You are on page 1of 12

WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA

TEKNOLOJIA

NUKUU ZA SOMO
(ZILIZORAHISISHWA)

MAARIFA YA JAMII

DARASA LA III
SURA 1: MAZINGIRA YETU
1.1 Vitu vinavyopatikana katika mazingira
Mazingira ni jumla ya vitu mbalimbali vinavyomzunguka mwanadamu. Vitu hivyo vinaweza
kupatikana nyumbani au shuleni. Pia, vimegawanyika katika makundi mawili, ambayo ni vitu
vilivyo hai na vitu visivyo hai.
Vitu Vilivyo Hai
Vitu vilivyo hai ni kama vile watu, ndege, miti, ng’ombe, nyasi, na wadudu.

Vitu Visivyo Hai


Vitu visivyo hai ni kama vile majengo, mawe, meza, kabati, kalamu, na chupa.

1.2 Vitu vinavyopatikana katika mazingira ya nyumbani


Vitu visivyo hai vinavyopatikana katika mazingira ya nyumbani ni kabati, vitanda, meza,
udongo, mawe, kuni, mkaa, baiskeli, vyombo, jiko, nguo.
Vitu vilivyo hai vinavyopatikana katika mazingira ya nyumbani ni kama vile mifugo mfano
ng’ombe, mbuzi, kondoo, kuku, bata, njiwa, mimea mfano michungwa, miembe, mikorosho,
miparachichi, mipera.

1.3 Vitu vinavyopatikana katika mazingira ya shule


Vitu vilivyo hai vinavyopatikana katika mazingira ya shule ni kama vile, ng’ombe, kondoo,
mbuzi, kuku, ndege, bustani ya maua na mboga mboga, mimea mingine.
Vitu visivyo hai vinavyopatikana katika mazingira ya shule ni kama vile, mawe, kabati, vitabu,
mipira, bendera, ngoma, meza, madawati, viti, majengo na udongo.

1.4 Kutunza mazingira ya shule


Tunahitaji kutunza mazingira ya shule ili kuyaweka katika usafi na kuepuka madhara
yatokanayo na uchafu.
Vitendo vinavyochafua mazingira ya shule
a) kutupa takataka ovyo
b) kutotumia vyoo vizuri
c) kutofanya usafi eneo la shule
d) kutofuta vumbi darasani
e) kutoondoa tandabui kwenye majengo ya shule

Mambo yanayopaswa kufanywa ili kuboresha mazingira ya shule


a) kutengeneza na kupanda miti, nyasi na maua
b) kusafisha mazingira ya shule
c) kutunza na kumwagilia miti, nyasi na maua
d) kutupa takataka katika shimo la taka
e) kufanya usafi wa kina wa shule
f) kutumia vyoo ipasavyo
g) kutumia vyombo maalumu vya kukusanyia takataka
h) kutoa elimu juu ya utunzaji wa mazingira

Madhara ya kutokufanya usafi wa mazingira ya shule


a) kuhifadhi wadudu na wanyama hatarishi
b) kusababisha magonjwa ya mlipuko kama vile kuhara
c) kukosekana kwa hewa safi
d) mandhari ya shule kutopendeza na kutovutia

1.5 Usafi wa Madarasa


Vitendo vya usafi vinavyofanyika darasani
a) kufagia darasa kila siku
b) kufuta ubao mara baada ya matumizi yake kuisha
c) kutoa buibui waliotanda darasani
d) kufuta vumbi kwenye madawati

Faida za kufanya usafi wa darasa


a) hutusaidia tusichafue nguo
b) hufanya darasa lipendeze
c) husaidia kuharibu mazalio ya wadudu
d) husaidia kuwa na mazingira safi ya kusoma
e) hupunguza uzalishaji wa vimelea vya wadudu
f) huleta hewa safi

Madhara ya kutofanya usafi wa darasa


a) kupata magonjwa kama kifua na mafua
b) kuchafua sare ya shule
c) kuwa makazi ya wadudu

1.6 Kupanda miti, nyasi na maua


Faida za miti katika mazingira ya shule ni:
a) huleta kivuli
b) hutunza maji kwenye ardhi
c) hupunguza kasi ya upepo
d) hupendezesha mazingira

1.7 Faida ya mazingira safi


a) kuepuka maambukizi ya magonjwa kama vile kuhara, malaria, na tauni
b) kufanya mazingira yawe ya kupendeza na kuvutia
c) kupata hewa safi
d) mazingira safi huepusha uharibifu wa vyakula mashambani na nyumbani
SURA 2: HALI YA HEWA YA MAZINGIRA YETU
2.1 Kubaini jotoridi katika mazingira yetu
Jotoridi ni hali ya hewa ya ubaridi au joto. Jotoridi hupimwa kwa kutumia kipimo kinachoitwa
kipimajoto.
Kufahamu jotoridi la mazingira tunayoishi hutusaidia;kupanga shughuli zetu; pia hutuwezesha
kuchagua nguo za kuvaa katika siku au kipindi husika.

2.2 Athari za joto na baridi kwa wanyama na mimea


Athari za joto kwa wanyama na mimea
(a) hukausha mazao
(b) husababisha kifo
(c) husababisha njaa

Mbinu za kujikinga na hali ya hewa ya joto


a) kukaa kwenye kivuli
b) kujipulizia upepo kwa pangaboi
c) kuweka vitu kwenye jokofu

SURA 3: UTAMADUNI WETU


3.1 Kusalimiana kwa matendo mbalimbali
Utamaduni ni mtindo wa jumla wa maisha ambao hujumuisha asili, mila na desturi, jadi na
itikadi zinazotawala katika jamii fulani. Utamaduni wa jamii huweza kudumishwa kwa
kufanya matendo mbalimbali kama vile;
a) kusalimiana
b) kucheza michezo mbalimbali
c) kuimba nyimbo za asili
d) kucheza ngoma za asili
e) kusaidiana kwenye shida
f) kushirikiana kwenye furaha

Kusalimiana
Watoto wenye tabia njema husalimiana. Zifuatazo ni faida za kusalimiana.
a) kunawezesha watu kujuliana hali
b) kiashirio cha tabia njema
c) kumuonesha mtu unamjali
d) kunawezesha mtu kupata msaada stahiki
e) kusalimiana husaidia kudumisha utamaduni

Matendo ya kusalimiana
a) kushikana mikono, kwa mfano Wazaramo.
b) kupiga goti, kama vile Wasukuma
c) kubusiana mikono kwa mfano Wahehe.
d) kupigana mabega kama vile Wakinga
e) kushika kichwa

3.2 Kucheza michezo ya kiutamaduni


Kila jamii ina michezo yake ya asili kama sehemu ya kudumisha utamaduni. Jamii mbali
mbali hucheza michezo ya asili kulingana na mazingira na shughuli wanazofanya. Baadhi ya
michezo inayochezwa na jamii za Kitanzania ni kama vile; mchezo wa bao, kulenga shabaha,
kurusha mkuki na mbio, kucheza ngoma, kupiganisha mafahali au majogoo, kukimbiza kuku.

Faida za michezo ya kiutamaduni


(a) kukuza uwezo wa kufikiri na kuamua
(b) kujenga umahiri wa kupambana na kujilinda na maadui
(c) kujenga ukakamavu
(d) kuongeza ujuzi wa kufanya kazi
(e) kuburudisha
(f) kurithisha desturi za jamii.

3.3 Kuimba na kucheza ngoma


Jamii nyingi hushiriki katika kuimba nyimbo na kucheza ngoma za asili. Nyimbo na ngoma
hizo ni njia nyingine ya kudumisha utamaduni wetu. Faida za kucheza ngoma za utamaduni
ni:
a) kupata burudani
b) kuimarisha viungo vya mwili
c) kuleta hamasa katika shughuli mbalimbali
d) kudumisha utamaduni
e) husaidia kujenga umoja na ushirikiano miongoni mwao

3.4 Ngoma zinazochezwa na baadhi ya makabila nchini Tanzania


Hapa Tanzania, ngoma huchezwa kwa nyakati tofauti kama vile, nyakati za mavuno na
sherehe kama vile harusi, jando na unyago, kwenye matamasha na sikukuu zakitaifa, kwenye
makongamano. Baadhi ya ngoma hizo ni kama vile;
(a) Ngoma ya Mbeta – kabila la Waluguru
(b) Ngoma ya Mtingo na Iringi – kabila la Wachaga
(c) Ngoma ya Bugobogobo na Beni – kabila la Wasukuma
(d) Ngoma ya Mdumange – kabila la Wasambaa
(e) Ngoma ya Lizombe – kabila la Wangoni
(f) Ngoma ya Mganda – kabila la Wanyasa na Wamanda
(g) Ngoma ya Kasimbo na Enchuma – kabila la Wahaya
(h) Ngoma ya Sindimba – kabila la Wamakonde
(i) Ngoma ya Mdundiko – kabila la Wazaramo
(j) Ngoma ya Kisese – kabila la Wapare
(k) Ngoma ya Lindeku – kabila la Wamatengo
(l) Ngoma ya Chera – kabila la Wadigo

Vifaa vinavyotumika wakati wa kucheza ngoma


Vifaa vinavyotumika wakati wa kucheza ngoma za asili ni: njuga, maleba, ngoma, filimbi,
zeze, bati, manyanga na baragumu

SURA 4: UHUSIANO MWEMA


4.1 Dhana ya familia
Familia ni kikundi cha watu walio na uhusiano. Uhusiano wao unaweza kuwa wa damu, ndoa
au kuishi pamoja. Uhusiano mzuri unaanza kwa kuwatambua watu unaoishi nao.

4.2 Aina za Familia


Hapa Tanzania kuna aina sita za familia ambazo ni; familia ya awali, familia ya mzazi mmoja,
familia ya mume na mke, familia ya watoto yatima, familia ya makubaliano na familia pana.
(a) Familia ya awali; ni fmailia yenye baba, mama na watoto wao.
(b) Familia ya mzazi mmoja; ni familia yenye mama na watoto. Pia inaweza kuwa ya baba na
watoto tu. Familia hii hutokana na kutengana, kuachana kwa wazazi wawili au kufariki kwa
mzazi mmoja.
(c) Familia ya mume na mke; ni familia ya mume na mke waliooana ambao hawajapata mtoto.
Familia hii huwa na idadi ya watu wawili.
(d) Familia pana; ni familia kubwa zaidi ambayo ina watu wengi kuliko familia zingine.
Familia hii inaweza kuwa na baba, mama, watoto, babu, bibi, shangazi na mjomba.
(e) Familia ya watoto yatima; ni familia ya watoto wanaoishi peke yao na kujitegemea bila ya
wazazi. Hakuna mwanaukoo wala marafiki waliojitolea kuishi na watoto hawa.
(f) Familia ya makubaliano; ni familia ya makubaliano kati ya watu wanaoishi pamoja. Kwa
mfano mke, mume wanaolea watoto wa wenzao.

4.3 Kufahamu uhusiano na watu unaoishi nao katika familia


(a). Babu; ni baba wa mama au baba yako.
(b). Bibi; ni mama wa baba au mama yako.
(c). Shangazi; ni dada wa baba yako.
(d). Mjomba; ni kaka wa mama yako.
(e). Kaka; ni mtoto wa kiume wa mama au baba yako.
(f). Dada; ni mtoto wa kike wa mama au baba yako.
(g). Binamu; ni mtoto wa kike au wa kiume wa shangazi au mjomba wako.
(h). Shemeji; ni mume wa dada yako au mke wa kaka yako.
(i). Mama mdogo; ni dada mdogo wa mama yako.
(j). Mama mkubwa; ni dada mkubwa wa mama yako.

4.4 Kujenga uhusiano mzuri na marafiki


Kujenga uhusiano mzuri na wanafamilia ni muhimu. Pia, ni vizuri kujenga uhusiano mzuri na
marafiki. Rafiki ni mtu unayempenda na kumwamini. Unaweza kujenga uhusiano mzuri na
marafiki kwa kula nao pamoja, kucheza nao pamoja, kusoma nao pamoja na kushirikiana nao.
Faida za kuwa na marafiki ni: unapata msaada pale unapohitaji na unajenga udugu.
Hasara za kuchagua marafiki wabaya ni: unaweza kukosa msaada na pia utapoteza maadili
mema.

SURA 5: VIONGOZI WA NCHI YETU


5.1 Viongozi wakuu wa nchi
Tanganyika ilipata Uhuru wake tarehe 9 Disemba mwaka 1961. Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania ni muungano wa nchi mbili ambazo ni Tanganyika na Zanzibar na iliundwa mwaka
1964.
Katika muda wote kumekuwa na viongozi wakuu mbalimbali. Viongozi hawa ni marais na
mawaziri wakuu. Rais huchaguliwa na wananchi kwa kupigiwa kura. Waziri Mkuu huteuliwa
na Rais kutoka miongoni mwa wabunge waliochaguliwa na wananchi.
Marais wa Tanzania tangu muungano na mchango wao kwa taifa
Mwaka Awamu Jina la Rais Mchango kwa Taifa
 aliongoza harakati za kudai Uhuru
 alishiriki kuanzisha muungano ati ya
Tanganyika na Zanzibar
Julius Kambarage  aliasisis mfumo wa ujamaa na
1964-1985 Kwanza
Nyerere kujitegemea
 aliasisi misingi ya elimu kwa wote
 alidumisha amani, umoja na
mshikamano
 kuanzisha sera ya soko huria
1985-1995 Pili Ali Hassan Mwinyi  kuruhusu kuanzishwa kwa mfumo wa
vyama vingi
 kuongeza uwazi katika utendaji wa
serikali
Benjamin William
1995-2005 Tatu  kuanzisha mfumo wa ubinafsishaji
Mkapa
 kuboresha mfumo wa ukusanyaji
mapato ya serikali
 kuboresha miundombinu mfano
barabara na madaraja
 ujenzi wa shule za kata na vyuo vya
2005-2015 Nne Jakaya Mrisho Kikwete
elimu ya juu
 Mapambano dhidi ya magonjwa mfano
malaria na UKIMWI
 elimu bila malipo kwa wote kuanzia
2015-2021 Tano John Pombe Magufuli
darasa la awali mpaka kidato cha nne
 kusimamia ulipaji kodi
 kupambana na ufisadi
 kupambana dhidi ya madawa ya
kulevya
 kusimamia uwajibikaji katika sekta za
umma
 kuimarisha ushirikiano wa kimataifa
 kuendeleza miradi ya kimkakati ya
kimaendeleo
 kuongeza ukusanyaji wa kodi serikalini
2021- Sita Samia Suluhu Hassan
 kuongeza fursa za elimu kwa watoto
wa kike
 kuongeza idadi ya miundombinu ya
mashuleni

Mawaziri wakuu wa Tanzania tangu Muungano wa Tanganyika na Zanzibar


Mwaka Awamu Majina ya Mawaziri Wakuu
1. Rashid Mfaume Kawawa
2. Edward Moringe Sokoine
1972-1985 Kwanza
3. Cleopa David Msuya
4. Salim Ahmed Salim
1. Joseph Sinde Warioba
1985-1995 Pili 2. John Samwel Malecela
3. Cleopa David Msuya
1995-2005 Tatu 1. Fredrick Truway Sumaye
1. Edward Ngoyay Lowassa
2005-2015 Nne
2. Mizengo Kayanza Pinda
2015-2021 Tano 1. Majaliwa Kassim Majaliwa
2021- Sita 1. Majaliwa Kassim Majaliwa
Julius Kambarae Nyerere alikuwa Waziri Mkuu wa kwanza wa Serikali ya Tanganyika.
Kuanzia tarehe 9 Disemba mwaka 1961 hadi tarehe 22 Januari mwaka 1962. Kuanzia mwaka
1962 hadi mwaka 1972 hakukuwa na cheo cha Waziri Mkuu hadi mwaka 1972 kiliporudishwa
tena.

5.2 Mchango wa viongozi wakuu wa Serikali ya Tanzania


Mchango wa viongozi wakuu katika taifa letu ni:
a) kusimamia ulinzi na usalama
b) kuboresha huduma za jamii mfano, afya na elimu
c) kujenga miundombinu
d) kudumisha umoja na mshikamano
e) kusimamia ulipaji kodi
SURA 6: KUSOMA RAMANI
6.1 Kubaini vitu vilivyomo darasani
Ramani ni mchoro wa kitu kama kinavyoonekana kutoka juu. Picha ni mchoro wa kitu kama
kinavyoonekana kikiwa mbele yako. Kwa kawaida, kila darasa huwa na vitu vifuatavyo; meza
ya mwalimu, madawati ya wanafunzi, kabati la vitabu, ubao, kiti cha mwalimu, michoro ya
ukutani, tenga la takataka.

6.2 Tofauti kati ya vitu halisi, picha na ramani


Tofauti Vitu halisi Picha Ramani
Vinaonesha umbo Inaonesha umbo la kitu Inaonesha umbo la
halisi kama kama kinavyoonekana kitu kama
kinavyoonekana kikiwa mbele yako. kinavyoonekana
Uhalisia
kutoka pande zote Picha huonesha umbo kutoka juu. Ramani
yaani vina urefu, upana bapa lenye urefu na huonesha umbo bapa
na kimo upana lenye urefu na upana
Ukubwa haulingani na Ukubwa haulingani
ukubwa halisi wa kitu. na ukubwa halisi wa
Ukubwa Vina ukubwa halisi Picha inaweza kuwa kitu au eneo. Mara
kubwa au ndogo nyingi ramani
kuliko kitu halisi inakuwa ndogo
Inachorwa kwa
Huchorwa kwa mkono
Hupatikana katika mkono kwenye
Upatikanaji au kupigwa kwa
mazingira karatasi, ardhi au
kamera
sehemu yoyote bapa

6.3 Jinsi ya kuchora ramani


Picha ni mchoro wa kitu kama unavyokiona mbele yako. Vile vile, ramani ni mchoro wa kitu
kama unavyokiona ukikiangalia kutoka juu. Hivyo, ramani huonesha sehemu ya juu tu.
Haioneshi kimo cha kitu.

SURA 7: MFUMO WA JUA


7.1 Vitu vinavyounda mfumo wa jua
Mfumo wa jua ni mpangilio au utaratibu wa sayari kuzunguka jua. Sayari ni gimba
linaloumbwa na miamba ambalo huzunguka jua kupitia njia maalumu. Vitu vinavyounda
mfumo wa jua ni kama vile:
(a) Jua
(b) Sayari
(c) Asteroidi
(d) Meteroidi
(e) Kometi
7.2 Kufafanua vitu vinavyounda mfumo wa jua
Mfumo wa jua umezungukwa na sayari nane ambazo ni: Zebaki, Zuhura, Dunia, Mirihi,
Sumbula, Sarateni, Zohali na Kausi. Vile vile, kwenye mfumo wa jua kuna vitu vingine kama
vile asteroidi, kmeti na meteroidi. Jua nalo ni sehemu ya mfumo wa jua.
Jua lina umuhimu mkubwa katika maisha yetu kama vile; hutupatia mwanga wakati wa
Mchana, hukausha mazao na nguo; husababisha mazao kukua.

SURA 8: KUTUNZA RASILIMALI ZETU


8.1 Kubaini na kutunza rasilimali za familia yetu
Rasilimali ni vitu tulivyonavyo katika familia na shule, ambavyo tukivitumia vizuri hutuletea
maendeleo. Vitu hivyo ni kama vile mifugo, ardhi, mazao, na vyombo vya nyumbani. Faida
zinazopatikana kutokana na rasilimali za familia yetu ni kama vile
(a). kujipatia fedha za kujikimu; baada ya kuziuza au kuuza bidhaa zinazozalishwa.
(b). kupata malazi na kivuli
(c). kupata chakula kama vile mayai, nyama, mazao, maziwa
(d). kutupatia mbolea

Vitendo vinavyoonesha matumizi mabaya ya rasilimali za familia ni:


(a). kuuza mifugo bila idhini ya familia
(b). kuiba baadhi ya rasilimali ya familia
(c). kuacha maji yakimwagika ovyo

Njia tunazotumia kutunza rasilimali za nyumbani kwetu ni:


a) kufuga mbwa
b) kujenga uzio
c) kuweka mlinzi
d) kupanda miti na maua
e) kufanya usafi wa mazingira
f) kutumia mbolea

8.2 Kubaini rasilimali za familia


Kuna rasilimali mbali mbali zinazopatikana katika familia. Rasilimali hizi hutofautiana kutoka
familia moja hadi nyingine. Zifuatazo ni rasilimali zinazopatikana kwenye familia nyingi;
nyumba, vyombo vya nyumbani, ardhi, mifugo, ardhi, mazao, fedha.

8.3 Kubaini na kutunza rasilimali za shule yetu


Vitendo vinavyochangia katika uharibifu wa rasilimali za shule yetu ni:
a) kutozitunza ipasavyo
b) kutozifanyia ukarabati wa mara kwa mara
c) kukosa ulinzi wa kutosha
d) kutosimamia ipasavyo
Njia za kulinda rasilimali za shule yetu ni:
a) kuwe na usimamizi wa kutosha
b) kuwepo na mlinzi
c) kuwe na ukarabati wa mara kwa mara
d) kila mtu awe mlinzi wa mwenzie katika matumizi ya rasilimali

SURA 9: UZALISHAJI MALI


9.1 Kutambua shughuli za uzalishaji mali katika familia
Shughuli za uzalishaji mali ni njia mbalimbali za kujipatia kipato. Shughuli hizo ni kama vile
uvuvi, kilimo, na ufugaji. Shughuli za uzalishaji mali huwasaidia watu kupata chakula na
fedha. Kwa mfano watu hulima ili kupata chakula. Pia, huuza mazao ili kupata fedha za
mahitaji kama vile kununulia nguo na kujenga nyumba.

9.2 Kubaini shughuli za uzalishaji mali


Shughuli za uzalishaji mali zinazofanyika katika sehemu ninayoishi ni:
(a). ufugaji wa nyuki na samaki
(b). kilimo cha bustani ya mbogamboga
(c). ufugaji wa kuku, ng’ombe, kondoo, na mbuzi
(d). uuzaji wa duka
(e). uvuvi wa samaki

9.3 Shughuli za uzalishaji mali katika familia


Shughuli za uzalishaji mali zinazofanyika katika familia yetu ni:
a) ufugaji wa samaki, kuku wa mayai
b) kilimo cha mazao ya chakula
c) uvuvi wa samaki
d) biashara
e) duka la vyakula,

Madhara ya kutoshirikiana katika kazi za uzalishaji mali ni:


a) kukosa umoja
b) kuleta migogoro katika jamii
c) kukosa ufanisi katika kazi
d) kupungua kwa kipato

SURA 10: KUTAMBUA FURSA KATIKA MAENEO MBALI MBALI


10.1 Kubaini fursa za shughuli za uzalishaji mali katika maeneo mbalimbali
Shughuli mbalimbali za kiuchumi hutegemea fursa zilizopo katika mazingira. Watu
wanaoishi sehemu zenye misitu hupasua mbao na kutengeneza samani. Wale wanaoishi
sehemu zenye mito, maziwa na bahari huvua samaki. Wale waliopo kwenye mikusanyiko ya
watu hupata fursa ya kufanya biashara. Watu wanaoishi sehemu zenye mvua wana fursa ya
kufanya shughuli za kilimo. Shughuli hizi za uzalishaji mali hujulikana kama shughuli za
kiuchumi.

10.2 Kutambua fursa zilizopo katika maeneo yenye rutuba


Fursa zilizopo katika sehemu zenye rutuba ni:
a) kilimo; mazao yanayostawi kwenye maeneo haya ni kama vile mpunga, maharagwe,
mahindi, viazi vitamu
b) ufugaji; mifugo kama vile mbuzi, ng’ombe, kondoo.
c) biashara; biashara za mazao ya kilimo na ufugaji.

10.3 Kubaini fursa zilizopo kwenye ardhi


Ardhi ndio msingi mkuu wa shughuli za kiuchumi kwa sababu shughuli zote hufanyika juu ya
ardhi. Shughuli hizi ni kama vile kilimo, ufugaji, viwanda, biashara.

10.4 Kutambua fursa zilizopo katika maeneo yenye mvua


Fursa zinazopatikana sehemu zenye mvua ni kilimo, ufugaji, biashara. Faida za mvua ni kama
vile: hukuza mazao; inaotesha majani kwa ajili ya mifugo; hutupatia maji na hutupatia
kitoweo/senene.
Madhara ya mvua nyingi ni kama vile, huleta mafuriko, husababisha mazalia ya mbu na
huharibu miundombinu.

You might also like