JINA LA MWANAFUNZI:________________________ TAREHE:__________
SEHEMU ‘A’ CHAGUA JIBU SAHIHI 1. Seli nyekundu za damu zilizokufa hutolewa mwilini kupitia__________ ( ) (a)mkojo (b)jasho (c)kinyesi. 2. Mtu anapoota moto anapata joto kwa njia ya ___________ ( ) (a)msafara (b)mpitisho (c)munururisho. 3. Lenzi mbonyeo hutumika hutumika kutengenezea miwani kwa ajili ya watu wasioona ___________ (a)mbali (b)karibu (c)pembeni. ( ) 4. Ni sehemu gani hupitisha gamete uke kutoka kwenye ovari hadi uterasi_________ (a)korodani (b)mirija ya falopia (c)ovari. ( ) 5. ___________ hutaga mayai majini hata kama yeye huishi nchi kavu. ( ) (a)kobe (b)kasa (c)chura. 6. ___________ huishi majini lakini hutaga mayai yake nchi kavu. ( ) (a)papa (b)kobe (c)mjusi (d)kasa. 7. Ni elimu ya uhusiano wa viumbe hai na mazingira inajulikana kama_____ ( ) (a)biolojia (b)ikolojia (c)msawazo asilia. 8. Sumaku imeundwa kwa ___________ (a)chuma (b)mbao (c)kioo. ( ) 9. Ebola ni ugonjwa unaosababishwa na ________ ( ) (a)bakteria (b)virusi (c)viroboto wa nyani. 10. Yafuatayo ni magonjwa nyemelezi isipokuwa __________ ( ) (a)malaria (b)pumu (c)fangasi. 11. __________ ni sehemu ya kiume ya ua. (a)stameni (b)pistil (c)ovari. ( ) 12. Kirefu cha neno ARV ni __________ ( ) (a)anti-virus retro (b)anti-retro virus (c)anti-virus. 13. Kitu kipi kati ya hivi vifuatavyo kina umbo maalumu ___________ ( ) (a)soda (b)karatasi (c)gesi. 15. ____________ ni mashinbe ya kielekroniki yenye uwezo wa kupokea, kuchakata, kuhifadhi taarifa na kutoa matokeo ya kazi kwa haraka kulingana maelekezo. (a)tarakishi (b)simu (c)kibodi. ( ) 16. Tunafanya mazoezi na kucheza ili ___________ (a)tuwafurahishe walimu (b)tuendelee kusoma (c)tuimarishe afya ya mwili. ( ) 17. ____________ ni msaada utolewao kwa majeruhi wa ajali mbalimbali kabla ya kupelekwa hospitalini (a)huduma ya kwanza (b)ajali ya moto (c)kuzirai. ( ) 18. ______ ni kifaa kilichotengenezwa kwa kutumia vioo bapa viwili hutumika kuangalia kwenye vizuizi. (a)lenzi mbonyeo (b)periskopu (c)lenzi mbinuko. ( ) 19. Sehemu yam mea inayotumika kusanisi chakula ni __________ ( ) (a)mizizi (b)matawi (c)majani. 20. Ni mnyama yupi kati ya wafuatao hana uti wa mgongo __________ ( ) (a)nyoka (b)samaki (c)konokono. 21. Samaki huvuta hewa kwa kutumia ____________ ( ) (a)mdomo (b)mapezi (c)matamvua. 22. Mmea hupata mahitaji yake ya hewa kwa njia ya vitundu vidogovidogo vinavyoitwa ____________ (a)vakuoli (b)stomata (c)kloroplasti. ( ) 23. ___________ ni kufyonza maji, madini na virutubisho kutoka kwenye udongo. (a)shina (b)majani (c)mizizi. ( ) 24. Hali ya joto mwili wa amfibia hubadilika kulingana na halijoto ya mazingira. Tabia hii huitwa ________ (a)poikilothemia (b)homeothemia (c)haemoglobini. ( ) 25. ____________ ni kitendo cha kurudishwa kwa miale ya mwanga inapotua kwenye sura nyororo ya kung’aa. (a)kuakisiwa kwa mwanga (b)kupinda kwa mwanga (c)kutokea kwa kivuli. ( ) 26. _____ huanzia mdomoni kulekea tumboni na kuishia kwenye utumbo mwembamba. (a)kongosho (b)utumbo mpana (c)mmeng’enyo wa chakula. ( ) 27. Ipi ni njia mojawapo ya kuzuia vidonda vya tumbo. (a)kuwa na mawazo mengi (b)kula kwa wakati (c)kula vyakula vingi vyenye aside. ( ) 28. Ni ugonjwa gani kati ya magonjwa yafuatayo huathiri mfumo wa upumuaji_________ (a)pumu (b)malaria (c) pepopunda. ( ) 29. Ni njia ya usafirishaji wa nishati ya joto katika vimiminika kwa mfano katika maji _______ (a)mpitisho (b)mnururisho (c)msafara. ( ) 30. ___________ ni kitu chochote chenye uzito na ambacho huchukua nafasi. (a)mawasiliano (b)maada (c)nishati. ( ) 31. Toroli ni nyenzo daraja la ngapi ___________ (a)kwanza (b)pili (c)tatu. ( ) 32. Ni mfuko ulio katika mwili wa kiumbe ambao husaga chakula __________ ( ) (a)tumbo (b)kongosho (c)umio. 33. ___________ ni ugonjwa ambao hutokea kwenye chembe hai za mwili. ( ) (a)kisukari (b)saratani (c)kipindupindu. 34. Hali joto ya mwili wa mammalia haibadiliki kulingana na mabadiliko ya hali joto ya mazingira huitwa ____ (a)homeothemia (b)poikolothemia (c)themomita. ( ) 35. ___________ unaota mbegu lakini hautoi maua. ( ) (a)mchungwa (b)mvinje (c)mhindi. 36. Ni ute wenye neva za fahamu ulio ndani ya pingili za uti wa mgongo_____ ( ) (a)uti wa mgongo (b)ugwe mgongo (c)kongosho. 37. Ni sehemu zipi za ua zinazodondoka baada ya utungisho kukamilika ___________ (a)ovuli, chavua, ovary (b)sepali, ovary, stigma ( ) (c)sepali, petali, stigima, staili na stameni. 38. Zipi ni hatua za kuzaliana na kukua kwa mende___________ ( ) (a)yai buu mende (b)yai lava buu mende (c)yai tunutu mende. 39. Kazi kubwa ya bakteria na fangasi waishio kwenye udongo ni _________ ( ) (a)huzalisha mboji (b)huongeza hewa (c)usanisha chakula. 40. Ni sehemu ipi ya ua hubadilika kuwa tunda ___________ ( ) (a)ovari (b)ovuli (c)stigima. 41. Kitendo cha mmea kupoteza maji kupitia kwenye majani huitwa________ ( ) (a)osmosis (b)transpiresheni (c)fotosinthesisi.
JAZA NAFASI ZILIZO WAZI.
42. Maji + Mwanga + Umbijani + N = Fotosinthesisi. N inamaanisha nini ______________________ 43. Wanyama huvuta hewa ya oksijeni kutoka wapi _____________________________ 44. Aina za mabadiliko katika maada ni A__________________ B_________________ 45. UKIMWI ni ___________________________________________________________ 45. Alama hii ya kifaa cha umeme huitwa ______________________