Professional Documents
Culture Documents
Jaribio La Kiswahili Kidato Cha 4
Jaribio La Kiswahili Kidato Cha 4
JARIBIO LA KISWAHILI
KIDATO CHA NNE
Maelekezo
1. Karatasi hii ina sehemu A, B na C zenye jumla ya maswali kumi na mbili (12).
2. Jibu maswali yote katika sehemu A na B, maswali matatu (3) kutoka sehemu C.
3. Zingatia maagizo ya kila sehemu na ya kila swali .
4. Simu za mkononi na vitu vyote visivyoruhusiwa havitakiwi katika chumba cha mtihani.
5. Andika Jina lako katika kila ukurasa wa karatasi yako ya kujibia.
1
SEHEMU A (Alama 15)
Jibu maswali yote katika sehemu hii.
1. Chagua herufi ya jibu sahihi katika vipengele (i) hadi (x), kisha andika herufi ya jibu hilo
katika Karatasi yako ya kujibia.
2
(viii) …….ni kipashio kinachokamilisha au kujazia neno kuu.
A Kijalizo
B Sentensi
C Chagizo
D Igizo
(x) ……ni kielezi au kirai husishi ambacho kinafanya kazi kama kielezi.
A Chagizo
B Mizani
C Ushairi
D Visakale
2. Oanisha maana za dhana za uandishi zilizo katika Orodha A kwa kuchagua herufi ya
dhana husika katika Orodha B , kisha andika herufi husika katika karatasi yako ya
kujibia.
Orodha A Orodha B
(i) Wasikilizaji au watazamaji wa A. Ngonjera
kazi za fasihi. B. Hadhira
(ii) Ni msimuliaji wa kazi za fasihi. C. Fanani
(iii) Hii ni kazi ya fasihi andishi D. Hadithi fupi
E. Mafunzo
yenye kisa kimoja.
F. Mapisi
(iv) Ni nasaha anazotoa mtunzi. G. Riwaya
(v) Maelezo ya historia bila kutia H. Shairi
mambo ya kubuni.
3. Eleza maana ya vidahizo vifuatavyo na kisha tunga sentensi moja (1) kwa kila kidahizo.
a) Kinyenyezi
b) Matandu
c) Matlaba
d) Sandali
e) Uzimbezimbe
4. Tunga sentensi mbili zinazoonesha kishazi huru na tatu zinazoonesha kishazi tegemezi.
6. Kwa kutumia mifano, thibitisha ubantu wa Kiswahili kwa hoja madhubuti tano (5).
3
7. Kwa kutumia vitabu viwili vya tamthiliya mbili ulizosoma chagua wahusika wawili na
uoneshe kutokukubalika kwao katika jamii. (Toa hoja tatu kwa kila mhusika)
Wakati wa ukoloni mabepari wa Kijerumani walianzisha kilimo cha pamba huko Kusini
mwa Tanzania. Waliwalazimisha Wamatumbi kufanya kazi katika mashamba yao.
Pamba iliyopatikana ilipelekwa Ujerumani. Kama anavyosema kibarua mmoja aliyeteswa
na mabepari hao, " Wakati wa kilimo kulikuwa na dhiki sana. Sisi vibarua tuliokamatwa
tulikaa mstari wa mbele, tukilima. Nyuma yetu kulikuwa na mnyapara , kazi yake
kutupiga kwa mijeledi . Nyuma ya mnyapara alikuwepo jumbe, na kila jumbe alisimama
nyuma ya watu hamsini. Na nyuma ya majumbe alisimama Bwana Kinoo mwenyewe.
Lo! Hapo shuhudia kifo."
Juu ya dhiki zote walizopata yaani dhiki ya njaa, dhiki ya maonevu, dhiki ya kulimishwa
na kupigwa, watu walistahimili wakavumilia kwa sababu hawakuweza kupigana, kwani
hawakuwa na umoja. Vilevile walijua kuwa nguvu ya Mjerumani ilikuwa kubwa.
Wakangoja.
Katika mwaka wa 1904 akaja mtume , jina lake Kinjeketile. Karibu na kwao Ngarambe
kulikuwa na bwawa la maji kaitika kijito cha Mto Rufiji. Kinjeketile alipandwa na pepo
aitwaye Hongo, aliyekuwa akikaa katika bwawa hilo.
Kinjeketile aliwafundisha Waafirka maana ya umoja, akawapa moyo kwa nguvu ya maji.
Waafrika wakawa na umoja na nguvu. Watu wengi waliosikia jina lake walikuja
kumuunga mkono.
Maswali
a) Andika kichwa cha habari kinachofaa kwa habari uliyosoma kisichozidi maneno matano.
b) Eleza wazo kuu linalojitokeza katika habari uliyoisoma.
c) Ni mambo gani yanayothibitisha kwamba ni kweli Wamatumbi waliteswa? Taja mambo
matatu.
d) Toa maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumika katika kifungu cha habari
ulichosoma.
(i) Mnyapara
(ii) Mijeledi
(iii) Walistahimili
(iv) Sadaka
(v) Mtume
4
SEHEMU C (Alama 45)
Jibu maswali matatu (3) kutoka katika sehemu hii.
9. Andika risala inayohusu wahitimu wa kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Paradiso.
USHAIRI
Wasakatonge - M.S. Khatibu (DUP)
Malenga Wapya - TAKILUKI (DUP)
Mashairi ya Chekacheka - T.A. Mvungi (EP & D.LTD)
RIWAYA
Takadini - Ben J. Hanson (MBS)
Watoto wa Mama N’tilie - E. Mbogo (H.P)
Joka la Mdimu - A.J. Safari (H.P)
TAMTHILIYA
Orodha - Steve Reynolds (MA)
Ngoswe Penzi Kitovu cha Uzembe - E. Semzaba (ESC)
Kilio Chetu - Medical Aid Foundation (TPH)
10. “Washairi ni wataalamu wazuri na waliobobea katika kutumia taswira zinazotoa ujumbe
kwa jamii.” Tumia taswira tatu kwa kila diwani kati ya diwani mbili zilizoorodheshwa
kuthibitisha kauli hiyo.
11. Jadili kukubalika kwa wahusika wawili kama kielelezo halisi cha wanajamii kati ya
Takadini, Maman’tilie na Brown Kwacha kutoka katika riwaya mbili ulizosoma. Toa
hoja tatu kwa kila mhusika.
12. Waandishi wa tamthiliya wamemchora mwanamke katika sura tofauti. Thibitisha kauli
hii kwa kutumia waandishi wawili (2) wa tamthiliya mbili (2) ulizosoma. (Toa hoja tatu
kwa kila tamthiliya uliyosoma)