You are on page 1of 7

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

SHULE YA MSINGI YEMEN CHANG’OMBE

MTIHANI WA MAZOEZI DARASA LA SABA

SOMO: KISWAHILI

MUDA: SAA 1:00 APRIL 2020

MAELEKEZO
 Mtihani huu una jumla ya maswali arobaini na tano (45).
 Jibu maswali yote katika kila sehemu.
 Soma maelekezo yote yaliyoko katika karatasi maalum kisha
jibu kwenye daftari.
SEHEMU A: SARUFI

Chagua jibu sahihi kutoka kwenye machaguo kisha siliba herufi ya jibu hilo katika

karatasi maalumu ya kujibia (OMR) uliyopewa

1. Waziri Mkuu ____________ Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania


kwenye mkutano mkuu wa viongozi wa nchi za Afrika uliofanyika hivi karibuni
mjini Addis Ababa.

A. Alimwasilisha C. Alimuakisha E. Alimkasimisha [ ]

B. Alimwakilisha D. Alimkaimisha

2. Ungejua mapema _____aondoke.

A. Usingekubali C. Ungalikubali E. Usingakubali [ ]

B. Usingalikubali D. Usingelikubali

3. Neno ua lipo katika ngeli ipi?

A. I-YA B. I-ZI C. LI-YA D. KI-VI E. U-ZI [ ]

4. Neno lipi kati ya haya yafuatayo ni kinyume cha neno haba?

A. Nyingi B. Ndogo C. Tele D. Kidogo E. Wengi [ ]

5. Nomino inayotokana na kitenzi ongoza ni:

A. Uongo B. Muongo C. Ongozwa D. Uongozi E. Ngozi [ ]

6. Ng’ombe wamo zizini. Neno zizini limetumika kama aina ipi ya maneno?

A. Kielezi B. Kitenzi C. Kiwakilishi D. Kivumishi E. Nomino [ ]

7. Neno moja linalowakilisha kiti, meza, kabati na dawati ni:

A. Samani B. Darasa C. Shule D. Dawati E. Mbao [ ]

8. Mwanamke mzee sana hujulikana kama:

A. Kapela B. Mjane C. Shaibu D. Mhenga E. Ajuza [ ]

9. Mariamu alisukwa na dada yake. Neno alisukwa lipo katika kauli ipi?

A. Kutendeka B. Kutendewa C. Kutendwa D. Kutenda E. Kutendea [ ]

1
10. ________________ kuyatunza mazingira yetu ili tuepukane na magonjwa ya
milipuko.

A. Tuna budi B. Hatuna budi C. Si budi D. Siyo budi E. Tunayo budi [ ]

11. Wingi wa neno uma ni:

A. Mauma B. Vyuma C. Mima D. Miuma E. Nyuma [ ]

12. Neno lipi kati ya haya yafuatayo lina maana sawa na neno jazba?

A. Chuki B. Woga C. Hofu D. Hasira E. Huzuni [ ]

13. Alisema ondokeni hapo upesi. Sentensi hii ipo katika kauli gani?

A. Halisi B. Taarifa C. Thabiti D. Murua E. Tata [ ]

14. Mtoto wa nzige hujulikana kama:

A. Kifaranga B. Kinda C. Kimatu D. Kibwenzo E. Kichanga [ ]

15. Tutakuwa na tafrija fupi ya kuwatakia kila la heri wanafunzi wa darasa la saba
katika mtihani wao. Neno tafrija lina maana sawa na neno lipi kati ya haya
yafuatayo?

A. Simanzi B. Karamu C. Mkutano D. Kalamu E. Ibada [ ]

16. Amekula upesi upesi ili awahi shule. Neno upesi upesi ni aina gani ya neno?

A. Kihusishi B. Kielezi C. Kitenzi D. Kiwakilishi E. Kihisishi [ ]

17. Walikuwa na mipango __________ kuhusu maendeleo ya kijiji chao lakini


walishindwa kuitekeleza kutokana na uhaba wa fedha.

A. Mamluki B. Lukuki C. Rukuki D. Lutuki E. Kuki [ ]

18. Kisawe cha neno tamati ni:

A. Mwanzo B. Mwisho C. Katikati D. Nadra E. Aghalabu [ ]

19. Neno mwanafunzi lina silabi ngapi?

A. Sita B. Tatu C. Mbili D. Tano E. Nne [ ]

20. 20.Meli iliyokuwa imebeba ________ ya vyakula imeshatia nanga baharini.

A. Mzigo B. Sherehe C. Shehena D. Shena E. Makuli [ ]

2
SEHEMU B: METHALI,NAHAU NA VITENDAWILI

21. Methali ipi kati ya hizi ina maana sawa na methali isemayo : Maji yakimwagika
hayazoleki?

A. Hakuna lenye mwanzo lisilokuwa na mwisho D. Lakuvunda halina ubani

E. Mbio za sakafuni husishia ukiongoni

C. Asifuye mvua imemnyea [ ]

22. Alizia methali hii : Mpofuka ukongweni_____________

A. Hakumbuki njia C. Haishi kutapatapa E. Hakumbuki ujanani

B. Hatosheki D. Hapotei jia [ ]

23. Baba kafa kaniachia pete. Jibu la kitendawili hiki ni lipi?

A. Ajusi B. Nyoka C.Konokono D. Jongoo E. Shanga [ ]

24. Baada ya kumsubiri kwa muda mrefu bila kutokea, Mwasiti aliamua kuondoka.
Nahau ipi kati ya hizi zifuatazo ina maana ya “kuamua” ?

A. Kata tama C. Kata shauri E. Poteza matumaini

B. Shika usukani D. Kufa moyo [ ]

25. Mwombela ajifanya juu chini kuhakikisha anafaulu masomo yake. Nahau
kufanya juu chini ina maana gani?

A. Kutumia kila njia C. Kutumia nguvu nyingi E. Kukata tama

B. Kurukaruka D. Kuanzia juu kwenda chini [ ]

26. Tegua kitendawili hiki : Fimbo ya babu ina mafundo

A. Muwa B. Upele C. Uzi D. Kamba E. Fenesi [ ]

27. Neno lipi linakamilisha Methali isemayo______ hula na wa kwao

A. Mtafutaji C. Mdharau mwiba E. Mwenda tezi na umo

B. Mchuma janga D. Mchumia juani [ ]

28. Kinyonga ni jibu la vitendawili vifuatazo ISIPOKUWA:

A. Tajiri wa macho C. Bwana afya wa porini E. Tajiri wa rangi [ ]

B. Akitembea huringa hata kama yupo hatarini D. Huuawa na uzazi wake

3
29. Masikini huyu hata umchangie namna gani haridhiki . Jibu la kitendawili hiki
ni:

A. Pua B. Macho C. Tumbo D. Mdomo E. Shimo la taka [ ]

30. Nini maana ya nahau shika usukani?

A. Kuwa wa mwisho B. Ongoza C. Endesha gari D. Samehe E. Tamani [ ]

SEHEMU C: USHAIRI

Soma kwa makini shairi lifuatalo kisha jibu maswali yanayofuata

1. Nimekaa nikawaza, bila majibu kupata,

Kwa kweli inashangaza, Temeke hadi Tabata,

Wengine wanajiuza, wapate pesa za Bata,

Dada zetu wa mjini, wengi wanasikitisha.

2. Watuvalia vimini, watembea nusu uchi,

Wapo kule Buguruni, hadi Mtoni Kijichi,

Wanajificha gizani, kamwe hawataki tochi,

Dada zetu wa mjini, wengi wanasikitisha.

MASWALI:

31. Shairi hili linahusu nini?

A. Maisha ya mjini C. Maisha ya Buguruni E. Mavazi ya akina dada

B. Tabia za akina dada wa mjini D. Dada zetu wa vijijini [ ]

32. Shairi hili lina beti ngapi?

A. Mbili B. Nane C. Kumi na sita D. Tatu E. Tano [ ]

33. Mshororo wa mwisho katika kila ubeti wa shairi hili hujulikana kama:

A. Ubeti B. Vina C. Kiitikio D. Mshororo E. Mkarara [ ]

34. Kisawe cha neno tochi kama lilivyotumika katika shairi hapo juu ni?

A. Balbu B. Kurunzi C. Dainamo D. Rununu E. Nywila [ ]

4
35. Shairi hili lina jumla ya mishororo mingapi?

A. 16 B. 2 C. 8 D. 12 E. 4 [ ]

36. Vina vya mwisho katika ubeti wa pili wa shairi hili ni:

A. Ni B. Za C. Ta D. Hi E. Chi [ ]

SEHEMU D: UTUNGAJI.

Panga sentensi zifuatazo kwa kuzipa herufi A, B, C,na D ili zilete mtiririko
mzuri.

37. Mama aliniamsha asubuhi na mapema [ ]


38. Ilikuwa ni siku ya sherehe ya kuzaliwa kwangu [ ]
39. Mama alibeba zawadi alizoniandalia tukaelekea ukumbini [ ]
40. Nikaenda kuoga na kuvaa gauni langu jipya na viatu vyekundu [ ]

SEHEMU E: UFAHAMU

Soma kwa makini kifungu cha habari kifuatacho kisha jibu maswali
yanayofuata

Basi hilo lilikuwa likitokea Morogoro kuelekea mikoa ya nyanda za juu Kusini. Mara
baada ya kufika eneo la Kitonga lilipinduka chini. Taarifa kutoka kwa baadhi watu
waliokuwa karibu na eneo la tukio hilo zinadai kuwa ajali hiyo ilisababishwa na kufeli
kwa breki za basi hilo huku likiwa katika mwendo mkali. Kulikuwa na abiria 67
ambapo abiria 33 walifariki papo hapo na wengine kujeruhiwa vibaya. Abiria
waliojeruhiwa walikimbizwa haraka katika hospitali ya taifa Muhimbili ambako
wanaendelea kupatiwa matibabu hadi hivi sasa. Hata hivyo, taarifa kutoka hospitalini
hapo zinadai kuwa tayari majeruhi 7 kati ya 34 waliopelekwa hospitalini hapo tayari
wameshaaga dunia na wengine wanaendelea kupatiwa matibabu katika vyumba vya
wagonjwa mahututi.

MASWALI:

41. Kifungu cha habari hapo juu kinahusu nini?


_____________________________________
42. Kwa mujibu wa kifungu cha habari hapo juu nini chanzo cha ajali ya basi
hilo?__________________________________________________________
43. Je, ni watu wangapi wamepoteza maisha kutokana na ajali ya basi
hilo?________________________(Andika jibu lako kwa maneno)

5
44. Je, ni majeruhi wangapi wa ajali hiyo wanaendelea kupatiwa matibabu katika
hospitali ya taifa ya Muhimbili?
______________________________________________________
45. Neno majeruhi kama lilivyotumika katika kifungu cha habari hapo juu lina
maana gani?

You might also like