You are on page 1of 5

OFISI YA RAIS

TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

MKOA WA KIGOMA

MTIHANI WA UTAMILIFU MKOA DARASA LA VI, NOVEMBA 2023

MUDA: SAA 1:30 SOMO: SAYANSI NA TEKNOLOJIA

SEHEMU A: CHAGUA HERUFI YA JIBU SAHIHI.


1. Hatua ya pili ya kufanya jaribio la kisayansi ni ___________________________
(A) Kubaini tatizo (B) Kutafsiri matokeo (C) Kuchambua data (D) Kubuni dhanio
2. _________ ni matokeo ya mpambano kati ya kinga ya mwili na kitu kingine kinapoingia ndani ya
mwili au kimegusa sehemu fulani ya mwili.
(A) Chavua (B) Vimelea (C) Mzio (D) Malengelenge
3. Kizingiti cha mgando wa maji ni nyuzi ______za farenhaiti.
(A) 100⁰C (B) 212⁰ (C) 32⁰ (D) 0⁰C
4. ___________ni sehemu zenye vyumba zinazotumika kuhifadhi vitu katika majokofu ,kabati,au
ukutani.
(A) Shubaka (B) Jokofu (C) Samani (D) Boksi
5. Bwawa la kuzalishia umeme kwa njia ya maji linalopatikana Iringa ni_________
(A) Mtera (B) Pangani (C) Hale (D) Nyumba ya Mungu
6. Chanzo cha vitamini ni pamoja na________ (A) Chapati (B) Embe (C) Ugali (D) Nyama
7._____ni taarifa iliyohifadhiwa katika jalada au kwenye kompyuta ______________
(A) Faili (B) Barua pepe (C) Intaneti (D) Ruta
8. Sehemu ya kuonesha namba za simu huitwa_________________
(A) Spika (B) Maikrofoni (C) Skrini (D) Risiva
9. Sauti iliyorejeshwa baada ya kukutana na kitu kigumu huitwa _______________
(A) Mrudio (B) Mwale akisi (C) Sauti (D) Mwangwi
10. kizio cha kani ya msukumo wa umeme ni ______
(A) Ampia (B) Volti (C) Ohm (D) Newton
11.Elimu inayoonesha uhusiano wa viumbe hai na mazingira yao huitwa ___________
(A) Austronomia (B) Unajimu (C) Ikolojia (D) Jiolojia
12. Moja wapo ya sifa ya taswira katika kioo bapa ni ____________________
(A) Ukubwa wa taswira ni sawa na ukubwa wa kiolwa (B) Hutokea mbele ya kioo
(C) Huwa imelala (D) Upande wa kushoto huwa kushoto
13.kitendo cha mmea kupoteza maji kwa njia ya mvuke kupitia kwenye majani huitwa ___________
(A) Respiresheni (B) Translokesheni (C) Osmosis (D) Transpiresheni
14. Mdudu yupi kwenye ukuaji hupitia metamofosisi kamili?
(A) Mende (B) Panzi (C) Nzi (D) Nzige
15. Sehemu ya kike ya Ua huwa mbegu ?
(A) Ovuli (B) Stigma (C) Ovari (D) Pistili
16._______________ni kiumbe kinachotokea baada ya muunganiko wa gametiume na gametiuke.
(A) Kijusi (B) Mtoto (C) Kiinitete (D) Zaigoti
17. Kwa kawaida kiwango cha msukumo wa damu kwa mtu mzima kinapaswa kuwa ___________
1105 160 90 120
(A) mmHg B) mmHg (C) mmHg (D) mmHg
70 90 60 80
18. Mtu mwenye tatizo la upungufu wa damu mwilini (anemia) anapaswa kula vyakula vyenye wingi
wa _______________
(A) Machungwa na wanga (B) Madini ya ayani (C) Fati (D) Protini
19. Kazi kubwa ya __________ni kupokea takamwili na kurekebisha halijoto mwilini.
(A) Hemoglobini (B) Plazima (C) Elektroliti (D) Chembe sahani
20. Mshipa pekee wa ateri wenye vali ni ________________
(A) Ateri ya palmoneri (B) Ateri ya renali (C) Aota (D) Ateri ya shingo
21. Jambo gani hupaswi kumfanyia mtu aliyeumwa na nyoka unapompa huduma za kwanza?
(A) Kumpeleka hospitali
(B) Kumwondolea wasiwasi
(C) Kumwondolea vitu vya kubana
(D) Kumpa dawa na kinywaji chenye kafeini
22._____________ni mrija mwembamba ambao husafirisha chakula kutoka kwenye majani kwenda
sehemu mbalimbali za mmea ili kuhifadhiwa.
(A) Zailemu (B) Vena (C) Floemu (D) Translokesheni
23.______________ni ujumbe unaotayarishwa kwa kutumia tarakilishi na kusambazwa kwa njia ya
intaneti.
(A) Google (B) Barua pepe (C) Mtandao jaribu (D) Nywila
24.Baadhi ya visakuzi vya mtandao ni _______________
(A) Safari, Instagram, WhatsApp (B) Intaneti, Explorer, Facebook
(C) Google, Youtube, Safari, TigoPesa (D) Google, Chrome, Safari, Mozilla Firefox
25. Faida mojawapo ya programu jedwali ni ________________
(A) Kuandika nukuu (B) Kutengeneza majarida
(C) Kuandaa matokeo ya mitihani (D) Kuandaa mitihani
26.____________ni kitendo cha maji kusafiri kutoka myeyuko hafifu kwenda myeyuko mzito.
(A) Fototropizimu (B) Osmosis (C) Difyusheni (D) Fotosynthesis
27._________________ni sehemu ya mtambo wa kuzalisha gesivunde ambayo huhifadhi malighafi
ya kutengeneza gesi.
(A) Silo (B) Neli (C) Mpare (D) Daijesta
28. Kundi la wanyama ambao halijoto ya miili yao haibadiliki kulingana na mazingira kisayansi huitwa
_______________
(A) Poikilothemia (B) mamalia (C) homoithemia (D) Protonomia
29. Mshipa upi wa damu huondoa damu chafu kwenye figo na kuirudisha kwenye vena kava?
(A) Aota (B) Ateri (C) Vena ya renali (D) Ateri ya renali
30. Mrija unaosafirisha mkojo toka kwenye figo hadi kwenye kibofu cha mkojo ni___________
(A) Urethra (B) Mrija wa manii (C) Ovari (D) Ureta
31. Ukibadili sentigredi 90⁰C itakuwa ni. Sawa na nyuzi ____________za farenhaiti.
(A) 102⁰ (B) 194⁰ (C) 172⁰C (D) 112⁰F
32. Mbu aitwaye _____hueneza ugonjwa wa malale.
(A) Mbung'o (B) Adesi (C) Anofelesi (D) Kyuleksi
33. Rangi ya fedha kwenye themosi hupunguza joto lisipotee kwa njia za___________
(A) Msafara (B) Mpitisho (C) Mnunurisho (D) Ombwe
34.__________________ni mashine rahisi ambayo hutumika kutanua mbao ,kupasua kuni, Mfano
patasi na shoka. (A) Roda (B) Wenzo (C) Gurudumu kepi (D) Kabari
35. Egemeo likiwa kati ya Mzigo na Jitihada itakuwa nyenzo daraja la ngapi ?
(A) kwanza (B) Tatu (C) pili (D) yote
36. Namba au neno la siri au kishazi cha viwambo inayotumika kuthibitisha utambulisho wako katika
kutumia huduma fulani mfano tarakilishi au simu huitwa__________________
(A) Pau (B) Tahajia (C) Fonti (D) Nywila
37.______________ hupokea na kuchakata kazi zote zinazoingia kwenye tarakilishi.
(A) Kiteuzi (B) Kichakato kikuu (C) Monita (D) Kibodi
38. Wavulana hubalehe kati ya miaka ______hadi ________
(A) 12-13 (B) 15 -16 (C) 11-12 (D) 8 -12
39. Mshipa upi huingiza damu safi kwenye moyo?
(A) Ateri ya mapafu (B) Vena ya palmonari (C) Vena kava (D) Aota
40. Ugonjwa wa kaswende husababishwa na bakteria waitwao___________________
(A) Neiseria (B) Himofilasi (C) Treponema (D) Klamidia

SEHEMU B: JIBU MASWALI YAFUATAYO KWA KUZINGATIA SWALI LILIVYO ULIZWA.

41. Andika kanuni ya kutafuta jumla ya data hizi kwenye programu jedwali =A6+B6+C6+D6+E6+F6

42. Ni kiasi gani cha mkondo wa umeme kitapita kwenye waya wenye ukinzani wa ohm 0.4 na
volteji 20

43.Taja mifano ya elementi mbili zinazounda virutubisho vikuu ( a) ______________ (b) __________

44. Tafuta ufanisi wa mashine iwapo roda ina magurudumu 5 na jitihada ya kuinua mzigo wenye
kg 48 ni Kg12

45. Musa alitumia Newton 100 kufanya kazi ya kuinua chuma kwa Jouli 150 je, Chuma hicho
kiliinuliwa kwa umbali gani?
MAJIBU SAYANSI NA TEKNOLOJIA DARASA LA VI

1. D 25. C
2. C 26. B
3. C 27. A
4. A 28. C
5. A 29. C
6. B 30. D
7. A 31. B
8. C 32. A
9. D 33. C
10. B 34. D
11. C 35. A
12. A 36. D
13. D 37. B
14. C 38. A
15. A 39. B
16. D 40. C
17. D 41. =SUM (A6 : F6)
18. B 42. Ampia 50
19. B 43. (a) Naitrojeni
20. A (b) Fosforasi
21. D (c) Potasiamu
22. C 44. Ufanisi ni 80%
23. B 45. Chuma kiliinuliwa umbali wa mita 1. 5
24. D

You might also like