You are on page 1of 25

USHAIRI MASWALI NA MAJIBU

atikaschool.org/ushairi-maswali-na-majibu

USHAIRI MASWALI NA MAJIBU MODEL31012023001


31/1/2023

0 Comments

​Soma shairi lifuatalo kisha uyajibu maswali.


Mungu naomba subira, subira nayo imani
Imani iliyo bora, bora hapa duniani
Duniani mwa kombora, kombora nayo hiani
Hiani pamwe ukora wenye kuhini.

Kuhini kwenye kiburi, kiburi na ufidhulu


Ufidhuli wa kudhuri, kudhuri wangu muwili
Muwili hata kiclari, kidari kuwa thakili
Thakili kisinawiri, kisinawiri misuli.

Misuli kuwa hafifu, hafifu kama muwele


Muwele wa hitilafu, hitilafu ya nduwele
Nduwele kutakilifu, kutakilifu milele
Milele kutoniafu, kutoniafu na vishale.

Vishale vinitomele, vitomele vikwato


Vikwato pia maole, maole kufanya mito
Mito ya matozi tele, tele mithili kitoto
Kitoto kilo vipele, vipele vyenye fiakuto.

1/25
Fukuto lanipa neno, neno hili kutamka
Kutamka wazi vino, vino subira kutaka
Kutaka imani mno, mno n’sipate wahaka
Wahaka wa matukano, matukano na mashaka.

Mashaka haya ya leo, leo yawe yamepita


Yaniepita na vilio, vilia vipishe nyota
Nyota njema ing’arao, ing’arao kunikita
Kunikita salamani, salamani nikadata.

​Maswali
a) Kwa nini nafsi neni inaomba subira na amani? (al.2)
b) Shairi hili ni la aina gani kwa kuzingatia (al.4)
(i) Mpangilio wa maneno
(ii) Mpangilio wa vina.
c) Kwa kutolea mifano eleza mbinu mbili za lugha zilizotumika katika shairi. (al.4)
d) Andika ubeti wa tatu kwa lugha nathari. (al. 4)
e) Kwa kutolea mifano, eleza jinsi uhuru wa kishairi ulivyotumiwa kutekeleza arudhi. (al.6)

Majibu
​(a) Ili asiwe na wasiwasi ya kutukanwa na huhiniwa aepuke kufanyiwa mabaya. 1 x 2 =2

(b) (i) Pindu/mkufu/nyoka (al.1)


Kwa sababu neno la mwisho katika mshororo wa mwisho wa ubeti linatumiwa kuanzia ubeti unaofuata. (al.
1)
(ii) Ukaraguni (al.1)
Vina vya kati na vya mwisho vinatofautiana kutoka ubeti mmoja hadi mwingine. (al.1)

(​ c) (i) Tashbihi
- Hafifu kama muwele
- Tele mithili kitoto.(al.2)
(ii) Uradidi/Takriri
- Subira’
- Bora, kombora, ukora
- Kiburi, kudhuri n.k.(al.2)

(d) (i) Misuli kuwa dhaifu sana kama ya mgonjwa.


(ii) Hasa mgonjwa mwenye tatizo la
(iii) Ambao unasumbua sana daima na (iv) usiopona kwa vishale. (zote4 x 1 = 4)

(​ e) (i) Inkisari - kuleta urari wa mizani k.m kilo — kilicho.


(ii) Tabdila - kuleta urari wa vina k.m. kudhuri — kudhuru maole — maozi.
- Kuleta urari wa mizani k.m nduwele — ndwele
muwili — mwili
(iii) Mazida - kuleta urari wa vina pia mizani.
- Vinitomele - vinitome.
Kutaja na matumizi (al.1)
Mfano (al.1)
Zote 3 x 2 = 6

Read More

0 Comments
USHAIRI MASWALI NA MAJIBU MODEL18012023003
18/1/2023

0 Comments

​Mkatanimkatika, harithihatorithiwa
Sinaninalolishika, walaninalochukuwa
Mlimwengukanipoka, hata tone la muruwa!
Mrithininiwanangu?

2/25
Sinango’ombesinambuzi,sinakondesinabuwa
Sinahatamakaazi, mupasayokuyajuwa
Sinamazurimakuzi, jinsinilivyoachiwa
Mrithininiwanangu?

Sinakazisinabazi, ilawingiwashakawa
Sinachembeyamajazi, mnonikukamuliwa
Nakwa’cheniupagazi, mgumukwenuku’tuwa
Mrithininiwanangu?

Sinasikuachajina, mkatahatasifiwa
Hatanifanye la mana, mnonikulaumiwa
Poleniwanangusana, sinakwenu cha kutowa
Mrithininiwanangu?

Sinaleosinajana, sinakeshokutwaliwa
Sinazizisinashina, walatawikuchipuwa
Sinawanangu mi sana, la kwacha nakuraduwa
Mrithininiwanangu?

Sina utu sinahaki, milayangumeuliwa


Nyumayanguilidhiki, nambeleimekaliwa
N’nawananamikiki, hadin’tapofukiwa
Mrithininiwanangu?

Sinai la keshokwenu,wenyewekuiongowa
Muwanekwanyingi,mbinumwendepasikupuwa
Leo siyo, keshoyenu, kamamutajikamuwa
Mrithininiwanangu?
(Kina cha maisha A.S.Mohammed)
​MASWALI
a) Elezahaliyamzungumzajikatikashairihili ( alama 4)
b) Elezadhamirakuuyamshairikulitungashairihili (alama 2)
c) Ni nanianayezungumziwananafsinenikatikashairihili? (alama 2)
d) Elezatoniyashairihili (alama 2)
e) Fafanuambinutatuzalughazlizotumiwakatikashairihili (alama 3)
f) Tambuabahariyashairihiliukizingatia. (alama4)
a. Mizani
b. Vina
g) Andikaubetiwamwishokwalughayanathari/tutumbi. (alama 3)

MAJIBU
​a) Hali yamzungumzaji. (al 4)
- maishayenyeumaskinimkubwa.
- maishayasiyokuwanamatumaini.
- maishayaliyokosathamani.
- maishayenyekusikitisha.

b) Dhamirakuuyamshairi (al 2)
- kuwahimizawanawemaishaniilikuhakikishamaishamemaya baadaye kwa vile
haliyasasaniyakimaskini.

c) mzungumziwa – watoto (al 1)


nafsineni – mzazi (al 1)

d) toniyashairi (al 2)
- masikitiko
- kutamauka/kukosamatumaini
- yakuhuzunisha

e) mbinutatuzalughazilizotumika. (al 3)
- sitiari – mkatanimkatika
- Balagha – mrithininiwanangu?
- takriri – sina

3/25
f) Bahariyashairiukizingatia. (al 4)
mizani – msuko
vina - ukara

g) Ubetiwamwisho – lughayanathari. (al 3)


mshairianamatumainikwambawanawewataimarishamaishayaoyabaadaye
Anawashauriwafanyebidii, wakabilianenamatatizobilahofu.

Read More

0 Comments
SWALI NA JIBU LA USHAIRI MODEL16012023001
16/1/2023

0 Comments

​Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.

​Hukuja hapa kwa wingi,


Vitimbi vya kila namna,
Kunambia nikuruzuku,
Kimwana awe mwenzio,
Hukumtwaa mwanangu,
Kisema mno walavu,
Vipi wangeuza ngoma,
Mapepo wampigia?

Siwe uloandaa,
Harusi ya kukata na shoka,
Masafu ya magari, yakilalama jua kali,
Hadi kanisani kungia, mimbari wa kusimama,
Kasema utamuenzi, hadi yenu mauko?
Vipi jicho lageukia, mitaani vipaa mwitu?

Hukunabia we fidhuli,
Mwanangu utamtunza?
Taandamana naye daima,
Ja chanda na pete?
Hukumwonjesha tamu, ya ulaghai huyuno?
Midisko wampleka, kizingizia mapenzi,
Vipi wamtezea shere, mwangu kumliza?

Lini taacha dhuluma hizino humfanyiazo,


Tuchukua lini majukumu,
Ya kumlea na vifaranga?
Huachi kulia u waya
Wanao kitelekeza
Nadhiri zako za nitakipu promise,
Zi wapi mwana balaa?

Lini tafumbua maozi, uone huyu nduli,


Alotwala wengi wapendi,
Kwa jicho la nje kuwangia,
Imeanguka miamba mingapi, nayo ngangania kufia dodani,
Zinduka mwana zinduka,
Ailayo waangamiza.
​Maswali
(a) Hili ni shairi huru. Thibitisha. (al 2)
(b) Mwandishi anaibusha masuala kadhaa ya kijamii. Yadokeze (al 2)
(c) Bainisha nafsineni katika shairi hili (al 1)
(d) Eleza toni ya utungo huu. (al 1)
(e) Bainisha matumizi ya: -
Mistari mishata
Mistari kifu

4/25
(f) Eleza kwa kutoa mifano mbinu za kifasihi zilizotumika katika ushairi huu. (al 3)
(g) Eleza vile mshairi alivyotumia idhini ya kishairi katika utungo huu. (al 3)
(h) Bainisha umuhimu wa maswali ya balagha yaliyotumika katika ushairi huu. (al 2)
(i) Andika ubeti wa tatu kwa lugha tutumbi. (al 4)

majibu
Shairi la pili Majibu
(a)
​(i) Hakuna urari wa mishororo katika kila ubeti
(ii) idadi ya vipande hailingani katika kila mshororo
(iii) Hakuna mpangilio maalum wa vina.
(iv) Hakuna urari wa mizani katika kila mshororo 1x2
(b) Masuala yanayoibuliwa na mwandishi.
(i) Dhuluma katika ndoa
(ii) Ukosefu wa uaminifu katika ndoa
(iii) Kutowajibika kwa waume
(iv) Tatizo la ukimwi. 1x2
(c) Nafsineni katika ushairi.
(i) Mtaalam katika masuala ya ndoa;
(ii) Mzazi
(i) Mshauri
(ii) Mlezi 1x1
(d) Toni ya utungo huu.
(i) Malalamishi
(ii) kushauri
(iii) Kuzindua
(iii) Huzuni, hasira (ghadhabu)
(e) Mistari mishata
(i) Hukuja hapa kwa wingi
(ii) Siwe uloandaa.
Mistari kifu.
(i) kusema hapa kwa wingi
(ii) Huachi kulia u waya
(f) Mbinu za kifasihi
(i) maswali ya balagha
(a) Hakuja hapa kwa wingi?
(b) Vipi wangeuza ngoma, mapepo kunipigia?
(c) Vipi wamtezea shere, mwanangu kumuulizia?
(ii) Tashbihi
Taandama naye daima ja chanda na pete
(iii) Utohozi
Walavu
midisko
Nitakipu promisi
(iv) Sitiara / jazanda
Vipaa mwitu – wasichana wengine
Nduli – ugonjwa hatari
Kifaranga – watoto
Miamba – watu mashuhuri
(iv) Kuchanganya ndimi; - nitakipu promise
(vi) Tashihisi / uhuishaji
Masafu ya magari yakilalama jua kali
Vipi jicho lagoukia mitaani vipaa mwitu?
Nadhiri zako za nitakipu promisi, zi wapi mwana
(vii) Nahau / msemo
Kufia kidondani – kupata hasara unapofuata kitu unachokiona cha thamani.
-​Kukata na shoka, kucheza shere. 1x3

5/25
(g) Idhini ya kishairi iliyotumika.
(i) kuboronga sarufi / kufinyanga sarufi
Hadi kanisani kuingia – kuingia hadi kanisani
Hadi yenu mauko – hadi mauko yetu
Mwanangu kumuliza – kumuliza mwanangu.
(ii) Insksari.
Kunambia – ukaniambia
Wanao – wanawako
Tachukua – utachukua
(iii) Lahaja
Huyuno
Mauko
Nitakupiku
Nduli
Maozi
Kuwangia
(iv) kikale
Tezea
Huyuno
Mauko
Nitakupiku
Kuwaingia
Maozi
(iv) Tabdila
Twala twaa
Inkisari – taacha 1x3
(h) Umuhimu wa maswali ya balagha
Kuleta msisitizo wa ujumbe unaoangaziwa
Kumfanyia tashtiti mwanaume kwa yale anayotenda
Kumzindua mwanamume aweze kutekeleza majukumu yake ya ndoa 1x2
(i) Wewe mjeuri uliniahidi ungemtunza mtoto wangu na ungeishi naye daima mapenzi ya dhati lakini
ulimwingiza kwenye mapenzi ya hila kwa kumpeleka disko. Kwa nini unamchezea shere mwanangu
kwa kumliza = 1x4

Read More

0 Comments
SWALI NA JIBU LA USHAIRI MODEL15012023001
15/1/2023

0 Comments

​Soma shairi hili kisha ujibu maswali


Naingia ukumbuni,nyote kuwakariria
Ushairi niwapeni, hoja nitawaachia
Mnipe masikioni, shike nachoelezea,
Taifa sio taifa, pasi kuwa maadili.

Naaanza kwa usalendo, nchi yetu tuipende,


Yadhihirishe matendo, nchi yetu tuilinde,
Wa kila mtu muwendo, usije kawa mpinde,
Taifa sio taifa, pasi kuwa maadili.

Wote tuwe na umoja, tuuache ukabila,


Kabila lisiwe hoja, mwenza kunyima hela,
Taifa letu ni moja, Mkenya ndilo kabla,
Taifa sio taifa, pasi kuwa maadili.

Linda demokrasia, uongozi tushiriki,


Haki kujielezea, wachotaka na hutaki,
Change naweza tetea, demokrasia haki,
Taifa sio taifa, pasi kuwa maadili

6/25
Tena adili usawa, mgao rasilimali,
Bajeti inapogawa, isawazishe ratili,
Idara zilizoundwa, faidi kila mahali,
Taifa sio taifa, pasi kuwa maadili.

Tuwe na uadilifu, twache tamaa ya hongo,


Tusiwe na uadilifu, wa kuwa watu waongo,
Tukomeshe uhalifu, kisha tuache maringo,
Taifa sio taifa, pasi kuwa maadili.

Ubinafsi si adili, ila ni kusaidiya,


Ukiwa nayo maali, asiyenacho patiya,
Kama mtu mswahili, ubinafsi achiya,
Taifa sio taifa, pasi kuwa maadili.

Na invyoelezea, katiba ni kielezi,


Tutii kwa mazoea, hadi kijacho kizazi,
Kwa hayo nitawachia, hiyo ya ziada kazi,
Taifa sio taifa, pasi kuwa maadili.

MASWALI
(​ a) Shairi hili ni la aina gani? Toa sababu (al 2)
(b)
​(i) Onyesha aina mbili za uhuru wa kishairi uliotumiwa katika shairi hili (al 2)
(ii) Bainisha umuhimu wa uhuru wa kishairi uliotaja hapo juu (i) (al 2)
(c) Bainisha kipengele kifuatacho cha kimtindo katika shairi hili (al 1)
Usambamba
(d) Eleza toni ya shairi hili. (al 1)
(e) Bainisha nafsineni katika shairi hili (al 1)
(f) Ainisha shairi hili kulingana na:-
(i) Mpangilio wa vina
(ii) Idadi ya vipande katika ubeti (al 2)
(g) Changanua muundo wa ubeti wa nne. (al 3)
(h) Eleza aina mbili za urudiaji katika shairi hili (al 2)
(i) Andika ubeti wa pili kwa lugha nathari. (al 4)

MAJIBU
(a) Tarbia. Lina mishororo mine katika kila ubeti (al 2)
(b
(1) Aina mbili za uhuru wa kishairi
(i) Inkisari – nachoelezea - ninachoelezea
(ii) Kuboronga sarufi
- ya ziada kazi – kazi ya ziada
- wa kila mtu mwende – mwende wa kila mtu
(iii) Tabdila – kusaidiya – kusaidia
patiya – patia
achiya – achia
(iv) Mazida: maali - mali
Muwendo – mwendo 1x2
(b
(2) Umuhimu wa uhuru wa kishairi uliotajwa hapo juu.
(i) Inkisari – kupata urari wa mizani
(ii) Kuboronga sarufi – kupata urari wa vina
(iii) Kuboronga – kuleta mahadhi katika shairi
(iv) Tabdila – kupata urari wa mizani
(v) Mazida – kupata urari wa mizani
​(c ) Usambamba
(i) Taifa sio taifa
(ii) Pasi kuwa maadili 1x1
(d) himiza/ nasihi / shawishi = 1x1
(e) mwananchi / raia / mzalendo / mkereketwa =1x1

7/25
(f) kuanisha shairi kulingana na:
(i) mpangilio wa vina
Ukaraguni.
(ii) Idadi ya vipande katika ubeti
Mathnawi 1x2
(g) Muundo wa ubeti wan ne.
(i) Vina vya kati ni ‘a’ na vya nje ni ‘ki’
(ii) Mizani ni kumi na sita katika kila mshororo
(iii) Vipande ni viwili, ukwapi na tao
(iv) Mishororo ni minne
(v) Kibwagizo ni taifa si taifa, pasi kuwa maadili 1x3
(h) Aina mbili za urudiaji
(i) Neno – mf taifa, maadili
(ii) Sauti – mf u, a
(iii) Silabi – mf nde, a, li, ngo
(iv) Sentensi / mshororo – taifa sio taifa, pasi kuwa maadili. 1x2
(i) Ninaanza kwa kuwaelezea kuwa tuwe wazalendo na matendo yetu yaonyeshe tunailinda nchi yetu
kwa mienendo mizuri kwa sababu nchi haikamiliki bila kuwa na matendo mema

Read More

0 Comments
​SOMA SHAIRI LIFUATALO KISHA UJIBU MASWALI MODEL25122022001
25/12/2022

0 Comments

​SOMA SHAIRI LIFUATALO KISHA UJIBU MASWALI MODEL25122022001


Ulimwengu ulimwengu, ulimwengu naratibu
Yaliyo kichwani mwangu, nataka kuyatubu
Wayasome ndu zangu, wa mbali na wa karibu
Cha wenye raha na tabu, ulimwengu ni kiwanja.

Ulimwengu ni kiwanja, cha wenye raha na tabu


Wengine wanajikonja, kwa wengine ni adhabu
Kucha na kutwa twahanja, kutafuta matulubu
Cha wenye raha na tabu, ulimwengu ni kiwanja.

Ni uwanja wa balaa, aliniusia babu


Mna mambo yamejaa, ya faraja na kusibu
Na machache ya kufaa, ila mengi ya udubu
Cha wenye raha na tabu,ulimwengu ni kiwanja.

Ni kiwanja cha Amina,Saidi Ali Rajabu


Wengine kitu hatuna, tunaishia kababu
Wale wamejaza sana, wanashindwa kuhesabu
Cha wenye raha na tabu, Ulimwengu ni kiwanja.

Ni uwanja wa urongo, na kweli pia ajabu


Kichwa hudanganya shingo, tumbo kiuno chasibu
Usitumai ubongo, wa nduguyo na swahibu
Cha wenye raha na tabu, ulimwengu ni kiwanja.

Ni uwanja wa walevi, pombe kwao ni dhahabu


Mara vile mara hivi, wakilewa majudhubu
Maneno ya kiujuvi, hujipaka hata shabu
Cha wenye raha na tabu, ulimwengu ni kiwanja.

​ i kiwanja wenye dini, wamtiio wahabu


N
Mashekhe msikitini, humo humfanya muhibu
Mapadiri kanisani, huvihubiri vitabu
Cha wenye raha na tabu, ulimwengu ni kiwanja.

8/25
​ i uwanja wa malofa, lofa mtu mwenye tabu
N
Kusema sana kashifa na moyo kisebusebu
Tunakaribia kuja, kwa kushindwa kujimudu
Cha wenye raha na tabu, ulimwengu ni kiwanja.

Ni uwanja wa faraja, alowajali habibu


Na wengine sitotaja, msinambe ninagubu
Ni uwanja wa viroja, vigumu kuvikutubu
Cha wenye raha na tabu, ulimwengu ni kiwanja.

maswali
(a) Lipe shairi hili anwani ifaayo. (alama 1)
Ulimwengu ni kiwanja
Changamoto ulimwenguni 1 x 1 = alama 1

(b) kwa kutoa mfano, eleza mbinu zozote mbili za lugha zilizotumika katika
shairi.(alama 2)
(b) Istiara/ jazanda – ulimwengu ni kiwanja
Msemo – kutwa kuchwa
Ukinzani/tanakuzi – wenye raha na tabu
Uhuishaji – Kichwa kudanganya shingo (zozote 2x1 = alama 2)

​(c) Eleza jinsi uhuru wa mshairi ulivyotumika katika shairi. (alama 2)


(c) Inkisari – naratibu – ninaratibu
Ndu zangu – ndugu zangu.
Kuboronga lugha – wenye kitu hatuna – wengine hatuna kitu
Utohozi – shehe – sheikh
Padre – padre (2 x 1 = 2)

(d) Andika ubeti wa tatu kwa lugha tutumbi. (alama 4)


(d) babu alimshauri kuwa ulimwengu ni uwanja wa balaa ulionjaa mambo ya faraja na kusibu. Pia alisema
kuwa kuna machache ya kufaidi na mengi ya kuudhi. Kwa hivyo ulimwengu ni kiwanja kwa walio na raha
na walio na taabu.
​(4x1 = alama 4)

​(e)Taja na ueleze bahari zozote mbili zilizotumika katika shairi hili.(alama 2)


​(e) (i) Tarbia – mishororo minne kwa kila ubeti
(ii) Mathnawi – vipande viwili kwa kila mshororo
(iii) Pindu – sehemu ya mwisho kuanzia ubeti unaofuata.
(iv) Ukara – vina vya mwisho vinatirirka na vya kati havitiririki. (2x1 = alama 1)

​(f) Eleza umbo la shairi hili. (alama 4)


(f) (i) Mishororo minne kwa kila ubeti
(ii) Vipande viwili kwa kila mshororo – ukwapi na utao.
(iii) Lina beti tisa.
(iv) Vina vya mwisho vinatiririka na vya kati vinabadilika
(v) Lina kibwagizo – che wenye raha na tabu, ulimwengu ni kiwanja.
(vi) mizani ni 8,8 kwa kila mshororo
4x1 = 4

​(g) Eleza toni ya shairi hili. (alama 1)


(g) masikitiko (alama 1)

​(h) Fafanua dhamira ya mshairi. (alama 2)


(h) Kufahamisha watu hali ilivyo ulimwenguni. Kwamba kuna mazuri na mabaya ili wajihadhari. (1x2= 2)

9/25
​(i) Eleza maana ya msamiati ufuatao kama ulivyotumika katika shairi.(alama2)
(i) Malofa:
(ii) Udubu:
(​ i) Malofa – maskini
(ii) Ndubu – upumbavu (alama 2)

Read More

0 Comments
​Soma shairi kisha ujibu maswali MODEL23122022002
23/12/2022

0 Comments

​SOMA SHAIRI KISHA UJIBU MASWALI MODEL23122022002


Nizike Ningali Hai!: Hassam Muchai
Kipusa Binti Hamadi, siku n’takuwa kimba
Nizikwe Kifudifudi, na yoyo kuyumbayumba
Takuwa bure biladi, matozi ungayasomba
Nizike ningali hai, n’kifa hutonizika

Tena ningaumwa ungo, na mapumu kuugua


Lioze ini na nyongo, na pua zisipumua
Takuwa sina kinyongo, mradi nimeshatua
Nizike ningali hai, n’kifa hutonizika

Nizike sasa mwenzangu, nizike ningali hai


Singojee kufa kwangu, uanze kurairai
Kulilia kifo change, ni bure hakukufai
Nizike ningali hai, n’kifa hutonizika

Nikifa hutonizika, kimwana sanda nunua


Manukato ya kupaka, na nguo za kuanua
Nivishe sione shaka, Washindwe kupambanua
Nizike ningali hai, n’kifa hutonizika

Tena nikande misuli, nikande pande kwa pande


Siate kiwiliwili, shingo, miguu ikande
Umalizapo kiwiliwili, mwenzangu niende shonde
Nizike ningali hai, n’kifa hutonizika

MASWALI
A) Dhamira ya matunzi wa shairi hili ni gani? (Al 2)
B) Bainisha nafsineni katika shairi hili (Al 2)
C) Eleza toni ya shairi hili (Al 2)
D) Changanua muundo wa shairi hili (Al 5)
E) Fafanua maana ya kibwagizo cha shairi hili (Al 2)
F) Eleza mbinu nne ambazo mshairi ametumia kutosheleza mahitaji ya kiarudhi (Al 4)
G) Bainisha bahari ya shairi hili (Al 3)

MONGOZO / MAJIBU
​ ) Dhamira ya mtunzi wa shairi hili ni gani?
a
Kuhimiza watu kutendea wenzao mema wakiwa wangali hai

b) Bainisha nafsineni katika shairi hili


Kipusa Binti Hamadi – Kipusa Binti Hamadi, siku n’takuwa kimba

c) Eleza toni ya shairi hili


Toni ya kushauri – Kipusa Binti Hamadi anatoa ushauri kwamba azikwe angali hai.

10/25
​ ) Changanua muundo wa shairi hili
d
i) Lina ubeti 5
ii) Kila ubeti una mishororo minne
iii) Kila mshororo una vipande viwili isipokuwa ubeti wa tano , mshororo wa pili wenye vipande vitatu
iv) Vina vya ndani na vya nje vinabadilika katika ubeti
v) Lina kibwagizo – Nizike ningali hai, n’kifa hutonizika
vi) Kila mshororo una mizani 16

e) Fafanua maana ya kibwagizo cha shairi hili


Nisaidie ningali hai kwa maana nikifa hutaweza kunisaidia

f) Eleza mbinu nne amabazo mshairi ametumia kutosheleza mahitaji ya kiarudhi


i) Kufinyanga sarufi
Matozi ungayasomba – ungayasomba matozi
na mapumu kuugua – na kuugua mapumu
sanda nunua – nunua sanda

ii) Lahaja
Matozi – machozi
siate – siache

iii)Tabdila
hutonizika – hutanizika
zisipumua – zisipumue

iv) Inkisari
takuwa – nitakuwa
singojee - usingojee

g) Bainisha bahari ya shairi hili


i) Tarbia – lina mshororo minnne katika kila ubeti
ii)Mathnawi – Kila mshororo una vipande viwili isipokuwa ubeti wa tano, mshororo wa pili wenye vipande
vitatu.
iii)Ukaraguni – Vina vya kati na vya nje vinabadilika katika kila ubeti. ​

0 Comments
​Soma shairi kisha ujibu maswali model23122022001
23/12/2022

0 Comments

​SOMA SHAIRI KISHA UJIBU MASWALI MODEL23122022001


Ndugu ona mbwa yule, ambaye ananyekenya;
Yaone mabuu yale, ambayo yamchezeya;
Kuwa leo yuafile, mwili yanautaniya;
Jana awile jasiri!

Juzi shujaa awile, pasiwe kumfikiya;


Kwenye makani yale, alipojisururiya;
Leo kuwa yuafile, mainzi yamchekeya;
Jana awile Jasiri!

Mijino mikubwa ile, ambayo ‘mejitokeya;


Yali kiwaliza wale, karibu walosogeya;
Tena akibweka yule, waoga walijinyiga;
Jana awile jasiri!

Kamwe kuishi milele, kupe ukajinyonyeya;


Walo chini yako wale, muhali unawaziya;
Ameshindwa yule pale,sembuse wewe sikiya;

11/25
Jana awile jasiri!

Kama walo hai wale, yafaa kuzindukiya;


Ni dunia maji male, muhimu kujiwaziya;
Wazipunguze kelele, na kwingi kujishauya;
Jana awile jasiri!

MASWALI
​ afanua ujumbe wa shairi hili (Al 2)
F
a) Eleza muundo wa shairi hili (Al 5)
b) Eleza toni ya shairi hili (Al 2)
c) Ainisha shairi hili kwa kuzingatia (Al 3)
i) Ruwaza ya mistari
ii) Ruwaza ya vipande
iii) Ruwaza ya mizani
d) Eleza mbinu nne ambazo mshairi ametumia kutosheleza mahitaji ya kiarudhi (Al 4)
e) Bainisha sifa mbili za anayezungumziwa katika shairi hili (Al 2)
f) Eleza tamathali mbili za usemi zilizotumiwa katika shairi hili (Al 2)

MWONGOZO / MAJIBU
​ ) Fafanua ujumbe wa shairi hili
a
Shairi linazungumzia jinsi walio na nguvu wasivyowazia walio chini yao na kuwahimiza watu kuzinduka na
kupunguza kelele pamoja na kujishaua

​ ) Eleza muundo wa shairi hili


a
I) Lina beti 5
II) Kila ubeti una mishororo minne
III) Kila mshororo una vipande viwili isipokuwa kibwagizo chenye kipande moja.
IV) Lina kibwagizo – jana awile siri!
V) Vina vya kati na vya nje vinatiririka isipokuwa ubeti wa kwanza, mshororo wa kwanza wenye kina
tofauti
VI) Kila mshororo una mizani 16 isipokuwa ubeti wa pili, mshororo wa pili na ubeti wa tano, mshororo wa
kwanza yenye mizani 15.
VII) Kibwagizo kimekamilika kwa alama hisi!

b) Eleza toni ya shairi hili


Toni ya kushauri – nafsineni anawashauri watu kuzinduka na kupunguza kelele na hali ya kujishaua/kujisif

c) Ainisha shairi hili kwa kuzingatia:


I) Ruwaza ya mistari
Tarbia – Kila ubeti una mishororo mine
ii) Mathnawi – Kila mshororo una vipande viwili isipokuwa kibwagizo chenye kipande kimoja
iii) Ruwaza ya mizani
Msuko – Kibwagizo kina mizani michache kuliko mishororo mingine

d) Eleza mbinu nne ambazo mshairi ametumia kutosheleza mahitaji ya kiarudhi


i) Tabdila
Yamchezeya – Yamchezea
Yanautaniya – Yautania n.k.
ii) Inkisari
‘mejitokeya – imejitokea
Walosogoya – waliosogea
iii) Kikale – awile – alikuwa
iv) Kufinyanga sarufi – kwingi kujishauya – kwingi kujishaua

e) Bainisha sifa mbili za anayezungumziwa katika shairi hili


i) Mwenye vitisho – alipobweka/alipozungumza waoga walijinyia
ii) Mwenye ubinafsi – Hakuwawazia waliokuwa chini yake
f) Eleza tamathali mbili za usemi zilizotumiwa katika shairi hili
i) Jazanda – mbwa
ii) Taswira – mabuu yakimchezea mbwa
iii) Tashihisi- mainzi yamchekea
iv) Chuku – Tena akibweka yule, waoga walijinyinya
v) Sitiari – ni dunia maji male

12/25
Read More

0 Comments
​YALIMWAGIKA
21/12/2022

0 Comments

​YALIMWAGIKA
Lilianza kama wazo, nikawaza,
Niwe na watoto,
Si vikwazo, ghafla mama yao akapatikana,
Kwa rutuba yake,
Akavimba
Kumbe ni mapacha,
furaha!

Majina walishapewa,
Imani kudumu, watazaliwa,
Tungo wakatungiwa,
Amani na Imani,
Baba yao ni malenga
Anatayeita maneno.
Maneno yanaitika.
Nikasubiri.

Wazazi walitamani kupakata,


Amani na Imani
Iwe yao burudani, siyo kama zamani
Wachezee zuliani.
Baba niwaweke kifuani
Na migongoni bila susu, kwa mama yao
Si mtoto hutizama kisogo cha ninake?
Tukangoja!

Furaha kote nyumbani iliwatanda,


Kuyaona makinda yao, kwa kitanda,
Wadondokwe udende, wawapende!
Mama anyonyeshe, kiwatazama machoni,
Kuwagusa mashavuni, waliapo.
Watulie Amani na Imani.

Ukutani ni kiwimbo, baba alishawatungia,


Kushotoni ni wa kike, kuumeni kijanadume
Watulie, Baba yao aliwazia
Wazo likaanza kupokwa.
Hospitali wakiwasili.

Wiki zikajenga miezi


Tamati ikajongea
Kawanunulia mavazi
Walifaa kuvaa
Hawakuvaa!
Vijulanga miezi saba, pukachaka!
Kifo ni mwewe, kikaninyakulia.
Amani na Imani.
Tunalia!
Pema peponi wanetu!

​MASWALI

13/25
a) Eleza jinsi usimulizi ulivyotumika kwenye shairi. (alama 1)
b) Eleza sifa tatu zinazoafiki shairi hili kuwa huru. (alama 3)
c) Shairi hili ni la tanzia. Thibitisha. (alama 1)
d) Tambua mandhari ta tanzia. (alama 1)
e) Tambua nafsineni kwenye ubeti wa kwanza. (alama 1)
f) Eleza toni ya shairi. (alama 2)
g) Onyesha mifano miwili ya matumizi ya sadfa katika shairi. (alama 3)
h) Andika ubeti wa mwisho kwa lugha tutumbi. (alama 4)
i) Eleza maana ya msamiati huu kulingana na shairi. (alama 4)
i.Vijulanga
ii.Susu
iii. Akavimba
iv ..Kiwimbo

YALIMWAGIKA MWONGOZO
​ ).Eleza jinsi usimulizi ulivyotumika kwenye shairi.
A
Ushairi umesimulia safari kabla ya ndoa na katika ndoa.

​ .Eleza sifa tatu zinazoafiki shairi hili kuwa shairi huru.


b
● Idadi ya mishororo katika kila ubeti si sawa.
● Idadi ya vipande katika kila mshororo si sawa.
● Idadi ya mizani katika kila mshororo inatofautiana.
● Limechukua miundo mbali mbali lilivyoandikwa.
● Shairi hili halina kibwagizo.
● Vina vyake vinachanganywa/halina mtiririko wa vina.
● Shairi hili lina alama nyingi za uakifishaji.

​ ).Shairi hili ni tanzia


c
Kuna kifo cha mapacha waliotarajiwa kuzaliwa na walisuburiwa sana na wazazi zao.

​ .Tambua mandhari ya tanzia


d
Hospitalini ndiko walikofia mapacha.

​ ).Tambua nafsineni kwenye ubeti wa kwanza


e
Baba / bwana mtarajiwa/mwanamume.

f​ ).Eleza toni ya shairi.


Toni ya huzuni /majonzi kutokana na kifo cha mapacha Amani na Imani.

​ ).Onyesha mifano miwili ya matumizi ya sadfa katika shairi.


g
● Baba anawaza kuhusu watoto na kumpata mke papo hapo wa kuoa.
● Msemaji anasema akataka’ watoto’ na ghafla ujauzito unakuwa wa mapacha.
● Watoto wanapewa majina Imani n Amani na baadaye mimba kugundulika ni ya mapacha kiume na kike.

H).Andika ubeti wa mwisho kwa lugha tutumbi.


Muda uliendelea kusonga wakisubiri watoto wao kuzaliwa.
Wakanunuliwa mavazi mbalimbali wakitarajiwa kuwapokea japo halikutimia.watoto wakafa mimba ikiwa
ya miezi saba na kuombolezwa.

i​).Eleza maana ya misamiati ifuatayo.


● Vijulanga -Vitoto
● Susu-kitambaa cha kuzuia haja za mtoto.
● Akavimba-akawa mjamzito
● Kiwimbo.- wimbo mfupi

Read More

0 Comments
​Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali MODEL21122022001
21/12/2022

0 Comments

14/25
​Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.
Hizi bombo mwaanika, wa ndizini nashtuka,
Peupe mwazianika, kwenye jua kukauka,
Zingine zimeraruka, aibu zinatufika,
Anikeni kwa kuficha, za ndani mkisafisha.

​ ako kule kwenye bafu, mwaziweka hizo chafu,


N
Hilo nalo nakashifu, mkitoa nitasifu,
Kuziweka maji chafu, hilo ndilo ninahofu,
Anikeni kwa kuficha, za ndani mkisafisha.

​ wenye meza wazileta, wana wenu wakipata,


K
Wageni wakijateta, aibu haitatupata?
Muondoeni utata, hizo zenu twazipata,
Anikeni kwa kuficha, za ndani mkisafisha.
Kwa heshima tudumuni, tufaapo za mwilini,
Tamaduni jifunzeni, msiige uzunguni,
Za bafuni zi jikoni, zi watoto makononi,
Anikeni kwa kuficha, za ndani mkisafisha.

Wino wangu kibindoni, nitatua tamatini,


Za ndani ziwe za ndani,msonyeshe hadharani,
Za bafuni si jikono, msiweke kabatini,
Anikeni kwa kuficha, za ndani mkisafisha.

​MASWALI
a) Pendekeza kichwa mwafaka katika shairi hili. (alama 1)
b) Eleza toni ya shairi hili. (alama 1)
c) Tambua nafsineni katika shairi. (alama 1)
d) Jadili matumizi ya mitindo ifuatayo ya lugha katika shairi hili.
i. Kinaya (alama 2)
ii. Usambamba (alama 2)
iii. Balagha (alama 1)
e) Onyesha kuwepo kwa uhuru ufuatao katika shairi. (alama 3)
i. Tabdila
ii. Kubananga sarufi
iii. Inkisari
f) Andika ubeti wa mwisho kwa lugha mjazo. (alama 4)
g) Eleza muundo wa shairi hili. (alama 5)

MWONGOZO
​1. Pendekeza kichwa mwafaka.
Aibu, Aibu kwetu

​ .Eleza toni ya shairi hili


2
● Toni ya kukasifu/kushtumu/kukejeli mienendo ya kutojali.
● Toni ya kughadhabika Kwa kutojali.
● Toni ya kushauri kuhusu heshima na usiri.

3. Tambua nafsineni wa shairi


Mhusika ambaye amepata aibu kutokana na mienendo ya watu kuanika
mavazi ovyo ambayo anahisi ni vibaya.

​ . Jadili matumizi ya mitindo ifuatayo


4
● Ni kinaya kuwa angependa mavazi fulani yafichwe ilhali yamefichwa bafuni.
● Ni kinaya kuwa anataka zikauke bila kuanika /ilhali zimefichwa.
● Ni kinaya kuwa wageni wanaibika ilhali wenyewe huzitumia na huanika kwao
Usambamba
● Miundo sawa ya mistari/mishororo-anikeni kwa kuficha,z ndani mkisafisha.
● Urudiaji wa maneno –anika,kuficha.
● Urudiaji wa silabi-ka(ubeti wa kwanza) fu(ubeti wa pil) ta (ubeti wa tatu)
Balagha
● Ubeti wa mwisho mshororo wa pili-aibu haitatupata?

15/25
5. Andika ubeti wa mwisho kwa lugha ya mjazo/Nathari.
Mshairi anasema kuwa nguo za ndani zinazoanikwa ovyo/popote,watoto/wana huzipata na kutembea
nazo hata mezani kwa wageni.Hili huleta aibu kubwa na hivyo hushauri watu waanike kwa tahadhari.

6. Onyesha kuwepo kwa uhuru ufuatao katika shairi


● Tabdila –muondoeni badala ya mwondoeni.
● Kubananga sarufi-anikeni kwa kuficha,za ndani mkisafisha. Badala ya mkisafisha za ndani mzianike kwa
kuficha.
● Inkisari-tufaapo badala ya tunapofaa.

7. Eleza muundo wa shairi hili


● Shairi hili lina beti tano.
● Kila ubeti una mishororo minne.
● Shairi hili lina kibwagizo ambacho ni :anikeni kwa kuficha , za ndani mkisafisha.
● Idadi ya mishororo inatoshana kaika kila mshororo;kumi na sita.
● Kila mshororo una vipande viwili, ukwapi na utao.
● Vina vyake vinatofautiana kutoka ubeti mmoja hadi mwingine.

Read More

0 Comments
USHAIRI MASWALI NA MAJIBU MODEL16122022002
16/12/2022

0 Comments

USHAIRI MASWALI NA MAJIBU MODEL16122022002


​Naingia ukumbini, nyote kuwakariria,
Ushairi niwapeni, hoja nitawaachia,
Mnipe masikioni, shike nachoeleza,
Taifa sio taifa, pasi kuwa maadili.

​ aanza kwa uzalendo, nchi yetu tuipende


N
Yadhihirishe matendo, nchi yetu tuipende,
Wa kila mtu mwendo, usije kawa mpinde,
Taifa sio taifa, pasi kuwa maadili.

​ inda demokrasia, uongozi tushiriki,


L
Haki kujielezea, wachotaka na hutaki,
Changu naweza tetea, demokrasia haki,
Taifa sio taifa,pasi kuwa maadili.

​ uwe na uadilifu, twache tamaa na hongo,


T
Tusiwe na udhaifu, wa kuwa watu waongo,
Tukomeshe uhalifu, kisha tuache maringo,
Taifa sio taifa, pasi kuwa na maadili,

​ binafsi si adili, ila ni kusaidia,


U
Ukiwa nayo mali, asiye nacho patia,
Kama mtu mswahili, ubinafsi mtu achia,
Taifa sio taifa , pasi kuwa na maadili.

​ a inavyoelezea,katiba ni kielezi,
N
Tutii kwa mazoea, hadi kijacho kizazi,
Kwa hayo nitamwachia, hiyo ya ziada kazi,
Taifa sio taifa, pasi kuwa maadili.

maswali
​ ) Eleza mambo yoyote manne ambayo mshairi anashauri taifa lifanye ili kuwa
a
na maadili. (alama 4)
a) Eleza mambo yoyote manne ambayo mshairi anashauri taifa lifanye ili kuwa na maadili. (alama
4)

16/25
1. Kuwa wazalendo/kuipenda nchi yao
2. Kuwa na umoja/ kuacha ukabila
3. Kuwa na mgao sawa wa raslimali
4. Kuacha tama
5. Kukomesha uhalifu
6. Kuacha maringo
7. Kutii katiba
8. Kuacha ubinafsi na kusaidiana. Zozote 4x1

​b) Eleza mtindo wowote ule uliotumika katika shairi hili. (alama 2)
a) Eleza mtindo wowote ule uliotumika katika shairi hili. (alama 2)
Msemo – nipe masikioni- nipe sikio
Jazanda / istiari- kawa upinde
Takriri – kawa mpinde
Tashbihi – kama mtu mswahili
Utohozi – demokrasia, bajeti. Zozote 2x1

​ ) Ainisha shairi hili kwa kuzingatia vigezo vifuatavyo:


c (alama2)
i. Mpangilio wa vina
ii. Vipande katika mshororo.
a) Ainisha shairi hili kwa kuzingatia vigezo vifuatavyo: (alama2)
(i) Mpangilio wa vina
Ukaraguni- vina vya kati na vya mwisho vinabadilika toka ubeti hadi mwingine
(ii) Vipande katika mshororo.
Mathnawi- limegawika katika vipande viwili

​d) Bainisha nafsi neni katika shairi hili. (alama 2)


​Mwananchi/raia/mzalendo/mkereketwa

​e) Eleza toni ya shairi hili. (Alama 2)


​Kunasihi/kushawishi/kuhimiza

f​ ) Eleza umuhimu wa aina mbili za uhuru wa kishairi zilizotumiwa katika ubeti


wa nne. (alama 4)
Kubananga/kuboronga sarufi -uongozi tushiriki
Umuhimu- kuleta urari wa vina
Utohozi- demokrasia
Umuhimu- kuleta urari wa vina
Inkisari - pasi badala ya pasipo
Umuhimu- kuletya urari wa mizani

Aina =1 2x2 =4
Umuhimu =1
​g) Andika ubeti wa pili kwa lugha tutumbi. (alama 4)
​ aanza kwa kueleza uzalendo kwamba tuipende nchi yetu. Matendo yetu yaonyeshe kuwa tunaipenda
N
nchi yetu.Tabia ya kila mtu ionyeshe msimamo . Nchi haikamiliki bila ya kuwa na matendo mema. 4x1=4

Read More

0 Comments
SIPENDI KUCHEKA - USHAIRI MASWALI NA MAJIBU MODEL16122022001
16/12/2022

0 Comments

​SIPENDI KUCHEKA

17/25
​ ana jambo nanatukiya, kwangu hilo ni muhali
P
Kitenda naona haya, kujishusha yangu hali
Sipendi unipe hidaya, sipendi kutenda hili
Sipendi mimi kucheka

​ ipendi mimi kucheka , kuchekea mawa


S
Sipendi ya dhihaka, kwangu nyemi hiwi
Sipendi kwa hakika, mwovu kistawika
Halafuye nikacheka!
Maskini akiteswa
Yatima akinyanyaswa
Mnyonge naye akinyonywa
Sipendi hata ikiwa
Unazo nguvu najuwa
Ni hili sitatekezwa

​ bona lakini nicheke, kwayo furaha?


M
Na wewe ukajiweke, uli na siha
Na yatima pweke, wa anahaha?
Amenyimwa haki yake, hanayo raha!
Na moyo wangu ucheke, kwa ha! ha! ha!
Kucheka kwa kuchewa mimi katu sitacheka.

maswali na majibu
a) Hili ni shairi la aina gani? Thibitisha jibu lako kwa kutaja mifano miwili.
(alama 3)
Shairi huru
Hakuna urari wa vina
Vipande vinatofautiana
Idadi ya mishororo inatofautiana
Mizani haijitoshelezi.

b) Kwa nini mshairi hataki kucheka. (alama 3)


Atakuwa anajishusha hadhi
Hapendi kuchekea mabaya
Hapendi dhihaka
Hapendi kucheka mnyonge aliyenyimwa haki
Anaona haya kucheka

c) Eleza umbo la ubeti wa tatu wa shairi hili. (alama 4)


Una mishororo sita
Mishororo mitano ya kwanza imegawika katika vipande viwili huku miwili ya mwisho ikigawika katika
kipande kimoja
Haina urari wa vina
Vina vinatofautiana toka ubeti mmoja hadi mwingine.

d) Tambua nafsineni katika shairi hili. (alama 2)


​Mtetezi wa wanyonge

e) Tambua toni ya shairi hili. (alama 1)


​Toni ya huzuni/malalamiko/masikitiko

f) Dhihirisha matumizi ya uhuru ufuatao katika shairi hili. (alama 2)


i. Tabdila
ii. Kuboronga sarufi
i. Tabdila - najuwa badala ya najua
ii. Kuboronga sarufi - sipendi mimi kucheka- mimi sipendi kucheka

g) Andika ubeti wa pili kwa lugha ya nathari. ( alama 3)

18/25
​ shairi anasema hapendi maskini akiteswa na mayatimakunyanyaswa naye mnyonge akinyonywa. Hata
M
ikiwa anayewanyanyasa ana nguvu, anajua kuwa hili halitamtikisa

h) Eleza maana ya misamiati ifuatayo kama ilivyotumika katika shairi hili.


(alama 2)
i. Hidaya
ii. Nyemi
i. Hidaya- zawadi
ii. Nyemi – furaha

Read More

0 Comments
USHAIRI MASWALI NA MAJIBU MODEL14122022003
14/12/2022

0 Comments

​USHAIRI MASWALI NA MAJIBU MODEL14122022003


​ ti
E
Mimi niondoke hapa
Niondoke hapa kwangu
Nimesaki, licha ya risasi
Vitisho na mauaji, siondoki

​ imi
M
Siondoki
Siondoki siondoki
Niondoke hapa kwangu!
Kwa mateke hata na mikuki
Marungu na bunduki, siondoki

​ apa
H
Siondoki
Mimi ni Pahame!
Niondoke hapa kwangu!
Fujo na ghasia zikizuka
Na kani ya waporaji, siondoki

​ aki
H
Siondoki
Kwangu siondoki
Niondoke hapa kwangu!
Nawaje; waje wanaokuja
Mabepari wadhalimu, siondoki

​ amwe
K
Siondoki
Ng’oo hapa kwangu!
Katizame chini mti ule!
Walizikwa babu zangu, siondoki

​ endi
S
Nende wapi?
Si hapa kitovu changu
Niondoke hapa kwangu
Wangawa na vijikaratasi
Si kwamba hapa si kwangu, siondoki

​ atu
K
Siondoki
Sihitaji karatasi

19/25
Niondoke hapa kwangu
Yangu mimi ni ardhi hii
Wala si makaratasi, siondoki

​Maswali
a) Shairi hili ni la aina gani? Kwa nini (alama 2)
b) Taja masaibu anayopitia mzungumzaji (alama 4)
c) Eleza toni ya shairi hili (alama 2)
d) Eleza muundo wa shairi hili (alama 3)
e) Tambua matumizi ya mbinu ya usambamba (alama 2)
f) Andika ubeti wa tano kwa lugha nathari (alama 4)
g) Tambua idhini moja ya mtunzi (alama 1)
h) Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumika katika shairi (alama 3)
(i) Karatasi
(ii) Nimesaki
(iii)kitovu

majibu / mwongozo
​ . - Ni shairi huru kwa sababu mshairi ametumia (i) mishata mf. katu, eti, niondoke
a
- Shairi lina umbo la paa la nyumba
- Matumizi ya alama za uakifishaji kwa wingi (al. 2)

​ . (i) Anatishwa kwa risasi


b
(ii) Kupigwa mateke na mikuki
(iii) Kuponda mali yake
(iv) Kuletewa hatimiliki bandia (mwalimu akubali hoja nyingine yoyote) Al. 4

c​ . (i) Huzuni
(ii) Ujasiri (2 x 1)
(iii) Uchungu

​ . Shairi lina beti saba


d
Kila ubeti una mishororo sita
Lina umbo la paa la nyumba (3 x 1)

e. Usambamba – Ni urudiaji wa kiwango cha sentensi, kirai (n.k)


mf.
​(i) Niondoke, mimi niondoke hapa, niondoke hapa kwangu
(ii) Siondoki, siondoki, siondoki niondoke hapa kwangu (2 x 1)

f​. Mshairi anasema kamwe hatoki kwake. Anaashiria chini ya mti waliozikwa babu zake na kusisitiza
kwamba hawezi akaondoka (al. 3)

g. Inkisari –
​(i) Sendi – Siendi Nende wapi – Niende wapi
(ii) Kuboroga sarufi mf yangu mimi ni ardhi hii – Ardhi hii ni yangu mimi (1 x 1)

h. Karatasi – Hati miliki


Nimesaki – Nimebaki
Kitovu – Asili
(al. 3 x 1)

Read More

0 Comments
USHAIRI MASWALI NA MAJIBU MODEL13122022002
13/12/2022

0 Comments

Soma shairi na kujibu maswali

20/25
Huketi mahali tuli, nikaaza peke yangu
Na niazalo ni hili, lililo moyoni mwangu
Naifikiri ajali, siku ya kunyoka kwangu
Naliliya roho yangu, itakufa iyondoke

Itakufa initoke, katika jasadi yangu


Ndugu zangu niwepuke, kwa kadhwa ya Bwana M’ngu
Kitandani waniweke, wanioshe ufu wangu
Naliliya roho yangu, itakufa iyondoke

Tanyoshwa sina kauli, waliye wendani wangu


Wanitakase muwili, sina langu wala changu
Sanda ikisha waswili, wanikafini wenzangu
Naliliya roho yangu, itakufa iyondoke

Nikisha sanda kutiwa, iletwe jeneza yangu


Nitiwe kwa kupokewa, na mikono ya wenzangu
Wende nami sawa sawa, hadi baiti ya M’ngu
Naliliya roho yangu, itakufa iyondoke

(A. Nassir, ‘Maskini roho Yangu,’ Malenga wa Mvita, 1971:170)

Maswali
(a) Kwa kuzingatia vina taja bahari ya shairi hili. (alama 1)
Ukara (1x1=1)
(b) Orodhesha mifano ya uhuru wa kishairi iliyotumika na sababu zake. (alama 3)
● Lahaja
Nikaaza – nikawaza (kudhirisha ubingwa / asili / usuli/utamu/ladha
● Tabdila/tafsida
Naliliya – nalilia
(kudumisha mdundo/mapigo ya kisauti / ainisha mapigo)
● Inksari
Niwepuke – niwaepuke
(kudumisha urari wa mizani)
● Kufinyanga lugha kisarufi
Nikisha sanda kutiwa – Nikisha kutiwa sanda.
(kudumisha urari wa vina)
*Mwalimu atathmini jibu la mwanafunzi [3 x 1 = 3]
(c) Shairi hili linajitosheleza. Thibitisha kwa kutolea mifano mitatu. (alama 3)
[shairi hujitosheleza kimaana na kimuundo]
(i) Kimaana – ujumbe kwamba nafsineni analilia roo yake siku atakapokufa umejitokeza wazi katika shairi
lote. Kila ubeti wajenga maana hiyo.Ninaililia roho yangu itakapotengana nami baada ya kufa/kifo
change. (4 x 1 = 4)
(ii) Kimuundo; kila kipengee ni hoja.
Kuna urari wa:
● Vina katika ubeti (kivyake)
● Mizani 8:8
● Mishororo minne minne katika kila ubeti
● Vipande: ukwapi na utao (2 x 1= 2)
(d) Andika ya ubeti wa kwanza kwa lugha nathari. (alama 2)
Huwa ninakaa pahali peke yangu na kuwaza.
Kile ninachofikiria kimo moyoni mwangu. Jambo ambalo huwa ninafikiria juu
yake ni kuhusu siku ya kufariki kwangu(bila kutarajiwa / kupangia). [2 x 1 = 2)
(e) Changanua vipengele vya kimtindo vyovyote vitatu katika utungo huu. (alama 3)
(i) Jazanda:
Siku ya kunyoka – siku ya kifo
(ii) Uzungumzi nafsia.
Matumizi ya nafsi ya kwanza: Huketi mahali tuli, nikaaza peke yangu.
(iii) Tashihisi /uhaishaji/uhuishi
Sanda ikisha waswili itakufa iyondoke.
(iv) Mjalizo [ni matumizi kuleta msisitizo sina langu wala changu, [kama nipe nikupe, nishike nikushike]
Sina langu sina changu
(v) Takriri
Sawa sawa
Kibwagizo

21/25
Silabi
(vi) Utohozi
Wanikafini – put in coffin
(3 x 1 = 3)
(f) Dhihirisha matumizi ya taswira. (alama 3)
(i) Taswira Mwendo
wende nami sawa sawa, hadi baiti ya M’ngu / sanda ikisha waswili.
(ii) Taswira oni.
Huketi mahali tuli, nikaaza peke yangu.
(iii) Mguso
Wanitakase muwili
Nitiwe kwa kupokewa, na mikono…..
(iv) Taswira hisi
Naililia roho yangu
Wanitakase muwili
(3 x 1 = 3)
(g) Tolea mifano mitatu ya takriri zilizotumika. (alama 3)
(i) Maana
Nitiwe kwa kupokewa, na mikono ya wenzangu
(ii) fungu la maneno / mshororo
Nalilia roho yangu, itakufa iyondoke
(iii) Takriri silabi
na - naliliya
- naililiya
- naifikiri nk
Takriri ya vina vya mwisho na kati
(iv) Takriri ya neno:
M’ngu
Sanda
Sawa sawa
(3 x 1 = 3)

Read More

0 Comments
USHAIRI MASWALI NA MAJIBU MODEL13122022001
13/12/2022

0 Comments

​Soma shairi lifuatalo kasha ujibu maswali.


​Daima alfajiri na mapema
Hunipitia na jembe na kotama
Katika njia iendayo kondeni
Kama walivyofanya babuze zamani;
Nimuonapo huwa anatabasamu
Kama mtu aliye na kubwa hamu
Kushika mpini na kutokwa jasho
Ili kujikimu kupata malisho.

​ napotembea anasikiliza
A
Videge vya anga vinavyotumbuiza
Utadhani huwa vimemngojea
Kwa usiku kucha kuja kumwimbia;
Pia pepo baridi kumpepea
Rihi ya maua zikimletea
Nao umande kumbusu miguu;
Na miti yote hujipinda migongo
Kumpapasa, kumtoa matongo;
Na yeye kuendelea kwa furaha
Kuliko yeyote ninayemjua
Akichekelea ha hahaha ha….

22/25
Na mimi kubaki kujiuliza
Kuna siri gani inayomliwaza?
Au nikujua au kutojua?
Furaha ya mtu nifuraha gani
Katika dunia inayomhini?
Ukali wa jua wamnyima zao
Soko la dunia la mkaba koo;
Dini za kudhani zamsonga roho
Ayalimia matumbo ya waroho;
Kuna jambo gani linamridhisha?
Kama sikujua ni kutokujua
Laiti angalijua, laitia ngalijua!.
(T. Arege)

​MASWALI.
a) Eleza hali ya mzungumziwa katika shairi hili. (alama.4)
b) Huku ukitoa mifano, onyesha aina mbili za uhuru wa kishairi uliotumiwa katika shairi hili. (alama.2)
c) Fafanua aina mbili za taswira ukirejelea ubeti wa pili. (alama.2)
d) Maswali ya balagha katika shairi hili yanasisitiza maudhui yapi? (alama.2)
e) Bainisha vipengele viwili vya kimtindo katika shairi hili. (alama.2)
f) Bainisha aina mbili za urudiaji zilizotumiwa katika shairi hili. (alama.2)
g) Eleza toni ya shairi hili. (alama.2)
h) Bainisha nafsineni katika shairi hili. (alama.1)
i) Eleza muundo wa shairi hili. (alama.3)

​MWONGOZO WA USHAIRI.
​ )i) Mwenyetumaini /tamaa – kubwahamu
a
ii) Mwenyebidii- alfajirina,mapema, kutokwanajasho.
iii) Anayefurahiamandhari – anapotembeaanasikilizavidege….
iv) Mtulivu- kunasiriganiinayomliwaza?
v) Aliyedhulumiwa – soko la dunialamkabakoo.
vii) Aliyeridhika- kunajambogani? (2x2=2)

b) Inkisari – babuze – babuzake.


ii) Kufinyangasarufi/miundongeuyakisintaksia- kubwahamu – hamukubwa. 2x1=2)

c)i) Taswiramnuso/harufu – rihiyamaua


ii) Taswiramguso – kumpapasa, kumbusumiguu.
iii) Taswirauskivu – anasikilizavidege.
iv) Taswirayamwendo – yeyekuendeleakwafuraha. (2x1=2)

d)i) Maudhuiyaunyanyasaji – katikaduniainayomhini?


ii) Ukosefuwahakikwabinadamumaskini – soko la dunialamkabakoo. (2x1=2)

e)i) Tashhisi- Umandekumbusu, mitikumpapasa, upepokumpepea.


ii) Kinaya- nafsineniinafurahiilhaliduniainamhini
iii) Tashbihi – kamamtualiyenakubwahamu (2x1=2)

f)i) Urudiajiwamaneno- kama – ubeti 1


-furaha – ubeti 3
ii) Urudiajiwasauti – a, a – ubeti 2, 3
-o,o – ubeti 3
iii) Urudidajiwasilabi – ma, ma, za, za, ha, ha (2x1=2)
g)i) Toni yauchungu- furahayamtunifurahaganikatikaduniainayomhini?
ii) Toni yakuajabia/kushangazwanajambo- kunajamboganilinamridhisha?
iii) Kuhuzunisha/masikitiko/kuhurumia- laitiangalijua.
1x2=2
kutaja-1
kueleza -1
h) Mteteziwahaki/aliyezinduka/anayelalamikiadhulumayawanyonge.
ii) Mtuanayemtazamamkulimakipita. (1x1=1)
I)i) Linabetitatu
ii) Kilaubetiunaidaditofautiyamishororonabetinyingine.

23/25
iii)
Kilamshororounakipandekimojaisipokuwaubetiwapilimshororowatisanamshororowamwishoubetiwamwisho.
iv) Shairihalinampangiliomaalumwavina
v) Idadiyamizanikatikamishororoinatofautiana. (3x1)

Read More

0 Comments
USHAIRI MASWALI NA MAJIBU MODELI 2362021544
23/6/2021

0 Comments

USHAIRI
Eti
Mimi niondoke hapa
Niondoke hapa kwangu
Nimesaki, licha ya risasi
Vitisho na mauaji, siondoki

Mimi
Siondoki
Siondoki siondoki
Niondoke hapa kwangu!
Kwa mateke hata na mikuki
Marungu na bunduki, siondoki

Hapa
Siondoki
Mimi ni Pahame!
Niondoke hapa kwangu!
Fujo na ghasia zikizuka
Na kani ya waporaji, siondoki

Haki
Siondoki
Kwangu siondoki
Niondoke hapa kwangu!
Nawaje; waje wanaokuja
Mabepari wadhalimu, siondoki

Kamwe
Siondoki
Ng’oo hapa kwangu!
Katizame chini mti ule!
Walizikwa babu zangu, siondoki

Sendi
Nende wapi?
Si hapa kitovu changu
Niondoke hapa kwangu
Wangawa na vijikaratasi
Si kwamba hapa si kwangu, siondoki

Katu
Siondoki
Sihitaji karatasi
Niondoke hapa kwangu
Yangu mimi ni ardhi hii
Wala si makaratasi, siondoki
​Maswali
a) Shairi hili ni la aina gani? Kwa nini (alama 2)
b) Taja masaibu anayopitia mzungumzaji (alama 4)

24/25
c) Eleza toni ya shairi hili (alama 2)
d) Eleza muundo wa shairi hili (alama 3)
e) Tambua matumizi ya mbinu ya usambamba (alama 2)
f) Andika ubeti wa tano kwa lugha nathari (alama 4)
g) Tambua idhini moja ya mtunzi (alama 1)
h) Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumika katika shairi (alama 3)
(i) Karatasi
(ii) Nimesaki
​(iii)kitovu

MWONGOZO WA KUSAHIHISHA - USHAIRI


1.
a.
Ni shairi huru kwa sababu mshairi ametumia (i) mishata mf. katu, eti, niondoke
Shairi lina umbo la paa la nyumba
Matumizi ya alama za uakifishaji kwa wingi (al. 2)
b.
(i) Anatishwa kwa risasi
(ii) Kupigwa mateke na mikuki
(iii) Kuponda mali yake
(iv) Kuletewa hatimiliki bandia (mwalimu akubali hoja nyingine yoyote) Al. 4
c.
(i) Huzuni
(ii) Ujasiri (2 x 1)
(iii) Uchungu
d.
Shairi lina beti saba
Kila ubeti una mishororo sita
Lina umbo la paa la nyumba (3 x 1)
e.
Usambamba – Ni urudiaji wa kiwango cha sentensi, kirai (n.k)
mf.
(i) Niondoke, mimi niondoke hapa, niondoke hapa kwangu
(ii) Siondoki, siondoki, siondoki niondoke hapa kwangu (2 x 1)
f.
Mshairi anasema kamwe hatoki kwake. Anaashiria chini ya mti waliozikwa babu zake na kusisitiza
kwamba hawezi akaondoka (al. 3)
g.
Inkisari –
(i) Sendi – Siendi Nende wapi – Niende wapi
(ii) Kuboroga sarufi mf yangu mimi ni ardhi hii – Ardhi hii ni yangu mimi (1 x 1)
h.
Karatasi – Hati miliki
Nimesaki – Nimebaki
Kitovu – Asili

(al. 3 x 1)
TUMA KWA PRINTA

Read More

0 Comments

25/25

You might also like