You are on page 1of 7

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

UMOJA WA WAKUU WA SHULE ZISIZO ZA SERIKALI-TANZANIA


(OHONGSS-T)
MIKOA YA MWANZA & KIGOMA
UPIMAJI WA KIUTIMILIFU KIDATO CHA PILI-MEI, 2023

MUONGOZO WA USAHIHISHAJI
021 KISWAHILI

SEHEMU A (Alama 15)


1. Mtahiniwa anatakiwa kuchagua herufi ya jibu sahihi na kisha aandike herufi hiyo
katika kisanduku cha kujibia.

SWALI (i) (ii) (iii) (iv) (v) (vi) (vii) (viii) (ix) (x)

JIBU B C B C A A C B C C

Vipengele 10 @ alama 01 = Alama 10


2. Mtahiniwa anatakiwa aoanishe maelezo yaliyo katika orodha A na dhana za kikamusi
zilizopo katika Orodha B kwa kuandika herufi ya jibu sahihi katika jedwali.

Orodha A (i) (ii) (iii) (iv) (v)

Orodha B B G A E C

Vipengele 5 @ Alama 1 = Alama 05

Ukurasa wa 1 kati ya 7
SEHEMU B (ALAMA 70)

3. Mtahiniwa anatakiwa kusoma kifungu cha Habari alichopewa na kujibu maswali.

(a) Msimamo wa mwandishi kuhusu uzalendo ni kuwa uzalendo ni mapenzi ya


kweli ya mtu kwa nchi yake, ni tabia ya ndani ya mtu ya kuzaliwa nayo.
(b) Mwandishi anatoa angalizo kuhusu uzalendo kuwa uzalendo hauanzi kwa
ulimwengu mzima bali unaanzia katika nchi yako mwenyewe. Pia uzalendo wa
kweli siyo kuchukua nchi nyingine.
(c) Usemi “kupinga pishi ya hoja zako kwa ukufi wa hoja zao” unamaanisha kuwa
kuna watu hupinga hoja za kweli kwa hoja zisizo na msingi ili kukwepa
ukweli.
(d) Kichwa cha habari hii kinaweza kuwa: UKWELI KUHUSU UZALENDO
(Vipengele 4 @ alama 2.5 = Alama 10)

4. Mtahiniwa anatakiwa atunge sentensi zenye vipashio alivyopewa


Mifano ya sentensi:

(a) Mwalimu alikuwa anafundisha wanafunzi darasani.


N Ts T N E
(b) Mwanafunzi hodari anatembea haraka.
N V T E
(c) Juma ni mwanafunzi mpole.
N t N V
(d) Alikuwa anatembea.
Ts T
(e) Yule wetu alikuwa anatembea kwa madaha.
W V Ts T H N
(Vipengele 5 @ alama 02 = Alama 10)

5. Mtahiniwa anatakiwa afafanue umuhimu wa kujifunza lugha ya Kiswahili kwa kutoa


hoja tano (5).

(a) Lugha ya Kiswahili itawasaidia wanafunzi kuelewa vyema masomo shuleni na


vyuoni na kupata maarifa yatakayowafanya wawe wenye weledi na umahiri
mkubwa katika Nyanja mbalimbali za Maisha.
(b) Lugha ya Kiswahili itawapa fursa wataalamu wa Kiswahili kuifundisha kwa
wageni ambao wanahitaji kujifunza lugha hii.
(c) Lugha ya Kiswahili inatumika kuwaunganisha watu wa Jumuiya ya Afrika
mashariki na bara la afrika kwa ujumla.

Ukurasa wa 2 kati ya 7
(d) Lugha ya Kiswahili imetambuliwa rasmi na UNESCO kama miongoni mwa
lugha za Kimataifa, hivyo basi itatoa fursa mbalimbali kwa wanaojifunza
katika masuala mbalimbali ya Kimataifa.
(e) Lugha ya Kiswahili inatumika katika shughuli mbalimbali za kijamii na
kiutamaduni kama vile mziki na michezo.
(Mtahini apime ukweli wa hoja zitakazotolewa na mtahiniwa na kuzipa
alama)
Vipengele 5 @ alama 2 = Alama 10.

6. Mtahiniwa anatakiwa afafanue tofauti tano (5) zilizopo baina ya lugha ya


mazungumzo na lugha ya maandishi.

(a) Uwasilishwaji: Lugha ya kimazungumzo huwasilishwa kwa njia ya


mazungumzo au masimulizi lakini lugha ya kimaandishi huwasilishwa kwa
njia ya maandishi.
(b) Mabadiliko: Lugha ya kimazungumzo hubadilika kulingana na mazingira,
wahusika, mada, wakati na madhumuni yake, lakini lugha ya kimaandishi
haibadiliki, pindi tu ikishaandikwa, hata kama ilikuwa na makosa, hadi
ifanyiwe marekebisho.
(c) Uhusiano na hadhira: Lugha ya kimazungumzo huwakutanisha ana kwa ana
mzungumzaji na msikilizaji, lakini lugha ya kimaandishi haiwakutanishi ana
kwa ana mwandishi na msomaji.
(d) Uhifadhi: Lugha ya kimazungumzo huhifadhiwa kichwani, lakini lugha ya
kimaandishi huhifadhiwa katika maandishi.
(e) Gharama: Lugha ya kimazungumzo haihitaji gharama nje ya ala za sauti ili
kuwezesha kutamka maneno vizuri lakini, lugha ya kimaandishi ina gharama
kubwa kwa sababu huhitaji vifaa vya kuandikia kama karatasi, kalam una vifaa
vingine ili iandikwe kwa ukamilifu.
(f) Uhai: Lugha ya kimazungumzo ni hai kwani huonesha ujumbe pamoja na
kudhihirisha hali ya mzungumzaji kama ana furaha, hasira, chuki na
huwashirikisha wasikilizaji katika vitendo kama vile: kushangilia, nk lakini
lugha ya kimaandishi siyo hai kwani haishirikishi wasikilizaji.
(g) Maandalizi: lugha ya mazungumzo haihitaji maandalizi makubwa ya mada,
lakini lugha ya maandishi inahitaji maandalizi ili kutafakari mambo
yatakayoandikwa na kuandaa vifaa kama vile kalamu, penseli, rula, karatasi
n.k
(Tofauti zozote zitakazotolewa zipimwe na mtahini na kupewa alama kwa
kadri zinavyostahili )
Vipengele 5 @ alama 2 = Alama 10.

Ukurasa wa 3 kati ya 7
7. Mtahiniwa anatakiwa kuonesha hasara tano (5) za kutumia misimu katika jamii.

(a) Huharibu lugha sanifu kutokana na kuwa si maneno sanifu.


(b) Huweza kuleta msamiati wa matusi na kuifanya lugha ipoteze hadhi na
heshima yake kwa jamii.
(c) Hupunguza hadhira hasa inapotumiwa kwa watu wasioielewa maana yake.
(d) Huzuka na kupotea, hivyo haiwezi kutegemewa sana katika mawasiliano.
(e) Husababisha utata katika mawasiliano kutokana na kuwa na maana nyingi.
(mtahiniwa anaweza kuonesha hasara zozote za kutumia misimu zipimwe
usahihi wake na kupewa alama)
Vipengele 5 @ alama 2 = Alama 10.

8. Mtahiniwa anatakiwa kuonesha jinsi methali alizopewa zinavyoweza kupotosha jamii


iwapo vitatafsiriwa vibaya.

(a) Haraka haraka haina baraka.


Watu wanaweza kufanya mambo polepole na kusababisha kuharibika au
kuchelewa kwa mambo kwa kuhofia kuwa na haraka.
(b) Tamaa mbele mauti nyuma.
Methali hii inaweza kuwafanya watu wasiwe ha hamasa ya kutafuta mafanikio
kwa kuhofia kuonekana wana tamaa.
(c) Mficha uchi hazai.
Methali hii inaweza kushawishi vijana kujirahisisha kimapenzi kwa kuhofia
kuwa wakijitunza watashindwa kuzaa.
(d) Si kila king’aacho ni dhahabu.
Methali hii inaweza kuwafanya watu wakaacha vitu au mambo mazuri kwa
kuogopa mvuto na uzuri wa vitu hivyo kuwa unaweza kuficha ubovu.
(e) Ajali haina kinga
Methali hii inaweza kuwafanya watu kutokuwa na hadhari au umakini na
kusababisha ajali kwa uzembe kwa kisingizio kuwa ajali haina kinga.
(Mtahini apime majibu ya mtahiniwa na kuona usahihi wa majibu hayo)
Vipengele 5 @ alama 2 = Alama 10.

Ukurasa wa 4 kati ya 7
9. Mtahiniwa anatakiwa kufafanua faida tano (5) za kuhifadhi fasihi kwa njia ya vinasa
sauti (tepurekoda). Majibu yanaweza kuwa:

(a) Njia hii inaweza kutunza kumbukumbu kwa muda mrefu na kumbukumbu
zilizohifadhiwa kwa njia hii hazipotei au kusahaulika.
(b) Lafudhi na sauti ya fanani huweza kuhifadhiwa kwa muda mrefu bila
kuathirika.
(c) Njia hii haibagui hadhira kwani huwanufaisha hata wasiojua kusoma na
kuandika.
(d) Njia hii huifanya fasihi simulizi iendane na wakati na mabadiliko ya
kiteknolojia yanayojitokeza katika jamii.
(e) Husaidia fasihi kuenea na kuwafikia watu wengi kwa haraka.
(Mtahiniwa anaweza kutoa faida zozote za kweli, zipimwe usahihi wake na
kupewa alama)
Vipengele 5 @ alama 2 = Alama 10.

SEHEMU C (Alama 15)

10. Mtahiniwa anatakiwa aandike barua rasmi yenye vipengele muhimu vifuatavyo:
(i) Anwani ya mwandishi.
(ii) Tarehe
(iii) Anwani ya mwandikiwa (mkuu wa shule)
(iv) Anwani ya mtu ambako barua inapitia (mwalimu wa darasa)
(v) Salamu
(vi) Kichwa cha barua
(vii) Kiini cha barua (lengo la barua)
(viii) Kimalizio cha barua.
(ix) Saini ya mwandishi.
(x) Jina la mwandishi
(xi) Cheo cha mwandishi.

Ukurasa wa 5 kati ya 7
MFANO WA BARUA:

SHULE YA SEKONDARI MAENDELEO,


S.L.P 10023,
TANDAHIMBA.
02/05/2023

MKUU WA SHULE,
SHULE YA SEKONDARI MAENDELEO,
S.L.P 10023,
TANDAHIMBA.

KK: MWALIMU WA DARASA,


KIDATO CHA PILI “A”,
SHULE YA SEKONDARI MAENDELEO,
S.L.P 10023,
TANDAHIMBA
Ndugu,
YAH: MAOMBI YA RUHUSA YA KUHUDHURIA SEMINA YA
UELIMISHAJI RIKA
Rejea mada tajwa hapo juu. Mimi ni mwanafunzi wa kidato cha pili “A” katika
shule yako. Nimechaguliwa kuhudhuria semina ya Uelimishaji Rika itakayofanyika
katika shule ya Sekondari Songambele iliyoko mjini Songea, kuanzia tarehe
15/07/2023 hadi tarehe 22/07/2023.
Naomba ruhusa ya kuhudhuria semina hiyo. Semina hiyo ninaamini itakuwa na
manufaa kwangu binafsi, lakini pia na kwa wanafunzi wenzangu, kwani tunatakiwa
baada ya kupata mafunzo hayo ya Elimu Rika tuwaelimishe na wanafunzi wenzetu.
Ninatanguliza shukrani za dhati na ninaamini ombi langu litakubaliwa.

Wako mtiifu,
B. Msomi
Bahati Msomi
(Mwanafunzi).

Ukurasa wa 6 kati ya 7
MGAWANYO WA ALAMA:

Anwani ya mwandishi -Alama 01


Tarehe -Alama 01
Anwani ya mkuu wa shule -Alama 01
Anwani ya mwalimu wa darasa -Alama 01
Salamu -Alama 01
Kichwa cha barua -Alama 01
Kiini cha barua -Alama 06
Kimalizio cha barua -Alama 01
Sain ya mwandishi -Alama 0.5
Jina la mwandishi -Alama 0.5
Cheo cha mwandishi -Alama 01

Jumla ya alama: 15

Ukurasa wa 7 kati ya 7

You might also like