Professional Documents
Culture Documents
Maarifa Ya Jamii
Maarifa Ya Jamii
MKOA WA KIGOMA
27. Mganga aliyewaaminisha Watanganyika katika vita vya Maji maji kuwa risasi za wajerumani
zitabadilika kuwa maji alikuwa nani?
A. Kinjekitile Ngwale B. Chifu Mangungo C. Kibanga D. Karl Peters
28. Mkutano wa Berlin ni mkutano uliojumuisha mataifa ya kibeberu kwa lengo la kugawana makoloni
barani Afrika. Mkutano huu uliitishwa na nani?
A. Karl Peters B. Vasco Da Gama C. Kansela Otto von Bismark D. umoja wa mataifa E.
Barthomeo Diaz
29. Mkataba uliofanyika mwaka 1890 kati ya serikali ya Uingereza na Ujerumani wenye madhumini ya
kurekebisha mipaka ya mwaka 1886 ulijulikana kama:
A. mkataba wa Hamaton B. mkataba wa freire C. mkataba wa Berlin
D. mkataba wa Heligoland E. mkataba wa Vienna
30. Uchaguzi wa kwanza hapa nchini uliohusisha vyama vingi vya siasa ulifanyika mwaka 1995. Je, ni
Rais yupi alichaguliwa?
A. Julius K. Nyerere B. Benjamin Mkapa C. Kikwete D. Magufuli E. A. H. Mwinyi
31. Ardhi ni rasilimali muhimu sana ambayo hubeba rasilimali nyingine. Ipi kati ya zifuatazo si rasilimali
inayopatikana ardhini?
A. gesi asilia B. mazao ya chakula C. maji D. madini E. watu
32. Bahari ya Hindi ni moja ya rasilimali zilizopo Tanzania je, ni aina gani ya rasilimali?
A. rasilimali ya kutengenezwa B. rasilimali ya Afrika C. rasilimali ya asili
D. rasilimali maalumu E. rasilimali kuu
33. Reli ya kati inayoanzia Dar es Salaam hadi Kigoma nchini Tanzania ilianza kujengwa mwaka 1905
kwa lengo la kusafirisha malighafi wakati wa ukoloni. Je, ni wakoloni wa taifa gani waliijenga reli
hiyo? A. Waingereza B. Wajerumani C. Wachina D. Wareno
E.Waitaliano
34. Wanafunzi wa shule ya msingi Mzinga walipewa kazimradi na mwalimu wao kuchora ramani ya dunia
kuonesha milima mirefu. Ni aina ipi ya kipimio cha ramani wataitumia kuchora ramani hiyo?
A. kipimio kikubwa B. kipimio cha kati C. kipimio kidogo D. njia ya mstari E. njia ya
uwiano
35. Kama utateuliwa kumuongoza Bi. Marion ambaye ni mtalii kutoka Austria anayetaka kupanda mlima
Kilimanjaro mkitokea Dar Es Salaam kwa ndege ya Dream Liner, ndege ya shirika la ndege la
Tanzania mtatua katika kiwanja gani?
A. Uwanja wa ndege wa Chunya B. Uwanja wa ndege wa Bukoba C. Uwanja wa ndege wa
Kilimanjaro D. Uwanja wa ndege wa Mwanza E. Uwanja wa ndege wa Mtwara
36. Makumbusho ni sehemu ambayo kumbukumbu za kihistoria huifadhiwa .Je mtu anayefanya kazi
katikati makumbusho huitwa______
A. Mwanakiolojia B. Mwanamakumbusho C. Mwangalizi wa makumbusho
D. Mtaalamu wa historia kuhusu utamaduni na maisha ya binadamu E. Mwanamziki
37. Ni tukio lipi kati ya haya yafuatayo lilitangulia kutokea hapa Tanzania ?_______
A.Kifo cha Abeid A. Karume B. Mapinduzi ya Zanzibar C. Kifo cha chifu Mkwawa D. Vita
vya Kagera E. Mfumo wa vyama vingi vya siasa.
38. Sensa ya watu na makazi ilianyika mara ya mwisho mwaka 2022 na ilisaidia kutambua idadi watu
katika nchi. Je ni lini Tanzania itafanya sensa nyingine?
A. 2024 B. 2032 C. 2030 D. 2025 E. 2027
39. Ndani ya familia nani anayestahili kuafanya majukumu yafuatayo maji, kukusanya kuni, safi wa
nyumbani na kupika?
A. Mama na baba B. Wanafamilia wenye uwezo wa kufanya kazi C. Mama na Binti yake
D.Mama, watoto, binti na kijana wa kazi E. Baba
40. Familia ya bwana Sangana inaishi sehemu ya bondeni ni janga gani linaweza kuikumba hiyo familia?
A. Mafuriko B. Moto C. Ukame D. Suunami E. Njaa
SEHEMU B: ANDIKA JIBU SAHIHI KWENYE KARATASI YAKO YA KUJIBIA