You are on page 1of 7

ELIMU PLUS EXAMINATIONS

STANDARD VII EXAMINATION

KISWAHILI

MUDA: SAA 1:40 Volume…….1


MAELEKEZO:
1. Mtihani huu una Sehemu A, B, na C zenye maswali Arobaini na tano (45)

2. Jibu maswali yote katika kila sehemu ya mtihani huu

3. Weka kivuli katika kila tarakimu ya namba yako ya mtihani kwenye nafasi
husika fomu ya OMR

4. Weka kivuli kwenye herufi ya jibu lililosahihi kwa swali 1-40. Kwa mfano jibu
ni C weka kivuli kama ifuatavyo.

(A) (B) (C) (D) (E)

5. Tumia penseli ya HB tu kujibu swali la 1 hadi la 40, na kalamu ya bluu au nyeusi


kwa swalu la 41 hadi 45

6. Simu ya kiganjani hairuhusiwi ndani ya chumba cha mtihani.

_______________________
ElimuplusExams Volume…1
SEHEMU A: (ALAMA 35)
Sikiliza kwa makini kifungu cha habari utakachosomewa kisha jibu maswali 1-5
kwa kuchagua jibu sahihi.

1. Ni serikali gani iliyoisamehe Tanzania deni la Dola za Marekani Milioni 203


(A) Kenya (B) Uganda (C) Marekani ( D) Brazili (E) Tanzania

2. Ni Waziri gani wa Tanzania aliyesaini mkataba kwa niaba ya


Tanzania?____________ (A) John Kijazi (B) Ummy – Mwalimu
(C) Emmanuel Nchimbi (D) Sonia Portella (E) Mwakyi Mwandosia

3. Mkopo waliosamehewa Tanzania na Brazili ulikuwa ni kwa ajili ya kujenga


barabara ya Morogoro-Dodoma mwaka______________________
(A) 1979 (B) 1797 (C) 2017 (D) 2007 (E) 1977

4. Ni Rais gani alikuwa Madarakani wakati Tanzania inasamehewa deni lake


na Brazili ? ________________________ (A)Wiliam Mkapa (B) John Pombe
Magufuli (C) Jakaya Kikwete (D) Samia Suluhu (E) Ally Hassani Mwinyi

5. Balozi Nchimbi__________________ Serikali ya Brazili kwa msamaha huo.


(A) Alichukia (B) Alisaidia (C) Alishukuru (D) Alikubali (E) Alilia

Chagua Herufi ya Jibu sahihi

6. Wanne wamenusurika dunia katika ajali ya treni iliyotokea mkoani


Dodoma. Neno wanne katika sentensi hii limetumika kama aina gani ya
kiwakilishi ?
(A) Wakati (B) Idadi (C) Kimilikishi (D) Kioneshi (E) Sifa

7. Katika neno ‘’wanasoma’’ kiambishi kinacho onyesha njeo ni kipi ?


(A) Mwerevu wa- (B) Upole wana (C) –na- (D) –som- (E) a

8. Mwanaume Yule amenyeshewa na mvua. Sentensi hii ipo katika aina gani
ya kauli katika kauli za utendaji.
(A) Kutenda (B) Kutendeka (C) Kutendewa (D) Kutendwa (E) Kutendea

9. Asha, Mwantumu, Mimi na Rozi tutafanya mtihani wetu wa kumaliza Elimu


ya msingi mwezi Agosti. Sentensi hii ipo katika nafsi ya ngapi ? (A) Kwanza
wingi (B) Tatu wingi (C) Pili wingi (D) Tatu umoja (E) Kwanza umoja.

10. Wingi wa neno jipya ni mapya. Je umoja wa neno ‘’Madhumuni’’ ni lipi kati
ya maneno yafuatayo? (A) Dhumuni (B) Madhumuni (C) Thumini
(D) Mathumuni (E) Mazumuni

_______________________
ElimuplusExams Volume…1
11. Mahali wanapo wekwa watuhumiwa ilikusubiria kesi zao kusikilizwa
huitwa?_______________
(A) Kizimbani (B) Kanisani (C) Mahakamani (D) Mahabusu (E) Gerezani

12. Kipande cha chuma kinachopigiliwa mlangoni, dirishani ili kuweza


kufungua na kufunga huitwa? _____________________
(A) Chomeko (B) Bawabu (C) Engo (D) Bawaba (E) Shata.

13. Mjomba Alex amenunua mbuzi wa maziwa neno lililopigiwa mstari


limetumika kama_________________
(A) Kielezi (B) Kihisishi (C) Kihusishi (D) Kiunganishi (E) Kivumishi.

14. Samaki wanaofugwa kwenye_________________la shule hawaruhusiwi


kuvuliwa ovyo.
(A) Leso (B) Pojo (C) Fuo (D)Lambo (E) Rodi.

15. Ili nyama isioze ni vema ihifadhiwe kwenye_________________________


(A) Jarife (B) Nduli (C) Jokofu (D) Pantone (E) Bucha

16. Katika maneno yafuatayo neno lipi lina maana sawa na neno “Posho”
(A) Kifungua kinywa (B) Ajira (C) Mshahara (D) Motisha (E) Tija.

17. Wanakijiji wa Mtakuja watachagua viongozi wa kijiji chao mapema.


Sentensi hii ipo katika wakati gani ?
(A) Uliopo (B) Unaoendelea (C) Ujao (D) Uliopita (E) Mtimilifu

18. Mimi sitahudhuria kabisa katika sherehe ile.Andika katika kauli taarifa ya
sentensi hii. (A) Alisema kwamba mimi sitahudhuria sherehe ile (B) Alisema
kwamaba yeye atahudhuria sherehe ile (C) Alisema” sitahudhuria
sherehe ile” (D) Alisema mimi sitahudhuria sherehe ile (E) Yote ni sawa.

19. Nomino tembo iko katika ngeli ya A-WA. Je,nomino ugonjwa ipo katika
ngeli gani?
(A) KI-VI (B) A-WA (C) U-YA (D) LI-YA (E) U-ZI

20. Kijana aliyegongwa na gari amefariki dunia. Hii ni sentensi gani kati ya aina
za sentensi?
(A) Ambatano (B) Tegemezi (C) Sahili (D) Changamano (E) Shurutia.

21. Kipi ni kinyume cha neno aghalabu, kati ya maneno yafuatayo?


(A) Ukwasi (B) Ukata (C) Rambirambi (D) Nadra (E) Ughaibuni

_______________________
ElimuplusExams Volume…1
22. Nyumba hii ina ________________ nyingi sana ndani. Lipi ni neno sahihi
linalokamilisha sentensi hii kwa usahihi.
(A) Thamani (B) Samani (C) Thamani (D) Dhamani (E) Zamani

23. Neno kadamnasi linajumla ya vokali ngapi?


(A)Mbili (B) Tano (C) Nne (D) Moja (E) Tatu.

24. Paa la shule limeezuliwa na upepo. Sentensi hii ipo katika kauli gani?
(A) Kutendwa (B) Kutendewa (C) Kutendea (D) Kutendeka (E) Taarifa

25. Maana ya neno adili ni utu wema. Je maana sahihi ya neno“tamalaki ni


(A) Tawanya (B) Tawala (C) Thibiti (D) Huduma (E) Chukua

26. Yusufu alipandwa na “ghadhabu” Nini maana halisi ya neno ghadhabu?


(A) Hadhabu (B) Chuki (C) Hasira (D) Woga (E) Aibu

27. Kifungu kipi cha maneno kinakamilisha methali ifuatayo kwa usahihi?
Mambo ni kingaja (A)Vitendo si kingaja (B) Mazoea huleta dharau
(C) Huenda yasije (D) Huenda yakaja (E) Tusiyasubirie sana

28. Chego ana shingo ngumu. Maana sahihi ya sentensi hii “kuwa na shingo
ngumu’’ ni__________________ (A)Kutokugeuka kwa shingo (B) Kuwa
mvumilivu (C) Kuwa mkaidi (D) Kuwa kigeugeu (E) Kuwa na shingo ndefu

29. Kiangazi chote na lala usingizi yakija masika nakesha,Tegua kitendawili hiki
(A) Mvua (B) Siku (C) Samaki (D) Jua (E) Chura

30. Wakazi wa mabondeni walianua malago baada ya nyumba zao


kuzingirwa na maji. Maana ya nahau anua malago ni_________________
(A) msaada (B) Kulalama (C) Kusikitika (D) Kuhama (E) Kubomoka.

31. Ana hupenda sana kuchagua vitu na mara nyingi huambulia vitu vibovu.
Je ni methali ipi kati ya zifuatazo inasadifu maelezo hayo?
(A) Ukitaka kuruka agana na nyongo (B) Mchagua nazi huibukia koroma
(C) Lisilokuwa na budi hutendwa (D) Mtaka cha uvunguni sharti uiname
(E) Mgaa na upwa hali wali mkavu.

32. Tegua kitendawili, Kwa mfalme hawa wanatoka hawa wanaingia. Jibu
lake ni________________________
(A) Nywele (B) Miguu (C) Nyuki mzingani (D) Moyo (E) Zipu

_______________________
ElimuplusExams Volume…1
33. Vitendawili vifuatavyo jibu lake ni kinyonga, Isipo kuwa kimoja, nacho ni kipi
?
(A) Huuwawa na uzazi wake (B) Humshindi Rosa kwa mavazi
(C) Tajiri wa rangi (D)Bibi kafa kaniachia pete
(E) Akitembea huringa hata akiwa hatarini.

34. Methali inayofanana na nguzo moja haijengi nyumba ni______________


(A) Kidole kimoja hakivunji chawa (B) Ahadi ni deni (C) Baniani mbaya
kiatu chake dawa (D) Mgonjwa haulizwi dawa (E) Kuuliza si ujinga

35. Malizia methali ifuatayo; Mimi nyumba ya udongo______________________


(A) kujengea (B) Hubomoka mapema (C) Watu wanaishi
(D) Si himili kishindo (E) Hufaa kuegemea

SEHEMU B: (ALAMA 05)


Panga sentensi zifuatazo kwa mtiririko sahihi kwa kuzipa herufi A,B,C,D na E

36. Kusoma habari tena kwa mara ya pili

37. Kupitia ufupisho wa habari ilikuondoa makosa

38. Kuandika ufupisho wa habari

39. Kusoma habari yote ilikubaini mawazo

40. Kubaini wahusika katika habari

_______________________
ElimuplusExams Volume…1
SEHEMU C (ALAMA 10) USHAIRI
Soma shairi hili kwa makini kisha jibu maswali yafuatayo.

Ewe ulo na busara, fikiri bibi na bwana,


Fikiri lilo tohara, na lile lilodhamana,
Pia fikiri izara, na ujana una mwisho,
Sihadawe na ujana, na ujana una mwisho,

Ujana ni jambo bora, umempamba rabana,


Tena umetia fora, ulitendalo hufana,
Basi usiwe mkora, akiba iweke sana,
Sihadawe na ujana, ujana una mwisho,

Kuweka jambo dharura, jikimu kuweka mwana


Siyo pato kulipura, kwa usiku na mchana
Ukitoweka ajura, elewa umekubana
Sihadawe na ujana, na ujana unamwisho

MASWALI
41. Badala ya kutumia neno Rabana mwandishi angeweza kutumia neno
gani?___________________________________________________________________
_________________________________________________________________________

42. Andika mizani za Shairi


hili_______________________________________________________________________
_________________________________________________________________________

43. Mwandishi wa Shairi hili ametumia aina gani ya


Kituo?___________________________________________________________________
_________________________________________________________________________

44. Vipi ni vina vya kati katika ubeti wa


tatu?____________________________________________________________________
_________________________________________________________________________

45. Mwandishi wa Shairi hili anatoa wosia kwa


nani?____________________________________________________________________
_________________________________________________________________________

_______________________
ElimuplusExams Volume…1
UFAHAMU WA KUSIKILIZA
Soma ufahamu kwa makini; Soma
mara tatu. (3)
Serikali ya Brazili imeisamehe Tanzania
deni la Dola za Marekani milioni 203 sawa
na shilingi bilioni 445 lililo tokana na
mkopo uliotolewa kwa ajili ya ujenzi wa
Barabara ya Morogoro-Dodoma mwaka
1979.
Balozi wa Tanzania nchini Brazili, Dk.
Emmanuel Nchimbi alisaini mkataba huo
kwa niaba ya Tanzania huku Wakili wa
Hazina ya Taifa, Dk. Sonia Portella Nunes
akisaini kwa niaba ya Serikali ya Brazili.
Balozi Nchimbi aliishukuru serikali ya Brazili
kwa msamaha huo ambao alisema
umeunga mkono jitihada za Rais Samia
Suluhu za kujenga uchumi imara kwa
Tanzania.
Aliihakikishia Brazili utayari wa Tanzania
katika kuimarisha ushirikiano wa kibiashara
na kiuchumi na Taifa hilo la Brazili.

_______________________
ElimuplusExams Volume…1

You might also like