You are on page 1of 5

JIMBO KATOLIKI LA KIGOMA

SEMINARI YA MT. YOSEFU ITERAMBOGO

MTIHANI WA ROBO MUHULA KIDATO CHA TATU

KISWAHILI

MUDA:SAA3 Jumatatu 27 Machi 2023 asubuhi

MAELEKEZO

1. Karatasi hii ina sehemu A, B na C zenye jumla ya maswali kumi na moja (11)
2. Jibu maswali yote kutoka sehemu A na B na maswali mawili kutoka sehemu C, swali la
kumi ni la lazima
3. Sehemu A ina alama kumi na sita (16), sehemu B ina alama hamsini na nne (54) na
sehemu C ina alama thelathini (30).
4. Zingatia maelekezo ya kila sehemu na ya kila swali.
5. Simu za mkoni na vitu vyote visivyoruhusiwa haziruhusiwi katika chumba cha mtihani.
6. Andika JINA LAKO KAMILI katika kila karatasi ya kujibia.

SEHEMU A (Alama 16)

Jibu maswali yote katika sehemu hii

1. Chagua herufi ya jibu sahihi katika vipengele (i) hadi (x), kisha andika herufi ya jibu hilo
katika kijitabu chako cha kujibia.
i. Baada ya kumaliza darasa la saba na kufanikiwa kufaulu kujiunga kidato cha kwanza,
mama alinunua zawadi ya kamusi yenye lugha ya Kiswahili, Kingereza na Kifaransa. Je
hii ni aina gani ya kamusi?

A. Kamusi thaniya D. Kamusi tathilitha


B. Kamusi mahuluti E. Kamusi tathidifu
C. Kamusi wahidiya

ii. Tulipowaona tulifurahi sana. Kiambishi kilichopigiwa mstari kwenye neno hilo kimefanya
kazi kama kirejeshi cha

A. Mahali D. Mtenda
B. Mtendwa E. Mtendewa
C. Wakati

iii. Kucheza kwake kunafurahisha. Neno lililokolezwa wino ni aina gani ya neno?

A. Kitenzi C. Kiwakilishi E. Kielezi


B. Kivumishi D. Nomino

1
iv. Usanifishaji wa lahaja ya kiunguja ulifanywa na wageni ambao ni

A. Waarabu C. Wajerumani E. Wafaransa


B. Waingereza D. Wareno

v. ‘Yule dada amenona’. Neno amenona katika sentensi hii ni kosa la

A. Upatanisho wa kisarufi D. Kimsamiati


B. Kimuundo E. Matamshi
C. Kimantiki

vi. Ni hadithi zipi zinazoelezea chanzo au asili ya maumbile fulani, zinazotumia wahusika
mbalimbali?

A. Vigano C. Ngano E. Soga


B. Tarihi D. Visasili

vii. Katika mpangilio wa ngeli za nomino, ni ngeli ipi inahusisha viumbe vyenye uhai tu:

A. Ngeli ya LI-YA C. Ngeli ya KI-VI E. Ngeli ya U-ZI


B. Ngeli ya I-ZI D. Ngeli ya A-WA

viii. Mifano ya maneno yaliyoundwa kwa njia ya uambatanishaji ni?

A. Shughulisha, polepole, mtutu D. Hatimiliki, utaifishaji, vilevile


B. Pigapiga, pigilia, mapigo E. Chajio, kifutio, chamcha
C. Barua pepe, pakashume, njiwa pori

ix. Bainisha kipengele cha maudhui ambacho kinachunguza jinsi mtunzi wa kazi ya fasihi
anavyoyaona maisha

A. Dhamira C. Mtazamo E. Falsafa


B. Ujumbe D. Mgogoro

x. Kauli mbalimbali ya vitenzi ni dhima ya

A. Mofu D. Mzizi
B. Mofu huru E. Mofu tegemezi
C. Mofimu

2. Oanisha kazi za alama za uandishi zilizopo katika Orodha A na alama za uandishi


zilizopo katika orodha B kwa kuandika herufi ya jibu sahihi.

2
ORODHA A ORODHA B

(I) Hutumika kukariri maneno yaliyosemwa au (a) Aya


kuandikwa na mtu mwingine. (b) Herufi kubwa
(II) Hutumika kuonesha kuwa herufi fulani (c) Alama za mtajo
imeachwa. (d) Mkato
(III) Hutumika kutenganisha siku, mwezi na mwaka. (e) Nukta pacha
(IV) Hutumika kuonesha kuwa maneno fulani (f) Ritifaa
yameachwa. (g) Nukta
(V) Kifungu cha sentensi kinachoeleza wazo moja. (h) Kinyota
(VI) Hutumiwa kuashiria vitu vilivyo katika orodha. (i) Nukta katishi

SEHEMU C (Alama 54)

Jibu maswali yote katika sehemu hii

3. (a) Bainisha kauli ya vitenzi inayojitokeza katika sentensi zifuatazo

(i) Tutapigiana simu (iii) Anapenda uyoga


(ii) Haukatiki hata kidogo (iv) Imbisha wimbo mpya

(b) Ainisha maneno yaliyokolezwa wino katika sentensi zifuatazo

(i) Embe lilitumbukia chubwi! (iii) Kuimba kunafurahisha sana


(ii) Juma hana kalamu ya mkaa (iv) Mungu wangu! tutashinda.

4. (a) Tunga tungo inayoendana na aina ya upatanisho uliopewa


(i) Nomino na umbo la o-rejeshi katika kitenzi
(ii) Kiwakilishi na mzizi wa amba
(iii) Nomino na kitenzi
(iv) Nomino na kivumishi cha pekee
(b) “Upatanisho wa kisarufi ni kigezo kimojawapo kati ya vigezo vya kuunda ngeli za
nomino”. Thibitisha dai hilo kwa kutunga sentensi ukitumia ngeli zifuatazo
(i) U-I (ii) LI-YA (iii) U-YA (iv) I-ZI

5. Umeteuliwa kushiriki shindano la uandishi wa ngonjera Tanzania. Tunga ngonjera


yenye beti nne (4) kuhusu sensa ya 2022.

6. (a) Eleza maana ya kishazi


(b) Andika sentensi zenye miundo ifuatayo bila kuongeza kishazi ambacho hukuulizwa.

3
(i) Kishazi hutu kimoja
(ii) Kishazi tegemezi kimoja na kishazi huru kimoja
(iii) Kishazi huru kimoja na kishazi tegemezi kimoja
(iv) Vishazi tegemezi viwili na vishazi huru viwili

7. Soma shairi lifuatalo kisha jibu maswali yanayofuata.


Nilikwenda kisimani, makusudi nizunguke,
Nikaokota njiani, johari ya nuru mwake,
Nina mmoja mwandani, nampa yeye aweke,
Kumbe aliitamani, kuifanya kuwa yake.

Hilo nilipobaini, acha lawama iruke,


Kalitia mdomoni, yakuwa nina makeke,
Kwa kuitaka kihuni, kutwa kutusi ni kwake,
Siri simpi fulani, ikawa silaha yake.

Siri iweke bwetani, kisha funga isitoke,


Siri weka ufichoni, ilinde isiondoke,
Siri pake ni moyoni, iweke isitirike,
Haiingi mashakani, asosema siri yake.

MASWALI

(i) Mtunzi wa shairi hili anazungumzia nini?


(ii) Taja dhamira moja inayopatikana ubeti wa tatu.
(iii) Taja methali moja inayobeba ujumbe wa shairi hili.
(iv) Bainisha kituo alichotumia mshairi katika shairi hili

8. Wewe ni meneja wa shule ya Seminari Iterambogo. Andika tangazo la nafasi za


kujiunga na masomo kidato cha kwanza kwa mwaka 2024 katika seminari yako.

4
SEHEMU C (Alama 30)

Jibu maswali mawili katika sehemu hii, swali la 10 ni lazima.

9. Ni kwa namna gani waandishi wa tamthiliya wametumia mandhari kuibua dhamira


katika kazi zao? Tumia hoja tatu kwa kila tamthiliya kati ya mbili ulizosoma.
10. “Waandishi wa vitabu vya riwaya wamejitahidi kuonesha uhalisia wa dhamira
mbalimbali zinazoigusa Tanzania moja kwa moja”. Onesha ukweli wa kauli hii kwa
kutumia hoja tano kutoka katika kitabu kimoja cha riwaya.
11. Kwa kutumia hoja tatu (3) kwa kila tamthiliya kati ya mbili ulizosoma, jadili kufaulu kwa
waandishi katika kipengele cha utumizi wa tamathali za semi.

You might also like