You are on page 1of 1

SHULE YA UPILI YA LANG’ATA

KISWAHILI KIDATO CHA KWANZA KAZI YA LIKIZO APRILI 2019

JIBU MASWALI YOTE.

1. ISIMUJAMII

Rejelea Kiswahili Fasaha Bk 1.

(a) Andika kanuni zinazoongoza mitindo mbalimbali ya lugha katika jamii.

(b) Eleza sifa kumi za mazungumzo ya nyumbani.

(c) Eleza sifa kumi za lugha ya shuleni.

(d) Eleza sifa kumi za sajili ya sokoni

(e) Eleza sifa kumi za sajili ya mtaani

2. SARUFI NA MATUMIZI YA LUGHA

(a) Andika irabu za Kiswahili –

Za mbele kati

Za mbele juu

Za nyuma kati

Za nyuma juu

Za chini

(b) Andika aina za konsonanti na uandike mifano yote ya kila aina.

(c )Eleza aina zote za maneno ya Kiswahili na utoe mifano miwili kwa kila aina.

(d)Andika ngeli zote za nomino na utoe mifano mitatu kwa kila ngeli katika umoja na wingi.

(e )Tunga sentensi mbilimbili kwa kila alama ya kuakifisha.

(f) Kiambishi ni nini?

(g) Andika aina za viambishi awali na utoe mifano.

(h) Andika aina za viambishi tamati na utoe mifano.

You might also like