You are on page 1of 3

OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOGIA


KATA YA MBEZI, MTIHANI WA UTAMILIFU DARASA LA NNE
MAARIFA YA JAMII
MUDA:1:30 JUMATANO SEPTEMBER 16, 2020
JINA_____________________________________SHULE_________________________
SEHEMU A: MACHAGUO

1.Chagua herufi ya jibu sahihi na uiandike kwenye nafasi ya mabano yaliyowekwa kila
swali
i.Mazingira huundwa na _________ ( )
A. wanyama na mimea B. mawe na miti C. viumbe hai na visivyo hai D. vitu
vilivyokufa
ii. Lifuatalo ni tabaka linalozuia mionzi ya jua isifike moja kwa moja kwenye uso wa
dunia ________ ( )
A. anga B. uchafuzi C. tabaka la ozoni D. joto la ulimwengu
iii. Zifuatazo ni shughuli zinazoharibu mazingira ISIPOKUWA __________ ( )
A. mbinu duni za kilimo B. ukataji miti ovyo C. upandaji wa miti D. ufugaji wa
wanyama wengi
iv. Kifaa kinachotumika kupima unyevu anga huitwa _________ ( )
A. hygromita B. kipima joto C. anemomita D. kipima mvua
v.______ ni shughuli inayohusisha ustawishaji wa mazao na ufugaji wa wanyama ( )
A. ufugaji huru B. ufugaji C. kilimo D. kilimo cha mazao
vi. Kipindi kirefu cha ukosefu wa mvua huitwa ____________ ( )
A. mafuriko B. tetemeko la ardhi C. ukame D. kimbunga
vii. Mchoro ambao huonyesha kitu kwa mbele huitwa __________ ( )
A. kitu halisi B. ramani C. picha D. alama za ramani
viii. Lugha iliyotumika kuwaunganisha wananchi wa Tanganyika wakati wa kupigania
uhuru ni ( )
A. kizanaki B. kiingereza C. Kiswahili D. kizaramo

Page 1 of 3
2. Oanisha fungu A kwa kuchagua herufi ya jibu sahihi kutoka fungu B

FUNGU A FUNGU B
i Kiasi cha unyevu angani ( ) A Mawingu
B Mvua
ii Hali ya hewa ya sehemu Fulani C Mwendo kasi wa upepo
inayonakiliwa kwa muda mrefu ( )
iii Hupimwa kwa kutumia baromita( ) D Unyevu anga
E Anga
iv Huonyeshwa kwa kupima uelekeo F Mgandamizo
wa upepo ( ) G Hali ya hewa
v Hukadiriwa kwa oktasi ( ) H Sura ya nchi
I Uelekeo wa upepo
vi Hupimwa katika milimita ( ) J Joto ridi

SEHEMU B: JAZA NAFASI WAZI


3.Soma kifungu cha habari ifuatayo, kisha jibu maswali yafuatayo

Mfumo wa jua ni mkusanyiko wa sayari nane na vitu vingine ambavyo huathiriwa na nguvu ya
jua., Mfumo wa jua unahusisha jua,sayari, mwezi, vimondo na mawingu.Jua ni kitovu cha
mfumo wa jua.Sayari zote hulizunguka jua kupitia njia za kubuni zinazojulikana kama
obiti.Mfumo wa jua una umbo kama yai linalojulikana kama tufe.Elimu ya anga inayohusisha
mfumo wa jua hujulikana kama Unajimu. Mtu anayejihusisha na mambo yanga huitwa Mnajimu.
Katika kujifunza mambo ya anga kifaa maalumu kinachoitwa darubini hutumika. Darubini
ilibuniwa ili kuwezesha kuona vitu vya mbali hasa vitu vya angani.

MASWALI
i.Neno “unajimu” kama lilivyotumika kwenye habari lina maana ya
_____________________________________________________________________________

ii. Mtu mwenye elimu ya unajimu huitwa


____________________________________________

iii. Kitovu cha mfumo wa jua ni ____________________________________________________

iv. Kwenye mfumo wa jua kuna sayari ngapi? _______________________________________

v. Taja vitu viwili vinavyounda mfumo wa jua


a. ____________________________ b. _____________________________________________

vi. Kifaa kinachotumika kuona vitu vya mbali kama vya angani huitwa _____________________

viii. Kupitia nini sayari hulizunguka jua? _____________________________________________

Page 2 of 3
4. Soma ramani ifuatayo kisha jibu maswali hapo chini

MASWALI

i.Mfumo wa ukabaila ulioshamili maeneo ya kuzunguka ziwa Victoria ulijulikana kama


_____________________________________________________________________________

ii. Ziwa lenye kina kirefu barani Africa limewakilishwa kwa herufi _________________________

iii. Rais wa kwanza wa nchi inayowakilishwa na ramani hii aliitwa


_____________________________________________________________________________

iv. Kwa upande wa mashariki nchi inayoonyeshwa kwenye ramani inapakana na ____________

Page 3 of 3

You might also like