You are on page 1of 7

HALMASHAURI YA WILAYA YA ……….

MTIHANI WA MAJARIBIO YA NUSU MUHULA WA I DARASA LA VI


SOMO: KISWAHILI
Muda: saa 1:30 Machi 2024
SEHEMU A (ALAMA 20)
1. Sikiliza kwa makini habari itakayosomwa na msimamizi kisha jibu kipengele cha i hadi v.
i. Mamba alikuwa rafiki wa nani? A. chura B. mbuni C. samaki D. nungunungu ( )
ii. Mamba alimjibu Rafiki yake sababu gani zilisababisha
koo lake liwashe? A. njaa B. upendo C. vijipele D. ugonjwa ( )
iii. Ni wahusika gani wanazungumziwa katika habari hii?
A. mbuzi na mbuni B. mamba na kenge C. bata na mamba D. mbuni na mamba ( )
iv. Mbuni alimuonesha dawa gani Rafiki yake ili kuliponya koo?
A. majani ya mti B. dawa ya maji C. vidonge D. alimkuna koo ( )
v. Ni kichwa gani kingefaa kwa habari uliyosomewa?
A. mbuni B. urafiki wa mbuni na mamba C. mamba D. koo ( )
2. Chagua jibu sahihi kisha andika herufi ya jibu hilo kwenye mabano
i. “Watoto wanachezea midoli”. Umoja wa sentensi hii ni upi? A. mtoto wanachezea midoli
B. mtoto anachezea midoli C. Watoto wanachezea midoli D. mtoto anachezea mdoli ( )
ii. Mmwalimu amesema kwamba hapendi utoro. Hii ni aina gani ya kauli?
A. kauli halisi B. kauli taarifa C. kauli mazoea D. kauli tegemezi ( )
iii. “Sote tumemuona hapa”. Sentensi hii ipo katika wakati gani?
A. uliopo B. mazoea C. timilifu D. ujao ( )
iv. Kitenzi “amekanyagwa” kikiwa katika kauli ya kutendana kitakuwaje?
A. amekanyagia B. amekanyagiwa C. wamekanyagana D. wamekanyagiana ( )
v. “Sote hatuna budi kupiga vita rushwa kwa maendeleo ya taifa.
Neno “rushwa’ limeundwa na irabu ngapi? A. moja B. mbili C. tatu D. nne ( )
vi. Idadi ya silabi katika mstari wa shairi huitwa: A. vina B. mishororo C. ubeti D. mizani ( )
vii. Herufi I U B N D zikipangwa zinaleta neno lipi sahihi?
A. BINDU B. NDIBU C. BUNDI D. IUNDB
viii. “Fuata wema upate mema” methali ipi inafanana
kimaana na methali hii? A. tenda wema uende zako usingoje shukrani B. ukitaka
wema tenda mema C. fuata nyuki upate asali D. amani haiji ila kwa ncha ya upanga ( )
ix. Methali inayokinzana na methali isemayo, meno ya mbwa
hayaumani ni ipi kati ya hizi?... A. akili ni nywele kila mtu ana zake B. udugu kufaana na sio
kufanana C. damu nzito kuliko maji D. mtegemea cha nduguye hufa masikini ( )
x. Tegua kitendawili hiki, “amebeba mishale kila
anapokwenda” A. mwiba B. nanasi C. nyasi D. nungunungu ( )

3. Oanisha maneno ya kifungu A na yale ya kifungu B ili kuunda maana kamili.


KIFUNGU A JIBU KIFUNGU B
i. Kisawe cha neno gulio ( ) A. Maneno makali
ii. Kinyume cha neno rudi ( ) B. Nenda
iii. Soni ( ) C. Mnada
iv. Ana ulimi wa upanga ( ) D. Aibu
v. Mamba ( ) E. Kigwena
SEHEMU B (ALAMA 20)
4. Panga sentensi kwa kuzipa herufi A, B, C, D, E ili zilete mpangilio mzuri. (Kila kipengele kina alama 2)
i. Kengele ya kukusanyika ililia na mwalimu wa zamu alitoa matangazo. ( )
ii. Siku hiyo wanafunzi waliwahi kufika shuleni. ( )
iii. Walipoingia tu, walianza kujifunza wakiongozwa na walimu. ( )
iv. Walifanya usafi wa mazingira wakiongozwa na viranja. ( )
v. Baada ya matangazo wanafunzi waliingia darasani kwa ukakamavu. ( )

5. Soma habari hii kisha jibu kipengele cha i hadi v.


Mimi ninaitwa Ujima. Ni mfumo wa kwanza wa kiuchumi na kiutawala ambapo watu waliishi
na kushirikiana pamoja. Kila jambo hapa duniani lilipitia katika mfumo huu. Katika mfumo huu
umiliki wa mali kama mifugo na ardhi ulikuwa wa pamoja, hivyo hapakuwa na umiliki binafsi,
hapakuwa na ubaguzi wala matabaka baina yetu. Watu wote walikuwa sawa bila kujali jinsi au
rika. Hapakuwa na mgawanyiko wa kazi katika kutengeneza zana, uwindaji na ukusanyaji wa
matunda.

Pia katika mfumo huu zana zilikuwa duni sana kwa sababau zilitengenezwa kwa mawe na miti.
Hii ilisababisha kuwepo kwa uzalishaji mdogo. Katika mfumo huu hapakuwa na biashara wala
kubadilishana bidhaa baina ya watu katika jamii kwa sababu hakukuwa na ziada wakati wa
kuzalisha.

Uongozi ulikuwa mikononi mwa rika ambapo muundo wa majukumu katika jamii ulifanana na
hapakuwa na unyonyaji wala ukandamizaji miongoni mwa watu. Jamii ambazo ziliishi katika
ujima ni wasandawe, wahadzabe na watindiga kutoka jamii za kitanzania.
MASWALI
i. Pendekeza kichwa kinachofaa kwa habari uliyoisoma ……………………………………...
ii. Taja sifa mbili za mfumo zilizozungumziwa katika habari hii.
i. …………………………………………… ii. …………………………………………….
iii. Ni vifaa gani vilitumika kutengenezea zana wakati wa mfumo uliozungumziwa?
………………………………………………………………………………………………..
iv. Unafikiri ni kwa nini hapakuwa na biashara wala kubadilishana bidhaa baina ya watu katika
jamii kipindi cha mfumo huu? ………………………………………………………..
v. Ni jamii zipi za kitanzania ziliishi katika mfumo uliozungumziwa katika habari hii?
………………………………………………………………………………………………..
SEHEMU C (ALAMA 10)
6. Wewe ni Malenga uliyebobea katika kazi yako, Shairi lifuatalo limeandikwa bila kuzingatia
alama za uandishi. Liandike upya kwa kuweka alama zote zilizokosekana.

Matunzo yalo muhimu palizi hata mbolea


Maji yasiwe adimu kumbuka kupogelea
Na viwavi wasidumu kusitisha ghasia
Maua ni kitu bora mazingira kuyapamba
Bayana kukutajia utajiri natangaza
……………. DISTRICT COUNCIL
………… PRIMARY SCHOOL
STANDARD VI MID-TERM TEST - ENGLISH LANGUAGE
Time: 1:30 hours March 2024

SECTION A: ANSWER ALL QUESTIONS ACCORDING TO THE INSTRUCTION GIVEN


(Each item carries 1 marks)
1. Listen carefully to the passage read by the invigilator and then answer item i to v
i. To whom does Rahma live? A. her mother
B. her father C. her parents D. her aunt E. her relatives ( )
ii. Where do Rahma and her aunt live? A. at Michungwani village B. at Uhuru village
C. at Lundamatwe village D. in Ilengititu town E. at Mwembechai village ( )
iii. Where did Rahma go on the mentioned day?
A. to the market B. to school C. home D. her aunt E. at Mwembechai village ( )
iv. How Rahma rides? A. careless B. carefully C. attentively D. fastest E. slowly ( )
v. What things did Rahma go to buy? A. B. flour and sugar
C. cooking oil and water D. buns and cakes E. mangoes and bananas ( )
2. Choose the most correct answer and write its letter in the bracket provided
i. I usually…………… to the church on Sunday. A. going
B. go C. goes D. Gone E. am going ( )
ii. We …… playing football at the moment. A. was B. were C. is D. are E. Have ( )
iii. She has ……. all the food. A. eat B. eating C. ate is eating E. eaten ( )
iv. Does he ……. football? A. play B. plays C. playing D. played E. will play ( )
v. My uncle ……………………. at home yesterday. A. arrives
B. arrived C. arrive D. has arrived E. will arrive ( )
3. Choose the correct word from the bracket to fill in tha blanks
i. ………………………. you work hard, you will pass your examination. (Unless, If, Either)

ii. This house is ……………………………………..… It belongs to us. (ours, we, ourselves)

iii. The girl ……………….……..you were talking about is my cousin. (which, whom, whose)

iv. She is …………………………..……………….……young to get married. (so, too, much)

v. She cut herself ………………… a knife while she was preparing potatoes. (in, with, from)

4. Match the items of list A with the corresponding word from list B by writing the
letter of the correct answer in the baracket provided
Item List A Answer List B
i. Mwajuma is my uncle’s wife ( ) A. Sad
ii. Our cow has just given birth to a ( ) B. April
iii. Desks, chairs and tables ( ) C. Aunt
iv. What is the opposte of the word ( ) D. Calf
happy E. Furniture
v. A month comes after March ( )
SECTION B: COMPOSITION (10 MARKS)
5. arrange the sentences below by using letters A, B, C, D and E to get a logical story

i. It is found in Tanzania country. ( )


ii. And it is an attractive area for tourist. ( )
iii. The highest peak of Mount Kilimanjaro is 5,895 meters high ( )
iv. It has two snow peaks, Kibo and Mawenzi. ( )
v. Mount Kilimanjaro is the highest Mountain in Africa. ( )
SECTION C: (20 MARKS)
6. Fill in the blanks with the correct word

i. Is there ……………………………… water in the bucket?

ii. The thief entered in the kitchen …………………………. the window.

iii. That is ………………………….. car. It is mine.

iv. Where …………………………… you going?

v. He travelled ………………….. car from Mwanza to Iringa.

7. Read the following passage then answer item i to v.

Irene and Moureen are twins. They live in Kyela. They are in class three at
Kajunjumele Primary school. Their sister Eliza is in class five at Itunge Primary School.
It is a boarding school.
One day Irene and Moureen decided to write a letter to their sister. They wanted to tell her
about their progress in studies.

QUESTIONS

i. What are the twin’s names? ........................................................

ii. What is their sister’s name ..........................................................

iii. Where do the twins live ..............................................................

iv. What is the name of their school? ...............................................

v. What is Eliza’s school name? .....................................................


HALMASHAURI YA WILAYA YA ………….
MTIHANI WA MAJARIBIO YA NUSU MUHULA WA I DARASA LA VI
SOMO: SAYANSI NA TEKNOLOJIA
Muda: saa 1:30 Jina la mtahiniwa: Machi 2024
SEHEMU A: MASWALI YA KUCHAGUA (ALAMA 20)
1. Chagua kisha andika herufi ya jibu sahihi kwenye mabano
i. Hewa ni maada yenye sifa mbalimbali. Je, ni ipi siyo sifa ya hewa? A. haionekani B. ipo katika hali
ya gesi na inachukua nafasi C. ina uzito D. haina rangi wala harufu E. haipitishi sauti ( )
ii. Wanafunzi wa darasa la tatu walikuwa wakijadiliana juu ya tabia mbalimbali za mwanga. Je, nini
hutokea pale mwale wa mwanga unapotoka media moja kuingia media nyingine?
A. hupinda B. huakisiwa C. husharabiwa D. hutawanyika E. hutawanyika ( )
iii. Huduma ya kwanza ni msaada wa haraka anaopatiwa majeruhi au mtu aliyeugua ghafla.
Je, utampa huduma ya kwanza gani mtu aliyepatwa na kwikwi? A. kulala chali
B. kujilowanisha kichwani C. kuoga maji D. kuziba pua E. kulalia ( )
iv. Utabiri wa matokeo ya jaribio au uchunguzi kabla ya kufanya uchunguzi wa kisayansi hujulikana
kama: A. kukusanya data B. hitimisho C. dhanio D. kugundua tatizo E. uchunguzi ( )
v. Karibia wanyama wote hupumua gesi ya oksijeni ambayo ina 20.9% angani lakini gesi hiyo
haipungui angani. Je, ni nini chanzo kikuu cha uzalishaji wa gesi hii angani?
A. wanyama B. mitungi ya gesi C. moto D. mimea E. uzalishaji viwandani ( )
vi. Wanafunzi wa darasa la tano walikuwa wakijadiliana kuhusu vifaa vinavyounda
tarakilishi ya mezani. Je, ni kifaa kipi hakihusiki kati ya hivi vifuatavyo?
A. kashamfumo B. kiteuzi C. kibodi D. monita E. printa ( )
vii. Kifaa ambacho hutumika kuonesha kazi inayofanyika au taarifa iliyomo ndani ya tarakilishi kinaitwa
A. kiteuzi B. kibodi C. kasha mfumo D. skirini au monita E. kichakato kikuu ( )
viii. Vifaa vinavyotumika kutoa taarifa kutoka kwenye tarakilishi huitwa vitumi toleo. Je, kipi kati ya
vifuatavyo siyo kitumi toleo? A. skana B. monita C. spika D. printa E. kipaza sauti ( )
ix. Ni gesi gani huhitajika na mmea ili kuweza kutengeneza chakula?
A. kabonidaiyoksaidi B. oksijeni C. naitrojeni D. haidrojeni E. salfu ( )
x. Ni ogani ipi ambayo inahusika kuchuja damu na kuondoa takamwili kwa njia ya mkojo?
A. ini B. ngozi C. kibofu D. mapafu E. figo ( )
2. Oanisha jibu sahihi kutoka kifungu A na kifungu B kwa kuandika jibu lako kwenye kisanduku

KIFUNGU A HERUFI KIFUNGU B.


i. Husafiri katika uelekeo wote ( ) A. Mwezi
ii. Husafiri katika mstari ulionyooka ( ) B. Jua
iii. Sauti iliyoakisiwa ( ) C. Sauti
iv. Kupinda kwa mwanga wakati unapopita kwenye midia tofauti. ( ) D. Mwanga
v. Ni chanzo kikuu cha nishati na mwanga ( ) E. Kupinda
F. Mwangwi
3. Andika jibu sahihi kukamilisha sentensi zifuatazo. (Kila kipengele kina alama 1)
i. Kitu chochote chenye uzito na kinachochukua nafasi huitwa: ……………………………………...
ii. Kitendo cha mizizi ya mmea kuota na kukua kuelekea kwenye maji huitwa: ……………………...
iii. Ni aina ipi ya udongo wenye chembechembe ndogo sana zinazotokea kutokana na mmomonyoko
wa miamba kutokana na athari za hali ya hewa? …………………………………………………..
iv. Hali ya kifaa cha umeme kuzuia umeme kutiririka huitwaje? …………………………………………
v. Kani ya msukumo wa umeme hupimwa kwa kifaa kinachoitwa: …………………………………………...
SEHEMU B: MASWALI YA MAJIBU MAFUPI (ALAMA 20)
4. Andika majibu sahihi kwenye nafasi ulizopewa. (Kila kipengele kina alama 2)
i Wanafunzi wa darasa la tano walikuwa wakijadiliana mishipa mbalimbali ya dam una kazi zake.
Je, ni mshipa upi waliubaini kwamba ndio mkuu ambao hutoa damu safi kwenye moyo na kuipeleka
sehemu mbalimbali za mwili? ……………………………………………………………
ii Kabonidayoksaidi na maji ya ziada ni takamwili itolewayo nje ya mwili wa mamalia na ogani ipi?
……………………………………………………………………………………………………….
iii Katika mfumo wa mmeng’enyo wa chakula, ni ogani ipi ambayo husharabu chakula?
………………………………………………………………………………………………………

5. Andika majibu sahihi kwenye nafasi ulizopewa. (Kila kipengele kina alama 2)

i. Joto husafiri kwa njia gani katika maada yabisi? …………………………………………………...


ii. Mamba na kenge ni baadhi ya Wanyama wenye uti wa mgongo. Je, Wanyama hawa hupatikana
katika kundi lipi? …………………………………………………………………………………..
iii. Ni kifaa gani ambacho hutumika kuhifadhi chakula katika hali ya ubaridi? ……………………….

6. Andika majibu sahihi kwenye nafasi ulizopewa. (Kila kipengele kina alama 2)

i. Wadudu huzaliana kwa kutaga mayai ambayo huanguliwa na kutoa viumbe hai vinavyofanana
na wadudu hao. Taja hatua za ukuaji wa mende kutoka hatua ya mwanzo hadi hatua ya mwisho.
………………………………………………………………………………………………………………..
ii. Kitendo cha mmea wa kijani kujitengenezea chakula chake huitwa: ……………………………….
iii. Jumla ya vutu vyote vinavyotuzunguka huitwa: …………………………………………………….
iv. Mkasi ni mashine rahisi ambayo inapofanya kazi egemeo huwa katikati ya mzigo na jitihada.
Je, mashine hii ni wenzo daraja la ngapi? …………………………………………………………...
SEHEMU C: MASWALI YA MAJIBU MAFUPI (ALAMA 10)
7. Jibu vipengele vyote kwa kufuata maelekezo ya swali. (Kila kipengele kina alama 2)

i. Tofauti ya potenshali katika ncha za waya ni volti 12. Kiasi cha mkondo wa umeme unaopita ni
ampia 0.4. Je, waya huo una ukinzani wa ohm ngapi? ……………………………………………..
ii. Roda huru moja ikitumika na roda tuli manufaa ya kimakanika na uwiano wa mwendo dhahiri huwa
na thamani inayolingana ambayo ni ngapi? …………………………………………………..

8. Chunguza michoro ifuatayo kisha jibu maswali yanayohusu michoro hiyo.


A
i. Taja jina la sehemu iliyoooneshwa kwa herufi C. …………………………….
B
ii. Eleza kazi ya sehemu iliyoooneshwa kwa herufi A.
C
…………………………………………………………………………………
D
………………………………..……..................................................................

iii. Taja kazi kuu ya kitumi hicho cha


tarakilishi.…………………………………
….…………………………………………
………….…………………………………
…………………..
UFAHAMU WA KUSIKILIZA

Siku moja mbuni alikuwa akipita kando ya mto. Alitaka kunywa maji na kumsabahi rafiki
yake. Mamba akajitokeza ukingoni mwa mto, wakaanza kuongea. Walipokuwa
wakizungumza, mbuni aligundua kuwa sauti ya mamba haikuwa ya kawaida. Ilikuwa
inakwaruza kidogo. Akamuuliza, “rafiki yangu mbona leo sauti yako imebadilika?” Mamba
akajibu, ‘ndiyo! Koo langu linawasha ninatamani kulikuna lakini kila nikiingiza vidole
havifiki huko. Labda pana vijipele vidogo. Mbuni akasema “pole sana, chuma majani ya mti
ule! Uyatumie”.

UFAHAMU WA KUSIKILIZA

Siku moja mbuni alikuwa akipita kando ya mto. Alitaka kunywa maji na kumsabahi rafiki
yake. Mamba akajitokeza ukingoni mwa mto, wakaanza kuongea. Walipokuwa
wakizungumza, mbuni aligundua kuwa sauti ya mamba haikuwa ya kawaida. Ilikuwa
inakwaruza kidogo. Akamuuliza, “rafiki yangu mbona leo sauti yako imebadilika?” Mamba
akajibu, ‘ndiyo! Koo langu linawasha ninatamani kulikuna lakini kila nikiingiza vidole
havifiki huko. Labda pana vijipele vidogo. Mbuni akasema “pole sana, chuma majani ya mti
ule! Uyatumie”.

LISTENING COMPREHENSION

Rahma lives with her aunt at Mwembechai village. One day she went to the market
on a bicycle to buy mangoes and bananas. Alyays she rides carefully to avoid road
accident.

LISTENING COMPREHENSION

Rahma lives with her aunt at Mwembechai village. One day she went to the market
on a bicycle to buy mangoes and bananas. Alyays she rides carefully to avoid road
accident.

You might also like