You are on page 1of 2

HALMASHAURI YA WILAYA YA TABORA

MTIHANI WA MAJARIBIO DARASA LA NNE TARAFA YA UYUI


SOMO LA URAIA NA MAADILI OKTOBA 2019
SEHEMU A
1.Chagua herufi ya jibu sahihi
(i). Rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania anaitwa … (a) Aman Abeid
Karume (b) Julius Kambarage Nyerere (c) John Pombe Magufuli (d) Jakaya Mrisho Kikwete [ ]
(ii). Bendera ya taifa ina rangi ngapi? (a) tatu (b) mbili (c) nne (d) moja [ ]
(iii).Watu wanaoishi eneo moja huitwa … (a) wanandugu (b) wanajamii (c) wananzengo (d) walevi [ ]
(iv).Rangi ipi huwakilisha madini kwenye bendera ya taifa? (a) njano (b) bluu (c) kijani (d) nyeusi [ ]
(v). Uwezo wa kukabiliana na changamoto huitwa (a) uadilifu (b) ujasiri (c) kipaji (d) kuaminika [ ]

SEHEMU B
2.Oanisha fungu A na fungu B ili kupata maana halisi
Na. Fungu A Fungu B
i. Malengo A. Maneno yanayotolewa kushauri jambo.
ii. Uwajibikaji B. Kielelezo cha uhuru wa taifa letu
iii. Madawa ya kulevya C. Mihadarati, bangi na pombe.
iv. Nasaha D. Mambo yanayotarajiwa.
v. Ajira za utotoni E. Kutimiza majukumu.
F. Kuajiri watoto wenye umri mdogo.

SEHEMU C
3.Andika NDIYO katika sentensi sahihi na HAPANA katika sentensi isiyo sahihi
(ii). Wanafunzi wanaruhusiwa kucheza mdako barabarani. …………………………………………….……
(ii). Wanafamilia wanapaswa kusaidiana wakati wa matatizo tu. ………………………………….……..
(iii). Njia bora ya kumfundisha mwanafunzi mvivu ni kumchapa tu. ………………………………………
(iv). Mti au kifaa kinachotumika kutundikia vitu kama vile bendera huitwa mlingoti ………………
(v). Mtu mwenye mapenzi na nchi yake huitwa mzalendo ……………………………………………………
SEHEMU D
4. Jaza nafasi zilizoachwa wazi kwa kuchagua maneno kwenye mabano:-
(i). Mtu ambaye huiwakilisha nchi katika nchi nyingine huitwa ……… (balozi, mkimbizi)
(ii). Kitendo chawatu wawili au zaidi kufanya kazi pamoja huitwa ……… (ushirikiano, uhusiano)
(iii). Eneo dogo la utawala lililopo mjini huitwa ……………. (kijiji, mtaa)
(iv). Vitu vyenye thamani alivyonavyo mtu au nchi huitwa …….. (rasilimali, ujasiriamali)
(v). Mfumo wa utawala ambapo wananchi hushirikishwa katika maamuzi ………. (demokrasia, utawala)
SEHEMU D
5. Jaza nafasi zilizo wazi katika jedwali
Na. Mkoa Kabila
i. ………………………………… Wanyamwezi
ii. Iringa …………………………..
iii. ……………………………….. Waha
iv. Shinyanga na Mwanza …………………………..
v. ……………………………….. Wasambaa
MOCK TARAFA YA UYUI
URAIA NA MAADILI DARASA IV OKTOBA 2019
Na. Jibu

1. (i)C
(ii)C

(iii)B
(iv)A

(v)B
2. (i)D

(ii)E
(iii)C

(iv)A
(v)F

3. (i)HAPANA
(ii)HAPANA

(iii)HAPANA
(iv)NDIYO

(v)NDIYO
4. (i)Balozi

(ii)Ushirikiano
(iii)Mtaa

(iv)Rasirimali
(v)Demokrasia

5. (i)Tabora
(ii)Wahehe

(iii)Kigoma
(iv)Wasukuma

(v)Tanga

You might also like