You are on page 1of 8

CamScanner

CamScanner
CamScanner
CamScanner
CamScanner
MWONGOZO WA USAHIHISHAJI WA SOMO LA KISWAHILI 2023 (CSSC)

1. (alama 10 @1)
i ii iii iv v vi vii viii ix x
D D B D C E C E A C

2. (alama 6 @1)

FUNGU A i ii Iii iv v vi
FUNGU B D E G I C B

3. a) Mwanafunzi aandike vitenzi vishirikishi 6 kwa kutumia sentensi (Alama6@1)


 Ni/si - mfano (mimi ni/si mwalimu)

 Ndiye/siye- mfano ( huyu ndiye/siye mwizi )

 Alikuwa/ hakuwa - mfano (Mtoto alikuwa/ hakuwa mgonjwa)

 Ana/hana - mfano (bibi ana/hana mjukuu)

 Lipo/halipo – mfano (gari lipo/halipo ndani)

 yumo/hayumo – mfano (babu yumo/hayumo ndani)

b) Mwanafunzi atumie neno vizuri katika sentensi (Alama 03@01)

 Vizuri vimepangwa kabatini

 Viatu vizuri vimenunuliwa

 Mtoto anatembea vizuri

4. a) Sababu za utata (Alama 5@01)


i. Neno kuwa na maana zaidi ya moja mf mbuzi, kaa, paa,panga
ii. matumizi ya kauli ya kutendea mf. Amenipigia nini?
iii. matumizi ya lugha ya picha . Mf ua
iv. kutozingatia alama za uandishi. Mf baba Juma ameondoka
v. kutumia maneno bila kuzingatia muktadha. mf

b) Kutunga sentensi kwa kutumia maneno tata (Alama 04 @01)


a. Vua
 mjomba anavua samaki
 Mtoto amevua nguo
 Mwenyekiti amejivua uongozi
b. Shuka
 wanafunzi wametandika mashuka mekundu
 waliokuwa juu wote wameshuka chini.

5. (a) Mwanafunzi atoe maana ya lahaja (alama 1½)


Lahaja - ni muunganiko wa vilugha vinavyofanana katika maumbo na matamshi kuungana kuunda lugha
moja mfano Kiunguja, Kimtang’ata, Kingazija n.k

(b) Kiini hoja za mchango wa lahaja katika Kiswahili (alama 7½ @1½)


i. Usanifu wa lugha
ii. Mitindo mbalimbali ya mzungumzaji
iii. Kuchangia misamiati kwenye lugha ya Kiswahili
iv. Kupamba mazungumzo ya wazungumzaji wa lugha ya Kiswahili
v. Kusaidia katika machapisho mbalimbali yanayohusu lugha ya Kiswahili mfano Kiunguja,
kimombasa n.k

6. a) Mwanafunzi ataje hatua nne za uchanganuzi wa sentensi (alama 4 @1)


i. Kutambulisha aina ya sentensi
ii. Kuonesha sehemu kuu za sentensi
iii. Kuonesha vipashio vya kiima na kiarifu
iv. kuonesha aina za maneno
v. kuandika sentensi upya

(b) Mwanafunzi achanganue sentensi kwa njia ya Ngoe

S. SAHILI (alama 1)

KN KT (alama 1)

N V V T N V (alama 2)

Walimu wetu wapendwa wametupa kazi ya kufanya (alama 1)

(JUMALA ALAMA 09)


7. (a) mwanafunzi asome ufahamu na kujibu maswali
i. UMUHIMU WA KUJIAJIRI NA KUFANYA KAZI KWA BIDII, TUSITEGEMEE AJIRA N.K
(Alama 01)
ii. Kutokujituma na kujishughulisha, kukaa tu bila kufanya kazi (Alama 01)
iii. Watu wajishughulishe/wajiajiri kwenye kilimo (alama 01)
iv. Ni muundo wa moja kwa moja (alama 01)

(JUMLA ALAMA 04)

(b) UFUPISHO: Uzingatie mambo yafuatayo

i. Kichwa kikiwepo asikatwe alama, pia hakina alama


ii. Kiini chenye aya 2 juu ya umuhimu wa kujiajiri (alama 03)
iii. Lugha nzuri yenye kufuata ufasaha (alama 01)
iv. Idadi ya maneno husika (100) (alama 01)

(JUMLA ALAMA 05)

8. Kichwa (alama 01)


- Mwanzo wa barua kushoto (alama 01)
- Kiini jinsi ya kupiga vita mapenzi ya jinisa moja (aya 3 alama 02@ = alama 6)
- Mwisho anuani ya mwandishi (alama 01)

9. Utangulizi (alama 1½)


Kiini: sifa za fasihi simulizi (alama 2@ = alama 12)
 Kuwepo kwa fanani na hadhira
 Kuwa na uwanja wa kutendea
 Ni mali ya jamii nzima
 Hupokea mabadiliko ya papo kwa papo
 Huhifadhiwa kichwani
 Haina gharama

Hitimisho (alama 1½)

10. Utangulizi (alama 1½)


Kiini: (alama 2@ = alama 12)
Ukosefu waa elimu umepelekea mambo yafuatayo:
KILIO CHETU
 Kuongezeka kwa maambukizi ya virusi vya UKIMWI
 Mimba katika umri mdogo
 Mmomonyoko wa maadili

ORODHA

 Maambukizi ya virusi vya UKIMWI


 Kutokea kwa vifo
 Kukosekana kwa uwajibikaji katika shughuli mbalimbali
Hitimisho (alama 1½)

11. Utangulizi (alama 01½)


Mkufunzi ni mtu anayetoa maarifa kwa jamii/ wamafunzi wa vyuo. utambulisho wa kukubali kauli kwa
kutambulisha washairi wawili kwa herufi kubwa

KIINI: Hoja sita za jinsi ya waandishi wanavyoweza kutoa mafundisho kwa jamii (2@ Jumla 12)
- Waandishi ni wakufunzi wa kufundisha Uongozi bora - mfano: (Wasakatonge)
- Waandishi ni wakufunzi wa kupiga vita Rushwa
- Waandishi ni wakufunzi wa kufundisha jinsi ya kutumia mali vizuri – mfano: (malenga wapya)

Hitimisho (alama 01½)

You might also like