You are on page 1of 2

KIDATO CHA PILI

KAZI YA NYUMBANI, APRILI MWAKA 2020

Jibu maswali yote

a) Taja vigezo vitatu vinavyotumiwa kuainisha konsonanti kisha uvitumie kuainisha


konsonanti zifuatazo:
i) /h/
ii) /k/
iii) /n/
iv) /y/
v) /d/

b)i) Eleza tofauti kati ya Kikundi Nomino (KN) na Kikundi Tenzi (KT)

ii) Onyesha Kikundi Nomino na Kikundi Tenzi katika sentensi zifuatzo.


i) Yule mfupi ameokolewa na wavuvi.
ii) Kitoto hicho chake kinasumbua sana.
iii) Sisi sote hatupendi watu wanaopenda ufisadi
iv) Wewe utapewa zawadi kesho.

c)i) Eleza maana ya sentensi sahili.

ii) Tunga sentensi tano sahili

iii) Changanua sentensi zote sahili ulizozitunga katika swali la (c(i)

d) Huku ukitoa mifano eleza tofauti ya dhana zifuatazo:


i) Silabi

ii) Viambishi

iii) Mofimu

e) Huku ukitoa mifano, onyesha mambo tofauti yanayowakilishwa na mofimu


tegemezi.

f) Eleza tofauti kati ya aina zifuatazo za nomino.


i) Nomino dhahana na kitenzi-jina

ii) Nomino za wingi na za makundi

g)i) Eleza maana ya vivumishi vya pekee.

ii) Taja vivumishi vya pekee tofauti na ueleze matumizi ya kila kimoja.
Isimujamii
1|Page
Eleza sifa za lugha inayotumika katika maamkizi na mazungumzo mtaani.

Fasihi Simulizi
i) Eleza maana ya maigizo

ii) Taja vipera tofauti vya maigizo

iii) Eleza sifa na umuhimu wa maigizo

iv) Eleza sifa za visasili na umuhimu wake.

2|Page

You might also like