You are on page 1of 3

OFISI YA RAIS - TAMISEMI

HALMASHAURI YA WILAYA YA UVINZA


MTIHANI WA KUJIANDAA KUMALIZA ELIMU YA MSINGI - 2023
SOMO: KISWAHILI DARASA: VII MUDA: SAA 1:40
MAELEKEZO:
 Mtihani huu una maswali 45
 Jibu maswali yote kama ulivyoelekezwa
SEHEMU A
Sikiliza habari itakayosomwa na msimamizi kisha jibu maswali yanayofuata kwa kuchagua
herufi ya jibu sahihi
1. Habari hii inahusu nini? _______A. umoja B. Tanzania C. utamaduni D. wageni E. ulaya [ ]
2. Nchi gani inasifika kuwa na ukarimu?
A. Asia B. Ulaya C. Amerika D. Tanzania E. India [ ]
3. Ni vipengele vipi vya utamaduni vimetajwa katika habari hii? _______
A. amani na desturi B. upendo na mila C. amani na upendo D. upendo E. mila na desturi [ ]
4. Wageni wanaotoka Tanzania hutoka katika jamii za nchi gani? ______
A. Ulaya tu B. wenyeji wa Tanzania C. Umerika asia na Ulaya D. Uganda na Ulaya E. Asia tu [ ]
5. Kichwa cha habari hii cha faa kiwe ______
A. Mila B. Desturi C. Utamaduni D. Umoja E. Amani [ ]

Katika swali la 6 – 35 chagua herufi ya jibu sahihi kisha iandike kwenye mabano uliyopewa.
6. Katika maneno yafuatayo ipi ni nomino ya dhahani? ________
A. unakuja B. umeenia C. utalima D. uelewe E. ulisoma
7. Neno lipi ni tofauti na mengine?_____ A. embe B. chungwa C. ndizi D. ng’ombe E. papai [ ]
8. “Nitatetema kama Mayele” Kiambishi cha njeo katika neno nitatetema ni kipi? _____
A. nita B. -ta C. te D. –a- E. tema [ ]
9. Walimu walifundisha masomo vizuri. Sentensi hii ipo katika wakati gani? ____
A. uliopita B. ujao C. uliopo D. mazoea E. usiodhihirika [ ]
10. Neno “paka” lina silabi ngapi? _____ A. mbili B. nne C. tano D. moja E. sita [ ]
11. Umoja wa neno nyaraka ni _________
A. waraka B. nyaraka C. miwaraka D. wawaraka E. kanyaraka [ ]
12. Hadi sasa hakuna mtu_________ aliyekamatwa kuhusika na wizi.
A. yoyote B. wowote C. yeyote D. yote E. vyovyote [ ]
13. Mahali ambapo anaishi Rais wa nchi huitwa? _______
A. nyunbani B. makao ya Rais C. ikulu D. ngome E. banda [ ]
14. Neno “kitongoji” lina konsonati ngapi? _______ A. moja B. mbili C. tano D. tatu E. kumi [ ]
15. Wahenga walisema “hakuna marefu yasiyokuwa na ncha” nini maana ya methali hii? ______
A. hakuna kitu kisicho kirefu B. hakuna kitu kisicho na ncha C. hakuna jambo lenye mwanzo mrefu
D. hakuna jambo lisilokuwa na mwisho E. hakuna marefu yasiyokuwa na mafupi [ ]
16. “Angeliamka” mapema asingeliachwa na ndege. Kipi ni kiambishi cha masharti katika sentensi hii? _______
A. –a- B. –nge- C. –ngeli- D. angel E. –ili- [ ]
17. Mzee Juma ameishi Morogoro ____miaka kumi.
A. toka B. kwa C. tangu D. kipindi E. tangia [ ]
18. Ni neno lipi kati ya haya yafuatayo lipo katika kundi la majina?_______
A. mlimani B. peponi C. mweusi D. utoto E. kwaya [ ]
19. Kama ungeliimba vizuri _____ zawadi.
A. ungelipewa B. ungepewa C. ungalipewa D. ungapewa E. ukipewa [ ]
20. Kitabu chako ni kizuri ukienda dukani nami ninunulie ________. Ni kifungu kipi cha maneno kinakamilisha
sentensi hiyo? ___ A. kama hivyo B. kama hiko C. kama hicho D. kama iko E. kama icho [ ]
21. John husafisha eneo lake mpaka muda wa kuingia darasani unapowadia. Neno wadia lina maana gani? ___
A. kuwasili B. kuisha C. kufika D. kusogea E. rejea [ ]
22. Kila mtu atalipitia darasa hili apende asipende. Darasa hili ni lipi ? ________
A. kifo B. elimu ya msingi C. elimu ya awali D. dini E. semina [ ]
23. Mzee Mpili alizunguka mbuyu, nini maana ya nahau zunguka mbuyu? _______
A. kutoa rushwa B. kupiga rushwa C. kupokea rushwa D. kuleta rushwa E. kula rushwa [ ]
24. Mihogo iliyotoka Kidahwe haipikiki, imekaa sana. Neno lililopigiwa mstari liko katika kauli gani ya utendaji?__
A. Kutendeana B. Kutendewa C. Kutenda D. Kutendana E. Kutendeka [ ]
25. Asha “anapia uvivu” maana yake maneno yaliyopigiwa mstari ni ______
A. kutabili kazi B. kula uvivu C. kukaa raha D. kuamka na uvivu E. kukaa huku ukifanya kazi [ ]
26. __________________ mbele kiza. Methali hii inakamilishwa na maneno yapi kati ya haya yafuatayo?
A. Usiku B. Ujinga mwingi C. Werevu mwingi D. Ubishi mwingi E. Upendo [ ]
27. Malizia methali hii. “Mwenda tezi na omo ________”
A. ni mnafiki B. marejeo ngamani C. hafai kwenye raha D. uakufa naye E. hufaidi siku ya iddi [ ]
28. “Gari lile liliendeshwa na mdogo wangu.” Hii ni kauli ya ______
A. kutendeka B. kutendewa C. kutenda D. kutendwa E. kutendana [ ]
29. Tegua kitendawili kisemacho Kondoo wetu ana nyama nje ngozi ndani. ________
A. Nywele na kichwa B. Katani C. Uyoga D. Chungwa E. Filigisi [ ]
30. Siwema ni msichana mzuri lakini ana mkono wa birika. Maana ya nahau iliyokolezwa ni ipi? _____
A. Mchoyo B. Mwizi C. Muongo D. Kusengenya E. Msahaulifu [ ]
31. Tegua kitendawili hiki “bomu la machozi baridi” _______
A. nywele B. moshi C. miguu D. ngozi E. gesi [ ]
32. Maana ya nahau “kufa moyo” ni ipi ? _______
A. kufariki B. kuugua sana C. kuchoka sana D. fia ndani ya moyo E. kukata tama [ ]
33. Samaki mkunje angali mbichi. Methali ipi kati ya hizi ina maana sawa na hii ? ______
A. samaki huanza kuoza kichwani B. ukitaka riba ziba C. jino la pembe si dawa ya pengo [ ]
D. sikio la kufa halisikii dawa E. ngozi ivute ingali maji
34. Methali ipi haifanani na zingine kati ya hizi? ________
A. sikio la kufa halisikii dawa B. chombo cha kuzama hakina usukani
C. siku ya kufa nyani miti yote huteleza D. maji yakimwagika hayazoleki [ ]
35. Maana ya “fuja mali” ni ________
A. kuiba mali B. kutumia mali ovyo C. kuhifadhi mali D. kutumia mali kibali E. kuitumia mali [ ]

SEHEMU B: UTUNGAJI
Panga sentensi zifuatazo katika mfuatano sahihi kwa kizipa herufi A, B, C, D na E.
36. Zima taa ulale, kuna radi sana. [ ]
37. Nilikuwa chumbani kwangu nikisoma kitabu cha hadithi. [ ]
38. Ilikuwa ni wakati wa usiku. [ ]
39. Mara nilimsikia baba akiniita, Bura! Bura! [ ]
40. Siku hiyo kulikuwa na mvuya kubwa iliyoambatana na radi. [ ]

SEHEMU C: USHAIRI - Soma shairi lifuatalo kisha jibu maswali yafuatayo


Ukiwepo darasani, mwalimu msikilize,
Kisichotiwa mizani, angalia usimeze,
Kilopita kipimoni, ndicho ukitekeleze,
Elimu ni ufunguo, kila mtoto sikia.

Mazoezi darasani, yatakufanya uweze,


La kufanya akilini, kuchagua ipendeze,
Uzio ubaini, jamii usipumbaze,
Elimu ni ufunguo, kila mtoto sikia.

MASAWALI
41. Shairi hili lina jumla ya beti ngapi? ......................................................................
42. Taja vina vya mwisho katika ubeti wa kwanza…………………………………………………..
43. Kila ubeti wa shairi hili una mishororo mingapi? ....................................................
44. Ubeti wa pili una mizani mingapi? ……………………………………………………………………
45. Mstari unaojirudiarudia katika kila ubeti unaitwaje? ………………….…..……………………
HABARI YA KUSOMA
Utamaduni ni mfumo wa maisha ya watu na jinsi wanavyoishi na
taratibu zao za kijamii, kiuchumi na kisiasa. Tanzania ni moja ta kati ya nchi
zinazosifika duniani kwa ukarimu, amani na upendo kwa wageni, licha ya
kuwa na makabila zaidi ya mia moja na ishirini ambayo yote hutunza mila na
desturi zao, watanzania wanaishi kwa umoja, upendo na mshikamano. Hali
hiihuwavutia watu wa mataifa mengine na wengine na wengine hupenda
kuishi Tanzania.

Wageni hawa hutoka katika jamii za nchi tofauti zikiwemo zile za Asia,
Ulaya na Amerika.

You might also like