You are on page 1of 8

1.

“…anachukua vidonge vyake na kuvimeza kabla ya kuketi kwenye kochi


mpya.”
(a) Weka dondoo hili katika muktadha wake. (alama 4)

(b) Tambua aina za taswira katika dondoo hili. (alama 2)


(c) Eleza umuhimu wa mandhari ya dondoo hili. (alama 4)
(d) Eleza nafasi ya mwanamke ukijikita katika utamaduni wa jamii ya “Bembea
ya Maisha”. (alama 10)

2. “Wakati mwingine maisha haya hukufanya kijisikia kama abiria kwenye gari
liendalo kwa kasi. Unatamani dereva apunguze mwendo lakini unakumbuka
kuwa safari bado ni ndefu na hutaki kufika ukiwa umechelewa. Basi unatulia
japo ndani una wasiwasi, hutulii. Lakini huwezi kushuka maana safari
itaganda. Kwa hivyo, unajitahidi tena, japo wakati mwingine unajikuta
umetambaliwa na uchovu, shaka na tuhuma.”
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
(b) Changanua mtindo katika dondoo hili. (alama4)
(c) Dhihirisha umuhimu wa mzungumziwa wa maneno haya katika kuijenga
tamthilia ya “Bembea ya Maisha”. (alama 6)
(d) Eleza namna maisha yanamfanya mzungumzaji “kujisikia kama abiria
kwenye gari liendalo kwa kasi”. (alama 6)

3. a. Changanua mtindo katika kifungu kifuatacho (alama 10)


‘‘Mwanangu usitake sana kuhoji alacho kuku. Utachafukwa roho umchukie
kuku bure. Wala usitake kujua nyuki ameitengenezea nini asali. Hutaila.
Maadamu yameshakuja,yapokee. Mtoto akinyea kiganja hakikatwi wala
hatuulizi kwa nini. Ni maumbile. Maumbile hayo,sawa na vidole, hayafanani.
Sawa na watoto wachezeao bembea, tumeicheza na tungali tunaicheza sehemu
yetu kwa zamu. Haidhuru iwe ya kamba au chuma. Muhimu ni kwamba
tumeshirikiana kusukumana kwenye bembea ya maisha. Upo wakati inakuwa
raha tele na upo wakati inakatika na kutubwaga. Hiyo ndiyo raha hasa ya
maisha. Ni sawa na chombo kinachomenyana na mawimbi katika bahari.
Hutufanya kuwa macho katika safari…”

b. Fafanua namna mandhari ya dondoo hili yalivyochangia usukaji wa


tamthilia. (alama 10)
4. ‘‘Walishasema baada ya dhiki ni faraja, Faraja ni zao la dhiki. Leo hii
kikapu cha mama kimejaa ndago.”
a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
b) Eleza vipengele viwili vya kimtindo kwenye dondoo. (alama 4)
c) Eleza maudhui mawili yanayodokezwa kwenye dondoo. (alama 2)
d) Eleza sifa za msemaji.(alama 5)
e) Kwa kutolea mifano mwafaka eleza dhiki alizopitia mama ambaye sasa
kikapu chake kimejaa ndago. (alama 5
5. (a) ‘Hizo juu-chini chini-juu ndizo utamu wake. Ni kama maisha kwa jumla.
Yana pandashuka ndiyo lakini pandashuka hizo ndizo hutupa kuridhika
hatimaye tunapozishinda.’ Thibitisha kuwa maisha yamejaa pandashuka
ukirejelea tamthilia: Bembea ya Maisha (alama 10)
(b) ‘Umenirudisha nyuma kweli katika siku zile za ujana wangu. Asubuhi niko
skuli majira ya alfajiri…’’
(i) Eleza mbinu ya kimtindo inayojitokeza katika dondoo hili.
(ii) Fafanua mifano mingine minane (8) ya matumizi ya mbinu hii katika
tamthilia (alama 8)

6. “Mwenyewe ona ulivyokonda kama ng’onda!”


(i) Yaweke maneno haya katika muktadha wake.
(ii) Tambua mbinu mbili za lugha katika dondoo hili. (alama 4)
(iii) Eleza umuhimu wa msemaji wa maneno haya. (alama 6)
(iv) Fafanua umuhimu wa mandhari ya dondoo hili.

7. a) Changanua mtindo katika dondoo lifuatalo. (alama 6)


(Anajisemea) “ Bunju ni mmoja wenu. Nyote ni wanangu.” Hayo ni maneno ya
mama. Wakati huo sikuona. Sasa ninaona. Wanasema mwenye macho haambiwi
tazama. Kweli ilioje! Japo hutokea wakati tukalalamika, ninafikiri Bunju ni
zawadi nzuri kwetu. Leo tungekuwa wapi bila Bunju? Maji yangezidi unga.
Hebu fikiri ! umepata ajali mbaya. Inakuacha mahututi. Anapita mtu katika
gari lake. Anakufanyia mpango wa flying doctors, ndege inafika kukupeleka
hospitali.
b) Kwa kurejelea tamthilia ya Bembea ya Maisha jadili changamoto saba
zinazoikumba asasi ya ndoa. (alama 14)
8. “Maji yangekuwa yamewafika shingo basi wangeshindwa kuishi pamoja.
Ndoa ni bembea.”
a) Fafanua muktadha wa dondoo hili.
b) Bainisha tamathali moja ya usemi inayojitokeza. (alama 2)
c) Eleza sifa nne za msemaji wa maneno haya. (alama 4)
d) Mwandishi wa Bembea ya Maisha ameshughulikia suala la uwajibikaji kwa
kina. Thibitisha. (alama 10)
9. “Mwanangu binadamu mchoyo kwa lake lakini mkarimu ajabu kwa la
mwenziwe. Atakukarimu kwa la mwenziwe na atakupa nyongeza usiohitaji
lakini lake atalizika katika giza la kina cha moyo wake. Ndiyo hulka yake
mwana wa Adamu.”
a) Eleza muktadha wa maneno haya.
b) Jadili namna chanya msemaji na wenzake wajinsia ya kike walivyosawiri wakati
ka tamthilia ya Bembea ya Maisha. (alama 6)
c) Fafanua umuhimu wa mazungumzo kati ya msemaji na msemewa katika
tamthilia ya Bembea ya Maisha (alama 10)
10. Jadili maudhui yafuatayo kwa kutolea mifano maridhawa kama
yanavyoshughulikiwa katika tamthilia ya Bembea ya Maisha.
a) Mabadiliko
b) Migogoro
11. ``Walishasema, baada ya dhiki ni faraja, Faraja ni zao la dhiki. Leo hii
kikapu cha mama kimejaa ndgo.”
a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
b) Tambua vipengele vya kimtindo katika dondoo hili. (alama 2)
maudhui mawili yanayodokezwa katika dondoo hili. (alama 4)
d) Eleza sifa za msemaji. (alama 5)
e) Fafanua dhiki alizopitia mama ambaye kikapu chake kimejaa ndago. (alama
5)

12. Ukilazwa tayari unakuwa umeonja seli. Hata wahudumu wenyewe hawana
mlahakamwema. Amri na vitisho kama askari. Unashindwa kama uuguze moyo
ama ugonjwa. Katika wodi hewa iliyojaa harufu ya dawa imezagaa, vitanda
vimesalimu amri mpaka shiti zikagura. Yaani hali nzima haikupi matumaini ya
kutoka ukiwa bora. Matumaini yanadidimia. Tumaini lako unaliweka sala.
a) Fafanua muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
b) Tambua toni mbili katika kifungu hiki. (alama 2)
c) Chambua mbinu za kimtindo katika kifungu hiki. (alama 5)
d) Eleza namna mandhari ya dondoo hili yalivyochangia kujenga hadithi
Bembea Ya Maisha. (Alama 9)
13. "... wakati mwingine mwindaji huwa mwindwa. Hata kijijini wanaishi
watu . Watu hao hawakumbwi na dhiki kiasi hiki. Ya nini kung'ang'ana
kuyatafuta maisha kama kwamba hayapiti? Maisha ni mshumaa uso mkesha!
Ukijiachia sana peupe hata upepo unaweza kuuzima kabla ya kulika hadi
nchani.” a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
 Msemaji ni Sara
 Msemewa ni Asna
 Walikuwa nyumbani kwa Asna/servant’s quarter.
 Sara ana maoni kuwa Asna angehamia kijijini kumsaidia.
b) Bainisha toni katika kauli hili
 Toni ya kushauri- Maisha ni mshumaa uso mkesha
c) Eleza vipengele vinne vya kimtindo alivyotumia msemaji kufanikisha
uwasilishaji wa ujumbe.
 Methali-mwindaji huwa mwindwa
 Swali ya balagha- ya nini kung’ang’ana kuyatafuta maisha kama kwamba
hayapiti?
 Nidaa- Maisha ni mshumaa uso mkesha!
 Jazanda/ sitiari- Maisha ni mshumaa uso mkesha( maisha ni mafupi na hayapo
daima)
 Mdokezo - …wakati mwingine
 Tashihisi / uhuishi - upepo unaweza kuuzima kabla kulika hadi nchani.
 kweli kinzani – mwindaji – mwindwa
 msemo/nahau - Maisha ni mshumaa uso mkesha!
d) Eleza umuhimu wa msemaji katika kuendeleza ploti ya tamthilia hii.
 Sara ametumiwa kuonyesha athari ya migogoro katika ndoa. Maradhi ya moyo
anayogangua ni tokeo la mzozano baina yake na mumewe Yona.
 Kupitia kwake tunaona alivumilia ndoa yake na kufanya juu chini ili wanawe
wapate elimu ili kuboresha mustakabali wao.
 Aidha, anahakikisha kuwa binti zake Neema na Asna wanapata elimu.
 Ni mfano wa wanawake wenye bidii. Hata akiwa hospitalini, akili yake inafikiria
mazao yake aliyoyaacha shambani.
 Kupitia mazungumzo baina yake na Asna, yanamsawiri Asna kama kijana
aliyekengeuka kiasi cha kutotaka kuingia katika ndoa.
 Kupitia kwake tunaelezwa kuhusu usuli wa kutopika. Sara anaeleza kuwa kwa
sababu ya ugonjwa wake hangeweza kupika.
 Sara alisemwa na kutukanwa na wanajamii kwa sababu ya kuwapata watoto wa
kike pekee. Hii ilipelekea Yona kuingilia ulevi.
 Baadhi ya matukio katika maisha ya wahusika fulani yanaangaziwa katika
nyumba yake. k.m Dina anaangaziwa kama mwenye utu kwani anaenda kumpikia
kwa kuwa alikuwa mgonjwa.
 Kupitia mazungumzo baina yake na Yona, tunapata kujua kuwa Neema ndiye
aliyewasomesha wanuna wake hadi chuo kikuu.
 Pia, Sara anatujuza kuwa Neema ndiye aliyewaajiri wafanyakazi nyumbani
kwake.
 Ametumiwa kuonyesha uwajibikaji wa Neema. Neema anagharamia matibabu ya
Sara na pia anampa babake/Yona pesa za kwenda kwa wazee wenzake.
 Kupitia kwake tunafahamu kuwa Bunju ndiye aliyemsaidia Neema baada ya
kupata ajali na kulipia gharama za hospitali ilhali Bunju hakuwa amemjua Neema.
 Kupitia mazungumzo baina yake na Neema na Asna tunapata kujua kuhusu tofauti
baina ya hospitali za mjini na kijijini. Huduma za hospitali mjini ni mzuri lakini za
kijijini zinalinganishwa na seli na wahudumu hawana mlahaka mwema.
 Hatima ya mgogoro baina ya Sara na Yona. Yona anaachana na mila na tamaduni
za kutopika kwa Mwanaume.
 Anaonyesha jinsi utamaduni ulivyowakandamiza wasichana –Sara anamwambia
Asna kuwa siku zao elimu ya wasichana ilifanyiwa bezo na kuwa Sara aliachia
darasa la saba.
 Kuonyesha mustakabali wa Sara wa kumsamehe,Yona-Yona anamwomba Sara
msamaha kwa kuwa hakujua upeo wa ugonjwa wa moyo.
14. (a) Fafanua umuhimu wa mazungumzo kati ya Luka, Beni na Yona katika
kujenga tamthilia ya “Bembea ya Maisha”
 Yanaonyesha sifa ya Luka kuwa ni mkarimu -anawakaribisha wenzake kwake
nyumbani kwa chakula cha mchana na kinywaji.
 Kuonyesha mila na utamaduni - Luka anadokeza kuwa kitendo cha kula pamoja
kwa wazee kilikuwa kinafanywa na wazee wao kwani mavuno ya kwanza huonjwa na
wazee na kutoa baraka. (uk. 58)
 Yanachimuza ukengeushi - Beni anasema kuwa tatizo la watu siku hizi ni kuzitupa
mila zao kabisa. (uk.58) Wajukuu wa Yona hawafahamu lugha yao ya asili. (uk-59)
 Yanadhihirisha mchango wa dini - Yona anaeleza dini,imechangia watu kuona
mila kuwa chafu. (uk.58)
 Yanaonyesha mabadiliko katika malezi - Yona anaambia wazee wenzake kwa
malezi kule mjini yameachiwa kina yaya. (uk.59)
 Yanaonyesha jinsi mila na tamaduni zilikuwa kandamizi kwani hazikuruhusu
mtoto wa kike kuenda shule au kuridhi kitu – kulingana na Luka.(u.k 60)
 Yanadhihirisha jinsi hao kina Luka walivyomshinikiza Yona kuoa mke mwingine
apate mtoto wa kiume.(u.k 60)
\  Yonadhihirisha sifa za Beni jinsi ana wivu kwa watoto wa Yona kwani hataki
Luka awataje katika mazungumzo yake.
 Yanachimuza ufanisi wa watoto wa Yona – Luka anasema walikuwa nyota ya jaha.
Neema anarudi kijijini akiwa na gari.
 Yonaonyesha thamani ya mtoto wa kike ilivyopanda na nafasi yake kupanuka
kwani zamani walikuwa wakiwategemea waume zao laikini sasa hali ni
tofauti(u.k.60)
 Yonaonyesha maudhui ya uhafidhina – Luka anamuona Neema kama si wao tena
baada ya kuolewa.
 Yanachimuza hekima ya Luka – Luka anamuuliza Beni kuwa lipi muhimu kati ya
tiba au mtu kuja kumpikia mwenzake? (uk.61)
 Yanaonyesha sifa za Yona hapo awali kuwa alikuwa mualimu mwenye bidii - Yona
anasema angefika kazini majira ya alfajiri, kiboko mkononi, siku nzima kazi tu,
aliweza kufunga vitabu kwenye baskeli kwenda kuvisahihisha wikendi. (uk. 62)
 Yanadhihirisha mabadiliko katika nyanja ya elimu - Yona anasema siku hizi
huwezi tena kumnyoosha mtoto kwa kiboko. (uk.62)
 Yanachimuza athari za pombe - jinsi pombe ilivyomfanyaYona kuwa mtumwa
akashindwa kuishi bila kulewa (uk62)
 Yanaonyesha uvumilivu au stahamala za Sara wakati Yona alipokuwa mlevi. Yona
anasema Sara alimsaidia kulea na kusomesha watoto na kwamba bila yeye chombo
kingezama. (uk-62)
 Yanaonyesha jinsi Yona alivyoanza kutumia tembo alipokuwa chuoni. Wenzake
walimpa mvinyo kumrai kuonja. (uk. 62)
 Yanadhihirisha uongo wa Beni- kuwa mtoto wake ni fundi wa mitambo na wala si
injinia. (uk. 63)
 Yanaendeleza ploti- tunatambulishwa kuwa Luka,Beni na Yona ni marafiki na
walishiriki vileo pamoja.
(b) "Bembea inapolika na kukatika haiwi mwisho wa michezo.Huungwa na
mchezo kuanza tena." Thibitisha ukweli wa kauli hii kwa kutolea mifano
mwafaka tamthiliani.
 Neema nusura apoteze uhai wake katika ajali Lakini Bunju akamnusuru kwa
kumpeleka hospitalini.
 Neema na Bunju baada ya kugombana kuhusu mchango wake Bunju katika
matibabu ya Sara, Neema anaamua kumuelewa Bunju hivyo ndoa yao kuendelea
vyema.
 Baada ya changamoto ya kutopata watoto iliyoyumbisha ndoa baina ya Sara na
Yona, hatimaye walijaliwa watoto watatu.
 Maradhi ya moyo yalipomlemea Sara kiasi cha kukata tamaa na maisha, Neema
anajitolea kuhakikisha mamaye amepata matibabu murua hivyo kumrejeshea
matumaini.
 Japo Yona na Sara walikosa mwana wa kiume na kusimangwa na wanajamii,
mabinti zao wanakuwa wembe masomoni hivyo kuwapa furaha katika ndoa yao.
 Neema alipoonekana kukata tamaa kutokana na kile alichokiona kuwa ni ubahili
wa Bunju, Sara alimpa wasia uliompa nguvu zaidi katika ndoa yake.  Yona baada
ya kugundua kuwa ulevi wake unaangamiza familia yake, anaapa kutolewa tena na
kumhudumia mkewe Sara.
 Yona na Beni walipotofautiana kuhusu watoto wao,Luka anafaulu kutuliza hali na
wazee hawa kuendelea na sherehe zao.
 Baada ya kumsababishia mkewe maradhi ya moyo,Yona anamwomba Sara
msamaha kwa kuwa hakujua upeo wa ugonjwa wa moyo.
 Mgogoro baina ya Sara na Neema kuhusu Yona unaisha Neema anapogundua
upendo wa Yona Kwao anapoacha utamaduni wa kutopika chakula.
 Mgogoro baina ya Sara na Yona unaisha. Yona anapoachana na mila na tamaduni
za kutopika kwa mwanaume.
 Tatizo la Sara la kushindwa kumpikia mkewe linasuluhishwa na jiraniye Dina
anapokuja kumsaidia.
15. Asubuhi niko skuli majira ya alfajiri, kiboko mkononi. Anayekuja baada
yangu hata kama hajachelewa ana lake.
a) Eleza muktadha wa dondoo hili (alama 4)
 Haya ni maneno ya Yona
 Akimjibu Beni
 Wamo kwa Luka nyumbani
 Beni alikuwa amemkubusha zama zile akiwa mwalimu alikuwa na nguvu za
kujipikia
b) Tambua mbinu mbili za mtindo katika dondoo hili (alama 4)
 Kisengere nyuma-anaeleza alivyokuwa akifika asubuhi na mapema na kuwaadhibu
walio chelewa alipokuwa mwalimu
 Utohozi- skuli
 Taswira- kiboko mkononi
 Kinaya-kuadhibu mtoto ambaye hajachelewa
c) Bainisha toni inayojitokeza katika dondoo hili (alama 2)
 Toni ya majigambo/kiburi/majivuno/majitapo
d) Fafanua sifa mbili za msemaji kutoka kwenye dondoo (alama 2)
 Mwenye bidii- anarauka asubuhi na mapema kwenda kazini
 Katili- aliwaadhibu hata wasiochelewa waliofika baada yake kufika.
 Mwenye majitapo/kiburi- 2x1=2
e) Onyesha jinsi elimu ilivyosawiriwa katika Tamthilia Bembea ya Maisha
(alama 8)
 Elimu ina gharama; Sara anaambia Yona kulipia elimu ya Chuo kikuu si
lelemama. Jambo hili limewashinda hata wanaume wenye mishahara minono
serikalini (uk. 1), Shule ya bweni anakosomeaMina inagharimu pesa nyingi(uk.27).
 Elimu inamsaidia mwanamke kuolewa; Yona anamwambia Sara kwamba Neema
hangepata ndoa ikiwa hangejinyima mengi ili kumwelimisha(uk.2).  Elimu
hupalilia vipawa; Bela anaambia Dina kuwa Lemi huimba na kucheza shuleni;Lemi
amwonyesha Bela minenguo na miondoko waliyoifanya shuleni (uk.22).
 Wazazi huthamini alama na nambari wanayoshikilia watoto katika mitihani;
Neema anaona ni heri Lemi ameongeza alama ilhali Bunju anasema afadhali
angepunguza alama lakini apande nafasi darasani (uk.26).
 Shule huwa na wanafunzi wa viwango tofauti kimasomo; Neema alikuwa mwerevu
darasani nao watoto wa Dina wakawa hawaitikiwi na elimu japo walijawa hekima
na nidhamu.
 Elimu hufinyanga maadili;Lemi huendesha mambo yake kwa udhu na adabu.
Hutuzwa mara nyingi kwa kuwa kubeli(uk.26).
 Vijana wameelimika lakini hawana ajira; Asna hana kazi licha ya kuwa na
shahada.
 Bidii ya Salome masomoni inamsaidia kupata ufadhili wa kuendeleza masomo
ng’ambo(uk.28).
 Elimu inawakengeusha vijana; Asna anahiari kuishi mjini bila kazi kuliko kurudi
kijijini;anaona akirudi kijijini watu watamshangaa(uk.31).
 Elimu ya wasichana ilipuuzwa zamani, ilidharauliwa; Sara aliachia masomo
darasa la saba akaolewa
 Ni wajibu wa wazazi kusaidia wanao kusoma; Neema anamsaidia Lemi
kusoma(uk.47), Bunju humsaidia Lemi kufanya homework (uk 49).
 Elimu humsaidia binadamu kuishi na kutatua matatizo yake; Sara anamwambia
Asna kutumia elimu waliyompa kutegua mitego ya ndoa na kuendesha maisha
yake(uk.53).
 Ulevi huathiri utendakazi wa walimu;Yona anakosa kuwajibika hadi anafutwa
kazi (uk. 56).
 Elimu ni chombo cha maendeleo na ufanisi; Neema anarudi kijijini akiendesha
gari safi (uk.61).
 Walimu walitumia kiboko kurekebisha wanafunzi wakati Yona alipokuwa
mwalimu. Leo sivyo.
 Vijana hushinikizwa na marika kuingilia ulevi;Yona alishinikizwa na vijana
wenzake chuoni kuingilia ulevi.  Watoto wanafaa kupelekwa shule bora(boarding)
inayotia matumaini zozote 8x1=8
16. Kumbuka mrina haogopi nyuki. {kimya} Marehemu mama yangu alizoea
kutuambia kuwa nguvu hazimwishi mwanadamu wala hazipotei bure;
humalizwa tu na mabuu. Mwanangu, usifanye hofu. Nikujuavyo mimi,
hukuingia katika bahari si yako. Wala hakuna refu lisilokuwa na ncha. Yote
yana mwisho eti! Ipo siku yote yatapita. {kimya} Mkulima hodari libasi yake
huwa imechakaa na kuchoka lakini moyoni anabaki safi kama theluji kwa
kutosheka na tija ya sulubu zake. Huwezi kumlinganisha na mkulima wa nguo
safi zilizopigwa pasi zikanyooka.
a) Changanua mtindo katika kifungu hiki (alama 6)
 Methali-mrina haogopi nyuki,/ hakuna refu lisilokuwa na ncha.
 Kisengere nyuma- marehemu mamangu alizoe kutuambia…
 Jazanda- bahari
 Tashhisi- libasi yake huwa imechoka na kuchakaa
 Tashbihi- safi kama theluji
 Kinaya- mkulima wa nguo safi
 Taswira- nguo kuchakaa/ nguo safi
 Nidaa- yote yana kikomo eti! Zozote6x1
b) “Mila na desturi zetu zimewajenga hivyo walivyo na sisi hivi tulivyo”. Imani
na itikadi huthaminiwa sana na jamii zetu. Jadili ukweli wa kauli hii kwa
kurejelea tamthilia ya bembea ya Maisha (alama 10)
 Yona anaambia Sara kuwa fimbo ya mzee(majukumu) hurithi mtoto wa kwanza(uk,
2).
 Dina anaambia Kiwa watu waliuliza na wanauliza nani atarithi ardhi ya Yona
 Yona anataka kujua sababu ya Sara kutomwandalia chochote(uk. 13)'  Sara
anaambia Dina mila imewafanya wanaume kuwaachia wanawake kazi zote za
nyumbani.
 Sara anaambia Dina watu wakijua mume anamsaidia mke jikoni watasema hadhi
yake imeshushwa, kwa mizani ya jamii mwanamke atakuwa amejivua nguo (uk. 14).
 Neema anamwambia Bela kuwa wazee wake hawawezi kulala kwa mkwe wao (uk.
24).
 Wazazi waBunju walipokuwahaihawakuwahi kuja kuishi kwake(uk.29).
 Bunju anaambia Neema kuwa hawezi akakaa na wazazi wa Neema kwake, ni
laana.
 Sara anaambia Asna kuwa ikiwa Yona ataonekana akiteka maji kisimani kijiji
kitasema kwamba amewasomesha watoto ambao wamemweka Sara jijini ili Yona
ataabike; watamdharau(uk 45).
 Luka anaambia Yona na Beni kuwa zamani ilikuwa ni desturi mavuno ya kwanza
kuonjwa na wazee ili kutoa baraka(uk.58).
 Sara anaambia Neema binti za mama anayemzuia mumewe kufanya atakayo
(anayemtilia mguu wa kausha) hawaolewi, huzeekea nyumbani (uk. 66).
 Sara anamwambia Neema utamaduni haumruhusu mwanamke kushindana na
mwanamume
 Kulingana na Sara, hekima si hekima itokapo kwa mwanamke(uk. 68).
 Wanawake ni wategemezi kwa waume zao.
c) Onyesha jinsi msemewa hakuingia katika bahari si yake (alama 4)
 Msemewa- Neema: (mwanafunzi aangazie mafanikio ya Neema)
 Licha ya kuwa msichana anafaulu kuchukua fimbo ya Yona kwa kuwasaidia yeye
na mamake Sara.
 Anaweza kusoma na hata kuwashinda wanaume.
 Anafanikiwa kupata kazi na kutomtegemea mumewe kwa kila jambo.
IV. Alifaulu kuendesha gari mjini jambo lililowashinda wanaume.
 Anafaulu kumsomesha Asna hadi chuo kikuu jambo lililowashinda wenye
mishahara minono.
 Anafaulu kugeuza fikra za mumewe za kutosaidia wakwe zake
 Anafulu kujengea wazazi nyumba

You might also like