Professional Documents
Culture Documents
Kiswa f3t3 07092021 001
Kiswa f3t3 07092021 001
102/3
KISWAHILI
KARATASI YA 3
FASIHI
MUDA: SAA 2 ½
SEHEMU A : TAMTHILIA
Timothy Arege: Mstahiki Meya
Swali la lazima
1. “Fahamu hili. Anayeliogopa tope kumwangukia hawezi kujua njia nzuri ya kulisafisha ……..”
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili. ( alama 4 )
(b) Fafanua sifa za anayerejelewa. ( alama 6 )
(c ) Onyesha jinsi uozo unavyodhihirika katika baraza. ( alama 10)
SEHEMU B : RIWAYA
Ken Walibora : Kidagaa Kimemwozea
Jibu swali la 2 au la 3
2. “…. Lakini wewe kijana si tayari wafanyakazi…..”
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
(b) Fafanua sifa zozote mbili za msemewa. ( alama 4 )
(c ) Kwa kutolea mifano mwafaka, eleza jinsi mbinu ya kinaya ilivyotumiwa
kuelezea hali ya maisha ya msemaji. ( alama 12 )
SEHEMU YA C USHAIRI
Jibu swali la 4 au 5
4. VITA VYA NDIMI
Huyo !Amshike huyo !
Hakuna bunduki wala kifami
Bomu na risasi hata hawazijui
Lakini mno wanashambuliana
Kwa ndimi zilizonolewa kwa makali
Vipande vya matusi silaha zao
Magharibi sasa
Jua linapungia mkono machweo
Nalo giza likinyemelea kwa kiburi na
Kasi
Sisikii tena sauti za mIsonyo
Mate ya watesi yamekauka
Makanwa yao yamelemewa na uchovu
Sasa wameshikana mikono
Ishara ya suluhu
Maswali
(a)Hili ni shairi la aina gani? (al.1)
(b) Eleza dhamira ya mshairi (al.2)
(c) Eleza sifa za utunzi alizotumia mshairi (al.3)
(d) Taja tamathali zozote tatu alizotumia mshairi (al.3)
(e) Eleza toni ya mshairi katika beti tatu za awali (al.1)
(f) Eleza hatima ya yanayozungumziwa kwenye shairi (al.2)
(g) Mshairi ametumia alama hisi kwingi. Eleza umuhimu wake (a.2)
(h) Itambue nafsi neni katika shairi (al.1)
(i) Andika mishororo ya kwanza mitatu ubeti wa 4 kwa lugha ya nathari (a.3)
(j) Toa maana ya msamiati huu (al.2)
(i) Kombora
(ii) Misonyo
Maswali ya shairi.
(h) Eleza maana za maneno yafuatayo kama yalivyotumika katika shairi. ( alama 2 )
(i) Kitu
(ii) Mtovu