You are on page 1of 10

102/3

KISWAHILI
KARATASI YA 3
FASIHI
MACHI/APRILI 2023
MUDA: SAA 2 ½

TATHMINI YA PAMOJA YA MOKASA I – 2023


Kenya Certificate of Secondary Education – (KCSE)

Maagizo

a) Jibu maswali manne pekee.

b) Swali la kwanza ni la lazima.

c) Chagua mengine matatu kutoka sehemu nne zilizobaki yaani: Riwaya, Tamthilia,

Hadithi Fupi na Ushairi.

d) Usijibu maswali mawili kutoka katika sehemu moja.

e) Majibu yaandikwe katika kijitabu cha majibu utakachopewa.

f) Hakikisha kuwa kurasa zote zimepigwa chapa sawasawa na kwamba maswali yote yamo.

g) Karatasi hii ina kurasa 8 zilizopigwa chapa.

@MTHIHANI WA PAMOJA WA MOKASA Ukurasa wa 1


SEHEMU YA A: FASIHI SIMULIZI
1. Lazima
Soma utungo ufuatao kisha ujibu maswali.

Zimepita siku ayami

Siku chungu tangu giza lipotanda

Wakati lipotazama kwa kiwewe na shauku

Pumzisho kipania, roho kupigania

Ziraili alipokakamaa aushiyo kufakamia.

Nilikwita kwa sauti

Ela mpenzi hukunitika

Machoyo litunga mbele

Kumkabili huyu nduli

Nikabaki kunyongonya

Jaala kitumainia,

Mtima kijiinamia

Hatima kungojea.

@MTHIHANI WA PAMOJA WA MOKASA Ukurasa wa 2


Ya mwisho lipopumua,

Alfajiri ya kiza kuu

Nalidhani wanichezea,

Mizaha yako kawaida

Lijaribu kupulizia

Hewa toka langu pafu,

Tumaini kiniambia pumzi zangu takuhuisha

Sikujua hizo likuwa juhudi za mfa maji muhebi.

Macho libaki kutunduiya, tabasamuyo kitaraji

Kumbe mwenzangu kaniacha!

Ukiwa ulinivaa, ukungu ukatwandama

Pa kuegemea sikujua fundo chungu linisakama

Tabibu alipoingia na kutangaza rasmi mauko.

Ilikuwa kana kwamba ndo jana lipofunga nikahi,

Kumbukizi zilinijia kwa chozi teletele

Japo kifo ni faradhi ndwele hino halieleweki

Ama jicho la hasidi,

Limekuangaza jamani?

@MTHIHANI WA PAMOJA WA MOKASA Ukurasa wa 3


Koja hili ninalokuwekea,

Kando ya kasri hili la shakawa

Ni hakikisho toka kwangu, nitatamba sana njia

Kutafuta alotwendea kinyume kutupoka,

Mauko kutuleteya.

a) (i) Ainisha utungo huu kwa kuzingatia kipengele cha maudhui. (alama 1)

(ii) Andika sababu tatu kuthibitisha jibu lako la a(i). (alama 3)

b) Bainisha sifa mbili za jamii inayosawiriwa wa utungo huu. (alama 2)

c) Fafanua vipengele vinne vya kimtindo ambavyo vimetumiwa kufanikisha uwasilishaji wa

utungo huu. (alama 4)

d) Tungo za aina hii zinaendelea kufifia katika jamii yako. Fafanua hoja tano utakazotumia

kuishawishi jamii yako kukinga dhidi ya hali hii. (alama 5)

e) Unanuia kutumia mbinu ya kushiriki kufanya utafiti kuhusu tungo za aina hii. Eleza sababu

tano za kuchagua mbinu hii. (alama 5)

SEHEMU YA B: RIWAYA

Assumpta Matei:Chozi la Heri

Jibu swali la 2 au la 3

2. … alijua kwamba msimamo wake huu ungempalia makaa. Lakini alihiari kupoteza riziki yake
ili kuyaokoa maisha ya wanyonge wasio na hatia.
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
(b) Fafanua sifa za anayerejelewa katika dondoo. (alama 4)
(c) Huku ukirejelea wahusika riwayani, thibitisha kuwa hiari ya wahusika inawafanya kujipalia
makaa. (alama
12)

@MTHIHANI WA PAMOJA WA MOKASA Ukurasa wa 4


3. … kisha ninaanza kumsimulia yaliyojiri kana kwamba ni mgeni wa hali hii. Ninajua kwamba
simsimulii … bali pia Mamia ya Wahafidhina ambao huenda hawajaishuhudia hali hii.
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
(b) Eleza umuhimu wa usimulizi wa msemaji katika kujenga riwaya ya Chozi la Heri. (alama16)

SEHEMU YA C: TAMTHILIA

Jibu swali la 4 au la 5

4. “ Maradhi! Madhila yake hayasemeki. Yakimla mtu humthakilisha. Humwacha hoi hana
mbele wala nyuma.Yakitaka huzichezea dawa mwajificho. Dawa zikiingilia huku, maradhi
hutokezea pale hali pesa zinakwenda, shughuli zinasimama ... Dunia ina mitihani tosha lakini
panapo maradhi sugu, uzito wake haumithiliki.”
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
(b) Bainisha mbinu nne za kimtindo zilizotumiwa kwenye dondoo. (alama 4)
(c) Huku ukirejelea hadithi, eleza sifa sita za msemaji wa kauli hii. (alama 12)

5. Sara: Nilipopata harufu ya mahamri nilijua bila shaka kwamba baba yako ameingia jikoni.
Neema: Mama sijaona baba akipika hivi karibuni.
Kwa kurejelea nukuu zilizotolewa hapa juu, fafanua usasa na utamaduni vilivyosawiriwa
tamthiliani. Kila upande utawe na hoja kumi kumi. (alama 20)
SEHEMU YA E: HADITI FUPI

Rachel Wangari: Fadhila za Punda

6. “Nisikuone tena ofisini mwangu, mwanamke wewe. Kuja kuniaibisha, wapinzani wangu

waseme nimeshindwa kumdhibiti mke wangu, sembuse kaunti nzima!”

a) Bainisha muktadha wa dondoo hili. (alama 4)

b) Eleza toni katika muktadha huu. (alama 2)

@MTHIHANI WA PAMOJA WA MOKASA Ukurasa wa 5


c) Asasi ya ndoa imo hatarini. Jadili ukweli wa kauli hii kwa kurejelea mandhari ya dondoo hili.

(alama 4)

d) Jadili namna mbinu zifuatazo zilivyotumiwa na mwandishi wa hadithi Msiba wa Kujitakia. (alama 10)

(i) Kinaya

(ii) Mbinu rejeshi

Clara Momanyi: Mapambazuko ya Machweo

7. “…umeniita tukae hapa kando ya barabara kwa nini lakini?

a) Weka dondoo hili katika muktadha wake. (alama 4)

b) Eleza sifa zozote nne za Mzee Makucha. (alama 4)

c) Fafanua changamoto zinazowakumba msemaji na msemewa pamoja na wenzao katika

hadithi hii ya Mapambazuko ya Machweo”. (alama 6)

d) Jadili visababishi vyovyote sita vya matatizo yanayowakumba wahusika katika hadithi ya

Harubu ya Maisha. (alama 6)

SEHEMU YA D: USHAIRI

8. Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali

Soma waliosoma, masomo wa zama soma,

Soma hata wangasoma, wasome na kusosoma,

Soma mwisho watasoma, kusoma kuyosoma,

Soma somato msoma, wasoma wambe kusoma.

@MTHIHANI WA PAMOJA WA MOKASA Ukurasa wa 6


Soma ya leo msoma, soma siwache wasoma,

Soma akiliyo choma, kisomo cha waliosoma,

Soma hata wangasoma, mizomo haitachoma

Soma somato msoma, wasoma wambe kasoma.

Soma ja samaki shoma, kusoma kuno kushoma,


Soma wa jana mshoma, bado kitu hajashoma,
Soma kuno ndo kusoma, kushoma bila kuchoma,
Soma somato msoma, wasoma wambe kasoma.

Soma waseme wasoma, ya kwamba hawajasoma,

Soma wakusome soma, mbwa wapi yuno msoma?

Soma wakisoma soma, washindwe yako kusoma,

Soma somato msoma, wasoma wambe kasoma.

Soma ya kusomea soma, yasosomwa pia soma,

Soma masomo kuchoma, masomo yaseme 'soma'!

Soma siwe ja mzoma, kuzoma siyo kusoma,

Soma somato msoma, wasoma wambe kasoma.

Soma walimwengu soma, visomo vyao kusoma,

Soma kusomoa soma, kushomashoma kusoma,

Soma kusoma msoma, kisichosomwa kusoma,

Soma somato msoma, wasoma wambe kasoma.

@MTHIHANI WA PAMOJA WA MOKASA Ukurasa wa 7


Soma hata ungasoma, jua bado hujasoma,
Soma kuna walosoma, kwao utakuwa joma,
Soma msomaji soma, hakuna tama kusoma,
Soma somato msoma, wasoma wambe kasoma.
(Hamisi Babusa)

Maswali

a) Eleza mbinu alizotumia mshairi ili kukidhi mahitaji ya kiarudhi. (alama 2)


b) Fafanua bahari katika shairi hili kwa kuzingatia vigezo vifuatavyo: (alama 3)
i) Idadi ya vipande

ii) Mpangilio wa maneno

iii) Mpangilio wa vina

c) Chambua ubeti ya nne kiarudhi. (alama 3)


d) Bainisha vipengele vya kimtindo katika shairi hili. (alama 2)
e) Fafanua aina zozote tatu za urudiaji katika shairi hili. (alama 3)
f) Andika ubeti wa mwisho kwa lugha nathari. (alama 4)
g) Eleza toni katika shairi hili. (alama 1)
h) Fafanua maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumika katika shairi hili. (alama 2)
i) Zoma

ii) Tama

-MWISHO-

@MTHIHANI WA PAMOJA WA MOKASA Ukurasa wa 8


@MTHIHANI WA PAMOJA WA MOKASA Ukurasa wa 9
MARKING SCHEME
Each subject is sh100 whether you want for one paper or paper 1,2,3

Text Elibrary 0700584968

@MTHIHANI WA PAMOJA WA MOKASA Ukurasa wa 10

You might also like