You are on page 1of 1

HALMASHAURI YA MANISPAA YA SONGEA

KAZI YA NYUMBANI (HOME PACKAGE) YA KUANZIA TAR 15 HADI TAR 21 JUNI 2020
SOMO: MAARIFA YA JAMII DARASA: IV
SEHEMU A
1. Chagua herufi ya jibu sahihi kutoka kwenye majibu uliyopewa
i. Mila na desturi ni miongoni mwa vitu vinavyounda (a) Historia (b)Utamaduni (c)Familia (d) Biashara
ii. Sura ya nchi ya wilaya yako ya Songea Manispaa ni ya ……………..…… (a) milima tu (b) mabonde tu (c)
tambarare na milima (d) uwanda wa juu
iii. Katika ramani ufunguo una kazi ya ..……. (a) kuelezea ramani (b) kufungua kufuli (c) mapambo
iv. Tanganyika na Zanzibar ziliungana rasmi mwaka ………(a) 1961 (b) 1977 (c) 1963 (d) 1964
v. Mahali ambapo malighafi zinatumika kutengenezea bidhaa huitwa (a) shuleni (b) kiwanda (c) chuo (d)
darasa
vi. Mawasiliano ni kitendo cha ………………….……. (a) kusemana (b) kubishana (c) kupashana habari (d)
simu
vii. Kuna aina ……….. za usafirishaji . (a) 1 (b) 2 (c) 3 (d) 4
viii. Mlima mrefu kuliko yote hapa Tanzania ni………….…. (a) Meru (b)Matogoro (c) Kilimanjaro (d) Urugulu

2. Oanisha kifungu A na majibu yaliyopo kifungu B ili kuleta maana kamili


FUNGU A FUNGU B
i. Michoro katika mapango ilipatikana …………………………… A. Pemba na Unguja
ii. Chama cha CCM kilitokana na muungano wa vyama vya ………… B. Familia
iii. Uvuvi, kilimo, uchimbaji madini na jenzi………………… C. Kondoa
iv. Zao la karafuu hulimwa …………………….. D. Shughuli za kiuchumi
v. Sehemu ambayo kumbukumbu za kihistoria hutunzwa kwa manufaa E. Makumbusho
ya kizazi kijacho……………….. F. TANU na ASP
vi. Baba, mama na watoto …………………. G. Ruvuma

SEHEMU B
3. Soma maswali yafuatayo kisha Jibu KWELI kwa sentensi iliyo sahihi na SIKWELI kwa sentensi isiyo sahihi
i. Mlima Kilimanjaro upo nchini Kenya. …………………………………………..
ii. Vumbi na moshi katika anga huchafua hewa…………………………………….
iii. Uchimbaji wa maduni una faida tu, hauna madhara kwa binadamu………………
iv. Ziwa Nyasa, bahari ya Hindi, ziwa Viktoria, ziwa Eyasi ni maziwa ya maji chumvi …………
v. Mafuriko husababishwa na jua kali……………………..
vi. Kabila maarufu hapa nchini kwa ufugaji ni Wamasai ………………………….
vii. Makao makuu ya Tanzania yapo Dodoma……………………….

4. Jibu maswali yafuatayo kutoka kwenye mchoro huu


Hospitali

Sokoni Mto

Kituo cha basi


Maswali
i. Hospitali ipo upande gani ………………………………..
ii. Upande wa kusini kuna kitu gani …………………………
iii. Mara zote mshale wa dira uelekea upande gani …………………..
iv. Kazi kuu ya kifaa hicho ni………………………………….

You might also like