You are on page 1of 3

Modi ya Data Nenda kwa Bila malipo

9+ 1 20

Ananias Edgartz
15 Mei saa 13:38 ·

Hivi kuna mtu aliyekula bata dunia hii kama Mobutu Sese Seko Kuku Ngbendu wa Zabanga?
Denis Mpagaze
________________________________________
Huyu bwana alikuwa tajiri wa kutupa ndani ya umaskini wa kunuka. Alitumia muda mwingi hapa duniani
kula bata. Na alikula kweli. Alikuwa na Meli ya kifahari maalum kwa kulia bata. Aliita Kamanyola.
Ilimzungusha ndani ya mto Congo akila na kunywa vya kutoka Ulaya. Alijenga Kasri kijijini kwake
Gbadolite lenye vyumba 100 na hoteli ya kitalii ya nyota 5 iliyoitwa Motel Nzekele. Kazi kubwa
zilizofanyika katika kasri hilo ilikuwa ni anasa kwenda mbele. Moja ya anasa kufuru kabisa ni ile ndoa ya
binti yake Yakpwa mwaka 1992. Shela yake tu iligharimu dola za Kimarekani 70,000 sawa na milioni mia
saba sabini na tano za Kitanzania. Keki ya harusi na mapambo viligharimu dola za Kimarekani 65,000
sawa na milino mia saba za Bongo, cheni na hereni viligharimu dola za kimarekani milioni 3. Zaidi ya
wageni 2500 waliokula mlo wa lobster na mayai ya samaki na kishushio cha shampeni nyekundu na
mvinyo kutoka Ufaransa kwa ndege ya kukodi.
Wakati wa ziara zake za majimboni aliandaliwa vibinti vibichi kabisa ili kumpa raha. Alisumbua sana enzi
zake huyu jamaa. Alikuwa anakwenda kunyoa Ubelgiji na watoto wake walisoma Ufaransa na kurudi
Kongo kila wikendi. Alijenga uwanja wa ndege wa kimataifa kijijini kwake, uwanja wenye uwezo wa kutua
ndege aina ya Concordi, ambazo mara kwa mara alizikodi kwenda shopping Paris na Uholanzi. Akiingia
shopping Hapana lilia lia kuomba punguzo la bei.
Aliwahamasisha viongozi wake kuiba kwa akili. Aliwaambia polisi na wanajeshi hawana akili kudai
mshahara na wakati wanabunduki.
Alikuwa na nyumba ya kifahari katikati ya jiji la Paris, hekalu la vyumba 32 Uswisi, Kasri la adabu huko
Uhispania na nyumba ya vyumba 30 huko Lausanne. Alipiga marufuku mwanasiasa yeyote kutamkwa
wala kuonekana kwenye TV zaidi yake.
Mke wake wa kwanza Maria Anttoinette alikufa baada ya kupigwa na Mobutu akiwa mja mzito. Baada ya
kifo, Mobutu alimuoa Bobi Ladawa, mchepuko wake wa muda mrefu. Ilikuwa amuoe mama 41,
mchepuko wake wa siku nyingi lakini siku chache kabla ya harusi mama 41 alipofuka macho. Ndumba?
Sijui. Lakini wakati wa ndoa yake na Bobi, Mobutu alimualika papa Paul wa II alipotembelea Kinshasa ili
awe mgeni rasmi, papa alikataa. Bobi Ladawa alikuwa na pacha wake waliofanana sana , tena mke wa
mtu lakini Mobutu alimpenda na kumuoa pia. Pacha akaacha mume wake akiwa na mtoto mmoja na
kufuata mdundiko. Mume wa huyo pacha alifariki miaka ya 90.
Mobutu alimuhasi Karl Bond Nguza, waziri wake wa mambo ya nje baada ya kuskia jamaa alimtongoza
mke wa Mobutu. Hapo kabla alitaka kumuua kwa risasi ila akaghairi. Akaamua kumhasi. Wahenga
walisema ukiua kwa upanga utakufa kwa upanga. Mobutu alikufa kwa kansa iliyoutafuna uume wake
yaani tezi dume.
Pamoja na kwamba Mobutu aliuchukia ukristo alijenga kanisa nyumbani kwake na kuwazika mke na
watoto wake.Kwa nini alichukia ukristo? Akiwa anajiandaa kwa mtihani wa darasa la 12, alitoroka
seminari na kwenda kumuona mchumba wake. Wakati anarudi mapadre walimkamata na adhabu yake
iliamuriwa asiende kidato cha tano na badala yake apelekwe jeshini. Mobutu aliumia sana kutokwenda
kidato cha tano. Aliposhika dola aliwapiga marufuku mapadri wa Zaire kubatiza watoto kwa majina ya
kizungu.
Mobutu alikuwa ni mtu wa visasi. Alimfanyia kitu kibaya sana Pierre Mulele ambaye alikuwa rafiki wa
Lumumba. Baada ya Lumumba kufariki Mulele alikimbimbilia Brazzaville. Mobutu alimtumia ujumbe
kumuomba arudi nyumbani ampe nafasi ya uongozi. Alivyorudi tu Mobutu alimkamata Mulele na kuanza
kumkata kidole kimoja baada ya kingine mpaka akafa.
Nyerere, Kaunda na Mobutu waliunda Mulungushi Club ili kujadili Ukombozi wa Afrika miaka ya sabini.
Lakini kila walilojadili Mobutu alivujisha siri kwa wafaransa. Mwalimu akaona ujinga, akaachana naye,
club ikafa. Lakini pia Nyerere alivyomwambia Mobutu anaongeza nchi kidikteta, Mobutu alimwambia
Nyerere kwamba Zaire si Tanzania kama haamini wabadilishane nchi na kama atakubali kuwa Rais wa
Zaire hatamaliza hata miezi mitatu, atapinduliwa na mwanamke.
Alimtia jela hayati Fránco Luambo Màkiadi kwa kumkosoa kupitia uimbaji wake. Akampa shariti la
kutumia akili yake kutafuta kitu kitakachomfurahisha ili amwachie huru. Frànco akamtungia kibao cha
kumfagilia kilichojulikana kama Candidat na Bisso Mobutu. Mobutu alifurahi mno, akamtoa kifungoni na
kumfanyia Frànco pati ya kufa mtu Ikulu kisha kumwachia huru.
Miaka miwili kabla ya kifo chake alijigamba kuwa tangu azaliwe hakuwahi kuugua kiasi cha kulazwa
hospitali. Alipougua hakupona.
Mobutu alikuwa mwoga sana, alipokuwa anasafiri kwenda nje ya nchi, aliondoka na waziri wa ulinzi,
mkuu wa majeshi na funguo za maghala ya silaha lazima awe nazo yeye kwenye briefcase yake.
Huyu bwana aliamini sana katika mambo ya ushirikina (ndumba). Aliajiri waganga 100 Ikulu. Miaka ya
1975 alikodi wachawi na waganga wote wa Zaire kwenda Ujerumani kwenye mechi kuwanga ili timu
ishinde. Walipigwa tisa kwa nunge.
Mobutu alipendwa sana na nchi za Magharibi kwa sababu alionekana kusimamia maslahi yao kwa
kupambana na ukomunisti. Alimuandaa mwanaye wa kwanza Nyiwa ili kumrithi lakini Nyiwa alikufa kwa
UKIMWI mwaka 1994. Ukomunist ulipokufa walimfyekelea kule kama maganda ya ndizi. Alifia Morocco
mwaka 1997 na kuzikwa na watu wasiozidi 6 pamoja na utajiri wote aliokuwa nao.

Penda Toa maoni

Wilondja Kipanga
Hatari kweli
mos 5 Penda Jibu Zaidi

Junior Prosper
alimiliki utajili wa hela zipatazo ngapi, mali kama nini..yaani madini, na vitega uchumi vingapi,
maana ndo utajili huo. Naviomba ndugu, maana huwa nasikia tu... Kuwa alikuwa rais tajili mno,
ila sijajua hadi sasa, sifa hzo zilitokana na nini.
mos 5 Penda Jibu Zaidi

Edgar Lucas
nakubali sana ndgu unakipaji kikubwa mungu azidi kukubariki
mos 5 Penda Jibu Zaidi

Roby DE Madrid
Nakukubal xan bro kwa kutujuza past events God bless you
mos 5 Penda Jibu Zaidi

Andika maoni... Chapisha

You might also like