You are on page 1of 4

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
NEW VISION EDUCATION PLATFORM [NEVEP]

MTIHANI WA MAANDALIZI YA UPIMAJI WA DARASA LA NNE


MOCK DURU YA KWANZA
JUMATANO: 21 OCTOBA 2020
KISWAHILI
Jina la mtahiniwa: _______________________________
Na/Usajili: ________________________________________
Jina la shule: ____________________________________
Wilaya: ____________ Mkoa: ___________________
MAELEKEZO
 Mtihani huu una jumla ya maswali matano. Kila swali lina vipengere vitano.
 Jibu maswali yote kwa kufuata maelekezo ya kila swali.
 Kumbuka hujaza taarifa zako zote hapo juu kwa usahihi.
 Udanganyifu wa aina yoyote hauruhusiwi katika mtihani huu.
KWA MATUMIZI YA WATAHINI TU
SEHEMU ALAMA SAHIHI ZA SAHIHI ZA
WASAHIHISHAJI WAKAGUZI
A.
B.
C.
D.
E.
JUMLA

@NEVEP 2020
SEHEMU A: IMLA
1. Sikiliza kwa makini sentensi zisomwazo na msimamizi kisha
ziandike kwa usahihi sehemu uliyopewa.
i. ___________________________________________________
ii. ___________________________________________________
iii. ___________________________________________________
iv. ___________________________________________________
v. ___________________________________________________
SEHEMU B: MATUMIZI YA LUGHA
2. Changua jibu sahihi kwa kuandika herufi ya jibu sahihi kwenye
kisanduku ulichopewa.
i. Wanafunzi walitembea ____________ miguu kutoka Posta hadi
Makumbusho.
A. Na B. Kwa C. Bila D. La [ ]
ii. Walikwenda maktaba kuazima vitabu wakamkuta _______
anapanga vitabu . [ ]
A. Mkutubi B. Boharia C. Banati D. Librariani
iii. Mama Salome alitaka kuwaona wachuuzi hivyo aliamua kwenda
_____________ kuwaona. [ ]
A. Mahakamani B. Barabarani C. Sokoni D. Baharini
iv. Nini wingi wa neno Mundu?
A. Miundu B. Mundu C. Mwundu D. Vyundu [ ]
v. Nini wingi wa sentensi “ Amenunua pakacha sokoni”
A. Wamenunua pakacha sokoni
B. Wamenunua pakacha sokoni [ ]
C. Wamenunua mapakacha sokoni
D. Wamenunua pakacha masokoni.
SEHEMU C: METHALI, NAHAU NA VITENDAWILI
3. Kamilisha kazi za kifasihi zifuatazo kwa kuandika jibu sahihi kwa
kila swali.
i. Ada ya muja hunena ___________________________________”
ii. Katika mchezo wa kukata na shoka kati ya timu ya Simba dhidi
ya timu ya Yanga. Kamsoko alicheza rafu. Nini maana ya nahau
“Cheza rafu”? ________________________________________
iii. Kitendawili “ Amefika kabla ya mjumbe hajarudi”
____________________________________________________
iv. Andika methali inayofaa kumshauri mtoto asiyependa kujisomea
na kutegemea kuibia kwa mwenzake darasani.
____________________________________________________
v. Nini maana ya nahau “ Fuja mali”
____________________________________________________
SEHEMU D: UTUNGAJI
4. Panga sehemu za barua zifuatazo kwa kuzipa herufi A, B, C, D na
E.
i. Lengo la barua [ ]

ii. Tarehe [ ]

iii. Anuani ya mwandishi. [ ]

iv. Salamu au maamukizi. [ ]

v. Mwisho wa barua. [ ]
SEHEMU E: UFAHAMU

5. Soma kwa makini habari ifuatayo kisha ujibu maswali yafuatayo


kwa makini.
Amina ni mtoto wa kike wa pekee wa mama Dauzeni. Mtoto huyu
anasoma darasa la nne katika shule ya maendeleo mkoani Mwanza.
Siku za Jumamosi na Jumapili huwasaidia wazazi wao kazi ndogo
ndogo za nyumbani. Kaka yake Amina husoma darasa la sita. Baba
yao watoto hawa ni mfugaji na pia ni mkulima. Mama yao watoto
hawa ni muuguzi katika zahanati ya kijiji cha maendeleo. Familia hii
huishi kwa furaha na amani.
Maswali
i. Familia hii ina jumla ya watu ___________________________
ii. Tofauti ya mfugaji na mkulima ni mfugaji hufuga
______________ na mkulima hulima _____________________
iii. Mziwanda katika familia hii ni ___________________________
iv. Taja tabia njema moja hufanywa na watoto wa familia
hii__________________________________________________
v. Ni nini kazi ya Muuguzi?________________________________

You might also like