You are on page 1of 4

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
SHULE ZA AWALI NA MSINGI UWATA
MTIHANI WA UTAMILIFU DARASA LA SABA
SOMO: KISWAHILI

MUDA: SAA 1:00 JUNE 2019

MAELEZO
1. Mtihani huu una jumla ya maswali arobaini na tano (45).
2. Jibu maswali yote katika kila sehemu.
3. Soma maelekezo yote yaliyoko katika karatasi maalum ya kujibia (OMR).
4. Jaza taarifa zote katika fomu ya OMR na ukurasa wenye swali la 41 hadi 45
katika karatasi ya maswali
5. Weka Kivuli katika kila tarakimu ya namba yako ya mtihani kwenye nafasi
husika katika fomu ya OMR
6. Weka kivuli kwenye herufi ya jibu lililo sahihi kwa swali 1 -40.
Kwa mfano kama jibu ni A weka kivuli kama ifuatavyo

7. Ukigundua kuwa herufi uliyowekea kivuli si jibu sahihi futa kivuli hicho kwa
umakini kwa kutumia kifutio safi kabla ya kuweka kivuli katika herufi mpya.
8. Tumia penseli ya HB tu katika kujibu swali la 1 hadi 40; na kalamu ya bluu au
nyeusi kwa swali la 41 hadi 45
9. Simu za mkononi, vikokotozi na vitu visivyoruhusiwa havitakiwi ndani ya
chumba mtihani.
SEHEMU A: SARUFI
Chagua jibu sahihi kutoka kwenye machaguo kisha siliba herufi ya jibu hilo kwenye
karatasi ya kujibia uliyopewa
1. Mwakipesile ni kijana mcheshi sana. Neno mcheshi ni aina gani ya neno?
A. Kivimushi B. Kiunganishi C. Kielezi D. Kitenzi E. Nomino [ ]
2. Mayai mabovu yametupwa jalalani. Sentensi hii ipo katika kauli gani?
A. Kutendeka B. Kutendwa C. Kutenda D. Kutendea E. Kutendewa [ ]
3. Ujasiri wake umemfanya afanikiwe katika maisha. Neno ujasiri katika sentensi hii limetumika
kama:
A. Kivimushi B. Kiunganishi C. Kielezi D. Kitenzi E. Nomino [ ]
4. Neno lipi linakamilisha sentensi hii kwa usahihi “penye nia________njia”.
A. Kunalo B. Panako C. Pana D. Mna E. Kuna [ ]
5. Neno bunge lipo katika ngeli ipi kati ya hizi?
A. I-ZI B. U-ZI C. LI-YA D. KI-VI E. U-YA [ ]
6. Neno lipi kati ya maneno yafuatayo halilandani na mengine?
A. Panzi B. Nzige C. Sisimizi D. Bundi E. Mende [ ]
7. _________ ya kusoma kwa bidii, hakufaulu mtihani wake.
A. Ingawa B. Endapo C. Badala D. Licha E. Walau [ ]
8. Neno lipi kati ya haya yafuatayo lina maana sawa na neno faragha?
A. Waziwazi B. Tupu C. Siri D. Shauku E. Aibu [ ]
9. Sisi sote ni watoto wazuri. Sentensi hii ipo katika nafsi gani?
A. Ya kwanza umoja C. Ya kwanza wingi E. Ya tatu umoja [ ]
B. Ya pili wingi D. Ya tatu wingi
10. Neno KINDUMBWENDUMBWE lina silabi ngapi?
A. Kumi na mbili B. Nane C. Tano D. Sita E. Tisa [ ]
11. Sentensi ipi kati ya hizi zifuatazo ipo sahihi?
A. Zimeibiwa Ng’ombe zetu D. Ng’ombe wetu zimeibiwa [ ]
B. Ng’ombe zetu zimeibiwa E. Ng’ombe wetu wameibwa
C. Ng’ombe yetu imeibiwa
12. Badili kauli hii iwe katika kauli halisi. Alisema kuwa hajisikii vizuri.
A. Hajisikii vizuri tena C. Najisikia vizuri E. Jisikie vizuri [ ]
B. “Sijisikii vizuri” D. Sikuwa najisikia vizuri
13. Ili tufaulu mtihani __________kujifunza kwa bidii.
A. Ni budi C. Ipo budi E. Pawe na budi [ ]
B. Hatuna budi D. Sina shaka
14. Kinyume cha neno nadharia ni:
A. Vitendo B. Ukweli C. Uongo D. Ubishi E. Kiburi [ ]
15. Mtaka cha uvunguni sharti ainame. Neno lililopigiwa mstari ni aina gani ya
neno.
A. Nomino B. Kihisishi C. Kitenzi D. Kielezi E. Kivumishi [ ]
16. Mama yupo lakini baba hayupo. Hii ni aina gani ya sentensi?
A. Shurutia C. Sahili E. Kinzani [ ]
B. Changamano D. Ambatano
17. Maria atakuwa anasali. Sentensi hii ipo katika wakati gani?
A. Ujao C. Uliopo mazoea E. Uliopo unaoendelea [ ]
B. Ujao unaoendelea D. Uliopita timilifu
18. Hali ya kuwa na mali nyingi au kipato kikubwa hujulikana kama:
A. Ukwasi B. Ukata C. Umasikini D. Ufedhuli E. Ufukara [ ]
19. Jembe la kulimia linalokokotwa na ng’ombe hujulikana kama:
A. Maksai B. Fahali C. Pilau D. Pirau E. Plau [ ]
20. Wingi wa neno ulimi ni:
A. Limi B. Milimi C. Malimi D. Ndimi E. Njimi [ ]

SEHEMU B: LUGHA YA KIFASIHI


21. Tegua kitendawili “ kamba yangu ndefu lakini haiwezi kufunga mizigo”:
A. Katani B. Barabara C. Jongoo D. Nanasi E. Karatasi [ ]
22. Nahau “ana ulimi wa panga” maana yake ni:
A. Ana maneno matamu C. Ana maneo makali E. Anasengenya [ ]
B. Anaongea sana D. Ni mwepesi kusamehe
23. Malizia mehali hii “lila na fila________”
A. Havitengani C. Havitangamani E. Havipotei [ ]
B. Haviungani D. Haviachani.
24. Kiota changu nimekizungushia boma la nyasi. Jibu la kitendawili hiki ni:
A. Ulimi na meno B. Nanasi C. Macho D. Mzinga wa nyuki E. Siafu [ ]
25. “ Inatupasa kuwapatia malezi bora watoto wetu angali wakiwa wadogo kabla hawajaanza
kuharibika wakiwa wakubwa”. Methali ipi kati ya hizi zifuatazo ina maana sawa na sentensi hii?
A. Samaki mkunje angali mbichi D. Lila na fila havitangamani [ ]
B. Mgaa gaa na upwa hali wali mkavu E. Baada ya dhiki faraja
C. Usiache mbachao kwa msala upitao
26. Kamilisha methali ifuatayo: dunia hadaa ulimwengu_________:
A. Mbaya B. Balaa C. Mzuri D. Shujaa E. Mchungu [ ]
27. Nini maana ya nahau kupiga uvivu?
A. Kufanya kazi kwa bidii C. Kutamani kitu E. Kwenda na wakati
B. Kukaa bila kazi D. Kufanya kazi nyingi [ ]
28. Kamilisha methali hii yaliyopita si ndwele___________
A. Tuachane nayo C. Tukumbuke ya sasa E. Tubaki hapa hapa [ ]
B. Twende na yaliyopo D. Tugange yajayo
29. Methali ipi kati ya hizi zifuatazo ina maana sawa na methali isemayo: Mkuki
kwa nguruwe kwa binadamu mchungu?
A. Hucheka kovu asiyefikwa na jeraha D. Pilipili usiyoila yakuwashia nini?
B. Nazi mbovu harabu ya nzima E. Penye miti hakuna wajenzi [ ]
C. Zimwi likujualo halikuli likakwisha
30. Nahau kaa chonjo ina maana gani?
A. Kuwa tayari C. Kimbia E. Kaa kimya [ ]
B. Kaa na silaha D. Jisalimishe

SEHEMU C: USHAIRI
Soma kwa makini shairi lifuatalo kisha jibu maswali yanayofuata
Nawauliza wahenga, wa bara na visiwani,
Na ndugu zangu waganga, nitoeni mashakani,
Hizi beti nazitunga, ili nipate amani,
Ni kipi kilicho bora, mchana au usiku.

Mchana unatufaa, kazini kujiendea,


Tusije tukafa njaa,watoto tuweze lea,
Usiku nao wafaa, tuweze kusinzia,
Ni kipi kilicho bora, mchana au usiku.
MASWALI
31. Shairi hili lina beti ngapi?
A. Nane B. Nne C. Sita D. Mbili E. Tatu [ ]
32. Neno wahenga kama lilivyotumika katika ubeti wa kwanza wa shairi hili lina maana gani?
A. Watu wa pwani C. Watoto E. Waganga [ ]
B. Watu wa bara D. Watu wa zamani
33. Mstari uliokolezwa wino katika kila ubeti wa shairi hili hujulikana kama:
A. Mshororo C. Ubeti E. Kibwagizo [ ]
B. Vina D. Mkarara
34. Vina vya kati na mwisho katika ubeti wa pili wa shairi hili ni:
A. a na a C. aa na ia E. nga na ni [ ]
B. aa na ea D. a na ea
35. Mshairi anasema mchana unatufaa kwa sababu:
A. Ndiyo muda wa kufanya kazi D. Ndiyo muda wa kusinzia
B. Ndiyo muda wa kupumzika E. Ndiyo muda wa kushinda njaa [ ]
C. Ndiyo muda wa kulea watoto
36. Kila ubeti wa shairi hili una jumla ya mizani ngapi?
A. Nne C. Kumi na sita E. Kumi na nne [ ]
B. Kumi na mbili D. Nane
SEHEMU D: UTUNGAJI
Pangilia sentensi zifuatazo kwa kuzipa herufi A,B,C na D ili ziweze kuwa katika
mtiririko wenye mantiki
37. Alipotazama upande mwingine akaona nyanya zimezagaa chini pembezoni mwa barabara [ ]
38. Alipoangalia katikati ya barabara aliona mtu amelala chini [ ]
39. Siku ya Jumatatu Bahati aliamka mapema na kwenda shuleni. [ ]
40. Njiani alikuta ajali ya mtu aliyeanguka na baiskeli. [ ]

SEHEMU E: UFAHAMU
Soma kwa makini kifungu cha habari kifuatacho kisha jibu maswali yanayofuata
Miongoni mwa mashujaa ambao hawawezi kusahaulika katika historia ya nchi yetu ni Mtwa
Mkwawa. Huyu alikuwa kiongozi wa kabila la wahehe mkoani Iringa. Baba yake Mkwawa aliitwa
Munyigumba. Mkwawa aliongoza mapambano makali dhidi ya wajerumani kuanzia mwaka 1891 hadi
mwaka 1898. Alifanikiwa kuwaua wajerumani wengi akiwemo aliyekuwa kamanda wa kikosi cha
Kijerumani aliyejulikana kwa jina la Emili Zelwiski. Mara baada ya kuuawa kwa kamanda Zelwiski
mnamo mwaka 1891, Gavana wa Ujerumani alimuaru wanajeshi wake wamtafute Mkwawa kwa nguvu
zote hadi wamkamate. Baada ya Mkwawa kugundua kuwa amezidiwa sana na Wajerumani akaamua
kujiua kwa kujipiga risasi yeye na mlinzi wake kwa kuhofia asikamatwe na Wajerumani.

MASWALI
41. Kwa mujibu wa kifungu hiki cha habari, ni shujaa gani hawezi kusahaulika kirahisi katika historia
ya nchi yetu?_________________________
42. Mkwawa alipambana na wajerumani kwa muda wa miaka mingapi?____________________
43. Kiongozi wa Kijerumani aliyeuliwa na jeshi la Mkwawa mwaka 1891 alikuwa nani?___________
44. Baba yake mkwawa aliitwa nani?_________________________________________
45. Kwanini Mkwawa aliamua kujiamua kujiua mwenyewe?_____________________________

You might also like