You are on page 1of 4

HOLY FAMILY NKUENE MIXED DAY SECONDARY SCHOOL

KIDATO CHA KWANZA

JINA…………………………………………………………………NAMBARI………

1. Taja aina mbili kuu za sauti. Alama 2

2. Taja ala zozote tano za kutamkia. Alama 5

3. Toa mifano miwili miwili ya: Alama 2

(i) Ala tuli-------

(ii) Ala sogezi----

4. Orodhesha sifa tatu zinazozingatiwa katika uonishaji

wa konsonanti . Alama 3

5. Taja : Alama 5

i. Kipasuo hafifu cha ufizi


ii. Kingongo cha midomoni
iii. Kiyeyusho cha kaakaa gumu
iv. Irabu ya nyuma juu
v. Irabu ya chini,tandazwa

6. Taja vipashio vinne vya lugha. Alama 4

7. Eleza maana ya silabi. Alama 2

8. Eleza maana ya sauti mwambatano. Alama 2

9. Tofautisha shadda na kiimbo. Alama 2

10. Onyesha silabi ya kuwekewa shadda katika


maneno haya. Alama 3

i. Nne
ii. Oa
iii. Sentensi

11. Huku ukitoa mifano, eleza miundo mitatu ya silabi

za Kiswahili. Alama 3

12. Andika maneno yenye miundo ya silabi ifuatayo. Alama 3

i. Irabu+ konsonanti+ konsonanti+ irabu

ii. Konsonanti+ konsonanti+ irabu+ konsonanti+ irabu

iii. Irabu+ konsonanti+ irabu

13. Andika maana ya maneno yaliyopigiwa mstari. Alama 3

Wahandisi hao walikarabati barabara hiyo barabara

14. Fafanua uamilifu wa kiimbo. Alama 3

15. Ainisha : Alama 3

Aliyempiga

16. Taja aina mbili za viambishi. Alama 2

17. Taja aina nane za maneno ya Kiswahili. Alama 8

18. Tunga sentensi moja ili kutofautisha vitate: Alama 2

(i) mahali/mahari

(ii) vua/fua
19. Eleza matumizi matatu ya kikomo. Alama 3

20. Andika sentensi iliyo katika:

(i) wakati uliopita

(ii) wakati uliopo

(iii) wakati ujao

21. Bainisha maneno katika sentensi ifuatayo. Alama 3

Yusuf na Daniel wamekwenda wapi jamani?

FASIHI SIMULIZI ( ALAMA 10)

1. Fasihi ni nini? Alama 1

2. Taja tanzu nne za fasihi andishi. Alama 2

3. Taja tanzu nne za fasihi simulizi. Alama 2

4. Eleza tofauti kati ya fasihi simulizi na fasihi andishi. Alama 5

ISIMU JAMII (ALAMA 10)

1. Eleza maana ya lugha Alama 1

2. Eleza dhima ya lugha katika jamii. Alama 4

3. Eleza kaida tano zinazodhibiti matumizi ya lugha katika jamii. Alama 4

You might also like