You are on page 1of 4

MsomiBora.

com
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
MTIHANI WA MUHULA WA I WA MASOMO KATA YA
KISWAHILI DARASA LA V MEI 2021.
SEHEMU A: CHAGUA HERUFI YA JIBU SAHIHI.
1. Mnacheza mpira. “Kiambishi cha nafsi kilichotumika katika
sentensi hii ni cha nafsi gani?. (a) ya tatu wingi (b) ya pili
umoja (c) ya kwanza wingi (d) ya pili wingi ( )
2. Mwalimu amesimama. “Ni sentensi ipi kati ya hizi zifuatazo
inakanusha sentensi hiyo?
(a) mwalimu alisimama (b) mwalimu hajasimama (c)
mwalimu hakusimama (d)mwalimu hatasimama ( )
3. Neno linalojumuisha maneno haya meza, dawati, kiti, kabati
ni lipi?
(a) Samani (b) Thamani (c) Dhamani (d) Zamani ( )
4. Chakula kitaletwa kutoka mjini. Sentensi hii ipo katika
wakati gani? (a) uliopo (b) uliopita (c) ujao (d) timilifu
5. Sikuwa na fedha za nauli _______________ sikusafiri. (a)
ninadhani (b) haya (c) pamoja (d) hivyo ( )
6. Kinyume cha neno polepole ni ________________ (a)
harakaharaka (b) taratibu (c) goigoi (d) nyamaza ( )
7. Nyumba wanamoishi nyuki huitwa _________________(a)
Banda (b) kiota (c) kasri (d) mzinga ( )
8. Mtu msafi wa mwili na mavazi huitwaje? (a) nadhifu (b)
shupavu (c) mwadilifu(d) goigoi ( )
9. Kuna kawaida mstari mmoja wa ngonjera huwa na mizani
___(a) sita (b) kumi na sita (c) kumi na mbili (d) nane ( )
10. Wao walikuwa hawana furaha. Taja aina ya nafsi katika
sentensi hii;
1
(a) nafsi ya pili wingi (b) nafsi ya kwanza wingi (c) nafsi
ya tatu wingi (d) nafsi ya tatu umoja ( )
11. Neno lipi ni kisawe cha neno peremende? (a) pipi (b)
biskuti (c) jojo (d) asali ( )
12. Neno lililo kinyume na neno “injika”ni __(a) bandika (b)
ipua (c) funua (d) funua ( )
13. Laiti kama ungalijua ni taabani ___________ (a)
ungelinihurumia (b) ungenihurumia (c)unganihurumia (d)
ungalinihurumia ( )
14. Mtoto huyu alikuwa na bidii darasani _____hakufaulu
mtihani.
(a) hivyo (b) hata hivyo (c) walau (d) badala yake ( )
15. Hawa _________________ wale vijana walioharibu kioo
cha gari la msimamizi (a) ndiye (b) ndivyo (c) ndiwo (d)
ndiyo ( )
SEHEMU “B”: ANDIKA NENO AMBALO NI TOFAUTI
NA MENGINE.
16. Ng’ombe, nyani, chui, njiwa, kondoo
17. Pede, Dama, ukuti, karata , chupa
18. Wali, ugali, chai, pilau, kande
19. Ukucha, kidole , mkono, kiwiko, uso
20. Shati, blnaketi, kofia, suruali, kaptura.
SEHEMU “C” METHALI, NAHAU NA VITENDAWILI
21. Andika kitendawili ambacho jibu lake ni ugonjwa ______
22. Kondoo wetu ana nyama nje na ngozi ndani ___________
23. Kula chumvi nyingi ____________________________
24. Mshika mbili ________________________
25. ________________________kiatu chake dawa.
26. __________________________nafuu ya mchukuzi.
2
27. Vunja mbavu _______________________________
28. Piga vijembe maana yake ni (a) sengenya (b) sema mtu
kwa mafumbo naye akiwepo (c) nong’onezana ( )
29. Usiwe na mkono mrefu maana yake ni (a) usiwe mchokozi
(b) usiwe (c) usiwe mwema (d) usiwe mwizi ( )
30. Andika neno sahihi kutokana na herufi hizi PANUD ___
SEHEMU “D”: ANDIKA MANENO YENYE MAANA
SAWA NA MANENO HAYA.
31. Msalani _____________________________
32. Fedha ______________________________
33. Msichana ____________________________
34. Abadani _____________________________
35. Kauza _______________________________
UTUNGAJI: PANGA SENTENSI ZIFUATAZO KWA
KUANDIKA HERUFI A,B,C,D na E.
36. Siku moja Rehema alipita karibu na lile pango akaumwa na
huyo nyoka.
37. Wanakijiji walipofika katika pango walimwona yule nyoka
wakamuua.
38. Wanakijiji waliposikia yowe walikimbilia ilikotokea sauti.
39. Karibu na kijiji cha MATEMA kulikuwa na pango kubwa.
40. Kwenye pango hilo alikuwa anaishi nyoka mkubwa.
SEHEMU E: UFAHAMU:
SOMA KWA MAKINI HABAI IFUATAYO KISHA JIBU
SWALI LA 41 – 45 KWA KUJAZA NAFASI
ZILIZOACHWA WAZI.
Mzee Likong’o alipokuwa anasema hayo, alielekeza
macho mahali palipokuwa na vigae vya chungu ambacho

3
kiliteketea katika moto ule. Akachukua vile vigae kisha
akasema, “Tandamu” waona vigae hivi vya chungu? Tandamu
akajibu “ndiyo, babu.
Mzee akaendelea, “kilikuwa chungu ambamo nilitia fedha
zangu sarafu na noti ambazo nilidunduliza kila mwaka.
Nilikuwa nikipata fedha hiyo kwa kuuza pamba. Ingawa
pengine nilipata fedha kichele tu, sikufuja mali ila nilijinyima
mengi na kuziweka ili zinifae wakati wa dhiki”
MASWALI:
41. Eleza maana ya neno “ kudunduliza” kama ilivyotumika
katika habari uliosoma.
42. Ni kwa nini mzee Likong’o aliweka fedha zake?
43. Katika habari uliosoma kifungu cha maneno “Nilipata
fedha kichele tu” kina maana gani?
44. Eleza mbinu ambazo mzee Likong’o alitumia kujipatia
fedha.
45. Kwa mujibu wa habari hii, Taja tukio lililosababisha
uharibifu wa fedha zilizowekwa na mzee Likon’go.

You might also like