You are on page 1of 4

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
Shule ya Awali na Msingi Isaiah Samaritan
“Mchepuo wa Kiingereza”
S.L.P: 2919 MBEYA
isaiahsamaritanschools@gmail.com
SIMU: 0756 994 562, 0713 604 889
Tawi la Mbeya
MTIHANI WA MWISHO WA MWEZI DARASA LA SABA-FEBRUARI 2020
SOMO: KISWAHILI
JINA: TAREHE:
MUDA: SAA 1 DAKIKA 30
MAELEKEZO
 Mtihani huu una jumla ya maswali 45
 Jibu maswali yote kutokana na maelekezo uliyopewa.

SEHEMU A: SARUFI
Chagua jibu sahihi kutoka kwenye machaguo kisha andika herufi ya jibu hilo kwenye
mabano
1. Ungeliniambia mapema nisingekubali uende. Kipi ni kiambishi cha masharti katika sentensi hii:
A. U B. –nge- C. –ngeli- D. Ungeli- E. –ili- [ ]
2. Kinyonga anatembea polepole. Neno lililokolezwa wino na kupigiwa mstari limetumika kama
aina ipi ya maneno?
A. Kitenzi B. Kiwakilishi C. Kivumishi D. Nomino E. Kielezi [ ]
3. Watoto wanapigana. Neno wanapigana lipo katika kauli ipi?
A. Kutendea B. Kutenda C. KutendanaD. Kutendwa E. Kutendewa[ ]
4. Kisawe cha neno werevu ni:
A. Ujinga B. Wema C. Uovu D.Ujasiri E. Ukatili [ ]
5. Viumbe wafuatao wapo kwenye kundi la ndege, ISIPOKUWA:
A.Bundi B.Mwewe C.Nzige D. Njiwa E.Kanga [ ]
6. Kule anakoishi bibi Mwamvita.
A. Ndimo B. Ndiko C. Ndipo D. Ndio E. Ndiyo [ ]
7. Kifaa kinachotumika kuwekea mishale hujulikana kama:
A. Ala B. Jibini C. Pingili D. Mkebe E. Podo [ ]
8. Umoja wa sentensi hii: “ Maji yamemwagika” ni:
A. Ji limemwagika C. Maji imemwagika E. Maji limemwagika [ ]
B. Mmaji umemwagika D. Maji yamemwagika
9. Laiti kama ningejua nisingekuamini. Hii ni aina gani ya sentensi?
A. Shurutia B. Tegemezi C. Changamano D. Sahili E. Ambatano [ ]
10. Naomba nimeze japo moja tu la maji maana nina kiu sana.
A. Fundo B. Tonge C. Futo D. Funda E. Lepe [ ]
11. Neno lipi la Kiswahili lenye maana linaweza kuundwa kwa kuondoa silabi moja katika
neno “birika”?
A. Kabi B. Kiri C. Rika D. Kari E. Baki [ ]
12.Neno mwanafunzi lina silabi ngapi?
A. Tisa B. Nne C. Tano D. Sita E. Saba [ ]
13. laweza kutokea:
A. Yeyote B. Wowote C.Popote D. Lolote E. Lelote [ ]
14.Wewe u mpole. Katika sentensi hii herufi u imetumika kama:
A. Kiunganishi C. Kihusisishi E. Kiwakilishi kimilikishi [ ]
B. Kitenzi kisaidizi D. Kitenzi kishirikishi
15.Neno gari lipo katika ngeli ipi?
A. U-ZI B. A-WA C. LI-YA D. KI-VI E. I-ZI [ ]
16.Mnyama aliyekufa bila kuchinjwa hujulikana kama:
A. Kibudu B. Mzoga C. Marehemu D. Hayati E. Mfu [ ]
17. Mwenge wa Uhuru umewasili kijijini kwetu. Sentensi hii ipo katika wakati gani?
A. Uliopo B. Ujao C. Timilifu D. Ujao E. Mazoea [ ]
18.Bunge ndicho chombo pekee chenye mamlaka ya kutunga na ku sheria.
A. Teuliwa B. Tegua C. Tumbua D. Tetea E. Tengua [ ]
19.Tunacheza mpira. Sentensi hii ipo katika nafsi ipi?
A. Nafsi ya kwanza umoja C. Nafsi ya pili wingi E. Nafsi ya tatu umoja [ ]
B. Nafsi ya tatu wingi D. Nafsi ya kwanza wingi
20.Neno lipi kati ya maneno yafuatayo ni kisawe cha neno aibu?
A. Furaha B. Faragha C. Shauku D. Soni E. Dharau [ ]

SEHEMU B: LUGHA YA KIFASIHI


21.Kamilisha methali hii: Kufa
A. Ni lazima B. Kwaja C. Kufaana D. Kunatisha E. Hakuishi [ ]
22. Kila ukiwakuta wamejitayarisha kupigana. Jibu lipi ni sahihi kuhusu kitendawili hiki?
A. Nywele C. Pamba E. Mvi [ ]
B. Manyoya D. Katani
23. Nahau kukata maini ina maana gani?
A. Kukatisha tamaa C. Kufurahisha E. Kukasirisha [ ]
B. Kushtua D. Kuhuzunisha
24. Methali ipi kati ya hizi zifuatazo inapingana na methali isemayo “ manahodha wengi
chombo huenda mrama”?
A. Penye watu wengi hapaharibiki neno D. Wingi si hoja [ ]
B. Usilolijua ni sawa na usiku wa giza E. Usimwage mtama kwenye kuku wengi
C. Heri kenda shika kuliko kumi nenda uje
25. Nyumba yangu imeungua mwamba wake umebaki. Jibu la kitendawili hiki ni:
A. Mfupa B. Jiwe C. Mlima D. Kuni E. Nazi [ ]
26. “Kwa kuwa unahisi dalili za ugonjwa malaria ni bora uwahi hospitali kwenda kupima
kabla ugonjwa haujashika kasi”. Methali ipi kati ya hizi zifuatazo inaendana na kifungu
hiki cha maneno?
A. Maji ukiyavullia nguo sharti uyaoge D. Usipoziba ufa utajenga ukuta
B.Hucheka kovu asiyefikwa na jeraha E. Ukiona vyaelea ujue vimeundwa [ ]
C. Mkuki kwa nguruwe kwa binadamu mchungu
27. Nahau ipi kati ya hizi zifuatazo ina maana ya kujiingiza matatizoni?
A.Kujipalia mkaa C. Kung’ata maneno E.Kushikwa sikio [ ]
B.Kuanika juani D.Kuwa na ulimi wa panga
28. Tegua kitendawili hiki: Viti vyote nimekalia isipokuwa hiki.
A. Moto B. Barafu C. Mwiba D. Kivuli E. Maji [ ]
29. Methali ipi kati ya hizi zifuatazo ina maana sawa na methali isemayo “ upele humwota asiye
na kucha”?
A. Cha mgema huliwa na mlevi D. Ngoma ikisifiwa sana mwishowe hupasuka [ ]
B. Mshindo mkuu huvuma mbali E. Penye miti mingi hapana wajenzi
C. Tamaa mbele mauti nyuma
30. Rajabu amefunga pingu za maisha hivi karibuni. Nahau ipi ina maana sawa na nahau
kufunga pingu za maisha?
A. Kushika usukani C. Kuandaa meza E. Kumwaga unga [ ]
B. Kula chumvi nyingi D. Kupata jiko

SEHEMU C: USHAIRI:
Soma shairi lifuatalo kisha jibu maswali yanayofuata
Maisha yaliyo bora, maneno yatamkika,
Walitaka zetu kura,kapuni wakatuweka,
Twaishi kama chokora, na siku
zinakatika,
Hakuna maisha bora, haya ni bora maisha.

Tanzania nchi yangu, yenye wingi wa


maneno, Amani hili ni jungu, latukwaza si
mfano, Mikononi nina pingu,yako’pi yenu
maono,
Hakuna maisha bora, haya ni bora maisha.

MASWALI
31. Shairi hili linazungumzia nini?
A. Maisha bora C. Amani E.Maneno yatamkika [ ]
B. Upigaji kura D. Maisha yaa gerezani
32. Kila mshororo katika ubeti wa shairi hili una mizani ngapi?
A. 8 B. 4 C. 5 D. 16 E. 12 [ ]
33. Vina vya kati katika ubeti wa pili ni :
A. u B. no C. ngu D. ra E. angu [ ]
34. Maana ya nahau kuweka kapuni kama ilivyotumika katika shairi hapo juu ni:
A. Kusaidia C. Kusahau E. Kusononeka [ ]
B. Kukumbuka D. Kushughulikia
35. Mstari uliokolezwa wino katika kila ubeti wa shairi hili hujulikana kama:
A. Mzani B. Kina C. Kituo D. Mkarara E. Ubeti [ ]
36. Kwa ujumla shairi hili lina jumla ya beti ngapi?
A. Nne B. Sita C. Mbili D. Nane E. Tatu [ ]

SEHEMU D: UTUNGAJI
Sentensi zifuatazo zimechanganywa. Zipange katika mtiririko mzuri kwa kuzipa
herufi A,B,C na D.
37. Kwa mara ya kwanza ulilipotiwa katika jimbo la Wuhan nchini China. [ ]

38.Ungonjwa wa homa ya mafua kali ni miongoni mwa magonjwa hatari zaidi duniani. [ ]

39. Mpaka sasa takribani nchi 30 duniani zimesharipoti kukumbwa na ugonjwa huu. [ ]

40.Ugonjwa huu husababishwa na virusi vijulikanavyo kama Korona. [ ]


SEHEMU E: UFAHAMU
Soma kwa makini kifungu cha habari kifuatacho kisha jibu maswali kwa usahihi
kama ulivyoulizwa
Haikuwa kazi rahisi kwa wanafamilia wote kuamini kuwa ameiaga dunia. Alikuwa ni kipenzi cha watu
wote katika familia yetu. Alimcha sana Mungu. Alijipenda sana na alikuwa ni mchapakazi.
Wafanyakazi wenzake walipoteza fahamu baada ya kusikia habari za msiba ule.
Alikuwa ni kitinda mimba katika familia yetu yenye watoto watano. Mimi nikiwa mkubwa wa wote
baada ya Juma, ndipo alipozaliwa yeye. Ilikuwa ni kama masihara pale tuliposikia kuwa amegongwa
na gari na hali yake si nzuri. Familia nzima tulikimbilia eneo la tukio lile. La hasha! Tulimkuta Zuberi
amefunikwa mwili wote. Nguo aliyofunikwa na wasamaria wema imetapakaa damu. Masikini sisi,
tumempoteza mdogo wetu. Sasa tumebaki mimi, Juma, Jose na Mina.

MASWALI
41. Mtoto aliyefariki kwa mujibu wa habari hii anaitwa nani?

42. Wasamaria wema ni watu gani?

43. Maneno La hasha! Katika kifungu cha habari hapo juu yametumika kuonesha hali gani?

44. Neno kitinda mimba kama lilivyotumika katika kifungu cha habari hapo juu lina maana gani?

45. Familia hiyo ilikuwa na watoto wangapi jumla?

You might also like