You are on page 1of 2

HALMASHAURI YA WILAYA YA URAMBO

MTIHANI WA MAJARIBIO

URAIA NA MAADILI DARASA LA TATU

MWEZI WA PILI 2023

1.SEHEMU A:chagua herufi ya jibu sahihi.

i.Matendo ya kujipenda ni __________.

(A)kupigana (B)kutukana (C) kupiga mswaki ( )

ii.Jumla ya mambo yote yanayotuzunguka huitwa _______________.

(A)nyumba (B)vichaka (C)mazingira ( )

iii.Bendera ya taifa ina rangi ______________.

(A)1 (B)4 (C)3 ( )

iv.Lugha ya taifa letu ni ________________.

(A) kiswahili (B)kiingereza. (C)kisukuma ( )

v.Faida mojawapo ya kuwashirikisha watoto katika kufanya maamuzi ni ____________.

(A)kuleta upendo na umoja (B)kuleta upendeleo (C)kuleta ugomvi ( )

vi.Wimbo wa taifa unapoimbwa shuleni tunatakiwa _______________.

(A)tukae chini. (B)tutulie na kusimama wima. (C)tukimbie haraka mstarini ( )

vii.____________ ni uwezo alionao mtu ambao humwezesha kufanya jambo.

(A)kipaji. (B)utamaduni (C)mwenge ( )

viii.Vitu vinavyotambulisha Taifa ni ____________.

(A)alama za miti (B)alama za taifa (C)maji. ( )

ix.Matendo yanayojumisha kujipenda na kujivunia shule ni______________.

(A)kutunza mazingira ya shule (B)kutoroka shuleni (C)kupigana shuleni( )

x.Wimbo wa Tanzania, Tanzania una beti ____________.

(A)Moja (B)mbil. (C)nne ( )


2.SEHEMU B:Oanisha sehemu "A" na "B" Ili kuleta maana iliyo sahihi

Fungu A Fungu B

i. Matendo ya kuwapenda wengine (A)Nembo ya shule,wimbo wa shule,sare


za shule na kauli mbiu .

(B)Kujithamini na kujikubali
ii.Matendo ya kujipenda
(C) theUchafu wa mwili na mavazi
iii.Kujipenda
(D)Kuoga na kufua nguo
iv.Vitu vinavyoitambulisha shule
(EKuwasiliana kwa lugha inayofaa
v.Matendo ya kutojipenda
(F)Kufyeka nyasi.

3SEHEMU C:Andika KWELI kwenye sentensi iliyosahihi na SI KWELI kwenye sentensi


isiyosahihi.

i.Kunawa kimono kwa sabuni baada ya kutoka chooni ni matendo ya kijijali_________.

ii.Wakati wa baridi tunapaswa kuvaa nguo nyepesi na kutembea kwenye mvua bila
mwanvuli_____________.

iii.Ugomvi,kutoamininika na kukosa amani ni mambo ya msingi katika maisha____________.

iv.Kupanda maua na miti ni utunzaji wa mazingira_______________.

v.Watu wanaowajibika kutunza rasilimali za shule ni walemavu____________.

4.SEHEMU D:Jaza nafasi zilizoachwa wazi kwa kuchagua jibu kutoka kwenye kisanduku

Sarafu,saa kumi na mbili asubuhi,uhuru,malezi,Raisi,saa kumi na mbili jioni

i.Bendera ya ___________ni ya rangi ya kijani kibichi.

ii.Kuna aina kuu mbili za fedha nazo ni noti na ___________.

iii.Maneno yanayoonekana kwenye nembo ya Taifa ni umoja na______________.

iv.Shule ni sehemu ya jamii inayowapatia watoto elimu na ______________ bora.

v.Bendera ya Taifa hupandishwa_______________.

You might also like