You are on page 1of 4

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
UMOJA WA SHULE ZA MCHEPUO WA KIINGEREZA MKOANI IRINGA
(IREMSA)

SIMU: 0759 407418/ 0768 565174/ 0759 96463

MTIHANI WA KWANZA WA UTAMILIFU DARASA LA NNE-MACHI 2020


SOMO : KISWAHILI
NAMBA YA MTAHINIWA :______________________
JINA LA MTAHINIWA:_______________________________
SHULE : ________________________________________
WILAYA : ______________________MKOA__________

Jumatatu , 4 Machi 2020 8: 00 -9:30 Mchana


MAELEKEZO KWA WATAHINIWA
1. Mtihani huu una jumla ya maswali matano (5)
2. Jibu maswali yote kwa kufuata maelekezo uliyopewa katika kila
sehemu
3. Ifanye kazi yako kuwa nadhifu
4. Kumbuka kujaza taarifa zako muhimu katika sehemu zilizoachwa wazi
hapo juu

***Mtihani huu una jumla ya karatasi nne zilizochapwa*********


SEHEMU A: IMLA
1. Sikiliza kwa makini sentensi zinazosomwa na msimamizi wa mtihani
kisha uziandike kwa usahihi.
i. ______________________________________________________________

ii. _______________________________________________________________

iii. _______________________________________________________________

iv. _______________________________________________________________

v. _______________________________________________________________

SEHEMU B: MSAMIATI, SARUFI NA MATUMIZI YA LUGHA


2. Chagua jibu sahihi kisha andika herufi ya jibu hilo kwenye kisanduku:
i. Neno Mchwa linaundwa na silabi zipi?
(a). M, c,h,w,a (c). M,chwa
(b). M, ch, w, a (d). M, ch,wa
ii. Neno HESHIMA lina irabu ngapi?
(a). Sita (c). Tatu
(b). Mbili (d). Tano
iii. Neno lipi kati ya linaweza kuundwa kwa kudondosha silabi moja katika neno
MWALIMU?
(a).Elimu (c). Wali
(b). Walimu (d). Mwali
iv. Lipi kati ya maneno yafuatayo halifanani na mengine?
(a). Mbuni (c). Kunguru
(b). Bundi (d). Nzige
v. Yakinisha sentensi hii: “Elimu haina mwisho”
(a). Elimu siyo mwisho (c). Kusoma kuna mwisho
(b). Elimu ni mwisho (d). Elimu ina mwisho

SEHEMU C: METHALI, NAHAU NA VITENDAWILI


3. (a). Kamilisha methali zifuatazo.
i. Umoja ni nguvu_________________________________________________
ii. ____________________________________ yasiyokuwa na mbu.
(b). Tegua vitendawili vifuatavyo

(iii). Fuu funika fuu funua_________________________________


(iv). Baba kafa kaniachia pete ________________________________________
(c). Nahau kata shauri ina maana gani? __________________________

SEHEMU D: UTUNGAJI
4. Weka alama za uandishi katika sehemu zilizoachwa wazi
Mfano: Unaitwa nani?

i. Mimi ni mwanafunzi ______

ii. Je, unasoma wapi_______

iii. Juma _____Anita na Jenifa wanasoma darasa la nne.

iv. Loooh_______ maji yamemwagika.

v. “Acheni kupika kelele_______Mwalimu alisema

SEHEMU E: UFAHAMU
5. Soma kwa makini hadithi ifuatayo kisha jibu maswali yanayofuata
Hapo zamani za kale kulitokea mgogoro mkubwa sana kati ya ndege na
wanyama. Juhudi zote za kumaliza mgogoro huu zilionekana kugonga mwamba
na hatimaye vita ilianza. Wakati majeshi hayo mawili ya wanyama na ndege
yakijiandaa kupigana, popo alisita kuchagua upande wa kujiunga nao kivita. Jeshi la
ndege lilifika nyumbani kwa popo na kumwambia “ Twende vitani ewe popo ndege
mwenzetu”
Popo alikataa na kusema “ Mimi ni mnyama na si ndege kama ninyi”.
Baadaye jeshi la wanyama nalo lilifika nyumbani kwa popo na kumwambia “
Twende vitani ewe popo mnyama mwenzetu”. Popo alikataa tena na kujibu “ Mimi
ni ndege na wala si mnyama kama ninyi”. Basi kukawa na ngurumo za kutisha za
wanyama shupavu kama vile simba, duma na tembo, na ndege shupavu kama vile
tai na mbuni. Majike wenye ndama na majike wenye makinda walihisi kiama chao
kimefika.
Kwa bahati nzuri sana, katika dakika za mwisho kuelekea vita, muafaka
ulifikiwa kati ya pande hizo mbili na vita ikaepukwa. Kukawa na amani badala ya
mapigano. Makundi yote mawili yakawa na shamrashamra za kusherehekea
kuepukana na mgogoro. Kuona hivyo, popo naye alitamani kuwa sehemu ya
shamrashamra hizo. Alikwenda kwa ndege akitaka kujiunga nao lakini ndege
walimfukuza. Baadayae akaenda kwenye kundi la wanyama nao walimfukuza. Popo
akabaki kuwa njia panda kwani hakuruhusiwa kujiunga na kundi la ndege au kundi
la wanyama.
MASWALI
i. Mgogoro uliotokea hapo zamani uliwahusu akina nani?

__________________________________________________

ii. Nini maana ya nahau kugonga mwamba kama ilivyotumika katika hadithi

hapo juu?________________________________________

iii. Neno kiama katika hadithi hapo juu lina maana gani?

_____________________________________________________

iv. Neno lipi katika hadithi uliyosoma hapo juu lina maana sawa na neno

shangwe?__________________________________________

v. Nani alibaki njia panda?_______________________________________

Kwanini?________________________________________________

You might also like