You are on page 1of 5

MWALIMU SIFUNA WHATSAPP 0791801250

NEW 2024
DONDOO NA
MAJIBU

M A PA M B A Z U K O
YA M A C H W E O

B Y M WA L I M U
SIFUNA
1
MWALIMU SIFUNA WHATSAPP 0791801250

0718055483
1. Mume wangu, ninapoandika waraka huu, naomba uelewe kuwa wanao wawili
wanazidi kuumia. Labda unadhani unayoyafanya ni siri ila usilolijua ni
kwamba kila ufanyalo nalifahamu.
a) Fafanua muktadha wa dondoo hili (alama 4)
 Ni maneno ya Bi suluhu katika barua kwa mumewe,
 Yaliyosomwa na Abigael
 Alikuwa kwenye chumba walipopatana Abigael na Bw. Suluhu.
 Barua ilikuwa ya kumjulisha Suluhu kuwa yote aliyoyafanya yalijulikana
b) Tambua umuhimu wa mandhari katika dondoo hili katika kujenga maudhui
(alama 4)
 Yachimuza maudhui ya uzinifu- Suluhu anashiriki mapenzi nje ya ndoa na
wasichana wadogo.
 Maudhui ya uozo- Bw. Suluhu ana wapenzi wengi na ambao ni wachanga.
Anashiriki mapenzi na Abigael bila kujali kuwa atamwambukiza ugonjwa.
 Kuimbua maudhui ya Unafiki- Suluhu anafikiri anapendwa na Abigael na hata
kufikiri kumwoa ilhali Abigael anajifanya na hata kupanga kumuua.
 Ukatili- Abigael anaisagasaga dawa kwa nia ya kumpa Suluhu ili apate nafasi ya
kumuua./ kuteguliwa kwa kitendawili cha kifo cha mamake
 Mapenzi- Suluhu anampenda Abigael na alitamani hata waoane. Anajiona kama
mfalme wakiwa na Abigael.
 Majuto- Abigael anajutia kuingilia ndoa ya Suluhu na mkewe baada ya kusoma
kisa cha Bi. Suluhu.
 Uwajibikaji- Abigael anaamua kuwajibikia maisha yake baada ya kusoma barua.
 Barua ile ilifichua kutowajibika kwa Suluhu kwa familia, wananchi waliomchagua
na kwa Abigael kwa kutomwambia ukweli kuhusu afya yake.
c) Bainisha hulka nne za mzungumzaji (alama 4)
Sifa za Bi. Suluhu
 Mvumilivu- anavumilia kusalitiwa kimapenzi na Suluhu Msiri - hakumwambia
yeyote siri z amumewe alizojua Mwajibikaji - aliweza kujitahidi na kuwalea wanawe
peke yake.
 Mwadilifu- ansema angeweza kumfanyia mumewe mengi hata kumpa sumu ila
hakuyafanya
 Mpelelezi/mpekuzi- anafanya uchunguzi wake na kujua mahusiano ya mumewe
 Mshauri mwema- anamshauri Suluhu kumwambia Abigael ukweli
 Mwenye mapenzi- alimpenda mumewe
d) Onyesha toni inayojitokeza katika dondoo hili (alama 2)
 Toni ya uchungu- anaumwa kuwa watoto wake wanaumia kwa matendo ya
mumewe.

2
MWALIMU SIFUNA WHATSAPP 0791801250

e) Dhihirisha kuwa kila alilolifanya mumewe lilijulikana (alama 6)


Alijua kwamba:
 Yule binti wa chuo kikuu aliyepanga ahitimu kabla ya muda wake aliishia
kumtunga mimba na kumwacha bila tumaini.
 Hata yule hawara mwingine aliyeishia kumpangia chumba kule mjini ili asijue
alimwambia kila kitu.
 Alimuua mama Abigael ila hakuwaambia polisi
 Alinyakua shamba la mamake Abigael.
 Alifuja pesa za wananchi kwa kuwalipa wasichana wa vyuo vikuu baada ya kula
uroda nao.
 Alishindwa kuleta maendeleo kwa kuwa alitafuta mbinu ya kumlipa Bw. Ngoma
pesa alizomkopesha za kampeni ya ubunge.
 Kuwa hajamwambia Abigael kuwa ameugua
2. “Poko! Ukiumwa na nyuki haina haja ya kujitwika jukumu la kuharibu
mizinga yote ya asali. Hujui faida ya nyuki ulimwenguni? Uliamua kuharibu
asali ya nchi.
Jadili maudhui ya ukiukaji wa haki za watoto katika hadith i ya ; i.
i. Mapambazuko ya Machweo (alama 10)
ii. Sabina (alama 10)
.
3. Siku moja alipokataa katakata kuandamana na mumewe, jungu lilifoka.
“Wewe mke sampuli gani usiyetaka kumuunga mko no mmeo?” Haya kaa
nyumbani. Kula na kulala tu, hujui jingine. Ona umbo lako sasa, kama
nguruwe. Si mke mrembo niliyeoa! Wanawake ni wengi…”
a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)

b) Bainisha vipengele vinne vya kimtindo katika dondoo hili (alama 4)


c) Fafanua nafasi ya mwanamke katika hadithi hii. (alama 12)
4. (a) Changanua mtindo katika kifungu hiki kutoka hadithi ya Fadhila za
Punda (alama 10)
Aligutuka kutoka kwenye usingizi wa mang‟amumang‟amu, roho mkononi,
pumzi zikimwenda mbio. Hakujua kilichomwamsha,hivyo alitega sikio
ndi!...Labda ghamidha itakuwa im ezidi, imefura kama hamri lililotiwa
hamira… Saa ya ukutani ilimwambia saa nane za usiku, wakati waja wamelala,
misono tu,…alipoiona hiyo missed call akajua basi…Aliamka kuelekea
kitandani kuuhitimisha usiku wake kwa sababu ni wazi mgeni haji tena. Akawa
anapita kioo kwenye verenda . Chenyewe kimepasuka…mbona ikawa
hivi?Mbona Luka kageuka kuwa kuwa mzigo wa moto, habebeki, habebeki
kamwe?

(b) Fafanua dhiki zinazowakumba raia katika hadithi ya Msiba wa Kujitakia


(alama 10)
5. “ Alishangaa kwa nini wakati wote huu hakuna mtu aliyejua shughuli i le
dhalimu iliyokuwa ikiendelea.”
a) Eleza muktadha wa dondoo hili (alama 4)

3
MWALIMU SIFUNA WHATSAPP 0791801250

b) Huku ukitoa mifano mwafaka, eleza jinsi ambavyo haki za watoto


zimekiukwa katika hadithi ya Mapambazuko ya Machweo (alama 8)
c) Jadili athari za suala linalorejerelewa katika dondoo hili kutoka hadithi ya
Kila Mchezea Wembe (alama 8)

“Sikupita kwingine. Nilishika tariki moja kwa moja hadi…Huko nilikuta t ayari
yamechacha…”
6. Tukaangaliana. Hapo nikaanza kuukagua mwili wake Naisoma hasa.
Akanishika mkono kunisaidia kusimama. Nikaitikia. Moyo ukamridhia huyu
mridhia wa muda. Mwendo wa aste aste mpaka alipokuwa ameegesha gari.
Tukapiga selfie. Takawa kama tumejuana kwa muda mrefu. Nyoyo zetu
zikakurubiana. Akanifungulia mlango wa gari . Tukatifua vumbi la beach na
kuondoka. Sijakutana na mwanamume kama huyu, pengine kuona kwenye
sinema! Alikuwa wa asili ya kiarabu. Mweupe, macho yake ya wastani meupe
kama theluji ila malegevu. Uso wenye umbo la embe dodo, kidevu kimenyolewa
vizuri utadhani kimechongwa na kuacha uso kung'aa Nwyele za singa zinanukia
udi hasa. Mwili wote unanukia riha ibura ya uturi Mikono imechongeka vizuri
kwa misuli ya wastani Kifua nacho ni cha ngao! Usiseme magu u manene
yaliyoketi vizuri kwenye kaptura lake la buluu Alikuwa hana tenge huyu
Nikajipata nimenasika hapo usoni, naye akaniangalia akitabasamu. Ndipo
nikaona meno yaliyojipanga vizuri, meupe ya kuacha mwanya wa kutia nakshi
tabasamu lake. Ngozi yake imetepweka kama jejeta.
a) i)Eleza aina za taswira katika utungo huu (alama 5)
ii) Fafanua mbinu zingine tano zinazobainika kwenye utungo huu.(Alama 5)
b) Thibitisha ukweli wa kauli iliyopigiwa mstari kwenye kifungu hiki ukirejelea
hadithi ya Nilitamani (alama 10)

7. Sabina "...Mizizi ya elimu ni michungu ila matunda yake ni matamu. Ikiwa


mnataka kuyaonja matunda ya elimu lazima mtie bidii kwani mtaka cha
mvunguni sharti ainame..."
a) Eleza muktadha wa dondoo hili (alama 4)
b) Tambua mtindo kwenye dondoo hili (alama 4)
c) Eleza nafasi ya mrejelewa. (alama 6)
d) Tambua toni kwenye dondoo (alama 2)
e) Jinsia ya kike imesawiriwa kuwa dhaifu na inazidi kudhulumiwa kila
kuchuo. Thibitisha ukweli wa kauli hii ukirejelea hadithi hii (alama 4)

8. “Yu wapi kirukanjia wako? Wajua yuko wapi? Uliacha mbachao kwa msala
upitao. Atakutunza nani, maana kwako fadhila za punda ni mashuzi!”
a. Yaweke maneno haya katika muktadha wake. (alama 4)
b. Taja mbinu mbili za lugha zilizotumika katika dondoo hili. (alama 2)
c. Bainisha toni ya dondoo. (alama 1)
d. Fafanu asifa zozote tatu za mzungumziwa. (alama 3)
e. Kwa kurejelea hadithi “Fadhila za Punda” onyesha ukweli wa kauli kuwa
fadhila za punda ni mashuzi kwa mifano mwafaka. (alama 10)

4
MWALIMU SIFUNA WHATSAPP 0791801250

9. Huku ukirejelea hadithi zifuatazo tano jadili maudhui ya migogoro kwa


kutoa mifano maridhawa. (alama 20)
i. Fadhila za punda
ii. Msiba wa kujitakia
iii. Mapambazuko ya machweo
iv Harubu ya maisha

contact us for answers 0791801250


ALSO AVAILABE
 BEMBEA DONDOO NA MAJIBU
 MAPAMBAZUKO DONDOO NA MAJIBU
 MAPAMBAZUKO ESSAYS AND ANSWERS
 +MIONGOZO YOTE
ENGLISH
 SAMARITAN ESSAYS AND ANSWERS
 FATHERS OF NATION ESSAYS AND ANSWERS
 SILENT SONG ESSAYS AND ANSWERS
 + ALL GUIDES

You might also like