You are on page 1of 15

121/1-Mtihani Wa Utimilifu 2024

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA


OFISI YA RAISI TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
(TAMISEMI)
MTIHANI WA UTIMILIFU KANDA YA KUSINI
(MIKOA YA LINDI NA MTWARA)

121/1 KISWAHILI 1
(Kwa watahiniwa walioko na wasiokuwa shuleni)
MTIHANI MAALUMU

Muda: Saa 3:30 2024

Maelekezo kwa Watahiniwa

1. Mtihani huu una sehemu A na B zenye jumla ya maswali nane (8).


2. Jibu maswali yote sehemu A na sehemu B jibu maswali matatu (3). Swali la
sita (6) ni la lazima.
3. Simu za mkononi na vitu vyote visivyoruhusiwa havitakiwi katika chumba cha
mtihani.
4. Andika namba yako ya mtihani katika kila ukurasa wa kijitabu chako cha
kujibia.

Mtihani huu una kurasa sita zenye maandishi

Page1 of 6 acsee0001
121/1-Mtihani Wa Utimilifu 2024

SEHEMU A (ALAMA 40)


Jibu maswali yote kutoka sehemu hii.

1. Soma kifungu cha habari kifuatacho kwa makini kwa makini kisa jibu maswali
yanayofuata
NAKUMBUKA enzi zile za utoto. Utoto ni raha sana japokuwa wakati wa
utoto mtu huwezi kuelewa, wewe unakuwa huna “presha” ya jambo lolote lile.
Kazi yako kula-kulala-kucheza!
Lakini dunia hii ni ya maajabu! Watoto wanatamani wangekuwa watu wazima ili
wafanye kila kitu, vile wapendavyo bila kuhitaji “ruksa” ya mtu awaye yote.
Wakubwa nao wanatamani wangerudi kuwa watoto ili waepukane na “joto la
jiwe” ya maisha, kwani wangekuwa chini ya vivuli vya wazazi wao. Kadhalika
wanatamni kurudi utotoni ili kurekebisha mambo fulani waliyokosea na kufanya
wapate joto ya jiwe ukubwani
Siku moja hivi karibuni tukiwa sebuleni, mimi, memsap na watoto wetu
wawili, tukitafakari dunia inavyozunguka palitokea kituko. Kituko hicho ndicho
kilichonifanya nione utoto ni kitu kingine!
Watoto nilionao ni wawili tu (mimi ni kizazi kipya kilichonionesha ile nyota ya
jangwani!) kwa kuwa wapo wawili tu wanajitahidi kupendana, kuonyesha
ushirikiano, umoja na mshikamano katika masuala yote
Ni hivi karibuni tu walifikia muafaka wa wao kwa wao wa “kutosemeana” kwa
baba au mama pale mmojawapo anapofanya makosa, mkataba huo ulikuwa ni siri
yao mpaka ulipofichuka siku hiyo tuliyobarizi pamoja sebuleni
Siku fulani nilikuwa nimeandaa makala moja ya “kauli ya mlalahoi”
niliyoipachika jina la “ng’ombe wa mayai na kuku wa maziwa”. Niliacha mezani
na kurandaranda nikitafuta uongo mwingine wa kuwavunja watu mbavu zao.
Asalale! niliporudi nilikuta yote imemwagikiwa na mchuzi. Mbona niligeuka
mbogo! kila mtu akawa anasema, “siyo mimi! siyo mimi!”. Nikafikiri labda ni
“Jini kizibo” limeamua kuchafua hali ya amani na masikilizano nyumbani kwetu
maana kila mtu “Siyo yeye!”
Siku hiyo tuliyobarizi niliikumbuka makala ile mwanana, nikawaza usumbufu
nitakao upata kuanza kuandaa, makala nyingine. Nikataka kukumbushia lakini
nikaona nitavuruga utulivu uliopo. Wakati namaliza kufikiri hivyo, mziwanda
wangu akaanza kumwambia kaka yake,
“Kaka! kaka! si unaona sijasema kwa baba! kaka mtu akamkonyeza akimkataza
asiendelee kuharibu mambo”. Lakini mdogowe hakumwelewa.
“Kaaka! si unaona sijasema kwa baba ulivyomwagia mchuzi makaratasi yake?”
alizidi kusisitiza.

Page2 of 6 acsee0001
121/1-Mtihani Wa Utimilifu 2024

“Alaa!” nikamaka. Yaliyofuatia utajaza mwenyewe!, lakini kabla sijageuka


kuwa “pilato” nikasikia taarifa za Ntukufu akiwashushua waandishi wa habari
kwa “kujigonga” kila wakati kumsifu yeye tu na kumpa utukufu wa utukufu
“alioukataa”
Kila alipoangalia TV aliona habari zake, aliposoma magazeti ya sebuleni, yeye tu;
ya mtaani? Yumo! Wenye kudai kuwa ameiga mtindo wa kuwagwaya waandishi,
wenye kumchora akijichana na samaki nchanga, mradi tu!
Wenye kumwita yeye Ntukufu japokuwa amerudia tena na tena “kukataa”
bado wapo. Hata mlalahoi anawashangaa maana yeye hazungumzii habari zake
wala kumwita Ntukufu!
Heri mimi sijasema.
Maswali
(a) Andika kichwa cha habari uliyosoma
(b) Mwandishi ana maana gani anaposema “mimi ni kizazi kipya kilicho iona ile
nyota ya jangwani”
(c) Ni kituko gani ambacho mwandishi amesema, kinachomfanya aone utoto ni
kitu kingine?
(d) ELeza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumika katika habari
uliyosoma?
(i) Joto ya jiwe
(ii) Chini ya vivuli vya wazazi wao
(iii) Memsap
(iv) Tulivyobarizi
(v) Nikamaka
2. Chagua herufi ya jibu lililo sahihi katika maswali yanayofuata
(i) Sehemu ya msingi ya neno ambayo pia haibadiliki badiliki huitwa
(A) Shina
(B) Mzizi
(C) Viambishi
(D) Mofu tegemezi
(ii) Dhima mojawapo ya mofu “ni” ni pamoja na
(A) Kudokeza urejeshi
(B) Kuunganisha sentensi
(C) Ukubwa wa kitu

Page3 of 6 acsee0001
121/1-Mtihani Wa Utimilifu 2024

(D) Kudokeza dhana ya idadi


(iii) hutumika kurejelea nomino au kiwakilishi ambacho kimetajwa
kabla ya kitenzi katika tungo.
(A) Upatanisho wa kisarufi
(B) Ngeli za nomino
(C) O-rejeshi
(D) Kiima katika sentensi
(iv) Ni tungo yenye uarifishaji mkamilifu ikihusisha pande kuu mbili
(A) Tungo kirai
(B) Tungo kishazi
(C) Tungo neno
(D) Tungo sentensi
(v) “Amepigwa na fimbo” mofu na katika tungo tajwa hudokeza dhana
gani?
(A) Kitenzi kishirikishi
(B) Kiunganishi
(C) Kihusishi
(D) Nafsi
(vi) ni kundi la majina linalouwiana kwa kuzingatia maumbo ya umoja
na wingi na upatanisho wa kisarufi
(A) Ngeli za nomino
(B) Upatanisho wa kisarufi
(C) O-rejeshi
(D) kira nomino
(vii) Zifuatazo ni alomofu za kauli ya kutendea isipokuwa
(A) le
(B) li
(C) e
(D) lik
(viii) Mfano mmojawapo wa muundo wa silabi za irabu pekee ni
(A) Baba
(B) Mbwa
(C) Springi
(D) Oa

Page4 of 6 acsee0001
121/1-Mtihani Wa Utimilifu 2024

(ix) Taratabu, kanuni na sheria zinazo mwongoza mtumiaji wa lugha kutumia


lugha hiyo kwa ufasaha hujulikana kama
(A) Umahiri katika lugha
(B) sarufi
(C) Ulumbi
(D) Ustadi
(x) “Ukuta umebomoka” sentensi hiyo ipo katika ngeli ya ngapi kwa kuzingatia
kigezo cha upatanisho wa Kisarufi
(A) Tatu
(B) Tano
(C) Sita
(D) Saba
3. Andika kweli kwa sentensi ambayo ina ukweli na sikweli kwa sentensi isiyo na
ukweli
(i) Neno linaloelezea zaidi kuhusu kitenzi huitwa kivumishi
(ii) Ni neno linaloelezea zaidi kuhusu nomino au kiwakilishi
(iii) Chagizo ni kielezi kinachokaa upande wa kiima wa sentensi
(iv) Tungo na sentensi hutofautiana zaidi katika miundo yake
(v) Tofauti ya msemaji inayosababishwa na athari za kimazingira huitwa
matamshi
(vi) Mofu “Ki” huweza kutumika kama sehemu ya mzizi katika neno
(vii) Irabu ni sehenmu ya neno ambayo huweza kutamkwa mara moja au kwa
pamoja kama fungu moja la sauti
(viii) Kwa ujumla kuna aina tano za mofu
(ix) Kuna baadhi ya mizizi inabeba uarifishaji mkamilifu kimuundo na
kimaana
(x) Konsonanti ni sauti inayotamkwa pasi na kuwepo kwa mzuio wa hewa
wowote kutokea mapafuni kwenda nje kupitia chemba cha kinywa na
pua

Page5 of 6 acsee0001
121/1-Mtihani Wa Utimilifu 2024

4. (a) Oanisha kati ya sehemu A na B


SEHEMU A SEHEMU B

(i)
Rejesta (A)Mataputapu
(ii)
Utata (B)Paka
(iii
MIsimu (C)Uhusisha lugha ya wavuvi
(iv)Umahiri katika (D)Uhusisha stadi kuu nne za lugha
lugha (E)Tofauti zianzojitokeza katika lugha kuu
(v) Lahaja moja
(F) Ulumbi katika lugha
(G) usababisha kuchanganyikiwa na hata
kupoteza mwelekeo

(b) Kwa kufuata mtirirko wa ngeli za nomino, onesha maumbo ya O-rejeshi


yanavyoweza kujitokeza katika ngeli za nomino kwa mtazamo wa kisasa.
(i)
(ii)
(iii)
(iv)
(v)

SEHEMU B (ALAMA 60)


Jibu maswali matatu (3) kutoka sehemu hii swali la sita (6) ni la lazima.

5. “Serikali ya awamu ya tano na sita imefanya jitihada za makusudi katika kukuza


na kuedeleza lugha ya Kiswahili nchini Tanzania baada ya uhuru” Thibitisha kauli
hiyo kwa kutaja hoja tano (5)
6. (a) Nini maana ya tafsiri
(b) Tasfiri ili iweze kuwa bora na nzuri, ni lazima mwisho wa mchakato wa
kutafsiri uifanyie tathmini, fafanua mbinu zinazotumika kutathmini tafsiri.
Taja hoja sita (6)
7. (a) Nini maana ya kadi ya mwaliko
(b) Taja mambo sita (6) muhimu yanayopaswa kuzingatiwa katika kuandika kadi
ya mwaliko.
8. Unafikiri ni kwa nini watumiaji wengi wa lugha ya Kiswahili hupenda
kuchanganya Kiingereza katika mazungumzo ya Kiswahil? Taja hoja tano (5).

Page6 of 6 acsee0001
121/1-Mtihani wa Utamilifu 2024

PRESIDENT’S OFFICE

REGIONAL ADMINISTRATION AND LOCAL GOVERNMENT

ADVANCED CERTIFICATE OF SECONDARY EDUCATION EXAMINATION

MTIHANI WA UTAMILIFU KANDA YA KUSINI KIDATOO CHA SITA

(MTWARA NA LINDI)

121/1 KISWAHILI 1

MUONGOZO WA USAHIHISHAJI

Page1 of 9 acsee0001
121/1-Mtihani wa Utamilifu 2024

1. Mwanafunzi anatakiwa ajibu maswali kutokana na habari aliyosoma kama


ifuatavyo
(a) Kichwa cha habari kinapaswa kiwe MAISHA ENZI ZA UTOTO (01
Alama)
(b) Mwandishi and maana kuwa “yeye ni mtu aliyezaa kwa kufuata uzazi wa
mpango au njia za kisayansi”
(02 Alama)
(c) Kitu kinachomfanya mwindishi aone utoto ni kitu kingine ni plae ambapo
alipokuta makala yake yamlalahoi ilipomwagikiwa na mchuzi na kisha
watoto kushindwa kumtaja aliyefanya kitendo hicho kwa kuteteana. (02
Alama)
(d) Kueleza maana ya maneno ya fuatayo
(i) Joto ya jiwe - ugumu wa maisha /hali ngumu ya maisha (01 Alama)
(ii) Chini ya vivuli vya wazazi wao - chini ya usimamaizi wa malezi ya
wazazi wao (01 Alama)
(iii) Memsap - maana yake mke/ mama watoto (01 Alama)
(iv) Tulivyobarizi - maana yake tulipumzika (01 Alama)
(v) Nikamaka - kufoka/ kuwa katika hali ya hasira (01 Alama)

Page2 of 9 acsee0001
121/1-Mtihani wa Utamilifu 2024

2. Mwanafunzi yampasa achague herufi ya jibu lililo sahihi katika maswali


yanayofuata
(i) B
(ii) D
(iii) C
(iv) D
(v) C
(vi) A
(vii) D
(viii) D
(ix) B
(x) C (@01 = 10 Alama)

Page3 of 9 acsee0001
121/1-Mtihani wa Utamilifu 2024

3. Mwanafunzi inapasa aandike kweli kwa sentensi ambayo ina ukweli na si kweli
kwa sentensi sisiyo na ukweli
(i) Si kweli
(ii) Kweli
(iii) Si kweli
(iv) Kweli
(v) Si kweli
(vi) Kweli
(vii) Si kweli
(viii) Kweli
(ix) Kweli
(x) Si kweli (@01 = 10 Alama)

Page4 of 9 acsee0001
121/1-Mtihani wa Utamilifu 2024

4. (a) Mtahiniwa anmepaswa kujibu kwa kuoanisha kati ya sehemu A na B kama


ifuatavyo
(i) Rejesta - C
(ii) Utata - B
(iii) misimu - A
(iv) Umahiri katika lugha - D
(v) Lahaja - E (@01 = 05 Alama)
(b) Mtahiniwa inapasa afuate mtiririko wa ngeli za nomino na aoneshe maumbo
ya O-rejeshi yanavyoweza kujitokeza katika ngeli za nomino kwa mtazamo
wa kisasa
(i) YE - O
(ii) O - YO
(iii) LO - YO
(iv) CHO - VYO
(v) O - ZO (@01 = 05 Alama)

Page5 of 9 acsee0001
121/1-Mtihani wa Utamilifu 2024

5. Mwanafunzi ataje hoja tano zinazothibitisha kuwa serikali ya awamu ya tano sita
imefanya jitihada kubwa katika kukuza na kuendeleza lugha ya Kiswahili baada
ya uhuru kama ifuatavyo
(i) Rais wa awamu ya tano Dkt John Pombe Magufuli alihamasisha watanzania
wote kutumia Kiswahili pasipo kuchanganya na lugha ya kigeni
(ii) Kuhutubia kwa mikutano ya ndani nje kwa viongozi wetu mfano Rais wa
awamu ya sita Mh Samia Suluhu Hassan
(iii) Kiswahili kupewa kipaumbele vyuoni, serikali awamu ya sita imewapa
kipaumbele cha mkopo wanafunzi wanasoma Kiswahili
(iv) Kiswahili kutumika mahakamani, kwa mara ya kwanza Rais John Pombe
Magufli wa awamu, ya tano aliruhusu Kiswahili kutumika Mahakamani
(v) Kuanzisha kampeni ya kukifanya Kiswahili kuwa lugha ya kimataifa
inayosema KISWAHILI SAUTI YA DUNIA (@04 = 20 Alama)

Page6 of 9 acsee0001
121/1-Mtihani wa Utamilifu 2024

6. (a) Mtahiniwa yampasa aeleze maana ya tafsiri kama ifuatavyo


Tafsiri ni mchakato wa uhasilishaji wa mawazo katika maandishi kutoka
lugha moja hadi nyingine
mfano Kiswahili kwenda Kiingereza. (02 Alama)
(b) Mwanafunzi afafanue mbinu zinazotumika kutathmini tafsiri kwa kutaja hoja
sita kama ifuatavyo
(i) Ulinganishaji wa matini
(ii) Kutumia tafsiri rejeshi
(iii) Kupima uasili
(iv) Kupima uelewekaji
(v) Kupima uelewekaji
(vi) Kupima ulinganifu (@03 = 18 Alama)

Page7 of 9 acsee0001
121/1-Mtihani wa Utamilifu 2024

7. (a) Mwanafunzi aeleze maana ya kadi ya mwaliko kama ifuatavyo


Kadi ya mwaliko ni karatasi maalumu zenye ujumbe wa kumkaribisha mtu
kwenye sherehe fulani (02 Alama)
(b) Mambo muhimu sita (6) yanayopaswa kuzingatiwa katika kuandika kadi ya
mwaliko ni kama yafuatavyo
(i) Jina la mwandishi na anwani yake
(ii) Jina la mwandikiwa au mwalikwa
(iii) Lengo la mwalikaji kwa ufupi
(iv) Tarehe ya mwaliko
(v) Mahali pa kukutania
(vi) Wakati wa kukutania
(vii) Jibu lipelekwe kwa nani (@03 = 18 Alama)

Page8 of 9 acsee0001
121/1-Mtihani wa Utamilifu 2024

8. Mtahiniwa atoe sababu za kuchanganya kiingereza katika mazungumzo ya


Kiswahili kama ifuatavyo
(i) Kasumba
(ii) Kuonesha umahiri wa lugha
(iii) Ukosefu wa msamiati
(iv) Kukidhi haja ya mawasiliano
(v) Kudhani kuwa ndio ujuzi wa lugha
(vi) Kuweka usiri katika mazungumzo (@04 = 20 Alama)

Page9 of 9 acsee0001

You might also like