You are on page 1of 5

MTIHANI WA KISWAHILI MOKO MKOA

SEHEMU A. SARUFI
CHAGUA HERUFI YA JIBU SAHIHI

1. Wengi wamekwenda ughaibuni. Katika sentensi hii neno wengi limetumika kama aina
gani ya maneno?
A, kivumishi b. kielezi c. kiwakilishi d. kitenzi e. kihisishi
2. Kauli ipi inaonyesha hali ya kutendwa?
a. Tumepika chakula chetu b. tunapikisha chakula chetu c. tulipikiwa chakula chetu d.
tumepikwa chakula chetu e. tunapika chakula chetu
3. Katika vifungu vya maneno vifuatavyo, kifungu kipi kipo katika kauli taarifa?
a. Unataka kuondoka lini? B. alitaka kukuuliza utaondoka lini? C. ni lini wewe
utaondoka? D. aliuliza utaondoka lin? E. aliuliza kuwa utaondoka lini?
4. Mwalimu wetu hakufika kazini leo. Kitenzi hakufika kipo katika hali gani?
a. Mazoea b. kuendelea c. timilifu d. matarajio e, kanushi
5. Wabunge wote wa jamhuri ya muungano wa Tanzania waliwasili Dodoma kuendelea na
kikao cha bunge. Neno wote limetumika kama aina gani ya maneno?
a. Nomino b. kiwakilishi c, kitenzi d. kivumishi e. kielezi
6. Neno lipi kati ya haya yafuatayo lina maana sawa na neno thubutu?
a. Ufidhuli b. ujasiri c. umahiri d. ukakamavu e. utashi
7. Kuzua kizaazaa ni msemo wenye maana gani?
A, ushabiki b. upendeleo c. malumbano d. masikitiko e. majungu
8. Mtu anayetafuta kujua jambo Fulani kwa kuuliza maswali huitwaje?
a. Mdaku b. mbeya c. mfitini d. mdadisi e. mwongo
9. Mtu __ atakaye shinda mashindano atapewa
a. Yoyote b. yeyote c. wowote d. wote e popote
10. Tulisafiri kwa ndege hadi Nairobi. Sentensi hii ipo katika nafasi ya ____
a. Kwanza wingi b. pili wingi c. tatu wingi d. pili umoja e. kwanza umoja
11. Ni neno gani lisilolandana na mengine kati ya haya?
a.nakala b. tangazo c. ilani d. masurufu e. mafunzo
12. Andika nomino MEZA kuwa kitenzi
a. Mezea b. mezesha c. mezeana d. kumeza e, mezeana
13. Katika maneno yafuatayo ni lipi ambalo ni nomino dhahania?
a. Unaimba b. uelewa c. unacheza d. ukisoma e. ulikimbia
14. Angelikula chakula kamwe __ sikia njaa
a. Angali b. angeli c. asingeli d. asingali e. ange
15. Neno lima katika kauli ya kutendana litakuwa
a. Limwa b. limana c. limiana d. lima e.limika

16. Kiambishi cha wakati katika kitenzi tunasoma ni _____


a. --- tu-- b. ---na -- c. ---so--- d. –ma—e. – nas—
17. Dada alimfulia mdogo wake nguo. Katika sentensi hii mtendwa ni ___
a. Dada b. mdogo c. nguo d. wake e. alimfulia
18. Neno masharti lina silabi ngapi?
a. Tatu b. mbili c. nane d. tano e. nne
19. Babu alikuwa analima shambani. Neno alikuwa ni aina gani ya kitenzi ?
a. Kitenzi kikuu b. kitenzi kitegemezi c. kitenzi jina d. kitenzi kishirikishi e. kitenzi
kisaidizi
20. Neno lipi kati ya maneno yafuatayo ni kisawe cha neno hifadhi?
a. Weka b. panga c. tunza d. ficha e. funga
21. Tulicheza mpira mchana kutwa. Katika sentensi hii watendwa ni nafsi ipi?
a. Ya tatu wingi b. ya pili wingi c. ya pili umoja d. ya tatu umoja e. ya kwanza wingi

SEHEMU B: LUGHA YA KIFASIHI:

22. Nahau isemayo “mtu mwenye ndimi mbili” ina maana ipi?
a. Mropokaji b. mwongo c. killimilimi d. kigeugeu e, mfitini
23. Methali isemayo “mgaagaa na upwa hali wali mkavu”inatoa funzo gani?
a. Bidii huleta mafanikio b. mafanikio ni matokeo ya kazi c. bidii huleta faraja d, bidii
ni kazi ya kuhangaika e. mafanikio ni ya lazima
24. “______ hufa masikini” kifungu kipi hukamilisha methal hiyo?
a. Anayeiba cha nduguye b. anayekula cha nduguye c. mtegemea cha nduguye d.
mkimbilia cha nduguye e. asiyethamini cha nduguye
25. Kuwa na ulimi wa upanga, maana yake ___?
a. Kusema uongo b. kusema maneno makali c, kupayuka d. kusema kweli e.
kuropoka
26. Tegua kitendawili hiki” nyumbani kwangu kuna jinni mnywa maji”
a. Pipa b. mtungi c. kibatari d. kinywa e. kikombe
27. Nini maana ya nahau hii “kufa kikondoo”
a. Kufa bila kujitetea b. kufa kiungwana c. kufa kishujaa d. kufa kawaida e. kufa kwa
kuugua sana.
28. Zulia la Mungu” tegua kitendawili hiki
a. Mbingu b. bahari c, kanisa d. ardhi e. jeneza

29. Mkaidi hafaidi mpaka siku ya Idd” methali hii ina maana gani?
a. Mtu asiyejali maonyo ya wakubwa huharibikiwa b. mzazi asiyemkanya mtoto wake
atamletea matatizo c. mkanye mtoto akiwa bado mdogo d. usitegemee mwanao
kuwa na tabia nzuri kama humfundishi e. unapokuwa na tabia mbaya utakosa vitu
vingi
30. Methali ipi kati ya hizi zifuatazo haitoi onyo kuhusu tabia ya mtu?
a. Kiburi si maungwana b. mtoto mkaidi mngoje siku ya ngoma c. asiyesikia la mkuu
huvunjika guu d. mtoto mwelevu hafunzwi adabu e. panya huuma huku akipuliza
31. Baada ya mazoezi makali ya viungo tulilala “usingizi wa pono” msemo usingizi wa pono
una maana gani?
A,. usingizi wa mang’amung’amu b. usingizi wa maruweruwe c. usingizi wa njozi d.
usingizi kushtukashituka e, usingizi mzito mno
32. Nyumba yangu ina milango mingi” tegua kitendawili hiki.
a. Kifo b. kichuguu c. mlima d. nyayo e. mvua
33. Kamilisha methali: mpenda chongo ________________
a. Huona kengeza b. hufurahi c. hupendwa na wengi d. si kipofu e. hupenda kengeza
34. Maana ya nahau “ kumeza maneno” ni __
a. Kuwa bubu b. kuficha siri c. kutoboa siri d. kunyamaza e. kufanya urafiki
35. Mtegemea nundu.haachi kunon” methali hii inafanana na ipi?
a. Ahadi ni deni b. hauchi hauchi unakucha c. haba na haba hujaza kibaba d.
atangaye san na jua hujua e. mtegemea cha nduguye hufa hali masikini

SEHEMU C: UTUNGAJI.

Panga sentensi hizi ili zilite mtiririko mzuri wa mawazo kwa kuzipa herufi A,B,C,D na E

36. Mlo kamili huwa na aina tatu za vyakula


37. Ili mwanadamu awe na nguvu na kuepuka magonjwa ya aina mbalimbali mwilini, ni
lazima ale chakula bora
38. Kazi moja wapo muhimu ya chakula tulacho ni cha kujenga mwili
39. Kula chakula bora ni mojawapo ya kanunu muhimu za afya
40. Chakula bora maana yake ni mlo kamili

SEHEMU D: UFAHAMU

Soma habari kasha jibu maswali namba 41-45 kwa kujaza nafasi wazi

Wanakijiji wa kijiji cha Bulambya huamini kuwa kazi ndio msingi wa maisha. Naye Semeni akiwa
mwenyekiti wa kamati ya Elimu ya kujitegemea anaamini kabisa kuwa kazi ni uhai. Yeye pamoja
na wenzake huamini kuwa kazi imestawisha na kufanikisha watu karne baada ya karne na kizazi
baada ya kizazi . kila anapopata fursa ya kuzungumza na wenzake,Semeni anaeleza kuwa kila
mtu apatacho kwa kazi yake mwenyewe humpa namna bora ya matumaini, furaha ya mtu
huvuna na kuonja matunda ya jasho lake kubwa na bora mno. Pia anaamini kuwa akineemeka
kwa nafasi yake hufurahia tija ya kazi yake mwenyewe na tija kama hii humfurahisha.

Katika msimu uliopita vijana wa kijiji cha Bulyaga walijifunga vibwebwe na kufuata mawaidha ya
wataalamu na viongozi wao. Walitumia muda wao mwingi kulima mazao ya mpunga,pamba na
mbogamboga. Lakini hutumia siku za jumamosi na jumapili kumwabudu Mungu, kupumzika na
kubadilishana mawazo.

Wanakijiji hawa huamini kuw wakiwa wavumilivu furaha yao haitakadirika wanayo imani na
uwezo wa kutimiza azma yao ya kujiletea maendeleo, Semeni akishirikiana a Azizi ambaye ndiye
mwenye kiti wa kijiji hicho huwatia moyo wanakijiji wenzao kwamba kama vile mtu
anavyokuwa na furaha akihitimu masomo baada ya mavuno kwa muda mrefu, ndivyo na wao
hufurahia mavuno baada ya kuvumilia shida nyingi wakati wa kilimo.

41. Mwandishi ameeleza kuwa wanakijiji wa Bulyaga wanayo imani na azma ya kutimiza
malengo yao . neno azma lina maana ____________________________
42. Semeni ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya kujitegemea anaamini kuwa ____________
43. Tunaweza kulinganisha habari hii na methali ipi_____
44. Habari uliyosoma ina aya ngapi?
45. Mwenyekiti wa kijiji cha Bulyaga anaitwa nani ?

MAJIBU YA KISWAHILI 17. C


18. A
1. C 19. E
2. C 20. C
3. E 21. E
4. E 22. D
5. D 23. A
6. B 24. C
7. C 25. B
8. D 26. C
9. B 27. A
10. A 28. D
11. D 29. E
12. D 30. D
13. B 31. E
14. C 32. B
15. B 33. A
16. B 34. B
35. C
36. D
37. B
38. E
39. A
40. C
41. KUSUDI
42. KAZI NI UHAI
43. MVUMILIVU HULA MBIVU
44. TATU
45. AZIZI

You might also like