You are on page 1of 2

HALMASHAURI YA WILAYA YA MERU

SHULE YA MSINGI MAKUMIRA


DARASA LA NNE
JARIBIO LA MAARIFA YA JAMII - JULAI 2020

1. i) Mtoto wa Mjomba anaitwa ____________


a) Shangazi (b) Binamu (c) Mama Mdogo
ii) Jotoridi hupimwa kwa kifaa maalumu kiitwacho ______________
a) Rula (b) Kipima joto (c) Moto
iii) Waziri mkuu wa serikali ya awamu ya tatu alikuwa ____________
(a) Fredrick Sumaye (b) Jakaya Kikwete (c) mizengo pinda
iv) Chimbuko la familia lilianza kwa ______________
(a) Babu na Bibi (b) Baba na Mama (c) Shangazi na Mjomba
v) Uhusiano ni
(a) Hali ya watu wawili au zaidi wenye malengo ya pamoja (b) Hali ya kugombana baina
ya mtu na mtu (c) Hali ya kufanya kazi peke yako
vi) Mfumo wa jua umezungukwa na sayari
(a) Mbili (b) Tatu (c) Nane
vii) Kifaa kinachozalizha msukumo wa hewa ni
(a) Jotoridi (b) Pangaboi (c) Jokofu
viii) Chombo kinachohifadhi vitu katika hali ya ubaridi ili visiharibike ni
(a) Jokofu (b) Maji (c) Barafu
ix) Tunaweza kutunza kumbukumbu za matukio ya masomo shuleni kwenye
(a) Stoo (b) Jikoni (c) Maktaba
x) Hali ya tabia ya mtu kupata mapato bila ya kufanya kazi huitwa
(a) Ujima (b) Unyonyaji (c) Ukabaila

SEHEMU B
JAZA NAFASI WAZI
2. i) ni muunganiko wa familia zenye asili au chimbuko la aina moja.
ii) ni mfumo wa kwanza wa kiuchumi na kitawala ambapo watu waliishi na
kushirikiana kwa pamoja
iii) ni mfumo wa uchumi na utawala ambapo ardhi ilikuwa msingi mkuu wa
uzalishaji mali.
iv) walikuwa watu wasio na ardhi waliofanya kazi kwaajili ya chakula tu.
v) ni sayari iliyo karibu sana na jua

SEHEMU C
ANDIKA NDIYO AU HAPANA
i) Katika maisha yetu ya kila siku hatutakiwi kuwa na uhusiano mwema
ii) Kukaa vikao vya usuluhisho, kuunda kamati za ulinzi na kutumia wazee wa kimila ni njia za
kutatua mgogoro
iii) Mifugo na ardhi ni raslimali
iv) Nyota na mwezi huonekana wakati wa mchana
v) Kodi ni malipo yanayotozwa baada ya kupanga na kutumia kitu kwa muda
SEHEMU D
OANISHA SEHEMU (A) NA (B) ILI KUPATA JIBU SAHIHI
SAFU A SAFU B
i) Wakati wa ujima ( ) A. Hujenga ukakamavu

ii) Unyonyaji ( ) B. Jumla ya mali aliyonayo mtu

iii) Michezo ( ) C. Jambo ambalo kamwa halikuwahi kushudiwa

iv) Raslimali ( ) D. Hapakuwa na uchaguzi

v) Sabika ( ) E. Hali au tabia ya mtu kupata mapato bila ya

kufanya kazi

F. Ulikuwa kiwango cha chini

G. Makabila ya watwana

You might also like