You are on page 1of 4

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

HALMASHAURI YA MANISPAA YA UBUNGO

MTIHANI WA UTAMILIFU KWA DARASA LA VII - 2023

01 KISWAHILI

MUDA: SAA 1:40


MAELEKEZO
1. Karatasi hii ina sehemu A,B, C na D zenye jumla ya maswali arobaini na tano (45)
2. Jibu maswali yote katika kila sehemu.
3. Soma maelekezo yote yaliyoko katika karatasi maalum ya kujibia (OMR)
4. Jaza taarifa zote katika fomu ya OMR .
5. Weka kivuli katika kila tarakimu ya namba yako ya mtihani kwenye nafasi husika
katika fomu ya OMR.
6. Weka kivuli katika herufi ya jibu sahihi kwa kila swali katika karatasi yako ya
kujibia (OMR) kwa swali la 1-40. Kwa mfano kama jibu sahihi A weka kivuli
kama ifuatavyo:-

[ A ] [ B ] [ C ] [ D ] [ E ]

7. Ukigundua kuwa herufi uliyowekea kivuli si jibu sahihi, futa kivuli hicho kwa
kutumia kifutio safi kabla ya kuweka kivuli katika herufi mpya.
8. Tumia penseli ya HB tu katika kujibu swali la 1 - 40 na andika kwa kutumia
kalamu ya wino wa bluu au mweusi kwa swali la 41 - 45.
9. Simu za mkononi haziruhusiwi katika chumba cha mtihani.

Ukurasa wa 1 kati ya 4
SEHEMU A:
Sikiliza kwa makini hadithi utakayosomewa na msimamizi, kisha jibu
swali la 1 - 5 kwa kuchagua jibu lililo sahihi kisha weka kivuli cha
herufi hiyo katika karatasi ya OMR.
1. Mtutu alipenda kufanya nini?
A. Kucheza na kupika B. Kuwinda na kupika C. Kucheza na kukimbia
D. Kucheza na kuwinda E. Kucheza na kusoma
2. Mtutu alimkuta Suli akifanya nini?
A. akisoma kitabu B. akiandika C. akiangalia picha D. akiwaza sana E. akinunua miwani
3. Mtutu aliwaza kitu gani kinaweza kumsaidia kusoma?
A. Kucheza sana B. kuwinda ndege C. kuvaa miwani D. kuvua miwani E. uvivu sana
4. Watoto wenzake waligundua nini baada ya kumsogelea Mtutu?
A. anasoma vizuri B. amevaa miwani C. amependeza sana D. amegeuza kitabu E. amelia sana
5. Hadithi hii inatufundisha nini?
A. Kusoma kwa bidii B. Kuvaa miwani C. Kucheza kwa bidii
D. Kuwinda kwa bidii E. Kuwa mvivu
SEHEMU B: SARUFI.
Chagua herufi ya jibu sahihi kisha weka kivuli cha herufi hiyo katika karatasi ya OMR.
6. Juu mboga, katikati kuni, chini chakula. Kiteguo cha kitendawili hiki ni ____
A. Maji B. Ufagio C. Samaki D. Muhogo E. Pera
7. Nahau ipi yenye maana ya “Kumaliza msiba”
A. Lala tanga B. Anua tanga C. endelea na tanga D. kulia sana E. kuhuzunika sana
8. Baba yetu jana alipiga maji sana. “Kupiga maji” ni aina gani ya lugha ya kifasihi?
A. Nahau B. Methali C. Msemo D. Insha E. Tenzi
9. Wao ni wakarimu sana. Neno “wao” katika sentensi hii liko katika nafsi gani?
A. Nafsi ya pili wingi B. Nafsi ya tatu wingi C. Nafsi ya kwanza umoja D.Nafsi tulivu E.Nafsi ya tatu
10. Mwalimu alisema “nitafundisha masomo yote” Hiyo ni aina gani ya kauli kati ya zifuatazo?
A. Tata B. Mazoea C. Halisi D. Taarifa E. Kutenda
11. Wote walijibu, “Tunapenda kula matunda”. Kauli taarifa ya sentensi hii ni ipi kati ya zifuatazo?
A. Wote walijibu kuwa, tunapenda kula matunda B. Wote walijibu kwamba, hatupendi kula matunda.
C. Wote walijibu kuwa wanapenda kula matunda D. Wote walijibu kuwa, wanakula matunda
E. Wote walijibu kuwa, wanapenda kula matunda kila siku
12. Nahau isemayo, “Kaza kamba” Ina maana ipi kati ya zifuatazo?
A. Kaza buti B. Kaza mkanda C. Ongeza akili D. Ongeza kamba E. Ongeza bidii
13. “Sijui kwanini ameamua kuolewa na kijana fukara kama yule”, Shangazi yake alijiuliza. Methali ipi
kati ya zifuatazo ina maana sawa na kauli hii?
A. Nyani haoni kundule B. habadi kibindoni C. Akufaaye kwa dhiki
D. Majuto ni mjukuu E. Kipendacho roho hula nyama mbichi
14. Mniwie radhi kwa kutamka haya. Nahau ipi ingetumika badala ya sentensi hiyo?
A. Shauku B. Piga chuku C. anika juani D. Ashakumu si matusi E. Mdomo mchafu
15. Mzee Jimbi alionekana kuwa na hekima na busara. Hivyo alitawazwa kuwa mfalme wa kijiji cha
Kaungeni, Msemo “alitawazwa” una maana gani kati ya hizi zifuatazo?
A. Aliapishwa B. alitangazwa C. alichaguliwa D. aliteuliwa E. alitenguliwa
16. Juisi hii haikunyweka kwa kuwa inasukari nyingi mno. Hii ni aina gani ya kauli kati ya zifuatazo?
A. Kutenda B. Kutendeka C. Kutendwa D. Kutendea E. Kutendana
17. “Kibatari” ni jibu la kitendawili kipi kati ya hivi vifuatavyo?
A. Napigwa faini kosa silijui B. Mwavuli wa mwitu una nguzo moja C. Amefika kabla
mjumbe hajafika D. Jini mnywa damu haangazi bila damu E. Hakuna adui anayeweza kumsogelea
18. Mti upi kati ya ifuatayo haulandani na mingine? Mchungwa, Mpera, Mchenza, Mkaratusi na Mparachichi.
A. Mpera B. Mparachichi C. Mkaratusi D. Mchenza E. Mchungwa
19. Watoto wameimba vizuri. Kipi ni kiambishi cha nafsi katika sentensi hii?
A. wa B. me C. nyi D. mba E. si
20. Hereni, sahani na bakuli ni nomino ambazo zipo katika ngeli ya?
A. li - ya B. u - zi C. zi - i D. i - zi E. ki - vi
21. Shaibu wengi huwa na busara na hekima hivyo hutumika kushauri vijana kuhusu maisha.
Neno “Shaibu” linafanana na neno lipi kati ya haya yafuatayo?
A. Ajuza B. Buda C. Mkongwe D. Bibi kizee E. Mchungaji
22. Mwalimu Mbesule alikuwa anafundisha darasani. “alikuwa” ni aina gani ya kitenzi?
A. Kikuu B. Tegemezi C. Kipole D. Kishirikishi E. Kisaidizi
23. Baba amedunduliza hadi amejenga nyumba, nini maana ya nahau “dunduliza”.
A. Kuweka kwa wingi B. Kuweka kidogo kidogo C. Kudundadunda E. Weka akiba
24. Bakari alitegewa kitendawili na babu yake na akategua kwa kusema “Mwangwi” Kitendawili hicho ni kipi?
A. Huku paa na kule paa B. Huko ng’o na huku ng’o C. Jinamizi laniita lakini silioni
D. Pikipiki E. Kila niendako ananifata
25. Neno “Ntamuti” lina silabi ngapi?
A. Tatu B. Mbili C. Nne D. Saba E. Tano
26. “Mandonga hakupigwa na dada yake” Sentensi hii ipo katika hali gani?
A. Uyakinishi B. Ukanushi C. Masharti D. Matarajio E. Mazoea
27. Sikitu hutandika kitanda chake vizuri kila anapoamka. Mdogo wake hufanya kinyume chake,
Je, mdogo wake hufanya nini?
A. hutanda B. hutundika C. hutenda D. hutandua E. hutumbuiza
28. Wingi wa sentensi isemayo “Bibi yangu anapenda kulima” ni upi?
A. Bibi zetu anapenda kulima B. Bibi zake wanapenda kulima C. Bibi zetu wanapenda kulima
D. Bibi yangu wanapenda kulima E. Bibi yetu anapenda kulima
29. Tunaimba kabla ya kuondoka shuleni. Katika neno tunaimba silabi inayoonesha wakati ni ipi?
A. tu B. -a C. -imb- D. -mb- E. -na-
30. Ni neno lipi linakamilisha sentensi hii kwa usahihi. Mwenyekiti__ hoja za wajumbe katika mkutano wa mtaa.
A. aliwakisha B. aliwakilisha C. aliwasilisha D. alikasirisha E. aliadhimisha
31. Wingi wa sentensi “Mche wa mnazi umestawi vizuri” ni upi kati ya sentensi zifuatazo?
A. Mche wa minazi umestawi vizuri B. Miche ya minazi imestawi vizuri C. Miche ya mnazi umestawi vizuri
D. Mche wa minazi imestawi vizuri E. Miche ya minanzi imestawi vizuri
32. Pikipiki ya Juma ilitumbukia bwawani taratibu. Neno lipi kati ya haya yafuatayo limetumika kama kielezi?
A. Taratibu B. Juma C. ilitumbukia D. pikipiki E. -ya-
33. Azania alishughulikia ndoa ya Kulinyangwa kinagaubaga hadi ikafanikiwa. Je, Azania alikuwa nani?
A. Sonara B. Mwashi C. Polisi D. Mshenga E. Hakimu
34. Neno lipi kati ya haya yafuatayo lina maana sawa na neno irabu?
A. Konsonanti B. Silabi C. Vokali D. Sauti E. Herufi
35. “IASRHA” ni herufi zilizochanganywa ambazo zinaweza kuunda neno lipi kati ya haya yafuatayo?
A. ARUSHA B. RUSHA C. ASHURA D. RAHA E. ISHARA
SEHEMU C:
Kwa kutumia maneno yaliyomo kwenye kisanduku, jibu swali la 36 - 40 kwa kuweka
kivuli katika herufi ya jibu lililo sahihi katika fomu yako ya kujibia ili kukamilisha
tangazo lifuatalo.

A. Saa 1:00 asubuhi, B. +25522863333, C. KUKATIKA KWA MAJI


D. LIMETOLEWA NA MENEJA WA DAWASCO E. MAMLAKA YA MAJI
36. ___________________________
37. ____________________________ Wilaya ya Ubungo inapenda kuwatangazia wateja wake wote
kuwa kutakuwa na tatizo la kukatika kwa maji tarehe 22- 03 - 2023 siku ya Jumamosi kuanzia
(38.) __________hadi saa 11: 00 jioni. Sababu ya kukatika kwa maji ni matengenezo makubwa
katika bomba kubwa linalotoa maji Ruvu. Maeneo yatakayokosa maji ni Kiluvya, Luguruni, Magarisaba,
Mbezi Luis pamoja na Kimara.
Mamlaka inaomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza.
(39.) _____________________
Wasiliana nasi kupitia
(40.) _____________________
SEHEMU D:
SOMA SHAIRI LIFUATALO, KISHA JIBU MASWALI YAFUATAYO.
Mwanangu sogea hapa, keti chini nakuasa,
Wosia huu nakupa, usije pata mikasa,
Dua hii si kapa, kuna mengi yanatesa,
Mwanangu hii dunia, kweli usitakabari.

Mosi, kiburi sitaki, hadaa hii dunia,


Kama upole hutaki, hekima kusukumia,
Utapata ya Samaki, machozi ninakwambia,
Mwanangu hii dunia, kweli usitakabari.

Pili, dharau ni mwiko, heshima kwa kila mtu,


Binadamu ndugu zako, kila mara kwako utu,
Wakubwa ni tunu kwako, dharau kwako si kitu,
Mwanangu hii dunia, kweli usitakabari.

MASWALI.
41. Taja vina vya kati katika ubeti wa tatu. __________________________
42. Katika ubeti wa kwanza mshororo wa tatu, mwandishi anazungumzia kitu gani? ______________
43. Neno “hadaa” kama lilivyotumika katika ubeti wa pili lina maana gani? ______________________
44. Mstari wa pili katika ubeti wa kwanza una mizani mingapi? ______________________________
45. Andika kichwa cha habari kinachofaa kwa shairi hili. ____________________________________

You might also like