You are on page 1of 3

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAISI- TAMISEMI


TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
EDUCATIONAL CONSULTATIONAL CONSULTATION AND MATERIALS FOR
PRIMARY AND SECONDARYSCHOOLS (ECOMAPS)
CONTACT: 0759820072 CONTACT: 0757826309

MTIHANI WA MWISHO WA MUHULA WA PILI- DARASA LA VI


SOMO:STADI ZA KAZI
JINA LWA MWANAFUNZI ______________TAREHE __DISEMBA; 2020
SEHEMU A: CHAGUA JIBU SAHIHI
1. Kwanini inashauriwa kutenganisha nguo kulingana na rangi kabla ya kufua? ____
a) Ili zifuliwe vizuri b) ili kuepuka kuchujiana c) ili zifuliwe haraka d) ili
ziwekwe alama
2. Kuna aina ngapi za pasi? ___________a) Nne b) tano c) tatu d) mbili
3. Zifuatazo ni sababu za kunyoosha nguo isipokuwa______a) Kuua wadudu b)
kuondoa mikunjo c) kuzikausha vizuri nguo d) kuwa pendezesha watu wengine
4. Kwanini inashauriwa nguo za rangi zipigwe pasi ndani tu? _______a) Ili zitoe
mikunjo kisawasawa b) ili kuepuka kupauka c) ili zisichanike d) ili zisichujianae
5. Tunaweza kusafisha pasi kwa kutumia vitu vifuatavyo isipokuwa __________
a) Makaratasi b) majiyalimau c) magadi soda d) mafutayataa
6. Ni mdhara gani unaweza pata ikiwa utavaa nguo ambazo hazijakauka vizuri?___
a) Utanenepa kupita kiasi b) unaweza pata magonjwa c) unaweza kuonekana
vizuri d) unaweza kupendeza
7. Maji yaliyochanganywa na chumvi husaidia kuondoa madoa yenye __a) Asili ya
matope b) vyakula c) kemikali kama wino d) asili ya wanyama kama damu
8. Ni nguo zipi huhitaji joto kali wakati wa kupigwa pasi? _________a) Polista na
kitani b) nailoni na pamba c) kitani na nailoni d) pamba na kitani
9. Viatu vyenye kisigino kirefu huweza kusababisha _______a) Maumivu ya misuli
b) maumivu ya magoti c) maumivu ya kichwa d) maumivu ya tumbo
10. Uvaaji wa soksi za pamba husaidia _______a) Kunyonya jasho la miguu b)
kutembea vizuri c) kupunguza joto la miguu d) kuzuia kuteleza
11. Ni aina gani ya pasi huweza kuonesha kiasi cha joto? ______________
a) Pasi ya mkaa b) pasi ya umeme c)pasi ya mafuta ya taa d) pasi yoyote
12. Kwanini hairuhusiwi kuweka viatu vya ngozi ndani ya maji? ____________
a) Vinaweza kupauka b) vitaharibika mwonekano wake c) vitayeyuka kwa
urahisi d) vitatoa harufu mbaya
13. Kuna umuhimu gani wa kuzima pasi baada ya kutumia? _______________

Prepared by ECOMAPS Contact us via 0759820072


a) Kuepuka kuunguza nguo b) kuzuia kutu kwenye uso wa pasi c) kuiwezesha
kudumu kwa muda mrefu d) kuepuka madhara na gharama.
14. Ipi kati ya taka zifuatazo haiwezi kudhibitiwa kwa njia ya urejelezaji?_________
a) Chuma chakavu b) karatasi c) bati chakavu d) mabaki ya vyakula
15. Taka zifuatazo zinafaa kwa mbolea isipokuwa______a) Vinyesi vya wanyama
b) maganda ya matunda c) majani ya miti d) vifuu vya nazi
16. Zifuatazo ni taka zinazofaa kutumika tena isipokuwa _____________
a) Matairi na vifuu vya nazi b) mifuko ya salfeti na vyuma chakavu c) chupa
za vipodozi na makopo ya viuatilifu d) majani makavu na karatasi
zilizotumika
17. Lipi kati ya matunda yafuatayo haliwezi kutumika kutengenezea juisi? _____
a) Embe b) nanasi c) chungwa d) nyanya
18. Yafuatayo ni mahitaji ya kuandaa kababu isipokuwa________
a) Nyama b) mafuta c) mayai d) hamira
19. Kipi kati ya vyakula vifuatavyo kinafaa kufungasha kwaajili ya safari? _______
a) Ugali na mchuzi wa samaki b) wali na maharage ya nazi c) viazi na samaki
wa kukaangwa d) kande zilizoungwa kwa nazi
20. ___huupatia mwili virutubisho vinavyo saidia mwili kujikinga dhidi ya magonjwa.
a) Matunda b) mayai c) nyama d) ugali
21. Uchongaji wa motifu unahitaji kuzingatia sifa zifuatazo isipokuwa _______
a) Usafi wa uchongaji b) usahihi wa umbo c) ukali wa vichongeo d) umbo
liwe na vijisehemu vidogovidogo
SEHEMU B: OANISHA KUNDI A NA KUNDI B
KUNDI A KUNDI B
22. Jumla ya mambo yote yanayo mzunguka A. Mategemezo
binadamu B. Baragumu na tarumbeta
23. Husaidia mboga zinazokwea zisianguke C. Mboji
kwenye udongo D. Mazingira
24. Kuondoa matawi na majani yasiyohitajika E. Pogolea
25. Vitamini C F. MATUNDA
26. Sehemu ya kusia mbegu kabla ya kuzipanda G. Marimba na vijiti
27. Ala zakupuliza H. Kitalu
28. Mchanganyiko wa vitu hai vilivyooza ambao I. Samadi
hutumika kama mbolea J. Nishati
SEHEMU C: JAZA NAFASI WAZI
29. Unawezaje kuondoa madoa yatokanayo na vyakula kwenye nguo zako? _____
30. Taja aina mbili za matuta ____________na ______________
31. Nini faida ya maua mazingira ya nyumbani? Taja faida moja _____________
32. __________ni ala ya nyuzi inayotoa sauti ya kuimbika.
33. Nini maana ya ala zamuziki? _________________________________
34. Nini maana ya ngonjera? ______________________________
35. Ngonjera hughaniwa na watu wangapi? _________________________
36. Ufundi wa kisanaa wakunakili picha, maumbo,alama au michoro katika wingi na
mfanano huitwa ________________
37. _____Ni kurekebisha maeneo mbalimbali ya picha kwa kusawazisha na kuhifadhi.

Prepared by ECOMAPS Contact us via 0759820072


38. Kuna hatua _____________wakati wa kusuka mkeka.
39. Taja aina mbili za wateja____________na _____________
40. Taja kifungashio kinachoweza kufungashia matunda _______________
41. Nini maana ya ujasiriamali? ____________________
42. Taja sifa mbili za mjasiriamali _____________na _______________
43. Chanzo kikuu cha mapato ya serikali ni___________________

Chora vitu vifuatavyo


44. Umbo la pembe tatu sawa
45. Ua

Prepared by ECOMAPS Contact us via 0759820072

You might also like