You are on page 1of 7

MWONGOZO WA KUSAHIHISHA KARATASI YA PILI 102/2

A. UFAHAMU

(a) Fafanua vikwazo vitano vya maendeleo ya nchi na jamii ( alama 5)

i) kutolewa kiasi fulani cha darahimu kama hongo

ii) miradi lengwa kunyimwa pesa zinazohitajika

iii) miradi ya kiwango cha chini

iv) miradi mingi kukosa pesa za kutosha na kuifanya kutokamilika ipasavyo

v) vifo kutokana na kuidhinishwa kwa kazi duni

vi) hasara – miradi iliyofanywa kuanza kufanyiwa ukarabati baada ya muda mfupi hivyo pesa zaidi
kutumika

vii) uharibifu wa mali – wakati majumba yanaporomoka

viii) ulemavu kutokana na ajali za maporomoko ya miradi duni

ix) Wafadhili wa miradi katika nchi hudinda kuipa pesa wakihofia matumizi yake mabaya hivyo miradi
mikubwa ambayo inaweza kuwa kitega –uchumi kwa watu wengi nchini inakosa kutekelezwa.

x)Wanatumia pesa za maendeleo katika safari zisizo na manufaa kwa taifa

xi) ubadhirifu wa pesa za umma na wasimamizi wa hazina ya maendeleo

xii) wasimamizi wa miradi kuidhinisha kazi duni (zozote 5x1)

(b) Taja na ueleze mbinu nne za kimtindo ambazo zimetumika katika kifungu (alama 4)

i) Sitiari – ufisadi ni jinamizi

ii) Methali – tamaa mbele mauti nyuma

iii)Msemo – kupakwa mafuta viganjani

- kijungu jiko

iv) Nahau – kupita mipakani/ ulaji rushwa

v) Takriri/ urudiadi – chauchau (zozote 4x1)

(c) Eleza jinsi washikadau mbalimbali wanavyoonyesha uwajibikaji kwa mujibu wa kifungu hiki. ( alama4)

i) Viongozi serikalini kukosa kuwalipa wafanyakazi au kuwapuja kwa kuwapa mishahara ya kijungujiko

ii) wasimamizi huwa wabadhirifu wa pesa zilizotengewa miradi mbalimbali.

1 of 7
iii) watumishi wa umma kutumia fedha za maendeleo katika safari zosozo na manufaa kwa taifa.

iv) wasimamizi wa miradi kuidhinisha kazi duni.

v) wafadhili wa miradi kukosa kutoa pesa kwa kuhofia matumizi mabaya ya fedha hizo.

vi) serikali na wananchi wanakosa kuangazia na kutekeleza miradi dhaifu.

( mwanafunzi anaweza kuonyesha kutowajibika au kuwajibika.

(g) Eleza maana ya vifungu vifuatavyo kulingana na muktadha wa matumizi yake kifunguni. ((alama 2)

(i) ghawazi – pesa/ngwenje

(ii) kupakwa mafuta viganjani - kuhongwa

Usahihishaji

Makosa ya hijai 6 x ½

Makosa ya sarufi yasipite ½ ya alama alizopata katika kila kijisehemu

B. UFUPISHO

a) Fupisha aya tatu za mwanzo kwa maneno 80. (alama 5)


 Kiswahili ni lugha ya Kiafrika inayoongewa katika nchi nyingi Barani Afrika.
 Lugha asilia mojawapo za Afrika
 Kiswahili kimeenea kote Afrika Mashariki na Kati.
 Wenyeji asilia waliokuwa wakiongea Kiswahili tangu awali ni Waswahili.
 Waswahili wanaendelea kutumia Kiswahili kama lugha yao ya mama.
 Makao ya Wasahili ni kaunti ya Pwani.
 Kiswahili kina lahaja nyingi kulingana na wanamoishi.
 Kutokana na lahaja hizi na nyinginezo za Kiswahili wataalamu wa lugha walibuni Kiswahili sanifu
 Kiswahili sanifu hutumiwa katika mafunzo shuleni, uandishi wa vitabu na mawasiliano ya kiserikali na
kibiashara. (Hoja 5)
b) Fupisha aya ya nne kwa (maneno 40) (alama 4)
 Kiswahili hakikuthaminiwa kama lugha ya Kiingereza.
 Kiswahili hakikufanywa somo la lazima katika rasimu za shule
 Hakikutahiniwa katika shule za msingi wala za upili.
 Hakikupewa umuhimu wowote. (hoja 4)

c) Onyesha jinsi mitazamo kuhusu lugha ya kiswahili ulivyobadilika ( maneno 50) ( alama 4)
 Kiswahili kilianza kutiliwa mkazo katika shughuli zote nchini Kenya.
 Ilionwa kama lugha yenye manufaa katika kuleta umoja na kuwaunganisha wananchi wote.
 Kiswahili kimepewa nafasi sawa katika ratiba za shule kama Kiingereza .
 Kinatahiniwa kama somo muhimu kuanzia shule ya msingi hadi shule ya upili.
 Mwanafunzi anayesoma Kiswahili, asipofaulu vizuri katika lugha ya Kiingereza ana nafasi ya kupata
kazi kama wengine. ( hoja 4)

2 of 7
a-5

b-4
c-4

ut – 2

makosa ya hijai – 6x ½
makosa ya sarufi - 6x ½

C. SARUFI NA MATUMIZI YA LUGHA (Alama 40)

(a) i) andika maneno yenye miundo ifuatayo: (alama 2)

Irabu ya juu nyuma + nazali ya ufizi ghuna + kipasuo cha ufizi ghuna + irabu ya chini kati

unda

ii) Kiyeyusho cha mdomo+ irabu ya juu tandazwa + kipua cha mdomoni +irabu ya chini

wima ( 2x 1)

b) Onyesha muundo wa silabi katika neno lifuatalo: ( alama 1)

mchwa

KKI

(c) Tia shadda katika meneno yafuatayo kuonyesha dhana katika mabano: ( alama 2)

i) Ala ( kifaa) – ’ala/ ala

ii) Ala! ( kihisishi) - a’ la / ala ( 2x 1)

(d) Tunga sentensi katika wakati ujao hali ya mazoea. ( alama 2)

Wageni watakuwa wakiingia ukumbini kabla ya wenyeji.

( kadiria sentensi za mtahiniwa) ( 2/0)

(e) Andika sentensi ifuatayo katika udogo. (alama 2)

Nyundo za wazee wale zimevunjwa na mwana wake.

Vijundo vya vizee vile vimevunjwa na vijana vya. ( 2/0)

(f) Tunga sentensi ukitumia kiwakilishi cha pekee chenye dhana ya “badala ya” katika ngeli ya U-ZI.

(alama 2)

Mwingine unahitajika na sonara.

3 of 7
Nyingine zinahitajika na masonara. ( 2/0)

(g) Akifisha ili kuonyesha usemi halisi (alama 2)

tanya ondoka hapa mara moja

½
Tanya1/2: 1/2Ondoka hapa mara moja!1/2 ( ½ x 4)

(h) Tunga sentensi ukitumia nomino dhahania inayotokana na kitenzi ‘silimu’ ( alama 2)

Uislamu una imani thabiti mno.

(i) Eleza matumizi ya mofimu ‘ji’ katika sentensi zifuatazo: (alama 2)

(i) Sauti hiyo inajirudia.

Ji- kirejeshi

(ii) Aliliua jitu hilo kwa mshale dhaifu.

Jitu – ukubwa ( 2x 1)

(j) Bainisha sehemu za kiuamilifu za sentensi ifuatayo. ( alama 2)

Aliwanunulia watoto mkate jana asubuhi.

Aliwanunulia – kiarifu

Watoto – yambwa tendewa/ shamirisho kitondo

Mkate – yambwa tendwa/ shamirisho kipozi

Jana asubuhi – chagizo (4x ½ )

(k) Eleza maana mbili za sentensi ifuatayo. (alama 2)

Mwalimu aliniambia wataenda kwake kesho.

i) watu fulani wataenda kwa mwalimu

ii) watu fulani pamoja na mwalimu wataenda kwa mtu mwingine (2x1)

iii) watu wengine wataenda kwa mwalimu

iv) watu wengine pamoja na mwalimu wataenda kwa mwalimu

(l) Onyesha miundo miwili ya nomino katika ngeli ya LI –YA ( alama2)

Tunda - matunda – nomino zisizo chukua mofimu ya umoja lakini huchukua ma- katika wingi

Jicho – macho – nimono ambazo huchukua mofimu ji – katika umoja na ma- katika wingi

4 of 7
(m) Chanaganua sentensi ifuatayo kwa kutumia mchoro wa matawi. ( alama 4)

Huyu ndiye mwizi aliyewaibia watu pesa na atafikishwa mahakamani baadaye

S1 U S2

KN KT KN KT

V t KN T E E

N s

Huyu ndiye mwizi aliyewaibia watu pesa na ᴓ atafikishwa mahakamani


baadaye

( ¼ x 16)

(n) Tunga sentensi ukitumia kishazi tegemezi chenye dhana ya kielezi cha mahali. (alama 2)

Wakulima wote wamekuwa wakimfuata anakoenda.

(o) Kanusha (alama 2)

Mwamu wangu alinilea na kunielimisha.

Mwamu wangu hakunilea wala kunielimisha. (2/0)

(p) Andika sentensi ukitumia kitenzi – cha katika kauli ya kutendewa. ( alama 1)

q) Onyesha mofimu katika neno (alama 3)

aliowapa

a – nasfi yatatu umoja / ngeli

-li- wakati uliopita

-wa – yambwa/ watendewa

- p- mzizi
5 of 7
a- kiishio

(r) Andika kitenzi kifuatacho katika hali iliyopo mabanoni ( alama 2)

- ja – (nafsi ya pili wingi)

Kujeni

Shangazi alichwewa akitoka soko. (1/0)

(s) i) Kiri ni kwa kukana na ___ghali__ ni kwa nafuu. Na sifu ni kwa_______kashifu____ (alama 1)

( ½ x2)

ii) ____Hewala___ ni kwa kukubaliana na jambo , simile ni kutaka kitu kinusurike na hongera ni
____kupongeza______. ( ½ x2) (alama 1)

(t) Tunga sentensi moja kuonyesha maana tofauti za neno ‘ua’ ( alama 2)

Ua wa shule yetu una ua linalopendeza. ( 2x 0)

(anaweza kutumia wingi wa ua)

D. ISIMU JAMII

“ Maafisa 3 wakana kusaidia mshukiwa wa mauwaji ya watoto kutoroka kituoni.

Maafisa watatu wa polisi jana walikana mashtaka ya kumsaidia mshukiwa wa mauaji ya watoto 13 kutoroka
kutoka kituo cha polisi…”

(a) Huku ukitoa sababu mbili, tambua sajili hii. ( alama 3)

Sajili ya magazetini/ matangazo

Sababu – kuwepo kwa anwani/mada yenye mvuto

- matumizi ya usemi wa taarifa/ lugha ya kuripoti ( sajili 1, sifa 2x1)

(b) Fafanua sifa zozote nyingine saba za sajili hii. (alama 7)

i) mara nyingi vichwa vya habari havizingatii sarufi – ili kuokoa nafasi katika gazeti/muda

ii) baadhi ya jumbe ya mambo ya kweli – ili kuvutia wasomaji/ wanunuzi/wasikilizaji/mtazamaji

iii) mada/ anwani huwa fupi sana nay a kuvutia- ili kuvutia wateja/ wasomaji wa gazeti/wasikilizaji

iv) lugha inayotumika hutegemea taarifa inayotolewa- kila taaluma ina msamiati wake.

v) ujumbe huandikwa/husomwa katika aya fupifupi/ kwa muhtasari- ili kuokoa nafasi katika
magazeti/muda

6 of 7
Vi) lugha yenye kauli/ sentensi ndefundefu- ili kufafanua hoja kikamilifu.

vii) matumizi ya tarakimu badala ya maneno- ili kuokoa nafasi/kusomeka haraka

viii) lugha ya kuvutia – “mwalimu aonja asali”

ix) matumizi mengi ya chuku- “ paka amla ndovu”

x) matumizi ya sitiari/jazanda- ili kutasfidi lugha

xi) matumizi ya lugha rahisi- ili kupasha ujumbe kwa watu wa matabaka yote.

xii) lugha ya maelezo – ili kupasha ujumbe kwa njia nyepese na kueleweka rahisi. (zozote 7x1)

xiii) matumizi ya tasfida – ili kuficha ukali

xiv) lugha ya picha / michoro – ili ujumbe ueleweke

7 of 7

You might also like