You are on page 1of 62

MITIHANI YA KUDURUSU KIDATO CHA TATU

Kenya Certificate of Secondary Education (K.C.S.E.)

KISWAHILI KIDATO CHA 3 2019/20


MTIHANI 1-11

MTIHANI 1
KARARASI 1
1. Lazima
Andika barua kwa mhariri wa gazeti ukilalamikia hali ya watu nchini kwetu kuhamia mataifa
ya nje kwa wingi.
2. Andika kuhusu umuhimu wa vijana katika kuimarisha mshikamano wa kitaifa.
3. Tunga kisa kitakachodhihirisha maana ya methali ifuatayo.
Usitukane wakunga na uzazi ungalipo
4. Tunga kisa kitakachokamilika kwa kauli ifuatayo:
“…niliipapia ile bilauri ya maji kwa pupa. Sikuwa na uhakika kuwa kiu yangu ingekatika.
Nikapiga mafunda mawili, matatu. Baada ya kugumia bilauri yote, ndipo nilipotambua kuwa
kweli maji ni uhai.”

KARATASI 2

MATUMIZI YA LUGHA (ALAMA 40)


a) i) Taja sauti mbili ambazo ni vikwamizo vya ufizi(Alama 1)
ii) Taja sifa mbili bainifu za vokali /u/ (Alama 2)
b) Yakinisha sentensi hii. (Alama 2)
Simba asiponguruma wanyama wote hawababaiki.
c) Andika upya sentensi ifuatayo kwa kufuata maagizo uliyopewa. (Alama 2)
Mbwa ambaye aliripotiwa kuwa ameibwa amepatikana katika bwawa la maji.
(Anza: Katika bwawa………………………..)
d) Changanua sentensi ifuatayo kwa kutumia njia ya matawi (Alama 4)
Mwanafunzi stadi amenunua kitabu kizuri.
e) Ukizingatia neno lililo katika mabano, andika sentensi hii katika hali ya kutotendeka.
i) Daraja hili(vuka) wakati wa mvua (Alama 2)
f) Andika katika ukubwa wingi (Alama 2)
Mtoto mjeuri akiletwa atarejeshwa kwao.
g) Andika katika usemi wa taarifa. (Alama 2)
“Tutawatembelea wazazi wetu leo jioni” Leo alimwambia Asha.
h) Tunga sentensi ukitumia nomino zifuatazo pamoja na kivumishi ___ingine.(Alama 2)
i) dau
ii) urembo
i) Bainisha yambwa katika sentensi hii. (Alama 2)

GOLDEN ELITE EDUCATIONAL CONSULTANCY P.O BOX 2345 KERICHO. FOR MARKING SCHEMES CALL OR
TEXT MR CHEPKWONY ON 072435I706 0R EMAIL kipkemoicos@gmail.com
Mbunge wa Mtondo Kaskazini atawajengea wanakijiji josho kisha aghurie Nairobi.
j) Tunga sentensi ukitumia viwakilishi vifuatavyo. (Alama 2)
i) Nafsi viambata
ii) Visisitizi
k) Fafanua maana ya sauti mwambatano. (Alama 2)
Andika mfano wa sauti mwambatano. (alama 1)
l) Tunga sentensi ya neno moja yenye visehemu vifuatavyo vya sarufi. (Alama 3)
i) Kiambishi kiwakilishi cha kiima
ii) Kiambishi kiwakilishi cha wakati uliopo
i) Kiambishi kiwakilishi cha kitendewa/mtendewa
ii) Shina la kitenzi
iii) Kiambishi cha kauli ya kutendesha
iv) Kauli ya kutenda
m) Fafanua miundo miwili ya ngeli ya LI-YA
(Alama 2)
n) Akifisha (Alama 3)
sikukuu ya madaaraka nilikwenda eldama ravine kumwona yohana akasema atakuja
kuniona
o) Eleza tofauti za kimaana baina ya sentenzi hizi. (Alama 4)
i) Jambazi kutoka dukani aliiba
ii) Kutoka dukani jambazi aliiba.
iii) Aliibia jambazi kutoka dukani.
i) Jambazi aliiba kutoka dukani.
p) Unda nomino mbilimbili kutokana na mizizi ifuatayo. (Alama 2)
i) -f-
ii) -l-

4. ISIMU JAMII (ALAMA 10)


a) Mbali na mtazamo unaoshikilia kuwa Kiswahili ni kibantu, taja mingine miwili.
(Alama 2)
b) Huku ukitoa mifano, thibitisha kuwa kiswahili ni kibantu. (Alama 8)

Karatasi ya 3
SEHEMU A. SWALI LA LAZIMA RIWAYA: CHOZI LA HERI
1. "Lakini itakuwaje historical injustice,nawe Ridhaa,hapo ulipo sicho kitovu chako?"
a. Eleza muktadha wa dondoo. (alama 4)
b. Eleza tamathali mbili za lugha zilizotumika kwenye dondoo hili. (alama4)
c. Fafanua umuhimu wa msemaji wa maneno haya. (alama6)
d. Ni mambo gani yaliyo wakumba wale ambao sio wa kitovu kinachorejelewa.(alama6)

SEHEMU B HADITHI FUPI:TUMBO LISILOSHIBA NA HADITHI NYINGINE


2. “Usiteketeze umati kama kuni zinavyoteketeza moto. Rudi,rudi kwa Mola wako.”
a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama4)
b) Fafanua sifa za msemewa. (alama6)
c) Tambua tamathali ya usemi iliyotumika hapo juu. (alama2)

GOLDEN ELITE EDUCATIONAL CONSULTANCY P.O BOX 2345 KERICHO. FOR MARKING SCHEMES CALL OR
TEXT MR CHEPKWONY ON 072435I706 0R EMAIL kipkemoicos@gmail.com
d) Ni kwa nini msemewa anatakikana kurudi kwa Mola wake?
(alama8)

AU
3. Huku ukirejelea hadithi ya Tumbo Lisiloshiba na Shibe Inatumaliza, fafanua maudhui ya
ukiukaji wa haki. (alama20
SEHEMU C. TAMTHILIA: KIGOGO
4. “Oooh bebi, miaka yaenda mbio sana, nayo sura yako inachujuka……”
a) Weka dondoo hili katika muktadha wake. (alama4)
b) Mhusika anayehusishwa na wimbo huu ana msimano gani wa kimapinduzi? (alama
8)
c) Taja sifa zozote nane za muhusika huyu. (alama8)

AU
5. Tamthilia ya ‘Kigogo’ ni kioo cha uhalisia wa maisha ya jamii nyingi za
kiafrika.Thibitisha
.(alama 20)

SEHEMU D: USHAIRI.
6. Lisome shairi lifuatalo kisha uyajibu maswali yaliyoulizwa.
WENYE VYAO WATUBANA
1. Wenye vyao watubana, twaumia maskini,
La kufanyiza hatuna, hali zetu taabani.
Kwa sasa kilo va dona, bei mia ishirini,
Wakubwa tuteteeni, wenye vyao watubana.

2. Washindana matajiri -kwa bei siyo utani,


Na pigo kwa mafakiri tunao hali ya chini,
Wazeni kutafakari, wanyonge tu madhilani,
Wakubwa tuteteeni,wenye vyao watubana

3. Limekuwa kubwa zogo, hakuendeki madukani.


Fungu moja la muhogo, sasa shilingi miteni,
Huo mkubwa mzigo , watulemaza kichwani,
Wakubwa tuteteeni ,wenye vyao watubana.

4. Si hichi wala si kile, hakuna cha afueni,


Bei imekuwa ndwele, wenye macho lioneni
Ukiutaka mchele, pesa jaza mfukoni,
Wakubwa tuteteeni ,wenye vyao watubana.

5. Waliko hao samaki, huko ndiko uchawini.


Wachuuzi hawacheki , zimewatoka huzuni,
Vibuwa havishikiki, kimoja kwa hamsini,
Wakubwa tuteteeni , wenye vyao watubana.

GOLDEN ELITE EDUCATIONAL CONSULTANCY P.O BOX 2345 KERICHO. FOR MARKING SCHEMES CALL OR
TEXT MR CHEPKWONY ON 072435I706 0R EMAIL kipkemoicos@gmail.com
6. Maisha yetu viumbe ,yamekuwa hilakini,
Vvenye vyao kila pembe ,wametukaa shingoni,
Nyama ya mbuzi na ng’ombe, sasa hali maskini,
Wakubwa tuteteeni wenve vyao watubana.

7. Maji vamezidi unga, kwa lodi wadarajani,


Kajitolea muhanga, kwa bei hawezekani,
Mvao wake wa kanga, ni shilingi elifeni
Wakubwa tuteteeni,wenye vvao watubana.

Maswali;
a) Fafanua toni ya shairi hili. (alama2)
b) Nini dhamira ya nafsi neni ? (alama2)
c) Andika ubeti wa sita kwa lugha tutumbi. (alama4)
d) Fafanua kwa kutoa mfano mbinu moja aliyotumia mshairi kutosheleza mahitaji ya arudhi
katika shairi hili. (alama2)
e) Taja na ueleze bahari mbili za shairi hili ukizingatia.
(alama4)
i) Vipande
ii) Vina
f) Taja kwa kutoa mifano katika shairi hili hadhira tatu lengwa. (alama6)

SEHEMU E : FASIIH S1MULIZ1


7. (a) (i) Ngano ni nini? (alama1)
(ii) Eleza tofauti iliyoko kati ya visasili na visakale. (alama2)
(iii) Fafanua umuhimu wa ulumbi katika jamii. (alama5)
(b) (i) Eleza umuhimu wa vitendawili katika jamii. (alama5)
(ii) Tega na utegue vitendawili vyovyote viwili vilivyo na lugha ya takriri na lugha ya
mlio. (alama4)
(iii) Taja sifa zozote tatu za methali. (alama3)

MTIHANI 2
KARATASI 1

1. Wewe ni Gavana wa gatuzi mojawapo katika nchi ya Kongomano. Wakaazi wa mji wa


Songambele wamekiuka sheria zilizowekwa na baraza la gatuzi hilo. Waandikie ilani
2. Jitihada za kumwinua mtoto wa kike zimepeleka kudhalilisha kwa mtoto wa kiume. Jadili.
3. Andika kisa kitachodhihirisha maana ya methali.
Ulimi huuma kuliko meno
4. Tunga kisa kitakapomalizika kwa kauli ifuatayo.
……………………. Nilijitazama na kujidharau. Kwani nini nilijiingiza katika hali hii?
Nilijuta.
KARATASI 2
A. MATUMIZI YA LUGHA
(a) Taja sauti mbili ambazo huitwa likwidi (alama 1)

GOLDEN ELITE EDUCATIONAL CONSULTANCY P.O BOX 2345 KERICHO. FOR MARKING SCHEMES CALL OR
TEXT MR CHEPKWONY ON 072435I706 0R EMAIL kipkemoicos@gmail.com
(b) Andika neon lililo na muundo wa silabi ufuatao (alama 1)
IKKI
(c) Ainisha viambishi katika neno lifuatalo (al. 2)
Yafutikayo
(d) Tambua aina mbili za sentensi ukizingatia uamilifu na utoe mfano mmoja kwa kila moja(ala.
2)
(e) Ainisha vielezi vya namna katika sentensi hii (ala. 2)
Mzee huyu mkongwe alicheka kijinga huku akila haraka haraka
(f) Ainisha vishazi katika sentensi ifuatayo (ala. 2
Kijana aliyezungumza na nyanyake ameingia katika darasa lililochafuliwa na wanafunzi
(g) Changanua sentensi ifuatayo kwa kielelezo cha mstari (ala. 3)
Mwanafunzi mwerevu sana aliyekuwa mgonjwa jana amepelekwanyumbani
(h) Bainisha shamirisho na chagizo katika sentensi ifuatayo (ala. 3)
Somo aliukata mti kwa kisu jana asubuhi
(i) Andika kwa usemi wa taarifa (ala. 3)
Karani: Njoo nikutume kwa babu yangu.
Karanja: Sitaki kupita njia ya kwa babu
(j) Eleza matumizi ya ‘ni’ katika sentensi hii (ala. 2)
Ingieni darasani mara moja ili niwape zoezi ambalo ni rahisi
(k) Eleza maana ya sentensi ifuatayo (ala. 2)
(i) Ningalisoma kwa bidii ningalipita mtihani
(ii) Ningesoma kwa bidii ningepita mtihani
(l) Andika katika udogo wingi (ala. 2)
Mti wa msonobari unatengeneza meza nzuri sana
(m) Tambua miundo yoyote mitatu ya ngeli ya LI-YA (ala. 3)
(n) Eleza maana tatu za sentensi ifuatayo (ala. 3)
Alisema angeenda kwao
(o) Andika upya sentensi ifuatayo katika hali sambavu (ala. 1)
Mwanafunzi anasoma darasani
(p) Tumia neno ‘hadi’ kuonyesha mahali na wakati katika sentensi (ala. 2)
(q) Yakinisha katika hali ya mazoea. (ala. 2)
Asiyeugua hahitaji daktari
(r) Tunga sentensi ukitumia neno ‘komaa’ kama (ala. 2)
(i) Kivumishi
(ii) Nomino
(s) Taja matumizi yoyote mawili ya kistari kirefu (ala. 2)

B. ISIMU JAMII
(a) Kwa nini kulikuwa na haja ya kusanifisha Kiswahili? Toa sababu tano (ala. 5)
(b) Fafanua sifa za lugha ya kazi (ala. 5)

KARATASI 3
“Tumbo Lisiloshiba na hadithi nyingine”
Swali la lazima
1. “Akanyangapo chini ardhi inatetemeka…………………..
Amejitia hamnazo. Kabwela kama mimi nina faida gani?
GOLDEN ELITE EDUCATIONAL CONSULTANCY P.O BOX 2345 KERICHO. FOR MARKING SCHEMES CALL OR
TEXT MR CHEPKWONY ON 072435I706 0R EMAIL kipkemoicos@gmail.com
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili (ala. 4)
(b) Fafanua mbinu tatu za lugha zilizotumiwa katika dondoo hili (ala. 6)
(c) Eleza madhila kumi yaliyompata Kabwela (ala. 10)

SEHEMU B:
Chozi la heri
Chagua swali la 2 au 3
2. “………….. wanahofia kusema wasije wakavikata viganja vinavyowalisha…………..
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili (ala. 4)
(b) Taja maudhui yanayojitokeza katika dondoo hili na ueleze (ala. 2)
(c) Kwa kutoa hoja kumi, eleza namna maudhui uliyotaja hapo juu (2b) yanavyojitokeza katika
riwaya (ala. 10)
(d) Eleza sifa nne za msemaji (ala. 4)
3. (a) Migogoro ni maudhui muhimu katika riwaya hii. Fafanua (ala. 10)
(b) Uozo umetamalaki katika jamii ya Chozi la Heri. Tetea kauli hii kwa kutolea hija kumi
zilizoelezwa (ala. 10)

SEHEMU C: TAMTHILIA
Kogogo
Jibu swali la 4 au 5
4. “Na mwamba ngoma huvuta wapi?”
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili (ala. 4)
(b) Tambua tamathali mbili za sauti zilizotumika katika muktadha huo (ala. 2)
(c) Fafanua sifa za msemewa wa maneno (ala. 6)
(d) Thibitisha ukweli kuwa kila mwamba ngoma huvuta kwake ukirejelea Tamthilia nzima ya
Kigogo (ala. 8)

5. “Utawala wa Majoka katika jimbo la Sagamoyo umejaa sumu ya nyokas”


Jadili usemi huo kwa kurejelea tamthilia ya Kigogo (ala. 20)

SEHEMU D: USHAIRI
Jibu swali la 6 au la 7
6. Shairi
La adhabu hili wingu, lataka kutunyeea
Himahima kwalo vungu, pasi nako kuchelea,
Kujikinga hili wingu, sije katunyeshea.

Wengineo hawajali, wasinayo wasiwasi,


Tahadhari hawabali, wajiunge nasi
Aidha watafakali, mengine yalo hasi.

Vua hili halibagui, jinsia wala umri,


Na kama hawajui, tuwajuze vizuri,
Kwani siso adui, kuwao msumari.

GOLDEN ELITE EDUCATIONAL CONSULTANCY P.O BOX 2345 KERICHO. FOR MARKING SCHEMES CALL OR
TEXT MR CHEPKWONY ON 072435I706 0R EMAIL kipkemoicos@gmail.com
Tangazo haliwapiku, wahimizwa kujikinge,
Wingu hili la usiku, ukicheza likuringe,
Latutia usumaku, daima likunyonge.

Vumilia kwalo vungu, nje kuna dhoruba,


Yavuma kwa machungu, bila lolote huba,
Tunza chako kijungu, fungia kwalo juba.

Japo nafika tamati, nawaacha tafakari,


Madhara linalo wananti, wingu hili sukari,
Daima mwape kujiseti, mjitunze kujijari

Maswali
1. Eleza ujumbe wa mwandishi katika ubeti wa nne (ala. 2)
2. Onyesha ufundi wa kimuundo wa mwandishi katika utunzi wa shairi hili (ala. 4)
3. Eleza namna jazanda imetumika katika utungo huu. (ala. 2)
4. Kwa kuzingatia idadi ya mishororo katika beti tambua aina ya ushairi huu (ala. 1)
5. Tamthini ustadi wa mshairi katika matumizi yaidhini ya kishairi (ala. 3)
6. Litie shairi hili katika bahari tatu tofauti (ala. 3)
7. Andika ubeti wanne kwa lugha ya tutumbi (ala. 4)
8. Eleza sifa moja ya nafsi neni katika shairi hili (ala. 1)

7. Ushairi
Soma shairi lifuatalo kasha ujibu maswali yanayofuata
1. Maendeleo ya umma
Sio vitu maghalani
Kama tele vimesaki
Lakini havishikiki
Ama havikamatiki
Ni kama jinga la moto
Bei juu

2. Maendeleo ya umma
Sio vitu gulioni
Kuviona madukani
Kuvishika mikononi
Na huku wavitamani
Kama tama ya fisi
Kuvipata ng’o

3. Maendeleo ya umma
Sio vitu shubakani
Dhiki ni kwa mafakiri
Nafuu kwa matajiri
Ni wao tu washitiri

GOLDEN ELITE EDUCATIONAL CONSULTANCY P.O BOX 2345 KERICHO. FOR MARKING SCHEMES CALL OR
TEXT MR CHEPKWONY ON 072435I706 0R EMAIL kipkemoicos@gmail.com
Huo ni ustiimari
lo! Warudia

4. Maendeleo ya umma
Ni vitu kumilikiwa
Na wanyonge kupatiwa
Kwa bei kuzingatiwa
Bila ya kudhulumiwa
Na hata kuhadaiwa
Hiyo ni haki

5. Maendeleo ya umma
Dola kudhibiti vitu
Vijapo nchini mwetu
Na kuwauzia watu
Toka nguo na sapatu
Pasibakishiwe na kitu
Huo usawa

6. Maendeleo ya umma
Watu kuwa na kauli
Katika zao shughuli
Vikaoni kujadili
Na mwisho kuyakubali
Maamuzi halali
Udikteta la

7. Maendeleo ya umma
Watu kuwa waungwana
Vijakazi na watwana
Nchini kuwa hakuna
Wote kuheshimiana
Wazee hata vijana

Maswali
(a) Toa anwani mwafaka ya shairi hili (ala. 1)
(b) Shairi hili ni la aina gani? Toa sababu zako (ala. 2)
(c) Eleza dhamira ya mwandishi kuandika shairi hili (ala. 3)
(d) Toa mifano miwili ya urudiaji katika shairi hili, Je urudiaji huu una kazi/majukumu gani?
(ala. 4)
(e) Onyesha matumizi mawili ya tamathali za usemi katika shairi hili (ala. 4)
(f) Eleza toni ya mshairi. Toa sababu (ala. 2)
(g) Nafsi neni ni nani? (ala. 1)
(h) Toa mfano mmoja wa twasira katika hili. Je, twasira hiyo inajengwa na nani (ala. 3)
SEHEMU E: FASIHI SIMULIZI
8. (a) Fafanua sifa za matambiko katika jamii (ala. 4)
GOLDEN ELITE EDUCATIONAL CONSULTANCY P.O BOX 2345 KERICHO. FOR MARKING SCHEMES CALL OR
TEXT MR CHEPKWONY ON 072435I706 0R EMAIL kipkemoicos@gmail.com
(b) Eleza tofauti kati ya maigizo ya kawaida na maonyesho ya sanaa (ala.
10)
(c) Taja shughuli zozote mbili zinazoonyesha matumizi ya Ulumbi katika jamii ya kisasa(ala. 2)
(d) Tofautisha dhana zifuatazo
(i) Miviga na maapizo (ala. 2)
(ii) Ngoma na ngomezi (ala. 2)

MTIHANI 3
KARATASI 1
1. Andika barua kwa mhariri wa gazeti la mwangaza ukimweleza kuhusu namna ya
kuimarisha umoja wa kitaifa.
2. Kuna njia tofauti zifaazo kutumiwa kuongeza nafasi za ajira nchini. Fafanua.
3. Andika kisa kinachofafanua matumizi ya methali: Jino la pembeni halisitiri pengo.
4. Andika kisa kinachomalika kwa: “Nilipoangalia jivu la nyumba yangu niligundua kuwa
juhudi zangu za miaka mingi zilikuwa zimeungua zote.”
KARATASI 2
1. MATUMIZI YA LUGHA ( AL 40)
a) Tambua vipashio viwili vya lugha. ( al 2)
b) Toa mfano mmoja wa ala tuli ya kutamka. ( al 1)
c) Eleza tofauti kati ya vitate vifuatavyo:
i. Shombo
ii. Chombo ( al 2)
d) Toa mfano wa mofimu tegemezi. ( al 1)
e) Tunga sentensi- moja huku ukitumia nomino dhahania na nomino ya jamii. (al 2)
f) Tunga sentensi kwa kutumia ( al 2)
i. Kielezi cha namna mfanano
ii. Kitenzi kishikirishi kipungufu.
g) Bainisha yambwa tendwa na yambwa tendewa katika sentensi ifuatayo. ( al 2)
Mwalimu alimtungia wanafunzi mtihani mwepesi
h) Eleza matumizi ya “ kwa” katika sentensi zifuatazo:- ( al 2)
i. Nilisafiri kwa nia ya kulihudhuria mkutano
ii. Alisoma kitabu kwa sauti ya juu
i) Badilisha usemi huu uwe wa taarifa
Fatuma: Lo!Umeyasikia mwenzangu?
j) Andika kwa wingi:
Msonobari huu ukipaliliwa vizuri utamfaidi seremala. ( al 2)
k) Changanua sentensi ifuatayo kwa njia ya matawi: ( al 2)
Magaidi walionaswa wamefikishwa mahakamani
l) Ainisha vihusishi katika sentensi ifuatayo: ( al 2)
Rais atasafiri kutoka Kenya hadi Uganda.
m)Andika vitenzi vifuatavyo katika kauli uliyoandikiwa:
i. Remba( kutenduka) ( al 1)
ii. Kunja (tendama) ( al 1)
n) Andika sentensi ifuatayo upya kwa kugeuza nomino kuwa kitenzi. ( al 2)
Alipewa sifa kwa kufanya kazi nzuri.
GOLDEN ELITE EDUCATIONAL CONSULTANCY P.O BOX 2345 KERICHO. FOR MARKING SCHEMES CALL OR
TEXT MR CHEPKWONY ON 072435I706 0R EMAIL kipkemoicos@gmail.com
o) Andika kisawe cha nahau ifuatayo:
Akina yakhe. ( al 1)
p) Sahihisha sentensi hii:
Mimi sikulangi chakula sikunywangi chai. ( al 2)
q) Eleza maana mbili za sentensi ifuatayo: ( al 2)
Ukienda sokoni uniletee kanga.
r) Andika sentensi upya kwa kutumia “amba” (al 2)
Azembeaye ndiye aumiaye.
s) Kanusha:
Ningefaulu katika mtihani wangu ningefurahi. (al 2)
t) Akifisha:
uui ni nani huyo aliyempiga mwanangu mama aliuliza kwa hasira. (al 3)
u) Bainisha viambishi awali na tamati katika neno lifuatalo: ( al 2)
Waliopendana.

2. ISIMUJAMII: (Alama 10)


“ Juma! Juma! Odijo anakuja! Tukitoe! Usisleki. akikuwahi atakushow dust, huyu ticha ni
mhostile noma … Imagine nimepoteza ile daftari ya zoezi …”
i. Lugha hii inatumika katika mazingira yapi? ( al 2)
ii. Tambua mbinu mbili za lugha katika kifungu hiki. ( al 2)
iii) Eleza ni kwa nini wazungumzaji wanapenda kutumia lugha kama hii katika mazingira
haya. ( al 6)

KARATASI 3
1. SWALI LA LAZIMA
Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.
Nakuliza kazungu, ndugu yangu kulikoni?
Umepikiwa majungu, au ni nira shingoni,
Aushi yako mizungu, nena usinifichani,
Mke kupiga mumewe, ni mila au mapenzi?

Tulikuwa tu mbioni, Zainabu kumnasa,


Ukanipiku mwandani na hata kutoa posa,
Arusi kitamaduni, ya kikwetu na kisasa,
Mke kupiga mmewe, ni mila au mapenzi?

Mebaki kulia ngoa, wingu jeusi Metanda,


Mahari ulishatoa, vibuzi kuku na punda,
Tosi akudonoa, mfano kanga wa manda,
Mke kupiga mumewe, ni mila au mapenzi?

Wikendi ikitimia, kazungu u mashakani,


Deki wairaukia, maana kuna wageni,
Kahawa wajipikia, mkeo yu kitandani,
Mke kupiga mumewe, ni mila au mapenzi?

GOLDEN ELITE EDUCATIONAL CONSULTANCY P.O BOX 2345 KERICHO. FOR MARKING SCHEMES CALL OR
TEXT MR CHEPKWONY ON 072435I706 0R EMAIL kipkemoicos@gmail.com
Mshahara ‘kipokea, mkabidhi mkononi,
Kidogo akugawia, uendee kinyozini,
Nje ukichelewa, utalala ukumbini,
Mke kupiga mumewe, ni mila au mapenzi?

Wewe u kamili mume, au kafiri mjusi,


Songa mbele umseme, tuone akikutusi,
Amri yake mtume, hapo umpe divosi,
Mke kupiga mumewe, ni mila au mapenzi?

Maswali
a) Lipe kichwa shairi ulilosoma. ( al 1)
b) Kwa kutoa sababu kamili. Litie shairi hili katika bahari zozote nne. ( al 4)
c) Andika ubeti wa pili katika lugha nathari. ( al 4)
d) Eleza muundo wa ubeti wa pili. ( al 4)
e) Kwa kutoa mfano mwafaka onyesha jinsi msanii ametumia uhuru wake. ( al 3)
f) Eleza msamiati ufuatao jinsi ulivyotumika katika shairi. ( al 4)
i. Ukanipiku
ii. Nira
iii. Aushi
iv. Posa

SEHEMU YA B – Tamthilia ya KIGOGO


2. “ Ulitaka wahamie wapi siku kama hizi? wamekuja kuuguza majeraha yao ya kufungiwa
soko”
a) Weka maneno haya katika muktadha wake ( al. 4)
b) Tambua mbinu mbili za lugha katika dondoo. ( al. 2)
c) Kando na kufungiwa soko wanasagamoyo wanauguza majeraha yepi mengine
yanayosababishwa na utawala wa majoka? ( al.
10.)
d) Fafanua sifa za msemaji wa dondoo hili. ( al.
4)
3. Tamthilia ya KIGOGO ni tamthilia ya tanzia dhibitisha kwa kufafanua mifano kumi.
( al. 20)
SEHEMU YA C – CHOZI LA HERI
“ Lakini itakuwaje historical injustice, nawe Ridhaa hapo ulipo sicho kitovu chako?”
a) Eleza muktadha wa dondoo hili. ( al. 4)
b) Eleza tamathali mbili za lugha zilizotumika kwenye dondoo hili. ( al. 4)
c) Fafanua umuhimu wa msemaji wa maneno haya. ( al. 6)
e) Ni mambo gani yaliyowakumba wale ambao walipo scho kitovu chao? ( al. 6)
5) Ukabila ni tatizo sugu katika nchi nyingi za Kiafrika. Tetea kauli hii ukilejelea Chozi la Heri.
( al. 20)
SEHEMU YA D.- (TUMBO LISILOSHIMBA NA HADITHI NYINGINE.)

6) “ Hakuna aliyeweza kukitegua kitendawili chenyewe lakini …”


a) Eleza mkutadha wa dondoo hili. ( al 4)
GOLDEN ELITE EDUCATIONAL CONSULTANCY P.O BOX 2345 KERICHO. FOR MARKING SCHEMES CALL OR
TEXT MR CHEPKWONY ON 072435I706 0R EMAIL kipkemoicos@gmail.com
b) Tambua tamathali ya usemi iliyotumiwa katika dondoo hili. ( al 2)
c) Fafanua chanzo na hatima ya kitendawili kinachorejelewa katika dondoo hili. ( al 10)
d) Eleza wasifu wa anayelejelewa katika dondoo. ( al 5)
7. Huku ukirejelea hadithi ya Tumbo lisiloshiba na Shibe inatumaliza, Fafanua madhui ya
ukiukaji wa
haki. (Alama 20)

SEHEMU YA E: FASIHI SIMULIZI


a) Maghani ni nini? (al. 2)
b) Eleza sifa za maghani . (al. 6)
c) Fafanua aina zozote tatu za maghani (al.6)
d) Taja na ueleze umuhimu wa maghani. (al. 6)

MTIHANI 4
MATUMIZI YA LUGHA
1. a) Kanusha sentensi zifuatazo; (alama 2)
(i) Uliugua malaria
(ii) Nimejenga kasri
b) Andika nomino mbili katika ngeli ya U – YA. (alama 2)
c) Andika nomino zinazoweza kuundwa kutokana na vitenzi vifuatavyo.(alama 2)
(i) Safiri
ii) Penda.
2. d) Andika kwa umoja (alama 2)
i) Machaka ya waridi hayazai maua meusi
ii) Walituandikia nyaraka ndefu.
e) Tunga sentensi kuonyesha matumizi ya kila kivumishi cha pekee ulichopewa.
(alama
2)
i) -Ote
ii) –o-ote
f) Onyesha vihisishi katika sentensi zifuatazo. (alama 2)
i) Sawa sawa tutakutana kesho.
ii) Nabii Musa! Eti kifaru hula nyama
3. g) Geuza sentensi zifuatazo katika usemi wa taarifa (alama 4)

i) “Mabasi hayapiti hapa siku hizi, kuna nini” Mazrui aliuliza


ii) Karen: Tafadhali usiukanyage mguu wangu
Kadzo: Ah! Mbona niukanyage?
4. Ukitumia mifano mwafaka, tunga sentensi kudhihirisha matumizi mbalimbali ya;
(alama
2)
i) Jinsi
ii) Ikiwa
5. i) Andika upya sentensi zifuatazo kulingana na maelezo. (alama 2)
i) Mchwa wamezila mbao zetu zote. (Anza na mbao)
ii) Sijali hata kama hunipendi. (Andika kinyume)
GOLDEN ELITE EDUCATIONAL CONSULTANCY P.O BOX 2345 KERICHO. FOR MARKING SCHEMES CALL OR
TEXT MR CHEPKWONY ON 072435I706 0R EMAIL kipkemoicos@gmail.com
j) Kamilisha jedwali hili (alama 4)
Kitenzi Kutenda Kutendana
Fa ……………………………….
………………………………
Cha ……………………………….. ……………………………...

6. Ukitumia mchoro wa matawi, onyesha muundo wa sentensi ifuatayo.(alama 4)


Mtoto huyu alikunywa maziwa mengi
7. Tofautisha maana za sentensi hizi. (alama 2)
i) Ningalipandishwa madaraka, ningalinunua gari
ii) Ningepandishwa madaraka ningenunua gari
8. Eleza matumizi ya ni katika sentensi hizi. (alama 2)
i) Njooni kwangu nyinyi nyote
ii) Duniani waja wote ni sawa
n) Taja aina ya vitenzi vilivyopigiwa mstari chini katika sentensi zifuatazo.
9. (alama 2)
i) Huyu ndiye aliyetukomboa.
ii) Baba amekuwa mgonjwa
10. II. a) Eleza maana ya semi zifuatazo (alama 2)
i) Kata bei
ii) Tia ngoa
11. b) Kamilisha majina haya ya makundi. (alama 2)
i) Mkungu wa ……………………………………………………………………..
ii) Thurea ya ………………………………………………………………………
c) Andika visawe vya; (Alama 2)

i) Sarafu …………………………………………………………………………..
ii) Daktari ………………………………………………………………………….
4. ISIMUJAMII
12. (a) Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali yanayofuata (alama 10)
A: Habari yako ndugu
B: Ndugu…… Ahh! (Anamsogelea) Bwana asifiwe!
A: Asifiwe sana ndugu!
B: Amen! Ahh ndugu yangu, imekuwa vipi umepotea hivyo?
A: Usiwe ha hofu ndugu. Nilikuwa nimeenda kuhubiri huko Nakuru. (Anatua
kidogo).
Ilinibidi niende huko, ili kutimiza amri ya Bwana.
B: Eeh, hata Yohana alienda kuhubiri ……………
A: Habari ya siku nyingi?
B: Nzuri, Bwana ameendelea kunineemeshea baraka zake
A: Amen!
B: Nimeona mkono wake katika kila jambo
A: Amen! Asifiwe Bwana
B: Amen
A: Ameendelea kunibariki sana. Shetani hana nafasi katika maisha yangu
B: Shetani ashindwe
GOLDEN ELITE EDUCATIONAL CONSULTANCY P.O BOX 2345 KERICHO. FOR MARKING SCHEMES CALL OR
TEXT MR CHEPKWONY ON 072435I706 0R EMAIL kipkemoicos@gmail.com
A: Ashindwe Ibilisi.
Maswali
13. i) Toa muktadha wa mazungumzo haya. (alama 1)
ii) Taja sifa zozote mbili zilizojitokeza katika mazungumzo haya. (alama 2)
14. iii) Huku ukitoa mifano mitatu onyesha tofauti iliyoko kati ya mazungumzo haya na
mazungumzo yanayoweza kutokea mahakamani.
(alama 3)
b) atatizo ya lugha katika matamshi yafuatayo yanasababishwa na nini? Andika lugha
sanifu
(i) Nipeko jai nikunyenge wakati nikikungojeanga (alama 1)
(ii) Tsambi sangu sote simeoswa na tamu ya Yesu. (alama 1)
(iii) Alienda kukojoa baada yake kuhara. (alama 1)
iv) Mimi ninakuja kwa hapa. (alama 1)
MTIHANI 5
MASWALI YA KIGOGO
1. Kwa kirejelea tamthilia ya kigogo, jadili mbinu - ishi tunazojifunza kutokana na kijana
Tunu. (alama 20)
2. “Ukitaka kukula asali kaa na nyuki!”
a) Eleza muktadha wa dondoo hili. [alama 4]
b) Bainisha mbinu iliyotumika katika dondoo hili. [alama 2]
c) Eleza jinsi wahusika hawa walivyofaidika kutokana na kukaa na nyuki. [alama 14]
i. Chopi
ii. Kenga
iii. Ngurumo
iv. Mamapima
3. Eleza jinsi mwandishi alivyotumia mbinu ya majazi. [alama 20]
4. “Shika hamsini zako wewe ... Hatutaki kufanya nira na mtu ...”
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
(b) Eleza tamathali ya usemi iliyotumika. (alama 2)
(c) Uongozi wa Majoka umesheheni sumu ya nyoka. Thibitisha kwa kudokeza hoja kumi na
nne. (alama 14)
5. . Utawala mbaya ni tatizo sugu linalozikumba nchi nyingi za kiafrika. Jadili, kwa
kurejelea matukio ishirini katika tamthilia ya Kigogo (alama 20)
6. “Ulitaka wahamie wapi siku kama hizi? Wamekuja kuuguza majeraha yao ya kufungiwa
soko.”
a) Weka maneno haya katika muktadha wake. (alama 4)
b) Tambua mbinu mbili za lugha katika dondoo hili (alama 2)
c) Kando na kufungiwa soko, Wanasagmoyo wanauguza majeraha yepi mengine
yanayosababishwa na utawala wa Majoka (alama 5)
d) Fafanua sifa za msemaji wa dondoo hili. (alama 9)
7. "Si haki. Unayazika matumaini yetu. Unaifukua kesho yetu. Unatupoka utu na heshima
yetu."
a) Fafanua muktadha wa maneno haya. (alama 4)
b) Eleza tamathali iliyotumika kwenye dondoo hili. (alama 2)
c) Onyesha vile mrejelewa alivyoyazika matumaini na alivyofukua kesho yao. (alama 14)

GOLDEN ELITE EDUCATIONAL CONSULTANCY P.O BOX 2345 KERICHO. FOR MARKING SCHEMES CALL OR
TEXT MR CHEPKWONY ON 072435I706 0R EMAIL kipkemoicos@gmail.com
8. Tamthilia ya Kigogo ni taswira kamili ya matatizo yanayokumba mataifa mengi barani
Afrika. Fafanua ukirejelea Tamthilia nzima. (alama 20)
9. “Kitabu si jalada, fungua ndani usome mambo. Kitanda usichokilalia kunguni wake
huwajui.”
a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (al.4)
b) Kwa kurejelea tamthilia ya kigogo, thibitisha ukweli wa dondoo hili. (al.14)
c) Taja tamathali za usemi zilizotumika katika dondoo hili. (al.2)

10. Eleza mbinu alizotumia majoka kuendeleza uongozi wake. (al.20)


11. “Oooh bebi, miaka yaenda mbio sana, nayo sura yako inachujuka……”
a) Weka dondoo hili katika muktadha wake. (alama 4)
b) Mhusika anayehusishwa na wimbo huu ana msimano gani wa kimapinduzi?
(alama 8)
c) Taja sifa zozote nane za muhusika huyu (alama 8)
12. Tamthilia ya ‘Kigogo’ ni kioo cha uhalisia wa maisha ya jamii nyingi za kiafrika.
Thibitisha. (alama 20)
13. “Mguu huu ni wako”
a) Eleza muktadha wa dondoo hili (al. 4)
b) Ni tamathali gani ya usemi iliyotumika katika dondoo hili. Eleza maana yake (al.2)
c) Msemewa alipewa ahadi zipi (al. 5)
d) Eleza sifa na umuhimu wa mzungumzaji (al. 9)
14. “Dalili ya mvua ni mawingu, lazima tuwe macho”.
a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
b) Bainisha tamathali ya usemi iliyotumika katika dondoo hili. (alama 2)
c) Ushauri uliotolewa na msemaji baadaye kama njia mojawapo ya kuwa macho ni wa
kidhalimu. Fafanua. (alama 4)
d) Eleza namna unafiki wa msemaji na upumbavu wa mnenewa unavyodhihirika katika
muktadha wa dondoo hili. (alama
e) Onesha jinsi ukweli wa kauli hii ulivyojitokeza baadaye katika tamthilia. (alama 4)
15. Jadili migogoro inayojitokeza katika tamthilia ya kigogo, kisha utathmini namna
ilivyosuluhishwa. (alama 20)
16. “ Do ! Do ! Simameni ! Simameni leo kutanyesha mawe! “
(i) Eleza muktadha wa dondoo hili. ( alama 4)
(ii) Fafanua mbinu za lugha zilizotumika katika dondoo (alama 4)
(iii) Dhihirisha kwa kuzingatia hoja sita jinsi mwanamke alivyosawiriwa katika
tamthilia ya “ Kigogo.” (alama 12)
17. Eleza kwa kutolea mifano mitano mitano jinsi mwandishi alivyofaulu kutumia mbinu za :
a) mbinu rejeshi (alama 10)
b) sadfa (alama10)
18. Eleza jinsi mbinu ya taharuki ilivyotumika kufanikisha maudhui katika tamthilia ya
kigogo. (alama 20)
19. "Maandamano na migomo ni tatizo sugu katika mataifa yanayoendeleaa." Kwa kurejelea
tamthilia ya kigogo, eleza chanzo na athari za maandamano na migomo. (alama 20)
20. Jadili jinsi maudhui ya uzalendo yamejitokeza katika tamthilia ya Kigogo (alama 20)
21. Jadili ufaafu wa anwani "kigogo" katika tamthilia ya kigogo. (alama 20)
GOLDEN ELITE EDUCATIONAL CONSULTANCY P.O BOX 2345 KERICHO. FOR MARKING SCHEMES CALL OR
TEXT MR CHEPKWONY ON 072435I706 0R EMAIL kipkemoicos@gmail.com
22. Mwandishi wa kigogo amewajenga wanawake kwa njia hasi na chanya. Jadili kauli hii
kwa kutolea mifano kutoka tamthilia (alama 20)
23. "Wananchi katika mataifa ya Afrika hukumbwa na matatizo ya viongozi wanafiki."
Thibitisha kauli hii kwa kutolea mifano kutoka tamthilia ya kigogo. (alama 20)
24. Fafanua jalada la tamthilia kigogo (alama 20)

MTIHANI 6
SEHEMU A

Fasihi Simulizi
1. Soma kisha ujibu maswali
Lala mtoto lala x2
Mama atakuja lala
Alienda sokoni lala
Aje na ndizi lala
Ndizi ya mtoto lala
Na maziwa ya mtoto lala
Andazi lako akirudi
Pia nyama ya kifupa
Kifupa, kwangu, wewe kinofu
Kipenzi mwana lala x2

Titi laja x2

Basi kipenzi lala


Baba atakuja lala
Aje na mkate lala
Mkate wa mtoto lala
Tanona ja ndovu lala

Maswali
(a) Huku ukithibitisha jibu lako eleza huu ni wimbo wa aina gani?

(b) Eleza sifa za wimbo wa aina hii

(c) Onyesha umuhimu wa wimbo huu

(d) Eleza amali kuhusu jamii zinazojitokeza katika wimbo huu

(e) Tambua mbinu zozote mbili za utunzi zilizotumika katika wimbo huu

(f) Taja vitendo viwili vinavyoambatana na uimbaji wa aina hii ya wimbo

(g) Wimbo huu una wahusika wangapi? Wataje

GOLDEN ELITE EDUCATIONAL CONSULTANCY P.O BOX 2345 KERICHO. FOR MARKING SCHEMES CALL OR
TEXT MR CHEPKWONY ON 072435I706 0R EMAIL kipkemoicos@gmail.com
2. Soma hadithi hii halafu ujibu maswali ulivyoulizwa
Hapo zamani za kale, Mungu alituma wajumbe wawili waende duniani. Wajumbe
hawa ni Kinyonga na Mjusi. Kwanza alimtuma Kinyonga na kumwagiza akaseme
“wanadamu hamtakufa.” Kinyonga alienda kwa mwendo wa kuduwaa, akasimama hapa
na pale akila matunda ya miti. Kwa sababu ya hali hii alichelewa sana kufikisha ujumbe
kwa binadamu.
Baada ya muda kupita, Mungu alimtuma Mjusi na ujumbe akaseme,
“Mwanadamu sharti kufa.” Mjusi aliunyanyua mkia akafyatuka pu! Mbio akawahi
duniani kabla ya kinyonga kuwasili. Kwa haraka alitangaza agizo kuu, “Wanadamu
sharti kufa!” Akarejelea haraka kwa Mungu. Baada ya muda kinyonga naye akafika
duniana na kutangaza, “Wanadamu hamtakufa!” Wanadamu wakapinga mara na kusema,
“La! Tumeshapata ujumbe wa Mjusi, wanadamu sharti kufa! Hatuwezi kupokea tena
neno lako! Basi kulingana na neno la mjusi, wanadamu hufa.

Maswali
(a) (i) Hadithi hii huitwaje?
(ii) Toa sababu zako
(b) Eleza sifa tatu zinazohusishwa na ngano za fasihi simulizi katika hadithi hii
(c) Kinyonga ni mhusika wa aina gani?
(d) Hadithi hii ina umuhimu gani?
(e) Taja njia zozote nne za kukusanya kazi za fasihi simulizi
(f) Tambulisha vipera hivi:-
(i) Kula hepi
(ii) Sema yako ni ya kuazima
(iii) Baba wa Taifa
3. (a) Fafanua sifa tatu za ushairi simulizi
(b) Wawe na kimai ni nini katika fasihi simulizi? Eleza faida zake
(c) Ainisha mambo yanayobainisha muundo wa nyimbo

(d) Jadili muundo wa kitendawili

(e) Bainisha tamathali za usemi zilizotumika katika methali zifuatazo:-


(i) Ujana ni moshi ukienda haurudi

(ii) Usipoziba ufaa utajenga ukuta

(f) Jadili kwa kina matatizo ambayo huenda yakakabili fasihi simulizi katika jamii ya kesho
kisha utoe mapendekezo ya jinsi ya kukabiliana na hali hii

4. Soma wimbo/shairi lifuatalo kisha ujibu maswali yanayofuata


MUITALIA ANAZWE
Saa kumi alfajiri
Sote tuliamshwa
GOLDEN ELITE EDUCATIONAL CONSULTANCY P.O BOX 2345 KERICHO. FOR MARKING SCHEMES CALL OR
TEXT MR CHEPKWONY ON 072435I706 0R EMAIL kipkemoicos@gmail.com
Safari tuliianza
Lazima tuimalize
Maji ukiyavulia nguo
Lazima uyaoge

Wazee kwa vijana waliimba


Muitalia lazima anazwe
Mashamba yao walilia
Uui! Jikaze wavulana
Hawataki rangi hii

Wengi wanauliza
Mwitalia alikuja lini? Na ataondoka lini?
Mnaze huyu mlowezi
Hatuchoki
Hatuchoki
Lazima yeye anazwe

Vifaranga na mbuzi
Mbavu zao zahesabika
Meee! Sauti zilihinikiza kote
Haya yote hakika, ni madhila ya Muitalia
Nguvu kweli tunayo
Simama mbele tunayo
Simama mbele uone !
Muitalia ondoka !
Au nikuondoe kwa nguvu

Maswali
(a) Taja madhila yaliyosababishwa na Muitalia katika makala haya.
(b) Thibitisha kuwa utungo huu ni wimbo.
(c) Eleza maana inayojitokeza katika mistari ifuatayo:-
(i) Mbavu zao zahesabika.
(ii) Haya yote hakika, ni madhilia ya Muitalia.
(d) Huu ni wimbo wa aina gain? Eleza ukitoa ushahidi
(e) Eleza kwa sentensi mbili au tatu shughuli muhimu za kiuchumi za watu wanaimba
wimbo huu
(f) Taja mbinu za lugha zilizotumiwa katika wimbo huu. Toa ushahidi
(g) Taja mafunzo mawili yanayotokana na wimbo huu

5. (a) Eleza maana ya miviga kisha uonyeshe inakotumika


(b) Eleza sifa za miviga
(c) Onyesha umuhimu wa miviga
6. Ni nini maana ya wimbo ?
GOLDEN ELITE EDUCATIONAL CONSULTANCY P.O BOX 2345 KERICHO. FOR MARKING SCHEMES CALL OR
TEXT MR CHEPKWONY ON 072435I706 0R EMAIL kipkemoicos@gmail.com
Ni nini maana ya nyimbo zifuatazo.

Tenzi
Kongozi
Sifo
Wawe
Tendi
(a) Eleza umuhimu wa nyimbo

(b) Eleza sifa za wimbo wa aina ya Bembelezi

7. (a) Nini maana ya khurafa/kharafa?


(b) Fafanua sifa tano za kharafa

(c) Elezea mbinu nne za kutongolea hadithi


8. (a) (i) Ngomezi ni nini katika fasihi simulizi?
(ii) Eleza sifa zozote mbili za ngomezi
(b) Onyesha tofauti kati ya vikundi hivi:
(i) Hekaya
Hurafa
(ii) Visakale
Visasili
(iii) Ngano za mtanziko
Ngano za mazimwi
(c) (i) Vitendawili ni nini?
(ii) Fafanua kwa mifano, mbinu zozote nne za lugha zinazopatikana katika vitendawili
(d) Soma kifungu hiki cha wimbo kisha ujibu maswali yafuatayo :
Kuumeni  : (Waliimba) Tumeupata mpilipili na maua yake. Chikicha x2
Kukeni  : (Wimbo wao kwa sauti tofauti)
Tausi waendaa x2
Tausi waenda wamuacha mama kwenye banda
Kuumeni  : (Wakijibu wimbo) Mwacheni aendee x2
Mwacheni aende akaone mambo ya nyumba
Kukeni  : Mama ataota nini x2
Ataota nini, hana mtu wa kumletea kuni
Kuumeni  : Ataota moto wa magunzi, wa magunzi, wa magunzi.
Twamchukua , kisura wetu, kisura wetu, kisura wetu.
Tausi ni wetu, sasa, ni kito chema, ni kito chema ni kito chema.
Maswali
(i) Wimbo huu ni wa aina gani na unastahili katika hafla gani ?

(ii) Fafanua ujumbe uliojikita katika utungo huu

9. Soma kifungu kifuatacho kisah ujibu maswali yafuatayo :

GOLDEN ELITE EDUCATIONAL CONSULTANCY P.O BOX 2345 KERICHO. FOR MARKING SCHEMES CALL OR
TEXT MR CHEPKWONY ON 072435I706 0R EMAIL kipkemoicos@gmail.com
(vigelegele vya harusi vililia alilili ; x3)
Kuumeni  : (waliimba) Tumeupata mpilipili na maua yake chikicha x2
Kukeni  : (wimbo wao kwa sauti tofauti) Tausi waendaa x2
Tausi waenda wamuacha mama kwenye banda.
Kuumeni  : (wakijibu wimbo) Mwacheni aendee x2
Mwacheni aende akaone mambo ya nyumba.
Kukeni  : Mama ataota nini x2.
Ataota nini, hana mtu wa kumletea kuni.
Kuumeni  : Ataota moto wa magunzi, wa magunzi wa magunzi. Twamchukua,
kisura wetu,
kisura wetu, kisura wetu.
Tausi ni wetu sasa, ni kito chema, ni kito chema ni kito chema.
(a) (i) Wimbo huu ni wa aina gani, na unastahili katika hafla gani ?

(ii) Bainisha wahusika Kuumeni na Kukeni


(iii) Fafanua ujumbe uliojikita katika utungo huu
(iv) Wimgo huu una umuhim;u gain hafia ulioimbiwa?
(v) Tambua mtindo uliotumika katika utungo huu
(b) Taja na ujadili aina nyingine sita za nyimbo

10. a) Taja sifa za tanzu zifuatazo za fasihi simulizi


i) Hurafa
ii) Mighairi
iii) Miviga
b) Eleza umuhimu wa ngomezi katika jamii
c) Eleza umuhimu wa mafumbo
d) Eleza tofauti kati ya malumbano ya utani na mawaidha

11. (a) Huku ukizingatia sifa za kimuundo za methali, jadili matumizi ya tamathali za usemi
sifuatazo:-
(i) Istiari/sitiari
(ii) Tashihisi
(iii) tashbihi

(b) Vitanza ndimi vina dhima gani katika jamii?

(c) Taja majukumu matatu ya nyimbo katika fasihi simulizi

(d) Eleza sifa tatu za ngano za mtanziko

(f) Eleza sifa tatu za Nyiso

(e) Fasihi simulizi ina sifa ya kuhifadhiwa akilini. Eleza udhaifu wa uhifadhi wa akilini
(al. 4)
12. (i) Eleza maana ya vitanza ndimi.
GOLDEN ELITE EDUCATIONAL CONSULTANCY P.O BOX 2345 KERICHO. FOR MARKING SCHEMES CALL OR
TEXT MR CHEPKWONY ON 072435I706 0R EMAIL kipkemoicos@gmail.com
(ii) Taja na ufafanue umuhimu wa vitanza ndimi katika jamii .

SEHEMU B
MASWALI YA FASIHI SIMULIZI
1. Swale la 1
a) Fafanua sifa tatu za kila mojawapo ya vipera vya fasihi simulizi vifuatavyo (alama6)
(i) Vitendawili
(ii) Methali
b) Mawaidha yana dhima gani katika jamii? Eleza (alama6)
c) Bainisha sifa za nyimbo. (alama4)
d) Eleza umuhimu wa nyimbo za kisiasa (alama4)

2. Swali 2
a) Eleza namna ambavyo hadhira wanahusishwa katika utambaji. (alama 8)
b) Taja sifa nne bainifu za hadithi. (alama 4)
c) Fafanua sifa nne za fanani/mtambaji bora. (alama 8)
3. swali 3
a) Methali ni nini? (alama2)
b) Ainisha sifa Tano za methali za Kiswahili (alama10)
c) Elezea umuhimu wa hadithi kama utanzu wa fasihi simulizi katika jamii (alama8)
4. Swali la 4
a) Maghani ni nini? (alama 2)
b) Eleza fani zifuatazo za maghani (alama 8)
1. Vivugo
2. Tondozi
3. Pembezi
4. Rara
c) Eleza maana ya neno ULUMBI (alama 1)
d) Bainisha sifa za mlumbi (alama 6)
e) Eleza umuhimu wa ulumbi (alama 3)
5. Swali la 5
a) Taja mbinu zozote tatu za kuhifadhi fasihi simulizi (alama 3)
b) Taja aina zozote tatu za vitendawili (alama 3)
c) Bainisha matumizi ya lugha katika vitendawili (alama 3)
d) Ngomezi ni nini? (alama 1)
e) Eleza ujumbe uliowasilishwa na ngomezi katika fasihi simulizi. (alama 3)
f) Fafanua sifa zozote nne za ngomezi. (alama 4)
g) Taja mifano mitatu ya ngomezi ya kisasa. (alama 3)

6. Swali la 6
a) Tofautisha baina ya
(i) Hurafa na Hekaya. (alama 4)
(ii) Hadithi za mazimwi na hadithi za mtanziko. (alama 4)
(iii) Usuli na visasili. (alama 4)
GOLDEN ELITE EDUCATIONAL CONSULTANCY P.O BOX 2345 KERICHO. FOR MARKING SCHEMES CALL OR
TEXT MR CHEPKWONY ON 072435I706 0R EMAIL kipkemoicos@gmail.com
b) He! He! He! Weee!
Unayeogopa kutahiriwa
Nani atatahiri badala yako
Eh, eh…. Ni babu yako
Eh, Eee!.... kisu kikali mno!
Lakini nitavumilia.
(i) Wimbo huu huitwaje? (alama 1)
(ii) Nini dhamira ya wimbo huu? (alama 2)
(iii) Taja sifa zozote tano za utanzu wa nyimbo kwa jumla.(alama 5)
7. Swali la 7
a) (i) Eleza maana ya misimu (alama 1 )
(ii) Kuchipuka kwa misimu kunategemea mambo mengi. Taja matano miongoni mwa
haya. (alama 5)
b) Eleza muhimu wa misimu katika jamii (alama 4)
c) (i)Nini maana ya ngomezi? (alama 2)
(ii) Ngomezi ina umuhimu gani? (alama 5)
d) Taja udhaifu wa ngomezi katika kuwasilisha ujumbe katika jamii (alama 3
8. Swali la 8
a) (i) Fafanua maana ya methali (alama 2)
(ii) Fafanua sifa tano za methali (alama 5)
b) Eleza majukumu matano ya methali
c) Eleza jinsi fasihi simulizi inavyohifadhiwa siku hizi
d) Taja njia nne za kukusanya fasihi simulizi
9. Swali 9
a) Taja majukumu manne ya Fasihi Simulizi. (alama 4)
b) (i) Mawaidha ni nini? (alama 1)
(ii) Fafanua sifa tatu za mawaidha. (alama 3)
c) Eleza maana na umuhimu wa aina hizi za nyimbo.
(i) Nyiso (alama 2)
(ii) Mbolezi (alama 2)
(iii) Vave (wawe) (alama 2)
d) Taja vijipera vitatu vya maigizo. (alama 3)
e) Fafanua sifa tatu za methali. (alama 3)
10. Swali la 10
a) Tofautisha baina ya ulumbi na soga (Alama 4)
b) Fafanua sifa za ulumbi (Alama 7)
c) Taja baadhi ya Miviga maarufu katika jamii za Afrika (Alama 3)
d) Eleza umuhimu wa Miviga katika jamii (Alama 6)
11. Swali la 11
a) Eleza maana ya tanzu zifuatazo za Fasihi Simulizi(alama 4)
i. Vitanza ndimi
ii. Vitendawili
iii. Ngano
iv. Nyimbo
b) Taja sifa mbili mbili za kila mojawapo wa vipera vya fasihi simulizi vilivyotajwa kati
(alama 8)
GOLDEN ELITE EDUCATIONAL CONSULTANCY P.O BOX 2345 KERICHO. FOR MARKING SCHEMES CALL OR
TEXT MR CHEPKWONY ON 072435I706 0R EMAIL kipkemoicos@gmail.com
c) Eleza umuhimu wa vitanza ndimi. (alama 4)
d) Fafanua uamilifu wa vitendawili katika jamii. (alama 4
12. Swali la 12
a) Maghani ni nini? (alama 2)
b) Eleza fani zifuatazo za maghani
i. Vivugo
ii. Tondozi
iii. Pembezi
iv. Rara (alama 8)
c) Eleza maana ya neno ULUMBI (alama 2)
d) Bainisha sifa nane za mlumbi (alama 8)
13. SWALI 13
a) Fasihi simulizi ina makundi manne makuu, yataje . alama 4
b) Kwa kila kikundi ulichotaja katika swali la (a) , toa mifano miwili ya vipera vya kila
kikundi na utoe maelezo mafupi ya vipera hivyo alama 8
c) Nyimbo huwa na jukumu gani katika usimulizi alama 2
d) Fasihi simulizi ina sifa ya kuhifadhiwa akilini . Eleza udhaifu wa uhifadhi wa akilini.
Alama 6
14. SWALI 14
a) Taja mbinu zozote nne zinazotumiwa kuhifadhi fasihi simulizi huku ukitolea mifano
(alama 4)
b) Eleza umuhimu wa kuhifadhi fasihi simulizi (alama 8)
c) Semi ni utanzu wa fasihi simulizi ambao ni mfupi na uundwao kwa maneno machache
au sentensi kadha.Taja na ujadili vipengele vyovyote vinne vinavyojumuishwa na kundi
hili( alama 8)
15. SWALI 15
a) Tofautisha kati ya methali na msemo. ( alama 2)
b) Toa mifano miwili miwili ya methali zinazozingatia tamathali zifuatazo;
i. Balagha (alama 2)
ii. Takriri ( alama 2)
iii. Ukinzano (alama 2)
c) (i) Fafanua vijipera vifuatavyo vya mazungumzo.
i. Utani ( alama 2 )
ii. Soga ( alama 2
iii. Ulumbi ( alama 2 )
iv. Taja sifa na umuhimu wa soga. ( alama 6 )
16. SWALI 16
a) Eleza kikamilifu sifa zozote tano za mtambaji katika fasihi simulizi(alama 10)
b) Fasihi simulizi aghalabu hutambulika kutokana na sifa zake kuu. Jadili.(alama10)
17. Swali la 17
a) Ngomezi ni nini? (alama 2)
b) Eleza umuhimu wa ngomezi katika jamii. (alama 4)
c) Methali zina umuhimu gani katika jamii? (alama 10)
d) d) Eleza jukumu la fomula za ufunguzi katika hadithi.(alama 4)
18. SWALI 18
a.Taja mifano minane ya tanzu fupi katika fasihi simulizi.
GOLDEN ELITE EDUCATIONAL CONSULTANCY P.O BOX 2345 KERICHO. FOR MARKING SCHEMES CALL OR
TEXT MR CHEPKWONY ON 072435I706 0R EMAIL kipkemoicos@gmail.com
b. Fafanua sifa zozote tatu za mawaidha katika fasihi simulizi.
c.Eleza umuhimu tatu wa ngomezi. (alama 3)
d. Eleza istilahi hizi za fasihi simulizi. (alama 3)
i. Maghani
ii. Mapisi
iii. Misimu / simo
e. Fafanua sifa zozote tatu ambazo mtambaji wa hadithi anastahili kuwa nazo. (alama 3)
f. Taja methali zozote mbili zilizo na dhana ya tashibiha. (alama 2)
g. Eleza sifa zozote mbili za nyimbo zinazotofautisha nyimbo na ushairi simulizi (alama 2)
19. SWALI 19
a) Taja na ueleze aina zozote tano za Hadithi. (alama 5)
b) Tofautisha kati ya
i. Mbolezi na Bembezi
ii. Vitendawili na chemsha bongo. (alama 4)
c) Eleza umuhimu wa vitanza ndimi (alama 3)
d) Taja na ueleze sifa nne ambazo mtambaji anapaswa kuwa nazo.(alama 4)
e) (i) Fafanua maana ya methali. (alama 2)
(ii)Taja methali zinazohusu:Kuliwaza.
20. SWALI 20
a) (i)Ngano ni nini? [alama 1]
(ii)Eleza tofauti iliyoko kati ya visasili na visakale [alama 4]
(iii)Fafanua majukumu yoyote muhimu ya ngano katika jamii. [alama 5]
b) (i) Eleza umuhimu wa vitendawili katika jamii. [Alama 3]
(ii) Tega na utegue vitendawili vyovyote viwili vilivyo na lugha ya takriri na lugha ya
mlio.[alama 2]
c) Taja sifa zozote tatu za methali. [alama 3]
d) Taja methali yoyote iliyo na lugha ya balagha kisha ueleze maana yake ya ndani [alama
2]
21. Swali la 21
a) (i) Eleza umuhimu wa nyimbo katika usimulizi.( Alama 2)
(ii) Taja na kueleza tanzu / aina za nyimbo ( Alama 10)
b) Tofautisha semi hizi
i) Nahau na misimu (Alama 2)
ii) Eleza maana ya nahau hizi (Alama 4)
a. Hawapikiki katika chungu kimoja
b. Yeye ni jamvi la wageni
c. Amemwaga mtama
d. Amechomekwa mizizi
c) Taja na kufafanua misimu yoyote miwili. (alama 2)
22. SWALI 22
a) Fafanua fani zifuatazo za fasihi simulizi (alama 6)
i. Ngano za mtanziko
ii. Mazingira
iii. Kifunga nyama

GOLDEN ELITE EDUCATIONAL CONSULTANCY P.O BOX 2345 KERICHO. FOR MARKING SCHEMES CALL OR
TEXT MR CHEPKWONY ON 072435I706 0R EMAIL kipkemoicos@gmail.com
b) Umeombwa kusimulia darasani mighani wa Fumo Liyongo, eleza namna
utakavyofanikisha uwasilishaji wako. (alama10)
c) Je, ni vipi jamii ya kisasa inaendeleza Fasihi Simulizi (alama 4)
23. SWALI LA 23
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali
Ndimi Kisoi, dume la ukoo mtukufu
Ulojipambanua kwa mabingwa
Wachezaji hodari wa ngoma
Ndimi dume liloingia nyanjani
Makoo yakatetemeka
Yakang’ang’ania gozi kusakata nami
a. Tambulisha kipera kinachojitokeza katika kifungu hiki. (alama 2)
b. Eleza sifa tano bainifu za kipera hiki katika fasihi simulizi.(alama 10)
c. Fafanua umuhimu wa kipera hiki. (alama 8)
24. SWALI LA 24
a) Taja na ueleze vipera vya maghani. (alama 10)
b) Eleza maana ya miviga. (alama 2)
c) Fafanua sifa nne za miviga katika jamii. (alama 8)
25. SWALI LA 25
a) Huku ukitoa hoja sita linganisha aina mbili kuu za fasihi.(alama 6)
b) Jadili vipengele sita vya kuzingatia katika uchanganuzi wa hadithi.(alama 6)
c) Jadili sifa mbili za vitanza ndimi kwa kurejelea sauti.(alama 2)
d) Tambua istuiatu zinzotokana na maelezo haya.
(i) Msimulizi wa fasihi simulizi anaitwaje kwa jumla? (alama 1)
(ii) Shujaa katika mighani pia anaweza kuitwa nani? (alama 1)
(iii) Sherehe za kitamaduni ambazo hufungwa na jamii katika kipindi fulani
maalum huitwaje? (alama 1)
(iv)Mavazi au vifaa vinavyotumiwa na wasanii kuakisi hali halisi ya mambo wakati
wa kuwasilisha fasihi huitwaje? (alama 1)
(v) Mtambaji wa hadithi hutumia ujuzi gani anapoibadilisha hadithi yake moja kwa
moja mbele ya hadhira bila kuathiri usimulizi wake?(alama 1)
(vi)Wanaosimuliwa ili kuonyesha kazi ya fasihi simulizi hupewa jina hili. (alama 1)

GOLDEN ELITE EDUCATIONAL CONSULTANCY P.O BOX 2345 KERICHO. FOR MARKING SCHEMES CALL OR
TEXT MR CHEPKWONY ON 072435I706 0R EMAIL kipkemoicos@gmail.com
26. SWALI LA 26
a) Eleza sifa tano za miviga. (alama 5)
b) Huku ukitoa mifano, onyesha udhaifu wa miviga. (alama 5)
c) Taja aina za miviga ambayo hupatikana katika jamii ya kisasa. (alama 5)
d) Eleza nafasi ya miviga katika jamii. (alama 5)
27. SWALI LA 27
a) Eleza vipengele vitano vya fasihi simulizi ambavyo hujitokeza katika fasihi andishi.
(alama 10)
b) Fafanua sifa tano za ushairi simulizi.(alama 10)
28. SWALI LA 28
a) Fafanua mambo yanayochangia kubadilika kwa fasihi simulizi. (alama 10)
b) Eleza maana ya lakabu. (alama 2)
c) Sifa za lakabu ni zipi? (alama 4)
d) Kwa nini lakabu ni muhimu katika jamii. (alama 4)
29. SWALI LA 29
a) Eleza maana ya maigizo katika fasihi simulizi.(alama 2)
b) Tofautisha aina mbili kuu za maigizo. (alama 8)
c) Kwa kutoa hoja sita, eleza umuhimu wa maigizo katika jamii.(alama 6)
d) Kwa kutoa mifano minne, onyesha jinsi misimu huzuka.(alama 4)
30. SWALI LA 30
a) Miviga inafaaa kupigwa marufuku katika jamii ya kisasa. Thibitisha kauli hii kwa
kutoa hoja nane (alama 8)
b) Taja mifano sita yangomezi za kisasa (alama 6)
c) Ni jukumu la jamii kudumisha Fasihi Simulizi. Dhihirisha (alama 6)
31. SWALI LA 31
Ewe malaika wangu
Uloshuka toka mbinguni
Mbingu kapasua kwa heri
Siku nipokukopoa
Ulinitia furaha iliyopasua kifua
Tabasamu kipajini pako
Ilinitia tumaini, ikanisahaulisha zingizi
GOLDEN ELITE EDUCATIONAL CONSULTANCY P.O BOX 2345 KERICHO. FOR MARKING SCHEMES CALL OR
TEXT MR CHEPKWONY ON 072435I706 0R EMAIL kipkemoicos@gmail.com
Ikayayeyusha madhila, ya utasa wa miaka kumi
Ikapeperusha mbali, cheko la ukewenza.
Sasa napolia, wanitonesha jeraha
Wanirejesha misri, kwa vitimbi vya Firauni
Kwa vitisho vya muhebi
Talaka kuahidiwa, hadi mbingu
Lipofungua milango ya heri.

Silie mwana silie, walimwengu watakusuta,


Tangu hapo tanabahi
Vidume humu mwenu
Kulia havikuumbiwa,
Machozi na kekevu ni za kike fahamu,
Jogoo halii daima huwika
Nikikuona kigugumika hivi wanitia hangaiko
Tumaini kuzima
Udhaifu kiandama
Moyo kutia hamaniko,
Ananipigania nani?
Watesi king’ang’ania
Changu kujitwalia?

Maswali.
a) Thibitisha aina ya utungo huu. (alama 2)
b) (i) Bainisha jinsia inayoongolewa kwenye utungo huu. (alama 1)
(ii) Thibitisha jibu lako la hapo juu (i) (alama 1)
c) (i) Elesa nafsineni katika utungo huu. (alama 1)
(ii) Toa sababu mbili kuthibitisha jibu lako la hapo juu (i) (alama 1)
d) Eleza sifa tano za utungo huu. (alama 5)

GOLDEN ELITE EDUCATIONAL CONSULTANCY P.O BOX 2345 KERICHO. FOR MARKING SCHEMES CALL OR
TEXT MR CHEPKWONY ON 072435I706 0R EMAIL kipkemoicos@gmail.com
e) Huku ukitoa mifano, bainisha vipengele sita vya kimtindo ambapo nafsineni
imetumian kufanikisha uwasilishaji wa utungo huu. (alama 6)
f) Eleza majukumu tano ya utungo huu. (alama 5)
32. SWALI LA 32
  Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali
Sungura alivyokwepa kuliwa na simba
Wanyama wa pori waliamua siku moja kumtuma mnyama mmoja kila siku alikoishi simba
kama chakula. Siku moja ilikuwa zamu ya sungura kwenda huko. Sungura alikuwa mjanja
sana. Alipanga mpango mzuri wa kumwangamiza simba.
Alienda alikoishi simba muda mrefu baada ya muda wa chakula wa simba. Alimkuta simba
akiwa na hasira kubwa sana.
``Kwa nini umechelewa jinsi hii?`` aliuliza kwa hasira.
‘Bwana wee,`` alisema sungura kwa sauti ya upole.
``Nilichelewa kwa sababu simba mwingine alinikimbiza. Nilitaabika sana kabla ya kupata
upenyu wa kutoroka.``
``Simba mwingine? Je, katika pori hili?`` aliuliza samba.
``Ndiyo bwana mkubwa. Najua anakoishi. Tuandamane nikakuonyeshe,`` alisema sungura.
Simba alijitayarisha kuandamana na sungura. Sungura aliongoza njia hadi walipofika mahali
palipokuwa na kisima kikubwa. Sungura alimgeukia na kusema, ``Anaishi hapa. Tafadhali
njoo umuone!``
Simba alisogea ulipokuwa ukingo wa kile kisima. Aliyatupa macho huko na kukiona kivuli
chake. Alidhani kuwa huyo alikuwa simba mwingine. Kwa hasira kubwa alifungua kinywa na
kunguruma. Alimwona huyo simba mwingine akikenulia meno. Simba hakuweza kusubiri,
alijitosa kisimani apambane na simba huyo. Huo ulikuwa mwisho wake. Sungura aliondoka
akicheka akifurahi kuwa sasa wanyama hawataliwa tena na simba.
Maswali
a) i) Andika aina ya hadithi hii (alama 1)
ii) Taja sifa tatu za kutambulisha aina hii ya hadithi (alama 3)
iii) Fafanua umuhimu wa aina hii ya hadithi kwa jamii (alama 3)
b) Kwa kutoa mifano taja aina mbili ya fomyula ya: (alama 4)
i)Kuanza hadithi
ii) Kumalizia hadithi
c) Eleza sifa nne za mtambaji bora katika fasihi simulizi (alama 4)
d) Tofautisha kati ya vipera viwili vya fasihi simulizi.
i)Mighani na maghani (alama 2)
ii) Lakabu na misimu (alama 2)

33. SWALI LA 33
a) Taja aina nne za nyimbo (alama 4)
b) Eleza umuhimu wa nyimbo katika jamii (alama 8)
c) Taja na udhibitishe sifa nne za kimtindo za methali. (alama 8)
34. SWALI LA 34
(a) Fafanua maana ya Hodiya katika jamii nyingi za kiafrika. (alama.2)
(b) Fafanua sifa zozote nne za hodiya katika jamii husika, (alama.8)
GOLDEN ELITE EDUCATIONAL CONSULTANCY P.O BOX 2345 KERICHO. FOR MARKING SCHEMES CALL OR
TEXT MR CHEPKWONY ON 072435I706 0R EMAIL kipkemoicos@gmail.com
(c) Hodiya ilikuwa na umuhimu upi katika jamii husika. (alama 10)

35. SWALI LA 35
(a) Maigizo ni nini ? (alma 2)
(b) Tofautisha aina mbili kuu za maigizo (alama 8)
(c) Eleza umuhimu wa michezo ya watoto katika jamii husika (alama 10)
36. SWALI LA 36
Soma hadithi hii kasha ujibu maswali
Ilikuwa alfajiri yenye baridi. Umande ulitapakaa kote. Ukungu ulitanda hivi kwamba
hungeweza kumuona mtu alikuwa hatua chache mbele yako. Ndovu alipoamka, alikuta fisi
mlangoni pake. Fisi alikuwa amemlimia ndovu shamba lake, lakini alikuwa hajalipwa ujira
wake.
Kila alipomwendea ndovu kwa ajili ya malipo yake, fisi alitiliwa huku na kutolewa
kule.”Leo ni leo”,fisi alimwambia ndovu.”Nimevumilia vya kutosha. Kila siku ninapokuja
kuchukua pesa zangu, hukosi hadithi mpya ya kunisimulia. Leo sitoki hapa bila pesa zangu!”
Fisi alipomaliza kumwaga joto lake, ndovu alimwambia: “Sikiliza fisi. Mimi nimeheshimika
kote kijijini. Naona haja yako ni kunivunjia heshima –mbele ya familia yangu na wanakijiji
kwa jumla. Sikulipi pesa zako, mpaka ujifunze kuwaheshimu wazee. Nakuamuru uondoke
hapa mara moja, kabla sijakasirika! Nataka uende popote, unapofikiria kwamba unaweza
kupata msaada. Ukienda kwa chifu, usisahau kwamba tunakunywa na yeye. Ukienda polisi,
mkuu wa kituo amejaa tele mfukoni mwangu. Ukienda mahakamani, hakimu tulisoma darasa
moja. Popote uendapo, hakuna yeyote atakayekusikiliza”
“Zaidi ya hayo, hakuna yeyote atakayekuamini.Mimi naitwa Bwana pesa.Kwangu umeota
mpesapesa na kustawi. Nani ataamini kwamba naweza kushindwa kulipa vijisenti vichache
ninavyodaiwa na fisi?”
Fisi alisikiliza kwa makini majitapo ya ndovu. Aliamua kumpasulia ndovu mbarika: “Bwana
ndovu najua kuwa wewe una nguvu na uwezo mkubwa wa kifedha.Lakini hayo yote mimi
hayanihusu ni yako na familia yako. Sitakuruhusu unidhulumu kilicho haki yangu.
Usiutumie uwezo uliopewa na Muumba kuwaonea na kuwanyanyasa maskini wasio mbele
wala nyuma” alimaliza usemi wake na kuondoka huku machozi yakimdondoka.
Fisi alipofika nyumbani, aliwasimulia fisi wanyonge wenzake yaliyomsiba.Fisi
walikusanyika na kulizingira boma la ndovu huku wakisema: “Tunataka haki itekelezwe!
Dhuluma lazima ikome! Unyanyasaji lazima ukome!” Ndovu aliposikia kelele langoni
mwake, alipiga simu kwenye kituo cha polisi.
Mara, kikosi cha polisi wa kupambana na ghasi kiliwasili. Fisi walipigwa mijeledi na
kuezekwa marungu. Waliojifanya mabingwa walipigwa risasi. Fisi waliosalia walikimbilia
makwao, huku wakichechemea kwa maumivu. Mpaka wa leo fisi wangali wanatembea kwa
kuchechemea.
(a) Usimulizi huu ni wa aina gani? Toa sababu. (alama 2)
(b) Eleza tamathali za usemi zilizotumika katika hadithi hii. (alama 4)

GOLDEN ELITE EDUCATIONAL CONSULTANCY P.O BOX 2345 KERICHO. FOR MARKING SCHEMES CALL OR
TEXT MR CHEPKWONY ON 072435I706 0R EMAIL kipkemoicos@gmail.com
(c) Eleza sifa za ndovu katika hadith hii. (alama 5)

(d) Fafanua jinsi kisa hiki kinavyo dhihirisha methali: ‘Mwenye nguvu mpishe(alama3)
(e) Je, hadithi zina umuhimu gani katika jamii? (alama 6)

37. SWALI LA 37
(a) Eleza dhima nne za hojaji katika utafiti wa fasihi simulizi. (alama4)
(b) Fafanua vizisingizi vyovyote vinane katika ukusanyaji wa fasihi simulizi. (alama16)
38. SWALI LA 38
Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali yanayofuata
Nimekuita hapa kwa sababu moja
Unaelewa kile ulichofanya!
Nimekupa muda wa kutosha kujiasa na kutambua
Haja ya kuomba msamaha lakini umepuuza!
Kama kweli wewe ni mwanafunzi wangu!
Nimekufunza maarifa, maadili na hata haja ya kufanya bidii masomoni.
Mara kadha nimekusaidia kihali na kifedha
Nimekutafutia wafadhili wa masomo yako
Sasa umesahau hayo yote!
Umeanza kunivunjia heshima.
Unanyemelea vitu vyangu na kuiba,
Ninapokuuliza unagombana nami kama mtoto wa rika yako!
Kule nje walichafua jina langu ukisema ati mimi ni mchawi.
Miungu nawaone chozi langu,
Wasikie kilio changu.
Mizimu na waone uchungu wangu
Radhi Baraka wala fanaka yoyote wasikupe
Usiwahi kufurahia hata siku moja masomo yako.
Na iwapo utakuwa mwalimu, wanafunzi wako wakutendee mabaya Zaidi!
MASWALI
(a) Tambulisha kipera hiki cha fasihi simulizi ( alama 2)
(b) Eleza sifa zozote tano za kipera hiki cha fasihi simulizi ( alama 10)
(c) Mbali na muktadha uliorejelewa taja kwa kutolea mifano miktadha mingine minne
ambamo kipera hiki huhusishwa ( alama 4)
(d) Taja umuhimu wa kipera hiki katika jamii ( alama 4)

39. SWALI LA 39
“ Ukichukua mama chukua na mtoto”
(a) Tambilisha kipera cha fasihi simulizi (alama 2)
(b) Fafanua sifa zozote tano za kipera hiki (alama 10)
(c) Eleza mambo yoyote manne yanayozingatiwa wakati wa kuainisha misimu (alama 8)
40. SWALI LA 40
(a) Taja aina nne za ngomezi za kisasa. (alama 2)
GOLDEN ELITE EDUCATIONAL CONSULTANCY P.O BOX 2345 KERICHO. FOR MARKING SCHEMES CALL OR
TEXT MR CHEPKWONY ON 072435I706 0R EMAIL kipkemoicos@gmail.com
(b) Eleza sifa nne za maapizo. (alama 2)
(c) Eleza kikwazo vitatu vinavyokumba Fasihi simulizi. (alama 3)
(d) (i) Ni nini maana ya vivugo (alama 1)
(ii)Eleza sifa zinazotambulisha vivugo (alama 4)
(iii) Fafanua majukumu ya vivugo (alama 8)
MTIHANI 7
Ushairi
1. SHAIRI ‘A’.
Umekata mti mtima
Umeangukia nyumba yako
Umeziba mto hasira
Nyumba yako sasa mafurikoni
Na utahama
Watoto Wakukimbia

Mbuzi kumkaribia chui


Alijigeuza Panya
Akalia kulikuwa na pala
Kichwani
Mchawi kutaka sana kutisha
Alijigeuza Simba
Akalia na risasi kichwani

Jongoo kutaka sana kukimbia


Aliomba miguu elfu
Akaachwa na nyoka

Hadija wapi sasa yatakwenda


Bwanako kumpa sumu ?
Hadija umeshika nyoka kwa mkia
Hadija umepitia nyuma ya punda

SHAIRI ‘B’
Piteni jamani, Piteni haraka
Nendeni, nendeni huko mwendako
Mimi haraka, haraka sina
Mzigo wangu, mzigo mzito mno
Na chini sitaki kuweka

Vijana kwa nini hampiti ?


Kwa nini mwanicheka kisogo ?
Mzigo niliobeba haupo.

Lakini umenipinda ngongo na


GOLDEN ELITE EDUCATIONAL CONSULTANCY P.O BOX 2345 KERICHO. FOR MARKING SCHEMES CALL OR
TEXT MR CHEPKWONY ON 072435I706 0R EMAIL kipkemoicos@gmail.com
Nendako
Haya piteni ! Piteni haraka ! Heei !

Mwafikiri mwaniacha nyuma !


Njia ya maisha ni moja tu.
Huko mwendako ndiko nilikotoka
Na nilipofikia wengi wenu
Hawatafika.

Kula nimekula na sasa mwasema


Niko nyuma ya wakati
Lakini kama mungepita mbele
Na uso wangu kutazama
Ningewambia siti miaka
Mingi.

(a) Haya ni mashairi ya aina gani ? Toa saabu


(b) Washairi hawa wawili wanalalamika. Yafafanue malalamishi yao
(c) Onyesha jinsi kinaya kinavyojitokeza katika tungo hizi mbili
(d) Ni vipi Hadija :-
(i) Amekata mti mtima ?
(ii) Amepita nyuma ya Punda
(al.2)
(e) Toa mifano 2 ya uhuru wa mashairi kwa kurejelea mashairi haya
(f) Kwa kurejelea shairi ‘B’ eleza maana ya:-
(i) Mzigo
(ii) Siri
(iii) Kula nimekula
(iv) Niko nyuma ya wakati

2. Sinisumbuwe akili, nakusihi e mwandani.


Afya yangu dhahili, mno nataka amani
Nawe umenikabili, nenende sipitalini
Sisi tokea azali, twende zetu mizumuni
Nifwateni sipitali, na dawa ziko nyumbani?

Mababu hawakujali, wajihisipo tabani


Tuna dawa za asili, hupati sipitalini
Kwa nguvu za kirijali, Mkuyati uamini
Kaafuri pia kali, dawa ya ndwele fulani
Nifuateni sipitali, na dawa ziko nyumbani?

Mtu akiwa hali, tumbo lina walakini,


Dawa yake ni subili, au zongo huanoni
Zabadili pia sahali, kwa maradhi yalo ndani
GOLDEN ELITE EDUCATIONAL CONSULTANCY P.O BOX 2345 KERICHO. FOR MARKING SCHEMES CALL OR
TEXT MR CHEPKWONY ON 072435I706 0R EMAIL kipkemoicos@gmail.com
Au kwenda wasaili, wenyewe walo pangani
Nifwateni sipitali, na dawa ziko nyumbani?

Mtu kwenda sipitali, ni kutojuwa yakini


Daktari k’ona mwili, tanena kensa tumboni
Visu visitiwe makali, tayari kwa pirisheni
Ukatwe kama fagili, tumbo nyangwe na maini
Nifuateni sipitalini, na dawa ziko nyumbani?

Japo maradhi dhalili, kutenguliwa tegoni


Yakifika sipitali, huwa hayana kifani
Wambiwa damu kaliti, ndugu msaidieni
Watu wakitaamali, kumbe ndiyo bunani
Nifwateni sipitali, na dawa ziko nyumbani?

Mizimu wakupa kweli, Wakueleze undani.


Maradhiyo ni ajali, yataka vitu thamani
Utete huku wawili, wa manjano na kijani
Matunda pia asali, vitu vyae shamoni
Nifuateni sipati, na dawa zi langoni?

Maswali
(a) Lipe shairi hili kichwa mwafaka

(b) Mtunzi alikuwa na lengo gani alipotunga shairi hili

(c) Mbona mshairi hataki kwenda hospitalini

(d) Eleza umbo la shairi hili


(al. 6
(e) Kwa nini mshairi alitumia ritifaa katika ushairi ?

(f) Andika maana ya maneno haya kama yalivyotumiwa kwenye shairi :-


(i) Dhalili
–.............................................................................................................................
(ii) Azali
-...............................................................................................................................
(iii) Sahali -..........................................................................................................................

(iv) Tumbo nyanywe


.............................................................................................................

3. WAFULA KABILIANA NA KISU


Ee mpwa wangu,
Kwetu hakuna muoga,
Uoga ukikufikia, huenda ni wa akina mamayo,
GOLDEN ELITE EDUCATIONAL CONSULTANCY P.O BOX 2345 KERICHO. FOR MARKING SCHEMES CALL OR
TEXT MR CHEPKWONY ON 072435I706 0R EMAIL kipkemoicos@gmail.com
Fahali tulichinja ili uwe mwanamme,
Eewe mpwa wangu, kisu kikali ajabu !
Iwapo utatingiza kichwa,
Uhamie kwa wasiotahiri.

Wanaume wa mbari yetu,


Si waoga wa kisu,
Wao hukatwa kuanzia macheo hadi machweo,
Wewe ndiye wa kwanza,
Iwapo utashindwa,
Wasichana wote,
Watakucheka,
Ubaki msununu,
Simama jiwe liwe juu,
Ndege zote ziangamie.

Simu nimeipokea,
Ngariba alilala jikoni,

Visu ametia makali,


Wewe ndiye wangojewa,
Hadharani utasimama,
Macho yote yawe kwako,
Iwapo haustahimili kisu,
Jiuzulu sasa mpwa wangu,
Hakika sasa mpwa wangu,
Hakika tutakusamehe, mwaka kesho unakuja.

Asubuhi ndio hii,


Mama mtoto aamushwe,
Upweke ni uvundo,
Iwapo utatikisa kichwa,
Iwapo wewe ni mme,
Kabiliana na kisu kikali,
Hakika ni kikali!

Kweli ni kikali!
Wengi wasema ni kikali!
Fika huko uone ukali!
Mbuzi utapata,
Na hata shamba la mahindi,
Simama imara,
Usiende kwa wasiotahiri
Maswali
(a) Hili ni shairi la aina gani ? Thibitisha
(b) Ni nani anayeimba shairi hili na analiimba kwa nani ?
GOLDEN ELITE EDUCATIONAL CONSULTANCY P.O BOX 2345 KERICHO. FOR MARKING SCHEMES CALL OR
TEXT MR CHEPKWONY ON 072435I706 0R EMAIL kipkemoicos@gmail.com
(c) Toa ithibati kwenye shairi hili kuthibitisha kuwa msimulizi ana taasubi za kiume
(d) Taja kwa kutolea mifano mbinu zozote nne za uandishi katika shairi hili
(e) Taja shughuli zozote mbili za kiuchumi za jamii inayorejelewa katika shairi hili
(f) Eleza kwa mifano, uhuru wa kishairi katika shairi hili
(g) Msamiati ufuatao umetumika kwa maana gani katika shairi hili ?
(i) Mbari
(ii) Msununu
(iii) Ngariba
(iv) Uvundo

4. HATIMA YANGU

1. Mke wangu wameshanipoka


Ndugu zangu, wamedai ububu
Wazazi kuzoea kunigombeza

2. Juzi mali lilimbikiza


Furaha lilitanda
Makanwa yalijaziwa
Hoi hoi ikawa desturi

3. Kilabu tulikwenda
Nyama tulichoma
Mahali tulizuru
Tuliteremsha!

4. Leo mambo yamenigeuka


Wao masahibu siwaoni
Matumbo yakaninguruma
Kama radi ya mvua

5. Nyumbani nimebaki pweke


Mke amenitoroka
Watoto wameparara
Skuli kugharamia
Imegeuka balaa belua

6. Ndipo nimeamua
Afadhali kitanzi badala ya balaa
Kumbe kupanga ndiyo maana
Maisha na waasia

(a) Eleza mambo muhimu yanayoelezwa katika shairi hili

GOLDEN ELITE EDUCATIONAL CONSULTANCY P.O BOX 2345 KERICHO. FOR MARKING SCHEMES CALL OR
TEXT MR CHEPKWONY ON 072435I706 0R EMAIL kipkemoicos@gmail.com
(b) Fafanua sifa mbili za anayezungumza katika shairi

(c) Dondoa na ufafanue mbinu zozote mbili za lugha katika shairi hili

(d) Eleza maana ya:-


(i) Ndugu zangu wamedai ububu

(ii) Kumbe kupanga ndiyo maana

5. 1. Nitampa nani, sauti yangu ya dhati


Kwa kipimo gani, ingawa kiwakatiti
Amefanya nini, la kutetea umati
Kipimo ni kipi?

2. Yupi wa maani, asosita katikati


Alo na maoni, yasojua gatigati
Atazame chini, kwa kile ule wakati
Kipimo ni kipi?
3. Alo mzalendo, atambuaye shuruti
Asiye mafundo, asojua mangiriti
Anoshika pendo, hata katika mauti
Kipimo ni kipi?

4. Kipimo ni kipi, changu mimi kudhibiti


Utu uko wapi, ni wapi unapoketi
Nje kwa mkwapi, au ndani kwa buheti
Kipimo ni kipi?

Maswali
a) Eleza umbo la shairi hili
b) Taja na ueleze jinsi mwandishi alivyotumia uhuru wa ushairi
c) Eleza ujumbe unaowasilishwa na mshairi
d) Andika ubeti wa tatu katika lugha ya nathari
e) Taja bahari tatu zinazojitokeza katika shairi na utoe sababu
f) Eleza msamiati ufuatao kama ulivyotumika katika shairi hili
i) Katiti
ii) Gatigati
iii) Mangiriti

6. KIPI NIKITENDE?
. Tayari ni sarakani, niambie yote johara,
Mosi nimpe shukrani, kanizaa bira zira,
Wapo haiko hisani, ningefaa kwa uparara,
Kipi takachokitenda, ni nene heko kwa mama?
GOLDEN ELITE EDUCATIONAL CONSULTANCY P.O BOX 2345 KERICHO. FOR MARKING SCHEMES CALL OR
TEXT MR CHEPKWONY ON 072435I706 0R EMAIL kipkemoicos@gmail.com
. Miezi tisa tumboni, yote nina kajinyima,
Kanikopa uchunguni, safari ndefu kazima’
Kama kinda kiotani, kiniasa huyu mama’
Kipi takachokitenda, ninene heko mama ?

. Baba siku jana madadi, kawa vingaito mambo,


Kaolewa na asadi, kachalazwa kwa wimbombo,
Kaona – bali jadili, kuchao puani bombo,
Kipi takachokitenda, ninene heko mama?

. Kila kuchao zarani, kupalilia kondeni,


Kachanika mpinini, chungu povuka motoni,
Kaviyariya fingani, kinijali jikoni,
Kipi tukachokitenda , ninene heko mama?

. Wa siku hizi vijana, wakahujuru nyumbani,


Wengine wao jagina, kawa lofa mutaani,
Hali ukashiba nina, afikapo tu, “kongoni!”
Kipi takachokitenda, ninene heko mama?
. Nawe bwana siwe maya, vita hasha kiwa kombo,
Tena simfanye yaya, ya kikoa ndio mambo,
Simtende ya hizaya, siwe mwao kila jambo,
Kipi takachokitenda, ninene heko mama?

. Sasa jamvi nakuja, kisa nimesakarika,


Naomba niliyotaja, tatia manani kaka,
Nenayo yasiwe ngoja, ili nipokee baraka,
Mema nitamtendea, apate futahi pia.

Maswali
(a) Eleza umbo la shairi hili

(b) Kwa nini msanii amshukuru mamaye ?

(c) Ni kina nani wanaokashifiwa na msanii ? Kwa nini ?

(d) Onyesha tofauti katika ujumbe iliyoko katika beti nne za kwanza na mbili zinazofuata

(e) Toa majina mengine yenye maana sawa na haya yaliyotumiwa katika shairi hili :
(i) Mama
(ii) Dawati
(iii) Imara/thabiti
(f) Eleza maana ya maneno haya kama yalivyotumika kaika shairi:

(i) Kawa vangaito mambo


GOLDEN ELITE EDUCATIONAL CONSULTANCY P.O BOX 2345 KERICHO. FOR MARKING SCHEMES CALL OR
TEXT MR CHEPKWONY ON 072435I706 0R EMAIL kipkemoicos@gmail.com
(ii) Wimbombo
(iii) Kongoni

7. Soma shairi hili kisha ujibu maswali yanayofuata


MWANAMKE
1. Namwona yu shambani,
Na jembe mkononi,
Analima,
Mwanamama,
Mavuno si yake,
Ni ya mume wake.

2. Namwona viwandani,
Pia maofisini,
Yu kazini,
Hamkani,
Anabaguliwa,
Na anaonewa.

3. Namwona yu nyumbnai,
Mpishi wa jikoni,
Yaya yeye,
Dobi yeye,
Hakuna malipo,
Likizo haipo.

4. Namwona kitandani,
Yu uchi maungoni.
Ni mrembo
Kama chombo,
Chenye ushawishi,
Mzima utashi.

5. Namwona mkekani,
Yuwamo uzazini,
Apumua,
Augua,
Kilio cha kite,
Cha mpiga pute.

6. Kwa nini mwanamke,


Ni yeye peke yake,
Heshimaye,
Haki anakosa,
Kwa kweli ni kosa
GOLDEN ELITE EDUCATIONAL CONSULTANCY P.O BOX 2345 KERICHO. FOR MARKING SCHEMES CALL OR
TEXT MR CHEPKWONY ON 072435I706 0R EMAIL kipkemoicos@gmail.com
(Muhammed Seif Khatib)

7. (a) “Shairi hili ni la kukatisha tamaa”. Fafanua dai hili kwa kutoa mifano minne
(b) Eleza umbo la shairi hili
(c) Andika ubeti wa tatu katika lugha ya nathari
(d) Taja tamathali ya usemi iliyotawala katika shairi zima utoe mifano miwili ya jinsi
ilivyotumika
(e) Onyesha mifano miwili ya ubabadume inayojitokeza katika shairi hili
(f) Eleza maana ya maneno yafuatayo jinsi yalivyotumiwa katika shairi:
(i) mzima utashi
(ii) maungoni

8. KIACHE KINACHONG’AA
Katu siwe na harara, wala moyo kukupapa,
Usichukue hasira, na moyo kutapa-tapa,
Utaharibu na sura, mwishowe uende kapa,
Kiache kinachokwepa, mbeleye kina madhara

Mbeleye kina madhara, kile kinachokukukwepa,


Mbele yake ni hasara, si chema kitakutupa,
Hutaipata ijara, kuchuma ama kukopa,
Kiache kinachokwepa, mbeleye kina madhara

Hicho jangwa la Sahara, si mnofu ni mfupa,


Hakina njema ishara, humtupa mwenye pupa,
Kibovu kama tambara, hupasuka kama chupa,
Kiache kinachokwepa, mbeleye kina madhara

Kitaleta ufukura, si huko wala si hapa,


Kina mengi mazingira, na mbele kitakuchapa,
Sijitie usogora, ukavimbisha mishipa,
Kiache kinachokwepa, mbeleye kina madhara

Si kazi yenye ujira, mshahara kukulipa,


Ya cheo chenye kinara, na heshima wakikupa,
Mbele haina imara, japo leo wajitapa,
Kiache kinachokwepa, mbeleye kina madhara

Japo kazi ya biashara, kutwa wauza makopa,


Uwe mtu na kipara, Mwananchi ama Yuripa,
Bora uwe na busara, fedha tajaza mapipa,
Kiache kinachokwepa, mbeleye kina madhara
Usione kinang’ara, huku chapiga marapa,
Ukimbilie kupora, moyo wako kukuzipa,
Kitakugeuza chura, mbele yake utaapa,
GOLDEN ELITE EDUCATIONAL CONSULTANCY P.O BOX 2345 KERICHO. FOR MARKING SCHEMES CALL OR
TEXT MR CHEPKWONY ON 072435I706 0R EMAIL kipkemoicos@gmail.com
Kiache kinachokwepa, mbeleye kina madhara

Usitupe sarara, nyuma kisogo kuipa,


Ukaenda kwa papara, kiumbe mbele kitanepa,
Kwanza tumia fikira, uchague njema chapa,
Kiache kinachokwepa, mbeleye kina madhara

Na sisemi masihara, hakika kweli nawapa


Mlio pwani na bara, wa Mufindi na wa lupa
Maneno haya kitara, muarifu na Wachepa,
Kiache kinachokwepa, mbeleye kina madhara

Tamati niliyochora, ya shikeni si kuepa


Kisha muwe na basira, na Mola kumuogopa,
Kinachokwepa si nyara, ufunge ndani ya kwapa,
Kiache kinachokwepa, mbeleye kina madhara

(a) Eleza hii ni bahari gani ya shairi


(b) Eleza dhamira ya mshairi
(c) Fafanua hasara nne zinazoletwa na tamaa - vile ving’aavyo

(d) Taja na ueleze mbinu mbili za kifasihi zilizotumika katika shairi

(e) Andika ubeti wa tano katika lugha ya nathari

(f) Eleza maana ya maneno haya kama yalivyotumika katika shairi


(i) Kuchuma
(ii) Kisogo kuipa

9. Alipokwenda kwao, mamaye alimwambia,


Nipa fedha au nguo, nataka kwenda tumia!
Nikosapo hivi leo, nipa kisu tajitia ! 
Huzunguka akilia kwa maana ya uketo

Ndipo mamaye kawaza, pamwe na kuzingatia,


Fedha zako umesoza, na leo zimekwisha,
Kisu sikukukataza, twaa upate jitia!
Mbele zangu n’ondokea! Wende na ukiwa wako!

Ulipogeuka nondo, nguo ukazingilia,


Kakaka kwa vishindo, usisaze hata moya,
Leo wanuka uvundo, wambeja wakukimbia!
Mbele zangu n’ondokea ! Wende na ukiwa wako!
Ukijigeuza nyama, kama Simba ukilia,
Watumwa ukawaegema, ukawla wote pia,
GOLDEN ELITE EDUCATIONAL CONSULTANCY P.O BOX 2345 KERICHO. FOR MARKING SCHEMES CALL OR
TEXT MR CHEPKWONY ON 072435I706 0R EMAIL kipkemoicos@gmail.com
Pasi kuona huruma, kutoa wahurumia,
Mbona hukuzingatia? Wende na ukiwa wako!

Si mimi naliokupa, ukata huo, sikia!


Kwamba utakuja hapa, nipate kuondolea,
Naapa thama, naapa, sina la kukutendea!
Mbele zangu n’ondokea! Wende na ukiwa wako!

Tamati, nalikomile, ni hayo nalokwambia,


Hapahitaji kelele na kujirisha mabaya,
Na kwamba yakutukie, sema yapate n’elea!
Zidi radhi kuniwea ! Wende na ukiwa wako!

Maswali
(a) Lipe shairi hili anwani mwafaka
(b) Ni maudhui gani yanayojitokeza katika shairi hili

(c) Taja na ueleze tabia za mnenewa katika shairi hili

(d) Mshairi ametumia uhuru wa utunzi. Taja sehemu mbili alikotumia uhuru huo
(e) Eleza umbo la shairi hili
(f) Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumiwa katika shairi :-
(i) Uketo
(ii) Ukata

10 . Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali


Msituni nikakuta, nyuki wamo mzingani,
Kwa juhudi wanakita, mara nje mara ndani,
Husuda wameikata, hata hawasengenyani,
Nyuki ni wadudu duni, wanashinda kwa umoja

Mchwa nao nikaona, wamejenga masikani,


Wafanya bidii sana, uvivu hawatamani,
Wao husaidiana, tena hawadanganyani,
Mchwa wadudu wa chini, wanaishi kwa umoja

Nalo jeshi la siafu, hutandawaa njiani,


Laenda bila ya hofu, maana ajiamini,
Silaha zao dhaifu, meno, tena hawaoni
Wa kuwatadia nini ? Kwani wanao umoja.

Nao chungu wachukuzi, nyama warima njiani,


Masikini wapagazi, mizigo yao kichwani,
Ingawa si wachokozi, wakali ukiwahini,
GOLDEN ELITE EDUCATIONAL CONSULTANCY P.O BOX 2345 KERICHO. FOR MARKING SCHEMES CALL OR
TEXT MR CHEPKWONY ON 072435I706 0R EMAIL kipkemoicos@gmail.com
Katu hawafarakani, wanadamu kwa umoja.

Sisi ni wana Adamu, mbona hatusikizani,


Tusitietie hamu, ukubwa kuutamani,
Wachache wataalamu, tuwasadi kwa imani,
Hii “Huyu awezani,” yatuvunjia umoja

Maswali
(a) Lipe shairi hili anwani mwafaka.

(b) Ni sifa zipi nne zinazopewa wanaozungumza.

(c) Onyesha jinsi mwandishi alivyotumia uhuru wake katika shairi hili.

(d) Eleza muundo wa shairi hili.

(e) Andika ubeti wa mwisho kwa lugha nathari.

(f) Taja mafunzo mawili unayopata kutokana na wahusika wanaozungumziwa.

(g) Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumiwa katika shairi hilo.

(i) Chungu
(ii) Tuwasadi

11. Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.

Twamshukuru Mwenyezi. Kamwe wingi ukarimu


Alo na kiti cha enzi, Mola wetu akramu
Kutupa kitu azizi , lugha kutakalamu
Lugha ni kitu kitamu, ujuwapo kutumia

Lugha mkuu mlezi , aleaye binadamu


Hata wanyama ja mbuzi, wema lugha wafahamu
Hafuguwa simulizi, izaayo tabasamu
Lugha huwa ni imamu, ujuwapo kutumia

(3) Lugha hodari mkwezi, akweaye tata ngumu


Huzifyeka pingamizi, zizushazo uhasama
Ikazidisha mapenzi, wapendanao kudumu
Lugha huyeyusha sumu, ujuwapo kutumia

(4) Lugha ndiye mpagazi, mazito kuyahudumu


Pia hupanga vizazi, pasi mbari kudhulumu

GOLDEN ELITE EDUCATIONAL CONSULTANCY P.O BOX 2345 KERICHO. FOR MARKING SCHEMES CALL OR
TEXT MR CHEPKWONY ON 072435I706 0R EMAIL kipkemoicos@gmail.com
Aidha hufanya kazi, ikawa mustakumu
Lugha kwayo ni timamu, ujuwapo kutumia

(5) Lugha ni mpelelezi, maovu kuwakasimu


Huwatowa palo wazi, kashuhudia kaumu
Yasifiwa na wajuzi, kuwa ni kitu adhimu
Lugha mkuu hakimu, ujuwapo kutumia

(6) Lugha huizuwa kazi, kutatiza mahakimu


Huwaacha kanwa wazi, wakili kitakalamu
Muhalifu na jambazi, wakaishinda hukumu
Urongo huwa timamu, ujuwapo kutumia

(7) Lugha iwe ni kiongozi, Kizungu au Kiamu


Iwekapo waziwazi, silabi na tarakimu
Huyakimu maongezi,yakasikizwa kwa hamu
Lugha huwa ni muhimu, ujuwapo kutumia.

(8) Lugha ni mapinduzi, wanyonge na wajukumu


Kadhalika ni jahazi, ya nahodha muhitimu
Kufa maji haiwezi, si vina si miizamu
Lugha maji zam-zamu, ujuwapo kutumia

Maswali.
(a) Eleza maudhui ya shairi hili

(b) Eleza muundo wa shairi hili

(c) Andika ubeti wa nne katika lugha ya nadhari/ nadharia

(d) Taja huku ukitoa mifano, mbinu tatu za lugha alizotumia mshairi kuwasilisha ujumbe

(e) Eleza maana ya msamiati kama ulivyotumika


(i) Azizi

(ii) Uhasimu

(iii) Adimu.

12. Soma mashairi yafuatayo kisha ujibu maswali :-


SHAIRI A:
Tunda la elimu zote, wasema wanazuoni,
GOLDEN ELITE EDUCATIONAL CONSULTANCY P.O BOX 2345 KERICHO. FOR MARKING SCHEMES CALL OR
TEXT MR CHEPKWONY ON 072435I706 0R EMAIL kipkemoicos@gmail.com
Ni kwamba mtu apate, kumtambua manani.
Ndipo hadhi aipate, akumbukwe duniani.

Elimu bila ukweli, haizidi asilani


Giza na nuru muhali, katu havitengamani,
Uwongo uje kwa ukweli, itue nuru moyoni.

Elimu ni kama mali, haichoshi kutamani,


Ni bora yashinda mali, taji la wanazuoni,
Elimu njema miali, iangazayo gizani.

Mtu hachomwi na mwiba, na viatu mguuni,


Ulimwengu una miiba, tele tele majiani,
Elimu ukiishiba, U salama duniani.

Wafu ni wasiosoma, watazikwa ardhini,


Hai ndio waulama, wapaao maangani,
Elimu jambo adhima, aso nayo maskini

Elimu ina malipo, utayalipwa mwishoni


Pale uitafutapo, ujira usitamani
Mwanachuoni afapo, mbingu huwa na huzuni.

Haki ya kuheshimiwa, ni yao wanachuoni,


Wao wameongolewa, na ni taa duniani.
Kweli wanapojua, watoe bila kuhini.

Elimu bila amali, mti usio majani,


Haumtii kivuli, aukaliaye chini,
Inakuwa mushkeli, wa kushuri insani,

SHAIRI B
Inakera moyo
Hii anga ambayo
Huwasonya njiani
Watokao mashambani
Wa kusalimu kwa bashasha
Wanaoshinda kivulini.

Chini ya mwembe
Wa umma.

Inakera moyo
Hii sebule ambayo
Huwahini mezani
GOLDEN ELITE EDUCATIONAL CONSULTANCY P.O BOX 2345 KERICHO. FOR MARKING SCHEMES CALL OR
TEXT MR CHEPKWONY ON 072435I706 0R EMAIL kipkemoicos@gmail.com
Wagotao nyundo kutwa
Wa kukabili chakula
Wanastarehe daima

Chini ya paa
La umma.
Maswali
(a) Pendekeza kichwa kifaacho kwa kila shairi la A na B

(b) Haya mashairi ni ya aina gani?

(c) Taja sifa zozote tatu za kishairi katika shairi B

(d) Taja mbinu ya lugha iliyotumiwa :-


(i) Katika mshororo wa mwisho wa ubeti wa saba katika shairi la A

(ii) Katika ubeti wa nne wa shairi la B

(e) Fafanua kwa mukhtasari maudhui ya mashairi yote mawili

(f) Andika ubeti wa mwisho wa shairi la A katika lugha nathari

(g) Taja na uonyeshe jinsi idhini ya ushairi ilivyotumika katika shairi la A

(h) Fafanua maana ya maneno haya kama yalivyotumika katika shairi:-

(i) Maulama
(ii) Wameongolewa
(iii) Wagotao
(iv) Huwahini

13. Soma shairi na kisha uyajibu maswali yafuatayo:-


CHEMA HAKIDUMU
Chema hakidumu, kingapendekeza,
Saa ikitimu, kitakuteleza,
Ukawa na hamu, kukingojeleza,
Huwa ni vigumu, kamwe hutaweza.

Chema sikiimbi, kwamba nakitweza,


Japo mara tumbi, kinshaniliza,
Na japo siombi, kipate n’ongeza,
Mtu haniambi, pa kujilimbikiza.

Chema mara ngapi, kinaniondoka,


Mwahanga yu wapi? Hakukaa mwaka,
GOLDEN ELITE EDUCATIONAL CONSULTANCY P.O BOX 2345 KERICHO. FOR MARKING SCHEMES CALL OR
TEXT MR CHEPKWONY ON 072435I706 0R EMAIL kipkemoicos@gmail.com
Kwa muda mfupi, aliwatilika,
Ningefanya lipi, ela kumzika?

Chema wangu babu, kibwana Bashee,


Alojipa tabu, kwamba anilee,
Na yakwe sababu, ni nitengenee,
Ilahi wahhabu, mara amtwee.

Chema wangu poni, kipenzi nyanyangu,


Hadi siku hini, Yu moyoni mwangu,
Yu moyoni ndani, hadi kufa kwangu,
Ningamtamani, hatarudi kwangu.

Maswali
(a) Eleza dhamira ya mwandishi
(b) Fafanua umbo la shairi hili
(c) Andika ubeti wa kwanza kwa lugha ya nathari

(d) Taja na kutoa mfano mmoja wa tamathali yoyote ya lugha inayojitokeza katika shairi
(e) Taja mbinu nne za uhuru wa mshairi huku ukitolea kila mbinu mfano

(f) Eleza maana ya maneno yafuatayo kulingana na vile yalivyotumika:-


(i) Nitengenee
(ii) Ningamtamani
(iii) Ikitimu

14.. Soma shairi na kisha uyajibu maswali yafuatayo:-


1. Ni sumu, sumu hatari
Unahatarisha watoto
Kwa ndoto zako zako leweshi
Za kupanda ngazi
Ndoto motomoto ambazo
Zimejenga ukuta
Baina ya watoto
Na maneno laini
Ya ulimi wa wazazi

2. Ni sumu, sumu hasiri


Unahasiri watoto
Kwa pupa yako hangaishi
Ya kuwa tajiri mtajika
Pupa pumbazi ambayo
Imezaa jangwa bahili
Badala ya chemichemi
Ya mazungumzo na maadili
Baina ya watoto na mzazi
GOLDEN ELITE EDUCATIONAL CONSULTANCY P.O BOX 2345 KERICHO. FOR MARKING SCHEMES CALL OR
TEXT MR CHEPKWONY ON 072435I706 0R EMAIL kipkemoicos@gmail.com
3. Ni sumu, sumu legezi
Unalegeza watoto
Kwa mazoea yako tenganishi
Ya daima kunywa ‘moja baridi’
Mazoea mabaya ambayo yanafunga katika klabu
Hadi saa nane usiku
Huku yakijenga kutofahamiana
Baina ya watoto na mzazi

4. Ni sumu, sumu jeruhi


Unajeruhi watoto kwa pesa,
Kwa mapenzi yako hatari
Ya kuwaliwaza watoto kwa pesa
Zinawafikisha kwenye sigara na ulevi
Na kisha kwenye madawa ya giza baridi
Barabara inayofikisha kwenye giza baridi la kaburi la asubuhi

Maswali
(a) Pendekeza kichwa kwa shairi hili

(b) Fafanua maudhui ya shairi hili

(c) Ni kwa njia gani kinachozungumziwa kinajenga ukuta?

(d) Dondoa tamathali mbili za usemi zilizotumika katika shairi na uzitolee mfano

(e) Eleza umbo la shairi hili


(f) Uandike ubeti wa nne kwa lugha nathari

(g) Eleza maana ya vifungu hivi vilivyotumika katika shairi ;

(i) Giza baridi


(ii) Yanakufunga katika klabu

MTIHANI 8
MASWALI YA ISIMUJAMII
1. “Haya basi. Beba mmoja! Beba mmoja! Dada njoo. Nafasi ni ya mmoja. Ni mbao tu. Bei ya
chini kuliko keki. Usiachwe, bei ni poa.”
a. Taja sajili inayorejelewa na maneno haya. (alama 2)
b. Fafanua sifa nane za sajili hiyo. (alama 8)
2.
a) Ukiwa mkaguzi mwalikwa katika mashindano ya Kiswahili, fafanua na kueleza mambo
yanayochangia wanafunzi kufanya makosa ya kisarufi na ya kimatamshi katika lugha
ya Kiswahili. Alama 5
b) Eleza umuhimu wa Isimu Jamii. (alama 5)
GOLDEN ELITE EDUCATIONAL CONSULTANCY P.O BOX 2345 KERICHO. FOR MARKING SCHEMES CALL OR
TEXT MR CHEPKWONY ON 072435I706 0R EMAIL kipkemoicos@gmail.com
3. a) Eleza matatizo matano yaliyokumba maenezi ya Kiswahili kabla ya uhuru nchini Kenya
(alama. 5)
b)Fafanua sifa tano za lugha inayotumiwa darasani (alama 5)
4. (a) Eleza dhana ya uwingi lugha. (alama 2)
(b)Fafanua mambo manne yanayochangia uwingi lugha katika jamii. (alama 8)
5. a)Eleza sababu tano zilizochangia katika maenezi ya Kiswahili katika Afrika Mashariki
kabla ya Uhuru. (al.5)
b)Eleza hatua tano ambazo zimesaidia kuikuzalugha ya Kiswahili baada ya Uhuru nchini
Kenya. (al. 5
6. a) Eleza istilahi zifuatazo za isimu jamii. (al.4)
(i) Lugha ya taifa.
(ii) Lugha sanifu.
(iii) Lugha rasmi.
(iv) Lahaja.
(b) Fafanua maswali sita yanayochangia kustawi kwa lugha ya Kiswahili nchini Kenya.
(al.6)
7. a)Tofautisha kati ya uwili lugha na wingi lugha. (alama 4)
b)Taja sababu sita zinazosababisha watu kubadili na kuchanganya ndimi. (alama 6)
8. a)Eleza mambo yaliyochangia katika maenezi ya Kiswahili katika Afrika Mashariki kabla ya
uhuru
(b)Eleza sifa tano za lugha rasmi.
9. (a) Eleza sababu tano zinazomfanya mtu kufanya makosa ya matamshi na sarufi katika
mazungumzo yake.(al5)
(b) Eleza sababu tano zinazowafanya vijana kupenda kutumia misimu katika mawasiliano
yao. (alama 5)
10. a)Eleza maana ya lugha ya taifa.
(alama2)
b)Eleza majukumu manne ya Kiswahili nchini Kenya kama lugha ya taifa.
(alama8)
11. Fafaua jinsi shughuli zifuatazo zitachangia kukua kwa lugha ya Kiswahili na kufaikisha
ajenda ya amani na maridhiano nchini Kenya.
i) Vyombo vya habari na mawasiliano. alama 2)
ii) Uchapishaji ( alama 2)
iii)Dini ( alama 2)
iv)Siasa ( alama 2)
v) Sanaa na maonyesho ya muziki. ( alama 2)
12.
a) Kwa nini kulikuwa na haja ya kusanifisha lugha ya Kiswahili. Toa sababu tano ala 5)
b) ……………..Sote tunajua kwamba ni kudura. Makiwa
i. Tambua sajili iliyotumika katika dondoo hili ala 1)
ii. Eleza sifa nne za sajili hiyo ala 4)
13.
MHUSIKA 1: Nidhamu , Mheshimiwa Sudi. Hili ni onyo dhidi ya tabia hiyo.
MHUSIKA II: Nisamehe Bwana………………………
MHUSIKA I: sasa ninakaribisha swali la tatu. Mheshimiwa Mambo, uliza swali lako.

GOLDEN ELITE EDUCATIONAL CONSULTANCY P.O BOX 2345 KERICHO. FOR MARKING SCHEMES CALL OR
TEXT MR CHEPKWONY ON 072435I706 0R EMAIL kipkemoicos@gmail.com
MHUSIKA III:Ninaomba kufahamishwa ni kwa nini Waziri wa Maji ameshindwa
kusambaza
huduma za maji katika kijiji cha Walalahoi.
Maswali
a) Bainisha sajili ya makala haya. (al. 2)
b) Fafanua sifa za sajili hii. (al. 8)
14. Hujambo bwana: You look familiar, have we ever met before.... Sijui nilikuona wapi?
a) Bainisha sajili ya makala haya kwa kutoa mifano mitatu kwenye makala.
alama 2)
b) Fafanua sifa nyingine nne za sajili hii ambazo zingejitokeza katika makala haya.
(Alama 4)
c) Kwa kutumia mifano mwafaka eleza kaida nne za matumizi ya lugha.
(Alama 4)
15. Soma Makala yafuatayo kisha ujibu maswali.
A: Jina?
B: Ouma James
A: Umri?
B: Miaka ishirini
A: Una shida gani
B: Ninaendesha sana. Pia kichwa chaniwanga ajabu. (Anatiririkwa na machozi)
C: Anachukua stethoskopu na kumpima) Utapata nafuu hivi karibui ukinywa dawa
nitakazokupa.
Maswali
a) Tambua rejesta inayorejelewa na Makala haya. ( al 2)
b) Fafanua vitabulishi vine vinavyohusishwa na rejesta hiyo. ( al 8)
16. (a) Eleza istilahi zifuatazo (Alama 4)
i) lugha
ii) misimu
(b) Andika sifa zozote sita za lugha utakayotumia kuwatangazia watu kinyang’anyiro cha
soka. (Alama 6)
17. “….watu wa kaunti ya makueni wamesahaulika kabisa. Ningependa kuelezwa kinagaubaga
kama hawa ni wakaenya au la. Order! Order! Mheshimiwa Tata.
La! Tumekuwa marginalized kwa muda mrefu sana……
(i) Hii ni sajili gani?
(Alama 2)
(ii) Eleza sifa nne za sajili iliyotajwa.
(Alama8)

18.
a) Taja na ufafanue nadharia tatu zinazoelezea asili ya lugha ya Kiswahili
(alama 6)

GOLDEN ELITE EDUCATIONAL CONSULTANCY P.O BOX 2345 KERICHO. FOR MARKING SCHEMES CALL OR
TEXT MR CHEPKWONY ON 072435I706 0R EMAIL kipkemoicos@gmail.com
b) Eleza maana ya istilahi zifuatazo za isimujamii
(i) Lafudhi
(Alama 2)
(ii) Rejesta (Alama 2)
19. Eleza sifa zozote tano za lugha ya siasa (alama 10)
20.
a) Eleza maana ya sajili. (alama 2)
b) Fafanua umuhimu wa sajili katika jamii. (alama 10)
21. Soma dondoo lifuatalo kisha ujibu maswali yanayofuata.
Mwatani: Rusha hiyo ball haraka tumechelewa five minutes. Twende daro.
Omoshi: Harakisha mode anacome.
Bwana Kipiti: Nendeni darasani haraka! Kisha kiranja awape vitabu vyenu vya insha ili
mwandike barua.
Mwatani: Sawa mwalimu. Samahani kwa kuchelewa uwanjani.
Omoshi: Je, tutaandika barua rasmi au barua ya kawaida?
Bwana Kipiti: Mwandike barua rasmi. Je, mnakumbuka muundo wake?
Omoshi na Mwatani: Ndio mwalimu. Ulitufundisha jana. Asante sana mwalimu.
Bwana Kipiti: Kumbukeni idadi ya maneno. Idadi ya maneno ni muhimu katika uandishi
wa insha.
Maswali
a) Eleza sajili katika dondoo. (alama 2)
b) (Eleza sifa nane za sajili hii zinazopatikana katika dondoo. (alama 8)
22. i) Eleza maana ya lakabu. (alama
1)
(ii) Eleza dhima ya lakabu katika jamii.
(alama 4)
23 a) Eleza mitazamo mine kuhusu chimbuko la Kiswahili. (alama 4
b)Eleza njia za uundaji wa maneno katika lugha ya Kiswahili. (alama 6)
24. (a) Ali: Wee kuja hapa. Wewe ni nani? Sema haraka!
25. Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali yanayofuata.
“Ndugu na madada, sote tumealikwa katika karamu hii ya Bwana kabla ya kujongea mezani
pake, Bwana. Pana haja ya kutakasa nyoyo zetu na kujutia madhambi yetu. Sisi sote ni
watenda dhambi na inastahili kumwendea ili aweze kutuondolea madhambi yetu.”
Maswali
(i) Weka maneno haya katika sajili yake. (alama 2)
(ii) Nini kimekufanya uchague sajili uliochagua katika swali (i). (alama 1)
(iii) Eleza sifa za matumizi lugha katika sajili hii. (alama 7)
26. a) Eleza nadharia tatu kuhusu chimbuko la Kiswahili. alama6)
b) Fafanua istilahi zifuatazo: (alama 4)
i. UwiliLugha
ii. LinguaFranka
iii. Misimu
iv. Sajili
27. (a) (i) Eleza maana ya krioli. (alama 2)
(ii) Eleza sifa zozote tatu za krioli. (alama 3)

GOLDEN ELITE EDUCATIONAL CONSULTANCY P.O BOX 2345 KERICHO. FOR MARKING SCHEMES CALL OR
TEXT MR CHEPKWONY ON 072435I706 0R EMAIL kipkemoicos@gmail.com
(b) (i) Eleza maana ya Lingua Franka (alama 2)
(ii) Tambua sifa zozote tatu za Lingua Franka (alama 3)
28.
a) Eleza majukumu matatu ya lugha ya taifa. (alama 3)
b) Fafanua mtindo wa lugha uliotumiwa katika taarifa ifuatayo huku ukieleza sababu za
matumizi ya vitambulisho maalum vya lugha. (alama 4)
Wananchi, mimi sina mengi. Hapana katika nyinyi asiyenielewa. Sina la kusema, ila
ninawakumbusheni kuwa mnahitaji kiongozi atakayeshughulikia maslahi ya taifa zima.
Mtu huyo ni mimi na ninajitahidi niwezavyo kujenga masoko, barabara, shule zaidi na
mazahanati na maisha yenu yatakuwa ya raha zaidi.
c) Thibtisha kuwa adabu za lugha hazizingatiwi miongoni mwa wanajamii siku hizi. (alama
3)
29. a) Eleza sababu zozote sita zinazochangia kufa kwa lugha. (alama 6)
b) Taja mambo yoyote manne yanayofanywa na serikali yetu kuimarisha lugha ya Kiswahili
(alama4)
31. Eleza makosa matano yanayoweza kutokea wakati wa mazungumzo. (alama 10)
MTIHANI 9
MASWALI YA CHOZI LA HERI

1) "Moja ya mambo yanayijitokeza katika Chozi la Heri ni migogoro ya kinasaba." Jadili.


2) Jadili maudhui ya nafasi ya mwanamke katika riwaya ya Chozi la Heri.
3) "Si kufua, si kupiga deki, si kupika, almradi kila siku ilikuwa na adha zake."
a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
b) Eleza mbinu ya lugha ambayo imetumika kwenye dondoo. (alama 2)
c) Eleza kwa kifupi madhila aliyoyataja msemaji. (alama 2)
d) Eleza kwa mifano jinsi haki za watoto zimekiukwa katika riwaya ya Chozi la
Heri. (alama 10)
4) "Hakuna msiba usiokuwa na mwenzake."
a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (Alama 4)
b) Eleza tamathali ya usemi katika dondoo hili.
c) Eleza sifa za anayerejelewa.
d) Fafanua matatizo wanayoyapitia wakimbizi wa ndani kwa ndani.
5) “Mabadiliko ni aushi”. Huku ukirejelea riwaya ya Chozi la Heri, thibitisha kauli hii.
6) Eleza jinsi Uongozi bora umedhihirika katika riwaya ya chozi la heri
7) Onyesha jinsi Udhaifu wa uongozi umebainika katika jumuiya ya chozi la heri
8) Fafanua Mbinu ambazo viongozi wanatumia kujidumisha mamlakani katika chozi la
heri

GOLDEN ELITE EDUCATIONAL CONSULTANCY P.O BOX 2345 KERICHO. FOR MARKING SCHEMES CALL OR
TEXT MR CHEPKWONY ON 072435I706 0R EMAIL kipkemoicos@gmail.com
9) Ukiukaji wa haki za binadamu ni jambo la kawaida katika chozi la heri. Jadili
10) Utamaduni umeangaziwa kwa mapana katika chozi la heri. Jadili
11) Eleza jinsi mwanamke amesawiriwa kwa njia chanya katika riwa ya chozi la heri
12) Riwaya ya chozi la heri imemsawiri mwanamke kwa njia hasi .jadili
13) Eleza jinsi mwanamke anavyoendeleza ukiukaji wa haki za binadamu katika chozi la heri
14) Jadili Nafasi ya vijana katika ujenzi wa jamii
15) Fafanua jinsi Vijana wamechangia kurudisha nyuma maendeleo ya jamii katika chozi la
heri
16) Dhuluma imekita mizizi katika jumuiya ya chozi la heri. Jadili
17) Eleza jinsi Suala la ukoloni mamboleo limejitokeza katika riwaya ya chozi la heri
18) Suala la ufisadi limeshughulikiwa katika Chozi la heri kwa njia mbalijnbali. Fafanua njia
hizo
19) Fafanua matumizi ya mbinu ya Sadfa katika chozi la heri
20) Hotuba ni kipengele cha kimundo. Eleza jinsi kipengele hiki kimetumiwa katika
kufanikisha ploti wa riwaya ya chozi la heri
21) Fafanua matumizi ya mbinu ya Uigizaji/Tamthilia ndani ya riwaya ya chozi la heri
22) Eleza ufaafu wa anwani Chozi la Heri
23) Athari ya vita katika nchi ya Wafidhina ni kioo cha bara la Afrika. Jadili
24) Jadili dhana ya chozi katika riwaya ya Chozi la Heri
25) Mwanamke katika jamii hii ametwezwa na kutwazwa jadili
26) Akikosa la mama hata la mbwa huamwa kwa kurejelea methali hii eleza umuhimu wa
mashirika ya misaada
27) Jamii ya Chozi la Heri ni taswira ya jinsi ukabila unavyoathiri bara la Afrika
28) Malezi ya watoto katika riwaya ya Chozi la Heri ndicho kitovu cha ufanisi na matatizo
yote yanayowapiku watoto
29) Utumizi wa afyuni katika jamii umeleta mathara mengi . Thibitisha
30) Jadili athari na dhiki zinazotokana na uongozi mbaya
31) Mla, naye huliwa zamu yake ikifika . kwa kurejelea riwaya ya Chozi la Heri thibisha
ukweli wa kauli hiyo
32) Riwaya ya Chozi la Heri imejaa aina mbalimbali za migogoro jadili.
33) Uozo wa maadili na kuvunjwa kwa haki ni jambo ambalo lilikuwa la kawaida katika nchi
ya Wahafidhina. Thibitisha
GOLDEN ELITE EDUCATIONAL CONSULTANCY P.O BOX 2345 KERICHO. FOR MARKING SCHEMES CALL OR
TEXT MR CHEPKWONY ON 072435I706 0R EMAIL kipkemoicos@gmail.com
34) Riwaya ya Chozi la Heri ni ya Utamaushi jadili kauli hii
MTIHANI 10
MASWALI YA TUMBO LISILOSHIBA NA HADITHI NYINGINE
1. Alifa chokocho na Dumu Kayanda: Tumbo Lisiloshiba na hadithi nyingine
“Doa ndio kawaida inayobainisha maisha ya mwanadamu.”Onyesha ukweli wa kauli hii kwa
mujibu wa hadithi za: Shogake Dada ana Ndevu, Mame Bakari, Shibe Inatumaliza na
Mtihani wa Maisha. (alama 20)
2. Na kwa nini hazitaki kuukemea mfumo huu wa maisha? Mfumo wa mwenye nacho
kuendelea kupata na msinacho kuendelea kukosa?
a) Eleza muktadha wa dondoo hili (alama 4)
b) Fafanua maudhui mawili yanayodhihirika katika dondoo hili (alama 4)
c) Tambua na ueleze sifa sita za msemaji (alama 6)
d) Eleza athari ya “msinacho kuendelea kukosa” katika jamii husika
(alama 6)
3. Fafanua jinsi suala la elimu limeshughulikiwa katika Tumbo Lisiloshiba na Hadithi Nyingine
kwa kurejelea hadidhi zifuatazo:
a) Mapenzi ya Kifaurongo alama 5)
b) Shogake Dada ana Ndevu (alama 5)
c) Mtihani wa Maisha (alama 5)
d) Mwalimu Mstaafu (alama 5)
4. “… Basi niache nitafute pesa. Muhimu mniunge mkono…”
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili (alama 4)
(b) Fafanua sifa zozote nne za mzungumziwa (alama 4)
(c) Fafanua athari ya vitendo vya mzungumzaji wa maneno haya katika jamii (alama 12)
5. Jadili suala la uozo wa maadili katika jamii huku ukirejelea hadithi zozote nne katika diwani
ya Tumbo Lisiloshiba na Hadithi Nyingine (alama 20)
6. Eleza nafasi ya vijana katika jamii ukerejelea hadithi fupi zifuatazo.
a) Mapenzi ya kifa urongo (alama 5)
b) Shogake Dada anaDevu (alama 5)
c) Mame Bakari (alama10)
7. Ndoto ya mashaka: Ali Abdalla Ali
“Sasa nimechoka mja. Nimechoka hata naradua kufa kuliko kuishi. Hadilini haya
mashaka ya kutengenezwa? Mashaka ya mashaka!
a) Eleza muktadha wa dondoo hili (alama 4)
b) Tambua mbinu mbili za lugha zilizotumika (alama 4)
c) Fafanua mambo sita yanayomfanya mrejelewa aradue kufa. (alama12)
8. “Kwetu tunapigania mikono ielekee vinywani. Mzoea vya sahani, vya vigae haviwezii”
a) Eleza muktadha wa dondoo hili (al 4)
b) Tambua tamathali mbili za usemi zinazojitokeza katika dondoo hili
c) Fafanua sifa nne za msemaji (al 4)
d) Jadili maudhui ya utabaka ukirejerea hadithi husika (al 10)
9. Jadili maudhui ya usaliti katika hadithi;
GOLDEN ELITE EDUCATIONAL CONSULTANCY P.O BOX 2345 KERICHO. FOR MARKING SCHEMES CALL OR
TEXT MR CHEPKWONY ON 072435I706 0R EMAIL kipkemoicos@gmail.com
a) Mapenzi ya kifaraurongo (al 10)
b) Mame Bakari (al 10)
10. “Madhila ya mtoto mvulana katika karne ya ishirini na moja ni mengi.” Tetea kauli hii kwa
hoja ishirini ukirejelea hadithi ya Mapenzi ya Kifaurongo, Masharti ya Kisasa na Ndoto ya
Mashaka. (alama 20)
11. Salma Omar: Shibe Inatumaliza
(a)“ Sijali lawama mnonilaumu”
(i) Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
(ii) DJ na wenzake wanaonekana kufurahia maudhui ya wimbo huu. Thibitisha. (alama 6)
(b) Alifa Chokocho: Shogake Dada ana Ndevu
“…tumshukuru kwa jinsi alivyomwongoza na kumwelekeza kwenye njia iliyonyooka”
Ukirejelea wasifu wa Safia, tetea na upinge kauli hii. (alama 10)
12. Kwa kurejelea hadithi ya mapenzi ya kifaurongo, onyesha jinsi jamii imegawanyika
kitabaka kuegemea.
i. Kielimu
ii. Kikazi
iii. Kiuchumi (alama 20)
13. SHIBE INATUMALIZA
“Ndugu yangu kula kunatumaliza”
“Kunatumaliza au tunakumaliza”
a) Eleza muktadha wa dondoo hili (al. 4)
b) Fafanua maana kitamathali katika kauli ‘Kula tunakumaliza’ (al. 10)
c) Kwa mujibu wa hadithi hii, kwa namna gani wasemaji wanadai kula kunawamaliza? (al.6)

14. ‘MAME BAKARI’


Kwa mujibu wa hadithi hii, ubahaimu anaotendewa mwanamke unakuwa na athari mbaya
kwake, onyesha kwa mifano mwafaka. (al. 10)
‘MASHARTI YA KISASA’
“............... mapenzi ni mateso, ni utumwa, ni ukandamizaji, ni ushabiki usio na maana.”
Thibitisha ukweli wa kauli hii kama unavyojitokeza kwenye hadithi. (al. 10)
15. Jadili jazanda za anwani katika hadithi zifuatazo
a) Shibe Inatumaliza (alama8)
b) Mtihani wa maisha (alama6)
c) Mkubwa (alama 6)
16. MAPENZI YA KIFAURONGO
“Kutazama shule za vijijini kumwibua bingwa katika mtihani wa kitaifa ni kama
kutarajia kupata maziwa kutoka kwa kuku.”
a. Eleza muktadha wa dondoo hili (alama 4)
b. Tambua mbinu moja ya lugha kwenye dondoo hili. (alama 2)
c. Jadili maudhui yafuatayo katika hadithi hii
i) Mabadiliko (alama 5)

GOLDEN ELITE EDUCATIONAL CONSULTANCY P.O BOX 2345 KERICHO. FOR MARKING SCHEMES CALL OR
TEXT MR CHEPKWONY ON 072435I706 0R EMAIL kipkemoicos@gmail.com
ii) Uozo (alama 5)
17. “... maendeleo yanadai mchango wa kila mtu, maskini na tajiri”
a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
b) Taja na ueleze sifa nne za msemaji katika dondoo hili. (alama 4)
c) Mambo yepi mengine ambayo msemaji huhojiana na wenzake wanapokutana ? (alama
6)
d) Taja na ueleze maudhui matatu yanayojitokeza katika dondoo hili.(alama 6)
18.Kwa kurejelea hadithi zozote tano katika diwani ya, ‘Tumbo lisiloshiba na hadithi nyingine.’
Jadili maudhui ya nafasi ya wazazi katika malezi. (alama 20)
19. “…..ilmuradi mawazo yanamwadhibu sasa”
a. Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
b. Fafanua sifa za anayerejelewa katika dondoo hili. (alama 6)
c. Onyesha mawazo yanayomwadhibu anayerejelewa na dondoo hili. (alama 10

20.
a. “ Mamangu siku ile aliniamsha mapema.”
i) Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
ii) Tathmini umuhimu wa usimulizi wa mzungumzaji katika kuendeleza dhamira ya hadithi hii.
(a 8)
b. Onyesha jinsi mashaka linavyomwafiki mhusika mwenyewe katika hadithi ya “Ndoto ya
Mashaka”(alama 8)

21. i) Sekta ya elimu ina changamoto nyingi.Thibitisha kwa kurejelea hadithi zifuatazo :(alama
20)
a) Mapenzi ya Kifaurongo
b) Shogake dada ana Ndevu
c) Mwalimu Mstaafu
d) Mtihani wa maisha
22 ‘’ Hakikubakia hata chakula kidogo cha sadaka ya mwenye njaa… ‘’
i) Thibitisha ukweli wa kauli hii kwa hoja kumi ukirejelea hadithi ya Tumbo Lisiloshiba
(al 10)
ii) Jadili uhalisia wa hadithi ya Tumbo Lisiloshiba katika jamii ya leo kwa kutoa hoja kumi.
(al 10)
23. "Mame Bakari" (Mohamed Khelef Ghassany)
"Dunia we' dunia. Dunia ya mwenye nguvu, si ya mimi dhaifu wa nguvu. Dunia ya msumari
moto juu ya donda bichi."
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (Alama 4)
(b) Ni mbinu ipi iliyotumika katika dondoo hili? (alama 2)
(ch) Taja baadhi ya maamuzi ya maana yaliyofanywa na msemaji wa dondoo.(alama 6)

GOLDEN ELITE EDUCATIONAL CONSULTANCY P.O BOX 2345 KERICHO. FOR MARKING SCHEMES CALL OR
TEXT MR CHEPKWONY ON 072435I706 0R EMAIL kipkemoicos@gmail.com
24. "Tulipokutana Tena" (Alifa Chokocho)
"Hivi ndivyo maisha yapasavyo kuwa-huru kabisa."
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
(b) Ukirejelea hadithi, thibitisha kuwa mmoja wa wahusika hawa hakuishi maisha
ya awali inavyopasa. (alama 16)
25. Fafanua maudhui ya umaskini yanavyojitokeza katika hadithi Tumbo Lisiloshiba na
Tulipokutana Tena. Zingatia hoja nne nne kwa kila hadithi. (alama 20)
26.. "Shogake Dada ana Ndevu" (Alifa Chokocho)
“Halindwi, hujilinda yeye mwenyewe. Hujilinda ndani sikwambii nje."
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
(b) Onesha tamathali mbili za usemi kwenye dondoo. (alama 2)
(ch) Fafanua sifa saba za anayerejelewa katika kauli hii. (alama 14)
27. Kwa kurejelea hadithi zozote tatu katika diwani ya Tumbo Lisiloshiba na Hadithi
Nyingine, jadili vile waandishi walivyoshughulikia suala la mapuuza katika jamii. (alama 20)
28. "Mtihani wa Maisha" (Eunice Kimaliro)
“ilmuradi mawazo yanamwadhibu sasa. “
(b) Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
(c) Fafanua sifa sita za anayerejelewa katika dondoo hili. (alama 6)
(d) Taja mambo mbalimbali yanayochangia adhabu ya mrejelewa wa dondoo hili.
(alama 10)
29..Kwa kurejelea hadithi zozote tatu katika Tumbo Lisiloshiba na Hadithi Nyingine, onesha
vile waandishi walivyotumia mbinu ya taswira. (alama 20)
30. "Kauli yake ni kama maji ya moto yasiyoweza kuchoma nyumba."
a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (Alama 4)
b) Taja na ueleze umuhimu wa tamathali moja ya usemi iliyotumika katika dondoo.
(Alama 2)
c) Fafanua sifa za wapuuzaji wa kauli iliyotolewa. (Alama 8)
d) Jadili dhima sita za mrejelewa katika dondoo. (Alama 6)
31 "Shibe Inatumaliza" (Salma Omar Hamad)
"Ubadhirifu unaotendeka katika jamii unatokana na uzembe na mapuuza ya wanajamii. Onesha
ufaafu wa kauli hii kwa kurejelea hadithi: Shibe Inatumaliza
32. "masharti ya kisasa" (alifa chokocho)
GOLDEN ELITE EDUCATIONAL CONSULTANCY P.O BOX 2345 KERICHO. FOR MARKING SCHEMES CALL OR
TEXT MR CHEPKWONY ON 072435I706 0R EMAIL kipkemoicos@gmail.com
"...nataka ujue kwamba mimi ni mwanamke wa kisasa, na mwanamke wa kisasa hutafuta
mwanamume wa kisasa."
(a) Eleza muktadha wa maneno haya. (Alama 4)
(b) Anayesema haya alikuwa na sifa zipi? (Alama 8)
(ch) Anayeambiwa maneno haya alijua maana ya usasa? Thibitisha. (Alama 8)
33. "Nasema nizikeni hapa."
a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
b) Taja na uelezee sifa za mnenaji wa dondoo hili. (alama 6)
c) Fafanua maudhui yoyofe matano yanayoshughulikiwa katika hadithi hii, (alama 10)
34. a) Mashaka ni jina la kimajazi katika hadithi ya "Ndoto ya Mashaka". Jadili. (alama 10)
a) Onyesha namna asasi ya ndoa ilivyoshughulikiwa katika hadithi hii. (alama 10)
35."Kumekucha na makuchakucha yake."
i. Fafanua ukweli wa kauli hii ukirejelea hadithi ya "Ndoto ya Mashaka" (alama 14)
ii. Eleza umuhimu wa mhusika Mashaka. (alama 6)
36.“Sekta ya elimu imekumbwa na changamoto katika jamii”. Fafanua kauli hii ukirejelea
diwani ya Tumbo Lisiloshiba na Hadithi Nyingine. (alama 20)
37.'Jazanda inatumika katika hadithi ya "Kidege ".' Fafanua. (alama 20)
38. 'Maudhui ya mapenzi yameshughulikiwa vilivyo katika diwani ya Tumbo Lisiloshiba na
Hadithi Nyingine.' Thibitisha kauli hii. (alama 20)
39."Umdhaniye ndiye kumbe siye." Thibitisha ukweli wa kauli hii ukirejelea hadithi zozote
tano katika diwani ya Tumbo Lisiloshiba na Hadithi Nyingine. (alama 20)
40. “Kesho kama sote tutaamka salama……….kama tutafungua milango ya nyumba zetu”….
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili (alama 4)
(b) Eleza tamathali mbili za lugha zilizotumiwa katika dondoo hili. (alama 4)
(c) Eleza sifa sita za msemaji wa maneno haya. (alama 6)
(d) Hadithi hii inaakisi mambo mengi yanayotendeka katika bara la Afrika.
Taja mambo sita (alama 6)
41 .Ukengeushi huzorotesha maendeleo ya kijamii. Jadili kauli hii ukirejelea hadithi ya
‘Mkubwa’. (alama 20)
42. Kwa kuzingatia hadithi zozote tano eleza uozo wa jamii kama unavyojitokeza katika tumbo
lisiloshiba (Diwani) (alama 20)

GOLDEN ELITE EDUCATIONAL CONSULTANCY P.O BOX 2345 KERICHO. FOR MARKING SCHEMES CALL OR
TEXT MR CHEPKWONY ON 072435I706 0R EMAIL kipkemoicos@gmail.com
43 “Kesho panapo majaaliwa. Kesho kama sote tutaamka…….. kama tutafungua milango ya
nyumba zetu zinazosimamia juu ya ardhi hii adhimu…”
a) Eleza muktadha wa dondoo hili (al. 4)
b) Eleza sifa nne za msemaji (al. 4)
c) Taja mbinu zozote mbili za lugha zinazojitokeza katika dondoo hili (al. 2)
d) Kwa kurejelea hadithi nzima onyesha namna jamii ya kisasa ina tumbo lisiloshiba (al.
10)
44. “Rasta twambie bwana!”
a) Weka dondo katika muktadha (ala 4)
b) Taja mbinu zilizotumiwa na mwandishi katika dondoo hili (ala 2)
c) Ni kwa vipi mzungumziwa anamchukulia mwalimu mkuu kama hambe? (ala 4)
d) Je, mtihani wa maisha ni amwani faafu ya hadithi hii. (ala 10 )
45. Usiteketeze umati kama kuni zinavyoteketeza moto.Rudi rudi kwa mola wako.

a. Eleza muktadha wa dondoo hili.


b. Fafanua sifa za msemewa
c. Tambua tamathali ya usemi iliyotumika hapo juu.
d. Ni kwa nini msemewa anatakikana kurudi kwa mola wake?
MTIHANI 11
INSHA
MTIHANI 1
1. LAZIMA
Wewe ni mkurugenzi wa kampuni ya mzalendo. Kumekuwa na utepetevu na uzembe kazini.
Waandikie wafanyakazi memo kuwaonya dhidi ya jambo hili.
2. Andika insha kuhusu jinsi raia wanavyoendeleza matumizi mabaya ya ardhi.
3. Usalama unazidi kuzorota jimbo la Meru. Jadili chanzo chake na jinsi ya kutatua.
4. Andika kisa kitakachomalizikia kwa maneno :
... kweli binadamu heshi vituko. Niliyemdhania kuwa ndiye kumbe siye.

MTIHANI 2
1. LAZIMA
Katika ofisi ya ubalozi wa Kichina, kuna nafasi ya kufundisha wageni kazi fupi ya Kiswahili
na Kiingereza. Andika Tawasifu utakayoambatanisha na ombi lako.
2. ‘Mvua ya masika imeleta hasara nyingi hapa nchini kuliko faida’. Jadili.
3. Andika kisa kinachothibitisha ukweli wa methali, ‘Kutangulia sio kufika’.
4. Mara tu nilipovuka daraja la ule mto, nilijua kwamba maisha yangu yalikuwa yanachukua
mkondo mpya….

MTIHANI 3
1. SWALI LA LAZIMA
GOLDEN ELITE EDUCATIONAL CONSULTANCY P.O BOX 2345 KERICHO. FOR MARKING SCHEMES CALL OR
TEXT MR CHEPKWONY ON 072435I706 0R EMAIL kipkemoicos@gmail.com
Suala la ufisadi limekuwa donda dugu nchini. Andika mahojiano kati ya mwenyekiti wa tume
ya kupambana na ufisadi nchini na mwandishi wa habari kuhusu mbinu za kupambana na
donda hili.
2. Vijana wa kisasa wanakabiliwa na changamoto mbalimbali za maisha. Fafanua huku
ukipendekeza hatua zifaazo kuchukuliwa ili kuzikabili changamoto hizo.
3. Tunga kisa kitakachodhihirisha maana ya methali ifuatayo:
Uzuri wa mkakasi ndani kipande cha mti
4. Tunga kisa kinachoanza kwa maneno yafuatayo
Nilipigwa na butwaa nilipomwona, sikujua nifurahi au nihuzunike …..

MTIHANI 4
1. Andika tahariri kwa gazeti la mwananchi ukieleza hatua zinazochukuliwa nchini ili
kumwendeleza kielimu mtoto msichana.
2. Kupunguza mishahara ya watumishi wa umma ni hatua mwafaka kama maendeleo ya nchi
yatafanikiwa. Jadili
3. Andika insha itakayoafikiana na methali. ‘Baniani mbaya kiatu chake dawa’.
4. Andika insha itakayomalizikia kwa:
…………… Walipofungua mlango huo hatimaye, wengi hawakuweza kuzuia hisia zao.
Waliangua vilio kwa maafa waliyoshuhudia.

MTIHANI 5
1. Lazima
Wewe ni katibu mkuu wa wizara ya kilimo. Mmefanya mkutano wa kuzungumzia mikakati ya
kupambana na baa la njaa nchini. Katika mkutano wenu, katibu mkuu wa chama cha msalaba
mwekundu amealikwa. Andika kumbukumbu za mkutano huo.
2. Kugatuliwa kwa huduma za matibabu kutoka serikali kuu kumeleta maumivu kuliko tiba
kwa wananchi. Jadili
3. Tunga kisa kinachobainisha maana ya methali: Mbaazi ukikosa kuzaa husingizia jua.
4. Nilikuwa natazama Runinga ya Tupashe Habari, mara nikaona picha ya mtu ambaye
nilimfahamu… Endeleza

MTIHANI 6
1. Wewe ni mhariri wa Gazeti la Mamboleo. Andika tahariri ukieleza athari za mitandao ya
kijamii.
2. Mazingira bora ni muhimu katika maisha ya binadamu. Jadili.
3. Mwenda tezi na omo marejeo ni ngamani.
4. Nilikuwa nimetoka nyumbani nikielekea mjini, mara nikasikia mngurumo wa radi
ulioandamana na umeme…… Endeleza
MTIHANI 7
1. LAZIMA
Umepata nafasi ya kumhoji Msimamizi mkuu wa Baraza la Mitihani nchini, kuhusu athari
za wizi wa mtihani wa Kitaifa katika shule za Sekondari. Andika mahojiano haya.
2. Pendekeza njia za kukabiliana na ongezeko la visa vya utovu wa maadili miongoni mwa
vijana katika jamii.
3. Andika kisa kinachooana na methali mchelea mwana kulia hulia mwenyewe.

GOLDEN ELITE EDUCATIONAL CONSULTANCY P.O BOX 2345 KERICHO. FOR MARKING SCHEMES CALL OR
TEXT MR CHEPKWONY ON 072435I706 0R EMAIL kipkemoicos@gmail.com
4. Tunga kisa kinachomalizika kwa maneno haya.
. . . hapo ndipo iliponipambazukia kuwa nilikuwa naogelea baharini pekee kinyume na
wenzangu wote.

MTIHANI 8
1. Wewe ni katibu wa kamati ya wataalamu wanaoshughulikia jinsi ya kukabiliana na uhaba wa
maji. Andika kumbukumbu za mkutano wenu. (alama 20)
2. Hatua ya serikali kuu kumpa kila mwanafunzi wa darasa la kwanza tarakilishi ni ya manufaa
sana. Jadili (alama 20)
3. Mwenye kovu usidhani kapoa. (alama 20)
4. Lo! Jambo lililotendeka katika makazi ya jirani yetu usiku huo lilikuwa la kutisha sana.
Kumbe baba watu alikuwa amegeuka kuwa hayawani. Hayawani mla watu...........(alama 20)
MTIHANI 9
1) Insha ya lazima.
Ukiwa gavana wa kaunti mojawapo hapa nchini, umeandaa kikao na mbunge na afisa wa
masuala ya kiusalama jimboni ili kujadili mikakati ya kupambana na visa vya ukosefu wa
usalama. Andika mazungumzo yenu.
2) Uhuru unaopewa vijana leo katika nchi yetu una madhara zaidi kuliko faida Jadili.
3) Andika insha itakayodhihirisha maana ya methali:-
Mtaka cha mvunguni sharti ainame.
4) Andika insha itakayokamilika kwa manano haya:-.. Mstakiwa alimwangalia hakimu kwa
macho ya huruma kisha akamwangalia mkewe na wanawe akatamani kuwaomba
msamaha lakini hukumu ilikuwa imetolewa.

MTIHANI 10
1. Ukiwa waziri wa Elimu nchini, umealikwa kuwazungumzia wanafunzi wa Kidato cha nne
katika shule ya Ufanisi. Andika tawasifu utakayowasilisha.
2. Wananchi ndio wakulaumiwa kutokana na kuzorota kwa usalama nchini Kenya. Jadili
3. Andika insha itakayoafikiana na methali
Baniani mbaya kiatu chake dawa
4. Tunga kisa kinachomalizia maneno yafuatayo:
. ....Nilijitolea kafara na msaada wangu ukazaa natija kwa wengi.

MTIHANI 11
1. Wewe ni katibu wa Chama cha Mazingira katika kaunti yako. Mwandikie Waziri wa
Mazingira mdahilishi/ barua pepe ukimwelezea madhara ya mafuriko na jinsi ya kutafuta
suluhisho.
2. “Elimu bila malipo inafaida na hasara.” Jadili.
3. Tunga kisa kitakacho bainisha maana ya methali:
Ajizi ni nyumba ya njaa.
4. Andika kisa kitakachomalizika kwa maneno yafuatayo:
………Niliachwa kinywa wazi.
Haikuwahi kunipitia akilini kuwa binadamu anaweza kumtendea bi

MTIHANI 12

GOLDEN ELITE EDUCATIONAL CONSULTANCY P.O BOX 2345 KERICHO. FOR MARKING SCHEMES CALL OR
TEXT MR CHEPKWONY ON 072435I706 0R EMAIL kipkemoicos@gmail.com
1) Rafiki yako amekualika katika uzinduzi wa kazi wa kazi alizozichora na.kukupa jukumu Ia
kuandaa wasifu wake ambao utawasomea walikwa wengine. Andika wasifu utakaousoma
katika hafla hiyo.
2) Fafanua umuhimu wa kuwepo maungano kati ya mataifa ya Afrika Mashariki.
3) Andika kisa kinachofafanua maana ya methali “Kikulacho ki nguoni mwako”
4) Andika insha itakayoanzia kwa “Hatungekaa pale tena tukiwa tumejikunyata kama kuku
walionyeshewa na kuitazama hatari iliyokuwa imetukondolea macho.Ilibidi tutafute njia
za kujinusuru …"

MTIHANI 13
1. Insha ya lazima
Andika mahojiano baina ya waziri wa usalama wa kitaifa na waandishi watatu wa habari
kuhusu hali ya usalama nchini
2. Pendekeza hatua zinazopaswa kuchukuliwa kukuza umoja wa kitaifa
3. Mla cha mwenziwe na chake huliwa
4. Tunga insha itayoanzia kwa maneno yafuatayo .
Alfajiri ya siku iliyofuata ilinipata nje ya mlango wa hospitali kuu ya kijito. Punde si punde
milango ya wodi ikafunguliwa. Machozi yalinitiririka njia mbili nilipotupa macho kwenye
kitanda alicholazwa mamangu. Hakuwepo………

MTIHANI 14
1. Lazima
Wewe ni mkaazi wa eneo ya Tuzindukane na unataka kuwania Ugavana katika Kaunti ya
Malishoni. Andika tawasifu utakayowasilisha kwa raia ili waweze kukuchagua.
2. Tatizo la kigaidi ni changamoto kubwa sana katika usalama na maendeleo ya kiuchumi
hapa nchini.Jadili.
3. Kelele za mlango haziniasi usingizi.
4. Andika insha inayomaliziz kwa :
………………Kijasho chembamba kilianza usoni huku akionyesha wasiwasi.Nilitambua
wazi kuwa yeye ndiye aliyefanya kitendo hicho hasi!

MTIHANI 15
1. Andika barua kwa mhariri wa gazeti la Zindukeni ukitoa maoni kuhusu sekta ya usafiri
wa pikipiki.
2. Fafanua njia mbalimbali za kustawisha michezo nchini.
3. Andika insha inayoafikia methali, Ukiona vyaelea vimeundwa.
4. Tunga kisa kinachoanza kwa maneno yafuatayo:….Nilijaribu kuuinua mguu wangu
uliojaa maumivu kutokana na

MTIHANI 16
1) Wewe ni mwalimu wa ushauri nasaha wa shule yenu. Andika hotuba ambayo unaweza
kutolea wazazi kuhusu mambo yanayosababisha muamana wa kifamilia kuimarika.
2) Jadili mambo yanayosababisha maasi ya vijana.
3) Abebwaye hujikaza
4) Andika kisa kinachoanza kwa kifungu kifuatacho: Hali nzima ilikuwa fujo tupu. Wasiwasi
na hatari
GOLDEN ELITE EDUCATIONAL CONSULTANCY P.O BOX 2345 KERICHO. FOR MARKING SCHEMES CALL OR
TEXT MR CHEPKWONY ON 072435I706 0R EMAIL kipkemoicos@gmail.com
GOLDEN ELITE EDUCATIONAL CONSULTANCY P.O BOX 2345 KERICHO. FOR MARKING SCHEMES CALL OR
TEXT MR CHEPKWONY ON 072435I706 0R EMAIL kipkemoicos@gmail.com
For all other resources including opener exams 2020, mocks, post mocks, notes,schemes of
work and many more,please don’t hesitateto contact us

GOLDEN ELITE EDUCATIONAL CONSULTANCY P.O BOX 2345 KERICHO. FOR MARKING SCHEMES CALL OR
TEXT MR CHEPKWONY ON 072435I706 0R EMAIL kipkemoicos@gmail.com

You might also like