na sehemu yoyote ya adhabu ya kwanza.
.. haitakuwa halali kwa mahakama kuamuru … kifungo kwa
kukosa kulipa faini itatimulizwa … ya kwanza chini ya fungu 29 (iii) (a)
au pamoja na adhabu hiyo.

Wafungwa 37. …….. hukumu yapitishwa chini ya Kanuni hii juu ya … ikiwa
wafungwa
waliotoroka ya kifo, faini au adhabu ya kutandikwa … ya kanuni hii hukumu hiyo
watumike baki ya itatimizwa mara kifungo, itatimizwa kwa mujibu wa kanuni zifuatazo,
vifungo
wakamatwapo
tena.
(a) …. mpya ni kali zaidi kuliko ile ambayo mfungwa …
akitumika alipotoroka, adhabu mpya itaanzia .. atatumika
muda wowote uliobaki katika kifungo cha kwanza ambacho
hakikumalizika wakati alipotoroka….adhabu yake mpya;
(b) Iwapo adhabu mpya si kali zaidi kuliko ile ambayo
mfungwa huyo alikuwa akitumika alipotoroka, basi adhabu
mpya itaanza baada ya kumaliza muda uliobakia wa
kifungo chake cha kwanza ambao ulikuwa haujamalizika
wakati alipotoroka.

25
Kuachilia kwa 38.-(1) Iwapo mahakama ambayo imemuona mtu na hati kwa
sharti au bila ya
sharti Sh. 1961 kuangalia mambo yalivyo na namna ya kosa hilo na tabia ya mkosaji
No.5 huyo, yaona kwamba haifai kutoa adhabu, na kwamba pia si sawa kutoa
amri ya kumuweka mkosaji huyo aachiliwe kabisa au, iwapo mahakama
hiyo yaona kwamba yafaa, yaweza kumuachilia kwa sharti kwamba
asitende kosa ndani ya muda utakaowekwa na amri hiyo ambao hautazidi
miezi kumi na mbili toka tarehe ya amri hiyo.
(2) Amri ya kuachilia kwa sharti iliyotajwa katika kifungu
itajulikana kama “amri ya kuachilia kwa sharti” na muda utakaowekwa
kwenye amri yoyote ya namna hiyo utajulikana ni muda wa kuachiliwa
kwa sharti.
(3) Kabla ya kutoa amri ya kuachilia kwa sharti, mahakama
itamueleza mkosaji kwa lugha ya kawaida kwamba wapo atatenda kosa
jingine ndani ya muda wa kuachiliwa sharti, atapasiwa adhabu kwa kosa
la mwanzo.
(4) Iwapo amri ya kumuachilia mkosaji imetolewa chini ya fungu
hili, mahakama yaweza kumuamuru kulipa fidia yoyote iliyoamriwa chini
ya fungu 31 au gharama zozote zilizoamriwa chini ya fungu 32 ya Kanuni
hii.

Kutenda kosa tena 38A.-(1) Iwapo yaonekana na kadhi au hakimu yeyote kwamba
Sh.1961 No. 5 f.3
mtu aliyeachiliwa kwa sharti ameonekana na hatia kwa kosa ambalo
amelitenda ndani ya muda wa kuachiliwa kwa sharti, kadhi au hakimu
huyo aweza kutoa Kuitwa Shaurini kwa mtu huyo kuhudhuria mahli na
wakati utakaotajwa au hati ili akamatwe;
Isipokuwa kwamba hakimu huyo hataitoa kuitwa shaurini
hiyo au hati ya kukamatia hiyo ila kwa taarifa ya maandishi na juu ya
kiapo.
(2) Kuitwa shaurini hati ya kukamatia inayotolewa chini ya fungu
hili itamuamuru mtu aliye na hatia huyo kuhudhuria au kuletwa mbele ya
mahakama ambayo iliamuru aachiliwe kwa sharti.
(3) Iwapo mtu ambaye ameachiliwa kwa sharti ameonekana na
hatia na hakimu kwa kosa ambalo amelifanya ndani ya muda wa
kuachiliwa kwa sharti, hakimu huyo aweza kumweka mtu huyo
korokoroni au kumuachilia kwa dhamana, pamoja na wadhamini au bila
ya wadhamini, hadi atakapoweza kuletwa au kuhudhuria mbele ya
mahakama ambayo imetoa amri hiyo ya kuachilia kwa sharti.
(4) Iwapo yathibitishwa kwa kuitosheleza mahakama ambayo
imetoa amri ya kuachiliwa kwa sharti kwamba mtu aliyetolewa amri hiyo
ameonekana na hatia kwa kosa ambalo amelitenda ndani ya muda wa
kuachiliwa kwa sharti, mahakama hiyo yaweza kumpitishia hukumu
yoyote ambayo ingeliweza kumptitishia kama mahakama hiyo ingemuona
na hatia kwa kosa la mwanzo.
(5) Iwapo mtu ambaye ametolewa amri ya kuachiliwa kwa sharti
na hakimu, akionekana na hatia na Mahakama kuu kwa kosa ambalo
amelitenda ndani ya muda wa kuachiliwa kwa sharti, Mahakama Kuu

26
yaweza kumpitishia hukumu ambayo mahakama iliyotoa amri hiyo
ingeliweza kumpitishia kama mahakama hiyo ingelimuona na hatia kwa
kosa la mwanzo.
(6) Iwapo chini ya masharti ya fungu hili mtu ambaye
ameachiliwa kwa sharti anahukumiwa adhabu kwa kosa ambalo lilitolewa
amri ya kuachiliwa kwa sharti, amri hiyo itakomea hapo.

Matokeo na hatia 38B.-(1) Kwa kufuata masharti ya kifungu (2), iwapo mtu
na kuachiliwa
Sh.1961 No.5 f.3 ameonekana na hatia akiachiliwa kabisa au kwa sharti chini ya masharti
ya fungu 38. Kuonekana kwake na hatia ya kosa hilo hakuatafikiriwa
kwamba si kuonekana na hatia kwa ajili nyingine yoyote isipokuwa kwa
ajili ya mashauri ambayo yalitolewa amri hiyo na kwa ajili ya mashauri
yoyote ya baadaye ambayo yaweza kufanywa juu yake chini ya masharti
ya fungu 38A.
Isipokuwa kwamba iwapo mtu ambaye ameachiliwa kwa sharti
baadaye akahukumiwa chini ya fungu la 38A kwa kosa ambalo lilitolewa
amri hiyo, fungu hili litakoma kutumika kwa ajili ya kosa ambalo naye
atafikiriwa kwamba ametiwa hatiani kwenye tarehe ya hukumu hiyo.
(2) Hakuna jambo katika fungu hili ambalo litadhuru–
(a) haki ya mtu yeyote ambaye ameonekana na hatia na
kuachiliwa kabisa au kwa sharti kuchukua rufani kupinga
kuonekana na hatia kwake au kuitegemea hukumu hiyo iwe
kingamizi yake kwa mashtaka yoyote ya baadaye kwa kosa
hilo hilo; au
(b) kurejesha au kurudisha mali yoyote kwa matokeo ya
kuonekana na hatia kwa mtu huyo.

SEHEMU YA II
UHALIFU

Kigawe ch I. – makosa ya Kuvunja Utulivu

SURA YA VII
UHAINI NA MAKOSA MENGINE JUU YA MAMLAKA YA UTAWALA

Uhaini C.A. 39.-(1) Mtu yeyote ambaye yumo katika utii wa Jamhuri ya
ACT.2 F.36
Tanganyika–
(a) akifanya vita na Jamhuri ya Tanganyika, au
(b) akiambatana na maadui wa Jamhuri katika nchi ya Tanganyika
au mahali pengine; au
Mtu huyo atakuwa amekosa kosa la uhaini na kosa likithibiti atapasiwa
kupata adhabu ya kifo.

Kuchochea 40. Mtu yeyote ambaye anamchochea sengazuwa (mgeni) yeyote


mashambulio
kushambulia Tanganyika kwa nguvu za silaha mtu huyo amekosa kosa la
uhaini na atapasiwa kupata adhabu ya kifo.

27
Kuficha uhaini 41. Mtu yeyote ambaye–
(a) atakuwa mfichaji uhalifu wa uhaini; au
(b) atajua kwamba yuko mtu yeyote mwenye nia ya kutenda uhaini
na akaacha kutoa taarifa ya jambo hilo, kwa haraka ya kutosha,
kwa Bwana Shauri, Hakimu au Ofisa Mkuu wa Polisi au
akaacha kufanya juhudi ya kutosha ya kuzuia utendaji wa kosa
hilo, mtu huyo amekosa kosa kubwa liitwalo “kupurukusha
uhaini” na atapasiwa kifungo cha maisha.

Makosa 42. Mtu yeyote ambaye atakuwa na nia ya kutimiza lolote katika
makubwa ya
kihaini C.A. madhumuni haya yafuatayo, yaani –
Act 2 f.36
(a) kushika silaha ndani ya Tanganyika ili kwa lazima ya kwa
nguvu kuilazimisha serikali igeuze mwengo wake au
maongozaji yake au ili kutia lazima au nguvu juu ya baraza la
taifa (Bunge) au ili kulitishia au kulifadhaisha Bunge;
(b) kumchochea mtu yeyote kufanya mashambulio ya silaha katika
Tanganyika.
Na akadhihirisha nia hiyo kwa tendo lililowazi, au akatangaza kwa
kuchapisha au kwa kuandika, mtu huyo amekosa kosa kubwa na atapasiwa
kifungo cha maisha.
Kuletesha vita 43. Mtu yeyote ambaye bila ya mamlaka ya halali atafanya, au
vya wenyeji
kusaidia au kushauri ufanyaji na au utayarishaji wa vita vyovyote au
shughuli za kivita kwa namna yoyote kupigana na chifu wa kienyeji au kwa
namna yoyote kupigana na kikundi cha wenyeji, mtu huyo amekosa kosa
kubwa na atapasiwa kifungo cha maisha.

44. Limebatilishwa: C.A. Sheria 2 fungu 36.

Kuchochea uasi 45. Mtu yeyote ambaye, kwa kusudi anajaribu kutimiza yo yote
C.A. Act 2 f.8
katika madhumi haya yafuatayo, yaani–
(a) kumshawishi mtu ye yote anayetumika katika jeshi la vita la
Tanganyika au yeyote katika jeshi la polisi aache wajibu na utii
wake juu ya Jamhuri; au
(b) kuwachochea watu wo wote na namna hiyo kutenda kitendo
cha uasi au kutenda kitendo chochote cha uhaini au cha uasi;
(c) kuwachochea watu wowote wa namna hiyo kufanya au
kujitahidi kufanya mkusanyiko wa uasi,
Mtu huyo amekosa kosa kubwa na atapasiwa kifungo cha maisha.

Kuwasiaidi 46. Mtu yeyote ambaye–


askari jeshi au
maafisa wa (a) atasaidia ua kuwa msalata wa tendo lolote la uasi kwa, au
polisi katiak (b) atamchochea kufanya fitina au kutotii amri ya halali yoyote
vitendo vya kutoka kwa mkubwa wake.
uasi
Akida mdogo yeyote au yeyoTe wa daraja ya chini katika jeshi la vita la

28
Tanganyika au ofisa wa polisi yeyote mtu huyo amekosa kosa dogo.

Kushawishi 47. Mtu yeyote ambaye kwa njia ya namna yoyote iwayo–
askari jeshi au
maofisa wa (a) atauma au kushawishi au atajaribu kutuma au kushawishi
polisi kutoroka kutoroka kwa; au
(b) atasaidia au atakuwa msalata wa utorokaji wa; au
(c) baada ya kuwa na sababu ya kuamini kwamba ni mtorokaji
akamficha au kumsaidia kumficha.
Akida mdogo au askari wa daraja ya chini wajeshi la vita lililotajwa au ofisa
wa polisi yeyote, mtu huyo amekosa kosa dogo na atapasiwa kifungo cha
miezi sita.

Kusaidia 48. Mtu yeyote ambaye–


mateka kwa
vita kutoroka (a) ………….. kwa kusudi atamsaidia adui wa Jamhuri ambaye
C.A. Act.2 f.36 ………..vita katika Tanganyika kutoroka gerezani au
…………. Kama alikuwa gerezani au kafungiwa .. na kama
aliachiliwa kwa ahadi ya kua hatatoroka kutoroka kutoka nje
ya Tanganyika, mtu aliyefanya ….. kosa kubwa na atapasiwa
kifungo cha maisha;
(b) .. au bila uhalali atamwachia kutoroka mtu yeyote .. iliyotajwa
katika fasili iliyopita, atakuwa ….. dogo.

Maelezo 49. … ya mafungu 51, 52, 53, 54, 55, 56, 57 na 58 ya ……


Sh.1955 No.49
f.4 lachanganya –
… Tanganyika;

……… mambo yote yaliyoandikwa au kupigwa chapa, ……. Au


kumbukumbu nyingine gamba la filimu, … kuchukua sauti, filimu ya
senema au chombo …. …. Chaweza kutoa meneno au mawazo ama .. kitu
chochote kikiwa ni sawa na hivyo vilivyo … si sawa kilicho na maelezo ya
kitu fulani kwa namna, umbo au tabia nyingineyo au kwa namna unaweza
kutoa, kueleza au kupeleka maneno au .. au utoaji wa mara ya pili wa
tangazo;
…. Kila tangazo linalotolewa kila baada ya muda … kwa sehemu au kwa
idadi fulani kwa vipindi vilivyokuwa maalum:
…. Maana ya tangazo lililo na makusudi ya kufitini.

Uwezo wa …ataona kwamba uingizaji wa tangazo lolote .. manufaa ya watu, kwa hiari
kuzuia kuingiza
matangazo yake kamili .. uingizaji wa tangazo hilo kwa kutoa amri, ….anaweza kupiga
Sh.1955 No.49 marufuku uingizaji wa toleo … lililopita au litakalokuja kwa amri ile ile au
f.5 kwa …

… kwamba uingizaji wa matangazo ya mtu … ni kinyume cha manufaa ya


watu anaweza kutoa amri ya kupiga marufuku uingizaji wa matangazo hayo
ama yote pia ama kwa kufuata vidakizo au masharti yaliyotajwa na anaweza
kwa amri hiyo hiyo aliyokwisha toa au kutoa amri nyingine kuiga marufuku

29
uingizaji wa matangazo ya badaye ya mtu huyo, ama yote pia ama kwa
kufuata vidakizo au masharti yaliyotajwa.

Makosa 52. – (1) mtu yeyote ambaye ataingiza, atatangaza, atauza, atatoa
yanayohusu
matangazo kwa ajili ya kuuza, atagawanya au atazalisha tangazo lolote ambalo
ambayo uingizaji wake umepigwa marufuku kwa mujibu wa fungu la 51 au dondoo
uingizaji wake lolote la tangazo hilo mtu huyo amekosa na kwa kosa la kwanza atapasiwa
umpigwa
marufuku C.A. kifungo cha miaka miwili au kutozwa faini ya shilingi elfu mbili au yote
Act 2 f.12 mawili pamoja kifungo na faini pia na kwa kosa lifuatalo ni kifungo cha
miaka mitatu; na tangazo hilo au dondoo hilo la tangazo litahodhiwa na
jamhuri.
(2) Mtu yeyote ambaye bila ya udhuru wa halali analo
mikononi mwake tangazo lolote ambalo uingizaji wake umepigwa
marufuku kwa mujibu wa fungu la 51 au analo dondoo la tangazo hilo mtu
huyo amekosa na kwa kosa la kwanza atapasiwa kifungo cha mwaka mmoja
au kutozawa faini ya shilingi elfu moja au adhabu zote mbili hizo na
dondoo la tangazo hilo litahodhiwa na Jamhuri.

Upelekaji wa 53.-(1) Mtu yeyote ambaye atapelekewa tangazo lililopigwa


tangazo
lililopigwa marufuku kwa mujibu wa fungu la 51 au dondoo la tangazo hilo bila yeye
marufuku wa kujua au kuwa shauri moja au kapelekewa kwa maombi aliyofanya kabla ya
sheha au kituo uingizaji wa tangazo hilo kupigwa marufuku au kuwa nalo mikononi
cha polisi C.A.
Act.2 f.12 tangazo hilo ni lazima bila kukawia mara tu atakapojua yaliyomo katika
tangazo hilo au dondoo lake alipeleke kwa Sheha au kwa afisa muangalizi
wa kituo cha polisi; walio karibu naye zaidi na tangazo au dondoo lake
ambalo limeingia mikononi mwake kabla uingizaji wa tangazo kupigwa
marufuku basi mara tu amri ya kupiga marufuku uingizaji wa tangazo hilo
itakapotoka alipeleke tangazo hilo au dondoo lake kwa Sheha wa karibu
naye zaidi au kwa afisa mwangalizi wa kituo cha polisi kilichoko karibu
naye zaidi na asipofanya hivyo atakuwa amekosa na atapasiwa kifungo cha
mwaka mmoja au faini ya shilingi elfu moja au adhabu zote mbili, na
tangazo hilo au dondoo lake litahodhiwa na Jamhuri.

(2) Mtu ambaye atatekeleza masharti ya kifungu cha (1) au ambaye


ataonekana amekosa chini ya kifungu hicho hatapasiwa na kuonekana na
kosa la kuingiza au kuwa nalo tangazo hilo au dondoo lake.
Uwezo wa 54. – (1) Ye yote katika maafisa wafuatao, yaani –
kukagua
vifurushi (a) afisa yeyote wa Idara ya Posta ambaye si chini ya cheo cha
Su.455 d.18 mkuu wa posta;
(b) afisa yeyote wa Idara ya forodha ambaye si chini ya cheo cha
Mnyapara;
(c) afisa yeyote wa polisi ambaye si chini ya cheo cha muamuzi
(inspector);
(d) afisa mwingine ye yote aliyepewa mamlaka kwa ajili hiyo, na
Waziri atakayekuwa na madaraka kwa mambo ya ndani,
anaweza kuzuia, kufungua na kukagua kifurushi au bahasha yo yote

30
anbaye ana tuhuma nayo kuwa ina tangazo au dondoo la tangazo
ambalo kwa mujibu wa fungu la 52 ni kosa kuliingiza, kulitangaza,
kuliuza, kulitoa kwa kuuza, kuligawanya, kulizalisha au kuwa nalo;
na wakati huo wa kukagua anaweza kumzuia mtu yeyote
anayeingiza au kugawanya au kutia posta kifurushi hicho au bahasha
hiyo au yule mtu ambaye mikononi mwake anacho kifurushi hicho
au bahasha hiyo.

(2) Ikiwa tangazo hilo lolote la namna hiyo au dondoo lake


litaonekana katika kifurushi au bahasha hiyo kifurushi chote au bahasha
yote iatwaliwa na kufungiwa na afisa huyo na huyo mtu aliyeingiza au
kugawanya au kutia posta kifurushi hicho au bahasha hiyo au yule
alieyeonekana navyo mikononi mwake anaweza kukamatwa hapo hapo na
kushtakiwa kwa kutenda kosa chini ya fungu la 52 au la 53 kama
atakavyokuwa.

55. – (1) “nia ya ufitina” ni ile nia–


(a) ya kuleta chuki au kudharau au kuchocheza, kutopenda
mamlaka ya halali ya Jamhuri au Serikali; au
(b) ya kuwataharakisha wakazi wowote wa Tanganyika kujaribu
kuleta mageuzo, kwa njia isiyokuwa ya halali ya jambo lolote
katika Tanganyika lililowekwa na sheria; au
(c) ya kuleta chuki au kudharau au kuchamua kutopenda
usimamiaji haki katika Tanganyika; au
(d) ya kuchamua kutoridhika na kutopendana kati ya mbari mbali
mbali za wakati wa Tanganyika.
(2) Kitendo, hotuba au tangazo haliwi la fitina kwa sababu tu
kwamba lakusidia –
(a) kuonyesha kwamba serikali imeongozwa vibaya au imekosea
katika mwenendo wake wowote; au
(b) kutaja makosa au upungufu katika serikali au Katiba ya
Tanganyika kama ilivyowekwa na sheria, au katika usimamiaji
haki kwa makusudi ya kutaka kusawazisha makosa hayo au
upungufu huo; au
(c) kushawishi wakati wowote wa Tanganyika kujaribu kwa njia
ya halali kuleta megeuzo ya jambo lolote katika Tanganyika
kama ilivyowekwa kwa sheria; au
(d) kutaja, kwa makusudi ya kutaka yaondoshwe, mambo yoyote
ambayo yanaleta au yanaelekea kuleta hasira za chuki na uadui
baina ya mbari mbali mbali za wakati wa Tanganyika.
(3) Katika kufikiria kama kitendo chochote kilichotendwa,
maneno yoyote yaliyosema au hati yoyote iliyotangazwa vilikuwa kwa nia
ya fitina au si ya fitina itachukuliwa kwamba kila mtu atahesabiwa kuwa
ameyakusudia matokeo yoyote yaliyotokea kwa kawaida kutokana na tabia
yake wakati huo na hali ilivyokuwa wakati akiwa na tabia hiyo.
56. (1) Mtu ye yote ambaye–

31
(a) atafanya au atajaribu kufanya, au kujitayarisha kufanya au kula
njama na mtu yeyote kufanya kitendo chochote kwa nia ya
fitina;
(b) atatamka maneno yoyote kwa nia ya fitina;
(c) atachapisha, kutangaza, kuuza kutoa kwa kuuza, kugawa au
kuzalisha tangazo lolote la fitina;
(d) ataingiza tangazo lolote la fitina na iwapo hana sababu ya
kuamini kwamba tangazo hilo ni la fitina.
mtu huyo ni mkosaji na atapasiwa. Kwa kosa la kwanza na kifungo cha
miaka miwili au kutozwa faini ya shilingi elfu mbili au adhabu zote mbili
pamoja na kwa kosa lifuatazo atapata kifungo cha miaka mitatu na tangazo
lolote la fitina litahodhiwa na Jamhuri;
(2) Mtu yeyote ambaye analo mikononi mwake bila udhuru wa
halali, tangazo la fitina mtu huyo amekosa na atapasiwa kwa kosa la
kwanza na kifungo cha mwaka mmoja au faini ya shilingi elfu mbili au
adhabu zote mbili na kwa kosa lifuatialo atapata kifungo cha miaka miwili;
na tangazo litahodhiwa na Jamhuri.
(3) Itakuwa ni utetezi wa kutosha kwa mashtaka chini ya
kifungu kilichotanguia iwapo mtu aliyeshtakiwa na kujua kama tangazo hilo
lilikuwa la fitina wakati lilipoingia mikononi mwake na mara tu alipoyajua
yaliyomo katika tangazo hilo akalipeleka kwa Sheha wa karibu naye zaidi
au kwa afisa muangalizi wa kituo cha polisi kilicho karibu naye zaidi.
(4) Mtambo wowote wa kuchapia ambao umetumiwa au kwa
sababu ya namna umetuhumiwa kutumiwa kwa kuchapisha au kuzalisha
tangazo lolote la fitina mtambo huo waweza kukamatwa au kuhifadhiwa na
afisa wa polisi kungojea kesi na kuhukumiwa makosa au kuruhusiwa
tangazo lolote hilo la fitina; na iwapo mtu ye yote ataonekana na makosa ya
kuchapa au kuzalisha tangazo la fitina mahakama yaweza, baada ya adhabu
nyingine yoyote kutoa amri kwamba mtambo huo uhodhiwe na Jamhuri na
mahakama inaweza kutoa hukumu hiyo, iwe mtu huyo aliyehukumiwa
makosa wakati wa kuchapwa au kuzalishwa tangazo hilo mtambo wa
kuchapia ulikuwa ni mali yake au sivyo. Mtambo wa kuchapia
utakaohodhiwa kwa mujibu wa kifungu hiki utauzwa na fedha
zitakazopatikana, zikipunguzwa gharama za uuzaji, zitatiwa katika Hazina.
(5) Iwapo mwenye mali, mtangazaji, mchapaji, au mhariri wa
gazeti kama lilivyoelezwa katika Sheria ya Magazeti, ataonekana na
makosa ya kuchapisha au kutangaza tangazo la fitina katika gazeti
mahakama baada ya adhabu nyingine yoyote iliyotoa, na ni sawa kama
ilitoa amri chini ya kifungu cha (4) cha fungu hili au sivyo, inaweza kutoa
amri ya marufuku utoaji wa gazeti hilo kwa muda usiozidi mwaka mmoja.
(6) Wakati wowote mahakama itakapoombwa na wakili Mkuu
wa Serikali na kuchukua dhamana, kama ipo, ya kuwa na tabia nzuri kama
mahakama itakavyoona yafaa kuamuri, mahakama hiyo inaweza kutangua
amri yoyote iliyoitoa ya kuhodhi au kutwaa mtambo wa kuchapishia au ya
kupiga marufuku utangazaji zaidi wa gazeti fulani.
(7) Mahakama kabla ya kutoa amri ya kuhodhi au kutwaa

32
mtambo wa kuchapishia kwa mujibu wa fungu hili ni lazima itoshe kwamba
mtambo huo wa kuchapishia ndio hasa mtambo ambao ulitumika kwa
kuchapishia au kuzalishia tangazo hilo la fitina.
(8) Popote iwapo mtambo wa kuchapishia umewekwa katika
hifadhi au umetwaliwa kwa mujibu wa fungu hili Mkuu wa Polisi kwa
hiyari yake anaweza –
(a) kufanya mtambo huo au sehemu yake iondolewe; au
(b) kufanya sehemu yoyote ya mtambo huo ifungwe ili kuzuia
kutumika.
Isipokuwa kwamba mwenye mtambo huo au ajenti wake atakuwa na
haki ya kuufikia mtambo huo ili kuuweka katika hali
itakayowezesha mtambo huo kufanya kazi.
(9) Mkuu wa Polisi au afisa wa polisi yeyote anayefanya kazi
kwa kufuata uwezo uliotolewa na fungu hili hatapasiwa na kulipa hasara
yoyote itakayopatikana katika mtambo wa kuchapishia iwe hasa ilipatikana
kwa kupuuza kwake au vinginevyo madhali hasa hiyo kwenye mtambo huo
haikufanywa kwa kunuia.
(10) Mtu yeyote ambaye atatumia au kujaribu kutumia mtambo
wa kuchapishia uliowekwa katika hifadhi au uliotwaliwa kwa kufuata
kifungu cha (4) cha fungu hili mtu huyo amekosa na atapasiwa kifungo cha
muda usiozidi miaka mitatu.
(11) Mtu yeyote ambaye atachapisha au kutangaza gazeti kwa
kuvunja amri iliyotolewa chini ya kifungu (5) cha fungu hili atakuwa
amekosa na atapasiwa kifungo cha muda usiozidi miaka mitatu.
(12) Katika fungu hili neno “mtambo wa kuchapishia”
linachanganya kiwanda cha kupiga chapa, mtambo wa kutolea nakala,
mashine ya taipureta, chombo cha kupigia picha maneneo au cha kutoa
nakala nyingi au cha kukatia herufi au mashine yoyote au chombo chochoe
ambacho kimetumika au kimehusiana na uchapishaji au uzalishaji wa
matangazo na herufi na vyombo vyovyote vingine vya mashine au mtambo
huo.

Mashtaka 57. (1) Hakuna mashitaka yatakayoanzishwa chini ya fungu la 56


Sh,1950
No.185, 4 G.N. ila iwe ni ndani ya muda wa miezi sita tangu kosa hilo kutendeka:
1961 No.236 Isipokuwa kwamba iwapo mtu –
(a) ametenda kosa hilo nje ya Tanganyika; au
(b) ameondoka Tanganyika ndani ya muda wa miezi sita baada ya
kutenda kosa hilo,
Mashitaka juu ya kosa hilo yanaweza kuanzishwa ndani ya miezi sita toka
siku ya kwanza mtu huyo alipoingia Tanganyika baada ya kufanya kosa hilo
au siku ya kwanza aliporudi Tanganyika baada ya kuondoka Tanganyika
kama itakavyokuwa.
(2) Mtu –
(i) kutenda kosa hilo; au
(ii) kuondoka Tanganyika,
asishtakiwe kwa kosa chini ya fungu 56 bila ya idhini ya maandishi ya

33
Mkurugenzi wa Mashitaka wa Serikali.

Ushahidi 58. Mtu yeyote asihukumiwe makosa chini ya fungu ….. kwa
ushahidi wa mtu mmoja bila ya ushahidi mwingine wowote.

59. Mtu yeyote ambaye –


(a) atalisha au atahudhuria na kuridhika na ulishaji wa kiapo cho
chote au kuchukua ahadi ya namna ya kiapo, kiapo ambacho
kina madhumuni ya kumlazimisha mwenye kukila atende kosa
lenye adhabu ya kifo; au
(b) atakula kiapo chochote cha namna hiyo au kuchukua ahadi
kama hiyo bila kulazimishwa kufanya hayo.
Mtu huyo amekosa kosa kubwa na atapasiwa kifungo cha maisha.

60. Mtu yeyote ambaye –


(1) atalisha au atahudhuria na kuridhika na ulishaji wa kiapo
chochote au kuchukua ahadi ya namna ya kiapo, kiapo ambacho kina
madhumuni ya kumlazimisha mwenye kukila atende moja wapo katika haya
yafuatayo, yaani –
(a) kujitia katika ujasiri wa kuhuni au wa fitina;
(b) kutenda kosa lolote lisilokuwa na adhabu ya kifo;
(c) kuvuruga amani ya watu;
(d) kuwamo katika chama, kikao au jumuia yoyote
iliyotengenezwa kwa makusudi ya kufanya kitendo chochote
katika hivyo vilivyotajwa;
(e) kutii amri au maamrisho ya halmashauri au kikundi cha watu
kilichoundwa bila ya uhalali au amri ya kiongozi au mkuu au
mtu mwingine yeyote asiyekuwa na mamlaka kwa sheria juu
ya jambo hilo;
(f) kuacha kutoa habari au kutoa ushahidi juu ya chama au jumuia
au mtu mwingineo;
(g) kuacha kudhihirisha au kufichua chama hicho au jumuia
yoyote ambayo si ya halali, au kuacha kudhihirisha au kufichua
kitendo chochote kisicho cha halali kilichotendwa au kitakacho
tenda au kiapo chochote kisicho halali kinachotaka kuliwa na
yeye au mtu mwingine au ahadi isiyokuwa ya halali inayotaka
kutolewa na yeye au mtu mwingine yeyote; au kuacha kufichua
au kudhihirisha uingizai wowote wa kiapo cha namna hiyo; au
(2) kula kiapo chochote cha namna hiyo au kuchukua ahadi yoyote
mtu huyo amekosa kosa kubwa na atapasiwa kifungo cha miaka saba.

61. mtu ambaye amekula kiapo au amechukua ahadi kama


ilivyotajwa katika mafungu mawili yaliyotangulia hawezi kufanya ni utetezi
wake kwa kudai kwamba yeye alilazimishwa ila iwapo ndani ya siku kumi
na nne toka kula kiapo hicho atamke kwa kutoa taarifa juu ya kiapo hicho,
mbele ya hakimu na kama ni mtumishi wa jeshi la vita la Tanganyika au

34
jeshi la polisi atoe taarifa mbele ya mkuu wake kueleza yote anayoyajua
kuhusu shauri hilo la kiapo na kutaja mtu au watu waliolisha kiapo au
kuhudhuria na mahali na wakati kiapo kilipolishwa au ahadi
ilipochukuliwa; au kama mtu amezuilika kwa nguvu fulani zilizotumika au
kwa ugonjwa atoe habari hizo ndani ya siku kumi na nne tangu
kuondokewa na kuzuilika huko.

62. – (1) Mtu ye yote ambaye –


(a) bila ya ruhusa ya Waziri atakayekuwapo wa mambo ya ndani,
atafundisha au kuchezesha kwata mtu yeyote mwingine juu ya
kutumia silaha au kufanya mazoezi ya kivita au mwenendo wa
kivita au kazi za kivita; au
(b) atakuwapo kwenye mkutano au mkusanyiko wowote wa watu
uliofanywa bila ruhusa ya Waziri atakayekuwapo wa mambo
ya ndani na ukawa wa madhumuni ya kufundisha au
kuchezesha kwata watu wengine juu ya kutumia silaha au
kufanya mazoezi au mwendo au kazi za kivita.
Mtu huyo amekosa kosa kubwa na atapasiwa kifungo cha miaka saba.
(2) Mtu yeyote ambaye katika mkutano au mkusanyiko wowote
uliofanywa bila ya ruhusa ya waziri atakayekuwapo wa mambo ya ndani
atafundishwa au kuchezeshwa kwata juu ya kutumia silaha au kuzoezwa
mambo au mwendo, au kazi za kivita au atakuwapo kwenye mkutano au
mkusanyiko huo kwa makusudi ya kufundisha au kuchezeshwa kwata mtu
huyo amekosa kosa dogo.

Tangazo la 63. – (1) Mtu yeyote ambaye atatangaza maneno yeyote ya


habari za
uwongo uwongo, uvumi au taarifa ya uwongo ambayo yaweza kuleta hofu na
ziwezazo ushituko kwa watu au kuvuruga amani ya watu mtu huyo amekosa kosa
kuleta hofu na dogo.
mshituko kwa
watu
(2) Itakuwa ni utetezi kwa mashitaka chini ya kifungu (1)
iwapo mshtakiwa atathibitisha kwamba kabla ya tangazo hilo alichukua
hatua za kuhakikisha ukweli wa maneno hayo au uvumi huo au taarifa hiyo
kiasi cha kuweza kumfanya aamini kwamba ni kweli.
Uchochezi wa 63.A – (1) Mtu yeyote ambaye bila ya udhuru wa halali atachapa
kutumia nguvu
Sh.1955 No.49 atatangaza au katika mkusanyiko wowote atatoa maneno yatakayoonyesha
f.6 G.N. 1961 au kuwa na maana ya kuwa ni lazima au ni vizuri kutenda kitendo chochote
No.236 bila ruhusa ya halali kilicho na kusudi la –
(i) kuleta kifo au maumivu ya mwili kwa mtu yeyote au mbari au jamii
yoyote ya watu; au
(ii) kupelekea kuharibu au kutia hasara mali yoyote,
mtu huyo amekosa kosa dogo na atapasiwa kifungo cha miaka mitatu.
(2) kwa ajili ya fungu hili neno “mkusanyiko: lina maana ya
mkutano wa watu watatu au zaidi.
(3) Mtu asishitakiwe chini ya fungu hili bila ya idhini ya
maandishi ya Mkurugenzi wa mashtaka wa Serikali.

35
Kuchamua 63.B – (1) Mtu yeyote ambaye katika mkusanyiko wowote atatoa
kutoridhika na
chuko kwa maneno ambayo huenda yakaleta kutoridhika kati ya wakazi wowote
madhumumuni Watanganyika au kuleta hisi za chuki kati ya mbari au jamii mbali mbali za
yasio halali watu wa Tanganyika, mtu huyo amekosa kosa dogo na atapasiwa faini
Sh,1955 No. 49
f.6 Sh.1959 isiyozidi shilingi elfu moja au kifungo cha muda usiozidi miezi kumi na
No.10 f.2 G.N. mbili au yote mawili faini na kifungo pia.
1961 No.236
C.A. Act 2 f.36
Isipokuwa kwamba hakuna mtu atakayekuwa amekosa chini ya
masharti ya fungu hili ikiwa maneno yake aliyoyatoa yalikuwa tu kwa ajili
ya moja au zaidi ya madhumuni haya yafuatayo, na uthibitisho wa hayo
utakuwa juu yake, madhumuni yenyewe ni –
(a) kuonyesha kwamba Serikali imeongozwa vibaya au imekosea
katika mwendo wake; au
(b) kutaja makosa au upungufu katika Serikali au siasa ya Serikali
au Katiba ya Tanganyika kama ilivyowekwa na sheria, au
sheria yoyote au katika usimamaji wa haki kwa kusudi la
kutaka kuondosha au kusahihisha upungufu au makosa hayo;
au
(c) kushawishi wakati wowote wa Tanganyika wajaribu kuleta
mageuzo ya jambo lolote katika Tanganyika kwa njia ya halali;
au
(d) kutaja kwa nia ya kuyaondosha mambo yoyote ambayo
yameleta au yanaelekea kuleta chuki kati ya wakazi wowote
wa Tanganyika au hisi ya chuki au uadui kati ya mbari au jamii
ya watu mbali mbali wa Tanganyika

(2) kwa ajili ya fungu hili neno “mkusanyiko” lina maana ya


mkutano wa watu saba au zaidi.

(3) Mtu hatashitakiwa kwa kosa chini ya fungu hili bila ya idhini
ya maandishi ya Mkurugenzi wa Mashitaka wa Serikali.

64. Mtu yeyote ambaye bila ya hali yoyote ile au bila udhuru
utakaotosha kwa upande wa kumuumbua mtu mahsusi, atatangaza jambo
lolote kwa kukusudia lisomwe au kuonyesha ishara yoyote au maonyesho
ya wazi yanayoweza kutweza, kukebehi kumletea chuki au dharau mfalme,
mtawala balozi au mkuu yeyote wa kigeni kwa nia ya kuharibu amani na
urafiki kati ya Tanganyika na nchi yake mtu huyo amekosa kosa dogo.
65. Mtu yeyote atakuwa ametenda kosa dogo ambaye ataenda moja
wapo katika matendo haya yafuatayo bila ruhusa ya Rais yaani –
(a) atakakaetayarisha au kufanya msafara wowote wa manowari au
wa jeshi la vita kwenda kushambulia tawala za dola yoyote
iliyo rafiki au atakayeshughulika na maandalio au mafanyo ya
msafara au kusaidia au kuajiriwa kupewa cheo chochote katika
msafara huo, au
(b) atakayepokea hali ya kuwa yeye ni raia wa Tanganyika, au

36
kukubali kupokea ujumbe au shughuli yoyote ya kazi za kijeshi
la vita au za kimanowari za dola yoyote ngeni iliyo na vita na
dola ya kirafiki, au atakayeshawishi; akiwa ni raia wa
Tanganyika au si raia wa Tanganyika, mtu mwingine yeyote
kupokea au kukubali kupokea ujumbe wowoe au shughuli
yoyote ya kazi za kijeshi au za kimanowari za dola hiyo ngeni
iliyokwisha tajwa; au
(c) atakayeitoka, hali ya kuwa yeye ni raia wa Tanganyika, au
kwenda kujipakia katika chombo chochote kwa nia ya kuitoka
nchi ya Tanganyika kwa kusudi la kupokea ujumbe wowote au
shughuli yoyote ya kazi za kijeshi au za kimanowari za dola
ngeni yoyote iliyo katika vita na dola ya kirafiki; au
atakaeshawishi, akiwa ni rais au si rais wa Tanganyika, mtu
yeyote mwingine kuitoka au kujipakia katika chombo chochote
kwa nia ya kutoka nchi ya Tanganyika kwa kusudi kama hilo;
au
(d) atakayepakia, akiwa ni nahodha au mwenye chombo chochote
kwa makusudi, katika chombo chake au kujishughulisha katika
kupakia au anaye katika chombo hicho mtu aliyejiandikisha
uaskari wa vita bila ya uhalali; au
(e) atakayeunda, kukubali kuunda, kuundisha, kutayarisha,
kusafirisha au kuruhusu kusafirisha chombo chochote au
atakayetoa ujumbe wowote kwa chombo chochote, kwa nia au
kwa kujua au kuna sababu ya kutosha kuamini kwamba
chombo hicho au ujumbe huo utatumika katika kazi za kivita
au za kimanowari za dola ngeni iliyo katika vita na dola yoyote
ya kirafiki.

Isipokuwa kwamba mtu anayeunda, kuundisha au kutayarisha


chombo kwa namna moja wapo katika hizo zilizokwisha tajwa, anafanya
hivyo kwa kutimiza mkataba uliofanywa kabla ya kuanza vita kama hivyo
vilivyokwisha semwa mtu huyo hatapasiwa na adhabu yoyote katika
adhabu zilizotajwa katika fungu hili kuhusu uundaji huo au utayarishaji
huo iwapo –
(i) wakati wa Rais kutoa ilani ya kuonyehsa kutopendelea upande
wowote katika vita, yeye atatoa mara moja kwa Waziri
atakayekuwapo wa mambo ya ndani habari za uundaji,
uundishaji au utayarishaji wa chombo hicho na kupasha habari
zote za mkataba na mambo yote yanayohusu kufanywa au
kuwa yatafanywa chini ya mkataba huo kama zitakavyotakiwa
na Waziri huyo wa mambo ya ndani; na
(ii) atatoa dhamana na kuchukua au kuruhusu kuchukuliwa hatua
zozote, kama zipo, kama zitakavyoelezwa na Waziri
atakayekuwapo wa mambo ya ndani ili kuhakikisha kwamba
chombo hicho hakiwezi kuchukuliwa au kusafirishwa au
kuondolewa bila ya ruhusa ya Rais mpaka mwisho wa vita

37
hivyo vilivyotajwa kabla.

Uharamia 66. Mtu yeyote ambaye atakosa kosa la uharamia au uhalifu wowote
unaoungana na au unahusiana au kufananana na uharamia mtu huyo
atapasiwa na kushtakiwa na kupewa adhabu kwa kufuata sheria ya England
itakayokuwapo ikifanya kazi.

SURA YA IX
MIKUSANYIKO ISIYO HALALI NA GHASIA NA MAKOSA MENGINE YA
KUVUNJA UTULIVU WA WATU

67.-73. (Zimebatilishwa: Sheria 1954 No. 11 f.33)

Mafafanuzi 74. Iwapo watu watatu au zaidi watakusanyika kwa nia ya kutaka
kutenda kosa, au wakiwa wamekusanyika kwa kutimiza madhumuni
Fulani kwa pamoja wakajiweka katika hali ambayo itawafanya watu
walio jirani wawe na sababu ya kuogopa kwamba watu hao
waliokusanyka watavunja amani, au kwa kukusanyika kwao kutachochea,
bure bure bila ya sababu ya maana, watu wengine wavunje amani, basi
mkusanyiko huo utakuwa mkusanyiko usio halali. Haitazamwi kama asili
ya mkusanyiko huo ilikuwa halali iwapo baada ya kukusanyika
walijiweka kwa madhumuni mamoja katika hali hiyo iliyokwisha tajwa
kabla.

Mkusanyiko usio halali unapoanza kutumiliza madhumuni


yake uliyoyakusanyikia kwa njia ya kuvunja amani na vitisho kwa watu
mkusanyiko huo utaitwa ghasia na watu waliokusanyika watasema kuwa
wamekusanyikkwa ajili ya ghasia.

Adhabu ya 75. Mtu yeyote atakayeshiriki katika mkusanyiko usio halali


mkusanyiko usio
halali amekosa kosa dogo na atapasiwa kifungo cha mwaka mmoja.

Adhabu ya ghasia 76. Mtu yeyote atakeyeshiriki katika ghasia amekosa kosa dogo.

Kutoa ilani kwa 77. Hakimu yeyote au, kama hayupo, afisa wa polisi yeyote aliye
wafanyi ghasia
kutawanyika C.A. juu ya cheo cha muamuzi au akida wa jeshi la vita la Tanganyika,
Act.2 f.7 atakayeona watu kumi na mbili au zaidi wamekusanyika kwa ajili ya
ghasia au akachelea kwamba ghasa karibu itafanywa na watu kumi na
mbili au zaidi waliokusanyika machoni pake, anaweza kutoa au kutolesha
ilani kwa jina la Rais, kwa namna atakaoona yafaa, kuwaamrisa wafanyaji
ghasia hao au watu waliokusanyika hivyo kuwa watawanyike kwa amani.

Kutawanyika kwa 78. Ikiwa utapita muda wa kufaa baada ya ilani hiyo kutolewa
wafanyi ghasia
baada ya ilani baada ya ilani hiyo kufanywa ikazuiwa kwa nguvu, ikawa watu .. na mbili
kutolewa au zaidi wataendelea kukusanyika pamoja kwa ghasia, mtu yeyote
aliyepewa mamlaka ya kutoa ilani hiyo, au afisa wa .. yeyote, au mtu

38
mwingine yeyete mahali pa afisa huyo, au wa …. Yeyote, aliyepewa
mamlaka ya kutoa ilani hiyo, au afisa wa …. Mtu huyo aliyepewa
mamlaka au afisa huyo wa polisi, anaweza …… mambo yote
yaliyolazimu ili kuwatawanya watu hao wanaoe… kukusanya au
kuwakamata wote au mmoja wao yeyote, na …. Mtu yeyote atakaidi
anaweza kutumia nguvu zote zitakazolazimu kushinda ukaidi huo na
hatapasiwa na mashitaka yoyote ya jinai …. Madai kwa kudhuru au
kumuu mtu katika kutumia nguvu hizo.

Ghasia baada ya 79. Ikiwa ilani imetolewa ya kuaamrisha watu waliojitia …


ilani
ghasia au waliokusanyika kwa ajili ya kufanya ghasia, kutawa …. Kila
mtu ambaye atashiriki au atendelea kushiriki katika ghasia au mkusanyiko
huo baada ya kupitia muda wa kufaa toka ilani kutolewa mtu huyo
amekosa kosa kubwa na atapasiwa kifungo miaka mitano.

Kuzuia ua 80. Mtu yeyote ambaye kwa kutumia nguvu atazuia au … utoaji
kupinga utoaji wa
ilani wa ilani kama ilivyo katika fungu la 77 lililotajwa amekosa .. kubwa na
atapasiwa kifungo cha miaka kumi; na kama utoaji ilani utazuiwa kwa
nguvu kila mtu ambaye atashiriki au ataend….. kushiriki katika ghasia
hiyo au mkusanyiko huo huku akijua kwamba ilani juu ya jambo hilo
imezuiwa kwa nguvu mtu huyu atapaswa kifungo cha miaka mitano.

Wafanyi ghasia 81. Watu wowote ambao wamekusanyika pamoja kwa kufanya
kubomoa
majengo n.k. ghasia wakibomoa au kuharibu, au kuanza kuboma au kuharibu jengo
lolote, njia ya reli yoyote, mtambo au matengenezo yoyote ya uhalali
watu hao wamekosa kosa kubwa na kila mmoja atapasiwa kifungo cha
maisha.

Wafanyi ghasia 82. Watu wowote ambao wamekusanyika pamoja kwa kufanya
wakihasiri
majengo n.k. gharia wakihasiri kitu chochote katika vitu vilivyotangulia …. Katika
fungu lililopita bila ya uhalali watu hao wamekosa kosa kubwa na kila
mmoja wao atapasiwa kifungo cha miaka saba.

Kuyaingilia kwa 83. Watu watakaokusanyika kwa ghasia na bila ya halali na nguvu
ghasiareli, magari
n.k. wakazuia, wakafingiza (hinder) au kupinga upakiaji au upakuaji wa reli
yoyote gari au chombo chochote au uwekaji au upitaji wa gari; au
utwekaji au kusafiri kwa bahari kwa chombo chochote bila ya uhalali na
kwa nguvu wakajipakia reline, garini au chombo ni kwa nia ya kufanya
hayo yaliyotajwa, wote watakuwa wamekosa kosa dogo.

Kutembea na 84. Mtu yeyote anayetembea na silaha katika hadhara bila ya


sialaha hadharani
jambo la halali kwa namna ambayo inaweza kuleta utisho kwa mtu yeyote
mtu huyo amekosa kosa dogo na silaha yake yaweza kuhodhiwa.

Kuingia kwa 85. Mtu yeyote ambaye kwa ajili ya kutaka kumiliki ataingia
nguvu
katika ardhi yoyote au makao yoyote kwa namna ya nguvu ni sawa nguvu

39
.. kama zilikuwa za mabavu hasa yaliyotumika kwa mtu mwingine yeyote
au ni kutishia au ni kuvunja nyumba yoyote kupita ndani au ni …
kukusanya idadi ya watu isiyo kawaida, mtu huyo amekosa kosa dogo
liitwalo “kuingia kwa nguvu”.
Haidhuru kama anayo haki ya kuingia katika ardhi hiyo au hana
isipokuwa kwamba mtu anayeingia katika ardhi au makao ambayo ni yake
mbali yake lakini yamo katika ulinzi wa mtumishi wake au mlinzi wake
haambiwi kama ametenda kosa la kuingia kwa nguvu.

Kuzuwia kwa 86. Mtu yeyote ambaye atakuwa nayo mikononi mwake ardhi bila
nguvu
ya haki yoyote na akashikilia kuwa nayo ardhi hiyo kwa namna ambayo
huenda ikaleta uvunjaji wa amani au kusababisha woga wa uvunjifu wa
amani juu ya mtu mwenye haki kwa sheria kuwa nayo ardhi hiyo, mtu
huyo amekosa kosa liitwlao “kuziwia kwa nguvu”.

Mapigano 87. Mtu yeyote ambaye atashiriki katika mapigano mahali pa


hadhara amekosa kosa dogo na atapasiwa na kifungo cha miezi sita au
kutozwa faini isiozidi shilingi mia tano.

Kusai mapiganao 88. Mtu yeyote ambaye atamsai mtu mwingine kwa mapigano ya
ya wawili
watu wawili, au atajaribu kuchochea mtu mwingine afanya mapigano ya
watu wawili au atajaribu kuchochea mtu mwingine amsai mtu mwingine
kwa mapigano ya watu wawili, mtu huyo amekosa kosa dogo.

Matusi, mzozo na 89.- (1) Mtu ye yote ambaye–


kutishia utumiaji
wa nguvu (a) atatumia maneno ya kinyaa, ya matusi au ya usafihi kwa mtu
Sh.1948 No.46 f.2 mwingine yeyote kwa namna ambayo huenda ikaleta
Sh.1948 No.46 uvunjifu wa amani; au
f.7 Act, 1962
No.12 f.2 (b) atazozana au kwa namna nyingine yeyote ataleta fujo kwa
namna ambayo huenda ikaleta uvunjifu wa amani.
mtu huyo amekosa kosa dogo na atakapoonekana na hatia atapasiwa
kifungo cha miezi sita.
(2) Mtu ye yote ambaye–
(a) kwa kusudi la kutaka kutishia au kumsumbua mtu yeyote
anatishia kuchoma nyumba au kuivunja au kuihasiri nyumba
yoyote; au
(b) kwa kusudi la kumshtua mtu yeyote atafyatua bunduki au
atatenda jambo lolote la kuvunja amani,
mtu huyo amekosa kosa dogo na atapasiwa kifungo cha mwaka mmoja.

Kuvinjari Sh.1955 89A.-(1) Mtu yeyote atakayevinjari nyumba yoyote au mahali


No.49 f.8 G.N.
1961 No.236 penginepo, au karibu karibu na nyumba hiyo au mahali hapo kwa kusudi
la –
(a) kumzuia mtu yeyote mwingine asifanya tendo ambalo kwa
sheria anaweza kulifanya; au
(b) kumlazimisha mtu yeyote mwingine kufanya tendo ambalo

40
kwa sheria anaweza kujizuia,
Mtu huyo amekosa kosa dogo na atapasiwa kifungo cha miezi sita;
Isipokuwa kwamba masharti ya fungu hili hayatatumika katika
kuvinjari ambako ni halali kwa mujibu wa sheria zinazohusu vyama vya
wafanyakazi au migogoro yao.
(2) Mtu hawezi kushitakiwa chini ya fungu hili bila ya idhini ya
maandishi ya Mkurugenzi wa Mashitaka wa Serikali.

Kutishia Sh.1961 89B.-(1) Mtu yeyote ambaye kwa dhuluma na bila ya mamlaka ya
No.f.4 G.N. 1961
No.236 sheria atamtishia mtu yeyote mwingine kwa nia ya kutaka kumlazimisha
mtu huyo mwingine –
(a) ajizue kufanya kitendo chochote ambacho ni haki yake
kukifanya; au
(b) afanya kitendo chochote ambacho ana haki kujizuia
asikifanye, mtu huyo amekosa kosa dogo na akionekana na
hatia atapasiwa kifungo cha mwaka mmoja.
(2) katika fungu hili neno–
“kutishia” lina maana ya kumfanya mtu akilini mwake awe na sababu ya
kuogopa kupata madhara yeye mwenyewe au mtu yeyote katika
ukoo wake au yeyote katika watu wanaomtegemea au kuogopa
utumiwaji wa nguvu kwa mtu yeyote au uharibifu wa mali yoyote;
neno –
“kuhasiri” linachanganya madhara kwa mtu kuhusu biashara, kazi amali
au njia nyingine ya kupatia pesa na vile vile linachanganya
dhuluma yoyote inayoweza kushitakiwa.

(3) Mtu hawezi kushitakiwa kwa kosa chini ya fungu hili bila ya
idhini ya maandishi ya Mkurugenzi wa Mashitaka wa Serikali.

Kushawishi watu 89C.-(1) Mtu yeyote ambaye, kwa nia ya kukinza, kuzuia,
wasisaidie
mipango ya kupinga au kuvunja mpango wowote wa kujitolea uliokubaliwa na Mkuu
kujitolea Act wa Mkoa au Mkuu wa Wilaya au mpango wowote wa kujitolea wa namna
1962 No. 61 f.2 iliyokubaliwa na Mkuu wa Mkoa au Mkuu wa Wilaya, atamshawishi au
kujaribu kumshawishi mtu yeyote aliyejitolea kufanya kazi za mipango
hiyo au kusaidia asifanya hivyo, mtu huyo amekosa na akionekana na
hatia atapasiwa faini isiyozidi shilingi elfu moja au kifungo cha muda
usiozidi miezi sita au yote mawili faini na kifungo pia.
(2) Katika mashitaka yoyote kwa ajili ya kosa lililofanywa
kinyuma cha fungu hili Shahada ya mkuu wa Mkoa au mkuu wa Wilaya,
kama itakavyokuwa, kwamba mpango wa kujitolea uliotajwa au
ulioelezwa ulikubaliwa na yeye katika tarehe hiyo iliyotajwa au kwamba
mipango ya kujitolea ya namna hiyo iliyoelezwa ilikubaliwa na yeye
katika tarehe iliyotajwa au kabla ya tarehe hiyo, basi shahada hiyo
itakuwa ni ushahidi uliokamilika wa matukio hayo.

Mkusanyiko kwa 90. Watu wowote ambao watakusanyika pamoja kwa idadi ya
ajili ya kufanya

41
magendo watu wawili au zaidi kwa kusudi la kuteremsha, kuchukua au kuficha
bidhaa yoyote iliyolazimu kulipwa ushuru wa forodha na ipasiwayo na
kuhodhiwa chini ya sheria inayohusu forodha watu hao wamekosa kosa
dogo na kila mmoja wao atapasiwa kifungo cha miezi sita ua kutozwa
faini isiyozidi shilingi elfu mbili.
91.-93. [Zimebatilishwa Sh.1958 No. 19 f.15]

Maafisa wa kazi 94. Mtu yeyote ambaye, ni mtumishi wa Serikali, na kwa ajili ya
za kusimamia
mali ya aina utumishi wake amepewa kazi za kimahakama au za kusimamia mali ya
maalum au wa aina maalum, au kuhusu uendeshaji wa kiwanda chochote, biashara au
kazi za maalum kazi ya aina maalum, na akiwa amepata au anayo, kwa wazi au kwa siri,
maslahi ya binafsi katika mali hiyo, kiwanda, biashara au kazi hiyo
anatimiza kazi zote hizo kwa ajili ya mali hiyo, kiwanda, biashara, au kazi
ambayo anayo hayo masilahi ndani yake au atimiza kazi yake ya
kimahakama kuhusu tabia ya mtu yeyote anayehusikana na kazi hizo mtu
huyo ni mwenye hatia ya kosa dogo, na anapasiwa kifungo cha mwaka
mmoja.

Mdai ya uwongo 95. Mtu yeyote ambaye ni mtumishi wa Serikali, yumo katika
ya maafisa
cheo cha kumtaka au cha kumuwezesha kutoa kumbukumbu au taarifa
kuhusu kiasi chochote ambacho kimelipwa au chadaiwa kuwa kimelipwa
kwake au kwa mtu mwingine yeyote; au kuhusu jambo jingine fedha au
utoaji wa bidhaa kwa mtu yeyote akifanya kumbukumbu au taarifaa
kuhusu hayo hali anajua kwamba kumbukumbu au taarifa hiyo kwa jambo
lolote mahsusi ni ya uwongo, mtu huyo ni mwenye hatia ya kosa dogo.

Kutukana 96. Mtu yeyote ambaye yumo katika kazi ya Serikali anayetenda
madaraka G.N.
1961 No.256 ua kuamrisha kitendwe kwa kutukanisha madaraka ya kazi yake, kitendo
chochote cha dhuluma ambacho chadhuru mwingine mtu huyo ni mwenye
hatia ya kosa dogo.
Iwapo kitendo hicho chatendwa au chaamriwa kwa ajili ya faida,
yeye ni mwenye hatia ya kosa kubwa, na anapasiwa kifungo cha miaka
mitatu.
Mashtaka kwa kosa lolote chini ya fungu hili au fungu mojawapo
kati ya mafungu mawili ya mwisho yaliyotangulia hayaanzishwa ila kwa
idhini ya Mkurugenzi wa Mashtaka wa Serikali.

Maafisa kutoa 97. Mtu yeyote ambaye aruhusiwa au atakiwa na sheria kutoa
shahada za uongo
shahada yoyote, kuhusu jambo lolote ambalo, kwa sababu ya shahada
hiyo haki za mtu yeyote zaweza kuharibiwa, akatoa shahada ambayo ….
Kwamba ni ya uongo katika jambo lolote muhimu mtu huyo … mwenye
hatia ya kosa dogo.

Kulisha kiapo 98. Mtu yeyote anayelisha kiapo, au yeye mwenyewe afanya
kisichoruhusiwa
na sheria uthibitisho au kiapo cha aina yeyote kuhusu jambo lolote ambalo kwa

42
sheria hana mamlaka yoyote kufanya hivyo, yeye ni mwenye hatia ya
kosa dogo na apasiwa kifungo cha mwaka mmoja.
Isipokuwa kwamba fungu hili halitatumika kwa kiapo au
uthibitisho wa aina yoyote iwapo kiapo hicho kimelishwa na, au
uthibitisho huo umefanywa mbele ya hakimu, korona au mlinzi wa amani
katika jambo lolote lihusikalo na utunzaji wa amani au adhabu ya makosa
au lihusikalo na uchunguzi juu ya vifo vya ghafla, wala fungu hili
halitatumika kwa kiapo kilicholishwa au uthibitisho wa aina yoyote
uliofanywa kwa ajili ya jambo ambalo ni halali kwa mujibu wa sheria ya
nchi nyingine, au kwa ajili ya kutia nguvu kwa maandishi hati ambayo
yakusudiwa kutumiwa katika nchi nyingine.

Kujipa mamlaka 99. Mtu yeyote ambaye–


ya uongo
(1) si afisa wa kimahakama, akijipa mamlaka ya kutenda kama
afisa wa kimahakama; au
(2) bila ya mamlaka anajipa kutenda kama mtu mwenye kupewa
mamlaka na sheria kulisha kiapo au anafanya uthibitisho wa
aina yoyote au kufanya kitendo kingine chochote kihusikacho
na watu ambacho chaweza tu kufanywa na watu
walioruhusiwa na sheria kufanya hivyo; au
(3) anajitokeza kuwa ni mtu aliyeamriwa na sheria kutia sahihi
hati inayothibitisha yaliyomo kwenye daftari yoyote au
kumbukumbu iliyowekwa na mamlaka ya halali, au
inayothibitisha kweli yoyote au tukio, akaitia sahihi hati hiyo
kama kwamba ameruhusiwa kufanya hivyo ambapo
haruhusiwi, na ajua kwamba, kwa kweli haruhusiwi hivyo,
mtu huyo ni mwenye hatia ya kosa dogo.

Kujifanya 100. Mtu yeyote ambaye–


mtumishi wa
Serikali
(1) ajifanya kuwa ndiye mtu yeyote aliye mtumishi wa Serikali
katika wakati ambao mtumishi huyo ahitajiwa kufanya tendo
lolote au kuhudhuria mahali popote kwa sababu ya kazi yake;
au
(2) ajitokeza kwa uwongo kuwa ni mtu aliyeajiriwa katika kazi
ya Serikali, na ajitia kufanya kitendo chochote au kuhudhuria
mahali popote ili afanya kitendo chochote kwa aibu kwa kazi
hiyo.
Mtu huyo ni mwenye hatia ya kosa dogo.

Kutishia 101. Yoyote ambaye atoa kitisho chochote cha kumjeruhi mtu
kuwajeruhi
watumishi wa yeyote aliyeajiriwa katika kazi ya Serikali, au kutoa kitisho hicho kwa
Serikali mtu yeyote ambaye aamini kwamba ahusika naye, ili kumshawishi mtu
huyo kufanya kitendo chochote au kuvumilia au kuchelewesha kufanya
kitendo chochote ambacho chahusika na utimizaji wa kazi za Serikali za
mtu huyo, basi yeye ni mwenye hatia ya kosa dogo.

43
SURA YA XI
MAKOSA YAHUSUYO USIMAMIAJI WA HAKI

Ushahidi wa 102.-(1) Mtu yeyote ambaye, katika kesi yoyote, au kwa ajili ya
uwongo
kuanzisha kesi yeyote, kwa kujua, akitoa ushahidi wa uwongo kuhusu
jambo lolote ambalo ni muhimu kwa hoja yoyote inayotegemea au
inayokusudiwa kutolewa katika kesi hiyo, mtu huyo ni mwenye hatia ya
kosa dogo liitwlao “ushahidi wa uwongo”.
Haidhuru ikiwa ushahidi huo unatolewa kwa kiapo au kwa mujibu wa idhini
nyingine yoyote inayoamriwa na sheria.
Namna na kawaida zilizotumiwa kwenye kulisha kiapo hicho au
zinazomlazimisha mtoa ushahidi huo kusema kweli hazidhurishi neno
iwapo atazikiri namna na kawaida hizo zilizotumiwa hasa.
Haidhuru neno iwapo ushahidi wa uwogo huo unatolewa kwa mdomo au
kwa maandishi.
Haidhuru neno iwe mahakama hiyo imekamilika au baraza hilo lipo mahali
panpotakiwa au sivyo, iwapo yafanya kazi hasa kama mahakama au baraza
katika kesi ambayo yatolewa ushahidi huo.
Haidhuru neno iwe huyo mtu anayetoa ushahidi huo ni shahidi afaae au
sivyo, au kwamba ushahidi huo wakubalika katika kesi hiyo au sivyo.

Kushawishi (2) Mtu yeyote ambaye asaidia, ashiriki, ashauri, atuma, au


ushahidi wa
uwongo ashawishi mtu mwingine kutoa ushahidi wa uwogo, ni mwnye hatia ya kosa
dogo liitwalo “kushawishi ushahidi wa uwongo”.

Maelezo ya 103. Mtu yeyote ambaye, ameapishwa kwa halali kuwa mkalimani
uwongo ya
wakalimani katika kesi kwa makusudi, akatoa maelezo muhimu katika kesi hiyo,
maelezo ambayo ajua kuwa ni ya uwongo, au ambayo haamini kuwa ni
kweli, ni mwenye hatia ya kosa dogo liitwalo “ushahidi wa uwongo”.

Adhabu kwa 104. Mtu yeyote anayefanya kosa la kutoa ushahidi wa uwongo au
ushahidi wa
uwongo kushawishi ushahidi wa uwongo anapasiwa kifungo cha miaka saba.

Ushahidi juu ya 105. Mtu hawezi kuonekana na hatia kwa kosa la kutoa ushahidi wa
shtaka la kutoa
ushahidi wa uwongo au la kushawishi ushahidi wa uwongo kwa ushahidi wa shahidi
uwongo mmoja tu kuhusu uwongo wa habari yoyote inayoambiwa ni uwongo.

Ushahidi wa 106. Mtu yeyote ambaye, kwa kusudi la kuidanganya baraza yote
kutunga
katika kesi–
(1) atunga ushahidi kwa njia yoyote nyingine isiyokuwa ya
ushahidi wa uwongo au ya kushawishi ushahidi wa uwongo; au
(2) kwa makusudi autumia ushahidi huo wa kutunga, ni mwenye
hatia ya kosa dogo, na anaasiwa kifungo cha miaka saba.

Kuapa uwongo 107. Mtu yeyote anayeapa uwongo au kufanya uthibitisho au


matamshi ya uwongo mbele ya mtu yeyote anayeruhusiwa kulisha kiapo au

44
kupokea matamshi ya jambo lolote lihusulo watu katika hali ambayo kuapa
uwongo hulo au kutoa matamshi ya uwongo huo kama kukitendwa katika
kesi kungelikuwa ni sawa na kutoa ushahidi wa uwongo, mtu huyo ni
mwenye hatia ya kosa dogo.

Kudanganya 108. Mtu yeyote afanyae hadaa au udanganyifu, au, kwa makusudi
mashahidi
atoa au adhihirisha maelezo yoyote ya uzushi, ishara au maandishi ya
uwogo, kwa mtu yeyote aitwae au atakayeitwa kuwa ni shahidi katika kesi
yeyote kwa kusudi la kuharibu ushahidi wa shahidi huyo, ni mwenye hatia
ya kosa dogo.

Kuharibu 109. Mtu yeyote ambaye, kwa kujua kwamba kitabu chochote, hati
ushahidi
au kitu cha namna yoyote iwayo chahitajika au chaweza kuhitajiwa kwenye
ushahidi katika kesi, kwa makusudio akakiondosha au kukiharibu au
kukifanya kisisomeke au kisifahamike kwenye ushahidi mtu huyo ni
mwenye hatia ya kosa dogo.

Njama kupinga 110. Mtu yeyote afanya kosa dogo, ambaye–


haki na
kuingilia (a) kula njama na mtu mwingine yeyote kumsingizia mtu yeyote
mashahidi na kosa lolote la jinai au kufanya jambo lolote ili kukinga,
Sh.1961 No.5 kuzuia, kukaidi au kupotosha njia ya haki; au
f.5
(b) kwa kusudi la kukinga njia halisi ya haki, amshawishi,
amzuwia au amkataza mtu yeyote mwenye lazima ya halali ya
kuhudhuria mahakamani na kutoa ushahidi akiwa ni shahidi,
asihudhurie kutoa ushahidi huo, au anayejitahidi kufanya
hivyo.

Kufifilisha 111. Mtu yeyote ambaye aomba, apokea, au akubali au ajaribu


makosa
makubwa kupokea au kupata mali yoyote kwa ajili yake mwenyewe au mtu mwengine
yeyote kwa ajili ya mapatano yoyote au kwa kufahamu kwamba atafifilisha
au kuficha kosa kubwa, au ataepuka au kukomesha, au kukawilisha shtaka
la kosa kubwa hilo, ni mwenye hatia ya kosa dogo.

Kufifilisha 112. Mtu yeyote ambaye, ameleta au ajisingizia kuleta shtaka, juu
mashtaka
yapasayo ya mtu mwingine lihusikalo na sheria ya adhabu au sheria yeyote ili apate
adhabu adhabu kwa kosa lolote ambalo limetendwa au lasema limetendwa naye,
akalififilisha shtaka hilo bila ya amri ya idhini ya mahakama ambayo
analipeleka au atalipeleka, ni wenye hatia ya kosa dogo.

Tangazo la 113. Mtu yeyote ambaye–


mali iliyoibiwa
(1) atangaza kutoa zawadi hadharani ili arejeshewe mali ambayo
imeibwa au imepotea na katika kutoa zawadi hiyo atumia
maneno ya kwamba hakuna maswali yatakayoulizwa, au huyo
mtu anayetoa mali hiyo hatakamatwa au kudhuriwa; au
(2) atangaza hadharani kumrejeshea mtu yeyote ambaye labda
amenunua au ametanguliza malipo ya fedha kwa njia ya

45
kukopa kwa ajili ya mali yoyote iliyoibiwa au kupotea,
kumrejeshea mali hiyo iliyoibiwa au kutangulizwa au kiasi
kingine chochote cha fedha au zawadi kwa ajili ya kurejeshwa
kwa mali hiyo; au
(3) achapisha au atangaza ahadi kama hiyo, mtu huyo, ni mwenye
hatia ya kosa dogo.

Kudharau 114.-(1) Mtu yeyote ambaye–


mahakama
(a) aonyesha ukosefu wa adabu, kwa matamshi au tabia, kwenye
kesi yoyote, ndani ya jengo au mahali jirani ya jengo hilo
ambamo kesi hiyo yasikilizwa au yafanywa, au mbele ya mtu
yeyote ambaye anaisikiliza au anaifanya kesi hiyo; au
(b) amehitajiwa kutoa ushahidi katika kesi akakosa kuhudhuria au,
amehudhuria lakini akataa kuapishwa au kuthibitishwa, au
ameapishwa au kuthibitishwa, lakini akakataa bila ya kuwa na
sababu ya halali kujibu swali au kutoa hati, au abaki chumbani
ambamo kesi hiyo inasikilizwa au inafanywa, baada ya
mashabiki kuamriwa kutoka chumbani humo; au
(c) aleta pingamizi au fujo wakati kesi hiyo ikiendeshwa; au
(d) wakati kesi hiyo ikiahirishwa, atumia matamshi au maandishi
yanayogeuza kesi hiyo, au yawezayo kuharibu wazo la mtu
yeyote mwenye upendeleo au kinyume cha wadaawa wowote
wa kesi hiyo au yanayokusudiwa kupunguza mamlaka ya mtu
yeyote ambaye kesi hiyo yasikilizwa au yafanywa mbele yake;
au
(e) atangaza habari za ushahidi uliochukuliwa kwenye kesi yoyote
iliyoamriwa iendeshwe faraghani; au
(f) bila ya haki ajaribu kumuingilia au kumshawishi shahidi juu ya
ushahidi ambao ameshautoa au kabla ya kutoa ushaidi huo
uhusikao na kesi; au
(g) amfukuza mtumishi kwa sababu ametoa ushahidi kwa niaba ya
mdaawa fulani katika kesi; au
(h) achukua tena ardhi kutoka kwa mtu yeyote ambaye punde tu
ameimiliki ardhi hiyo kwa hati ya mahakama; au
(i) afanya kitendo chochote kwa makusudi cha kutoheshimu kesi
yoyote au mtu yeyote ambaye kesi hiyo yaendeshwa au
kufanywa mbele yake tu huyo ni mwenye hatia ya kosa dogo,
na anapasiwa kifungo cha miezi sita au kutozwa faini isiyozidi
shilingi mia tano.
(j) … kosa lolote kinyume cha fasili (a), (b), (c), (d) au (i) ZA
….linafanywa machoni mwa mahakama, mahakama yaweza …
mkosaji kizuizini na wakati wowote kabla ya mahakama …
siku hiyo yaweza kuhukumu kosa hilo kwa kufuata ….
Kumtoza mkosaji huyo faini ya shilingi mia nne au, kulipa,
kumtia kifungoni kwa mwezi mmoja.
(k) …ya fungu hili yatahesabiwa kuwa ni ziada, na si kwamba …

46
wa Mahakama Kuu kutoa adhabu kwa kosa la mahakama.

Kuzuia au 114A. Mtu yeyote ambaye–


kukinga
uwasilishaji au (a) ….. kusudi akinga, au kwa kusudi azuwia au kwa njia yeyote ..
utimilizaji wa au apinga, uwasilishaji wa kuitwa shaurini inayopelekwa
hati Sh.1961 ….mwenyewe au kwa mtu mwingine yeyote, notisi, amri , hati
No.5 f.6
ya kukamatia au hati nyengineyo ambayo … na mahakama
kupelekwa kwake yeye mwenyewe …. Mtu mwingine, kama
itakavyokuwa; au
(b) ……kusudi akinga, au kwa kujua azuwia, au kwa njia yoyote
… apinga utimilizaji wa kwita shaurini yoyote, notisi, ya
kukamatia au hati nyingineyo ambayo imetolewa …, au
kumkinga, kumzuia, kumuingilia, kupinga … na halali ya
utilimizaji wa hati hiyo; au
(c) …… ili kuepuka kuwasilishiwa kwita shaurini yoyote, … hati
ya kukamtia ua hati nyingine ambayo ime …. mahakama,
(d) …. Yenye hatia ya koso dogo na atapasiwa aonekanpo na …
muda uziozidi mwaka mmoja

SURA YA XII
…………. KUWAKINGA WATUMISHI WA
MAHAKAMA YA SHERIA

kUTOA 115.-(1) Mtu yeyote ambaye atamtoa au atajaribu kumtoa kwa


nguvu ….. yeyote kwenye ulizi wa halali –

(a) ……aliyemo katika ulinzi huo amehukumiwa kifo au kifungo


cha maisha au ameshtakiwa kwakosa lenya adhabuya kifungo
cha maisha, mtu huyo ni mwenye hatia ya kosa na anapasiwa
kifungo cha maisha; na
(b) …mwingine huyo ametiwa gerezani kwa shtaka au yumo
katika adhabu kwa kosa lolote lisilokuwa katika hayo yaliyo…
mtu huyo ni mwenye hatia ya kosa kubwa, na kifungo cha
miaka saba; na
(c) …. vyoyote, mwenye hatia ya kosa dogo.
…… anayetolewa yumo kwenye ulinzi wa mtu asiyekuwa ….. lazima
apaswe habari ya ukweli huo kwamba …. Yumo kwenye ulinzi kama huo.

Kutoroka 116. …ambaye, yumo kwenye ulinzi wa halali, akitoroka …


kwenye ulinzi
wa halali mwenye hatia ya kosa dogo.

Kutohudhuria 116A.-(1) Mtu yeyote ambaye ameruhusiwa kufanya kazi nje ya


na kwenye kazi
ya kifungo cha gereza, kwa kufuata masharti ya fungu 87 la Sheria ya Magereza, akikosa
jela baridi kuhudhuria katika saa iliyowekwa, au kutokuwapo kwenye kazi yake, yeye
Sh.58 Sh.1951 ni mwenye hatia ya kosa dogo ila atakapoitosheleza mahakama kwamba
No. 32 f.2
alikuwa na udhuru wa maana na wa halali kwa kutohudhuria huko.

47
(2) Adhabu yoyote ya kifungo ambayo inatolewa kwa kosa dogo
kwa mujibu wa kifungu (1) cha fungu hili itajumlishwa kwenye kifungo
chochote ambacho muhukumiwa huyo apasiwa nacho na kile ambacho
amehukumiwa kukitumikia chini ya kifungu (7) cha fungu la 87 la Sheria
ya magereza.

Kusaidia 117. Mtu yeyote ambaye–


wafungwa
kutoroka (a) amsaidia mfungwa kutoroka au kujaribu kutoroka kwenye
ulinzi wa halali; au
(b) apeleka kitu chochote au afanya kitu chochote kupelekwa
ndani ya gereza kwa kusudi la kumwezesha mfungwa
kutoroka;
Mtu huyo ni mwenye hatia ya kosa kubwa, na apasiwa kifungo cha miaka
saba.

Uondoshaji n.k. 118. Mtu yeyote ambaye, mali yoyote imetiwa tanzi au
wa mali yoyote
iliyokamatwa imechukuliwa kwa hati ya mamlaka ya mahakama yoyote, kwa kujua, na
kwa halali kwa kusudi la kuzuwia au kupinga tanzi hilo au hati hiyo, aipokea,
aiondosha, aizuiwa, aificha, au aitoa mali hiyo, mtu huyo ni mwenye hatia
ya kosa kubwa, na apasiwa kifungo cha miaka mtiatu.

119. [Imeebatilishwa Sheria 1961 No. 5 f.7]

SURA YA XIII
MAKOSA YA MCHANGANYIKO KUITENDEA SERIKALI

Udanganyifu 120. Mtu yeyote aliyeajiriwa katika kazi ya Serikali ambaye katika
wa uvunjaji
uaminifu kwa kufanya shughuli za kazi yake, afanya udanganyifu wowote au uvunjaji
watumishi wa uaminifu ambao utadhuru watu, iwe udanganyifu huo au uvunjaji uaminifu
Serikali huo ungekuwa ni jinai au sivyo lau kama ungetendewa mtu raia, mtu huyo
ni mwenye hatia ya kosa dogo.

Kupuuza kazi 121. Kila mtu aliyeajiriwa katika kazi ya serikali ambaye, kwa
ya Serikali
makusudi, atapuuza kufanya shughuli yoyote ambayo yamlazimu kuifanya
kwa mujibu wa mila ya Kiingereza au sheria yoyote, mtu huyo atakua na
hatia ya kosa dogo, ila iwapo shughuli hiyo itakuwa na hatari kubwa zaidi
kuliko ile ambayo mtu hodari na mwenye juhudi ya kawaida aweza
kuikabili.

Kutoa taarifa 122. Mtu yeyote ambaye atoa taarifa yoyote kwa mtumishi wa
ya uwongo kwa
mtumishi wa Serikali kwa kujua au kwa kuamini kwamba taarifa hiyo ni ya uwongo, kwa
Serikali kusudi la kumfanya mtumishi huyo, au kwa kuamini kwamba taarifa hiyo
yaweza kumfanya mtumishi huyo–
(a) kufanya au kutofanya jambo lolote ambalo lampasa alifanya au
asilifanye kama angejua hali ya ukweli wa taarifa hiyo ulivyo;
au

48
(b) kutumia uwezo wa halali wa mtumishi huyo ili kumdhuru au
kumuudhi mtu yeyote,
Mtu huyo atakuwa ni mwenye hatia ya kosa dogo, na atapasiwa kifungo cha
miezi sita au faini ya shilingi elfu moja au yote mawili faini hiyo na kifungo
hicho.

Kutotiii wajibu 123. Kila mtu ambaye, kwa makusudi, hatii sheria yoyote kwa
wa Sheria
kutenda kitendo chochote ambacho chakatazwa na sheria au hatii sheria
kwa kutotenda kitendo chochote ambacho chahusika na watu au sehemu
yoyote ya watu, mtu huyo ni mwenye hatia ya kosa dogo, na isipokuwa
yaonekana kwamba sheria ilikusudia kutoa adhabu nyengine, atapasiwa
kifungo cha miaka miwili.

Kutotii amri za 124. Kila mtu ambaye hatii amri yoyote, hati ya kukamatia au
halali
amri inayowekwa, kutolewa au inayotokana na mahakama yoyote mtumishi
wa Serikali au mtu wa cheo chochote aliyeamriwa kufanya kazi ya Serikali,
mtu huyo ni mwenye hatia ya kosa dogo, na isipokuwa adhabu nyengine
yoyote au namna ya kesi kwa kutotii huko kuelezwa, atapasiwa kifungo cha
miaka miwili.

124A. Mtu yeyote ambaye atenda kitendo chochote au atamka


maneno yoyote au atangaza maandishi yoyote, kwa kusudi la kusafihi au
kufanya idharauliwe au idhihakiwe bendera rasmi ya taifa au alama rasmi
ya Tanganyika, au mfano wowote au picha yoyote ya bendera rasmi au
alama rasmi ya Tanganyika, mtu huyo atakuwa amekosa na atakapoonekana
na hatia atapasiwa faini isiyozidi shilingi elfu moja au kifungo kisichozidi
miezi kumi na mbili au yote mawili faini hiyo na kifungo hicho.

Kigawe cha III. – Makosa yatayodhuru watu kwa jumla

SURA YA XIV
MAKOSA YAHUSUYO DINI

Kusafihi dini 125. Mtu yeyote ambaye atavunja, kuharibu au kuchafua mahali
ya watu
wowote popote pa kuabudia a kitu chochote kinachoitakidiwa kitakatifu na watu wa
aina yoyote kusudi la kusasfihi dini ya aina yoyote ya watu au kwa kujua
kwamba watu wa aina Fulani huenda wakafikiria uvunjaji, uharibifu na
uchafuaji huo kuwa ni usafihi kwa dini yao mtu huyo amekosa kosa dogo.

Kufuja 126. Mtu yeyote ambaye kwa hiyari ataleta fujo katika mkusanyiko
mikusanyiko ya
dini wowote uliokusanyika kwa uhalali kufanya ibada au sharahe za dini
amekosa kosa dogo.

Kuingia 127. Kila mtu ambaye kwa kusudi la …………………… yoyote au


maziarani bila
idhini kusafihi dini ya mtu yeyote au kwa kujua kwamba mtu yeyote huenda
……………………………………….. atatenda kitecho cha kuingia bila

49
idhini mhali popote pa ibada au mahali popote maziara au kufanywa mahali
pa kuweka mabaki ya maiti au atafanya dharau yoyote kwa maiti ya
binadamu au atafanya fujo kwa watu wowote waliokusanyika kwa ajili ya
mazishi mtu huyo amekosa kosa dogo.

Kuzuia maiti 128.(1) Mtu yeyote ambaye………….. ……………………….


kuzikwa Act
1963 No.15 f.2 …………………………………..……………………………………………
………………………………………………………………………………
…………………yeyote au mtu yeyote ambaye akiwa na wajibu wa
kufanya maiti ya mtu yeyote izikwe akapuuza kutimiza wajibu wake kwa
makusudi na bila halali ya kufanya hivyo, mtu huo atakuwa amekosa kosa
dogo.
(2) Katika kifungu cha (1) “Waziri” ina maana ya Waziri
mwenye madaraka kwa wakati uliopo juu ya mambo yanayohusu afya.

Kutamka 129. Mtu yeyote ambaye kwa dhamiri hasa ya kumuudhi mtu
maneno kwa
nia ya kuudhi yeyote juu ya imani yake ya dini akatamka maneno yoyote au akafanya
imani ya dini sauti yoyote itakayosikiwa na mtu huyo au akafanya ishara mbele ya mtu
huyo au akaweka kitu machoni pa mtu huyo, mtu afanyae hivyo amekosa
kosa dogo na atapasiwa kifungo cha mwaka mmoja.

SURA YA XV
MAKOSA KINYUME CHA UTU

Ufafanuzi wa 130. Mtu yeyote ambaye bila halali atamuundama mwanamke au


kubaka
msichana bila idhini yake, au kwa idhini yake ikiwa idhini kaipata kwa
nguvu au kwa njia ya kuhofisha au kutishia kwa namna yoyote au kwa hofu
ya kuumizwa kiwiliwili, au kwa njia ya madanganyo juu ya namna ya
kitendo chenyewe kilivyo au, kwa upande wa muolewa, kwa kujifanya ni
mumewe, mtu huyo amekosa kosa kubwa liitwalo “kubaka”.

Adhabu ya 131. Mtu yeyote ambaye atatenda kosa la kubaka atapasiwa adhabu
kubaka
ya kifungo cha maisha pamoja na kutandikwa au bila kutandikwa.

Jaribio 132. Mtu yeyote ambaye atajaribu kubaka amekosa kosa kubwa na
atapasiwa kifungo cha maisha pamoja na kutandikwa au bila ya
kutandikwa.

Kupoka 133. Mtu yeyote ambaye kwa dhamira ya kumwona au kmuundama


mwanamke wa umri wowote au kumfanya aolewe au kuandamiwa na mtu
mwingine yeyote, akamchukua mwanamke huyo au kuzuia bila ya radhi
yake, mtu huyo amekosa kosa kubwa na atapasiwa kifungo cha miaka saba.

Kupoka 134. Mtu yeyote ambaye bila halali atamchukua msichana


wasichana
walio chini ya asiyeolewa aliye chini ya umri wa miaka kumi na sita kutoka katika ulinzi
miaka kumi na au hifadhi ya baba yake au mama yake au mtu mwingine mwenye uangalizi
sita

50
wa halali na madaraka juu ya msichana huyo, na akamchukua bila ya radhi
ya baba yake au mama huyo au huyo mtu mwingine, mtu huyo amekosa
kosa dogo.

Sshambulio la 135.-(1) Mtu yeyote ambaye bila halali atamfanyia shambulo la aibu
aibu kwa
wanawake mwanamke yeyote au msichana yeyote, amekosa kosa kubwa na atapasiwa
Sh.1954 No. 47 kifungo cha miaka kumi na nne.
f.3
(2) Iwapo shitaka la shambulio la aibu chini ya fungu hili linahusu
msichana aliye chini ya umri wa miaka kumi na mbili itakuwa si utetezi juu
ya shitaka hilo kudai kwamba alikubali mwenyewe kutanyiwa kitendo cha
aibu hicho.
Isipokuwa kwamba itakuwa ni utetezi wa kutosha juu ya shitaka lolote la
namna hiyo ikiwa itadhihirishwa mbele ya mahakama ambayo shitaka hilo
linapelekwa kwamba mtu huyo aliyeshitakiwa alikuwa na sababu ya
kutosha kumfanya aamini na ikiwa kwa hakika aliamini kwamba msichana
huyo alikuwa na umri wa kuzidi miaka kumi na mbili.

51

You might also like