You are on page 1of 4

HALMASHAURI YA WILAYA YA SERENGETI

MTIHANI WA MAJARIBIO (MOCK) KATA YA UWANJA WA


NDEGE
SOMO LA SAYANSI DARASA LA SABA : MARCH 2015

JINA
MUDA SAA SAA 1:30
Chagua herufi ya jibu sahihi kisha weka kivuli kwenye
herufi ya jibu sahihi katika karatasi yako ya kujibia
1. Mtu anayefanya mazoezi mara kwa mara anaweza kuepukana na ugonjwa ufuatao;-

A. ukimwi B. shinikizo la damu C. malaria D. anemia E. surua.


2. Virutubisho vifuatavyo huhitajika kwa kiasi kikubwa kwa mama anayenyonyesha ili
kutengeneza maziwa

A. kabohaidreti na mafuta B. vitamini na chumvichumvi za madini C. protini na vitamini

D. protini na chumvi za madini E. kabohadreti na protini.


3. Ugonjwa wa damu unaosababishwa na hitilafu katika hemoglobin ndani ya seli
nyekundu za damu ni;-
A. saratani B. malaria C. anemia selimundu D. homa ya matumbo E. kichocho.
4. Huduma ya kwanza inayoweza kutolewa kwa kwa mtu mwenye kwikwi ni;-
A. kumunywesha maji safi na salama mfululizo B. kumlaza chali C. kumpigapiga kifuani na
mgongoni
D. kumziba pua na mdomo E. kumpa dawa ya kutapika
5. _____________ ni ugonjwa ambao ukikaa kwa muda mrefu mwilini bila kutibiwa husababisha njia
ya mkojo
kuziba na uvimbe kwenye korodani kwa mwanaume.

A. Trikonoma B. Kaswende C. Kisonono D. Ukimwi E. Klamedia


6. Ipi kati ya zifuatazo siyo dalili ya ugonjwa wa pepopunda.

A. kupata homa kali B. kutokwa na vipele mwilini C. kushitukashituka na kukaza misuli

D. kupata maumivu makali kwenye uti wa mgongo E. kukaza kwa shingo.


7. Uvuvi wa samaki wa kutumia baruti ni njia mojawapo ya;-
A. kukuza sayansi B. kuua magugu maji yanayochafua mazingira
C. kuharibu mazalia ya samaki na kuchafua mazingira D.kuondoa aina ya samaki
E.kuwafukuza papa wakali wasiwale samaki wadowadogo.
8. Hewa inayobadili maji maangavu ya chokaa kuwa rangi ya maziwa ni;-

A. oksijeni B. naitrojeni C. haidrojeni D. kabondayoksaidi E. kobonmonoksaidi


9. Mojawapo ya matukio yafuatayo yanaweza kusababisha tetemeko la ardhi;-
A. radi B. mwangwi C. mawimbi ya maji D. upepo mkali E. kulipuka kwa moto ndani
ya ardhi.
10. Wanyama walao mimea wakiongezeka sana watamaliza mimea na hivyo.

A. wanyama walao nyama watakufa B. watakosa hewa C. watakosa chakula na kufa


D. watanenepa sana
E. watakufa kwa joto.
11. Kani ya mvutano kati ya dunia na mwezi husababisha.

A. kupwa na kujaa kwa maji bahari B. tetemeko la ardhi C. kupatwa kwa mwezi D.
mawimbi ya bahari
E. majira ya mwaka.
12. Ipi kati ya mbolea zifuatazo ina karibu aina zote za elementi zinazohitajika na mimea.

A. Urea B. Samadi C. CAN D. SA E. NK.


13. Wanyama ambao miili yao imeundwa kwa chembe hai zaidi ya moja huitwa.
A. Amiba B. Protozoa C. Paramisiamu D. Fungi E. Metozoa.
14. Ipi ni sahihi kuhusu metamofosisi iliyokamilika?.
A. Yai,Lava,Mdudu (Insekta) B. Mdudu (Insekta), Pupa na Lava C. Yai,Lava,Pupa,Mdudu
(Insekta)
D. Pupa,Yai,Lava,Mdudu (Insekta) E.Yai,Pupa,Lava, Mdudu (Insekta).
15. Kinyonga hujilinda na maadui zake kwa kujibadilili rangi kufuatana na mazingira
alipo. Je, Nungunungu hujilinda kwa.
A. mbio alizonazo B. miiba aliyonayo mwilini C. mkia wake mrefu D. makucha yake
E. wepesi wake.
16. Ni kiumbe yupi kati ya hawa ni Reptilia?.
A. Chura B. Mjusi C. Panya D. Kuku E. Popo.
17. Kati ya wanyama hawa yupi huishi majini.
A. Mamba B. Kenge C. Nyangumi D. Kobe E. Kiboko.
18. Sehemu ya Pistili inayosafirisha chavua kutoka kwenye stigma kwenda kwenye ovari
huitwa;-
A. Staili B. Ovari C. Filamenti D. Stameni E. Petali.
19. Moja kati ya sifa zifuatazo siyo sifa ya mimea aina ya daikotilidoni.
A. ina mzizi mkuu B. ina ghala mbegu mbili C. veni zake ziko kama wavu D. wakati
wa kuota
mbegu, mche husukuma ghala juu ya ardhi E. veni zake ni sambamba.
20. Mwale wa mwanga unaposafiri kutoka media moja kwenda media nyingine.
A. hupinda B. hutoa cheche C. husharabiwa D. huakisiwa E. hunyooka
21. Ukweli ni kwamba;-
A. kinyonga huzaa B kinyonga hutaga mayai C. kinyonga hufa baada ya kuzaa D.
popo ni ndege
E. kerengende huishi majini.
22. Lipi kati ya mabadiliko yafuatayo siyo badiliko la kikemia.
A. maziwa kuchachuka B. tunda kuoza C. chuma kupata kutu D. kusagwa kwa
nafaka
E. chakula kumengenywa tumboni.
23. Chunguza kielelezo Namba 1 kisha jibu swali lifuatalo

Alama hii katika umeme huwakilisha?


A. fyuzi B. soketi C. taa ya umeme D. ukinzani E. voltimita.
24. Transifoma isipofanya kazi umeme.
A. utafifia B. utazimika C. hautaongezeka wala kupungua D. utaongezeka E.
utapungua
25. Chunguza kielelezo Namba 2 kisha jibu swali.

Ikiwa mkono utavuta mizani ya spingi nini kitatokea?


A. vipimo katika mizani ya spingi A vitakuwa sawa na vipimo katika mizani B
B. vipimo katika mizani ya springi A vitakuwa vikubwa kuliko mizani B
C. vipimo katika mizani ya springi B vitakuwa vikubwa kuliko mizani A
D. vipimo vitakavyosomeka ni vya mizani ya spingi A tu
E. vipimo vitakavyosomeka ni vya mizani ya springi B tu.
26. Kani inayobadili kani ya vitu vinavyozama ndani ya maji au katika aina yeyote ya
ugiligili ni;-
A. kani mnyanyuo B. kani kinzani C. kani mbadala D. kani ya kuteleza E. kani ya
msuguano.
27. Jicho la binadamu lina lenzi;-
A. mbonyeo B. mbinuko C. bapa D. dufu E. duara
28. Uchukuzi katika miili yetu hufanywa na;-
A. homoni B. damu C. hewa D. moyo E. figo.
29. _____________ni masalia ya viumbe hai yasababishwayo na hali joto la juu na kani eneo
kubwa.
A. maji B. miamba C. gesi D. volkano E. chumvi.
30. Gesi inayotokana na vinyesi vya wanyama huitwa.
A. oksijeni B. bayogesi C. hadrojeni D. kabondayoksaid E. kabonmonoksaidi.
31. Maada inayofanyika kutokana na muungano wa elementi mbili au zaidi huitwa.
A. elementi B. kampaundi C. molekyuli D. atomi E. oksijeni.
32. Chunguza kielelezo Namba 4 kisha jibu swali lifuatalo.

Nini kitatokea katika jaribio hili la kisayansi.


A. msumari utayeyuka B. betri litalipuka C. waya utaungua D. msumari utakuwa
mwekundu E. msumari utapata usumaku.
33. Mojawapo ya mambo yanayochangia uchafuzi wa hewa angani ni;-
A. ongezeko la viwanda B. uchimbaji wa madini C. ufugaji usiozingatia idadi ya
mifugo
D. utafiti wa gesi na mafuta E. ongezeko la misitu.
34. Kipi kati ya vifuatavyo watabiri wa hali ya hewa hukitumia kubaini kiwango cha jotoridi
mahali
fulani. A. barometa B. anemometa C. themosi D. amita E. themometa
35. Watu wanaozama katika kina kirefu cha maji hubeba mitungi iliyojazwa hewa ya ___ ili
kuwasaidia
katika upumuaji wakiwa majini.
A. oksijeni B. kabonmonoksaidi C. kabondayoksaidi D. uhai E. haidrojeni.
36. Ni kiasi gani cha umeme unaopita kwenye waya wenye ukinzani wa ohm 60 iwapo
tofauti ya
potenshali ni volti 12. A. 66A B. 5A C. 720 ohm D. 0.2 oh E. 50A
37. Mshipa wa damu unaotoa damu kwenye moyo kupeleka kwenye mapafu unaitwa;-
A. ateri kuu B. bronchioli C. ateri ya pulimonari D. vena ya pulimonari E. vena kava
38. Utando unaotolewa na chembe sahani ili kuzuia damu isiendelee kutoka kwenye jeraha
unaitwa;-
A. limfu B. plazma C. fibrinojeni D. hemoglobini E. uroto.
39. ________ ni homoni ambayo ikizidi mwilini msichana anaweza kuvunja ungo mapema
au kupata
mimba katika umri mdogo.
A. thairoksini B. adrenalini C. insulin D. testosterone E. estrojeni.
40. Fomula ya sukari aina ya glukosi ni. A. CHO B. Nacl C. HO D. 2HO E. HC
41. Miamba inayotokana na kupoa kwa lava hujulikana kama .
A. miamba migumu B. miamba tabaka C. miamba geu D. magma E. miamba moto.
42. Sehemu ya ubongo ambayo huhusika na mapigo ya moyo na upumuaji ni.
A. medulla oblangata B. selebramu C. selebellum D. neva mota E. neva sensori.
43. Ni kipi kati ya vifuatavyo kikikosekana mwilini husababisha ugonjwa wa beriberi.
A. vitamin C B. ayani C. vitamini B D. protini E. vitamini D.
44. Vitamini katika vyakula huweza kuharibiwa kwa;-
A. kupikwa na kukobolewa B. kupikwa na kukaangwa C.kupikwa kwa mafuta na
kupondwapondwa
D. kuondoa viini vya nafaka na kupikwa mno E. kupondwapondwa na kukaangwa.
45. Ni kipi kati ya vifuatavyo mtoto anaweza kurithi kutoka kwa wazazi wake.
A. saratani B. pumu C. ualbino D. polio E. surua
46. Chunguza Kielelezo Namba 5 kisha tafuta thamani ya X.
Sm 10 sm X

gm175 gm 350
A. sm 3 B. sm 5 C. sm 15 D. sm 10 E. sm2
47. Yupi kati ya hawa siyo mnyama mwenye uti wa mgongo
A. popo B. papa C. reptilia D. tandu E. amfibia
48. Mrija unaounganisha sikio la kati na koo la hewa huitwa;
A. folopio B. Eustachio C. neva za optiki D. koromeo E. pina.
49. Chunguza kielelezo Namba 6 kisha chagua herufi ya jibu sahihi.

Sehemu ipi mnyama huyu huitumia kusharabu oksijeni.


A. B B. C C. E D. A E. D.
50. Mbu aina ya Ades huneza ugonjwa wa;-
A. surua B. homa ya manjano C. matende D. malaria E. malale .

You might also like