You are on page 1of 5

PARADISE EDUCATION CENTRE

PEC-KISWAHILI
KIDATO CHA NNE

Muda; Saa 3 Tarehe; 27/06/2022

Maelekezo
1. Karatasi hii ina sehemu A, B na C zenye jumla ya maswali kumi na mbili (12).
2. Jibu maswali yote katika sehemu A na B, maswali matatu (3) kutoka sehemu C.
3. Zingatia maagizo ya kila sehemu na ya kila swali .
4. Simu za mkononi na vitu vyote visivyoruhusiwa havitakiwi katika chumba cha mtihani.
5. Andika Jina lako katika kila ukurasa wa karatasi yako ya kujibia.

1
SEHEMU A (Alama 15)
Jibu maswali yote katika sehemu hii.

1. Chagua herufi ya jibu sahihi katika vipengele (i) hadi (x), kisha andika herufi ya jibu hilo
katika Karatasi yako ya kujibia.

(i)…….. ni vikundi vya majina ya Kiswahili.


A Maneno
B Maumbo
C Ngeli
D Mtindo

(ii)… ni utaratibu unaotumika kuweka nomino katika matabaka yanayofanana.


A Upatanisho wa kisarufi
B O-rejeshi
C Ngeli za nomino
D Sarufi

(iii)….. ni neno au kikundi cha maneno ambacho hudokeza taarifa fulani.


A Kirai
B Kishazi
C Tungo
D Kijalizo

(iv)….. ni kirai ambapo neno lake kuu ni nomino.


A Sentensi
B Kiarifu
C Kirai Nomino
D Kiima

(v) ……ni tungo yenye kitenzi ambacho chaweza kujitosheleza.


A Kiimbo
B Mkazo
C Kishazi
D Neno

(vi) ……..ni kishazi kinachotawaliwa na kitenzi kikuu.


A Kishazi huru
B Simo
C Rejesta
D Lugha sanifu

(vii) ……….ni kishazi kinachotawaliwa na kitenzi Kisaidizi.


A Kishazi tegemezi
B Dhima
C Dhana

2
(viii) …….ni kipashio kinachokamilisha au kujazia neno kuu.
A Kijalizo
B Sentensi
C Chagizo
D Igizo

(ix) …….ni sehemu ya sentensi ambayo hujazwa na nomino.


A Shamirisho
B Beti
C Vina
D Vibwagizo

(x) ……ni kielezi au kirai husishi ambacho kinafanya kazi kama kielezi.
A Chagizo
B Mizani
C Ushairi
D Visakale

2. Oanisha maana za dhana za uandishi zilizo katika Orodha A kwa kuchagua herufi ya dhana
husika katika Orodha B , kisha andika herufi husika katika karatasi yako ya kujibia.
Orodha A Orodha B
(i) Wasikilizaji au watazamaji wa A. Ngonjera
kazi za fasihi. B. Hadhira
(ii) Ni msimuliaji wa kazi za fasihi. C. Fanani
(iii) Hii ni kazi ya fasihi andishi D. Hadithi fupi
yenye kisa kimoja. E. Mafunzo
F. Mapisi
(iv) Ni nasaha anazotoa mtunzi.
G. Riwaya
(v) Maelezo ya historia bila kutia H. Shairi
mambo ya kubuni.

SEHEMU B (Alama 40)


Jibu maswali yote katika sehemu hii.

3. Eleza maana ya vidahizo vifuatavyo na kisha tunga sentensi moja (1) kwa kila kidahizo.
a) Kinyenyezi
b) Matandu
c) Matlaba
d) Sandali
e) Uzimbezimbe

4. Tunga sentensi mbili zinazoonesha kishazi huru na tatu zinazoonesha kishazi tegemezi.

5. Toa maana tano za neno Mswahili.

6. Kwa kutumia mifano, thibitisha ubantu wa Kiswahili kwa hoja madhubuti tano (5).

3
7. Kwa kutumia vitabu viwili vya tamthiliya mbili ulizosoma chagua wahusika wawili na
uoneshe kutokukubalika kwao katika jamii. (Toa hoja tatu kwa kila mhusika)

8. Soma kifungu cha habari kifuatacho kisha jibu maswali yanayofuata:

Wakati wa ukoloni mabepari wa Kijerumani walianzisha kilimo cha pamba huko Kusini
mwa Tanzania. Waliwalazimisha Wamatumbi kufanya kazi katika mashamba yao. Pamba
iliyopatikana ilipelekwa Ujerumani. Kama anavyosema kibarua mmoja aliyeteswa na
mabepari hao, " Wakati wa kilimo kulikuwa na dhiki sana. Sisi vibarua tuliokamatwa tulikaa
mstari wa mbele, tukilima. Nyuma yetu kulikuwa na mnyapara , kazi yake kutupiga kwa
mijeledi . Nyuma ya mnyapara alikuwepo jumbe, na kila jumbe alisimama nyuma ya watu
hamsini. Na nyuma ya majumbe alisimama Bwana Kinoo mwenyewe. Lo! Hapo shuhudia
kifo."

Mjerumani alipofika nchini akaamrisha Wamatumbi kulipa kodi. Watu walimjibu, "Hudai
kitu. Hatuna deni kwako. Ikiwa wewe mgeni unataka kukaa nchi hii basi ni lazima wewe
utuombe sisi. Na sisi tutakuambia utoe sadaka kwa Miungu wetu. Wewe utatoa chochote na
sisi tutaifanyia karamu Miungu kwa niaba yako; tutakupa ardhi na wewe utakuwa na mahali
pa kukaa. Lakini siyo sisi wenyeji tukupe wewe sadaka. Hilo haliwezekani hata kidogo."

Juu ya dhiki zote walizopata yaani dhiki ya njaa, dhiki ya maonevu, dhiki ya kulimishwa na
kupigwa, watu walistahimili wakavumilia kwa sababu hawakuweza kupigana, kwani
hawakuwa na umoja. Vilevile walijua kuwa nguvu ya Mjerumani ilikuwa kubwa.
Wakangoja.

Katika mwaka wa 1904 akaja mtume , jina lake Kinjeketile. Karibu na kwao Ngarambe
kulikuwa na bwawa la maji kaitika kijito cha Mto Rufiji. Kinjeketile alipandwa na pepo
aitwaye Hongo, aliyekuwa akikaa katika bwawa hilo.

Kinjeketile aliwafundisha Waafirka maana ya umoja, akawapa moyo kwa nguvu ya maji.
Waafrika wakawa na umoja na nguvu. Watu wengi waliosikia jina lake walikuja kumuunga
mkono.

Maswali
a) Andika kichwa cha habari kinachofaa kwa habari uliyosoma kisichozidi maneno matano.
b) Eleza wazo kuu linalojitokeza katika habari uliyoisoma.
c) Ni mambo gani yanayothibitisha kwamba ni kweli Wamatumbi waliteswa? Taja mambo
matatu.
d) Toa maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumika katika kifungu cha habari
ulichosoma.
(i) Mnyapara
(ii) Mijeledi
(iii) Walistahimili
(iv) Sadaka
(v) Mtume

4
SEHEMU C (Alama 45)
Jibu maswali matatu (3) kutoka katika sehemu hii.

9. Andika risala inayohusu wahitimu wa kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Paradiso.

ORODHA YA VITABU KWA SWALI LA 10-12

USHAIRI
Wasakatonge - M.S. Khatibu (DUP)
Malenga Wapya - TAKILUKI (DUP)
Mashairi ya Chekacheka - T.A. Mvungi (EP & D.LTD)

RIWAYA
Takadini - Ben J. Hanson (MBS)
Watoto wa Mama N’tilie - E. Mbogo (H.P)
Joka la Mdimu - A.J. Safari (H.P)

TAMTHILIYA
Orodha - Steve Reynolds (MA)
Ngoswe Penzi Kitovu cha Uzembe - E. Semzaba (ESC)
Kilio Chetu - Medical Aid Foundation (TPH)

10. “Washairi ni wataalamu wazuri na waliobobea katika kutumia taswira zinazotoa ujumbe kwa
jamii.” Tumia taswira tatu kwa kila diwani kati ya diwani mbili zilizoorodheshwa
kuthibitisha kauli hiyo.

11. Jadili kukubalika kwa wahusika wawili kama kielelezo halisi cha wanajamii kati ya
Takadini, Maman’tilie na Brown Kwacha kutoka katika riwaya mbili ulizosoma. Toa hoja
tatu kwa kila mhusika.

12. Waandishi wa tamthiliya wamemchora mwanamke katika sura tofauti. Thibitisha kauli hii
kwa kutumia waandishi wawili (2) wa tamthiliya mbili (2) ulizosoma. (Toa hoja tatu kwa
kila tamthiliya uliyosoma)

………………………………….. MWISHO …………………………………………...

You might also like