You are on page 1of 4

HUDAIBYA EXAMINATION COMMITTEE (HEC)

CHAMAZI ISLAMIC SEMINARY


KIDATO CHA TATU – MTIHANI MUHULA WA PILI
021 - KISWAHILI

MUDA:MASAA 3:00
MAELEKEZO
01. Mtihani huu una sehemu A, B na C.
02. Jibu maswali yote toka sehemu A, B na maswali mawili (2 ) kutoka sehemu C.
03. Fuata maelekezo ya kila sehemu.
04. Andika jina katika kila karatasi ya kujibia.

SEHEMU A: ( ALAMA 15)


SARUFI NA UTUMIZI WA LUGHA
Jibu Maswalil yote.
1. Chagua herufi ya jibu sahihi katika vipengele (i) hadi (x) kisha andika herufi ya jibu
hilo katika karatasi yako ya kujibia
i. Ni vazi la nje la kazi za kifasihi ambayo hutumika kuelezea yaliyomo ndani ya
kazi hiyo
a) Wahusika
b) Fani
c) Falsafa
d) Maudhui
ii. Kusoma kwake kwa bidii kumempatia mafanikio neno kusoma ni
a) Kitenzi
b) Kitenzi kisaidizi
c) Kitenzi jina
d) Kitenzi kikurupushi
iii. Ni taratibu zipi zinazofuatwa na lugha fasaha
a) Kimaana, kimatamshi, kilafudhi, kimuundo
b) Kimatamshi, kimofolojia, kiufundi, kimaana
c) Kimatamshi, kimaana, kimuundo, kimantiki
d) Kimantiki, kifonolojia, kimaana na kilafudhi
iv. Mtindo unaotumika kuandika maana ya vidahizo hujulikana kama
a) Kiarifu
b) Kidatu
c) Lugha kienzo
d) Kibadala
v. Katika mjengo wa tungo ni aina gani ya tungo iliyo kubwa kuliko neno na ni
ndog kuliko tungo sentensi
A. Mofimu
Page 1 of 4
B. Tungo sentensi
C. Kishazi
D. Kikundi
vi. Katika uandishi wa matangazo mwandishi anapaswa azingatie mambo
yafuatayo isipokuwa:
a) Kichwa Cha tangazo
b) Anuani ya mwandishi wa tangazo
c) Kutaja aina ya bidhaa au huduma
d) Kuzingatia picha ya mhusika wa tangazo
vii. Nguvu inayotumika katika utamkwaji wa silabi za kiswahili
a) Kiimbo
b) Mkazo
c) Kidatu
d) Lafudhi
viii. Nasema Toka! Toka toka nasema Toka. Katika kipengele Cha lugha kauli
hiyo ipo katika aina Gani ya semi??
a) Tanakali sauti
b) Mdokezo
c) Sitiari
d)Takriri
ix. Kundi la sarufi linalohusika na maana ya misamiati hujulikana kama :
a) Sintaksia
b) Semantiki
c) Fonolojia
d) Mofolojia
x. Utata katika lugha huweza kutatuliwa na mambo yafuatayo isipokuwa
a) Kutumia maneno yenye lugha za picha
b) Kuzingatia alama za uandishi
c) Kutotumia maneno yenye maana zaidi ya Moja
d) Kutotumia maneno yenye viambishi vya kauli ya kutendea
2. Oanisha maana ya maneno katika orodha A kwa kuchagua herufi ya jibu sahihi
katika orodha B kisha andika jibu husika katika karatasi ya kujibia
Orodha A Orodha B
A. Urudiwaji wa maneno kwa lengo
i. Hekaya la kuweka msisitizo
B. Kunakili muigo wa sauti namna
ii. Nudhumu kinavyosikika
C. Semi yenye kufananisha vitu kwa
iii. Kibadala kutumia viunganishi
D. Hadithi zenye kukejeli na
iv. Takriri kufurahisha kwa lengo la
kupunguza ukali wa tukio
v. Sitiari E. Ushairi
F. Hadithi zenye mhusika mmoja
mjanja ambaye anatawala
hadithi nzima
G. Semi zenye kufananisha vitu pasi
na kuwepo Kwa viunganishi
Page 2 of 4
SEHEMU B (ALAMA 54)
Jibu maswali yote
3. Kwa kutumia mifano thabiti toa maelezo ya kutosha kuhusu dhana zifuatazo
i. Matambiko
ii. Urudufishaji
iii. Lakabu
iv. Mnyambuliko wa vitenzi
v. Mofu
vi. Kikundi kielezi (KE)
4. (a) Tungo sentensi huundwa kwa kuzingatia kanuni na vipashio vinavyohusika;
Tunga sentensi zenye sifa zifuatazo
i. Kishazi huru na kishazi tegemezi
ii. Muunganiko wa sentensi sahili mbili
(b) Changanua sentensi mbili ulizotunga hapo juu kwa njia ya kisanduku

5. Pigia mstari mofu zinazoonesha kauli mbalimbali huku ukionesha kauli


zinazopatikana katika sentensi hizo:
Mfano Watakavyoigiza________ kauli ya kutenda
i. Kaka ataadhibiwa ___________________________________
ii. Mwalimu h akuwasilisha barua yake________________________________
iii. Mwezi uliandama ________________________________
iv. Mazao yaliyovunwa ni machache mno_________________________________
v. Walichokozana wao wenyewe __________________________________
vi. Chakula kiliteketea chote _______________________________
6. Taja aina za ngeli inayowiana kwa kila nomino katika orodha ifuatayo Kisha Tunga
sentensi katika Hali ya umoja na wingi ukitumia nomino hizo
a. Kipofu
b. Kiti
c. Ngoma
d. Mtama
e. Bata
f. Maji

7. Tunga sentensi Moja (1) zikionesha matumizi ya viunganishi vifuatavyo


a) Kiunganishi Cha wakati
b) Kiunganishi Cha mahali
c) Kiunganishi Cha masharti
d) Kiunganishi Cha chaguo
e) Kiunganishi Cha kutofautisha

8. Wataalamu wa lugha wanadai ya kwamba Kiswahili ni kibantu; kwa kutumia


msingi wa ushahidi wa kiisimu (sayansi ya lugha) thibitisha dai hili Kwa hoja sita (6)

Page 3 of 4
SEHEMU C: ( ALAMA 30)
Chagua maswali mawili (2) kutoka sehemu hii
ORODHA YA VITABU:. WAANDISHI :
TAMTHILIYA:
Ngoswe Penzi kitovu Cha uzembe. E. Semzaba
Kilio chetu. Medical Aid Foundation
Orodha Steve Reymond ( MA)

RIWAYA:
Takadini. Ben J. Harrison ( MBS )
Watoto wa mama ntilie E. Mbogo (HP)
Joka la mdimu. A. J. Safari

USHAIRI:
Malenga wapya TAKILUKI
Wasakatonge. M. S Khatibu
Mashairi ya Chekacheka

9. Kwa kutumia diwani mbili ulizosoma onesha jinsi waandishi walivyofaulu


kuyaonesha matatizo mbalimbali yaliyopo katika jamii yetu ya Leo. Hoja tatu (3) Kila
diwani

10. Kwa kuzingatia kanuni za uandishi wa mashairi ya kimapokeo Tunga shairi lenye
beti nne kuhusu ukatili wa kijinsia

11. Wasanii wa kazi za fasihi hutumia mandhari mbalimbali kuiwakilisha kazi ya kifasihi.
Kwa kutumia tamthiliya mbili ulizosoma onesha mandhari tatu (3) katika Kila kitabu
zilizotumiwa na watunzi kufikisha maudhui katika jamii.

Page 4 of 4

You might also like